RIWAYA: MZANI

RIWAYA: MZANI

Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Posts
1,821
Reaction score
6,122
Naeza sema wewe ni mzuri ila siwezi kusema unauzuri wa kuisimamisha Dunia.Sijui uchawi gani huwa upo kwenye hisia za binaadamu hasa wa kiume tunajisahau sana hasa tunapoingia kwenye ulimwengu wa mapenzi.

Nilikuona kama wewe ni kiumbe kutoka sayari nyingine,lah kumbe ulikuwa sayari moja na mimi,ulikuwa mzuri machoni pangu, nikakutunuku shahada nyingi za upendo,nikabembeleza kila ilipobidi,ila ukasahau yote na ukaamua kuufuata utamu wa noti mpenzi wangu

Sasa si ungeniachia utu wangu wewe na pesa mkashiriki kumtia roho mbaya mkubwa wangu kazini nae kwa madara na pesa akanitia kitanzi cha uhuru nipo gerezani nikiishuhudia adha ya maisha magumu ndani ya uzi wa rangi ya chungwa,.

Tuse mpenzi nilitamani unifanye kivuli chako popote ulipo niwepo ila ukaamua kujitokeza usiku wa kiza ukiamini sintakuwepo kivuli mimi.unanifanya niyakumbuke mengi juu yako na hapo moyo wangu unadhihirisha vile ulivyokuwa umemea moyoni mwangu

Pua zangu hazijapoteza harufu nzuri ya manukato yako,viganja vyangu bado vinauhisi msuguo wa ngozi yako laini,papi zangu zinalimisi joto la papi ya midomo yako,kila nikifumba macho taswira yako inajijenga mara mia ya uhalisia wako..

Tuse wangu miguno yako kunako uwanja unamgunia nani ihali nipo kitanzini nikiwa sijui hatima ya kesho yangu,nyonga yako laini inamzubaisha nani wakati huu,eti Tuse inamaana kwa sababu ya pesa ukasahau vile tulivyovipanga kabla na baada ya ndoa? Basi Tuse ungeniacha angalau nipate mtoto mmoja tu na wewe iwe faragha yangu mh,.

Tuse japo nayaandika haya ila bado nazikumbuka nasaha za wazazi wetu siku ya harusi yetu,lakini Tuse kwanini usinifanyie jema moja tu uwaambie kwa kinywa chako wazazi wangu kuwa Mimi si muuaji? Kisha endelea na mambo yako,

Nishakusamehe Tuse mana hata nisipokusamehe haitasaidia kitu zaidi itanipa mateso ya nafsi yangu, nipo gerezani lakini bado akili yangu inautaka uhuru na inauaza kila siku,.

Tuse ulifundishwa na nani ukatili huo tena kwa mtu uliempenda miaka zaidi ya mitano,mtu alievunja ngome yako katikati ya miguu yako,mtu alijitolea kukufanya nawe uonekane ni mtu katika watu,mtu aliamua kufunga pingu za maisha na wewe Tuse

Eti Tuse hivi huko uliko unakula chakula unashiba kweli? Basi kama ni hivyo wewe ni ule uzao wa Lilith yule mke wa shetani,

Haki hainunuliwi nanyi hapo mmekopa tu nina imani siku mkilipa mtailipa na riba,.

Tuse moyo wangu unanambia mateso yangu yataisha na haki nitaipata ila sijui nani atakae kuwa amepoteza wakati huo japo nakuombea usipoteze chochote na ubaki tu kushuhudia mateso au furaha yangu mwanamke wewe,mwanakmke usie na huruma japo kidogo

Hivi nikuulize ulishawahi jiuliza mama yangu anapitia mateso kiasi gani ilihali Mama yeye akicheka kwa kupokea vizawadi vyako?

Na hata nisipotoka bado mzani upo hukumu ya mungu au mkono wenu ulioibeba haki yangu.....

*********
Alishusha pumzi baada ya kumaliza kusoma barua ile kutoka kwa mume wake alieko gerezani,kisha akaikunja vizuri na kuiweka kwenye mkoba mdogo ulioning'inizwa pembeni kidogo ya kitanda,kisha akaitazama saa iliokuwa ukutani nayo bila kuficha ikamueleza ilikuwa ni saa saba na nusu usiku,baada ya kusoma saa ile akageuka ili alale hapo akakutana na macho ya mtu yakimtazama kwa maswali ya viulizo '"ulikuwa unafanya nini?"
Hakujali akajilaza pembeni ya mwanaume yule kisha akachukua mkono mmoja akaupitisha kifuani kwa bwana yule huku akikirusu kichwa chake kuchanganua mambo.

Tuse hakulala vizuri ndoto nyingi zilimfanya asitishe zoezi la kusinzia na kutafakari mambo yalivyo hadi kufika hapo yalipo nafsi yake ikamsuta ila hakuwa na namna zaidi ya kukubali hali halisi na kupuuza yaliopita.

Ilikuwa ni weekend siku ya jumapili wafungwa wengi walitembelewa na ndugu zao,miongoni mwa watu waliopta ugeni alikuwa ni mfungwa namba 674 au kwa jina aliitwa Mayunga, alikuwa ametulia kwenye selo yake,punde akaja askari magereza na kumuita hakuwa na tabia ya kususia wageni,akanyuka na kwenda kukutana na mgeni wake,.

Hakuamini macho yake pale alipokutanisha macho yake na mgeni yule,alikuwa ni mwanaume yuleyule alimweka matatizoni,mwanaume aliemfanya awe hapo alipo kisa mapenzi,alijikuta anashikwa na hasira ila akaamua kujizuia asifanye lolote,mbele ya askari magereza na kwa upole kabisa akamuuliza mgeni wake
" Maganga mume wa Tuse nakusikiliza"
Maganga nae akamtazama kwa majivuno kisha akanena
"Unaonaje ukiacha kumwandikia mke wangu barua muuaji wewe mmh"..

Badala ya kukasirika Mayunga alicheka kisha kwa upole akatiksa kichwa na Kusema
"mshindi wewe ya nini kumsumbua hayawani muuaji alie gerezani?"

Bila kungoja majungu zaidi kutoka kwa Maganga akaanza kuzipiga hatua fupi fupi na kutoka kwenye chumba cha mazungumzo na uondoka zake huku nyuma akimuacha maganga akimtizama kwa chuki ya waziwazi.

[HASHTAG]#Niite[/HASHTAG] Bahati(kudo)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom