Six Man
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 253
- 893
RIWAYA; BRIEFCASE
MTUNZI; HALFANI SUDY
WhatsApp 0674 395733
Sehemu Ya Kwanza
ILIKUWA ni usiku wa saa sita. Anga la jiji la Dar es salaam lilikuwa limetulia baada ya kunyesha mvua kwa saa mbili mfululizo. Mvua liliyoiacha mitaa kadhaa ya jiji la Dar es salaam ikiwa imejaa maji kutokana na ujenzi wa hovyo wa barabara bila mfumo nzuri wa mifereji.
Katika nyumba moja iliyokuwepo katika mtaa wa Mbagala maji matitu kulikuwa na mtu mmoja akiwa amelala kitandani. Kijana alikuwa anajulikana kwa jina la Alex. Mfanyabiashara wa viatu katika soko la Tandika.
Alex alikuwa amelala fofofo katika chumba kidogo cha kupanga. Ndani ya chumba chake hakukuwa na kitu chochote kile cha zaidi ya kitanda kile dhaifu. Kwa kuangalia mwonekano wa chumba chake tu ilikuwa ni taswira ikiyoonesha hali yake ya kiuchumi. Alex alikuwa ni kijana mbangaizaji pale sokoni akimiliki biashara ya viatu visivyozidi kumi.
Historia ya Alex ilianza miaka ishirini na tano iliyopita huko wilayani Mkuranga. Alizaliwa katika kijiji kidogo cha Kisemvule, kijiji kilichopo wilayani humo. Alimaliza darasa la saba shule ya msingi Kisemvule na kubahatika kuendelea na Sekondari katika Sekondari ya Ally Hassani Mwinyi iliyopo Mkuranga mjini. Kidato cha nne ndio kilikuwa kikomo cha elimu yake ya darasani. Ndipo alipoingia mtaani akiwa na miaka kumi na saba tu. Biashara yake ya kwanza ilikuwa kununua nguo za mitumba mnadani na kwenda kuziuza mitaani. Baada ya miezi kadhaa alihamia Dundani alipokuwa akiishi na wazazi wake na kuhamia Mbagala maji matitu. Mwaka mmoja baadae akiwa anaishi Mbagala alibadilisha biashara ya nguo na kuanza kuuza viatu huko sokoni Tandale.
"Aaah nani tena ananipigia usiku huu" Alex alisema kwa sauti ndogo huku akiivuta simu yake aina ya Nokia ya tochi na kuiweka sikioni.
"Haloo Ha..loo" Alex alisema kwa sauti yenye usingizi.
"Bila shaka naongea na Alex" Sauti nzito iliongea simuni.
"Ndio"
"Sikiliza ninachokwambia kisha utekeleze."
"Wewe ni nani? Naongea na nani?" Alex aliuliza kwa pupa. Usingizi ulianza kumtoka.
"Huna sababu ya kujua jina langu. Una haja ya kujua nini ninachotaka kukwambia.
Ni hivi, kesho, saa nne asubuhi unatakiwa kwenda Posta. Unatakiwa kwenda nje ya ghorofa la RITA lilipo Posta. Unatakiwa kusimama tu pale. Atakuja mtu na kukupa briefcase, na maelekezo ya wapi pa kuipeleka briefcase utaelekezwa katika simu" Sauti ya kwenye simu ilisema.
"Sikuelewi kabisa bila shaka utakuwa umekosea namba brother" Alex alisema.
"Naongea na Alex Manda. Mtoto wa kwanza wa mzee Manda wa huko Dundani, Mkuranga. Elimu yako ya msingi ulisoma Kisemvule na baadae ukajiunga shule ya Sekondari Mwinyi. Ulimaliza. Ulipata daraja la tatu lakini haukuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano . Ndipo ulipojiingiza katika biashara ya kuuza nguo, na baadaye ulianza kuuza viatu ulivyohamia Mbagala maji matitu. Hauna mke, hauna mchumba. Kwa sasa umelala kitandani kwako, umevaa bukta bluu ya Chelsea ukiwa kifua wazi. Unataka nikwambie na miaka yako?" Sauti ya kwenye simu ilimaliza kwa swali.
"Mmmmh" Alex aliguna. " Wewe ni nani lakini?" Alex aliuliza tena.
"Utanijua kesho. Fanya nilichokuagiza. Sijataka kukwambia kwamba usipotekeleza hayo hutoliona giza la kesho. Nitakuua saa kumi kamili jioni. Kama unabisha, we bisha tu"
"Kaka, inamaana..." Alex alitaka kuongea. Ndipo alipogundua alikuwa anaongea peke yake simuni. Jamaa alikuwa amekata simu.
Alex aliamka. Alikaa kitandani akiwa haelewi kabisa ni balaa gani linamkuta. Aliwaza na kuwazua.
"Huyu jamaa ni nani? Anajua kila kitu kuhusu mimi. Amejua mpaka hii bukta niliyovaa. Haya ni mambo ya ajabu sana. Eti niende posta kesho kwenye jengo gani sijui, ni nani yule? Kwanini anipe mimi maagizo hayo?" Alex alikuwa anajiuliza mwenyewe.
Mara alisikia mlio katika simu yake. Ulikuwa mlio wa meseji. Alichukua simu yake na kuisoma ile meseji.
"Saa nne kamili asubuhi, mbele ya jengo la RITA. Usimuulize chochote atakayekupa briefcase. Chukua na utapigiwa simu ya maelekezo. Kuwa makini ili ulione giza la kesho"
Hadi anamaliza kuisoma hiyo meseji mwili mzima ulikuwa umeloa jasho. Ilikuwa ni meseji fupi lakini yenye ujumbe uliomtia hofu sana.
Hivi ndivyo simulizi hii inavyoanza, tuwe wote katika sehemu ijayo..