Hassan Mboneche
Member
- Jun 15, 2020
- 61
- 197
RIWAYA: MKOLONI MZAWA—2
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
SEHEMU YA 01.
Hali ilibadilika!
Waraka wa ushauri wa utafiti uliofanywa na Jackson ulipelekea raia wengi waishi kwa shida. Hasa walioshupalia kuona unatekelezwa na serikali.
Watu wengi, na kwa muda mfupi walijikuta wapo magerezani. Kwa sababu tu, wamemshauri na kumkosoa Rais kwa kushindwa kuufanyia kazi. Watekelezaji wa mateso hayo walikuwa chini ya Rais Sharabu. Kutoka idara mbalimbali za ki-ulinzi na usalama. Pasi na kusahau vijana kadhaa wa chama tawala, Chautu. Vijana waliojifanya wamekunywa maji ya bendera ya chama!
Kwa ujumla; Rais Sharabu hakuwa yule aliyeanza miaka ya nyuma ya utawala wake. Wa sasa alijaa ukatili; usiotambua haki na uhuru wa binadamu. Hasa baada ya vijana wake aliowakaimisha mamlaka kuuwawa, na kuona anafundishwa kazi. Hakutaka hilo!
Aliamini akifanyacho ndicho pekee kilichotimilika. Katu hakuhitaji kushauriwa, namna gani anapaswa kuongoza nchi.
Udhihirishaji wa hilo ulijitokeza pale mmoja wa wanachama wa chama tawala; mwanasiasa mkongwe kwenye ulingo wa siasa, toka enzi ya awamu ya kwanza. Mwanadiplomasia, na mwanausalama aliyehudumu kwa muda mrefu, Ndalama Machicho kufukuzwa uanachama. Alifukuzwa kwa sababu ya kushabikia ule ushauri wa utafiti, lakini msoma ripoti ya kufukuzwa kwake, alitaja sababu ya utovu wa nidhamu ndiyo chanzo cha kufukuzwa.
Hakuishia kufukuzwa. Alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi pia. Kesi iliyoendeshwa haraka na kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi au kulipa faini ya shilingi bilioni moja. Alitajiwa kiwango kikubwa, wakiamini hatoweza kujikomboa. Jambo lililowainua wanaharakati kuanzisha kampeni ya kumchangia afanikishe kupata kipato hicho kwa haraka.
***
“Lengo langu kumpoteza huyu jamaa kwenye ulingo wa kisiasa,” Rais Sharabu alitoa dukuduku lake akiwa na wageni wawili nyumbani kwake; mmoja wa kiume, mwingine wa kike.
“Ni sahihi mheshimiwa Rais. Maana ana kila dalili za kuwa tishio kwa upande wako,” yule wa kiume alichangia. M-baba; mwenye umbo la miraba minne, mrefu, rangi iliyopamba ngozi ikiwa ni nyeusi.
“Na ufanikishaji wa hili lazima uwateke wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama. Sio hao tu, wakuu wa baadhi ya taasisi za ki-serikali na zile zisizo za ki-serikali. Hii itasaidia mpango kwenda pasi na kizuizi,” yule mwanamke alichangia hoja. M-mama wa makamo; akadiriaye miaka arobaini na nne. Mnene wastani, mweupe.
“Ushauri wenu ni mzuri. Na nawaahidi kuutekeleza. Lakini kuna kizuizi.”
“Kipi?”
“Wale vijidudu-mtu waliofanya mauaji ya vijana niliowakaimisha mamlaka. Bado wananiumiza kichwa.”
“Kwa namna ipi?”
Pindi wanafanya mazungumzo haya kila mmoja pembeni yake kulikuwa na bilauri lililo na maji. Pasi na kusahau sahani ndogo iliyo na korosho. Walivitumia vitu hivi walipoingiwa na hamu. Yaani walivitumia kwa nadra sana.
“Bado wapo hai. Hiyo si salama kwangu. Ukizingatia ndiyo wenye vyanzo vyote vya ile ripoti.”
“Kwa hiyo unatakaje?”
“Nahitaji wauwawe. Usije kuta wanazalisha kila kukicha hizi nyaraka, halafu tunapata tabu huku ya kukimbizana na vidagaa. Inabidi wauwawe huko huko walipo, ili wa huku wakose sehemu ya kupata hizo nyaraka.”
“Ushauri mzuri. Naahidi kuufanyia kazi. Niachie hilo jukumu,” yule m-baba alisema. Afahamikaye kwa jina la Killa Lauma.
“Nakupa ruksa fanya. Ili mwisho tumzime huyu jamaa mazima. Asisikike, wala kuonwa na sura ya mwanatuleane yeyote zaidi ya familia yake.”
Yule mwanamke alikazia, “Ni jambo dogo hilo.”
