RIWAYA: Joto La Mshumaa

bioto

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
1,261
2,095
RIWAYA: JOTO LA MSHUMAA
MTUNZI: MUDHIHILI MNALI
SIMU: 0652667153
LINDI-RUANGWA
SEHEMU YA KWANZA 01
Anza nayo...............
Ndani ya kijiji kimoja kijulikanacho kwa jina la
BWAWANI. Kwenye familia moja ambayo ilikuwa
chini ya usimamizi wa bwana Mzee MAMBO SASA,
alikuwa anishi na familia yake mkewe pamoja na
mwanawe wa kike aliyejulikana kwa jina la SIKITU.
Katika maisha ya mzee huyo alijiwekea utaratibu
ambao ulihusiana na kumuweka mwanae katika
utaratiibu na desturi za adabu na heshima, pia
aliweza kumsomesha mwanae japokuwa ndani ya
kijiji cha Bwawani hakikuwa na muamko kabisa na
swala la usomeshaji wa watoto zao. Hivyo ilikuwa
ngumu sana katika maendeleo ya elimu ndani ya
kijiji hiko. Mzee Mambo sasa siku moja aliokaa na
mwanae na kumuambi mambo muhimu sana
ambayo hayakuenda mbali na maswala ya kumjenga
kielimu zaidi.
''Mwanangu mimi baba yako naomba nikueleze
jambo ambalo lina manufaa sana katika maisha
yako ya sasa pamoja na baadae, kwanza naomba
ushike sana masomo mkwani hata wengi wetu
wanasema kuwa elimu ni ufunguo wa maisha sawa
Sikitu''
Mzee Mambo sasa aliweza kumueleza mwanae
swala hilo huku sikitu akiwa makini sana katika
kumsikiliza baba yake. alionekana kumuelewa
vyema sana baba yake kutokana na umakini wake
wa kusikiliza.
''Baba nimekuelewa na nitafanya kama hivyo
unavyoniambia nifanye baba yangu''
baba yake hakuwa na neno zaidii ya kumsisitizia
kwa yale ambayo alishamueleza ayazingatie. lakini
Mzee huyo alionekana kuwa na shauku kubwa ya
kutaka kumueleza mengi sana mwanae juu ya
umuhimu wa hayo mambo kuyashika kwa makini.
''Nakuomba SIKITU uyashike sana haya mambo
usiwe kama wasichana wenzako hapa kijijini sitaki
hata kusikia ukifanya upuuzi kama wanaoufanya hao
wenzako, jitahidi ufikie hatua kama aliyofikia baba
yako mdogo ambae kwa sasa yuko mjini
nilimsomesha vyema mpaka kafikia pale na wewe
napenda ufikie kama alipo yeye, haya mimi
naelekea shambani nitakukuta baadae nikisharudi''
Mzee MAMBO SASA aliinuka na kuelekea ndani na
kuchukua baadhi ya vifaa kama jembe, panga na
dumu la maji. kwa kuwa ilikuwa majira ya asubuhi
yeye alikuwa kachelewa kidogo kutokana na mambo
ya nyumbani ambayo alikuwa akiyafanya hapo
nyumbani kwake. Alifanya haraka kuelekea
shambani huku akiwa anaimba nyimbo za hapa na
pale. Baada ya muda fulani aliweza kufika hadi
shambani na kumkuta Mmama sikitu akiwa
anaendelea kulima. Kumbe mama sikitu alitangulia
na kumuacha mumewe akiwa anaongea na mwanae
sikitu, Mzee huyo alimueleza mkewe kuhusu
mipango yake ya kutaka mwanae akae katika
maisha yenye mwenendo wa kusoma ili atofautiane
na wanawake wengine wa pale Bwawani. Baada ya
muda Mama sikitu aliweza kuondoka kwani alikuwa
tayari keshachoka hivyo akamuaga mumewe na
kumuacha mzee huyo akiendelea kupiga jembe.
Baada ya muda kupita naye aliweza kuchoka na
kuacha kuendelea kulima kisha akakusanya vifaa na
kuanza kuondoka. Akiwa njiani anakutana na Mzee
mwenzake alioyejulikana kwa jina la Mzee SIKUJUA.
Alisalimiana nae kisha wakaongozana pamoja katika
safari nzima ya kwenda majumbani kwao, Mzee
Sikujua alianzisha mazungumzo ambayo hata mzee
Mambo sasa aliweza kuchangia kwa ufasaha, lakini
kila muda ulipozidi mazungumzo hayo yali0onekana
kuwa chachu kwa Mzee Mambo Sasa.
''Bwana Sikujua unafahamu kuwa mwanangu kwa
kipindi hiki alichonacho nataka ajitahidi afike mbali
kupitia elimu yake mana bila kusoma hawezi
kuendelea kabisa kwa sasa'' Aliongea maneno hayo
kumueleza rafiki yake huyo
''Mh! Sawa lakini wewe hukusoma sasa mbona
maisha yako yako mazuri tu bwana Mambo Sasa,
alafu kwa biti wa kike haki ya nani nakuhakikishia
kuwa unamaliza fedha zako tu kumsomesha
mwanao wa kike hivyo cha kufanya acha
kumsomesha kabisa mwanao huyo na hizo fedha ni
boira upeleke kwenye mashamba na upate fedha
nyingi sana''
Maneno hayo yalimchoma kabisa bwana Mambo
sasa hivyo alimuangalia sana bwana Sikujua na
kumtoa umaana kabisa kwa mtu mzima kama huyo.
'' yani wewe nilikuona kama mtu mkubwa wa umri
na utakuwa na mawazo mazuri yenye maendeleo
lakini una ukubwa wa mwili na miaka lakini hakuna
kitu kabisa kichwani mwako unafikiria pumba tu
yani niache kumsomesha ,mwanangu kwa akili zako
finyu kweli '' Mambo sasa alionekana kukasirika
sana
'' kwa hiyo unanitukana mimi, sasa hii taarifa
itawafikia viongozi wa kijiji kuwa umenitusi kama
uanaona kuna ubaya wa haya niliyokuambia basi
tutaona nani mjanja na kama huyo mwanao utafikia
hatua ya kumsomesha mbali na akafika mjinga
wewe, yani wewe ni mdogo kabisa kwangu na
unanitukana mimi tutaona'' Mzee Sikujua nae
hakuwa mbali aliweza kujibu mashambulizi na hapo
pakawa hapaeleweki kabisa na mtafaruku ulitaka
kufika mbali ndipo alitokea bwana mwingine kijana
kwa umri ambae nae alikuwa anatokea shambani na
kuwakuta wakiw wanazozana hapo wazee hao
wawili. Aliamua kuwatawanya kwa busara sana
ambazo ziliweza kueleweka kwa Mzee Mambo sasa
na si kwa Sikujua.
'' Jamani wazee wangu mbona mnataka kufikia
mbali hivyo nyinyi ndio tunawategemea hapa kijijini
na ndio kioo ambacho mnatufunza sisi vijana na
kutukanya pale tunapokosea sasa mkionekana
mnazozana hapa njiani sisi mnatufunza nini ambao
tunawaona cha kufanya nendeni mkae chini na
mtatue msije kufika pabaya jamani''
Kijana huyo alimaliza na kuwaondoa kwani
walikaribiana na kutaka kuonyeshana umwamba.
lakini mzee sikujua hakutaka kuelewa chochote
kabisa zaidi ya kuendelea kuongea maneno
makubwa ambayo hayakuwa na sitara kwa Mee
mwenzake.
'' Yani nakuambia kuwa utanitambua siji kukusaidia
kwa chochote yani unanitukana mimi kuwa ni
mpumbavu nisiyejua kufikili na nina ukubwa wa umri
lakini sina akili sawa mimi naenda lakini
utanitambua''
Mzee Sikujua aliondoka na kumuacha kijana na
Mzee Mambo sasa wakiwa wanaongea. Walirudi na
kuachana pale kisha Mzee Mambo sasa akaenda
nyumbani. Ulipita muda sana mpaka jioni wakiwa
nyumbani hapo walikaa kama familia na Mzee
Mambo sasa akiwa na mawazo juu ya ugomvi ule
ambao ulijitokeza muda mchache uliopita. Hali hiyo
iliweza kuonekana kwa mkewe na sikitu ambae
alikuwa karibu sana na mama yake. kutokana na
hali ya maisha yao yalivyo yalikuwa ni ya duni sana
ndio maana mzee huyo alijikita zaidi kwenye kilimo
cha korosho na kupata fedjha ambazo zinatumika
kumsomeshea mwanae ambae yuko shule ya
msingi Bwawni darasa ;la saba akiwa anakaribia
kumaliza elimu yake.
'' Mume wangu mbona leo hauko sawa kabisa kama
siku zote kuna nini ambacho kinakusibu maana
tangu mchana nimekuacha shambani uko na furaha
yako lakini umerudi aaah umebadilika kabisa'' Mke
wa Mzee huyo alihoji baada ya kumuona mumewe
hayuko kwenye hali ya kawaida kama alivyoizoea.
'' Ni kweli mke wangu lakini si ya kuzungumza sasa
hivi tutaongea baadae au ngoja kwanza sikitu ebu
kaangalie kwanza kuku kama wametimia ndani
humo alafu uje uniambie''
sikitu alinyanyuka na kuelekea kwenye banda la
kuku ambalo aliambiwa na kuwaacha wazazi wake
wakiendelea kuongea
'' Mke wangu nimemtoa mtoto ili nikueleze kuwa
nimegombana na mzee Sikujua'' Aliongea
kimyakimya
'' Heeee kwa yapi tena mume wangu mpaka
ugombane nae jamani''
'' Eh wakati narudi nyumbani, njiani tulikutana na
sikujua sasa akili yake anataka nisimsomeshe sikitu
kwa kuepusha gharama kubwa aliyoifikilia mimi
nikamuambia msimamo wangu juu ya huyu mtoto
ndipo ugomvi ulipoanzia lakini akawa ananitishia
amani jambo ambalo maishani mwangu siliogopi''
wakati wanamalizia maongezi ndipo sikitu alirejea
na kumuambia kuwa wameshatimia. Walilala usiku
huo mpaka asubuhi lakini mzee Mambo sasa
hakutaka kwenda shambani kwani hakuwa sawa
kiakili kutokana na mambo mengi sana
yanayoendelea pale kwake. Wakati huo anagongewa
mlango akiombwa atoke nje alivyotoka anakutana
na mwenyekiti ambae mkononi alikuwa na barua na
akapatiwa aisome baada ya salamu na kukabidhiwa
karatasi hiyo akaaga na kuondoka zake. Mzee huyo
aliduwaa sana kisha akaingia ndani na kutaka
kuanza kuisoma...........
 
SEHEMU YA PILI 02
Endelea................
Wakati huo anagongewa mlango akiombwa atoke
nje na alivyotoka anakutana na mwenyekiti ambae
mkononi mwake alionekana kuwa na karatasi ndipo
akapatiwa aisome hiyo ilikuwa ni barua. Baada ya
salamu na kumkabidhi karatasi hiyo ndipo akaaga
na kuondoka zake. Mzee huyo aliduwaa sana ndipo
akaingia ndani na kutaka kuanza kuongea alishika
tamaa kwanza huku akizungukazunguka ndani humo
huku akijiuliza kipi ambacho kimeandikwa ndani ya
karatasi hiyo. Alihifadhi kwenye koti lake na kutoka
nje huku akiangaza huku na kule na kuanza kumuia
Sikitu ambae hakujulikana wapi aliko.
''Mh! jamani huyu mtoto kaenda wapi jamani,.....''
Ndipo alirudi ndani na kuchukua karatasi ile pamoja
na kiti akatoka nje na kukaa barazani hapo
akafungua ile karatasi ile na kuangalia angalia.
Alionekana kutofahamu chochote ambacho
kimeandikwa ndani yake ndio maana akawa
anamhitaji mtoto wake Sikitu ili aweze kumsomea
barua hiyo. Akiwa kapumzika anwaza jinsi gani
mambo ambayo atayafanya kuhusu swala lake la
kumsomesha mwanae, Sikitu alifika na kumkuta
baba yake akiwa kazama kimawazo sana, alimuuliza
kulikoni kukaa na hali ile ambayo aliyonayo.
''Haa! mwanangu afadhali sana umefika nilikuwa
nakutafuta, embu kaa hapa kwanza mwanangu
unisomee hii karatasi maana macho yangu hayaoni
vizuri''
Mzee Mambo sasa aliweza kumuambia mwanae
atulie chini, Sikitu alikaa na kuchukua karatasi ile
ambayo baba yake alimpatia ili aisome. Sikitu
alikaaa tayari kwa kuanza kuisoma huku baba yake
akiwa anasikiliza kwa makini sana.
''Husika na taarifa ya hapo juu kuwa Mzee Mambo
sasa unahitajika ofisi ya mtendaji wa kijiji kuja
kusikiliza shitaka lako bila kuchelewa''.
Sikitu alimaliza kusom kisha akamuuliza baba yake
kuwa ni kitu gani ambaho kakifanya mpaka ahitajike
huko ofisini, Baba yake aliona swali gumu sana
ambalo kaulizwa kwani alishindwa kuelewa shida ni
kitu gani na kwa kosa gani ambalo anaitiwa, Mzee
Mambo sasa alimuomba Sikitu ili akamuite kijana
mmoja ambae anaitwa SUSU, Sikitu alienda haraka
kule ambako alielezwa na baba yake, alifika pale
kwa bwana susu ambako aliambiwa kwenda
kumfuata na hatimae aliweza kumkuta na
kumuambia ile salamu ambayo aliagizwa na baba
yake.
Waliongozana mguu kwa mguu kuelekea kwa bwana
Mambo sasa, njiani sikitu aliweza kuuliza swali
kuhusu baba yake kama anweza kutambua nini
ambacho kimemtokea, kijana huyo alimueleza kuwa
hatambui chochote kuhusu jambo hilo na yeye
ankwenda kumsikiliza nini alichomuitia. Walipofika
hadi kwenye nyumba husika walimkuta mzee huyo
akiwa katulia tu, alionyesha furaha baada ya
kumuona kijana susu kwa kumuitikia wito wake ule,
walipata nafasi nzuri kwenye mwembe mmoja
uliopo karibu na nyumba yake.
'' Kijana nimekuita hapa kuna tatizo ambalo
limejitokeza ndani ya muda mchache tangu jana
pale ulipotuacha tukizozana na wewe ukatutoa
katika mzozo huo unakumbuka?'' kijana huyo
alionekana kuwa na wasiwasi na akawa anavuta
kumbukumbu, '' Haaa! sawa mzee wangu
nimekumbuka si pale jana nikiwa natoka shambani
mh sawa nini kimetokea?''
'' swa nashukuru sasa leo hii kaja mwenyekiti
mapema sana na kanipa hii karatasi '' Aliitoa na
kumpatia aweze kuisoma, ndipo kijana Susu
aliikamata vyema huku akiwa na shauku ya kutaka
kuisoma barua hiyo, alivyoimaliza alivuta pumzi
ndefu kisha akamuangalia vyema mzee huyo na
kushindwa kusema chochote
'' Ina maana Mzee susu kaamua kukupeleka katika
ngazi ya serikali kwa sababu gani sasa ambayo
mmeshindwa kuelewana''
'' Ndio hivyo haswaaa ndio maana nikakuita ili muda
wa saa sita tuende na wewe uwe kama shahidi
wangu pale nitakapohitajika kutoa ushahidi, yani leo
kanivurugia kila kitu leo''.
Alionyesha kuomba msaada mkubwa kwa yule
kijana ambae jana yake walivyozozana na mzee
mwenzke Sikujua aliwakuta sasa kidogo anaweza
kumsaidia kwa matatizo hayo aliyo nayo. Kijana
susu alikubali na akaomba kwenda kujiandaa kwa
ajlili ya hiyo. Mzee Mambo sasa alimuambia
mwanae sikitu kuwa aende akamuite mama yake
haraka sana ili amueleze habari hiyo kabla hajaenda
huko ofisini, Sikitu alikwenda hatimae baada ya
muda mchache alirudi na mama yake. Mzee huyo
alimueleza kila kitu na hatimae muda uliwadia
alitoka na kumpitia kijana susu na wote wakaelekea
ofisi ya mtendaji wa kijiji. Njiani walifundishana jinsi
gani ya kuepukana na kesi hiyo inayomkabili,susu
alikaa nje na Mzee Mambo sasa aliingia ndani na
kumkuta mwenyekiti,mtendaji pamoja na bwana
sikujua. mwenyekiti alionyesha kumkaribisha kwa
bashasha sana mzee huyo na kumueleza kuwa aketi
kwenye kiti kilicho karibu yake na waanze maongezi
yao.
''Bwana Mambo sasa kwanza tunashukuru na
kukupongeza kwa kuhitikia wito wetu hapa kwani ni
wachache wenye kutii amri hiyo je? unamfahamu
huyu mzee aliyokaribu yako'' mwenyekiti aliuliza
swali huku akimnyooshea kidole sikujua, '' Ndio
namfahamu vyema kabisa''
'' Sawa unakumbuka miaka sita iliyopita muliuziana
mashamba ya mikorosho lakini haukuweza
kummalizia fedha zake je? unakumbuka'' Mzee
mambo sasa alistaajabu sana kwani akili yake
haikuwa katika swala la jana kule shambani, alivuta
pumzi ndefu na ndipo akakohoa kidogo '' Kumbe
ndio hiyo kesi niliyoitiwa, ninachokumbuka
tuliandikishiana kuwa kila mwaka nampatia kiasi
cha fedha kadhaa na nilishamlipa imebaki ya
mwaka huu tu sasa sjajua tatizo ni nini'' mambo
sasa alijiamini sana kwa kuongea na kuwafanya
waulizaji wawe kimya muda wote.
'' lakini hatukukubaliana hivyo ulisema kuwa mwaka
jana ndipo unamalizia na kitendo na maneno yako
ambayo jana uliyaongea ndio yamenifanya nije
kushitaki hapa'' Sikujua aliongeam kwa jazba sana
hiuku akipayuka kwa sauti kali.
''Ngojeni kwanza musianze kulumbana hapa mupo
kwenye sheria ebu sema taratibu je ni maneno gani
ambayo aliweza kuyaongea hapo jana?'' mwenyekiti
aliuliza.
'' bwana huyu alisema kuwa hatoweza kunilipa
kabisa na pia akanitusi kwa matusi ya nguoni
ambayo kiukweli alinidhalilisha na shahidi ninae
atakuwa njiani anakuja anaitwa susu''
Aliongea bwana Sikujua kuwa susu ndie shahidi
yake lakini bwana mambo sasa alionekana
kushituka iweje awe susu wakati susu ndie shahidi
yake ambae kaja nae. Walimuita susu ambae
alielezwa kuwa yupo hapo nje kwa ajili ya kutolea
ushahidi, ajabu iliyoje susu aliongea kwa kujiamini
sana pia akamtetea bwana sikujua na kumfanya
mambo sasa kuduwaa, aliulizwa sikujua nini
ambacho anataka afanyiwe ili kupata fidia ya ile
kesi yake baada ya kuonekana yeye ndie mwenye
haki
'' nashukuru sana mimi nahitaji huyu bwana lile
shamba la mikorosho aniachie mpaka aje kulipa
kiasi ambacho tulikubaliana''
Mzee mambo sasa alijiinamia chini huku akitokwa
na machozi kwa ile ambacho anakisikia masikioni
mwake. Hivyo baada ya miezi kadhaa bwana
mambo sasa alikuwa hana hili wala lile kwani
hakuwa na hata fedha ya kujikimu kwani alikuwa
anategemea sana lile shamba lake la mikorosho
ambalo kwa sasa kazurumiwa, Ndipo akafikiria
jambo kuwa sasa kutokana na maisha yale hata
sikitu ataachan hata kusoma kutokana na mahitaji
muhimu kukosekana....
Mzee mambo sasa aliamua kuchukua uamuzi
mgumu sana ambao hata familia yake ilimshangaa
sana,,,,,,,
 
SEHEMU YA TATU 03
Endelea......................
Mzee Mambo sasa aliamua kuchukua uamuzi
mgumu sana ambao hata familia yake ilimshangaa,
kikubwa alichoamua ni kutaka kumuendea kijana
susu ambae alimfanya aweze kushindwa katika kesi
ile kumbe susu alikuwa tayari keshapangwa na
bwana Sikujua. Alimuita kwanza mkewe ndipo
akamuambia kuwa anahitaji kumuendea susu ili
akamuonyeshe adabu kwani hawezi kumyumbisha
kiuchumi namna ile, mkewe hakupenda kabisa
kumruhusu mumewe kwenda huko kwani kuna
uwezekano wa kufikia hatua mbali ya kuumizana. ''
Mume wangu nakuomba sana haitosaidia wewe
kwenda kwa huyo kijana kwani utasababisha
matatizo na kupata kesi kubwa zaidi'' Mume wa
Mambo sasa, alimuomba sana bwana huyo lakini
kwa mzee huyo hakuonekana kama muelewa hivyo
alinyanyuka na kuingia ndani, alichukua panga na
kuiweka kwenye kiuno chake ambacho uliweza
kushikiwa na suruali yake ambayo haikuwa na
mkanda kama kuishikia, alitoka nje na kuongoza
njia ya kwenda kwa susu kama alivyohitaji. Sikitu
alianza kulia kwa huzuni sana kwa kumuona baba
yake akielekea huko kusababisha matatizo
'' Baba tafadhali usiende baba yangu sasa
ukisababisha matatizo na ukafungwa mimi
atanisomesha nani babaaaaa naomba usiende baba
yangu hukoo'' Alikuwa analia kwa uchungu huku
akigalagala chini mama yake alimuinua na
kumuingiza ndani huku wakijawa na huzuni kubwa.
''baba sikitu tatizo ni nini jamani mume wangu
mpaka unataka kufanya hayo, mimi sijapendezwa
kabisaa aaaah eeeh mungu weee tuone sisi na hizi
shida zetu mnusulu mume wangu huko aendako''
Mzee Mambo sasa alidhamiria kabisa kwenda
kuufanya unyama ambao aliuhitaji, lakini maneno ya
mama sikitu kama yalifanya kazi kumuomba mungu
amuangalie bwana huyo huko aendako, ndipo mzee
huyo alisimama kidogo akisuasua alite,mbea mbele
karibu na shamba moja hivi humo njiani na
kuwakuta watu wengi wakilima kama vibarua hivi,
alijiuliza sana kichwani mwake kwa lile ambalo
anakwenda kulifanya kwa bwana susu.
'' Mh! hivi nikienda kumpiga na panga huyu kijana
alafu nikifanikiwa kuua au kumjeruhi nitaishia jela
alafu mwanangu atashindwa kusoma pamoja na
mkle wangu wataishi maisha magumu sana, lakini
haya maisha mpaka lini sina thamani tena mimi
hapa kijijini...ngoja nifanye jambo kwanza''
Aliamua kuwasogelea wale watu ambao walikuwa
wanalima pale akamfikia mama mmoja na
kumshtua kwanza ili apate kumuuliza jambo. '' Heee
mama MENGI, habari ya asubuhi ndugu?''
