RIWAYA : MKONO WA CHUMA.
MTUNZI : ALEX KILEO.
SEHEMU YA THELATHINI NA TATU.
_______________
ENDELEA........
________________
Ila Tom hakukubali kushindwa kirahisi, akainua chuma tena na kulenga kichwa cha Ray Charles, ila shabaha yake haikuwa makini, akajikuta anapiga bega la kulia la Ray Charles, na mlio mkali wa vyuma kugongana ukasikika. Tom bado alitaka kujaribu tena, akainua chuma na kuishusha kwa nguvu katika kichwa cha Ray Charles, ila kabla haijafikia kichwa cha Ray Charles, Ray Charles alidaka lile bomba la chuma, kisha akalitupa chini, akakamata shingo ya Tom na kumkaba, kisha akamnyanyua juu, Tom akaanza kutapatapa huku akikosa pumzi, Ray Charles akamtupa Tom chini, Tom akaanza kupapalika huku amejishika shingo,
"wewe ni nani na kwanini unayafanya haya?" Ray Charles aliuliza huku akimtazama Tom aliyekuwa anakohoa. Ray Charles akainama na kuishika tena shingo ya Tom, akamuinua juu na kumpigiza katika meza ya mbao iliyokuwepo hapo, mpaka meza ikavunjika, kile kishindo cha meza kavunjika, kikamshtua mpenzi wake Tom aliyekuwa amelala muda wote, mpenzi wake Tom alipokurupuka usingizini tu, akakutana na Ray Charles aliyekuwa anamtazama pia, mpenzi wa Tom alipotuma macho pembeni chini, akamuona Tom akiwa anaugulia maumivu huku akilia, mpenzi wake Tom akapiga kelele ila haikusaidia kitu usiku ule, maana Ray Charles alimvuta mguu na kufanya mpenzi wa Tom aanguke chini ya kitanda, kisha Ray Charles akamgonga kidogo tu kwenye mshipa chini ya kidevu, mpenzi wa Tom akalegea na kupoteza fahamu, kisha Ray Charles akamgeukia Tom,
"sipendi kuua, ila unanilazimisha kufanya hivyo" Ray Charles aliongea huku akimtazama Tom ambaye alichanganyikiwa, alijua mpenzi wake amekufa,
"sijajua kwanini umenivamia kwangu na kuniletea fujo?" Tom aliongea huku akilia,
"ile video umeipata wapi, na kwanini uisambaze? Hujui unanichafua mimi? au na wewe ni mshirika wa yule mwanamke muuaji? Maana wewe ulikuwa chini ya Minja ambaye anashirikiana na yule mwanamke muuaji. Unataka nini kutoka kwangu?" Ray Charles aliongea huku akimtazama Tom kwa hasira,
"ni kweli nimerusha hiyo video, nilikuwa nataka nionane na wewe, maana sikuwa na njia nyingine ya kukutafuta" You aliongea huku akiwa bado yupo chini.
"uonane na mimi?" Ray Charles aliuliza huku akitabasamu,
"ndio" Tom aliinuka huku akiwa anajishika shingo kwa maumivu,
"unanitafutia nini?! " Ray Charles aliuliza,
"nataka nikuambie kuwa yule mwanamke hauwezi kumkamata, ukiondoa akili tu, ana nguvu sana, ni bora mngeachana nae tu" Tom aliongea huku akimpiga piga kifuani Ray Charles, ila Tom hakuwa anampiga tu, alikuwa akimchunguza huyu ni mtu wa aina gani, maana alimpiga na chuma mara mbili ila ukasikika mlio kama amepiga chuma vile, sasa hapo Tom alikuwa akimchunguza huyu mtu kavaa nguo za chuma vipi?
"wewe ni nani kwake?" Ray Charles aliuliza huku akimkamata tena shingo Tom,
"sikiliza bro, mimi nina mengi sana ya kuongea na wewe" Tom aliongea huku akijaribu kujinasua mkononi mwa Ray Charles,
"una mengi ya kuongea na mimi?" Ray Charles aliuliza huku akimsogeza jirani Tom,
"ndio" Tom alijibu,
"sawa, twende tukaongee" Ray Charles aliongea,.