***
MEXICO CITY
Baada ya kutoroka nchini Tuleane, katika mtawanyo wa kujigawa, Jackson alielekea jijini Mexico. Makazi yakawa hotelini. Ifahamikayo Los Cabos Corridor. Hapa ndipo yalikuwa maficho yake. Kwa uwezeshi wa kiuchumi wa Kamishna wa intellijensia dhidi ya tuhuma za mauaji ya viongozi yaliyofanywa na kina Luteni Mwaipeta.
Huku hakukosa amani. Kwani muda mwingi alikuwa mwenye furaha tele-kwa kujichanganya katika makundi ya watu mbalimbali, waliojihusisha na utoaji wa burudani zenye kukonga nyoyo. Burudani kemkem, alizokosa kuzishuhudia pindi awapo Tuleane.
Burudani hizo zilikuwa zinafanyika hatua chache tu, toka lilipo jengo la hoteli. Katika uwanda wa fukwe ya bahari ya Pacific.
Utamu wa burudani ukamkutanisha na mzee-kijana afahamikaye kwa jina la Kinyonga. Sharif Kinyonga! Wakajikuta wanatengeneza urafiki ulioshinikizwa na rangi ya ngozi zao. Nyeusi! Walivyodadisiana kwa kina, wakapata kufahamiana fika, ni watu wa taifa moja. Tuleane!
“Mimi ni mwenyeji wa Butu,” Kinyonga alisema. Wakiwa wameketi kando kidogo na fukwe ya bahari wakizikosha mboni na roho, kwa michezo ya watu waliopo baharini.
Pembeni, mwa kila mmoja kulikuwa na bilauri zilizojaa kinywaji. Ambacho walikitumia mara chache sana waonapo koo limekauka-hivyo linahitaji kilainishi.
“Nimeshawahi kupasikia. Ni Nyoli hiyo?” Jackson alichombeza.
“Zamani. Kwa sasa ni Mali.”
“Una muda gani huku?” Jackson aliuliza.
“Miaka mingi sana...” Kinyonga alisema na kutulia kwa sekunde chache. Akazihamisha mboni zake kutoka baharini na kumtathmini Jackson kwa nukta chache kisha aliendelea, “...na nimeshakuwa maarufu. Mitaa mingi ukiniulizia Black Nigga hawakosi kukufikisha kwenye makazi yangu.”
“Unafanya shughuli gani? Ya madawa?”
“Mbona umekimbilia madawa? Biashara zipo nyingi mdogo wangu.”
“Hiyo ndiyo maarufu kwa huku. Usije ukawa unawapelekea ndugu zetu madawa ya kulevya kule nchini.”
“Hapana. Sijihusishi na hizo mambo. Biashara yangu...”
Jackson akamkatisha, “Bora hata tumefahamiana. Nina imani unaweza hata kunishika mkono, maana nimekaa hapa naona natumia pesa tu, pasi na hata kuingiza. Kama kuna nafasi ya uhitaji wa mtu wa kukusaidia, mimi nipo.”
“Ondoa shaka. Nitakusaidia katika hilo.”
***
Hatimaye wakawa marafiki wa kushibana kwa muda mchache waliofahamiana. Jackson akapatiwa nafasi ya kumsaidia Kinyonga kwenye biashara zake. Biashara ya uuzaji wa vitu vya mtumba. Kama vile; nguo, majokofu, na vyombo vya ndani. Walikuwa wanavisafirisha kutoka Mexico kupeleka Tuleane. Kwenye miji ambayo Kinyonga alifungua matawi ya biashara yake.
Hakika walitokea kuaminiana. Kiasi kwamba Jackson alifanya mambo ya Kinyonga hata kama mwenyewe hayupo. Hususani safari za kibiashara. Alisafiri miji mbalimbali kufuata mizigo.
Hakuna aliyetokea kuwa na shaka na mwenzie. Japo chembe.
Miezi sita ya urafiki wao, wakabahatika kufunga safari ya mbali pamoja. Safari ya kuelekea jijini London nchini Uingereza. Iliyoratibiwa na Kinyonga kama ilivyo ada.
“Tukifanikiwa kuupata huo mzigo tunaoufuta, inabidi uende nao nchini,” Kinyonga alisema wakiwa ndani ya ndege.
Jackson akashtuka. Lakini hakuonyesha mshituko wake kwa uwazi.
“Nchini! Narudije?” alijiuliza akiwa mwingi wa hamaniko. Lililosafirisha sehemu yake ya ufahamu akumbuke matukio yaliyotokea kipindi cha nyuma kabla hajawasili Mexico.
“Ni jambo lisilowezekana. Siwezi kurudi nchini, hata kama uhitaji wake niwepo kwa dakika moja tu,” Jackson aliendelea kujisemeza. Awamu hii akijigeuza kidogo kwa lengo la kumwangalia Kinyonga. Na kumtathminisha anafananaje na ile kauli aliyoizungumza.
Cha kushangaza! Toka Kinyonga atamke ile kauli, alizihamishia mboni zake wajihini kwa Jackson. Akawa anamsaili, kapokeaje kauli yake?
