Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,447
SCOLASTICA TEMU
MTUNZI: INNOCENT NDASANYE
NAMBA: 0755 040 520
“KWA nini iwe hivi?” msichana huyu mrembo, Scolastica Temu alijikuta akijiuliza swali hilo mara nyingi huku akiwa chumbani peke yake akilia kwa uchungu.
Ulikuwa ni usiku, saa tatu kasoro dakika chache. Akatwaa kioo kidogo na kujitazama usoni. Akayaona macho yalivyo mekundu. Nywele zake hazikuwa katika mvurugiko wowote. Lakini akahisi maumivu ya mbali kwenye viwiko vya mikono. Alipojitazama vizuri mikononi akaziona vumbi. Hakushangaa, alijua ni matokeo ya kile kilichomkuta. Machozi yakaendelea kumtiririka mashavuni. Machozi ya uchungu.
Huu ulikuwa ni mwezi wa saba tangu alipoajiriwa katika kampuni ya uwakili ya Sam Advocates jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza miaka mitatu huko Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda alikosomea taaluma ya Sheria.
Alikuwa yeye kama yeye. Hakuwa na mdogo au mkubwa aliyemwita ndugu wa tumbo moja. Hata mama yake hakumjua. Hata baba yake hakumjua. Mimba yake ilipatikana wakati mwanamke mmoja wa mrembo wa Kimarangu aliyekuwa akifanya biashara ya mamalishe huko Kasulu mkoani Kigoma alipobakwa na dereva wa gari kubwa la mizigo lililokuwa likielekea Burundi. Mwanamume huyo aliitwa Temu. Jina la pili halikujulikana.
Tukio hilo la kubakwa lilitokea wakati mwanamke huyo na dereva walipokuwa wakijadiliana kuhusu biashara fulani ambayo wangeshirikiana. Kwa kuwa walifahamiana tangu wakiwa huko Marangu na ikatokea wakakutana hapo Kasulu, mwanamke huyo alijisikia kumwamini na kumchukulia huyo mwanamume kama ndugu yake.
Siku ya tukio, wakiwa ndani ya gari wakizungumzia hiyo biashara, ghafla, mwanamunme alimtolea kisu na kumtishia kumchoma kama asingemruhusu kufanya naye mapenzi. Janneth aligwaya na alipomtazama usoni akaziona dalili zote za kuua. Akamwachia mwili wake. Baada ya tukio hilo Janneth alitimuliwa humo garini huku akitishiwa kuuawa kama angeripoiti tukio hilo polisi.
Temu hakulala hapo Kasulu siku hiyo na hawakuonana tena!
Kubakwa huko kuliiunda mimba tumbon I mwa mwanamke huyo. Akaishi na mimba yake bila furaha moyoni, amani ubongoni. Miezi tisa ilipotimu, akajifungua salama motto mzuri wa kike. Akampatia jina la Scolastica. Alikuwa na hasira na Temu lakini ni ubini gani atampa huyu motto pale kwenye usajhili wa vizazi na vifo. Akamtaja baba yake yuleyule, baba mbakaji; Temu. Akawa ni Scolastica Temu.
Alimlea motto huyo katika mazingira magumu kwani biashara yake ya umama lishe ilitetereka na kujikuta akiwa katika hali ngumu. Hstimaye siku isiyo na jina, janneth a,liamka asubuhi na kwanagalia mwanaye huyo aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja na miezi kumi, akampakata na kumbusu. Mtoto akafurahi.
Akamketisha chini na kupatia chai na mayai ya kukaanga. Kisha akatwaa kalamu na karatasi na kuandika maandishi machache na kuiweka ndani ya bahasha. Juu ya bahassha hiyo akaandika KWA YEYOTE ASOME UJUMBE HUU. Akaiweka mezani ili iwer rahisi kuonwa. Mtoto alipotosheka, janneth akambeba na kumpeka kwa jirani ambako alimwomba mama huyo jirani akae na Scola wakati anakwenda kuteka maji bombani.
Hakwenda bombani, alirudi nyumbani ambako alikoroga dawa ya mimea kwenye kikombe, kisha akanywa. Akajilaza sofani Dakika chache baadaye alianza kutapika damu. Hakupumua zaidi ya dakika tano!
Maiti ya janneth iligundulika jioni baada ya jirani kutomwona akirudi. Na ndipo pia baada ya taarifa kufika Pilisi, na sakari kufika hapo, ikagundulika bahasha hiyo. Ndipo uliposomwa ujumbe uliokuwama.
MAISHA YAMEKUWA MAGUMU. NAMPENDA MWANANGU LAKINI ACHA NITANGULIE. TAFADHAQLIA WASAMARIA WEMA NITUNZIENI MWANAGU, MUNGU ATAWABARIKI.
Mtoto SCOLASTICA AKALELEWA NA jirani huyo kwa moyo mkunjufu. Akiwa ni mmumini mzuri wa kanisa, mzee Ndayikize alimlea motto huyo kama watoto wake wa kuzaa.
Umri wa kuanza shule ulipotimu, Scolastica alipelekwa kuanza masomo. Ada za masomo yake kuanzia elimu ya msingi hadi cghuo kikuu alilipiwa kwa msaada wa baadhi ya waumini wa kanisa wakishirikiana na mlezi wake, mzee Ndayikize.
Ni wakati yupo chuo kikuu ndiponaliposimuliwa kwa kina kuhusu historia yta maisha yake na kuoneshwa kaburi la mama yake. Sasa akatambua kuwa ana mlezi, hana baba wala mama. Watu walimfahamu mama yake, lakini hawakumjua baba yake na wala Janneth hakuwa kuwaambia lolote kuhusu mzazi wa kiume wa mwanaye.
Aliwapenda sana walezi wake hao na hata alipokuwa ameanza ajira katika kampuni hiyo ya uwakili alikuwa akiwatumia pesa mara kwa mara mara na mara mbili alikuwa ameshakwenda Kasulu kuwasalimia.
Ajira yake ilikuwa ikimpatia mshahara mzuri uliomweka katika maisha bora. Tayari alikuwa ameshanunua kiwanja eneo la Kigamboni na alikwishaanza ujenzi wa nyumba ya vyumba vinne.
Aliishi Kinondoni, jirani na Uwanja wa Biafra, akiwa amepanga vyumba viwili huku akijitegemea bafu, choo na jiko. Ilikuwa ni nyumba yenye mvuto nje na ndani…..
TUENDELEE?