Mama huyo aligeuka nyuma na kuonana uso kwa
uso na mambo sasa '' Mambo sasa haya karibu vipi
umekuja kutualika shambani kwako kulima au''
Swali alilouliza lilikuwa gumu sana kujibiwa kwani
aliona kama anamkejeli kabisa '' hapana nimekuja
kuuliza nani ambae anakatisha vipande hapa vya
kulima na analipa kiasi gani?''
''ina maana unataka kuja kulima na wewe? ''
''Naomba unijibu mama mengi swali langu''
'' Si yule mzee MAPATO pale mbelee, kipande
kimoja anakatisha shilingi elfu mbili tu'' Baada ya
kumuelekeza kuwa ni mzee mapato alinyanyua
miguu na kumfuata haraka sana alimueleza shida
yake kisha mzee mapato akamsogeza pembeni na
kuanza kuongea nae vizuri.
'' Hapana bwana wewe ni mzee mwenzangu pia sio
vizuri hawa vijana wakikuona unainamisha mgongo
cha kufanya leo hii nitakupa shilingi elfu sita
ambayo itakusaidia kwa miezi hii'' Mambo sasa
hakuamini kabisa baada ya kuambiwa kuwa
anasaidiwa tu japo hakupenda lakini kutokana na
shida ilimbidi kupokea ili akafanye matumizi yake
nyumbani. Mzee Mambo sasa aliondoka na kiasi
cha shilingi elfu sita, kipindi hiko ilikuwa fedha
nyingi sana pia ukizingatia ni maisha ya kijijini.
Alifika nyumbani mama sikitu na sikitu hawakuamini
kabisa kama karudi mzima bwana huyo kwani hofu
yao kubwa atarudi na alama yeyote itakayoashiria
kuwa kafanya mauaji kama aliyodhamilia. Aliwakuta
pia wakiwa na majonzi, aliwaita na kuwaeleza kuwa
alifikilia sana hivyo aliamua kuachana nalo,lakini
kwa bahati nzuri pale kwenye shamba la bwana
mapato niliwakuta watu wakilima na mimi nikaenda
kuomba kulima lakini alinikatalia ila akanipatia kiasi
hiki hapa kwa kunisaidia pia kaniambia kesho
nitaenda kwake kuongea nae zaidi kuhusu kutafuta
kazi zaidi ambayo itaweza kunisaidia katika mabo
yangu.
Walishukuru sana kwa hilo, baada ya yeye kuachana
na lile swala lake la kutaka kufanya mambo ya
ajabu. Majira ya jioni moja ya kijiwe cha kahawa
ndani ya hiko kijiji cha bwawani kwani pia
wanajishughulisha na ulimaji wa kahawa kama
mahitaji ya kawaida na si biashara kama maeneo
mngine ilivyozoeleka kama mikoa hiyo ya kagera,
eneo hilo alionekana mzee Mapato na bwana
sikujua wakipiga domo pale wawili tu huku
wakishushia na kahawa yao halisi,
'' Eeh! bwana sikujua nikuchekeshe, kuhusu ile kesi
uliyonihadithia wiki ziliozopita kuhusu bwana
Mambo sasa''
Mapato aliongea, '' Ehee kuna nini tena ''
'' leo hii si unafahamu kama nalimisha lile shamba
langu la mikorosho ili niwahi kupulizia salfa
mapema!''
'' Ndio nafahamu vizuri kabisa''
'' Sasa baada ya muda Mambo sasa leo akafika
pale mala akaanza kunililia mala nina shida sana
naomba vipimo nilime maana hali yangu sasa
haieleweki kule nyumbani......''
Bwana sikujua akawa hana mbavu kwa kucheka
sana huku akishikilia mdomo wake pamoja na
kuiweka kabisa kahawa yake chini. '' haaa haa haa
haa haa eeeeh ukamuambiaje sasa''
'' Mimi kumuonyeshea jeuli nikampa elfu sita ya
vipimo vitatu, alafu nikamuambia kuwa jioni aje
nimsaidie zaidi yani sasa hana jauli kabisa sasa hivi
na mpaka tutamkomesha anajifanya mzee wa
mambo sasa na kujifanya tajiri wa kijiji tena
ulivyomnyang`anya lile shamba nilifurahi sana''
Aliongea bwana Mapato huku akitikisa kichwa
kuonyesha msisitizo mkubwa sana kwa jambo
ambalo alikuwa analiongea. Mzee sikujua nae
hakuwa mbali aliweza kuongezea maneno ya
kumkashifu na kumfanyia vitimbi mzee mwenzao
huyo bwana Mambo sasa, '' yani hata mimi nataka
nihakikishe yule mtoto wake namtia mimba
kutokana na shida zao alafu nione sasa
wanachotaka kujivunia mana kwa yule binti, mzee
mambo sasa atakubali kuiba,kutapeli, kufanya kazi
ngumu ili mradi sikitu aingie shuleni''
Waliachana pale ndipo mzee sikujua akatoka na
kuelekea nyumbani kwake lakini njiani aliweza
kukutana na sikitu akitoka dukani kununua mboga,
kwa akili ya sikujua alijua fika kuwa ile ela
aliyofanya matumizi basi imetoka kwa Mapato,
alimuita binti huyo na kumuomba asogee karibu
yake kwa kuwa alimuona mwenye wasiwasi sana.
'' Sikitu nataka kukuambia kitu kizuri utakubali?''
aliuliza Mzee sikujua '' Mh! kitu gani hiko?''
'' Sawa leo jioni naomba uje kule nyumbani kwangu
kuna kazawadi kazuri nimekuandalia sawa'' Aliongea
bwana sikujua kwa kumshawishi sikitu lakini sikitu
alionekana mwenye kupinga
'' Sasa unavyokataa utafanya ukose masomo yako
na wewe unapenda sana kusoma ukikubali tu mimi
namrudishia baba yako mashamba yale ya korosho
na sasa yamezaa vyema atayatumia kupata fedha
nyingi za kukusomesha wewe, lakini iwe siri yetu
wawili wewe njoo alafu utaona nitakachokufanyia
kwa baba yako''
kauli yake ya kumrudishia mashamba baba yake
aliipenda kwani alifahamu kuwa atakuwa kamsaidia
sana baba yake bila kujua dhamira ya bwana huyo
kumuambia aende kwake majira ya jioni hayo. Sikitu
alikubali ndipo akaelekea nyumbani kwake na
bwana sikujua akelekea kwake pia akiamini kuwa
atafanikisha njama zake. Majira ya jioni Mzee
mambo sasa alimuambia mkewe wafuatane kwenda
kwa Mapato huku wakimsii mtoto wao asitoke pale
nyumbani ili asubirie kuku wamalizikie kuingia na
yeye abaki pale baadae wamkute.
Waliongozana mke na mume kuelekea kwa Mapato
wakati huo nyuma wakimuacha Sikitu na yeye
akiacha kazi aliyoambiwa na kwenda kwa bwana
sikujua kwa kuamini atawahi kurudi mapema na
kufanya kazi hizo alizoambiwa. Sikitu anafika kwa
mzee sikujua na kupokelewa kwa bashasha sana
lakini wakati anamuingiza ndani mwake Mama
Mengi aliweza kuwaona alishtuka sana baada ya
kumuona binti Sikitu akiingia ndani ya nyumba ya
Sikujua, Ilichukua muda sana sikitu kuwa humo
ndani wakati huo Mama na Baba yake tayari
wanarejea nyumbani wakiamini kuwa watamkuta
mtoto wao, walishangaa sana kuona kuku wakizagaa
nje ya nyumba hiyo na hapakuwa na mtu yeyote
ambae yupo karibu, waliimuita sana Sikitu bila
mafanikio ndipo walianza kuchanganyikiwa sana
pale.
Nyumbani kwa Sikujua mzee huyo alionekana
kukurupuka ndani mwake na kutoka kwa haraka
sana huku akifunga vizuri suruali yake akikimbilia
njia ya kwenda kwa bwana Mapato................
JE NINI KILIMTOKEA MZEE SIKUJUA?
 
SEHEMU YA NNE 04
Endelea.................................
....Nyumbani kwa Sikujua, mzee huyo alionekana
kukurupuka ndani mwake na kutoka kwa haraka
sana huku akifunga vizuri suruali yake akikimbilia
njia ya kwenda kwa bwana Mapato. alikimbia sana
kwa nguvu zake zote, ilikuwa jiono sana kiasi giza
likawa linaingia alipofika alifikia chini kwa kuanguka
hadi kwenye mlango wa Mapato. Mapato akiwa
ndani alisikia kelele za kuanguka ndipo akatoka kwa
nje, alimkuta Sikujua akiwa hoi paale chini pia
akitweta kwa hofu,
''Heeeh! vipi tena bwana mkubwa mbona hali hiyo
kipi kilichotokea huko?''
Mzee Mapato alimuuliza rafiki yake aliyeonekana
kuwa kwenye hali ya mshangazo kwake. Bwana
Sikujua alikuwa bado kabisa kuongea kwani alikuwa
anatapatapa kuongea, hivyo mapato hakuweza
kumuelewa vizuri baada ya muda ndipo akamshika
mkono na kuanza kumueleza jambo ambalo alitaka
kumuambia
''Bwana mapato naomba unisaidie kuna tatizo
nyumbani limenikuta naomba twende ukanisaidie ''
Mapato alimshangaa sana kwani ni jambo la ghafla
sana lakini haikuwa shida sana kwani walinyanyuka
na kwenda haraka haraka kwenda kwa bwana
Sikujua, wakati wapo njiani wanakutana na Mzee
Mambo sasa akiwa na hofu kubwa usoni mwake
uso ukiwa na jazba alipowakuta wawili hao hasa
bwana Sikujua hakumtaka hata kumuongelesha
kabisa alimuita bwana Mapato pembeni ili
amueleze tatizo lake
''Bwana Mapato, samahani kuna tatizo nyumbani''
mzee sikujua aliongea kumuambia mapato huku
akionekana kuwa na mshangao sana
''Mh! nini tena bwana Mambo sasa''
'' wakati nakuja kwako nyumbani kwangu tulimuacha
yule binti yangu Sikitu sasa nimerudi sijamkuta
alafu kuku wakiwa wamezagaa mlango umefungwa
na si kawaida yake kabisa hivyo unavyoniona hapa
nimechanganyikiwa kabisa ndugu yangu hapa
naelekea kwa mwenyekiti'' Mzee mapato alishika
mdomowake akishangaa sana kwa yale ambayo
aliambiwa
''Sawa ngoja niende kwa huyu ndugu kwani hata
yeye kuna tatizo alilokuja kuniambia pale kwake
limetokea nikitoka huko nitahakikisha nakuja kwako
ila ngoja usiharakie kwenda kwa mwenyekiti kwanza
kabla ya kumtafuta''
Mzee Mambo sasa alimuacha pale na yeye
akaelekea njia nyingine ili kumtafuta mwanae, Mzee
sikujua alimuuliza kuwa kakueleza nini huyu mzee, ''
Aaah! usijali eti kapotelewa na mwanae yule sikitu
ndio kaja kuniomba mimi ushauri afanyaje''
Alionekana kuduwaa sana sikujua na kuanza
kupooza hata mwili wake, mapato alimuuliza vipi
yuko vile lakini alisimama huku akiwa mnyonge
sana huku akielekea nyumbani kwake, walipofika
nyumbani Mzee Sikujua akamueleza Mapato '' Kaka
haya nendan humo ndani utakachokikuta hapo
kitandani kwangu ndio nilichokuitia ndugu yangu
mana nimeshindwa hata nifanye nini''
Aliingia ndani akiwa hana wasiwasi wowote baada
ya muda alitoka na kumshangaa sana hatimae mzee
mapato alimtandika kofi rafiki yake huku akimlaumu
sana kwa kile ambacho alikona kule ndani '' Sikujua
nini umefanya baba yake anamtafuta kule kumbe
wewe umemfanyia kitu cha ajabu ona sasa hatujui
kafa au kazimia bwana mbona unakurupuka hivyo
hata kama una nia ya kumkomesha baba yake lakini
si kumharibu huyu mtoto ona sasa unafanyaje sasa''
Mapato alifoka sana kuhusu swala lile aliloliona
kule chumbani kwa sikujua, '' Rafiki yangu
samahanindio maana nikaja kwako sasa ili tujue
unanisaidiaje, mimi sio mjinga kuja kwako naomba
uniambie nini nifanye'' Mapato alifikilia sana ndipo
akamuambia rafiki yake jambo kwa kumnong`oneza
sikujua walionekana kuingia ndani, baada ya kufika
ndani sikujua alifunua shuka ndipo akaonekana
sikitu akiwa hajitambui huku miguuni mwake
mukivilia damu nyingi pamoja na mapovu
mdodmoni, hali hiyo iliwashangaza sana na wakawa
wanaduwaa hawajui nini wanakifanya. walichukua
tenga pamoja na mkeka mkubwa hivi walimvirigia
vizuuri na kumfungia kamba nyingi ya kutosha alafu
wakamuweka kwenye tenga hilo, ''Sasa sikujua hapa
umeshaua na haitajiki mtu yeyote ajue zaidi yetu na
hapa tunaenda kumtupa mbali sana tena usiku
mkubwa sawa?''
Walikubaliana kwa pamoja ndipo wakaliandaa
vyema na wao wakakaa nje wakijadili kwa kuhusu
lile swala lililotokea,
Upande wa bwana Mambo sasa alienda hadi kwa
mwenyekiti na kumueleza lile tatizo lililotokea, Kwa
upande wa mwenyekiti alimueleza kuwa kesho
aende tena ndipo watamtatulia shida yake, taarifa ya
kupotea kwa sikitu ilikuwa haijaanza kusambaa kwa
haraka sana kwani walianza kumtafuta kimyakimya
kabla ya kuwashirikisha wanakijiji wote, alirudi
nyumbani akiwa hana furaha kabisa.
Alimkuta mkewe akiwa analia tu hana hata hamu ya
kuendelea na shughuli za pale nyumbani hii yote
kutokana na uchungu wa mwana. Majira ya saa
saba za usiku bwana sikujua na mapato walilala
pamoja ndipo wakafungua mlango tayari kwa
kwenda kumtupa sikitu, lile tenga walilipakiza
kwenye baiskeli huku sikujua akishikilia mbele
kunyoosha muelekeo na mapato akiwa anasukuma
kwa nyuma, walipita kwenye nyumba moja ndipo
wakakutana na mtu akiwa anajisaidia haja mbele ya
nyumba yake hawakutambulika kutokana na lile giza
lililotanda usiku ule, walifanikiwa kufika porini
maeneo ambayo ilionekana kuwa ngumu sana
kufikiwa na mtu yeyote kwa haraka, walilitua lile
tenga kutoka kwenye tenga na kulitupia humo
porini.
Walirejea na Mapato akaenda nyumbani kwake huku
akiwaza kwa lile swala ambalo wamelifanya alibaki
akishika tamaa akiwa kitandani kwake katulia, Kwa
upande wa bwana Sikujua alighaili hata kulala
kwenye kitanda chake hivyo akalala chini na
akaacha kitanda, hii yote kutokana na uoga wa lile
walilolifanya, Asubuhi na mapema sana Sikujua
aliamka na kufagia kama kawaida yake ilivyo,
alionekana Mama Mengi kupita pale nyumbani kwa
sikujua
'' Baba vipi hali, shikamooo''
'' Marhabaa, ''
''Baba naona jana ulikuwa na kabinti mambo yako si
mabaya sana''
Mzee sikujua alishtuka sana kwa kushangaa kuwa
alijuaje kuhusu ile mada wakati alipokuja yule binti
hakuna ambae aliona vipi huyu mama afahamu lile
jambo, baada ya hapo alionekana kugoma sana kwa
kauli ile ya mama Mengi
'' Wewee mama wewee kuwa na adabu kabisa
mbele yangu, uzee huu unione kuniambia maneno
hayo khaaa unanitukana ina maana hata baba yako
Mzee MANYENYE hanikuti kabisa kuwa na heshima
binti''
Mama Mengi alikuwa na mshangao kutokana na
yale maneno aliyoambiwa,
'' Sawa baba nilikuwa nakutania tu baba nisamehee
sitorudia'' Aliomba msamahaa kwa bwana Sikujua
'' samahani ya nini na sasa kuanzia sasa nisikie uo
upuuzi wako kokote wa kunisingizia nitakuonyesha
mjinga sana wewe nitokee hapa''
Mama Mengi aliondoka kwa aibu na haya aliyonayo
kutoka kwa Sikujua, Alinyoosha mbaliga zake za
miguu bila hata kuangalia nyuma,, Upande wa
Mambo Sasa akiwa kwa mwenyekiti anaonekana
kuandiaka moja ya karatasi aliyokabidhiwa na
hapohapo mwenyekiti akamuita kijana mmoja na
akawa anampa majukumu
''kijana naomba ukapige kengele ya kijiji ile ya
dharura kuna jambo tunahitaji kulifanya. Kengele
iligongwa kwa mlio wa dharura na sifa moja wapo
ya kijiji cha Bwawani wasikiapo kengele kama hizo
basi wao huitikia kwa haraka sana bila kukosa,
baada ya muda watu walifika pale wakiwa karibia
wote wakihitaji kusikiliza. Wengi wao walidhania
kuhusu swala la mazao yao ya pale, kwa kuwa
hawakuwa na dodoso yoyote kuhusu kupotea kwa
binti Sikitu.
Walionekana wazazi wa sikitu wakihuzunika
wakitokea ofisini kwa mwenyekiti na huku mama
yake sikitu akiwa analia kwa uchungu sana.
Mwenyekiti alinyamazisha watu na kuanza kuongea
ili kuwaeleza nini wameitiwa pale baada ya kengele
ya dharura kujitokeza, alionekana mzee sikujua,
mzee mapato na Manyeyepamoja na Mama Mengi
ndani ya kundi hilo la watu wakimsikiliza
mwenyekiti.
''Kwanza tunaomba radhi sana kwa usumbufu
uliojitokeza ila tatizo tulilonalo ni kuwa hawa wazazi
mnaowaona wameleta malalamiko yao juu ya
kupotelewa kwa mtoto wao anayejulikana kwa jina
la Sikitu'' watu walishangaa kwa pamoja kwa kile
kilichosikika masikioni mwao,
Zaidi kwa Mama Mengi, aliyeshangaa zaidi,
mwenyekiti aliendelea kwa kusema
'' lakini kutokana na maelezo yaliyotolewa tunatuma
laeo jeshi la kijiji yani sungusungu, pamoja
tunaruhusu wanakijiji kujumuika katika msako huu
wa huyo binti popote pale atakapoonekana, lakini
tunamhitaji mzee Mapato katika kutolea maelezo ya
mambo fulani kuhusiana na hili swala ahsanteni
tunaomba ushirikiano wenu. Wanakijiji waliondoka
wakiwa hawaamini kwa kile wakisikiacho. Mapato
alifika ofisini na kuulizwa baadhi ya maswali na
hivyo akaruhusiwa kuondoka ila pale atakapohitajika
basi asisite kuja.
Mzee sikujua hali haikuwa vizuri kabisa kwani
alichosikia pale kilimtia shaka juu ya maisha yake,
aliona dunia ndogo sana kwa wakati ule. Maneno ya
hapa na pale yalianza kusikika kila mahali na
wengine wakilaani vitendo vile vya ajabu ambavyo
vilianza mapema ile ndani ya kijiji chao. Kila kona
sasa walinzi wa usiku sungusungu walianza kutanda
kwa kasi kubwa sana na baadhi ya wanakijiji
wakishirikiana kumtafuta binti Sikitu aliyepotea.
Mzee Mapato alimendea sikujua na kumpasha
habari ile ambayo aliitiwa kule. ''Sasa sikujua
mambo si unayaona kuwa yamepamba moto kiasi
kwamba hali inakuwa tete kwa sasa, andaa fedha za
kutosha tumalize kesi hii kwani keshokutwa nitaitwa
pale na ndipo nitakapokwenda kumaliza kabisa.''
Mzee sikujua hakuwa na shida zaidi ya kuhitaji lile
swala asije kujulikana ''Lakini. kuna mama Mengi
huyu mtoto wa Mzee Manyenye jana wakati naingia
nae aliniona sasa sijui nafanyaje hapo'' Mapato
aliwaza kidogo kisha akasema
''Usijali usiku wa leo namfanyia dawa yake hawezi
kutuumbua rafiki yangu ''
waliagana pale lakini wakiwa na ahadi na wao
kuungana na watu wanaomtafuta sikitu ili kuficha
aibu yao.......
 
SEHEMU YA TANO 05
Endelea...................................
Mzee Mapato alimtoa wasiwasi rafiki yake Sikujua
kuwa atalifuatilia kwa umakini sana na pia
atajitahidi kumtia mkononi huyo mwanamke ambae
aliweza kumuona sikujua wakati akimuingiza ndani
Sikitu, pia waliagana kuwa wajitahidi sana kujiingiza
kwenye msako huo ambao unaendelea hapo kijijini
wa kumtafuta Sikitu ili na wao wasijulikane kuwa
ndio wahusika wa hilo tukio lao walilolifanya.
Nyumbani kwa Mambo sasa hali haikuwa nzuri
kabisa kwani furaha ilipotea kwa mara moja baada
ya kuondokewa na mtoto wao kipenzi, baba sikitu
hakuchoka aliamua kwenda shambani labda
atakuwa kakamatwa na mnyama alipita njiani huku
akiwa anaita jina la sikitu kama ataweza kuitika au
kuona hata dalili ya kuonekana kwake, kwa bahati
mbaya haikuweza kuwa bahati yake kwa siku hiyo
hivyo alirudi akiwa na kilio cha uanaume.
''Mwanangu nini kimekupata mama uko wapi baba
yako na mama yako tuna hangaika kukutafuta, ebuu
njoo mbele yangu niweze kukuona hata kwa mara
ya mwisho''. Aliongea peke yake Mzee mambo sasa
akiwa anarejea nyumbani. Alipofika nyumbani kwake
anakutana na bwana Mapato na yeye akiwa
anahuzunika machozi yakimtoka kwa unafiki,
mambo sasa alimkaribisha kwa kumshika mkono
na akitikisa kichwa kumaanisha ndio hayo
yaliyomkuta, ''Bwana rafiki pole sana pia nimekuja
kutoa kiasi cha fedha kuonyesha pole yangu
naomba upokee wewe ni mwanaume jikaze hayo ni
mapito ambayo unaweza kuvumilia na yakapita
kabisa'' Alipokea kisha akawa anamfuta machozi na
yeye akageuka nyuma na kuondoka.Haukupita muda
mwingi walikuja vijana kadhaa pale kwake akiwemo
na bwana Sikujua aliweza kuwepo pale kwenye
msako ambao ulikuwa unaendelea kufanyika vijana
hao walionekana kuchoka sana hivyo walikuja kutoa
taarifa juu ya msako wao. '' Baba dah tumezunguka
karibia kijiji kizima lakini hakuna dalili zozote
ambazo zinaonyesha kuwa yupo mwanao'' mzee
huyo alipewa taarifa lakini alionekana kutoamini
kabisa ''Ina maana mwanangu atakuwa kapotea
kweli jamani eeeh! aah Sikitu nini kimekukuta
mwanagu '' Walimtuliza asiendelee kulia pale,
walimuaga ili waelekee kwa mwenyekiti wakampe
taarifa juu ya kazi waliyotumwa. Baada ya wiki
kupita tayari yalishafanyika mazishi ya kimyakimya
huko aliko kuonyesha kuwa kama kafariki pamoja
na matanga kabisa na familia ilionyesha kuridhika
na ile hali ambayo imewatokea na kuona kawaida
kabisa japo machungu hayapingiki kutoka mapema.
