Sehemu ya pili
Kwa Mary Robert.2010
Unaweza kuwa si wa kwanza kwake, wala wa
mwisho kwake, Aliwahi kupenda kabla na anaweza
kupenda tena. Lakini kama anakupenda wewe,
unajali nini tena? Yeye si mkamilifu, na wewe pia
si mkamilifu, na wote wawili hamuwezi kuwa
wakamilifu pamoja, lakini kama anaweza
kukufanya ucheke, anakunfanya ufikiri mara mbili
na anakiri kuwa yeye ni binadamu a anatenda
makosa basi mshikilie yeye na mpe kwa kadiri
uwezavyo. Anaweza kuwa hakufikirii kila sekunde
katika siku, lakini atakupa sehemu ya utu na mwili
wake anayojua utaivunja YANI MOYO WAKE.
Usimbadilishe, usimchambue, usitegemee makubwa
zaidi ya yale awezayo kukupa au yale anayomudu.
Tabasamu pale akufurahishapo, muambie pale
anapokukasirisha, ana ummis pale anapokuwa
hayupo. HAPO UTAKUWA NA FURAHA YA MAPENZI
NA WASIWASI WA MAPENZI UTAONDOKA HII NI SEHEMU YA PILI.
Ile CD yenye ile simulizi iliendelea kusikika redioni na usingizi ulikatika kabisa, nilikuwa najiuliza huyu
Mary ndiyo nani na kafanya nini. Baada ya matangazo machache yule mtangazaji wa redio alirudi hewani na kusema kuwa sasa wataweka sehemu ya pili ambayo ni mahojiano kati ya Pamela na Mtangazaji. Nilijiweka tayari kusikiliza
na kwenye ile CD ilisikika sauti ya mtangazaji ikimwambia Pamela aeleze kila kitu alichotaka kukisimulia pale.
**PAMELA**
Patrick alikuwa ameanza kurudisha fahamu kitu ambacho nilikuwa nikikiota siku nyingi, ingawaje kitaaluma nilikuwa daktari tena mtaalamu wa
magonjwa ya akili na ubongo na taaluma yangu hainiruhusu kukata tamaa ya kumuhudumia mgonjwa ambaye bado anapumua vizuri ila kwa Patrick ilikuwa tofauti, kuna muda nilikuwa nakata
tamaa kabisa, alipotelekezwa pale hospitali niliamua kujibebesha mzigo mzima wa jukumu la kusimamia matibabu yake japo nilipata msaada mkubwa sana toka kwa dokta Anderson na mkewe Sara.
Historia ya maisha yangu kipindi cha nyuma ilinifanya kuwa mtu mkatili sana lakini sikuwa hivyo kwa Patrick. Yeye ndiye aliyeanza kunionyesha tumaini jipya lililopotea siku nyingi na
kunifanya nianze kuwa mtu wa tofauti kabisa katika maisha yangu.Nilizaliwa na kuwa yatima miaka mingi sana
iliyopita, nilikulia kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha masista na huko tulifundishwa tabia njema na namna ya kuishi na kila mtu, nilipofika
kidato cha nne nilianza kujihusisha na mapenzi,sikuwa na akili vizuri, nikajiingiza kwenye mapenzi na kijana Alex ambaye na yeye alikuwa ni yatima
pia ila mara nyingi tulikuwa tukionana pale walipokuwa wanakuja kusali kanisani. Nilimpenda sana Alex na niliamini kuwa alikuwa akinipenda
pia, nikiwa kidato cha tano nilipata ujauzito na sikujua cha kufanya,nilifukuzwa pale kituoni na
baada ya kukataa kusema nani alinipa ujauzito,nisingeweza kabisa kumtaja Alex kwakuwa ningekuwa nimemuharibia mipango yake ya kimaisha. Nilikuwa tayari kuubeba ule mzigo wa mimba kwakuwa nilimtakia mema hasa nikitegemea kabisa kuwa angekuja kuwa baba wa yule mtoto, hivyo ile mimba ilibaki kuwa ya kwangu na wala Alex hakutaka kusikia, siku moja
nilikwenda kama kawaida pale ambapo huwa tunakutana na nikamweleza kuhusu ujauzito ule na aliukana kabisa akasema hajawahi kuwa na mahusiano na mimi, nilimweleza kuwa nia yangu si
kumwambia yoyote kuwa yeye ndiye aliyenibebesha ujauzito ila nia yangu ni kumtaka tu ajue kuwa kuna kiumbe chake tumboni mwangu, alikuwa
mkali sana na kuniona kama nilikuwa Malaya,siku hiyo alinipiga sana na kunisababishia maumivu makali,niliondoka na kurudi kwenye magofu yanyumba za watu nilikokuwa nikilala na mchana nilikuwa nikila mabaki ya vyakula vya wahindi. Kila
mtu aliniona kama mimi ni Malaya lakini
sikujilaumu kwakuwa nilitambua athari za nilichokuwa nafanya na Alex ila niliamua kufanya kwakuwa nampenda.
