RIWAYA: NIACHENI NIKUFURU
MTUNZI: FAHAD MUSSA
EMAIL:
fahadmussa55@gmail.com
*****SEHEMU YA TATU*****
Ya Ngoswe mpe Ngoswe, na ya Mazoea muachie Mazoea. Ni miaka ishirini sasa imepita tangu tumzike Baba. Sitaki kukumbuka tena ya Baba na Mama, maana hata mimi sasa ninayo mengi tu yaliyonisibu, tena yanaweza kuwa makubwa kushinda yale yaliyomtokea Baba. Ila nikutoe hofu tu mpenzi msomaji, mama yangu bado mzima wa afya ingawa amezeeka sana sahizi, wajukuu ndio wanaomfariji. Nami kila ninapopata muda siachi kwenda kijijini kumtembelea huyu mama yangu kipenzi.
MIAKA KADHAA ILIYOPITA
Ni likizo yangu ya kwanza kuipata tangu niajiriwe miezi michache iliyopita kama Ofisa rasilimali watu katika halmashauri ya wilaya ya Chemba mkoani Dodoma. Ni likizo hii ndio iliyoharibu kila kitu katika maisha yangu. Ni likizo hii ndio niliyoitumia kwenda kijijini kwetu kulibeba Jini Jackline na kuja nalo mjini. Yes, sijakosea, "Jackline au Mama Glory" ni jini haswa, limeninyonya hadi mifupa baada ya damu kuisha.
Nilidhani ndoa ni 'kuvaa shera na suti' na kucheza kwaito ukumbini huku tukilishana keki, kumbe ndoa ni zaidi ya maumivu ya pilipili machoni. Shahada yangu ya "Usimamizi wa Rasilimali watu" niliyoipata chuo kikuu cha Makerere Uganda, nyumba niliyopewa na ofisi, gari na mshahara wa kukizi mahitaji yangu vilinitia jeuri nikajiona muda wa kuoa umetimia. Sikujua kwamba "MWANA KULITAKA, MWANA KULIPATA". Hakika nimelipata.
*******KIJIJINI SENG'WA********
........."Jack, nakupa hongera kipenzi changu kwa kuwa mvumilivu kwa kipindi chote hiki tangu ningali chuo hadi sasa nimeajiriwa, hongera sana", niliongea kwa sauti ndogo ya mahaba huku nikibinya binya matiti malaini ya malaika wangu Jackline, tukiwa watupu ndani ya chumba changu.
......"Usijali Singu, kuwa mvumilivu ni jukumu langu, nakupenda sana ndio maana nikaamua kukutunzia tunda lako.Mimi ni wako peke yako, na itabaki kuwa hivyo. Nakupenda pia laazizi wangu".Jack alinijibu kwa sauti yake laini huku akipapasa papasa ndevu zangu zilizochongwa kwa mpangilio maalumu.
........"Hii harusi ikishapita tu, naomba tukimbilie kwetuuuu tukajenge familia. Kuishi kibachela nimechoka, kila siku nakula mgahawani chakula kibovu wakati mpishi wangu upo hapa", niliongea kwa sauti ya manung'uniko huku nikigusa gusa kiuno chake kilaini.
......."Kuhusu hilo ondoa shaka mume wangu, hata mimi naogopa unavyokula huko hotelini wanaweza wakakutilia limbwata mwisho wa siku umsahau mkeo bureee", Jackline alinijibu kwa sauti yake ya kudeka iliyonifanya nisichoke kumsikiliza kila anapoongea.
Hatukuendelea kuongea tena, bali sauti za kitanda na Godoro ndizo zilizochukua nafasi kwa purukushani tulizokuwa tunazifanya pale kitandani. Hakika ni furaha iliyoje kuwa karibu na mtu umpendae, nae awe anakupenda. Hakika Jack ni miongoni mwa wasichana wachache sana wenye kupenda kujiweka "smart" na kuendana na ukisasa, tofauti na mabinti wengine pale kijijini ambao muda wote ukikutana nao ni wachafu, kuanzia nguo hadi ngozi. Hata kwa uzuri wa sura na shepu, Jack wangu hakuwa na mpinzani pale kijijini. Weupe wake wa ngozi ndo kabisaaa ulinivutia, kama mnavyojua sisi wasukuma tunavyopenda mabinti weupe. Ni heri usiwe na meno ila uwe mweupe tu basi inatosha, wakukuoa watajazana kwenu hadi ukimbie mwenyewe.
Tulimaliza kuvunja amri ya sita, na hatimae nikamsindikiza kurudi kwao nami nikarudi nyumbani.