Mzee Mambo sasa alitoa madaftari ya mwanae
pamoja na sare za shule akaweka pamoja kisha
akamuita mkewe mna kumueleza jambo kuwa ''Mke
wangu tumeshaondokewa na mwenetu sasa hizi
daftari zake pamoja na hizi sare nahitaji kwenda
kumpa mtoto wa Mama Mengi mjukuu wa
Manyenye ili akatumie mana hatuna jinsi sasa''
Mama Sikitu hakuwa na kipiingamizi kabisa hivyo
aliondoka navyo na kuelekea kwa mzee Manyenye.
Alikaribishwa kwa bashasha sana, alipokaa ndipo
akatoa ule mzigo na kuuweka chini ''Bwana
manyenye hivi huyu mjukuu waako yupo,alafu
kwanza habari za kushinda mana wee acha tu
hatujielewi hapa'' Alikurupuka bwana Mambo sasa
kutokana na ile hali ya kufiwa na mwanae. ''Usijali
kabisa bwana wee hapa wazima naaa huyuuuu
Mengiii mh katoka na mama yake hapa muda
mchache tu kabla hujafika wewe yani mmepishana''
Alionekana bwana mambo sasa akifungua ule
mzigo '' Bwanaaa hapa kuna mzigo huu utampatia
Mengi alizoacha mwenzake mana hata tukisema
tuzichome moto inakuwa uharibifu kabisa ambao
sio mzurii'' Manyenye aliupokea kwa mikono miwili
huku akishukuru sana ''Mhhh nashukuru sana rafiki
yangu mana hapa utakuwa umeturahisishia kwani
mimi pia nafuata ile sera yako bwana lazima
tusomeshe ili waje kusaidia hapo baadae''
walionekana kupongezana huku wakifurahishana.
''Sasa bwana mambo sasa kesho uje hapa asubuhi
sana mana nataka kwenda kuondoa mahindi yangu
kule shambani na wewe upate chochote bwana
sawa'' Wakati huo akianza kumsindikiza ''Haya
usijali ngoja niende kuandaa tenga langu kule kwa
ajili ya hapo kesho ahsante sana'' waliachana na kila
mmoja akaelekea kwake.
Njiani anaonekana SUSU akielekea njiani kutoka
pale kwake huku akiwa anaongea yeye mwenyewe
bila mtu mwingine kuongea nae ''Mh lakini
nafahamu kwa kile nilichokifanya miezi kadhaa
iliyopita wala sio kizuri ona sasa mwanae kafariki
na mimi sijui atanionaje, lakini haina shida ngoja
kwanza niende kwa bwana huyu Sikujua akanipe
tenga langu nikamsaidie Manyenye kesho mana
tenga la muda mwingi'' kumbe alikuwa anaenda kwa
sikujua kuchukua tenga lake ambalo aliliazima kwa
muda sasa, alipofika alimkuta akiwa nje kajiinamia
kana kwamba ana mawazo mazito yanayomkumba,
''Sikujua mzee wangu vipi mbona hivyo?'' alimuuliza
''Hapana mjukuu wangu nimetulia tu hapa'' susu
alikaa pembeni yake ''Haya babu nimekuja kuchukua
tenga langu kesho kuna kazi ya kumsaidia
Manyenye kurudisha mahindi shambani'' Mzee
sikujua alionekana kushtuka sana baada ya
kuambiwa hivyo wakati huo anakumbuka kuwa lile
tenga ndilo ambalo alimuwekea sikitu na kwenda
kumtupa porini. ''Susu ngoja niende kukuchukulia
jingine mana unakuwa na tenga lililochakaa kama
nini jamani'' aliingia ndani na kuchukua tenga jingine
ambalo jipya pia ni dogo alirudi nalo na kumpatia
''Khaa wee mzee vipi tenga langu lile ndilo nalihitaji
sio hili naomba tenga languu hili rudisha'' Alianza
kuwa na jazba bwana sikujua ''Wee kijana vipi
nakupa tenga jipya hulitaki umezoea shida wewe ''
Susu hakutaka kuelewa kabisa ''Yani nakuambia
kuwa nimekufanyia kazi yako kipindi kile
umemdhurumu Mambo sasa hukunipa hela yangu
leo unataka kunidhurumu mali yangu hapa sikubali
mpaka unipe tenga langu''. Hiyo ndio hali halisi
ambayo bwana sikujua ilimkumba na kushindwa
amueleze vipi kijana huyo '' Sawa ngoja kuna vitu
nimevihifadhi cha kufanya njoo asubuhi utalikuta
liko tupo'' aliondoka susu pale kwa sikujua huku
akiacha mikwara ya aina yake 'Mh! hapa itakuwaje
au niende kuangalia kule porini na nikalitoe lile
tenga na asubuhi akija alikute mana kachachamaa
huyu kijana asije akafumbua yaliyofichwa'. alijiuliza
sana ndipo akafunga mlango na akaelekea kwa
bwana Mapato.........
 
SEHEMU YA SITA 06
Endelea...............
Baada ya kuweza kufunga mlango aliongoza njia ya
kwenda kwa rafiki yake bwana Mapato, hatimae
alifika kwake na kuwakuta wakiwa wanakula bwana
Mapato pamoja na familia yake, aliishia kusimama
tu pale al;ipo akiwa hafahamu nini ambacho
anaweza kukifanya, alikuja rafiki yake huyo baada ya
kumuona kuwa haeleweki.
''Vipi mbona umeishia kusimama tu hapo na huji
kukaa'' aliuliza bwana Mapato
'' yani hapa hata hapakaliki kabisa yani
nimechanganyikiwa kabisa hapa unaponiona,''
aliongea bwana sikujua akiwa anataka kukaa chini,
kabla hajafika chini aliweza kuinuliwa na mapato na
kumsimamisha tena
''Aaah haifai bwana mbona unachoka hivyo ndugu
yangu ebu eleza bwana kipi kinakusibu''
Sikujua alivuta pumzi ndefu akimuangalia kwa
umakini sana rafiki yake huku na yeye akimtumbulia
jicho kwa kusubiri aambiwe kitu na sikujua
''Bwana wewe ni rafiki yangu sina haja ya kukuficha,
kama unakumbuka ile kesi ya mimi na bwana
Mambo sasa?''
sikujua aliuliza swali
'' Ndio naifahamu haswaa, ila ngoja tusogee huku
hpa mke wangu asije akasikia si unawajua hawa
wakipataga habari matumbo yao yanajaa upepo
hivyo bila kuutoa hawaoni sawa''
walisogea pembeni kando na pale nyumbani kwake
bwana Mapato ndipo mapato akakumbushia mada
ile ambayo iliwafanya wasogee pembeni.
''Haya niambie sasa hiyo kesi naikumbuka sana''
'' Sawa ile kesi mimi nilimdhurumu bwana Mambo
sasa, yani nilimtumia kijana mmoja aitwae Susu
anayekaa kwa yule mpiga ngoma maarufu bwana
MANUALI, unamjua'' Alimuuliza Mapato huku
akionyesha kwa mkono mahali amabapo anaishi
huyo Manuali na susu
''Hao tena bwana mbona nawapata si yule mzee
mtata mtata kwa dawa zake anazozitumia kutibu
watu na mambo mengine hata kukamata wachawi
hivi'' alimkumbushia Sikujua ili kumhakikishia kuwa
anamfahamu vyema
'' Haswaaaa sasa yule kijana nilimuahidi kumpa
kiasi fulani baada ya kushinda kesi pia
nilimuazimaga Tenga ambalo tumelitumia kumtupa
yule binti sasa kaja analihitaji tenga lake lakini
nilimpa jipya akakataaa katakata, ndipo
nikamuambia aje asubuhi atalikuta''
Mapato alionekana kuwa makini sana kusikiliza
akavua kofia yake ambayo aliiva akanyanyua mkono
wake akachagua kidole cha kati kukuna kichwa
chake kilichojaa mvi za kutosha, hii yote ilikuwa
kuonyesha jinsi gani mambo yalivyokuwa magumu
kwa pande zote.
''Sasa, hilo tenga mpaka alitake hilo lake na
akakataa jipya kwa nini pia alazimishe hivyo?""
''Mhhh wee huna taarifa kuwa kesho asubuhi kuna
kazi ya kuondoa mahindi kwenye shamba la bwana
Mnyenye ''
''Aaaa kweli hata mimi hapa alikuja asubuhi kunipa
hizo taarifa sasa wewe umeamuaje?''
aliuliza mapato kuhusu uamuzi wa sikujua juu ya
hilo swala.
''Mh! mimi nimeona ni bora turudi kulekule ili
tukalichukue lile tenga''
Walikubaliana vyema kuhusu swala la yeye na
bwana Mapato kwenda polini kuchukua tenga la
kijana Susu ili lisije kuzua tafrani.
Majira hayo upande wa bwana Mambo sasa majira
kama saa tano hivi za usiku yeye akiwa kalala na
mke wake, pia usingizi ukiwa umewakolea vilivyo,
ilisikika sauti ya binti wa kike ikiita ''Babaaa,
babaaa, Mamaa,Mamaaa, mbona mnaniachaa
nateketea bado sijafa mamaaa''
Bwana Mambo sasa aliamka ghafla na kuangaza
huku na kule kijasho kikimtoka, alimgusagusa
mkewe ambae alikuwa bado usingizini, "Mke wangu
amka haraka amka kwanza usikie" Mama huyo
aliamka akiwa na lundo tele la usingizi alifuta
baadhi ya ukungu ambao ulimfanya kutokuwa sawa
kwa kuona ''Nini mume wangu''
''Mke wangu nimesikia sauti ya mwenetu Sikitu
akituita''
Mama sikitu alikuwa kama mtu ambae kama
katoneshwa kidonda hivi '' Mume wangu acha hizo
kauli naumia moyoni, itakuwa ni ndoto hizo
zinakusumbua sikitu anakaribia mwezi tangu apotee
leo uniambie kakuita alafu usiku huu kweli''
Baba sikitu alimtuliza kidogo mkewe kisha pakawa
kimya kabisa ndipo kauli ya mkewe kuwa ilikuwa ni
ndoto likasimama kidete ndipo wakalala tena.
Safari ya kwenda polini ilikuwa imetawala tayali
katika akilini mwao, walisubili mpaka ilipofika
majira ya saa sita mwezi umetanda vyema ndipo
wakaanza mwendo taratibu sana na baiskeli yao.
Wakiwa njiani wanamalizia nyumba za kijiji cha
bwawani moja ya nyumba ilisikika ikifunguliwa
mlango japo hakujulikana ni nani. walitembea kwa
haraka sana kumuepuka huyo mtu ambae anatokeza
kwa nje, walitembea kwa muda fulani ndipo
wakafika eneo la tukio.
Upande wa huku watokako nyumba jirani na Bwana
Sikujua ilionekana kuungua moto hivyo kelele
zilianza kusikika
''Jamani weeeeeee nyumbaaaaaa motoooooooo
njoni mtusaidieeee''
Zilisikika sauti hizo zikiomba msaada kwa majirani
kweli walijitokeza kwa wingi sana huku wakisaidia
kumwaga maji juu ya paa ya nyumba hiyo kwani
iliezekwa kwa nyasi isipokuwa ya bwana Sikujua
ilikuwa ni ya bati'
Upande wa Mapato na Sikujua walishtuka bada ya
kusikia kelele hizo pamoja na moto ulioambatana
na moshi ukitanda kwenye kiza kizito kilicho
shindwa kufichwa na mwezi ulioanza kufifia
kutokana na dalili za wingu kutanda angani,
''Mapato angalia kule tunakotoka ule si moto na
nadhani nyumba itakuwa inaungua pale''
''Haswaa itakuwa hivyo sasa pia hizoooo kelele za
watu zikishamili sasa je hawatotushangaa sisi
wakati tunarudi''
''Hapa itabidi tufanye haraka hivi lile tenga ile siku
tulilitupia wapi?''
walianza kulitafuta bila kuwa na mafanikio lakini
walibahatika kukuta mkeka na kamba ambazo
walizitumia kumfungia baada ya kugundua kuwa
wameua,
''Jamani hivi hii si ndio ile kamba ambayo tulitumia
ile siku, kuna kamba tupu hapa na tenga hakuna
jamani''
walihangaika vya kutosha sana bila kufanikiwa
kuliona tenga walilolikusudia,Kila mmoja kwa
upande wake alichoka sana kiasi kwamba
walitamani ardhi ipasuke wasionekane au wawe na
uwezo ambao ungewawezesha kuliona tenga la
kijana Susu.
''Bwana sikujua hapa cha kufanya turudi alafu tupitie
pale nyumbani uchukuie kiasi cha fedha ambacho
kitasaidia kumpa huyo kijana na hilo tenga lako
jipya najua hawezi kukataa mbele ya fedha''
waliamua kurudi majira hayo ya usiku sana ndipo
wanakutana na baadhi ya watu wakitokea kwenye
tukio. Waliona hatari itawajia ndipo wakapitia
bwawani kabla ya kwenda huko kwao katikati ya
kijij walibahatika kupata chombo cha kubebea
wakateka maji na kuanza kukimbiza baiskeli yao
huku na wao wakikimbia walifanikiwa kukuta watu
bado wakihitaji maji bado hivyo iliwapa kunusurika
na kutambulika wao wanatoka wapi,
Ndipo alionekana mama Mengi akimfuata mzee
sikujua na kumuuliza
''Wee mzee wewe wakati watu wanahangaika kuzima
moto huu nyumba yako ilikuwa imefungwa mpaka
sasa hivi ulikuwa wapi?''
Swali hilo lilikuwa gumu lenye kuchoma moyo
ulioficha mengi ya siri kubwa sana; Alishindwa
kujibu zaidi aliondoka pale lakini bado aliendelea
kumfuata huku akisimamia msimamo wake wa
kutaka kujua yeye aliyekaribu kashindwa vipi kutoa
msaada hata wa kuondoa vitu mpaka matatizo
yanamkuta mwenye hiyo nyumba kwa kushindwa
kuokoa hata kitu kimoja.
''Naomba uniambie sikujua unafahamu kuwa wewe
una tabia mbaya sana siku hizi wewe mzee wewe''
Aliona sasa dharau zinazidi
'' Weeee mwanamke wewe kuwa na adabu hapa
tupo kwenye matatizo unafahamu baada ya kuona
hii dalili mimi nilikwenda kuwaita watu waje
kusaidia unajua kuwa huyu mzee mapato taarifa ya
hapa kapewa nani au unatukosea adabu tuu''
Mama Mengi hakuwa na neno aliona kama
kaumbuka lakini kichwani mwake alionekana
kumtilia shaka sana Mzee Sikujua.
Asubuhi na Mapema sana watu walijiimia kumpa
pole aliyekutwa na matatizo ya kuunguliwa na moto
nyumba yake pia walijiandaa akiwemo Mambo sasa
na mke wake. waliongozana shambani kwa bwana
manyenye. Kazi ilianza kuondoa mahindi na kuweka
sehemu moja ili baadae waweze kubeba kupeleka
kwa Manyenye. Mzee Mambo sasa alionekana
akiwa na bwana Manuali karibu huku kila mmoja
akishika mstari wake wa kuondoa mahindi
alisimama kidogo bwana Mambo sasa huku
akijiuliza
''Mh! ile ndoto au itakuwa kweli ila ngoja nimueleze
bwana Manuali labda anaweza kunipa mwangaza
kidogo''
Alimsogelea pale alipo bwana manuali ambae ni
mzee kidogo wa makamo alimsalimia kisha
wakaanza mazungumzo
''Bwana manuali nipo hapa nina shida moja kubwa
inayonisibu mpaka sasa'' Aliongea Mambo sasa
''Wewe tena usijali ongea nakusikiliza ''
''Bwana tangu nifiwe na mwanangu au kupotelewa
na mwanangu siku nyingi zimepita hapa"
Mzee Manuali alionekana kuacha ile kazi kidogo na
kumgeukia Mambo sasa na kumsikiliza vyema
"Haswaa nafahamu ndugu yangu"
"Sasa jana usiku kuamkia leo hii nilipo hapa nilisikia
sauti ya Sikitu mwanangu ikiniita mimi pamoja na
mama yake ikisema ""Babaaa,Babaaa
Mamaa,Mamaaa mbona mnaniacha mimi sijafa
babaaa"" alafu ilikuwa inamalizia kwa kilio kidogo
sasa sijaelewa mpaka sasa hivi bwana Manuali"
Mzee manuali alishika kidevu chake akitafakari nini
aseme kuhusiana na hilo swala alilonalo kwa rafiki
yake.
"Sawa nimetambua nini nitakusaidia cha kufanya
njoo jionijioni hivi leo tufanye dawa fulani na
maelezo kuhusu ilo pia njoo na mke wako" Mambo
sasa alishukuru sana
Wakati huo anaonekana Mapato kwa mbali
akiwashuhudia wanachokiongea alionekana kutikisa
kichwa huku akikunja uso ndipo akatokomea ndani
ya shamba ilo kujichanganya na watu wengine
 
SEHEMU YA SABA 07
Endelea.................
...Bwana Mapato alijichanganya kwenye kundi la
watu huku akiwa anaangalia nyuma kana kwamba
kuna mtu ambae anamtafuta au kumkimbiza,
alitwikia tenga lake huku akihitaji kuondoka lakini
kabla hata ajafanikiwa kuondoka ndipo kijana susu
aliweza kumfikia pale alipo huku akijishika kiuno
alichopoka mara moja na kwenda kumshikia lile
tenga lake lililojaa mahindi alishusha chini wakati
bwana mapato anahitaji kupandisha juu ya kichwa
chake, alimshangaa sana ndipo akashusha chini.
'' haya kilichokutuma uje unitue mzigo huu ni nini?''
Aliuliza bwana Mapato kumuuliza kijana huyo
ambae alikuja pale kwa ajili ya kumtua mzigo wake
badala ya kumsaidia kupandisha kichwani mwa
bwana mapato.
''Bwaana mzee sio kwamba nimekukosea heshima
hapana ila shida yangu kujua kuwa bwana sikujua
yuko wapi?"
Aliuliza swali ambalo lilimfanya Mapato kuangua
kicheko pale alipo, alipomaliza kucheka akamuuliza
swali
''Sasa kijana habari za sikujua unaniuliza mimi hapa
je kwake hukwenda?''
''Mimi sitaki kujua habari za kwenda kwake au
kutokwenda nilikwenda asubuhi lakini sikumkuta na
wakati tuliagana kuwa asubuhi ya l;eo nitalipata
tenga langu''
Alionekana kuongea kwa jazba sana kijana susu
huku akitumbua macho yake yaliyokuwa makubwa
kama ya paka
''sasa mimi unaniuliza nalala nae?''
''Wee si ndio rafiki yake bwana sasa mwambie
nikimaliza kazi hii nakuja kwake asiponipa tenga
langu sitojali yeye ni nani atanitambua''
aliondoka pale alipokuwa na bwana Mapato
akimuacha anafuta jasho kwa uchovu alioupata,
alimuangalia sana kijana huyo mwishowe akafyonya
tu na asijue amfanye nini kwa wakati ule.
''yani huyu kijana ngoja cha moto atakiona yani
kanichefua sana sasa habari za sikujua na mimi
wapi na wapi, tena alafu huyu sikujua ipo siku
nitamchoka mana naona naingia kesi ambayo
hainiusu kabisa ''
Majira ya mchana kila mmoja alikusanyika
nyumbani kwa mzee Manyenye, baada ya kumaliza
kazi ya kukusanya mahindi ambayo yalikuwa
shambani kwake. Kwa upande wa akina mama
walikuwa wakimaliza kazi ya upishi ili kuwaandalia
wale wote ambao walishiriki vyema sana katika
swala la kuondoa mahindi hayo shambani kwake.
Upande wa akina mama alionekana Mama Mengi
ambae waliambatana na mama wengin e pamoja na
mabinti kadhaa walikuwa na mazungumzo ya hapa
na pale.
''Jamani wanawake wenzangu sasa hivi tuwe makini
sana mana swala la kupotea watotot wetu sio zuri
tena hata ikibidi tuwe nao karibu sana''
Kauli hiyo iliwafanya hata wengine waweze kuacha
shughuli zao na kumgeukia mama Mengi ambae
alionekana kutopendezwa na matukio ambayo
yanajitokeza.
''Mh! ni kweli kabisa ila kuhusu huyu Sikitu jamani
inatia hata huruma yani kupotea wakati yeye alikuwa
ni mtoto mtiifu kwa wazazi wake jamani''
Mada hiyo iliwaumiza wengi sana lakini hata mama
mengi alionekana kuwa na mawazo sana, ndipo
mama mwengine ambae alikuwa kama rafiki yake
alimshitukia na akataka kumuuliza
''Mama Mengi, mbona kama unataka kulia kuna
jambo gani''
''hapana bwana dada wee ebu andaeni vyombo
huko tuwapelekee watu wananjaa sana''
Chakula kilikuwa tayari na ndipo sahani zilipelekwa
kwa wanaume. Wakiwa wanakula kijana susu
aliangaza macho yake akafanikiwa kumuona mzee
sikujua akiwa moja ya kundi la watu ambao
walikuwa wanakula, alikula harakaharaka ili aweze
kumuwahi.
Ilitoka sauti moja ambayo iliwashtua sana sauti hiyo
ilitoka kwa Mzee Mambo sasa ikisema
"Jamani mnakula mkiwa na furaha sana lakini mimi
chakula hakipandi hapa"
Alisema bwana Mambo sasa
''Sasa kwa nini tena iwe hivyo na wakati tupo hapa
pamoja kuna nini kimekufanya useme hivyo au
chakula hakijapikwa vizuri"
Sauti hiyo iliwafanya watu watulie sana na kusikiliza
maongezi ambayo yalikuwa yanatawala kwa muda
huo
"Jamani mtoto wangu sikitu jamani yani wanakijij
wote tumeshindwa hata kumuona kweli jamani aaah
mwanangu sikitu huko uliko bado nakupenda ssna
mwanangu ona ninavyohangaika hapa sina furaha
kabisa"
Baadhi ya watu walinyanyuka na kwenda kumpa
matumaini na pole kuhusu swala zito kama hilo,
fahamu kuwa ni bora kufiwa kwa kuwa unajua
hutomuona tena lakini si kupotelewa ambako huna
uhakika kama yupo hai au kafariki ndicho
kilichomtokea bwana Mambo sasa.