"wapi?" Tom aliuliza,
"kuzimu" Ray Charles alijibu na kumpiga ngumi kali ya kichwa Tom, Tom akalegeza shingo na macho yakapoteza nuru.
*************
Mkuu wa polisi alizidi kuwa na hali mbaya mara baada ya kupata taarifa kuwa yule mwanamke muuaji ametoroshwa hospital,
"ila niliambiwa niwaondoe Askari wote pale hospital" Mkuu wa polisi aliongea peke yake huku akizunguka zunguka ndani ya ofisi yake.
"au ni Rais anahusika? Ila hapana, shetani nipitie mbali" Mkuu wa polisi aliongea na kutikisa kichwa,
"utata kila siku" Mkuu wa polisi aliongea na kuinuka katika kiti, akakwapua kofia yake mezani na kutoka nje, alienda moja kwa moja katika gari yake, dereva alikuwa ndani ya gari,
"ebu nipeleke katika ile hospitali tuliyoenda jana" Mkuu wa polisi aliongea na kisha Dereva akawasha gari na kuiondoa kwa mwendo wa wastani.
Iliwachukua muda mfupi tu, wakaweza kufika katika ile hospital, mkuu wa polisi akatelemka kwa mwendo wa haraka na kuingia ndani ya jengo lile la hospital, akaelekea moja kwa moja upande wa uongozi wa ile hospital.
Alifika katika ofisi ya mkuu wa hospital, na kukaribishwa, kiongozi huyo wa hospital hakuwa na furaha, alionesha ana huzuni, wakasalimiana na mkuu wa polisi, kisha mkuu wa polisi akakaribishwa kwenye kiti, akaketi,
"kwanza poleni kwa kilichotokea usiku wa kuamkia leo" Mkuu wa polisi alianza namna hiyo.
"ni ngumu kupoa, kwanza ni fedhea kwa hospital yetu, hii habari imeshaanza kuvuja, na watu wataogopa Kuleta wagonjwa wao humu, tunaonekana hatuna ulinzi imara" Kiongozi wa hospital aliongea kwa jazba,
"imeanza kuvujaje?" Mkuu wa polisi aliongea na kushangaa kusikia hizo habari zimevuja,
"Kuna video inasambaa inamuonesha kijana mmoja akipambana na yule dada muuaji" Kiongozi wa hospital alijibu,
"walikuwa wakipambania wapi?" Mkuu wa polisi aliuliza, maana ilikuwa habari mpya kwake,
"wodini, yaani katika ile wodi aliyolazwa yule mwanamke muuaji" kiongozi wa hospital alijibu,
"una hiyo video hapo?! " Mkuu wa polisi aliuliza,
"ipo kule security room" Kiongozi wa hospital alijibu,
"ni jambo jema, hiyo imeturahisishia polisi ili tujue pa kuanzia" Mkuu wa polisi aliongea huku akionekana amepata nguvu kidogo,
"Sasa lakini hizo video hazitakiwi zioneshwe kwa watu wala kusambazwa, hii ni amri kutoka juu" Kiongozi wa hospital alizungumza,
"juu wapi?" Mkuu wa polisi aliuliza,
"sisi ndio tumeambiwa hivyo, hatukuwa na mamlaka ya kuhoji" Kiongozi wa hospital aliongea,
"sawa, je naweza kwenda kuziona video za tukio?" Mkuu wa polisi aliuliza,
"hakika, hilo linawezekana" Kiongozi wa hospital aliongea,
"basi twende huko security room ili nione hiyo video" Mkuu wa polisi aliongea kisha kiongozi wa hospitali akainuka na wakatoka nje, safari ya kwenda katika chumba cha ulinzi ikaanza, walitumia dakika mbili tu na kufika nje ya chumba kile, kiongozi wa hospitali akagonga hodi, mlango ukafunguliwa,
"Karibu mkuu" Kijana mmoja alimkaribisha kiongozi wa hospitali,
"nimekuja na mkuu wa polisi hapa, anataka kuona video za yule jamaa aliyeingia na kutaka kumuua yule mwanamke muuaji" Kiongozi wa hospitali aliongea huku akiingia ndani, nyuma yake alikuwepo mkuu wa polisi,
"sawa, video zipo" Kijana yule alijibu huku akizitafuta katika computer mojawapo kati ya nyingi zilizokuwepo katika chumba hicho,
"yah, hii hapa" Kijana aliongea alipoipata ile video, kisha akairuhusu icheze, yale matukio ya Ray Charles kuingia wodini kwa BQ yakaanza kuonekana vizuri, mkuu wa polisi akawa yupo makini kufuatilia kila tukio, aliangalia mwanzo mpaka mwisho wa yale matukio,.
