Kindo Emmanuel
Member
- Dec 5, 2021
- 34
- 25
ILIKUWA ni asubuhi chungu kuliko zote nilizopata kuamka. Nilitetemeka na mwili wote ulifukuta kwa maumivu yasiyomithilika, jasho halikuwa mbali namni. Nilihisi utumbo ukijinyongorota ndani kwa njaa niliyohisi na kila nilichojaribu kula nilitapipika mpaka nyongo. Nilihisi huenda nilikumbwa na homa ya matumbo au malaria kali.
Nilijiandaa na kujikongoja kwenda katika hospitali ya wilaya, bahati haikuwa mbali na niishipo.
Kama ada, huko nilikutana na foleni ikatishayo tama kwani ilijongea taratibu sana hivyo sikuwa na ajizi zaidi ya kusubiri tu zamu yangu.
Niliketi katika foleni nikiwatathmini wagonjwa waliokuja pale. Karibu wote walivaria nadhifu, wakina mama walinukia uturi. Nikahisi wote pale ugonjwa wowote uliowaleta si lolote wala chochote ukilinganisha na ugonjwa wangu, kama wangekuwa mahututi kama nilivyojisikia nauhakika wasingepata hata muda wa kujipara na kujikwatua vile kabla ya kuja pale hospitali. Niliwachukia wote na kuwatusi kimyakimya rohoni. Dua la kuku! Ndoyo, nilijua fika kuwa dua la kuku halimfiki mwewe lakini nilipowatusi nilijisikia afueni na burudani fulani moyoni japo haikuwa ni dawa ya ugonjwa wangu.
Matusi hayaui, ila humpunguzia kisirani mtukanaji.
Baada ya kusubiri kama masaa mawili hivi hatimaye jina langu likaitwa, nikajikokota hadi chumbani kwa dakitari.
Alikuwa mtu mzima hivi, kwa kumtazama haraka haraka ilionyesha alimzidi baba yangu kwa miaka kadhaa. Alijaa kwenye kiti chake cha enzi akijizungusha taratibu na lile umbo lake nene lakini lisilochukiza. Sikuweza kuona miguu yake iliyokuwa imefichwa na meza kubwa yenye nakshi za chuma. Alivalia shati la rangi ya buluu bahari, tai nyeusi huku kwa juu akijisitiri kwa koti jeupe la kidakitari. Kama ulivyohisi…..shingoni alininginiza kile kidubwana cha kusikilizia midundo ya moyo.
Alijikohoza kwa sauti ya chini nakambumbuluka na kurejeza umakini wangu katika kilichonileta mle ndani. Alinisabahi kwa sauti yake nzito lakini itiayo matumaini. Nilipokwisha kuketi akanisaili juu ya ugonjwa wangu name nilimjibu kwa namna vile nilivyojisikia, akawa anatikisa kichwa huku akiniangalia kwa umakini nyuma ya ile miwani yake ya kusomea.
Baada ya kuchukua maelezo yangu akanifanyia vipimo vyote lakini cha kustaajabisha sikugundulika na ugonjwa wowote ule. Nikaleta pingamini. Nilimwambia ya hakika kuwa hata pale hospitali nilifika kwa kujikongoja sana. Akaniabia kuwa anao weredi wa kazi yake kwa zaidi ya miaka ishirini na mitano na isitoshe vipimo huwa haviongopi. Lo! Nikakata tama. Akaniandikia vidonge vya Panadol na vingine vikubwa vikubwa vya rangi ya njano. Akasema nitumie kwa siku tatu kasha dalili zikiendelea nirudi tena.
Sikuwa na jinsi, nikachukua vile vidonge na kuondoka nikitukana tena kimoyomoyo.
Siku tatu zilipita nikiwa sijapata nafuu yoyote na hata niliporudi yalikuwa yale yale. Panadol….Vidonge vikubwa vikubwa vya rangi ya njano. Nilikereka na safari hii nilitamani nimtukane kwa sauti huenda ningepona kabisa, ila niliogopa askari waliokuwa pale jirani.