Siku tatu mbele nilianza kupata maumivu makali sana ya tumbo na baadaye nilianza kutokwa na damu mabongemabonge, sikuwa na wakumlilia
zaidi ya kumuomba mungu anisaidie, nilitokwa na damu siku mbili mfululizo huku maumivu ya tumbo yakizidi, sikuwa na dawa ya kumeza kwakuwa sikujua ni dawa gani nimeze na hata fedha ya
kununulia dawa sikujua ningeipata wapi, nilikaa nikitafuna majani ya alovera na baada ya kutokwa damu kwa muda wa siku mbili tumbo lilitulia na sikujua madhara ya kile kilichonitokea yatakuwa
wapi ila nilichofahamu ni kuwa mimba imetoka.Katika mihangaiko yangu jijini nilikutana na msichana wa umri kama wangu kwa kipindi hicho na yeye aliniambia anakwake hivyo tukakae nae na atanifundisha biashara, nilimkubalia kwakuwa sikuwa na machaguo ya kutosha na hapo alinipeleka kwake, palikuwa na chumba kimoja tu lakini kilichojaa vitu mbalimbali vya thamani,nilikaa pale siku moja lakini nilikuwa nimeshagundua kuwa alikuwa akijiuza,kuna muda
mwanaume alikuja pale na walianza kushikana mbele yangu, nilinyanyuka na kutaka kutoka lakini yule dada alinikataza na kuniambia kuwa ile ndiyo
biashara na natakiwa nijifunze, nilijizuia sana na kutaka kuondoka lakini bado maisha yale
niliyokuwa nikiishi yalikuwa ni hatari sana. Hivyo nilikubaliana na yule dada na tulianza biashara hiyo, nilifanya kwa shingo upande lakini kazi ilikuja
kunishinda pale wateja waliokuwa wakija pale walipotaka kufanya mapenzi na mimi kinyume na maumbile, nilikataa katakata na hapo yule msichana alinifukuza kwake, niliondoka na kwenda
kwenye kile kituo kuomba wanisaidie lakini walinikataa, hivyo ikabidi niingie mtaani tena,nilikutana na mzee mmoja akaniahidi atanipatia kazi nyumbani kwake na mimi nilikubaliana naye na hapo nilipata kazi ya ndani kwa huyo mzee,baada ya mwezi mmoja tu wa kazi vioja vilianza baada ya watoto wake wa kiume kuanza kunitaka,nilikataa mara nyingi lakini kuna siku wakati yule baba amesafiri tukabaki na wanae watatu wa kiume tu, siku hiyo nilitoka bafuni na kuingia chumbani kwangu, nilipovua kanga na kuanza kujifuta maji nilishtuka kuona wale vijana ndani ya
chumba changu, nikajifunika na ile kanga lakini walininyanganya na wawili walinishika kwa nguvu kisha waliniingilia kwa zamu, niliumia sana
kwakuwa walitumia nguvu nyingi sana lakini nilipanga kuja kumuambia baba yao japo waliniambia wangenifanyia kitu kibaya kama ningesema kwa baba yao. Mzee wao aliporudi nilimueleza ukweli lakini hakunielewa zaidi ya
kunifokea kuwa nimeleta umalaya wangu ndani ya nyumba yake, niliamua kunyamaza kimya na kuendelea na kazi zangu, ile nyumba hakukuwa na
mwanamke kwakuwa mke wa huyo mzee alikuwa nje ya nchi kwa masomo na hata watoto wake walikuwa ni watu ambao hawakuwa wakukaa nyumbani sana.