Baada ya wiki mbili, harusi kubwa ilifanyika pale kijijini, Mimi JOHNSON ALFREDY NZAGAMBA nikamuoa rasmi JACKLINE KASHINJE. Harusi ilifana sio siri, wenye kula walikula na wenye kulewa walilewa. Baada ya wiki moja za kukamilisha taratibu za kimila na kupokea baraka za wazazi, safari ya kurudi mjini ikaanza.
.........................................................................................
SHAIRI KWA JACK WANGU
Kama kupenda ni dhambi, niacheni niitende.
Sina shida ya maombi, motoni acha niende
Nipo radhi niwe zombi, au nife kama mende
Kwa Jack naweka kambi, niacheni nimpende
Kama kupenda ni kosa, wala musijisumbue
Kwa Jack nimeshanasa, sitaki muninasue
Kama zigo la kutesa, niache musinitue
Ole ataye mgusa, nipo radhi nimuue.
...........................**************...........................
Hilo ni shairi nililomtungia Jack wangu siku chache kabla hatujafunga ndoa. Ila leo hii ukiniambia nichague kimoja kati ya "kunyongwa" au "Kuliimba hili shairi", basi mimi nitachagua kunyongwa, kuliko kuimba huu ujinga niliouandikaga siku chache kabla ya harusi yangu na yule pepo mchafu "Jacline".
Naweza kukiri kwamba mwaka wa kwanza wa ndoa yetu na Jackline ulikuwa ni mwaka furaha sana. Tuliishi kwa upendo na amani. Najua kuna kupishana maneno ya hapa na pale ila mwisho wa siku tulielewana. Nilifanikiwa kujenga nyumba yangu ndani ya miaka miwili tangu nianze kazi, na pia hata ofisi nilihamishwa kutoka wilaya ya Chemba hadi makao makuu ya mkoa "Manispaa ya Dodoma. Hapa sasa ndipo mambo yakaanza kubadilika.
Mimi si mtu wa kujichanganya sana na watu, nina marafiki wachache sana tangu nihamie hapa makao makuu. Rafiki yangu mkubwa ni Idris na Godfrey. Hawa ndio watu ninaoweza kukaa nao na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusiana na kazi zetu na stori nyingine nyingi ingawa kicheo nimewapita, mimi ni Boss wao.
Godfrey, kama nilivyo mimi nae ameoa na ana watoto wawili, mimi bado sijabahatika kupata mtoto. Ila Idris yeye hajaoa ingawa anaishi na mpenzi wake "Roida", ni mwaka wa tatu tangu waanzishe mahusiano.
Siku ya Jumapili ya mwisho wa mwezi nilimualika nyumbani, Idris na mpenzi wake "Roida" ili tupate kujumuika kwa pamoja katika chakula cha mchana na kuzungumza mawili matatu kama marafiki na majirani.
.........."Shem samahani, unaweza kuturuhusu tuondoke na 'mamito' ili akapajue kwetu, maana kila mara unakuja wewe tu alafu misez hata hapajui", ilikuwa ni sauti ya Roida wakati wa kuagana akiniomba nimruhusu Jackline waondoke pamoja nae kuelekea kwao ili akapajue.
........."Usijali shemeji yangu, nyie nendeni tu hamna tatizo. Huwa nasahau kuja nae kwenu kisa mambo mengi kichwani yamenitinga, ni kweli ukisemacho.Ni muhimu akapafahamu munapoishi ili siku likitokea la kutokea iwe rahisi kuwasiliana", nilimjibu Roida huku tukiwa tunafungua lango la geti kuu kutoka nje.
.............."Wanawake bhana, yani hapa Roida ndo kafurahi mwenyewe ulimvyomruhusu aondoke na shemeji", akadakia Idris huku akimpigapiga Roida vikofi vya utani mgongoni.
............."Hahahahaha, ndo hivyo. Sitaki mwanamke mwenzangu ajifungie ndani tu wakati hata kwetu hapajui", alijibu Roida huku wakipanda kwenye gari lao 'TOYOTA Harrier New model'.
Jackline nae aliagana na mumewe na kumuahidi kuwa hatochelewa kurudi, hatimae akaingia garini na Idris akalitoa gari kuliingiza barabarani.
NYUMBANI KWA IDRIS
................"Roida, fanya basi kama nilivyokuelekeza, nahitaji kulala na Jack hata sahizi kama itawezekana", ilikuwa ni sauti ya Idris akimsisitiza Roida. Wawili hao wakiwa chumbani huku Jackline wakimuacha sebleni akiangalia luninga.
........."Usijali Iddy, Jack ushamnasa. Ngoja niende sebuleni nikaweke mambo sawa alafu nitakuja kukushtua", Roida alijibu huku akiinuka na kufungua mlango kuelekea sebuleni alipo Jackline.
*Roida na Idris wana mipango gani ya siri?. Je, hawa sio wapenzi?
USIKOSE SEHEMU IJAYO.
Sent using
Jamii Forums mobile app