"ebu ikuze picha ya huyo jamaa mvamizi" Mkuu wa polisi alimwambia yule kijana, kisha kijana akafanya kama alivyoagizwa, akaikuza sura ya Ray Charles na kuiweka katika kioo cha computer, mkuu wa polisi akashtuka,
"Ray Charles? Haiwezekani hii" Mkuu wa polisi aliongea na kufanya kiongozi wa hospitali na yule kijana mwingine wamtolee macho
"kumbe unamjua?" Kiongozi wa hospital aliuliza, lakini mkuu wa polisi akawa ametoa macho kuangalia tu picha,
"ni nani aliyezuia video isisambazwe?" Mkuu wa polisi aliuliza tena,
"kamanda, nilishakwambia nimepokea maelekezo kutoka juu, hii video haitakiwi kusambazwa wala kurushiwa mtu yeyote" Kiongozi wa hospitali aliongea kwa msisitizo,
"hii kitu inaniongezea utata, inawezekana aliyekupa hayo maelekezo, alifanya hivyo baada ya kuiona hii video na kumuona huyu mtu hapa" Mkuu wa polisi aliongea huku akitazama picha ya Ray Charles,
"hapana, maelekezo yalikuja mapema sana, wakati ndio kwanza tunafika hapa asubuhi ndio tuligundua wodi aliyolazwa yule mwanamke kuwa hakuna mtu na dirisha lilikuwa limevunjwa, kwa haraka haraka tukadhani ametoroka, ikabidi tuje huku upande wa camera, na hapo ndipo tukaona kila kitu, tukatoa taarifa wizara ya afya na kwa polisi, lakini akaja hapa waziri mpya wa katiba sheria, na kuzuia hiyo video isisambazwe kwanza, mpaka hapo baadae tutapotakiwa kufanya hivyo" kiongozi wa hospitali alieleza kwa urefu,
"sawa, ebu niwekeeni hiyo video katika simu yangu, nataka nikafanye uchunguzi wangu kumuhusu huyu mtu, na wala sio kufanya uchunguzi wa hili tukio" Mkuu wa polisi aliongea na kumpa simu yule kijana wa chumba cha ulinzi, kijana akaipokea na kuendelea kuishika huku akimtazama kiongozi wa hospitali,
"muwekee" Kiongozi wa hospitali aliongea kisha yule kijana akachukua waya na kupachika katika simu ya mkuu wa polisi, kisha akamuwekea ile video na kumrudishia simu yake,
"asanteni, ila kama nitagundua chochote pia kuhusu hii ishu, nitakuja kukupa taharifa" Mkuu wa polisi alimwambia kiongozi wa hospitali,
"haina shida kamanda, ila hujaniambia huyu mtu ni nani?" Kiongozi wa hospitali aliuliza,
"anaitwa Ray Charles, ngoja kwanza, nipe muda nimfuatilie alafu nikipata ukweli, nitakuja kukutaarifu" Mkuu wa polisi aliongea,
"sawa kamanda" Kiongozi wa hospitali aliongea,
"sawa, niwashukuru kwa ushirikiano wenu, asanteni sana. Naomba niondoke nikashughulikie hili jambo" Mkuu wa polisi aliongea na kupeana mikono, kisha mkuu wa polisi akatoka nje huku akishangaa kuona kuwa aliyefanya tukio lile ni Ray Charles,
"minja alishawahi kuniambia, ila sikumuamini, yaani Ray Charles yupo hai? Hii ni ngumu kueleweka" Mkuu wa polisi aliongea huku akiingia katika gari,
"Mkuu umeniongelesha?" Dereva wake aliuliza baada ya kusikia mkuu wake akiongea,
"hii dunia iache tu kama ilivyo, yaani ina mambo tata sana" Mkuu wa polisi aliongea huku akitoa tabasamu la mshangao,
"kama mambo yapi mkuu?" Dereva aliuliza,
