gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 759
- 1,250
RIWAYA: MZEE WA BUSARA MWANDISHI - SULTAN TAMBA
ANGALIZO, Riwaya hii ni ya zamani iliwahi kutamba kwenye magazeti ya kila wiki, leo nimewaletea mpate kuburdika.
MWANZO
NILIHISI kupagawa. Akili yangu ilikuwa mbali sana usiku huo. Sjiui mtanielewa nikisema kwamba nilikuwa kwenye ndoto katika bustani ya mfalme au peponi au ni mahali gani pazuri kiasi kile. Lakini ndivyo ilivyokuwa. Nilikuwa kwenye ndoto nzuri yenye kusisimua mwili na akili.
Naomba nikiri kwamba ilikuwa mara ya kwanza katika maisha yangu kujikuta nikijisikia raha na amani kiasi hicho.
Mwanga hafifu wa rangi nyekundu, harufu nyepesi zenye mchanganyiko wa manukato ya mti wenye thamani, viliniwehua sambamba na kungumanga ambazo nilizibwia muda mfupi uliopita.
Nilikuwa nimejipachika katikati ya mikono ya mwanaume ambaye ndio mara ya kwanza nakutana naye kimapenzi. Ni mwanaume ambaye sikumfahamu kabla ya siku hiyo. Ndiyo mara ya kwanza na ndiyo hapohapo nanasa mikononi mwake! Kutokana na hilo, sikuwahi kutambua kama ni fundi wa mapenzi kwa kiasi nilichomkuta nacho!
Asikwambie mtu, raha ya mapenzi ni pale unapokutana na mtu anayejua kupapasa, kukufikisha na kukugeuza atakavyo kitandani! Ni hilo tu, hakuna kingine. Hapo hata kama mwanaume atakuwa bubu, kipofu, mlemavu au yeyote mambo ndiyo hayo!
Nilichofanya wakati najiandaa kukabiliana naye, ilikuwa ni kukipamba chumba changu. Nilinunua udi, asumini na aina mpya ya pafyumu, Kwa sababu mwanaume mwenyewe alikuwa ana asili ya Kizanzibari nilijitahidi kufanya vile ambavyo watu wa huko nilisikia husisimka sana! Niliwahi kusikia stori nyingi vijiweni kwamba wanaume wa huko mara nyingi hupenda kupata harufu za manukato ya udi, pafyumu na vikorombwezo vingine.
Niliambiwa kwamba kama utabahatika kuvijua vitu avipendavyo mwanaume kama huyo na ukamtimizia, basi hata ukitaka akununulie ndege atafanya kila liwezekanalo akununulie! Na ndio maana nikasema pale mwanzo, raha ya mapenzi ni kuguswa pale ambapo ashki zimelalia!
Mawazo haya hasa nilipewa na mcheza shoo mwenzangu wa bendi yetu ambaye aliwahi kuolewa na bwana moja la kigunya kabla hawajashindana kwa mambo mengine. Hasa kilichonifanya nimkubali mwanaume huyu ni fedha zake. maana alikuwa nazo si mchezo!
Nilijikuta nikitamani kupiga kelele wakati mikono mikubwa yenye nywele kibao ilipokuwa ikitalii mwilini mwangu kwa mtindo wa kipekee. Mikoni ya mwanaume huyu ilitumia muda mwingi kuutengeneza mwili wangu ukae kwenye hali ya kuingia kwenye mambo. Hakuwa na haraka kama ile waliyonayo baadhi ya majibaba mengine ambapo ukifika nayo chumbani yakishaona paja tu yanataka mchezo moja kwa moja.
Mikono hiyo ilitembea ikitomasa maungo. Ilitembea ikipapasa ngozi ya mapaja yaliyokuwa yakimeremeta kutokana na kuakisiwa na mwanga wa taa pamoja na rangi nyekundu ya shuka niliyotandika kitandani. Kwenye kidole chake kimoja ambayo alikuwa na kucha ndefu aliitumia vilivyo kunikwaruza kwa upole kwenye maeneo ya uti wa mgongo na kwenye mizunguko ya matiti!
Niliwehuka!
Nilijinyonganyonga mikononi mwake huku nikishtukashtuka kwa kadri alivyokuwa akinisisimua, Nilihisi kulia, halafu nikahisi kupiga kelele, hasa pale aliponiweka tayari kwa ajili ya mambo.
"She...sh...Sheba.." niliita jina lake kwa taabu.
Hakuitikia. Aliendelea na zoezi alilojipangia, zoezi la kunipagawisha. Ghafla, nilihisi mabadiliko.
Kuna harufu mpya iliniingia na kuvuruga utulivu wote wa usiku huu. Si hivyo tu, kabla ya harufu hiyo, nakumbuka nilisikia kwa mbali mlango wa mbele ukifunguliwa kwa hadhari kubwa. Sheba hakujali harufu mpya, pengine hakuisikia.
Nikajikuta nikimtoa mwilini kwa nguvu na kukaa chini. Nikayatupa macho mlangoni! Sura yangu ikakutana na kiumbe dhahiri aliyesimama mlangoni. Kutokana na kupigwa na mwanga kwa upande mmoja, sikuweza kumtambua kirahisi. Nilikaza macho kumtazama. Kuna kitu kingine kikanishtua.
Alikuwa uchi!
Sheba alikuwa amelala kifudifudi, hajui kinachoendelea! Nilitamani kumshtua aone, lakini kuna ganzi fulani iliniingia na kunifanya niwe kama zuzu. Kwa muda, nikatumbua macho kumtazama kwa bidii huku nikiwa natetemeka.
Nikamtambua!
Alikuwa ni mzee Toboatobo! Baba mwenye nyumba wangu!
Bado sikujibu. Ulimi uling'ang'ania juu ya kinywa. Kitetemeshi changu kikaongezcka maradufu!
Mzee Toboatobo akatoka mlangoni kunifuata kwa kasi. Misuli ya ngozi ya shingo ilichachamaa pale nilipopiga kelele kwa nguvu.
Nikashtuka usingizini!!
Jasho lilikuwa linanitoka na mapigo ya moyo yalikuwa juu kama ya mwanariadha aliyemaliza mashindano ya mbio ndefu!
Nilifarijika kidogo kukuta kwamba kumbe ilikuwa ndoto! Sikujua ndoto hiyo ilikuwa na maana gani.
Miale ya mwanga wa jua ilipenya dirishani kwangu na kunifanya nifahamu kwamba hiyo ni asubuhi, muda ambao nilipanga kufuatilia mipango yangu ya chumba kingine baada ya kupewa notisi kwenye nyumba niliyokuwa nikiishi.
Kwa kuwa ilikuwa ni ndoto sikutaka kuipa nafasi sana akilini. Nikaenda bafuni kuoga tayari kwa kujiandaa na safari yangu!
ITAENDELEA...