Wiki tatu baada ya kubakwa na wale watoto,niliamka asubuhi na kujikuta chumbani kwa yule mzee, nilikuwa nimechoka na nilishangaa nilifikaje
lakini akili yangu ilikumbuka kuwa jana usiku yule mzee alileta juice na kunipa ili ninywe, nikagundua
kuwa aliniwekea kilevi kwenye ile juice na kunibeba hadi chumbani kwake. Kilichoniliza sio yeye kuniingilia kimwili bila ridhaa yangu ila ni yeye
kuniingilia kinyume na maumbile, nililia sana lakini hakuonekana kujali;
sio sawa ulivyonifanyia nilimuambia huku nikilia lakini hakunisikiliza.
binti wewe kazi yako hapa nyumbani ndiyo hiyo,yani wewe mimi nikulipe elfu 15 kwa mwezi na nikulishe na ulale kwangu kwa kazi ya kupika,
kudeki, kufua nguo za watu wote humu ndani na kufanya usafi mwingine tu?,,ni sawa hivyo kweli?Fedha yote hiyo kwa kazi ndogo tu ya kufanya
usafi aliniambia huku akicheka.
utajisikiaje kama binti yako ndo angefanyiwa hivyo nilimuuliza huku nikimtazama.
mwanangu hawezi kuwa beki tatu, tena nyamaza kabisa usianze kunihubiria hapa, kafungashe mizigo yako uondoke maana utatuwekea sumu huku ndani, fungasha nikitoka hapa uwe nje ya hii
nyumba, chukua fedha zako hizo alinisukuma na kunipa shilingi elfu 30, nililia sana lakini sikuwa na
mahali pa kwenda, nilikwenda polisi kuripoti lakini chakushangaza mwanamke mwenzangu aliyekuwa pale ambaye ni polisi alikuwa wakwanza kunifukuza na kuniita mimi Malaya, aliyeonyesha
nia ya kunisaidia alikuwa kijana mwingine askari lakini tulishindwana baada ya yeye kunitaka kimapenzi kama rushwa. Niliamua kumuachia mungu kila kitu lakini nilimchukia kila mwanaume
duniani na nilipanga kutokuja kuolewa wala kubeba ujauzito kwakuwa kama ingetokea ningezaa mtoto wa kiume nisingempenda kabisa.
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya ukimwi duniani ambapo shirika la misaada la marekani lilikuwa likifanya kampeni ya kupima kwa hiari, nilikwenda
kupima ili nijue afya yangu na hapo ndipo nilikutana na dokta Anderson, nilimueleza kila kitu kuhusu maisha yangu wakati alipokuwa akinipima,
na alisema kuwa angenisaidia kurudi shule na mpaka pale ambapo ningetaka kwenda kitaaluma.