''''Jamani tena naombea akijulikana kama kuna mtu
kijijini hapa ndio kafanya hivyio haki ya mtungi
shahidi kata awe mtu au mnyama akijulikana mimi
najitolea namchinja na mimi ""
Kumbe lile swala liliwauma wengi sana kiasi
kwamba walichangia kwa kuhitikia kuwa sawa
kabisa. Walimtuliza hatimae chakula kiliisha na watu
wakatawanyika lakini Mzee manyenye akamkabidhi
mahindi ya kutosha kama alivyomuahidi hapo
mwanzo kabla.
Majira ya jioni hivi bwana Mapato na sikujua
walikutana na wakawa wanaelekea shamba la
bwana Mapato ambalo alikuwa analimisha kwa
vipimo shilingi elfu mbili.
''Bwana sikujua wewe ni kama kaka yangu kwani
tunatokea ukoo mmoja tu, sasa nina jambo ambalo
nahitaji kukushirikisha kwa sasa ili uone unaweza
kufanya nini"
Sikujua alikuwa anatikisa kichwa kuashiria kuwa
yuko tayari kwa lolote.
''Sasa nikiwa kule shambani nilimsikia kwa masikio
yangu Baba sikitu na bwana Manuali wakiongea
jambo"
Alionekana kushituka sana baada ya kusikia hivyo
"Nini tena walichokuwa wakiongea"
Sikujua alikuwa na wasiwasi mpaka akawa
anasimama
"Kha! unasimama nini sasa twende nikuhadithie"
Alimuangalia huku akimuimiza waendelee na
mwendo
" Leo hii bwana Mambo sasa wanakutana majira ya
jioni lakini japo sijajua wanakutana kwa lengo gana
zaidi, lakini kama unaenda kwa manuali hakuna
jingine zaidi ya tiba" Hapo alinyong`onyea sana
sikujua kiasi akabaki kusimama akifikilia
""Sasa hawatakwenda kwa ajili ya lile swala lakini,
alafu mimi sikufanya kusudi ujue,""
"'weee mjinga hukuwaona wazee wenzako au hata
akina mama kama yule Mama Mengi ukaishi nae,
yani tangu mkeo kafariki umekuwa na tabu pamoja
na tamaa za kishetani kabisa sasa hata kama
atakwenda kwa ajili ya hilo swala wewe utafanya
nini?'"
Sikujua aliduwaa halijua ajibu nini pale
"Ukiacha hilo yule kijana akaja kunipiga mkwala
tena na mimi"
"Kijana yupi?"
"si huyo anayekudai tenga lako"
Walisimama kwa muda kidogo huku wakipitiapitia
shamba hilo, Sikujua alionekana kupata wazo
muhimu sana ndipo akataka kumshirikisha m
wenzake, lakini alikuwa na hisia mbaya na bwana
Mapato.
"Sasa bwana Sikujua mimi nataka kukusaidia jambo
fulani......"
Kabla hajamaliza aliweza kukatishwa na sikujua
ambae aliomba kumueleza jambo fulani,
''Au.....mimi ninawaza kuondoka ndani ya kijiji hiki
kabla hata hayajafika mbali mana nahisi haja zote
kunitoka kila siku zinapokuja" Alicheka sana bwana
mapato baada ya kusikia kuwa sikujua anataka
kuhama pale kijijini kukimbia ile kesi inayoanza
kufufuka taratibu. ""Wewe aliyekuambia kuwa
kukimbia kesi ndio kumaliza kesi nani, jikaze ujue
unalimaliza vipi, kwanza tukakague kule mpaka
tuhakikishe kuwa hatuoni hata alama moja ya
kuonyesha kuwa sikitu yupo au laa''
Sikujua alionekana kukubali lakini kwa nafsi yake
ilionekana kuwa na kipingamizi kikubwa sana juu ya
maamuzi ya kubaki pale. Waliondoka pale na kurudi
kijijini wakiwa wako makini sana, hadi sasa maisha
ambayo aalikuwa anaishi bwana sikujua ni ya
wasiwasi sana. walipanga kufika kwanza kwa bwana
Manuali ili kwenda kumuelza kuhusu huyo mjukuu
wake ambae anawatia jambajamba kila siku
zinapokwenda, walifika pale wakiwa na wasiwasi wa
kumkuta bwana Mambo sasa lakini haikuwa hivyo.
Waliodikia na kukaribishwa ndani, hawkautaka
kuingia ndani hivyo walimuita nje kwa mzungumzo
zaidi.
"Haya karibuni sana mana nilikuwa ndani humo nina
mgeni ila haina shida tuendelee nawasikiliza sasa"
Waliposikia kuna mgeni walishtuka sana japo
hawakujua rasmi kuwa ni nani, walijua kuwa ni
bwana Mambo sasa kwa hali yeyote ile
walimuomba bwana Manuali wasogee pembeni.
"Manuali, hapa tunashida moja,"
Walimueleza manuali aliyeonekana kushangazwa na
ujio wao huo, "Mh! haya nawasikiliza":
"Mmmmh tunashida kwamba mjukuu wako susu
alinipaga tenga lake, sasa lile tenga limeliwa na
mchwa na yeye alivyokuja kulihitaji nilishindwa
kumuambia kuwa li,meharibika kwani alikuwa na
hasiira sana, "
"kwa hiyo mlitakaje labda"
Aliuliza bwana Manuali
" Ehee ninachokihitaji tumpatie tenga jipya pamoja
na fedha kidogo ili tumalizane na hiyo kesi yake".
alivuta pumzi bwana manuali baada ya wao
kumaliza mazungumzo yao. "Jamani kuhusu huyu
susu mimi mtakuwa mnanishirikisha kwa makosa tu
kwani mambo yake anayafanya yeye kama yeye
ndio maana akajenga nyumba yake ile kwa hiyo
mkimuhitaji yeye mumuendee pale"
waliishiwa nguvu kabisa kwani matarajio yao ni
kuwa mzee huo angeweza kuwasaidia kwa namna
moja ama nyingine.
"Sasa utanisaidiaje ndugu yangu" aliuliza sikujua
"Labda tufanye kesho mapema sana
nitamsimamisha shughuli zake ili niweze kuongea
nae kwanza na nyinyi mkifika kesho tutayamaliza".
Walimaliza ndipo wakaondoka zao, kwa kuwa
ilikuwa jioni sana ambapo usiku ulikuwa unaingia
zaidi, Mzee manuali aliingia ndani, kumbe mule
ndani kulikuwa na bwana Mambo sasa akiwa ana
mazungumzo na Manuali. "bwana samahani
nilikuwa naongea na sikujua hapo nje haya
tuendelee na mazungumzo yetu"
Manuali alianza kwa kumueleza kuhusu lile tatizo
lake alilo nalo. " Ehee hapo kinachotakiwa kesho
mapema kama saa za mchana hivi nakuja kwako
kufanya dawa fulani ambazo zitamfukuza kama
atakuwa mzimu au ni ndoto za ajabu basi
zitaondoka kabisa, lakini hii dawa utaondoka nayo
utaiweka chini ya kitanda chako yani ulalie kichwani
na hii nyingine utampatia mkeo najua haitojitokeza
tena"
Aimkabidhi zile dawa kisha akamruhusu aende
nyumbani kwa kuwa ni usiku sana. Majira ya usiku
kama saa sita hivi, nyumbani kwa sikujua , mzee
huyo hakuweza kulala kabisa kwani alihisi kuna vitu
vinamuangaisha sana, ndoto za ajabu ambazo
alishtuka sana, mwishowe aka amka kabisa kwa
kukosa usingizi.
"Mh! Mbona kwenye ndoto namuona Sikitu, akiwa
ananikalipia kwa vitisho ina maana ni mzimu au
bado hajafa, mh lakini hapana hii ndoto inanitia
shaka"
Alishindwa kulala kabisa ndipo akakaa kwenye
kitanda chake huku akiwa anasikiliza milio ya
wadudu tu huko nje.
Ghafla sauti iliyokuwa ikitokea nje ikilalamika huku
ikitoa lawama kali sana, Sikujua alishtuka, ndipo
akaishikilia shuka yake vyema kutaka kujifunika
gubigubi,
""Aaah...Aaah...Mbona ulinidanganya babu, mbona
umeamua kunitesa na kunifanya niwe hivi baridi kali,
linanipiga nifungulie hata mlango, uliamua
kunitendea haya ili niwe hivi...ila ipo siku...."
Sikujua aliweweseka kweli huku kijasho kikimtoka,
alifikia hatua hata kuachia haja ndogo pale alipo na
usiku ulikuwa mkubwa sana kwake, alianza kulia
japo ni mzee lakini sasa yamemkuta na hakuamini
kabisa. Aliinuka na kuchukua meza pamoja na kinu
ambalo linatumikaga kutwangia nafaka, akaliweka
kwenye mlanga huku akitetemeka,
Asubuhi na mapema aliamka na alikuwa wa kwanza
kabisa kuamka, alifungua mlango ndipo alikuta
damu zikiwa zimetawala pale mlangoni, "
Ieeeewiiiie" alipiga yowe kali wakati huo Susu kama
kawaida yake alijiimia kwa bwana Sikujua kudai
tenga lake kama kawiada, alimkuta akiwa mlangoni
akizishangaa zile damu.
"Eeeeh babu jana tulikosana haya niambie liko
wapi?"
Hakujibiwa kabisa kwani yeye alikuwa anaangalia ile
damu tu. Alimuonyesha kwa mkono tu pale huku
akiwa anarudi nyumanyuma,
"Nini unachonionyesha?" Aliuliza susu "Susu hivi
huoni hizi damu, hapa mlangoni"
'Damu ziko wapi?" aliendeleaa kuonyeshwa lakini
susu alienda hadi pale kwenye mlango na
kukanyagakanyaga
"Hapa hakuna damu wapi angalia". Zamani sana
bwana sikujua alikuwa keshakimbia kuelekea kwa
kwa Mapato huku akipiga yowe
""Damuuuuu, damuuuuuu jamani damuuu". mapato
alishangaaa damuuu kivipi damu jamani,.
Alimuona rafiki yake kama mtu aliyechanganyikiwa
kabisa, sikujua alimuonyesha kuwa kwake kuna
damu na hataki hata kusogelea......
 
SEHEMU YA NANE 08
Endelea.............................
Ukimbiaji ambao alikimbia bwana Sikujua haukuwa
wa kawaida kabisa, aliweza kumshangaza hata rafiki
yake Mapato kwa ile kasi ambayo alikuwa nayo.
Hata alipoulizwa kuhusu ile damu ambayo alikuwa
anaitamka hakuweza kusema sentesi nzima
akaeleweka, alijisemea mwenyewe mapato kuwa
rafiki yake atakuwa kachanganyikiwa na si bure
kabisa. Alijitahidi kumtuliza ndipo mkewe bwana
mapato akaingia ndani na kuchukua kikombe
kilichojaa maji na kutoka nayo ili aje kumpaa
sikujua anywe.
yale maji yalisukumwa na mapato huku akifoka
kuwa haitajiki kupewa maji sasa hivi unaweza
kumuua, subiri apumzike kwanza. Wakati
wanaendelea kupumzika ndipo anajitokeza susu na
yeye akiwa kakunja sura yake akimaanisha kujawa
na hasira sana. "Mh! mtu wako huyo anakuja"
Alijisemea mapato, sikujua huwa anakosa raha sana
pindi anapomuona susu. Susu alipofika alisalimia
wote na kukaa kwenye benchi karibu na mapato.
"Mzee habari za asubuhi kwanza pili huyu bwana
sijamuelewa jinsi alivyotoka pale kwake". Alisema
susu, "Bwana wee yani hata mimi sijaelewa kabisa
kaja hapa anaweuka tu ndio tunamsubili apumzike
kidogo"
"Mh! haya bwana ila nilimkuta pale kwake, nilikuwa
na lengo la kuchukua tenga langu sasa nikamsikia
damuu, damuu nikashangaa sana ndipo nikafika
mpaka pale mlangoni sioni chochote ndipo
nikamuona kakimbia".
Kufikia hadi hapo susu alikuwa haamini kabisa,
ndipo mapato akaingia ndani na akatoka na tenga
kubwa na mkononi akiwa kashika kiasi cha fedha
mkononi.
"Sasa baba tumalizane hili tenga utalichukua alafu
hiki kiasi tunakiongezea hapa juu ili tumalizane
kabisa umuache mzee wa watu apumue wewe
mwenyewe si unamuona alivyo".
Susu alishika na kile kiasi cha fedha akakitia
mfukoni. akamuangalia mapato kisha akaanza
kuondoka "Ahsante yani hapa nimekubali basi tu ila
kuanzia leo asije kuniazima tena kitu changa, pia
akumbuke kesi niliyomsaidia lazima anipe hela
yangu baada ya mavuno kufika"
Aliondoka pale na kuwaacha wazee hao
wakiendelea na shughuli zao. Baada ya muda kupita
ndipo sikujua alikuwa na hali nzuri na akaanza
kumsimulia kilichotokea, wakati huo wakiwa wawili
tu mke wa mapato alishatoka. "Haya niambie rafiki
yangu nini kilichotokea"
"daah yani kwanza usiku nilishtuka baada ya kusikia
nikiitwa jina langu na binti nje, nilipoamka ndipo
nikamsikia kwa masikio yangu mawili Sikitu binti
wa mambo sasa akilalamika kwa kunilalamikia
mimi, isitoshe vitisho navyo vilikuwa vingi...nilipoa
mka asubuhi ajabu sasa ndipo nikaikuta damu
mlangoni na wakati huo susu anaingia yeye
akasema damu hiyo haioni ukweli nilijikuta nakimbia
huku sijielewi".
Mapato alimsikiliza kwa makini sana. "Sawa
nimekuelewa hilo linawezekana kwani baada ya
kufanya ule unyama na ikiwa kama alikufa kweli
yule binti basi, unatakiwa kuoga dawa aina ya
makombe yani uandikiwe makombe kisha yatiwe
maji alafu uoge kuondoa nuksi na mizimu yake isije
kukufuatilia tena"
"Fanya hivyo kabisa mana hapa nimekoma kabisa
na sina hata hamu"
Upande wa bwana Mambo sasa na mkewe wakiwa
barazani kila mmoja na majonzi yake japo muda
sasa tangu wapotelewe na mtoto wao. Mambo sasa
aliamua kuvunja ukimya ambao ulikuwa umetawala
kwa muda mrefu sana alimuita mkewe na
kumueleza habari ambayo baadae ilionekana
kuzuwa utata na malumbano baina yao.
"Mke wangu, kuna jambo nataka kukuambia na
linahitajika kulifanyia kazi muda huu"
Mkewe alistajabu kwanza
"lipi hilo mume wangu" aliuliza mama sikitu
"Nafahamu muda mwingi sana tangu tutoke
nyumbani SHIMOMO, kutokana na lile swala letu
mpaka wakatufukuza pale kijijini"
Mama sikitu alitulia kwanza
"Ndio nakumbuka ehee" Alionekana kuwa na uhitaji
wa kutaka kipi kitakachoendelea
"Usiwe na jazba mke wangu nia yangu kuwa tangu
tupotelewe na mwenetu hawana taarifa kabisa juu
ya hili swala pia sioni sababu ya kuendelea kuishi
kwenye miji hii ya watu hali hatuna furaha pia
hakuna ushirikiano ninachokihitaji sisi turudi kule
kijijini"
Mkewe alitikisa kichwa huku akipinga kabisa swala
la kurudi SHIMOMO, japo haikujulikana huko
shimomo kulitokea nini mpaka wao wafukuzwe na
wakakimbilia huku kijiji cha BWAWANI. "Hapana
kabisa baba sikitu, kwanza siamini kama mwenetu
kafa hapana pili sitaki kurudi kule ambako mimi
walinikataa nisiolewe na wewe na wakatufukuza kwa
kututishia kabisa kwamba tukiendelea mahusiano
yetu watatuua hapanaaa"
Ilimbidi Mambo sasa atumie akili ya ziada
kumshawishi mkewe ili akubaliane na yeye kwenye
swala hilo na hatimae mama sikitu alikubali.
Mzee Mambo sasa aliondoka muda huohuo na
kwenda kwa bwana Manyenye kumpa taarifa ya
kuondoka pale yani kuhama kabisa. "Bwana
manyenye, nimekuja hapa kukupa taarifa kuwa nina
hama kabisa hapa kijijini naelekea shishimo
nyumbani kwetu"
Manyenye alisimama kwanza huku akishika kiuno
chake kilichchoka kwa ajili ya uzee wake " Eeeeh
haya mbona mapya tena unaondoka alafu ndio nini
sasa"
"Ndo hivyo tunaenda kuhangaikia maisha sehemu ya
kwetu maana hapa hatuna kitegea uchumi sasa
nisije kuwa mzigo wa kijiji cha watu" Alisema
Mambo sasa,
"kuwa mzigo vipi tena na wewe mimi
nimeshakuzoea bwana kama kitegea uchumi nina
mikorosho yangu pale miambili na shamba la kule
juu kuna mikorosho themanini vijana wangu wavivu
na mikorosho inaungua tu moto mwaka hadi
mwaka sasa ni bora nikukabidhi ile themanini
uifanyie kazi kwa miaka tano najua utakuwa
umeshajijenga tena"
Mambo sasa alifikilia sana kabla hata ya kujibu
mana asije kukurupuka.
"Ahsante sana nashukuru sana ila nipe siku ya leo
na kesho nakuja kukupa jawabu zuri ngoja
nikaongee na mama watoto tujue tunafanyaje
kuhusu ilo" Bwana Manyenye alimuomba sana
asiondoke na kama uchumi isiwe sababu kabisa
yeye atamsaidia.
"Bwana fanya hivyo bwana kesho uje unipe jawabu"
Aliondoka pale na kumfuata bwana Mapato lakini
kwa bahati nzuri au mbaya alimkuta na sikujua
ambae kipindi cha nyuma alimdhurumu mikorosho
na yeye, alisalimia wote mana hata mambo ya
sikujua alishayasahau yani aliyaacha kama yalivyo.
"Bwana mapato nashukuru nimekukuta, lakini kuna
jambo ambalo tuliliongea kuhusu uniazime
mikorosho yako kadhaa unakumbuka?"
Mapato alikuna kichwa chake kwanza " Aaa hilo
nalikumbuka lakini kwa sasa hali ngumu labda
tufanye msimu ujao kwanza"
"Sawa ila sikuja kwa nia hiyo lengo kuja kuwaaga
siku zijazo ninaondoka hapa kijijini naelkea
nyumbani kwetu"
Mapato alishusha pumzi kwanza
"Sawa hilo ni jambo jema kwanza ni bora hata
ukapote mawazo ya kufiwa na mwanao sikitu mana
hata sisi tunahuzunika sana". Mambo sasa ndipo
akagundua kuwa kuna watu hawampendi kabisa na
wapo watu ambao wanamkubali aendelee kuishi
pale.
Mpaka jioni alivyorudi nyumbani alikuwa na
majawabu kamili ambayo yalimpa uhakika wa
kufanya maamuzi. Hakutaka kuchelewa alielekea
kwa bwana Manyenye na kumpa taarifa kuhusu
msimamo wake.
"Nimekubali kuendelea kuishi hapa lakini nitaenda
kijijini kwanza kwa siku tatu nikirudi nitakuja
kukuambia "
"Haina shida bwana mambo sasa wewe nenda
ukirudi utakuta huku nimeshakuandalia mambo yote
yako sawa"
Upande wa mwenyekiti anaonekana jamaa mmoja
hivi akiwa na shida ya kuonana na mtu mmoja pale
kijijini
"Kijana unaitwa nani?" Mwenyekiti aliuliza
"Mimi naitwa, KATUNJE" kijana huyo alijibu kuwa
anafahamika kwa jina la katunje.
"Katunje unatokea wapi?" Mwenyekiti aliuliza tena
huku akiandika mahali fulani iliyoonekana kama
sehemu ya kumbukumbu.
"Mimi natokea MLIMALONDO" alijibu pia kuwa
anatokea mlima londo.
"sawa hapa umekuja kwa lengo gani hapa kijiji
chetu kizuri cha BWAWANI"
"Baba hapa nimekuja kumtafuta ndugu yangu
anaitwa bwana CHITO"
Mwenyekiti alifungua kwenye orodha yake ya
wahamiaji wa pale lakini hakupat bahati ya kumpata
huyo mtu anayejulikana kwa jina la CHITO
aliendelea kufungua lakini hakulipata.
"Kijana hapa hakuna jina la mtu anayejulikana kwa
jina hilo na hatuna utaratibu wa kumpokea mgeni
bila kumuandikisha, mgeni wa mwisho hapa alikuwa
mzee ambae alikuwa na mkewe anaitwaa MZEE
MAMBO SASA basi hakuna mwingine.
kijana chito alishusha pumzi akaona hapa hatoweza
kupata msaada wa nguvu bila kufanya jambo la
kumshawishi mwenyekiti huyo.
"baba samahani huyo mambo sasa hata mimi kweli
simfahamu ila naomba nikae siku tatu tu nihangaike
hapa kijijini ili nimtafute mwenyewe nikibahatika
kumuona nitakuja kukuambia na nisipofanikiwa
basi,
Alikataliwa kabisa kupewa nafasi ile ya yeye kuishi
pale kwa siku tatu. Hivyo aliombwa aondoke pale
ukweli alifukuzwa kabisa kama mwizi, mfukuzaji
mmoja wapo alikuwa susu ambae alipewa kazi
hiyo. kijana Katunje aliondoka na kukimbilia sehemu
ambayo hakuifahamu lakini hakutaka kwenda mbali
na hapo kijijini, alifika porini sehemu iliyokaribiana
na msitu, alihisi kwa mbali kama kuna maji
yanatembea hivyo aliona vyema kuyafuata na
kwenda kujimwagia kidogo tena hata kunywa,
wakati anatembea alibahatika kuliona tenga ambalo
lilikuwa na damu pembezoni aliliacha lakini
alivyozidi kutembea alizikuta nguo za mtoto wa kike
zikiwa nazo zimegandia damu ya muda mrefu.
Aliachana nazo huku akiwa na wasiwasi sana
alitembea kwa utaratibu wenye umakini wa hali ya
juu kuhofia majanga ambayo anaweza kuyaona,
alisita kidogo akaona vyema arudi nyuma
akachukua tenga na zile nguo, aliendelea mbele
kuyafuata yale maji alipofika akaona bwawa kubwa
sana lenye maji mazuri ya kuvutia pia haikuonyesha
dalili ya watu kufika pale, aliliweka chini lile tenga
alitaka kuanza kunawa lakini alipopiga jicho
pembeni kwa usalama alimuona binadamu
aliyekondeana sana akiwa kalala kwenye moja ya
poli pembezoni mwa bwawa, alisimama akaenda
taratibu, alimuomba mungu kwanza amsaidie isije
kumdhuru kwa lile alifanyalo.
