Riwaya mpya: Mbwa wa geti

daah bonge ya kitu hii
 
Mkuu Kudo900 ulituahidi asubuhi na jioni hii kitu, tupe wepesi kwa ahadi yako Chief
 
Mbwa wa geti

Sehemu ya tano


Akajilegeza kidogo na kujikwaa na akaenda hadi chini,kisha akaanza kunyanyuka taratibu,yule mlinzi akamfuata kwa kasi kwa lengo la kumpiga na kitako cha bunduki lakini hakuwa amejua hila ya Zedi na tayari zedi alikuwa ameona pa kutorokea na hakutaka kuwa mzembe wakati amefuzu kozi nyingi za ukomando,njaa hakuisikia tena
Mlinzi aliekuwa nyuma ya Zedi akahadaika kwa kasi akaanza kumfuata Zedi aliekuwa akijinyanyua kutoka chini, lakini adhima yake haikutimia na kitendo bila kutarajia akajikuta akipokea teke safi kutoka kwa Zedi ,teke lile likamrdudisha nyuma hatua kadhaa lakini akakuta akikikabiliana na ngumi za kasi kutoka kwa Zedi na ndani ya dakika moja alikuwa amejaa mikononi mwa Zedi huku walinzi wengine wakiwa wamefika pale kwa ajili ya kutoa msaada

Mitutu ya bunduki zaidi ya kumi ilikuwa imemwelekea Zedi aliekuwa nyuma ya mlinzi mmoja aliekuwa amemkaba kwa kabari matata na kisha alimweka ngao mbele yake na nyuma yake hakuwa na shaka kwa sababu alikuwa ameufanya ukuta kuwa kinga yake na aliamini hakuna wa kuweza kumshambulia kutokea nyuma hata kama angelitokea kwenye mlango wa kuingia kule walikokuwa wakielekalea mwanzo,bado angeliwaona.

Zedi alipiga hesabu za kutumia mabega ya mateka wake kuparamia paa lililokuwa kichwani pake ni wakati huo aliposikia sauti ikitokea kwenye mlango waliokuwa wakielekea kabla hajafanya manjegeka kwa bwana yule alie mikononi mwake sasa.
Kill them all
Sauti aliitambua ilikuwa ni sauti ya Kabah nae hakutaka kuona risasi za SMG zijaa kifuani kwake .
Zedi ni mchawi wa mipango ya kujiokoa na pia ni mchawi wa mapigano huwa hakati tamaa hata kama amedhoofu vipi,na hili alilidhihirisha mbele ya Kabah na genge lake.
Zedi alimsukuma yule mtu aliekuwa amemweka kama ngao na mtu yule akaelekea kuwakumba walinzi walikuwa manajiandaa kushambulia,kisha kwa wepesi wa ajali ya bodaboda akachumpa kwenda juu kidogo na guu lake la kulia likatua katikati ya mgongo wa mateka wake aliekuwa ameanza kuchezea risasi na kwa kasi ile ile akaenda juu zaidi na mikono yake ikalikamata paa la jengo lile kisha kama nyoka awindae akajivuta na kukaa juu ya paa kwa namna ya pekee kabisa hadi walinzi wale wakaacha kushambulia wakabaki wakishangaa uwezo wa Zedi,hawakuamini kama angeliweza kuwatoka kwa namna ile ya ajabu kabisa..
Kabah alicheka,sio kama alifurahi la hasha,alicheka kwa fadhaa na chuki ya kutorokwa na Zedi na huku nafsi yake iki kiri kabisa ya kuwa Zedi akifanikiwa kutoka kwenye ngome yake basi mambo yake yatamwendea kombo.
****
Zedi akiwa juu ya paa ile akaona mbele yake hakuna nyumba hata moja,lilikuwa ni pori tupu,pori lenye miti mirefu na hapo nafsi yake ikapata nguvu,alipenda michezo ya porini na huo ndio ulikuwa wakati wake.
Akachumpa hadi chini na kisha akaanza kukimbia kusonga mbele kulikokuwa na miti mingi iliofunga na tayari kiza kilianza kukolea wadudu wa usiku walikuwa wanapiga miluzi kushangilia muda wao,lakini si wote waliokuwa wakishangilia kwa furaha maana wengine walijikuta wakishangilia kwa woga baada ya kusikia vishindo vya kitu kizito kikipita karibu yao,alikuwa ni Zedi akikimbia katikati ya pori asililolijua na tayari sasa nyuma yake alikuwa akikoswakoswa na risasi za waliokuwa wakimkimbiza huku wakiwa na amri moja tu wakimpata wamuue.
Zedi alipiga hesabu maana risasi zinatoka kwenye bunduki moja,hivyo mtu aliekaribu yake bila shaka ni mmoja haraka akatoka kwenye uelekeo ule aliokuwa anaendea na akajibanza kwenye mti,lakini akagairi kujificha hivyo na kama paka akauparamia mti ule kisha kama nyoka akajigeuza na kichwa kikatazama chini huku mikono ikiwa imeukama vyema mti ule mrefu,alitulia hata pumzi zake mwenyew hakuzisikia.