Nilirudia kidato cha nne kwa msaada wa fedha za mzee Anderson na mkewe Sara, walikuwa nje ya nchi lakini walikuwa wakinitumia fedha vizuri na
kwa wakati, nilianza kuona matumaini ya maisha tena na baada ya kumaliza kidato cha nne nilifaulu vizuri na kuchaguliwa kwenda kidato cha tano kilakala sekondari kwa mchepuo wa PCB (fizikia,
kemia na baiolojia), kidato cha sita nilifanikiwa kufaulu kwa daraja la kwanza na hapo ndipo dokta Anderson aliponichukua na kunipeleka kusoma
nchini Australia kama daktari na baadaye shahada yangu ya pili nilisomea mambo ya magonjwa ya akili, nilifanya kazi na dokta Anderson miaka yangu
yote mpaka nilipoomba uraia wa huko na kujivua uraia wa Tanzania, sikuwa na hisia na wanaume kabisa na mwaka mmoja kabla ya kumfahamu Patrick nilikuwa kwenye mahusiano na mwanamke
mwenzangu, nilikuwa msagaji lakini yote haya ni kwakuwa hisia zangu zilihama na kwenda kwa wanawake wenzangu.
Yaliyomtokea Patrick yalinikumbusha sana yaliyotokea Tanzania na hiyo ilikuwa sababu ya mimi kujitolea kumsaidia. Kwa ufupi Patrick
alirudisha hisia zangu juu ya wanaume,
mwanaume pekee niliyekuwa nikimuona kama mungu wangu ni mzee Anderson lakini wengine wote hata madaktari wenzangu niliofanya nao kazi
walinijua kuwa sikuwa nawapenda hata kidogo,wengi walijua kuwa mimi ni msagaji na walichukia tabia yangu hiyo lakini kwangu ilikuwa ni faraja na
nilijisikia vizuri sana kuwa kwenye mapenzi na mwanamke mwenzangu, nilimpenda sana na yeye alinipenda na alinipa kila nitakacho na wala
sikuhitaji mwanaume. Lakini uwepo wa Patrick pale hospitali ulinibadilisha taratibu na hata Nancy
ambaye ndiye alikuwa mpenzi wangu alianza kulalamika kuwa nimemsahau, nilimueleza ukweli kuwa kwasasa sitaweza tena kuwa naye kwakuwa
nahisi nampenda mtu mwingine. Alilia lakini nilipomueleza kiundani alinielewa. Kwa miaka sita
yote Patrick akiwa kitandania kama mfu nilikuwa naye pembeni, kuna muda nililala pembeni naye usiku kucha, kuna wakati nilikuwa siendi kwangu
baada ya kazi na badala yake nilikuwa nikikaa pale chumbani kusubiri mda atakaofungua macho,nilitaka japo kuisikia sauti yake, sura yake nzuri na
ya kitoto ilinifanya nimpende,nilimuonea huruma
kwa alichotendewa lakini pia niliona nina nafasi yakumsaidia, miaka sita na mwezi mmoja ulipotimia siku hiyo ilikuwa asubuhi nikaona manesi
wakikimbizana huku na huko na dokta Anderson alikuwa akikimbia kuelekea chumba alichokuwa amelazwa Patrick, sikujua kilichoendelea ila
nilijikuta nikianza kulia kwakuwa nilidhani Patrick amefariki kwasababu jana yake usiku hali yake
haikuwa nzuri, sikuweza kwenda kule kwakuwa nilikuwa naingia kwenye chumba cha upasuaji hivyo nilijikaza na kuingia na jopo la madaktari
wengine, tulifanya upasuaji kwa masaa manne mfululizo, baada ya kutoka nilikutana na dokta Anderson aliyekuwa anaonekana akitabasamu;
Ameamka na yuko salama kabisa aliniambia huku akinifata na kunikumbatia, niliona kabisa
machozi yakinitoka.
Natumaini furaha yako itazidi Pamela na kazi kubwa kwasasa ni kuhakikisha Patrick anakuwa salama na hali yake inarudi kama mwanzo,naamini hiyo ndiyo kazi kubwa uliyokuwa nayo kwasasa binti yangu alinieleza hayo na mimi
nilipata faraja sana, dokta Anderson aliielewa furaha yangu na siku zote alinichukulia kama Semphroza ambaye ni binti yake aishiye marekani
na mumewe. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu kabla ya Patrick kuamka.