Alipomfikia alihisi tu kama moyo unafanya kazi
lakini mwili haufanyi kazi haoni, mbavu zinaonekana
kakondeana zaidi ya maelezo, alifanya harakaharaka
kuchukua tenga lake aliloliokota na kuchukua zile
nguo na kuvisha lakini zilikuwa kama zinamfunika
tu, alimuweka kwenye tenga na kulitwikia kichwani,
alianza kunyoosha njia ya kwenda kijijini akiwa
njiani alisikia sauti ya mwnamke ikisema " Tafadhali
usinipeleke huko"
Alihisi kama ni mawazo tu aliyokuwa nayo lakini
alijiuliza yale mambo aliyofanyiwa na mwenyekiti
inawezekana huyu binti kafanyiwa jambo,
Aliamua kurudi na kutokomea nae msituni safari ya
kwenda kwao MLIMALONDO. Alitembea umbali
mrefu kiasi alianza kuchoka mpaka kiasi cha
chakula alichonacho alimlazimisha kumlisha yule
kiumbe ambae hata umbile alilipoteza la usoni,
alikula lakini si kama kawaida hapo ndipo akaona
kuwa ni mzima hivyo lazima amsaidie. Hatimae
wanafika kijiji cha MLIMALONDO bila watu
kufahamu kabisa. Aliingia nae ndani kwake na
kumhifadhi vyema, alifunga mlango wake na kwenda
kwa mzee mmoja maarufu kwa miti shamba hapo
MLIMALONDO, aliyejulikana kwa jina la KAUZIBE
"Babu nina mgonjwa wangu kule nyumbani naomba
ukamsaidie"
"wewe katunje ulisema unaenda bwawni kumtafuta
nduguyo chito sasa ndio huyo uliyekuja nae na sasa
ni mgonjwa au" aliuliza mzee KAUZIBE
"hapana twende huyo anakaribia hata kufa sasa hivi
baada ya hayo nitakuhadithia kipi kilitokea kwenye
safari yangu"
Waliambatana kwa pamoja kwenda kwa Katunje ili
kwenda kumtibia binti ambae hakufahamika ila kwa
huruma ya katunje ndio ilimfanya kuchukua
majukumu hayo.
 
SEHEMU YA TISA 09
Endelea.......................
Walipofika kwenye ile nyumba ya bwana KATUNJE,
alifungua mlango kisha wakaingia wote kwa
pamoja. Katunje alifunnua lile shuka na
kumuonyesha mtu huyo, kikweli mzee KAUZIBE
alishtuka kabisa mpaka mwili wake ukaanza
kutetemeka. Aliona kabisa kuna umuhimu wa
kumsaidia kwa haraka sana.
"Kauzibe hii ni hatari sana, tena sana usipoangalia
anaweza kukufia hapa, sasa ngoja nikachukue dawa
zangu haraka sana.". Aliondoka huku akiwa
anakimbia kwa haraka ili aweze kumkuta akiwa hai
binti huyo.
akiwa njiani mzee kauzibe alijiongelesha mwenyewe
" Mh jamani watu wanapona huyu alikuwa na hali
gani alinyimwa kula au anaumwa "
Alirudi haraka sana akiwa na furushi la mitishamba
yake ambayo aliona kuwa itamfaa., alianza
kukusanya dawa kutoka kwenye lile furushi, "haya
lete maji haraka sana". Katunje alifanya hivyo kwa
haraka ile ambayo mzee kauzibe alihitaji ili
amsaidie mtu huyo. Aianza kusugua kijitim kimoja
hivi huku akikinga sehemu baada ya kumaliza
akamuomba amuinue binti huyo ili amnyweshe.
"sasa katunje, hii dawa ninayompatia, itabidi uandae
sehemu ya kuhifadhia uchafu utakaotoka tumboni
kwake"
Katunje alifanya hivyo na akamuweka katika hiko
kifaa kwani alikuwa mwepesi sana. baada ya
kumywesha dawa ile alionekana kushtukashtuka
hivi, hatimae alitoa uchafu mwingi sana kwa njia ya
haja kubwa. Hata hivyo haja yake haikuwa na harufu
kali ilikuwa kama ni ya mtoto mdogo. baada ya
hapo mzee Kauzibe akasugua nyingine kwenye jiwe
na ikiwa inakingwa kwenye kifaa kingine.
"Haya katunje hii ninayompatia hapa ni kumpatia
nguvu mana hapo hana nguvu kabisa, lakini fanya
haraka umuandalie uji mzito sana akinywa hii anywe
na uji huo".
Katunje kwa kuwa alikuwa safarini hakuandaa
mazingira ya nyumbani kwake hivyo alitoka nje na
kwenda jirani kuomba moto ili aweze kumpikia uji
mgonjwa wake, wakati anayafanya hayo alikuwa
anatokwa na machozi sana kwa huruma sana,
alikuwa analani watu ambao walimtupa kule aliko.
alifanikiwa kuandaa uji mzito ambao ulikuwa
unatakiwa, ndipo mzee Kauzibe akamnywesha dawa
ile kwa nguvu sana japo alionekana kutohitaji
kutokana na uchungu uliopo, lakini pia nguvu ya
kufumbua macho haikuwepo kabisa hivyo
hawakujua kama macho yake mazima na masikio
yake mazima kwani hali ambayo alimkuta nayo
haielezeki. baada ya kufamikiwa kumywesha dawa
hiyo basi akanyweshwa uji huyo kwa kumlazimisha
sana mpaka ukaisha, akaambiwa amuwekee
mwingine."babuu huyu kashiba si unamuona".
"Hapana ukimsikiliza mgonjwa siku zote
hutomsaidia kabisa sasa fanya hivyo". Kweli alipika
mwingine lakini huku akiwa na wasiwasi, Hatimae
alimaliza na akanyweshwa kwa kulazimishwa
mpaka alipomaliza. Mzee kauzibe alimuaga na
kijana katunje na yeye akaenda zake kwake. Huku
nyuma katunje alifikilia sana kuhusu swala la kuishi
na yule binti kutokana na hali yake,aliingia ndani na
kwenda kulala kabisa. Hakuwa na usingizi kabisa
usiku mzima kwani alikuwa akimsikia binti yule
akilalama, aliamka na kumuangalia alikuwa
akitapika alafu akiwa kajishika tumbo lake huku
akitetemeka kwa baridi kali.
Alihangaika sana katunje kutokana na ile hali hivyo
alimtafutia nguo zake na kumfunika baada ya
kusafisha matapishi yale na kuyaweka kwenye
sehemu moja. hatimae alikuwa kimya ndipo akalala,
katunje alisimama huku akimuomba mungu
amsaidie sana katika kumhudumia binti huyo mpaka
hali yake itakavyokuwa vizuri. Majira ya asubuhi ya
siku ya pili Katunje aligongewa mlango na mzee
Kauzibe.
"Eti vipi kaamkaje mgonjwa wetu" aliuliza bwana
kauzibe
"Ahaa kweli, usiku nilimsikia akilalama nilipoamka
kumbe ilikuwa baridi kashikilia tumbo lake
nikamfunika na mashuka mengi ndipo nikaona kuwa
yuko sawa mpaka sasa hajaamka" Mzee kauzibe
alitikisa kichwa huku akifurahi sana kwa ile taarifa
aliyopewa.
"hapo sasa matumaini yanaonekana nadhani
akiamka nitampa dawa moja hivi kiboko ambayo
itamfanya awe kamili kabisa". Walishikana mikono
na kupongezana lakini mzee kauzibe alimuomba
aweze kumhadithia yaliyojiri huko atokako, "Ehee
katunje, nambie habari za huko utokako yapi
yamekukuta na huyu mgeni ulimkuta kwa hali gani "
Aliuliza ili aweze kupata taarifa nyingi zaidi.
"kweli nilizunguka kama mbwa mwizi kumtafuta
ndugu yangu, nilianzia kule nyumbani SHIMOMO
ambako kiukweli nilipita juu juu tu nilimpata ndugu
mmoja nikamuuliza akaniambia hayupo kaama
tangu kipindi cha nyuma, "
"ehee ukafanyaje sasa baada ya hapo" aliuliza mzee
kauzibe
"Ndipo nikatembea sana hata sikufahamu naenda
wapi hatimae nilifika kijiji kimoja kinaitwa
BWAWANI hapo nilifanikiwa kuonana na mwenyekiti
lakini kwa bahati mbaya iliyoje, majibu niliyoyapata
kuwa bwana CHITO hawamfahamu kabisa pale "
"hawamfahamu aaah kweli umepitia maisha
magumu wewe na ndugu yako ehee"
"basi nikaomba wanihifadhi pale ili ndani ya siku
tatu nimtafute ndugu yangu pale kijijini kama
sitomuona basi nirudi, lakini wakanikatralia na
kunitumia vijana wanifukuze, njia niliyokuwa
nikikimbilia kumbe ilikuwa naelekea msituni pia
karibu na bwawani"
mzee kauzibe alikuwa makini sana kusikiliza hatua
kila hatua "haya ikawaje"
"ndipo hapo wakaniacha na mimi nikaanza
kutembea ghafla nikaliona tenga lililopo ndani pale
mbele yake nikaona nguo zilizochakaa alafu
zimegandia damu, nikazikusanya mpaka bwawani
ajabu nataka kuanza kunawa yale maji ambayo eneo
hilo linaonyesha hapafikiwi na mtu kwani pachafu
sana, ndipo nikamuona huyu binti pembeni wadudu
wakimuingia masikioni na kachafuka yani kwa hali
ile mungu mkubwa jamani ndipo nikakutwa na roho
ya huruma nikamuweka kwenye tenga na kuja nae
huku".
Alikuwa anahadithia huku machozi yakimtoka kwa
wingi sana, kwani alionekana kuwa na uchungu wa
wale wanaowafanyia mabaya watu hasa wanawake
pia wadogo kama yule. Ukweli kwa muonekano wa
binti huyo ulikuwa wa kutosha kabisa kuwa na mtu
kwani maumbile yao huwa makubwa.
"Kijana kwanza hongera huo ndio utu na si
vinginevyo hakuna jambo zuri kusaidia watu wenye
shida kama hawa"
mala ghafla alisikika akitoa sauti humo ndani,
akigugumia kwa maumivu makali. walisimama na
kwenda ndani kwa haraka, walimkuta akishikilia
tumbo lake huku akijaribu kurusha miguu. "sasa
mzee tunafanyaje, hapa?"
aliuliza katunje,
"yani hapa naona sasa utumbo unafanya kazi na
mwili unaitikia unataka kurudi kwenye hali yake
sasa mpikie uji haraka sana". Baada ya muda
ulikuwa tayari na alinyweshwa.
Baada ya miezi kadhaa kupita upande wa kijiji cha
BWAWANI, mzee mambo sasa alikabidhiwa shamba
la mikorosho lenye mikorosho themanini, alianza
nayo kuitengeneza vyema sana kwa mara ya
kwanza. Ndipo mavuno yalipokaribia utata
ulipoanza, vijana wa mzee Manyenye, walikuja juu
kuwa yale ni mashamba ya baba yao hivyo wana
haki ya kufanya wakitakacho hivyo walianza
kuchukua korosho na kujiwekea wao majumbani
kwao, mzee mambo sasa aliligundua hilo mapema
sana akamshirikisha mzee manyeye ndipo
akawakemea sana vijana hao watatu.
wale vijana walikutana siku moja na kupanga njama
ambayo watamfanya mzee mambo sasa aache ile
mikorosho ambayo kaihudumia kwa muda mrefu
baada ya kupewa. Moja ya njia ni kuichoma moto
kabisa ili wakose kila kitu na kuwaacha wakiwa
watupu.
Kwa bwana Sikujua alikuwa vizuri na anaendelea na
shughuli zake lakini, muda huo alipita Mama Mengi
ambae binti yake yupo kama Sikitu aliyepotea kwa
muda mrefu. "Mzee naona unajisikia vizuri tu sasa
hivi"
kauli ya mama mengi ilimfanya ashtuke sana
sikujua,
"Wee mwanamke usiyekuwa na adabu unanitafuta
sasa hivi"
"sio kukutafuta hivi unakumbuka kuna siku nilikuona
unaingia na Sikitu chumbani kwako, alafu siku ya
pili tukasikia kapotea nilipokuuliza ukanitishia looo
mzee mzima na najua wewe ndio utakuwa
umehusika na hilo swala"
Mzee sikujua alipandwa na hasira sana kwani aliona
kuwa mama mengi ni nuksi kwake. "Wee mama
wewe kuwa na adabu fahamu kuwa hiyo ni kesi
kubwa sana unayonipakazia sitaki na nisikusikie
ukiniambia mambo hayo"
"sawa utanifanya nini sasa kwa sasa hivi? na ukileta
ujinga natangaza kijiji kizima hiki wajue na mzee
mambo sasa unajua alivyokuwa na hasira akijua">
mama huyo aliondoka pale akimuacha bwana
sikujua kijasho kikimtoka. alijifikilia mengi sana
kwani aliona sasa huyu mama atamfanya ajulikane
wakati mambo yalipita kitambo sana.
Akiwa nyumbani alisikia kauli ya watu ambao
walikuwa wanapita karibu hapo alipokuwepo,
"Nimesikia kuwa mama mengi leo jioni anamtaja
mtu aliyesababisha kupotea kwa Sikitu".
Sikujua hakuweza kuamini kusikia hayo maneno,
alisimama na kuwasimamisha wale watu waliokuwa
wakisema zile habari.
"jamani ina maana mama mengi anamfahamu
msababishaji kwa kupotea kwa sikitu?" aliuliza.
"ndio bwana sikujua anamfahamu japo hakutaka
kutuambia hivyo kasema leo jioni itapigwa kengele
na tutafika pale alafu atamtaja " Mzee sikujua
alionekana kuchanganyikiwa akijisemea moyoni
'huyu mama hanitambui kalianzisha ngoja nilimalize
mpumbavu sana'. "vipi bwana sikujua unawaza
nini?" walimuuliza baada ya kumuona kimya kwa
muda.
"hapana yani najifikilia kwa nini hakumtaja mapema
hivyo, inabidi, ataje haraka tumshughulikie sisi
wenyewe kabla ya bwana mambo sasa au
mnaonaje"
aliongea kwa kujipa ujiko ili asijulikane kuwa yeye
ndiye muhusika mkuu, "ni kweli jamani anachosema
bwana sikujua ila tunajiandaa sasa kwa ajili ya
kwenda kupokea ujumbe mzito huo, ".
waliachana pale, na yeye akakimbilia kwa Mapato,
kumueleza jambo lile hakika mapato alionekana
kumgeuka rafiki yake kwani alijiepusha kutajwa na
yeye kama alishiriki kwenye swala lile "Haaa ndugu
yangu hapo mimi sihusiki kabisa nimekusaidia vya
kutosha kufanya unyama tena sitaki".
"ina maana unanikana leo kwa kuwa umesikia
mtoto wa mzee Manyenye leo anaenda kunitaja".
Taarifa ilimfikia bwana Mambo sasa pa,moja na
mke wake hivyo walijianda vilivyo kusubilia jioni
kwa hamu tena waliona kuchelewa.Baada ya
mapato kujitenga na lile swala, alirudi nyumbani
bwana sikujua na akaingia ndani, alichukua kisu
kikali na akakinoa vyema yakawa na makali yote,
akatoka nje huku kile kisu akakiweka kwenye ala
yake yani hifadhio. alitembea mkuku mkuku huku
akiangaza huku na kule kama kuna mtu
anamuangalia, alifanya hivyo akiwa na nia yake yeye
mwenyewe anayoifahamu.
Hatimae alimuona Mama Mengi akliwa anachukuam
kuni kule ambako alimhisi lazima muda huo
atakuwepo, alipomuona akachomoa kisu chake na
kujificha njiani ili amsubiri apite amuonyeshee, kwa
kuhofia kuonekana alijificha na nguo usoni
akabakiwa na macho yakiangaza huku na kule,
Mama mengi alihisi hatari wakati anarudi, ndipo
mzee sikujua akamtokezea na kumsukuma hatimae
akadondoka chini na zigo lake la kuni. Hakufanya
ajizi yeyote, alimtumbukiza kisu tumboni bila
huruma na akahakikisha kimechanachana utumbo
wake vyema kisha akatoa,
Mama Mengi alilalamika sana tena sana ndipo
katika harakati za kutafuta uzima, alimshika nguo
yake ya usoni na kumfungua, "Aaaaah mzee sikujua
una..ni...iiiiuaaa ".
"Pumbavu haya nenda kaseme sasa huko kuzimu
kuwa nimembaka sikitu mpaka kifo chake unapenda
kuingilia kitu kisichokuhusu">
Aliondoka pale kwani alikimbia utadhani kuwa sim
kama mzee, alifika nyumbani kwake akachukua maji
na kuoga kwanza. baada ya hapo akachukua mkeka
akalala nje kama kawaida yake, hivyo ilimfanya kila
apitae kumuona pale alipo na kuondoa dhana ya
yeye kuwa kasababisha mauaji.
Kengele kama ada iligongwa na watu walifika pale
kama kawaida akiwemo mama sikitu na mumewe
akiwa na huzuni akiwa na hamu ya kumla supu huyo
atakayetajwa, mwenyekiti alitoa maelezo machache
ambayo yalimfanya kila muhusika pale atulie
kumsubiri mama Mengi, muda ulipita mtu
haonekani, ndipo aliulizwa baba mtu mzee
Manyenye, kuwa yuko wapi ndipo akaelekeza kuwa
yeye alienda kuchukua kuni na akirudi atajiandaa
kuja hapa.
Walitumwa vijana akiwemo susu, walikimbia
kuelekea huko walikoelekezwa muda mchache
wanrudi na mwili wa mama Mengi hakika hayupo
ambae aliamini kama mama mengi kafariki kwa
kuchomwa kisu.
Upande wa MLIMALONDO baada ya miezi ile kupita
hali ya yule binti ilikuwa nzuri na kuridhisha sana.
wakati ulifika wa kuhojiana ili kumfahamu vyema
ndipo walikuwepo na mabinti kadhaa ambao walitoa
ushirikiano wa kucheza nae na kumchekesha lakini
alikuwa na tatizo hajui kuongea, macho yamefunga
kama alivyomkuta kule mara ya kwanza lakaini
mwili ulianza kurudi hata mifupa na mbavu zilianza
kujificha.
KATUNJE alikuwa hana raha alijitahidi namna kila
namana binti arudi kama hali yake lakini akaona
labda tangu mwanzo alikuwa vile alivyo, hata jina
lake hakulifahamu kabisa kumbukumbu zilimpotea
ndipo wakampatia jina jipya ambalo watamzoesha
mpaka atalifahamu na kulitumia walimuita LYOTO.
Likiwa na maana ya joto jina hili alilitoa mzee
kauzibe ambae alilifafanua kama joto ni kama moja
ya changamoto ambayo unakutana nazo kama joto
linavyokuzidi na kushindwa kujizuia, hiyo ndio
maana halisi hivyo binti LYOTO alikuwa changamoto
kwao ndani ya kijiji cha MLIMALONDO.....
...................
 
SEHEMU YA KUMI 10
Endelea..............
Ilikuwa ni kizaazaa sana kwa tukio la kufa kwa
mama Mande pale kijijini, wasiwasi ulianza kutanda
kuonyesha kuna jambo ambalo lipo miongoni
mwao, wengi waliongea vile walivyofikilia na
kudhania nini kinaendelea pia wengine walifikia hata
kuwaongelea vibaya viongozi wao vibaya kuwa
wanahusika kwa namna moja ama nyingine.Upande
wa mzee manyenye alipatwa na presha kabisa
kutokana na ile hali.
Hayo yote yakiwa yanafanyika kwenye uwanja wa
mkutano karibu na ofisi za mwenyekiti, pamoja na
mtendaji wa kijiji cha bwawani.
watu walisindikiza haraka mwili wa marehemu hadi
kwenye nyumba ya mzee manyenye, huku wengine
wakijaribu kumpepea mzee manyenye. Kwa upande
wa Mzee mambo sasa na mkewe waliweza
kuondoka pale kwa haraka kwenda nyumbani kwao.
"Mke wangu hakika tunahitajika kuondoka haraka
sana mana hii inanionyesha picha mbaya sana hapa
kijijini". aliongea bwana Mambo sasa.
"Inakuonyesha picha gani eeeh"
"wewe huoni?, Mama mande katangaza kuwa
anamfahamu aliyesababisha mtoto wetu sikitu
kupotea na anataka kwenda kutuambia lakini muda
umefika inaletwa maiti yake unadhani hapo kuna
nini" Mama sikitu aliduwaa tu na kwenda kumshika
mumewe akimpokonya zile nguo alizokuwa
anazipanga tayari kwa safari.
"Sawa mume wangu ina maana kuwa yeyote ambae
atahitaji kufuatilia kupotea kwa mwenetu atafanywa
kama alivyofanywa Mama Mengi?"
Aliuliza mama sikitu, "Ndio na hapo ipo siku kabisa
muuaji huyo ina maana kamuua mwenetu, alafu
atakuja kutudhuru hata sisi ili kuondokana na hilo
lazima tuondoke"
"Lakini kule si kuna msiba alafu yule aliyekufa baba
yake kakufanyia nini na unataka tuondoke inafanana
kweli"
kauli hiyo iliweza kumuingia vyema bwana Mambo
sasa, Akamuelewa vyema mkewe ndipo
akamsogelea na kumkumbatia huku chozi likimtoka,
"Sawa mke wangu nimekuelewa na nakuahidi
mpaka tunamaliza maziko yote na kuhakikisha hali
ya mzee manyenye inakaa sawa ndipo tunaondoka".
Kijiji kizima kilirindima majonzi yenye mshangao
mkubwa sana, kwa upande wa bwana Mapato alihisi
jambo fulani kwani baada ya kutoka kule kwenye
mkutano uliozua mabaya alikwenda moja kwa moja
hadi kwa Sikujua kumuangalia kwanza. Alimkuta
akiwa analia chozi likimdondoka hivyo hata dhana
yake ya kwenda kumhisi vibaya ilitoweka kabisa.
Alimsogelea na kumuuliza kipi ambacho kinakuliza
rafiki yangu?. Sikujua aliongea huku akitetemeka
kwa hofu `ndugu yangu haya mauaji yaliyotokea
ukweli sina amani sasa` aliongea hivyo kumueleza
rafiki yake mapato, lakini mapato hakuridhika na
yale majibu aliyojibiwa na sikujua `lakini kwa nini
unachukua maamuzi mkononi, ninakutilia shaka`
alimueleza kweli kuwa anamtilia shaka.
`unanitilia shaka. kivipi unanitilia shaka' aliuliza
sikujua kwa mshangao wa dhati kabisa. "ndio
nakutilia shaka kwa sababu unakumbuka muda
ambao ulikuja nyumbani kuniomba eti ama mengi
kakutisha na mimi nikakuambia kuwa sitoweza
kukusaidia kwa hilo ukaniambia kuwa utajua la
kumfanya wewe mwenyewe si ndivyo".
Sikujua alikaa kimya sana huku mapigo ya moyo
yakimuenda kasi, jasho jembamba likimtoka mzee
huyo wa makamo, alimgeukia bwana Mapato na
kumueleza, "Ndugu yangu, sikia mimi sijasababisha
mauaji kabisa kwanza siwezi kuua nina kesi hii
naitaji niikwepe tena niweze kusababisha mauaji
kwa mtu nisiyemkosea wala kunikosea jamani".