Mtu yule aliekuwa anamkimbiza Zedi,akashangaa kuona anakimbia peke yake,akajua anategwa au amepigwa changa la macho usiku ule.
Akaanza kunyata huku sasa hofu ikiwa dhahiri moyoni mwake.
Alihofu vitu viwili,mosi alihofu viumbe ambao aliamini watakuwapo ndani ya pori lile usiku ule na pili alihofu kukutana na mtu yule aliemwona akidondoka kutoka juu ya paa la kambi yao,lakini kubwa zaidi akiogopa maana hakuwa na ruhusa ya kukimbiza mtu usiku ule na hata radio yake ya upepo ilikuwa haijapata uhai,hivyo ilimaanisha kazi alioifanya haikuwa na baraka zote kutoka kwa mkubwa wao.

Akagairi kuendelea mbele,

Ni wakati mlinzi yule akigeuka ili arudi alikotoka,hapo ndipo akakutana na kivuli cha mtu kikiwa kimesimama bila kutikisika.

Wakati mlinzi yule akiwa anajiandaa kushambulia,hakujua hata kimetokea nini akajikuta anaelekea kuanguka,lakini hakufika chini mkono wake wa kushoto ulikuwa umejaa kwenye mkono imara wa kivuli kile.

Mlinzi yule akavutwa kwa kasi kurudi juu na bila kutarajia akajikuta akipewa kichwa cha uso hadi akaona nyotanyota kisha likafuatia swali ambalo hakulitarajia kutoka kwa kivuli kile .

“Nioneshe njia ya kutokea katikati ya pori hili”

Mlinzi yule akawa hana cha kubisha akamweleza kinaga ubaga ya kuwa,eneo walilopo kilomita mbili mbele kuna ukuta mrefu sana,na hakuna aliewahi kuuvuka na huko pia kuna askari wengi sana.

Zedi akapagawa kuyasikia yale kutoka kwa mlinzi yule,akayarudisha macho yake kwa mlinzi yule na hapo masikio yake yakapata kusikia habari njema kidogo kutoka kwa mtu yule aliekuwa anaongea kiswahili na kiingereza kwa lafudhi ya kikenya.

Mtu yule alimwambia kuwa,njia pekee ni kupita kwenye mkondo wa maji machafu,mkondo ambao unapeleka maji yake kwenye mto Sariza,na chemba ya kupita ni moja na ipo hatua mia kutoka walipo.

Zedi ni mwanaintelejensia aliebobea,akayapima maelezo ya mtu yule na hapo akagundua jambo,mtu yule alisema ukweli,lakini kuna kitu zaidi kwenye macho ya mtu yule,alionekana kuutapika ukweli makusudi ili amwokoe Zedi,lakini kwanini atake kumsaidia,likabaki swali kichwani kwa Zedi na hakutaka kulipata,akasimama na kumwachia mtu yule kisha akaanza kupiga hatua kufuata uelekeo alioelekezwa.

Hakupiga hatua nne,akasikia mtu yule akimpa tahadhari
 
tuendelee

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…