Wakatazamana. Kwa mboni zilizojaa udadisi wa kila mmoja.
“Vipi, haupo radhi kwenda?” Kinyonga aliuliza.
Jackson akazidi kuingiwa na wasiwasi. Kwani hakuweza kujibu lile swali kwa haraka.
“Yanipasa kuwa active shooter. La sivyo nitampatia huyu jamaa nafasi ya kutaka kunichimbua undani wangu,” Jackson alijisemeza.
“Hapana. Nipo tayari.” Akajigeuza kutazama upande mwingine kwa ukakamavu.
Walivyowasili, baada ya kuteremka ndani ya ndege hawakutumia muda mrefu mahali hapo. Walivyokamilisha tu taratibu za kiusalama, walichanja mbuga kuelekea eneo la mapokezi. Ambapo wageni hupokelewa na wenyeji wao.
Wakati huo Kinyonga alikuwa mbele ya Jackson. Akipiga hatua za nguvu zilizoonyesha uhitaji wa kuwahi na kuondoka haraka eneo hilo. Walivyoliacha lango tayari kwa kuwafikia wapokezi, simu ya Jackson iliita. Ikamfanya apunguze mwendo na kuuongoza moja ya mkono wake kule alipoihifadhi.
Ujumbe wa barue pepe.
Alikutana na ujumbe kwenye akaunti yake ya barua pepe.
“Umaniki unahitajika. Kuwa makini, huku pameshachafuka,” ndivyo ulisomeka ujumbe huo.
Akapoa ghalfa. Na kujikuta akisimama mboni kamwangazia Kinyonga kwa jicho kali la udadisi. Alivyojumlisha na yale maswali aliyoulizwa ndani ya ndege, akazidi kuingiwa wasiwasi juu yake.
Alianza kumhisi si mtu mzuri kwa upande wake.
Kinyonga; mwanaume aliyebarikiwa urefu, mwili ulioshiba shiba kwa mazoezi, na rangi angavu iwakilishayo bara la Afrika, alikuwa bize na mwendo. Alikuja kumkumbuka Jackson alipomuona mpokezi wao. Akageuka nyuma ili ampashe uelekeo wanaopaswa kwenda. Butwaa likamuiva!
Alikumbana na sura za watu wengine si ile aliyoitaraji. Hakumuona Jackson.
“Shiit!” alimaka. Wakati huo akiangaza huku na kule lakini hakufanikiwa kumtia mbonini.
“Inawezekanaje?” aliendelea kujisemeza. Awamu hii alikwisha jikatia tamaa. Hivyo ikamlazimu kuendelea na safari. Sonona likimtukuta nafsini.
Alivyokutana na mpokezi, walilakiana kisha waliongoza eneo la maegesho. Ambapo gari ya kuwatoa mahali hapo iliegeshwa. Walipoifikia hawakukawia, waliingia ndani ya gari kisha safari ikaanza.
“Mbona upo peke yako?” mpokezi, ambaye ndiye aliketi kwenye kiti cha usukani aliuliza.
Kinyonga alianza kwa kusonya. Kisha alitokwa na kauli, “Nimekuja naye. Lakini sijajua kanitorokaje torokaje pale ndani.”
“Hajabakia mule mule ndani kweli?”
“Sina hakika.”
“Sasa tutaeleza nini kwa bosi?”
Kinyonga hakujibu. Aliishia kusonya, huku akiangaza kiudadisi mazingira wayapitayo.
“Simama kwanza. Rudi nyuma kidogo,” Kinyonga aliongea.
“Kuna nini?”
“Kuna mtu nimemuona kwenye ule uchochoro nahisi ni yeye.”
Dereva alitii.
Walipoufikia usawa wa uchochoro husika, Kinyonga aliteremka na kupiga hatua za mbio kuelekea alipomuona huyo mtu. Afananaye na Jackson.
Hakukosea. Alikuwa Jackson kama alivyobashiri. Kwani baada ya kumtoroka pale uwanjani alikuwa anafuatilia gari waliyopanda kina Kinyonga ki-mabavu.
Alivyomuona Kinyonga yupo mbio kuja alipo akajificha sehemu na kumtazamia kwa jicho la ulengaji shabaha. Wakati huo mapigo ya moyo yakimwenda kasi kwa hofu ya kufumaniwa.
“Lakini, kwa nini nimkimbie?” alijiuliza.
Ukawa mwanzo wa ukinzani nafsini mwake. Upande mmoja ulimuambia aendelee kuongozana naye. Upande mwingine ulimpa shinikizo la kutoongozana. Ulimuaminisha akimrudia, anaenda kufuata kifo chake. Akabaki njia panda!
ITAENDELEA...
HABARI NJEMA.
KITABU CHA RIWAYA YA NENDA KIPO SOKONI KWA BEI YA TSH. 10,000/=
WASILIANA NAMI KWA 0693097151 UJIPATIE NAKALA YAKO.