*******
Mary Robert nilisikia Patrick akitaja jina la yule mwanamke aliyemtelekeza, nililia kwa furaha japo
nilijua lengo langu la kuwa na Patrick lingekuwa gumu sana kama angekuwa bado anampenda Mary. Nilifanikiwa kukaa na Mary na kuongea naye miezi michache kabla ya yeye kuondoka, alikuwa
anaonekana kama msichana wa kisasa zaidi,alikuwa ni mtu wa kuongea na simu kila saa, mtu ambaye ni msiri sana na mtu anayekwenda na mda, hakuwa muongeaji sana wala hakutaka
kukaa na mtu mda mrefu, sikuweza kujua kama anampenda kweli Patrick au la japo baada ya yeye kuondoka ndiyo nilikuja kujua kuwa hakuwa mvumilivu.
Unamkumbukaje Mary Robert nilimuuliza Patrick ambaye alionekana akiwa ameduwaa huku machozi yakimtiririka.
sikumbuki, simkumbuki Mary, sielewi kitu alizidi kulia huku akitazama mbele kama alikuwa akiona kitu, nilimshika na kumkumbatia huku na mimi
machozi yakinitoka, ilionekana kama anajitahidi sana kukumbuka lakini haikumsaidia hiyo.
Tafadhali kama unajua chochote kuhusu Mary nieleze, yeye ni nani, anafanya nini kwenye maisha yangu aliniuliza huku akilia.Nilimuacha pale na kwenda kufungua kabati kisha nilitoa boksi lenye barua na pesa ambayo Mary
aliiacha kwenye mfuko pale hospitali kabla hajaondoka bila kuaga, sikuwahi kuisoma ile barua kwa miaka yote hiyo, wala sikuwahi hata siku moja
kutumia zile pesa. Nilifungua lile boksi na kutoa ile barua na yale mabunda ya pesa nikayaweka pale
kitandani kisha nilimkabidhi ile barua na yeye akaifungua, niliona machozi yakimtoka kila alipokuwa akisoma mstari mmoja wa ile barua,sikuwa najua ni nini kimeandikwa kule ndani mpaka nilipoichukua ile barua na kuanza kuisoma.
Nilitokwa na machozi na kumgeukia Patrick.Pamela ni nini kinaendelea mbona sielewi kila kitu aliniuliza huku machozi yakiwa yameufumba
uso wake, nilimuonea huruma kwakuwa nilielewa maumivu ayapatayo kwa hilo limtokealo. Ile barua ilisomeka hivi;
mpendwa mume wangu,Nakuandikia ujumbe huu kwa uchungu na masikitiko makubwa. Najua huwezi kupona tena katika maisha yako kwani daktari amenieleza kuwa
uwezekano wa wewe kurudisha kumbukumbu zako ni mdogo sana,,nilipenda kuwa na wewe Patrick na unalijua hilo lakini sikuwahi kufikiri kuwa nitakuja
kuishi na wewe katika hali hiyo uliyokuwa nayo,,honeymoon ndo chanzo cha yote, huwezi kunikumbuka hata mimi najua,,nilikupenda sana Patrick, lakini nina malengo mengi ya kuyatimiza
kabla ya kuingia kaburin hivyo sina budi kukuacha na kwenda kuendeleza maisha huko nyumbani,,nisamehe, sina jinsi ya kufanya zaidi ya
kwenda kuwaambia nyumbani kuwa tulipata ajali kwenye boti na ulipotelea baharini,,nimeacha kiasi
cha fedha cha kutosha naamini kitakusogeza,,ikiwa hutafanikiwa kuisoma barua hii na ikitokea
kuwa umepoteza maisha basi jua kuwa ninakazi kubwa ya KUMALIZIA MENGI NILIYOANZISHA NAKUPENDA,nakupenda sana ila siwezi kuendelea kuishi na wewe hapa maana itakuwa napoteza muda. MAISHA MEMA Patrick.
Mimi Mary
Ilisomeka sehemu ya barua hiyo.
ITAENDELEAAA...