Mapato alisimama na kumnyooshea kidole
"hakuna cha kupinga hapa, wewe ndio msababishi
na nimekuchoka, sasa kama unaweza njoo uniue
mimi kwani tukikuachia hivi utawamaliza watu".
Sikujua jicho lilimtoka kama kabanwa na mlango,
moyo wake ulionekana kama unaotaka kusema
jambo lililopoila likashindwa, "mapato naona sasa
umenichoka ila kama unaenda kusema huko wewe
nenda alafu mimi nitajua la kufanya". Mtafaruku
uliendelea pale wakiwa wawili zao.
"Wewe nenda ila kumbuka miaka nane iliyopita
undugu wetu uliunganishwa na nini, ulifanya tukio
gani kumbuka alafu leo unajifanya eti kwenda
kusema nenda na mimi naenda kutegua kile kitu
mbavu zako".
Baada ya hapo mapato alionekana kukaa kimya
sana bila hata kusema ndipo akamsogelea
mwenzake na kumuomba msamaha ili yaweze
kuisha na waendelee kufichiana yale mambo yao
wanayoyafahamu wao wenyewe.
Alirudi kwake bwana, Mapato huku akisubiri
matangazo ya kujua lini wanazika, alianza
kukumbuka miaka nane iliyopita baada ya
kukumbushwa na sikujua, urafiki wao ulianzia miaka
kadhaa ya nyuma iliyopita,
Siku moja, bwana mapato akiwa anatafuta kuni
ndani ya kijiji cha SONGAMBELE, huku akitembea
tembea na kuimba, aliukuta mti mmoja ambao
aliuona kama unafaa kwa kupata kuni,
alianza kukata tawi moja baada ya jingine, ghafla
wakati anaendelea alisikia sauti zikisemezana
maeneo ya bwawa ambalo lipo ndani ya kijiji chao,
bwawa hilo lilikuwa linatumika na watu kwa mabo
mengi sana hasa kama uvuvi pamoja na matumizi
ya nyumbani, alikaribia bwana mapato huku akitega
sikio kujua nini ambacho kinazungumzwa hapo,
alizisikia sauti za ajabu ambazo hakuwahi kuzisikia
kamwe, cha ajabu zaidi kwenye lile bwawa
ilionekana kama kuna watu ambao wanaogelea
lakini hawaonekani.
Alirudi kinyumenyume, na ndipo akaanza kukimbia
kurudi kijijini. Enzi hizo palikuwa panaongozwa na
kiongozi mmoja tu aliyejulikana kwa jina la
ZAMALIO, huyu mzee uongozi wake ulitegemea sana
nguvu za wale anaowaongoza, yani ushirikiano wa
wanakijiji wenyewe ndani ya songambele.
aliwapenda sana watu wake na alijitahidi kufanya
kila njia ili kuwafurahisha wanakijiji na wao
walimpenda,
Alipofika kijijini ndipo akaelekea kwa zamalio
kumueleza yale aliyoyashuhudia na kumchanganya,
ukweli ilikuwa ni habari nzito sana siku hiyo hivyo
bila kuchelewa walitumwa watu na wazee ambao
alihisi kuwa wanaweza kutambua kama kuna aina
yeyote ya ushirikina unaendelea hapo.
Walipofika kule karibu na lile bwawa, hawakuweza
kukuta chochote lakini ajabu walifika nyuki kutoka
sehemu ambayo hawakutambua walivamiwa kasoro
bwana Mapato, wengine walikimbia akabaki mzee
mmoja ambae walimvamia mpaka kifo chake
palepale, Mapato alishtuka na kuweuka pale na
asijue nini afanye, wakati anajiandaa kuondoka basi
alihisi kama kashikwa na kitu asichokifahamu,
""Mpato ahsante sana wewe ndie umetuona sisi na
wewe ndie unachaguliwa kuwa kiongozi wa
kutuletea watu hapa mpaka zamalio afike ""
alishindwa kuelewa ghafla alihisi kichwa
kikimbangua na mwili kubadilika kuwa na joto kali
alianza kutoka pale akiwa hajielewi kabisa, Siku ya
pili alikaa na kufikilia kile kilichotokea jana yake,
hakuamini kwa yale yote ambayo yamemfika na
kusababisha mtu kuda mbele yao.
Alinyanyuka na kwenda kwa kiongozi wake zamalio
ili akajue hata kama kuna kitu chochote ambacho
atakitambua kuhusu lile bwawa.
"Zamalio kiongozi wa songambele, nina maswali
mengi juu yako kuhusiana na lile bwawa, kwa lina
vitu gani ambavyo sisi kama wanakijiji
hatuvifahamu?" aliuliza mapato ili apate kujua zaidi
kuhusu kile alichoambiwa. Zamalio hakuweza
kabisa kumjibu vizuri ili kijana mapato afahamu.
"mh kijana, ni swala zito sana ambalo hata mimi
sikupata ufafanuzi kama wewe unavyohitaji
kufahamu hivyo kikubwa zaidi achana nayo tu"
Mapato hakuweza kabisa kuridhika, alirudi nyumbani
kwake. majira ya usiku hakulala kwani kuna vitu
aliweza kuvisikia hivyo alitoka nje na hatimae
anakutana na watu wa ajabu sana ambao walimpa
amri kali sana. "kijana, endapo usipotekeleza kauli
yetu huwezi kukaa salama." "Jamani nini ambacho
nimekosa na mnahitaji ninikutoka kwangu".
Walimcheka sana kisha wakamuuliza `unataka
tukuonyeshe, nini tunakihitaji? kumbuka wewe ndio
wa kwanza kabisa kutuona maeneo yale kwani
hatukutaka kuonekana sasa ili tufiche siri hii lazima
ufanye." walisambaa zao na kumuacha mapato
akihemwa. Muda ulipita bila mapato kufanya
shughuli ile ambayo aliambiwa ya kuwapeleka watu
karibu na bwawa, kwani tangu siku hiyo mzee
zamalio aliwakataza watu wakewasisogelee tena lile
bwawa. Sikum moja mapato alishuhudia kifo cha
mama yake mzazi lakini ilitokana na wale watu
wasiojulikana. baada ya miaka kama mitatu hivi
kupita ndipo wakamuambia atamkosa baba yake,
alikuwa mbishi sana mapato ndipo. wakamuua baba
yake mapato, haikutosha wakamueleza kuwa
asivyotekeleza wanaanza familia yake mmoja
mmoja.
Hapo ndipo alipokubali
siku ya kwanza alianza na mmoja wa watu wa
kiongozi wa zamaliom kumpeleka karibu na bwawa
lile, na akapotelea hukohuko, akifanya hivyo basi
anaona mabadiliko ya hali yake ya maisha kuwa
,mazuri, alianzisha mashamba na yakanawiri sana
zaidi ya wengine.
zamu ilipofika ya kumpeleka zamalio aliambiwa
kuwa amuue kwa mkono wake. Mapato kwa kuwa
alifaidika na akapendezwa na yale mafanikio
ambayo alikuwa anayaona haikuwa shida kwake.
Majira ya usiku wakati wanaomlinda kiongozi
zamalio wamelala, aliingia kiurahisi na kwenda
kumvamia mzee zamalio, akamkaba mpaka
alipohakikisha kuwa kafariki.
Aliondoka bila kufahamika, wale viumbe
walimpongeza sana kwa kazi ambayo aliifanya na
ndipo akaambiwa kuwa bado kazi ya kutunza siri.
Iliwezekana kupelekwa taarifa kwa mtu mmoja tu na
yeye anahitajika kutunza sana siri hiyo walimpeleka
na nyakati hizo hakuweza kuogopa kwani kafanya
nao kazi nyingi kunusuru maisha yake, Walimpeleka
hapo bwawani katikati wakamuonyesha kitu
ambacho kinafanana na pembe hivi, walimuambia
kuwa hiki ndio siri ya mafanikio yako kikija
kutolewa hapa huna maisha, pia hiki unaweza
kutumia pale unapoona kuwa maisha yako yanaenda
kubaya unafanya kazi ambayo itakuamuru ili upate
maisha mazuri.
Baada ya mwaka kupita iliwekwa tangazo kwa
wanakijiji wote kuwa yeyote atakayemfahamu
muuaji wa mzee Zamalio ni ruksa kumuua kwa
muda wowote apatikanapo, na kila kizazi kijacho
basi hii kauli iliweza kulithishwa jambo mapato
hakutambulika kama ni yeye ndie muhusika.
Ujio wa bwana sikujua ndani ya kile kijiji akiwa na
baba yake enzi hizo, mapato ndie aliwapokea kwa
kuwa yeye pekee ndie alionekana kuweza
kuwahudumia wenye shida hivyo aliweza
kuwakaribisha, waliishi kwa muda lakini vitendo vya
mapato vilimfanya baba yake sikujua afahamu kuwa
ni mtu wa aina gani, hivyo baada ya uchunguzi wao
kwa wao waliweza kumjua na yeye mwenyewe
akakiri kuwa kweli na akawa hadithia, baada ya
kupatwa kwa umauti baba yake sikujua walianza
kuishi kama ndugu. Mpaka wanafikia miaka ya
waliyopo yanampata sikujua kumbaka binti sikitu na
kumuua mama mengi, basi mapato alibaki kuumia
akikumbuka msaada wa baba yake sikujua mpaka
kumfanya atoke kwenye himaya ya watu waliokuwa
wakimtumikisha kuua watu, ndipo pia ikawa sababu
ya kuvunjika jina la SONGAMBELE na kuitwa
BWAWANI ili iwe rahisi kukumbuka pindi mtu
akikatazwa kuwa asikaribie lile bwawa.
Wakati anaendelea kukumbuka bwana mapato
yaliyopita
alishtushwa na mkewe ambae alimuita kwa ajili ya
chakula, kipindi hikohiko mambo sasa anafika kwa
mapato,
Upande wa KILIMALONDO binti LYOTO alionyesha
maajabu mpaka bwana KATUNJE na Mzee KAUZIBE
walifurahi sana siku hiyo........
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA 11
Endelea...............
Ndani ya kijiji hiko cha kilimalondo, ambako
alipatikana binti lyoto akitibiwa na Katunje pamoja
na Mzee kauzibe. Majira ya mchana lyoto akiwa
peke yake, katunje alifanikiwa kumuona akipikicha
macho yako na kutazama kitu kwa makini huku
akisogelea kwa ukaribu sana.
Kitendo hiko kilimfanya katunje apatwe na bashasha
kubwa sana kiasi ambacho alimsogelea zaidi ili
amkague kama kweli kile anachhokifikilia ni kweli.
alizidi kumshangaa huku lyoto akikisogelea moja ya
kijiti kilichopo karibu na yeye lakini akiangalia kama
wanavyoangalia kuku.
Katunje alienda muda huohuo kwa mzee Kauzibe
kumpasha habari ile. Hakika hata mzee huyo
alifurahi sana kwani aliona matumaini ya dawa zake
kuwa zinafanya kazi. walienda kumshuhudia wote
kwa pamoja wakiwa kwa mbali walimuona
akiendelea kupapasa vitu fulanifulani hivi, `Ina
maana anaanza kuona japo nilidhani kuwa ni kipofu
kumbe hata ni mzima kabisa binti wa watu'
Aliongea bwana Katunje, Mzee nae alipatwa na
hamu zaidi ya kumsogelea `katunje kumbe huyu
binti ni mzuri hivi haki ya nani'.
Katunje alivyosikia hivyo akamsogelea na
kumuambia mzee huyo. `Hapana babu usiingiwe na
tamaa kabisa huyu bado hajafikia hatua ya kufikilia
wanaume, lakini hata hivyo wewe mtibie mambo
mengine niachie mwenyewe' Ulikuwa kama utani
ambao ulikuwa unaendelea kwa wakati huo, ndipo
walipomkalibia na kuanza kuongea nae.
'Lyoto haya unaniona mimi babu yako?' aliuliza
mzee kauzibe.
lakini binti lyoto hakugeuka kabisa ndipo kauzibe
akamgeukia katunje. `Mh bado masikio hayafanyi
kazi ndio maana hajajibu' kweli alikuwa na matatizo
kama kutosikia kutoona kabisa na mwili kudhoofika
lakini kwa jitihada na hawa watu walijitahidi na
kumsaidia mpaka sasa angalau anaonekana kuona
mwili unaanza kurudi lakini tatizo kusikia. Kufikia
hapo waliandaa utaratibu mwingine wa kumpatia
dawa za kutosha ili aweze kuwa sawa zaidi kiafya.
Taarifa za kuja kwa binti huyo ndani ya kijiji cha
kilimalondo kilianza kutawala mwishoni huku
ambako hali yake ilianza kuwa nzuri sasa. Hata
watu walianza kwa kumshangaa baada ya kumuona
nje ya nyumba ya katunje.
Ndani ya kijiji hiko ambacho kuna kiongozi maarufu
ambae wanamtumikia kama bwana, aliishi takribani
miaka kadhaa na mkewe bila kufanikiwa kuwa na
mtoto ambae angeweza hata kumsumbuasumbua,
katika harakati zake na yeye aliweza kupata taarifa
hizo za kufika binti huyo mwenye matatizo kadhaa
ambayo alipatiwa na wale wanaomkusanyia habari
na kumpatia.
`KIMOLO njoo mara moja hapa' kiongozi huyo
aliweza kumuita mmoja wa wafanya kazi wake
waliopo pale ili aweze kumueleza jambo fulani,
kijana huyo alifika pale karibu na huyo mzee.
`Nimeitikia kiongozi wangu na pia nipo mbele yako
kutekeleza amri yako utakayoniagiza' Alimhakikishia
kiasi kwamba hata huyo mzee alifurahi.
`vizuri kijana wangu, sasa naomba uelekee
nyumbani kwa katunje ili ukamuangalie binti huyo
na ikiwezekana mueleze katunje afike hapa haraka.
Baada ya hiyo kauli hakukawia alitoka pale, hatimae
alimkuta katunje akimkogesha binti Lyoto maeneo
hayo ya kwake. Kimolo alifik Hdi pale karibu na
kumpa ishara kama ya heshima katunje kama ilivyo
kawaida ya hiko kijiji kuwa yeyote ambae yuko
anatembea amsalimie aliyetulia au kukaa, na yule
aliyekuwa akitembea mwendo mkali amsalimie
mwenye mwendo mdogo au wachache wawasalimie
wengi.
Katunje alimuitikia lakini kwa haraka sana
alimmaliza na akamshika mkono na kumuingiza
ndani mgonjwa wake, baada ya kuhakikisha kuwa
kamaliza ndipo akatoka na kufunga mlango na
kumkaribisha kwenye moja ya viti vilivyomo karibu
na pale kwake.
`bwana Kimolo karibu sana sijui leo umekuja na lipi
kutoka kwa mzee' alimuuliza huyo mjumbe
aliyetumwa na kiongozi wake. Alionekana
kushangazwa kwanza kabla ya kuanza na
mzungumzo yoyote.
`Ni kweli ujumbe kutoka kwa Mzee SWAI kuwa
anakuhitaji ufike harka sana kule kwake ikiwezekana
tuongozane sasa hivi au kama huna nafasi basi
fahamu kuwa kesho ufike mapema.'
Ktunje alishtuka sana baada ya hiyo kauli
`Huyu mzee swai ananiitia nini kwake, tangu lini
ananiita hakuwahi kabisa kufanya kitu kama hiki
jamani'. Kimolo aliondoka mbele ya katunje na
kurudi alikotokea, Katunje hakuridhika kabisa na lile
swala kwani alihisi kuna jambo baya ambalo litafika
mbele yake hivyo lazima aende kwa huyu mzee
akapate ushauri kwanza.
Siku ya pili yake kweli alijiimia kwa mzee kauzibe
baada ya kuhakikisha kuwa lyoto kamuweka kwenye
hali nzuri ya kiafya na mambo mengine.
`babu jana kuna yule kijana mtumwa wa swai huyu
anaitwa kimolo alikuja jana akaniambia kuwa mzee
swai ananiita sasa mimi nashangaa kuna jambo
gani kwani hajawahi hata kumleta mtu nyumbani
kwangu sasa iweje leo anihitaji?'
alimueleza bwana kauzibe.
`sasa wewe una wasiwasi gani kuitwa na mkubwa
wa kijiji hiki, nenda kwanza alafu msikilize kisha
ndipo utajua unasemaje kutokana na hiko
alichokuambia'.
Kweli baada ya muda alifika kwa mzee swai na
kuketi kwenye kiti ambacho alikabidhiwa `kijana
nimekuita hapa lwa jambo moja tu, nimesikia kuwa
unaishi na mtu ambae hakuwa hapa kabisa mwanzo
yani ni mgeni'.
Katunje akaona sasa ishakuwa balaa sasa.
`Mh ndio ninaishi nae lakini ni mgonjwa kabisa
hawezi hata kujitambua' mzee swai alimtazama kwa
jicho la kumtamani sana kijana katunje, `sijali yeye
ana hali gani, kwa nini unamleta mtu ndani ya kijiji
chetu bila hata taarifa'
Alishidwa kujibu kabisa swali lile ambalo aliulizwa
na mzee swai.
`Unakumbuka kuwa wewe ni mgeni hapa japo
umekaa miaka mingi sasa unajulikana kama
mwenyeji lakini mimi ndie niliyekukaribisha hapa
iweje wewe hukuleta taarifa ya kuwa umakwenda
kumchukua mtu ambae hatumfahamu kwanza
anatokea wapi?'.
Aliendelea kutundikwa na maswali mengi sana kiasi
aliona kuwa kweli ana makosa kwa kutokupeleka
taarifa kwanza na ili aweze kupewa ruhusa ya kukaa
nae huyo binti,
`sawa mzee wangu nimekosea kabisa kufanya hilo
jambo lakini sikuwa na budi kufanya hivyo kwani
ilikuwa kwenye mazingira ambayo sikuyategemea
ndani ya kijiji kimoja kinaitwa bwawani'.
Alipomaliza kueleza kutokana na swalli ambalo
aliulizwa ndipo akatulizwa asiendelee kusema lolote
kwa muda huo.
`ngoja katunje, kwanza una makosa ya kumleta mtu
bila taarifa pia tunaogopa kutuletea ugomvi na watu
wanaommiliki huyo mtu sasa naomba utuletee huyo
mtu kesho na sisi tutafanya juhudi kumrejesha kule
alikotokea tunao usafiri hapa na watu na wewe
ukiongozana nao'.
Katunje aliruhusiwa kurudi huku kichwa chake
kikiwaka moto kwa mawazo makubwa sana juu ya
binti yule aliyemzoea na kumfanya kama nduguye
au mtoto wake kabisa, `Ina maana nikubali kweli
kumpeleka kwa bwana Swai hivi wanatambua nguvu
niliyotumia kumsaidia huyu na wanajua kweli
wakimpeleka huko atakuwa kwenye hali gani aaah
aaah hapana siwezi'.
Alijiongelea mwenyewe huku akiwahi nyumbani
kwenda kuhakikisha kama lyoto atamkuta salama,
kweli aliweza kumkuta salama usalimini akiwa na
bwana Kauzibe, ndipo alimhadithia yaliyotokea kule
alikotoka kuhusu wao kumhitaji yule binti ili
wamrejeshe kijiji cha bwawani ili kuepusha ugomvi
na watu ambao wanammiliki yule binti. Mzee
kauzibe alishtuka lakini alionekana kama mwenye
kufahamu jambo fulani hivi.
`unajua katunje, mimi kama nilifahamu hilo kwani
yule mzee tangu awe kiongozi na kumuoa yule
mwanamke wake hawajawahi kumpata mtoto, sasa
unakumbuka kulitokeaga ugomvi mkubwa hapa
kijijini miaka kadhaa iliyopita'
Alivuta kumbukumbu kijana Katunje
`Aaaaah! sawailikuwa mzee swai na mzee Korongo,'
`Haswaaa kumne una kumbukumbu nzuri ule
ugomvi japo mzee korongo alifariki ilikuwa njama
za mzee huyu lengo lilikuwa mke wa korongo apate
mimba alafu mtoto atakayezaliwa ndipo amchukue
mzee swai na awe wake jambo ambalo mzee
korongo hakutaka kabisa sasa naona kama lina
amia kwa huyu binti lyoto'
Katunje alishtuka sana kisha akagundua mpango
mzima ambao mzee swai anataka kuuucheza kwa
mara ya pili baada ya kuushindwa kwa bwana
korongo.
`sasa babu hapa nifanye nini kuepukana na huyu
mzee mana kasema kesho nimpeleke'
`Hapana usimpeleke cha kufanya wewe mlete
kwangu alafu nyumba yako ufunge wakati huo wewe
na mimi tukipanga jinsi gani ya kumuweka salama
huyu binti na pia tufanye juhudi ya kujua kwake na
wazazi wake'.
Wazo la yule mzee alilikubali kwa asilimia karibia
zote bila upingamizi alikubali na kumuahidi kuwa
atafanya hivyo kunusuru maisha ya binti lyoto.
Kwa upande wa kijiji cha bwawani mzee Mapato
baada ya kumaliza chakula ambacho aliandaliwa
aliamua kupanga safari ya kwenda kule bwawani
japo haikufahamika anataka kwenda kufanya nini,
kabla hajaenda aliitwa na mtu nyuma yake,
alivyogeuka alimuona kuwa ni Mzee sikujua
alishtuka sana kwani alisha anza kumuogopa sana
kwa nyakati hizo.
alimsogelea na kumuuliza kipia mbacho kamuitia,
`mapato najua unaanza kunigeuka ila jua kuwa mimi
sifanyi kwa makusudi lakini najiokoa kwa aibu
nitakayoipata yule mama alikuwa kidomodomo sana
lakini sikuwa na jinsi' aliongea mzee sikujua
kumueleza bwana mapato.
`Aaah sikujua mimi na wewe tena hatuna shida
kabisa usijali'. limsogelea na kumkumbatia ili
kumuondoa kwenye mawazo ambayo alikuwa nayo
kwake. Sikujua alikubali na yeye kumkumbatia kisha
wakafuatana umbali flani na kuanza kuongea jambo
fulani, `sasa sikujua ujue ulivyonikumbusha kuhusu
miaka iliyopita nimekumbuka mengi sana, sasa
nikaona kuwa niende kule bwawani kuna kitu
ambacho niliambiwaga kuwa nikiwa nacho hiko hali
ya maisha yetu hapa yatabadilika kabisa'.
`Mh yani unataka kwenda wakati baada ya kwenda
kule kwa mzee manyenye ili tuonekane nisijulikane
kuwa kama ni mimi ambae niliyafanya yale.
Baada ya siku hiyo kupita, mazishi yalifanyika huku
mzee manyenye hali yake ikiwa inaendelea vyema,
kwa upande wa bwana Mambo sasa alidhamilia
kuhama pale na kutaka kurudi kijijini kwao
shimomo yeye na mke wake. Alikubali kabisa
kuacha lile shamba la mikorosho na kuwaachia
watoto wa mzee manyenye na kuepusha ugomvi
ambao aliwaza kuwa utakuja kutokea, kila mmoja
ndani ya kijiji kile aliweza kujua kuwa mzee mambo
sasa anaondoka pale kijijini. Majira ya jioni akiwa
mazingira ya kwake alijiwa na kijana mmoja hivi
alikuja na kumpa taarifa ambayo ilimsisimua mwili
na kupatwa na shauku ya kujua.