Siku moja jioni nikiwa nimejituliza janvini nikipunga upepo, rafiki yangu Wile akaja kunijulia hali. Alisikitika sana kuniona katika hali ile kwani nilikonda sana kwa mawazo na ugonjwa uiokuwa ukinisurubu. Alinipa pole na kunipa ushauri kuwa anamjua mtaalamu bingwa wa dawa za asili ana uhakika angeweza kunisaidia tatizo langu. Akadai kuwa anaishi katika kijiji Fulani huko milimani kama nilikuwa tayari anipeleke. Hakika adha niliyokuwa napitia sikutaka kumpinga, maana licha ya kusumbuka sana hospitalini sikukata tama moja kwa moja, niliamini siku moja ningepata matibabu kwa namna yoyote. Nani anataka kufa? Thubutu! Kifo kipo, lakini sikuwa tayari kufa kizembe.
Nilimweleza kuwa nipo tayari lakini pesa yote iliishia hospitalini, akaniondoa wasi na kunambia kuwa angesimamia zoezi lote kwa gharama zake mwenyewe. Nilimshukuru sana na kumkumbatia kwa furaha.
Kesho yake asubuhi na mapema alikuja nyumbani akakuta nilishajiandaa kwa safari, tukaondoka. Safari ilikuwa ni ndefu, tulipanda basi hadi katika hicho kijiji, kasha tukachukua bodaboda, tulipofika katika kijiji kingine ndani kabisa hakukuwa na usafiri mwingine zaidi ya baiskeli. Tukasogezwa mpaka mwisho wa ile barabara ya vumbi iliyokuwa imekomea mtoni… Tukavuka kwa moja ya mitumbwi iliyokuwa ikitumiwa pale kama usafirishaji kwenda ng’ambo ya kijiji kingine. Huko tulitembea sana tukipanda kuelekea kule mlimani alipokuwa huyo tabibu.
Tulifika tukiwa hoi kwa uchovu. Tulipokaribia katika zile nyumba za tabibu mwenyewe zilizokuwa zimeezekwa kwa paa la nyasi tukakaribishwa na sauti ya ajuza ikitokea katika moja ya zile nyumba au niseme tu vibanda. Alituambia tuvue viatu kule kule tulipokuwa akadai pale palikuwa mahali patakatifu. Mh! Niliguna moyoni. Utadhani alinisikia, akadai kuwa alishajua shida yetu kabla hatujafika pale na mimi ninayeguna ndiye mgonjwa mwenyewe. Toba! Mimi na Wile tukaangaliana. Yule bibi akatuambia tuingie kinyume-nyume, tukafanya kama alivyotaka.
Ndani mlikuwa na giza totoro lakini lililoturuhusu kuonana. Mlikuwa na kijidirisha kimoja tu kidogo kiichokuwa kinaingiza mwanga hafifu huku kikijitahidi kukinzana na harufu nzito ya ubani, udi na mchanganyiko mwingine nisioujua mle ndani. Yule bibi akasema nimpe kiganya cha mkono wangu, kasha akakitazama kwa dakika kadhaa. Akanitazama usoni kwa macho yake makubwa na mekundu. Niliogopa, mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakidunda kwa vurugu hata nikahisi anayasikia.
Akaniambia kuwa tatizo langu lilisababishwa na tego Fulani nilililikanyaga njia panda kwa bahati mbaya, tego hilo alitegewa mtu mwingine. Ila akanitoa hofu na kusema kuwa nilikuwa nimefika sehemu salama kwani yeye ndiyo mtaalamu kiboko ya mizimu na uchawi. Makubwa!
Alinichanja chale kadhaa sehemu za mwili wangu na kunipaka dawa Fulani nyeusi hivi ambyo ilikuwa inachonyota na kuwasha ilipokutana na damu.
Baada ya kumaliza matibabu ya awali, akasema akatupatia moja ya vile vibanda vyake ambacho kilikuwa mahususi kwa wagonjwa walalao na kutuambia kuwa kwakuwa muda ule ulishaenda hivyo kesho yake tungeenda kumalizia matibabu huko mlimani kwenye makaburi ya watu wa zamani.
Chumbani tulilala juu ya vitanda kilichofanyizwa kwa miti na kamba almaarufu kama teremka-tukaze. Juu yake palitandikwa ngozi ya ng’ombe. Usiku ulikuwa mrefu sana kwangu, sikuisha kujigeuza huku na kule kwani ile ngozi nilihisi inanichoma-choma. Ajabu nilipomtazama Wile yeye alikuwa anakoroma na wakati mwingine akijamba kwa utamu wa usingizi. Sikujua nilipitiwa na usingizi muda gani.
Kulipopambazuka Yule bibi alikuja kutuamsha akiwa na majembe mawili, koleo na sururu. Akasema tujiandae kwa safari ya kwenda kuchukuwa dawa yangu ya mwisho. Tulijiandaa haraka haraka na safari ikaanza.