"endesha gari bwana, acha mahojiano" Mkuu wa polisi aliongea kwa ukali na kufanya Dereva awe mpole, dereva akaondoa gari
***************
Hali ya BQ ilikuwa bado mbaya, siku ilishakatika bila fahamu kumrudia. Aliingia Rais katika chumba alichofungiwa BQ, Rais aliambatana na Ray Charles, Dizonga na vijana wengine watatu. Rais alifika na kumtazama BQ aliyekuwa ametulia tuli,
"hajapata chakula tangu amekuja hapa, si anaweza kufa huyu?" Rais aliuliza huku akimtazama Ray Charles,
"ni hatari, kweli anaweza kufa" Dizonga alijibu,
"tunafanyaje sasa?" Rais aliuliza,
"lakini mkuu si ulisema huyu anatakiwa kufa" Dizonga aliongea,
"hapana, bado muda wake wa kufa haujafika" Ray Charles alijibu,
"Sasa kama hatakiwi kufa, tunafanyaje ili tumuepushe na kifo, maana na siku ya leo ikipita, anaweza kufa huyu" Dizonga aliongea,
"tunafanyaje Ray, hatakiwi afe huyu?" Rais aliuliza huku akimuangalia Ray Charles, ambaye hakuwa na jibu muda huo,
"hatuwezi kupata daktari na kumeleta hapa kwa ajili ya matibabu ya huyu?" Dizonga aliuliza,
"hiyo haiwezekani, nafikiri madaktari wa hapa nchini wameshindwa kupata suluhisho la ugonjwa wa huyu dada, labda tuite madaktari wa nje" Rais aliongea,
"lakini mkuu Kuna haja ya kumletea madaktari kutoka nje wakati huyu hana umuhimu?" Kijana mmoja aliuliza,
"hana umuhimu? huyu ana mikataba muhimu sana, natakiwa kuipata ndipo na yeye afe, sasa unasemaje hana umuhimu?" Rais aliuliza huku akitabasamu,
"Sasa tunafanyaje ili kumuepusha na kifo? maana tangu amefika hapa hatujampatia chakula, na hatuna uwezo wa kumlisha kwa kuwa hatuna ujuzi wa kufanya hivyo" Dizonga aliongea,
"kwa hiyo huyu anakufa?" Rais aliuliza huku akimtazama Dizonga,
"tusipofanya hivyo, atakufa tu kwa njaa" Dizonga aliongea,
"na akifa bila kupigwa itakuwa aibu kwangu" Rais aliongea bila kuelezea kauli yake, vijana wake wakabaki Wanashanga,
"Sasa basi, vijana tokeni nje wote na mniache mimi na Ray Charles" Rais aliongea na kufanya vijana wote waende nje huku wakijiuliza kuna kitu gani Rais anataka kufanya.
Ndani alibaki Rais na Ray Charles, Rais akamtupia jicho BQ,
"Ray hauna njia yoyote ya kumsaidia huyu binti aamke?" Rais alimuuliza Ray Charles,
"bado sijapata njia mkuu" Ray Charles alijibu na kisha ukimya ukatawala mule ndani, baada ya dakika tano, Rais akamtazama Ray Charles,
"Ray" Rais aliita,
"naam" Ray Charles aliitika,
"muuwe huyu binti sasa hivi" Rais aliongea huku akielekea nje,
"lakini mkuu.." Ray Charles alitaka kuongea,
"hakuna cha lakini, fuata amri niliyokupa" Rais huku akipotea mlangoni, ndani akabaki Ray Charles akimuangalia BQ aliyekuwa amelala chini.
Ray Charles akamsogelea BQ na kumbeba, kisha akamtupa chini kwa nguvu, alafu Ray Charles akaondoa gloves mikononi, akabaki na mikono ya michuma mitupu, alishaamua kumpiga tu BQ ngumi za kichwa ili ammalize tu......
***********ITAENDELEA************
the Legend☆