Kwa upande wa kijiji cha kilimalondo, katunje
alimchukua binti lyoto na kuondoka nae akielekea
kwa bwana kauzibe, lakini kabla hajafika kule
aliweza kusimamishwa na mama mmoja ambae
alikuwa njiani mithili ya mshumaa akimsubilia yeye
apite pale. `mama shikamoo' alimsalimia mama
huyo
`marahaba samahani ebu njoo kwanza hapa
unaelekea wapi?' Aliulizwa swali huku akiwa
kambeba lyoto.. Katunje hakumficha chochote
mama huyo kwa kuwa anamfahamu vizuri kipindi
chote ambacho kaishi pale.
`Mh! hapana naomba usimpeleke huyo binti kwa
huyo mzee cha kufanya njoo umuweke nyumbani
kwangu, huyo mzee si mtu mzuri kabisa
nakuambia'.
Katunje alishangaa sana kuambiwa kuwa mzee
kauzibe kuwa si mtu mzuri kwa nini? alimuuliza
`kwa nini unasema mzee kauzibe ni mbaya na
wakati nilikuhadithia kuwa huyu aliyemtibia ni yeye
mpaka kufika hatua hii unayomuona'
Mama huyo alizidi kumsisitizia sana
`Katunje najua huwezi kuniamini kwa nini
nakuambia hivyo, sasa njoo umuweke nyumbani
alafu wewe nenda kaangalie kwa mzee kauzibe
kama kuna usalama ukiukuta njoo umchukue
niamini'. Hakutaka kupoteza muda kwani siku hiyo
ndiyo aliahidiwa kuja kuchukuliwa baada ya
kutompeleka kwa ridhaa yake, alifika hadi kwa
mama huyo na kumuweka ndani na yeye akaondoka
kwenda kwa mzee Kauzibe.
Hatimae anafika karibu na njia hiyo lakini hakuamini
macho yake baada ya kumuona kijana wa mzee
swai yani Kimolo akirandaranda maeneo ya nyumba
ya mzee kauzibe pia akamuoana mzee kauzibe
akitokea ndani na kufuata njia ambayo alikuwapo
yeye. Alijificha na kumuangalia anakoelekea,
"Kauzibe unaelekea wapi sasa ". kijana kimolo
aliuliza swali kumuuliza mzee kauzibe
"nimewaambia mjifiche hapo naenda kumuangalia
kwake kule ili nije nae hapo mbona mnakuwa na
haraka".
Hapo ndipo chozi lilianza kumtoka kijana Katunje
huku akiwa haamini kwa lile analoliona kusalitiwa
na mzee ambae alipata kumuamini kwa asilimia
zote.......
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI 12
Endelea.............
Kijana Katunje chozi liliendelea kumtoka pale alipo
na asijue nini afanye, akifikilia kuwa yule mzee ndie
ambae alimsaidia kwa kila kitu mpaka hali ya Lyoto
inaelekea kuwa sawa kabisa sasa iweje leo aweze
kumgeuka kiasi kile alishindwa kuamini.
Alijitoa pale kimyakimya hadi kwenye nyumba ya
yule mama ambae aliweza kumsaidia kumpa taarifa
kuhusiana na bwana Kauzibe kuwa hana roho nzuri.
Alipofika alifanikiwa kumkuta mama huyo
akimnawisha maji ambayo ndani ya chungu
ambacho kimehifadhi maji hayo yalikuwa
yamechanganywa na majani ambayo hakuyatambua
kabisa ni majani ya aina gani.
Hakutaka kuhoji kwanza ndipo akaa chini huku uso
wake ukiwa umejaa makunyazi kwa hasira kubwa,
"Vipi mwanangu katunje nipe taarifa huko utokako".
Aliuliza Mama huyo, "Mama wee acha tu yani sijui
bila wewe kunipa ile taarifa sijui ingekuwaje mpaka
sasa hali ya huyu mtoto, ukweli nimemkuta kauzibe
lakini maneno niliyoyasikia na yale niliyoyaona ni
ukweli mtupu kuwa ni mtu mbaya".
Mama huyo alivuta pumzi na kumshika bega
katunje kisha akamueleza "Mwanagu dunia ya sasa
si kama enzi zile za wazee wetu ambao walikuwa
wanafahamu thamani ya mtu kama huyu, si kila
ambae atakusaidia basi ujue kuwa anakusaidia kwa
moyo mmoja wakiwemo basi ni wachache ila wengi
wao wanadhamila fulani ndani mwake baada ya
kukupa huo msaada wao".
Kauli za mama huyo zilimuingia barabara kijana
Katunje huku akitikisa kichwa kuashiria kuwa
anaelewa vyema. Pia aliweza kuuliza kuhusu yale
maji ambayo alimkuta nayo akimnawisha mgonjwa
huyo. "Mama sasa hayo maji yanahusiana na nini".
aliuliza katunje, "Mh haya ninamnawisha baada
kumgundua kuwa ana tatizo la kutoona lakini haya
yatamsaidia kabisa hadi anafikia hatua nzuri ya
kuona".
Katunje alimuaga yule mama na kisha akatoka na
kwenda zake kule anakoishi kwenda kuangalia
mazingira yaliyopo. Alifika kwa bahati nzuri alimkuta
mzee kauzibe akiwa anamsubiri kwa muda mrefu,
kauzibe alipomuona tu katunje alinyanyuka kutoka
pale alipoketi na kumuwahi katunje na kumpa
habari kama mgeni aliyemsubiri kwa muda mrefu
bila mafanikio. "Katunje unafanya nini sasa mpaka
sasa hukumleta mtoto kule nyumbani unajua kuwa
wanakutafuta kijiji kizima hapa".
Alibaki kumuangalia tu bila kumjibu huku
akimmezea mate, alikumbuka asionyeshe sura ya
ukauzu ili asije kuharibu vitu "Babu usijali
nimemhifadhi sehemu salama kabisa haina shida
kwa hiyo". Kauzibe alimsogelea katunje huku
akionekana kuwa na mshangao mkubwa sana juu ya
lile swala, "Unasemaje haya umempeleka sehemu
salama wapi?". Aliuliza kauzibe.
"Babu elewa kuwa nimemuweka sehemu salama
lakini pia wewe si ulitaka aletwe kwako ili afichwe
sasa tatizo nini hata huko nilikomuweka yuko
salama". Alitikisa kichwa akiwa haamini kwa lile
alilokuwa akilisikia kutoka kwa kijana huyo katunje
na kumfanya apatwe na hasira ya ghafla. "yani wee
kijana unaniweka sehemu mbaya mimi kwa nini
hukufanya jinsi tulivyokubaliana sasa unadhani kule
nyumbani zile dawa nani akazinywe na wakati
nimeziweka kwa ajili yake yeye, eeeh!"
Alifoka sana hapo ndipo katunje aliamini maneno ya
yule mama. Ghafla kundi moja la vijana takribani
saba walifuatana huku mbele akionekana kijana
shupavu kutoka kwa Mzee Swai anaejulikana kwa
jina la Kimolo. Huyu kijana Mzee Swai anamuelewa
sana kuliko hata mtu yeyote kwani ndie anamsaidia
katika kazi zake muhimu,
Mzee kauzibe aliwaona lakini hakutaka kumsitua
katunje, Ndipo kwa msaada wa masikio yake
ambayo yalihisi kusikia sauti za miguu ambayo
ilikuwa inakaribia kwa kasi ndipo aligeuka na
kuwaona wakija huku wameshikilia mishale na
mikuki yao.
Katunje alijua hapa hakuna usalama kabisa wakati
anataka kujaribu kukimbia alidakwa kwa haraka
sana na vijana hao na kutiwa mikononi mwa kijana
Kimolo, ambae jinsi alivyo akimshika mtu ni ngumu
sana kutoka mikononi mwake. "Vijana nendeni
humo ndani kwake mkaangalie kamuweka wapi
huyo bionti", Walitoka na kuanza kuangalia ndani
kote hatimae wanatoka na zile nguo ambazo alikuja
nazo Lyoto zikiwa ndani ya tenga. Walikuja nalo
hadi pale kwa Kimolo na kumpatia.
"Kimolo, hivi ndivyo tumevikuta humo ndani,"
walimpa taarifa hiyo. Katunje alishangaa sana kwa
nini Mzee kauzibe anaachiwa na kupewa nafasi ya
kuondoka pale alafu yeye ndie kashikiliwa.
"Twendeni atakwenda kusema huyu wapi kamuweka
hawezi kutufanya sisi kama wajinga namna hiii"
Mwendo ambao alipelekwa kwenda kwa swai
haukuwa wa kawaida alipelekwa kama mwizi.
Upande nyumba ya yule mama akiwa ndani na binti
lyoto akimpa baadhi ya matibabu, alishangaa utokaji
wa katunje mpaka muda ule hakuweza kutokea
ilimbidi afunge mlango akimuacha ndani humo lyoto
akiwa kalala, aliongoza njia ya kwenda kwa kijana
katunje ili aweze kwenda kujua nini kimemtokea.
Akiwa njiani anakutana na mama mwingine ndipo
wakaanza kusalimiana, "Mama MWAIJA mbona
kanga kiunoni wapi tena?" Mama huyo aliyekuwa
anaelekea kwa katunje aliulizwa. "Mwenzangu kweli
kuwa uyaone naenda kwanza kwa katunje pale kuna
swala tulikuwa tunaliongea muda fulani si unajua
kuwa Mwanangu Mwaija ndie atakae muoa yule
baadae". Walianza kucheka kwanza.
"Mh! lakini nadhani huna taarifa kuhusu katunje
zilizomtokea " Alishtuka kitendo kilichomfanya
aache kucheka kwa bashasha kutokana na utani
ambao waliufanya muda mchache uliopita. "Mh!
hapana nini ebu nieleze kuna nini tena
kilichomtokea?".
Walijikuta wanaingia kwenye dimbwi la simanzi zito
kwa pamoja, "Wakati niko njiani kuelekea kisimani
nikaliona kundi likija mbele yangu, nilipowapisha
kumbe walikuwa vijana wa mzee Swai yani yule
Kimolo wakimburuta Katunje sasa sijaelewa kafanya
nini?" Kauli hiyo ilimfanya Mama MWAIJA kutoamini
kwa kile ambacho kakisikia kutoka kwa rafiki yake
huyo.
"Sawa ahsante kwa taarifa ngoja niende nyumbani
tutaongea kesho". Waliachana pale kila mmoja
akaelekea njia yake. Mama Mwaija alichoamua ni
kufika hadi kwa mzee Kauzibe ili amdadisi chanzo
nini kilichomfanya ashikwe na bwana Swai kipi
alichokosa zaidi. Uelekeo wake haulkuwa na faida
sana kwani hakumkuta mlengwa aliyemkusudia,
aligeuza na kuelekea nyumbani kwake.
Upande wa Mzee swai walichokifanya ni kumfunga
makamba ya kutosha mbali na himaya ya nyumba
yake hiyo. Mzee huyu anajulikana kama ni Mtemi
ambae alichukua uongozi kwa nguvu na kutaka
kuongoza vitu vyote yeye kama yeye binafsi.
Walianza kumtesa kijana Swai huku wakimlazimisha
aseme wapi kamuweka binti lyoto, Kwa ujasiri
aliokuwa nao kijana huyo alikubali kuumia lakini si
kuruhusu Lyoto aingie mikononi mwa watu hawa.
Waliendelea kumpa mateso mpaka Katunje akatoa
siri.
"Jamani nataja ila naomba msimfanye chochote
ndugu yangu,". walimcheka sana tena mbele ya
Kimolo hapashindikani kitu. "Haya sema haraka
kabla hatujakumaliza hapa"
"Jamani binti nimemuweka kwa mama Mwaija".
Kwa kuwa ilikuwa ni usiku hawakutaka kwenda
waliacha na kuhitaji asubuhi waende kumchukua
huyo mtu, baada ya kutajiwa wapi anapatikana,
jamani mateso kama huna uvumilivu utaongea
chochote ambacho utatakiwa kusema. Majira hayo
ya usiku, mlinzi mmoja alimuonea sana hruma
kijana Katunje, hivyo alimuendea na kumshika
mkono pale alipofungiwa, Katunje alishtuka kwani
alijua anakuja kudundwa tena ndipo alipomziba
mdomo na kumnong`oneza masikioni mwake,
"Usipige kelele nimekuja kukusaidia utoke hapa".
Katunje alitikisa kichwa mbele na nyuma mara
kadhaa kuonyesha kukubaliana na lile swala.
Alimfungua kisha akamuonyesha njia ya kupitia
ambayo hapakuwa na wale walinzi wa mzee swai.
Majira hayo kijana alichanja mbuga zote hadi
kuingia Kijijini kabisa kwani alipita njia ya nje ya
kijiji kutokana na nyumba ya mzee swai ilivyojengwa
na nafasi ya kutoroka pale.
Wakati huo mlinzi huyo aliona atajulikana kuwa yeye
ndie aliyemruhusu kwani alipewa kazi ya kumlinda
asiweze kudhurika na wanyama wala kukimbia,
alichukua kisu chake na kujikata mguuni pamoja na
mkononi huku damu zikimvuja alianza kupiga yowe
la maana pale akiomba msaada. Baadhi ya walinzi
waliamka na kuanza kuangaza nini wafanye, Ndipo
bwana Kimolo akafika na kumuuliza kipi kimetokea.
"Kimolo kijana aliomba maji ya kunywa, nilikwenda
kumpa ndipo akanipiga kichwa huku akanipokonya
kisu na kunikata humu kisha akakimbia njia hii",
Aliongea pasi na kuogopa ule uongo ambao alikuwa
akiutunga mbele ya mtu mbaya kama Kimolo asiye
penda mzaha ndani ya kazi. Alicheka kisha
akasema kuwa haina shida kwa kuwa tayari
wanafahamu wapi kawekwa hivyo watamfuatilia
huyo mama.
Majira hayo katunje alifika hadi kwenye nyumba ya
mama Mwaija na kugonga mlango kwa nguvu sana
akiomba afunguliwe, mama huyo alifungua kwa
haraka na kumuingiza ndani haraka na kuanza
kumhoji kulikoni majira yale ya usiku. "Mama
nimetoroka, nimetoroka " Alisema huku akiwa
mwenye jazba
"Umetoroka?" Alishangaa mama mwaija.
"Hali yangu mama si nzuri sasa namuomba LYOTO
niende nae kujificha polini usiku huu kabla hata
asubuhi hakujafika". Mama Mwaija alianza kukataa
sana haitowezekana kwani ni usiku na kwa nini
aende na binti huyo?
"Naomba unielewe kama nilivyokuelewa mimi
mwanzo tunakuja humu ndani, fahamu kuwa
nilipewa adhabu kubwa baada ya hapo nikafanikiwa
kutoroka lakini nilimtaja kuwa hapa kwako ndiko
umemhifadhi mtu huyu, sasa asubuhi watakuja hapa
wakimkuta lazima watamchukua na sijui wanaenda
kumfanyia nini".
Mama hakuwa na kipingamizi chochote juu ya hilo
alimkusanyia baadhi ya dawa na kumpatia nguo
nyingi ili amhifadhi na baridi. Japo na maumivu
aliyo nayo alikubali kumbeba na kuondoka nae
maeneo ya polini mbali sana na pale kijijini.
Majira ya asubuhi msako ulifanyika lakini
hawakuambulia kitu chochote. Ndani ya eneo la
mzee Swai anafuga mbuzi wengi sana. Kijana
mmoja ambae hufanya kazi kwa mzee huyo ya
kumuuzia mbuzi wake siku hiyo alifika pale akiwa
na baiskeli yake alimshika mbuzi ambae alihitajika
siku hiyo kuuzwa, Kwa bahati mbaya hapakuwa na
kitu cha kubebea ndipo KIMOLO akampatia lile
tenga na zile nguo ambazo alizifanyia kama kamba
baada ya kuzichana na kumfungia miguu mbuzi
huyo.
Safari hii ya kijana huyu muuza mbuzi wa Mzee Swai
ilienda mbali sana huku mbuzi wake akiwa ndani ya
tena hilo, hatimae anaingia ndani ya kijiji cha
BWAWANI huku akimnadi yule mbuzi. Huwa
anasafiri mbali sana ili apate kuuza kwa beim
kubwa na sehemu ambayo ni nadra kupatikana
mbuzi.
Watu walianza kufika taratibu pale uwanja wa
matangazo ambapo aliruhusiwa kutangaza bei ya
mbuzi huyo na kufanya mnada. Kwanza alimtoa
ndani ya tenga lile na kumfungua kamba ya zile
nguo. alimfunga kamba ya shingoni na kumuweka
kwenye mti uliokaribu na hapo. Hakika mbuzi
alinona na watu walimsifia sana.
Kwa mbali wanaonekana marafiki wawili MAPATO
na SIKUJUA wakiwa wanakaribia pale "Bwana wee
acha utani ngoja nikaangalie bidhaa tunaweza
kumnunua mbuzi na kumchinja kisha tukamla na
wanakijiji ili wasituone wabaya bwana au unaonaje"
Alisema bwana Sikujua.
Walifika pale na hapo vilevile Mzee Mambo sasa
alifika ili apate kujua nini kinaendelea. Hapakuwa
mbali sana nae SUSU anaingia akiwa na shauku ya
kujua nini kinaendelea. Susu alishtuka sana baada
ya kuliona lile tenga alilifananisha kama lile ambalo
lilipotea kipindi cha muda sana kwa bwana Sikujua,
nae Mee Sikujua aliliona lile Tenga na kulifananisha
na lile ambalo walienda kumtupia SIKITU.
Kwa upande wa Mzee Mambo sasa alimuangalia
sana yule mbuzi miguuni kwa ile nguo ambayo
alifungiwa nayo, machozi yalianza kumtoka baada
ya kuvuta taswira kuhusu mwane kupotea. Ndipo
Mzee MANYENYE akajitokeza kumnunua yule Mbuzi
na kijana akafunga tenga lake na kutaka kuondoka,
kabla hajaondoka ndipo susu alimfuata na
kumuuliza jambo "Kijana unakaa wapi mana unauza
Mbuzi wazuri sana", Susu aliuliza "Mimi naishi
KILIMALONDO tena karibu japo mbali ukifika uliza
kwa Mzee Swai utanipata".
Walipeana mikono na kijana akaondoka zake,
upande wa Mzee Mambo sasa alimfuata mzee
Manyenye hadi kwake, alipofika alimsalimu kisha
akaenda hadi miguuni kwa mbuzi na kumfungua lile
guo lililochanwa na kusema, "Hakika mwanangu
bado naamini yuko haiiii". Mzee Manyenye alishtuka
kuambiwa yuko hai "Wee yuko hai una maana gani
kusema hivyo?".
"Ndugu naamini yuko hai amini hilo kwa sababu hii
nguo ndio mara ya mwisho alivaa hii hatimae leo
naiona kipande cha kitambaa mwananguu kama upo
popote hakika nitakutafuta".
Upande wa Mzee sikujua hakuamini alimueleza
mapato alichokiona kuhusiana na ule mnada wa leo
uliowajia pale kwao.
Je nini kitatokea.........
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU 13
Endelea....................
Bwana sikujua alifikia hatua ya kuhamaki kabisa
kwani jambo ambalo limetokea punde lilimfanya
kuathirika kisaikolojia kabisa, kwa upande wa mzee
mapato alifikilia jambo fulani ndipo akamsogelea na
kumshika bega huku akimueleza jambo fulani.
"Unajua hapa kuna kitu ambacho nakihisi kipo na
tusipokichukulia hatua mapema basi tutajikuta
tunaingia sehemu mbaya". aliongea bwana mapato
akimueleza rafiki yake kwa jambo ambalo alilifikilia.
"Mh! unadhani mimi kuna kitu ambacho nitakipinga
mbele yako kwani najua wewe pekee ndio msaada
wangu mkubwa sana kwa sasa" na yeye alimtoa
wasiwasi na kumuahidi kuwa anamuamini sana
kuliko kitu kingine ndani ya kijiji cha bwawani,
Wakati wanaendelea kuongea wakati huo ndipo
anajitokeza kijana susu ambae alipita kama njia na
kuwakuta wazee hao wakiongea mada ambayo
alihisi kama inamhusu, Alijibanza mahali huku akiwa
makini katika kusikiliza kile ambacho
wanakiongelea wawili hao, alibaki kushika mdomo
tu kwa yale ambayo alikuwa anayasikia.
"Sasa bwana sikujua unajua mpaka sasa baada ya
kumpoteza mama Mengi basi hakuna mtu yeyote
ambae atajitokeza kuonyesha anatambua jambo
lolote katika lile".
Susu baada ya kusikia hayo alishindwa kuamini
kabisa kwa yale ayasikiayo ndipo mwili wake
ulianza kubadilika na kuanza kutetema kwa hofu
iliyochanganywa na hasira kubwa sana. `ina maana
hawa wazee wanahusika kwenye mauaji ya mama
mengi?". Kwa bahati mbaya hayo ambayo alikuwa
anayaongea ilimfanya kutoa sauti ambayo iliwafikia
vyema wazee hao wawili,
"Mh! kuna mtu anaongea huku nyuma ya nyumba".
Aliongea bwana sikujua, "Ngoja nipite huku" Mzee
sikujua alitoka kwa haraka sana na kuzunguka
upande wa pili na hatimae akamkuta kijana susu
kajiinamia akijitega kusikiliza.
Sikujua alichukua gongo la mti na kumtwisha nalo
kichwani kitendo kilichomfanya susu kutoa ukelele
mdogo sana ambao haukuwa rahisi kuusikia kabisa
hatimae akaanguka chini na akazimia palepale.
Alirudi na kumpasha taarifa rafiki yake, "Mapato
njoo haraka sana njooo" Mapato alishangaa kuitwa
vile haraka sana kuna nini, "Nini tena?" aliuliza
mapato.
"sasa huyu kijana alikuwa anatusikiliza mwanzo hadi
mwisho na unajua allivyo msumbufu sasa nimemtia
adabu kinachotakiwa sasa tumuweke ndani humo
haraka sana". Walifanya hivyo lakini huku mzee
mapato akihofu sana juu ya lile swala ambalo
mwenzake kalifanya bila hata kumshirikisha.
"Yani ndugu yangu sasa unazidi kabisa kwa hatua
hii mbona unafanya vitu vya hatari hili halijaisha
unalileta lingine jamani aaah!".
Walimuingiza ndani kisha wakamfunika mahali huku
wakimfunga kamba. "Mapato bila hivi haki ya
mungu huwezi kuishi vizuri kabisa hawa ndio
ambao wanatufanya tuishi kwa wasiwasi hapa kijijini
hatuna raha kwa ajili ya hawa vinyago bwana na
nasemaje yeyote ambae atajifanya kunifuatilia au
kufuatilia kesi hii basi halali yangu".
