Riwaya: Shani

Hyungnim

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
301
482
Taratibu na kwa hatua za madaha mrembo shani alinesanesa kuelekea klabu ya usiku ya POME night Club.Alitembea kwa kunyata bila wasiwasi huku akijua fika hakuna kinachomwangusha!
Naaam kwa urefu wake wa kati alinesa kwa mwendo wa kimiss wa katiwoku(cut_walk) huku kajipuliza kwa uturi makini.Urembo na uzuri wake ulizidi ndege tausi.Hata yule mrembo wa kihistoria Cleopatra wa misri hakuona ndani.
Alikuwa mseto wa kifaransa na kidigo.midomo myembamba,myekundu kiasi ilimfanya avutie zaidi.hakika alifinyangwa bila ubahiri.Makalio ya haja yalokuwa makubwa kiasi na kufanyiza mviringo mfanowe wa tufe yalitikisika bila papara na kumfanya kila apitapo madume wakware wapinde shingo zao kwa kuikodolea macho rasilimali makalio.kwa kizungu. Battacks resource!. Jama shani alinona,akanoga na kutuama ktk dimbwi la upendo.vipofu pia waligeuka kumtazama kustaajabu ulimbwende wake,wakang'ata meno kwa utamu wa haja,kimiminika laini kikiwachuruzika vinywani mwao.jambo la ajabu ni kuwa kila jibaba lililomwona lilihamanika,maungo yalichemka,kijasho chembamba kitoacho harufu ya kuudhi kiliwavaa....

Aliongeza mwendo na kutuama kidogo eneo la mapokezi.Binti wa mapokezi akamkaribisha na kumpeleka sehemu wakaayo watu walioneemeka.Anajikalisha kihasara huku eneo la kifuani kaliacha wazi kidogo,lipumue na kupata hewa safi ya oksijeni.Pembeni yake kajituliza Kachero Ufuta Hajiwa.Ni wazi utulivu kwake ulikuwa shaghalabaghala,mrembo shani alimvutia,akamhusudu haraka.

Shani anainuka haraka na kwenda kuuliza vitu fulani kwa dada wa mapokezi.Anapewa maelekezo kisha haraka anatokomea.Kachero anahamanika,sononeko la kumpoteza ghafla mrembo linamkwida.Akiwa katopea ndani ya fikara za huzuni,shani anatokeza akiwa mpya.Kavalia maridadi haswaa.Katinga kisketi kifupi,chepesi matirio inayoangaza na juu kavaa kitopu kinachoacha maziwa yake madogo mabivu nje hivi kiaina.Kayafunika kdg na kitopu kilichofungwa na kitambaa cha satini.Madume wakware wanapiga miluzi,huku mikono ikikamata nyeti zao na kudhidhibiti zisije twaa zahama,zipu kuchanika.Ashki ya kumfaidi Shani iliwavamia!

Akiisha kutambua anawasulubu majibaba aliongeza mbwembwe huku akimuelekea Kachero.Aliyabinua makalio na kuinama kisha akainuka na kuyatikisa kwa fujo,vidole kavitia mdomoni.Akamshika Kachero ambaye ni wazi alikuwa mahututi,joto la huba lilimpanda,akatamani kumfinyanga.

Wanagandamana na kuanza kufuatisha mapigo ya muziki uliokuwa ukitumbuiza.Sasa ni wazi hawautii tena muziki,huba linawazidia na wanaanza kupanda ngazi kuelekea chumbani.Mwanamke kadhamirua,kumtunuku chakula kitamu Kachero Ufuta.Kachero anasahau kilichomtwaa hapo,pasi kuchunguza uhalali wa huyo banati.Anajiaminisha kuwa hana tatizo kwani hata machoye hayajabeba uovu,ni meupe na angavu yasemezayo hisia za juu za mahaba.

Shani anaufunga mlango na ufunguo anauficha.Kamdhibiti haswaa kachero,hapumui.Anamvua shati na kumpapasa,huku akimpulizia hewa ya ujotojoto ktk sikio lake la kushoto.Anapiga ukelele wenye sauti zisizo dhahiri,ni wazi alitopea kwenye kisiwa cha maraha.Shani anatia vitu fulani kwenye glasi yenye pombe pasi kuonekana,anamywesha kachero funda 2.Baada ya dk 1 uzuzu unamvaa.Shani anachukua kifaa cha kurekodia sauti,kazi imewiva...
nini kitatukia?shani ni nani?
endelea kuwa karibu na Hyungnim....
 
Back
Top Bottom