Yule bibi alikuwa mbele akiongoza njia, kasha nikafuatia mimi na nyuma yangu akiwa Wile. Tulipita katika vichaka kwani njia ilikuwa imeshaota miti kwa kutopitwa kwa muda mrefu. Wakati mwingine ilitubidi kukata vichaka kwa kutumia panga ili tupenye ndani zaidi. Ndiyo! Tulizidi kusonga tukielekea sehemu za juu kabisa yam lima. Hatima tulifika maeneo ya makaburi. Kama alivyotudokeza awali…. Ni kweli yalionekana ni ya zamani sana kwani yalikuwa makuu kuu, yenye ufa na mengine yalibomoka kabisa. Tulizidi kusonga mbele tukikatiza kwenye makaburi yale.
Kuna kitu kilinishtua mno. Nilipotazama vizuri niligundua kuwa licha yay ale makaburi kuwa ni ya zamani na machakavu lakini mashahidi (Mawe yawekwayo juu ya kaburi) na misalaba yake ilikuwa mipya kabisa. Mtume! Na kilichonifanya nianze kutetemeka ni kwamba kwenye yale mawe na misalaba yaliandikwa majina ya watu ninaowajua kabisa tena walikuwa hai kule mjini. Yalikuwepo majina ya jirani za kama Mama Kidawa, Mzee Ndimbo, rafiki yangu Side Tozi, Mwajei hadi jina la mama mwenye nyumba yangu. Nikajiuliza alifariki lini wakati juzi tu alikuwa ananikoromea pesa yake ya bili ya umeme? Makubwa! Nilijikaza kisabuni nikiwa nimeishiwa pozi.
Tulipofika mbele Yule bibi akasimama na kutuambia kuwa tulifika sehemu husika. Nikasonga mbele na kuwa usawa wake. Tulikuwa tumesimama pembeni ya kaburi chakavu kama mengine yote pale. Ila hili msalaba wake uliandikwa jina langu, tena yote matatu kwa usahihi kabisa. Bibi akanitazama nay ale macho yake mekundu na kutabasamu. Akasema anajua kuwa nina najiuliza maswali mengi moyoni. Akaniambia kuwa nilishakufa kimiujiza zamani sana, na nilifanya jambo muhimu kwenda kwake maana ningeendelea kuumwa ugonjwa usiojulikana milele bila kufa kwakuwa nilishakufa tayali. Nilistaajabu nisielewe chochote, na nilikosa cha kuuliza. Akaendelea kuniambia kuwa dawa ya ugonjwa wangu ilikuwa mle ndani ya kaburi hivyo alitutaka tufukue kabiri lile. Laniki kabla ya kufukua akanitaka nimshike mkono kasha tukalizunguka lile kaburi mara kadhaa huku akizungumza maneno aliyoyajua mwenyewe. Alipomaliza tukaanza kufukua mimi nikisaidiana na Wile.
Tulichimba kwa muda mrefu mpaka tukalifikia jeneza ajabu tena ni kuwa lilionekana jipya. Yule bibi mtaalau akalinyunyuzia unga Fulani mweusi tena kasha katuambia tulitoe mle kaburini na kulipandisha juu. Tukatii.
Tulipolitoa nje Yule bibi akaniambia kuwa dawa yangu iko mle ndani ya jeneza, yaani ni Yule maiti alo ndani yake, akanikabidhi kisu kidogo kikuu kuu lakini kilikuwa kikali sana na kunambia kuwa kama nataka kupona na kuwa huru tena ilibidi nifunue lile jeneza na kukata kipande kidogo cha nyama ya marehemu nile. Lo! Niliwaza, nikawaza tena, kasha nikakata shauri. Nikasema liwalo na liwe lazima nile ili nipone. Nikalisogelea lile jeneza na kuliinamia, nilipotaka kulifunua nikashikwa bega. Nikainua shingo kuangailia ni nani aliyenishika kumbe alikuwa ni kondakta anataka nauli yake. Lo! Nikavuta pumzi na kuzishusha kwa ahueni. Kumbe likuwa naota tu.
Nilimlipa kondakta pesa yake, nikashuka kituo kinachofuata pale Tanki Bovu Mbezi nikampigia simu Wile na kumwambia kuwa nilipata udharura sitaweza kwenda kwake siku ile. Nikazima simu na kuchukua daladala nyingine kurudi nyumbani .