Kwa upande wa mzee MANUALI mjukuu wa Susu
ilifika mpaka mpaka jioni kwenye nyumba ya
mjukuu wake hamuoni kabisa. Alianza kupatwa na
wasiwasi mkubwa juu ya huyo mjukuu wake, ndipo
alipoanza kutembea kijijini hapo na kuulizia kwa kila
kijana mwenzake.
"Jamani hamjamuona susu majira haya?" alimuuliza
kijana mmoja ambae alijulikana kwa jina la
NDUNYA.
"Babu hapana japo susu ni rafiki yangu sana kwani
tangu tuachane pale uwanjani kwenye mnada wa
mbuzi nilimuona tu akiongea na yule kijana
aliyekuja kuuza baada ya hapo sijamuona tena"
Mzee alianza kuchanganyikiwa
"Ndunya unajua kuwa leo ni kitu cha ajabu sana
kwani hakuna hata siku moja ambayo alifika mpaka
sasa hivi yani kuchelewa kurudi".
Ndunya alisikitika sana baada ya kusikia taarifa
hiyo. "lakini babu susu ni kijana mkubwa sasa si wa
kumfuatilia sana labda tusubiri kesho mimi asubuhi
nitakuja mapema sana ili nijue kama karudi au laah
alafu tutajua nini la kufanya". Mzee huyo alikubali na
akarudi nyumbani kwake lakini hakuamini. Kijana
Ndunya alianza kutembea katika kila eneo ambalo
alijua kuwa lazima susu atapatikana lakini hakuweza
kupatikana, alifika hadi hadi kwa mzee Mambo sasa
na kumueleza jinsi mzee manuali anavyohangaika
kuhusu kijana wake Susu,
"Ndunya una maanisha kwamba?" aliuliza mzee
mambo sasa
"Ninacho maanisha kuwa mzee Manuali analalamika
kuwa kijana wake susu hajamuona mpaka sasa hivi.
Kwani sio kawaida yake kuchelewa kurudi lakini pia
hata mimi sijamuona" alimueleza kila kitu.
"Mh! hivi haya mambo mpaka lini jamani ila itabidi
lifanyike jambo sasa".
Ndunya aliondoka na kwenda nyumbani kwake.
Asubuhi na mapema sana, alionekana kijana Ndunya
nyumbani kwa mzee Manuali, jambo la kwanza
alifika kwenye nyumba ya kijana susu na kukuta
kufuli alishangaa sana ndipo akaenda kuchungulia
dirishani lakini hakuona chochote kabisa. Ndipo
akamgongea mlango mzee Manuali, alipotoka ndipo
akamueleza kitu, "Mzee kuna kitu hapa ambacho
nahisi sio kizuri susu hayupo kabisa mlango wake
umefungwa pale".
Mzee manuali alikaa kwa muda kidogo kisha
akaanza kufuta machozi yake, "Mjukuu wangu susu
ni kijana ambae alikuwa ananisaidia sana katika
kazi zangu za utabibu hapa nyumbani, sasa sijui
hata nifanye nini". Mala muda mchache anafika
mzee Mambo sasa akafika na yeye kuungana na
huzuni hiyo iloyomkumba bwana Manuali. Walijadili
jinsi gani watalifanya kabla hata hawajatoa taarifa.
Asubuhi hiyo ndani ya kijiji cha KILIMALONDO
anaonekana kijana KATUNJE akiamka huku pembeni
akiwa na binti LYOTO, "Daah haya maisha sasa
niliyoyaanza sasa itakuwaje " Alimuangalia yule binti
kwa muda sana kisha akajiuliza "Mh! sasa kwa nini
nilikubali kumchukua huyu mtu na huku anakuja
kuniletea matatizo kama haya au nimuue kabisa ili
niondokane na haya".
Alifikilia sana kwenye swala la yeye kutaka kumuua
binti huyo. Alisimama na kutembea mbele kidogo
na kuchukua gongo kubwa sana la mti. Alilinyanyua
na kumsogelea binti lyoto na kutaka kumshindilia
jiti hilo kichwani ili amuue kabisa ili aepukane na
yale ambayo aliyafikilia. Ndipo lyoto akageuka huku
akijinyoosha akitoka usingizini jinsi alivyo lyoto
ilimfanya Katunje afiche lile gongo na kulitupa
pembeni. Alianza kulia sana na kumkumbatia binti
huyo kwa uchungu mzito alio nao,
Alimuinua na kumkalisha huku akimuangalia kwa
makini sana. "Mbona unataka kuniua nimekosa
nini?" , Ilikuwa ni ajabu sana kusikia maneno
ambayo yalimtoka lyoto kumwambia katunje. "Ina
maana unaona sasa hivi?" Katunje alishindwa
kuamini kwa lile ambalo alilisikia kutoka kwa lyoto,
kwani ana muda mwingi sana akiishi na tatizo lake
la macho pamoja na masikio.
"Mh! samahani sana lyoto siwezi kukuua kabisa
naomba unisamehe na nakuahidi nitakulinda kwa
kila hali mpaka hali yako inaporejea" Lyoto alikuwa
anaonyesha dalili za kuona baada ya kuanza
kuonyesha viini vya macho.
"Ndio naona sasa hivi". Lyoto alijibu.
"Kha! ina maana kuwa pia unasikia vizuri sasa hivi!"
Alishangaa sana baada ya kujibiwa na lyoto.
Nyumbani kwa Mzee Swai palianza sasa kuamka
baada ya kutangaza rasmi kutafutwa kwa kijana
Katunje. Ndani ya kijiji hiko watu waliambiwa tayari
kuwa kwa yeyote ambae atahusika kumficha kijana
katunje basi atapewa adhabu. Kwa upande wa
Kimolo walifika kwa mama mwaija na kumkuta,
walimbeba mkuku mkuku kutokana na kauli ya
Katunje ya kuwa anahusika katika katika kumhifadhi
Binti lyoto.
Wanakijiji hawakuweza kuvumilia kwa hali ile ndipo
maandamano yalianza. vijana wa kijiji kile walijiunga
na kusambaa mitaani ili kuwafanya watu kupinga
yale ambayo yanaendelea kutendeka. Walifika
karibu najumba hilo la bwana Swai.
"Uonevu hatuutaki kabisa jamani huyo mama wa
watu kawakosea nini!".
Maneno ya watu yaliendelea huku wakishinikiza
katika swala la kuachiwa huyo mama ambae
alikamatwa. Kimolo alimuendea mzee Swai na
kumueleza jambo "Mzee unawasikia hao wanakijiji
wanavyoongea huko" Mzee Swai alisimama na
kusema "Hakuna kitu ambacho kitasababisha
kunirudisha nyuma kwenye shughuli zangu hata
kidogo ngoja niende hapo".
Alitoka nje na kuwaona wakiendelea kuongea.
"Nyinyi wanakijiji ebu kaeni kimya niwaeleze kitu"
watu walikaa kimya na kumsikiliza. "Nataka
niwaambie jambo sasa mnafahamu kuwa vijana
ambao tumewakaribisha sasa ndio wanakuwa karibu
katika kutuharibia utaratibu wetu wa hapa kijijini,
sasa mmoja wa haya mambo ni kijana Katunje,
tulimuita ili tumuulize kwa nini alichukua jukumu la
kumchukua mtu wakati yeye mwenyewe ni mgeni
hapa" Watu walianza kuelewa nini ambacho mzee
swai anazungumza "pia nataka munielewe huyu
mama ndie anahusika kumhifadhi huyo binti,
tumemkamata ili atueleze wapi kamuweka na nyinyi
nawataka sasa muelewe yeyote ambae atamkamata
kijana huyo basi atapatiwa mifugo ya kutosha
kutoka kwangu".
Kwa upande wa katunje aliandaa sehemu nzuri
ambayo iliweza kumhifadhi kisha akamuacha pale
lyoto na kwenda kutafuta chakula kwani hawawezi
kuishi pale bila kuwa na chakula, alitembea haraka
haraka hadi karibu na kijiji chao kwa bahati nzuri
alikutana na shamba la mihogo aliweza kung`oa
mihogo kadhaa na kuondoka nayo. Alifika hadi kule
eneo ambalo alimuacha lyoto na akaiweka chini.
Walianza kutafuna taratibu lakini Lyoto alionekana
kutoridhika na ile hali katunje alilitambua hilo ndipo
akanyanyuka na akamueleza amsubiri kwa muda
kidogo.
Katunje aliondoka na kuelekea kijijini kwa uharaka
ambao alikuwa anaufanya alifanikiwa kufika
mapema katika majumba ya kwanza kabisa na kijiji
chao, "sasa hapa nifanye haraka sana kupata sufuria
kadhaa za kupikia".
Alifika kwenye nyumba moja na kufanikiwa kuiba
sufuria na baadhi ya mahitaji ambayo aliyakuta kule.
Alirudi hadi kule polini ndipo alipoanza kuandaa na
kupika mihogo ile, hakika lyoto alionekana kufurahi
sana juu ya lile ambalo katendewa na kijana Katunje
ambae alimfahamu kama ndugu pekee wa karibu
sana.
Hatimae mama mwaija anafanikiwa kutolewa bila
hata kudhulika lakini taarifa ya kukimbia kwa kijana
Katunje wengi wao wanaifahamu sana. Majira ya
usiku wa saa nane katunje alifika kijijini kwao na
kufungua nyumba yake na kuchukua nguo zake zote,
wakati anatoka akiwa njiani alidondosha moja ya
nguo yake bila kufahamu kwani alikuwa anafanya
kwa uharaka sana, hakuishia hapo alifika hadi
kwenye nyumba moja na kuiba kuku mmoja bila
hata wenyewe kufahamu. Alipofika kule polini
alimkuta bado lyoto kalala.
Kwa kuwa alimfanya kama ndugu yake wa damu
hivyo hayo yote aliyafanya kwa lengo la
kumfurahisha lyoto na kumfanya ajisikie hali nzuri
sana kwani hata hapo sasa mwili wake ulizdi kurudi
na kuwa nzuri sasa. "Eeehee! huyu kuku ni
kumchinja kisha asubuhi na mapema nampika,
nishakubali kuwa maisha yangu sasa niyaweke
hukuhuku mpaka pale lyoto akikamilika na hali
yake." Aliyaongea hayo huku akimchinja kuku yule.
Ndani ya kijiji cha Kilimalondo majira ya asubuhi
Bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la UDEVU
kutokana na sehemu yake ya kidevu kuwa ndefu
sana ndipo wakampachika jina la utani ambalo
lilizoeleka sana na hata watu kumsahau kwa jina
lake halisi la MWANYALI.
Bwana kidevu alisikika akilalamika kuhusu kuibiwa
kwa kuku wake mkubwa sana alafu jogoo, wakati
huohuo mama mwaija anaenda kwenye nyumba ya
Katunje ndipo anakutana na mzee Kauzibe. mama
mwaija alishangaa sana asubuhi ile yote mzee huyu
kafuata nini kwenye nyumba ya katunje. Alichoamua
ni kukaa pembeni ili amuangalie kwa umakini nini
ambacho anakifanya pale.
Mzee kauzibe alisukuma mlango wa nyumba hiyo
bila mafanikio, ghafla bwana udevu anapita maeneo
hayo huku akiendelea kutangaza "jamani jamani,
kuku wangu nimeibiwa na huyo aliyeiba basi
naomba ajiangalie sana namhitaji kuku wangu".
Hapo ndipo mama mwaija alimshuhudia bwana
kauzibe akijibanza pembezoni mwa nyumba ya
katunje. Alishangaa kwanza kisha alimuona bwana
udevu akifika kwenye nyumba ile akigonga mlango
bila mafanikio na kuondoka zake baada ya yeye
kutoka ndipo kauzibe akajitokeza akiwa na gongo
kubwa akiwa na nia ya kuvunja kufuli ambayo
ilionekana pale mlangoni.
Mama Mwaija palepale alijitokeza huku akikohoa
kiunafiki ili ajue kama kuna mtu. Mzee kauzibe
alipatwa na mshangao sana. "Aaah! mama mwaija
kumbe upo hapa karibu ukiniangalia tu!". alisema
bwana kauzibe.
"Ndio hayo yote uliyoyafanya nimeyaona haya
kinachokufanya asubuhi yote hii kuja kuvunja
nyumba ya kijana aliyeijenga kwa nguvu zake nini?".
Swali ambalo aliuliza mama mwaija lilimfanya
ababaike sana kauzibe na kushindwa kujibu
chochote zaidi ya kubung`aa m,acho tu.
"Nakuuliza mzee wewe usiyekuwa hata na huruma,
wakati unaona kijana anavyopata matatizo na wewe
baada ya kumsaidia unamshindilia haaaa". Mzee
Kauzibe hakuwa na la kuongea wakati huo ndipo
akapata wazo la kumzubaisha mama mwaija "Mama
mwaija alipo kauzibe mimi napafahamu, ndio
maana kaniagiza nije kufungua mlango wake ili
nimchukulie kitu ambacho aliniagiza".
Mama mwaija hakuchoka kumuuliza maswali
ambayo yalimfanya bwana kauzibe ashindwe kabisa
kujitetea na hatimae na kuamua kuondoka, "sawa
unaweza kunionyesha wapi alipo huyo katunje?"
aliuliza mama mwaija " hapana siwezi kukuonyesha
kwani hataki ajulikane wapi alipo". Kauzibe alijitetea
"sawa mimi naenda kwa swai na kumuambia kuwa
kauzibe anafahamu wapi katunje kakimbilia sasa
ndipo utakija kuwatajia". Neno hilo lilimtoa kijasho
mzee kauzibe na kumfanya kuanza kuangaika pale
na asijue nini ambacho atakisema.
Ghafla wanaoinekana vijana kadhaa wa mzee swai
wakikaribia pale kwenye nyumba ya katunje, Baada
ya kushuhudia jambo hilo wote waliondoka pale
kuwaepuka watu hao ambao wanajulikana kuwa
wakorofi sana.
Kwa upande wa mzee swai alimuita kijana ambae
anatumika katika swala la kuuza mbuzi wake, kwani
huyu mzee alikuwa na mbuzi wengi sana. "Ehee
kijana sasa hivi mbuzi unauzaga wapi?' Swai
alimuuliza kijana huyo
"Kuna kijiji kimoja hivi kipo mbali kidogo na hapa
huko hakuna mbuzi kabisa inakuwa rahisi kufika tu
na watu hununua lakini wanendelea kuwahitaji tena
wengi wa kutosha".
Mzee swai alimsifu na kumuahidi mengi mazuri
sana katika kazi yake.
Ndani ya kijiji cha Bwawani wanaonekana Mambo
sasa na mkewe wakiondoka pale kijijini wakiwa
njiani kuelekea kijiji kimoja kiitwacho Shimomo,
walitembea kwa mwendo mrefu sana na hatimae
wanakaribia kijiji cha shimomo. "Mke wangu sasa
tunaingia ndani ya kijiji chetu cha shimomo
kinachohitajika wewe ujikaze na ujiamini kama
kutakuwa na kesi yeyote mimi ndie nitakae jibu"
Mambo sasa alimueleza mkewe.
"Sawa mume wangu ila naogopa sana wanaweza
wakatufanyia mabaya zaidi ya yale ya kwanza."
Mama sikitu aliongea kumueleza mumewe kuwa
hofu yake ni ile ya kufanyiwa kama mwanzo. "usiwe
na hofu pia naomba usidiriki kuniita jina la Mzee
Mambo sasa tena nadhani jina langu litafaa huku
ukiniita sawa?". Alimueleza mkewe kuwa asijaribu
tena kumuita jina ambalo alikuwa analitumia kijiji
cha Bwawani na badala yake amuite jina lake halisi
ambalo analitumia
"Mh! sawa lakini nilizoea lile jina ila nitajitahidi".
Hatimae wanaingia ndani ya kijiji hiko na kukuta
sherehe kubwa sana ambayo ilikuwa inaendelea
pale. Mambo sasa alimuomba mkewe akae
pembeni kwanza ili yeye akakague jinsi gani
wanaweza kuingia pale ndani ya kijiji kile, wakati
huo sherehe zimetanda kila kona watu wamelewa
sana baada ya kunywa pombe za kutosha.
Mama sikitu hakutaka kabisa kusikia swala la yeye
kubaki pale alfu mumewe aende kule alichokihitaji
yeye na mumewe waongozane hadi kule sehemu
husika.
Waliongozana wote kwa pamoja wakiwa
wameshikana mikono, haikujulikana kwa nini na nini
ambacho kiliwapata mwanzo. Walifika hadi kwenye
nyumba ambayo waliifahamu kuwa familia yake
ilikuwa pale kwa kipindi chote. Lakini
hawakubahatika kukuta mtu mkubwa zaidi ya mtoto
mdogo ambae baada ya kuulizwa aliweza kuelekeza
wapi ambapo wazazi wameelekea. Walitulia pale na
kumuacha kijana huyo mdogo akielekea kule
ambako zilikuwa zinaendelea sherehe za pale
kijijini.
Baada ya muda ndipo anatokea mzee wa miaka
kadhaa akiwa na yule kijana "Mke wangu kuwa na
ujasiri baba yangu yulee anakuja". Kweli alisimama
bwana Mambo sasa na kumfuata baba yake, hakika
mzee huyo aliangua chozi kwa kutoamini kabisa
kama aliye mbele yake ni mwane yeye. "Mwanangu
CHITO mwanagu kweli umerudi mwanangu". Kumbe
bwana Mambo sasa anafahamika kwa jina la CHITO
japo haikufahamika kwa nini alibadili jina kwa
kipindichote na ndio sababu ambayo ilimfanya
amuambie mkewe asizoee kumjuita kwa jina la
Bwana Mambo sasa.
"Baba mim i mwanao nimerejea tenanaomba
mnipokee baba yangu".
Walionekana kuwa na huzuni wote kwa pamoja huku
machozi yakiwatoka. walikaa mahali na kuanza
kuongea, Mzee huyo aliwaondoa shaka kabisa
kuhusu wao kupokelewa. "Mwanangu ondoa hofu
kabisa mana yule mtu ambae aliwazuia nyinyi na
kuwafanya hapa muondoke kafariki zamani sana,
hivyo ikatufanya sisi kama wanafamilia kuanza
kuwatafuta nyinyi mpaka sasa hatujafanikiwa lakini
leo kama maajabu unarudi mwanagu".
Mzee Chito alishtuka kidogo kutokana na kauli ya
baba yake iliyosema kuwa "kuwatafuta nyinyi"
ilimfanya kujenga swali hapo "Baba sijaelewa hapo
kwmba mlikuwa mnahangaika kututafuta na nani?".
"Mwanagu unanikumbusha mbali na hivi
ninavyokuona furaha yangu inazidi kupaa hewani,
nduguyo KATUNJE tangu hapa aondoke baada ya
wewe kufukuzwa basi na yeye akakasirika
akaondoka kabiosa na hatujui wapi ambapo kaenda
na kila kijiji tumefika lakini hatukupata taarifa
yeyote kuhusiana na yeye basi tukajua mmekufa
wanagu".
Hakika ilikuwa simanzi kubwa sana kwa chito.
"Baba baada ya kutoka hapa nilibahatika kupata
mtoto wa kike ambae tulimpa jina la mama yangu
kwa kumkumbuka SIKITU lakini unyama wa kile kijiji
tulichofikia basi wamemuua mtoto wangu hayupo
yani kapotea kwa mazingira ya kutatanisha baba".
Mzee huyo aliyejulikana kwa jina la MAMBO SASA
mwenyewe, alishtuka kwanza "Mjukuu wangu
wamemuua? kijiji gani hiko", aliuliza baba yake huku
mkewe chito akiwa mbali akisikiliza tu bila hata
kuchangia chochote. "Baba kinaitwa BWAWANI".
Mzee alivuta taswaira na kumbukumbu kisha
akauliza
"Hakuna jina lingine la hiko kijiji?" Ndipo chito
akakumbuka kisha akasema "ukweli sifahmu vyema
hiko kijiji kwani hata sisi kukifikia tulipata tabu na
muda mwingi lakini kina sheria kali ambayo ilikuwa
inatukataza kuwa tusifike kwenye bwawaa
amb......." kabla hajaendelea ndipo mzee huyo
alimkatisha na kumuambia jambo
"Eheeee! nakifahamu tayari kilikuwa kinaitwa
SONGAMBELE na alikuwa anaongoza mzee mmoja
kipindi sisi bi vijana aliitwa ZAMALIO".
alimkumbusha "Haswaa baba kweli
unakumbukumbu nzuri.
"Ni kwweli kwani nakifahamu na pia kilifutwa hiko
lakini hilo jina labda kifufuliwe sasa hivi na kupewa
jina hilo.". Basi walipokelewa vyema baada ya
kufika ndugu wengine.
Upande wa kijiji walichotoka tafrani ilikuwa kubwa
watu hawakai kwa amani kwani kila kukicha mambo
yalizidi kuwa mambo makubwa sana.
Sasa ndipo mzee mapato anamshawishi mwenzake
waende kwenye lile bwawa ambalo lilikatazwa kwa
muda mrefu sana ili kwa sababu bwana mapato
kapata ndoto ambayo ilimkumbusha jambo ambalo
linamhitaji kuelekea kwenye hilo bwawa, "Rafiki
yangu unataka kwenda tena kuanzisha mambo ya
ajabuajabu tena" alisema sikujua "hapana sasa hivi
kipindi cha mavuno kinakaribia sasa unadhani fedha
tunazipata wapi sasa". waliondoka hadi bwawani
ndipo mzee mapato akaingia katikati ya bwawa hilo
na kuchinja kuku kama kafara la damu pale na
kisha akachukua lile kitu kama pembe ambalo
lilihifadhiwa kwa muda sana katikati ya bwawa hilo.
Alilichukua na kuanza kusema baadhi ya vitu kisha
akaliacha na likazama tena chini na yeye akatoka.
bwana sikujua alimuuliza "Sawa sasa umemnuia
nani wa kufa "
Mapato hakuwa na wasiwasi sana kwani hakuwa na
wasiwasi wowote "niliyemnuia ni Mzee Mambo sasa
tutaenda kumshawishi pale kwake kwa
kumdanganya tumeuona mwili wake kwenye bwawa
na akija si ndo kaisha" walipongezana kwa fikra
walizonazo."sasa susu tunamfanya nini mana unajua
kuwa alipo pale hajala kabisa" walitulia kisha
mapato akasema "ahaa usijali akiwa msumbufu
sana tunampiga tena nyuma ya kichwa atapoteza
kumbukumbu kisha tunamuachia hatoweza kabisa
kutukumbuka". walirudi nyumbani lakini taarifa
wanayoipata kuwa mzee Mambo sasa kaondoka
hata bila taarifa yani kaama kabisa.... mapato
aliishiwa pozi kabisa kwani atampatia wapi na
wakati yeye ndie nia kubwa kwenye lile swala
pale.........
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE 14
Endelea....................
Taarifa ya kuondoka kwa Mzee Mambo sasa
ilishaenea kijiji kizima, nz kila mmoja alishangaa
kwa upande wake. Taarifa ilipofika kwa mwenyekiti
na yeye ilimchanganya ilimbidi atumie akili ya ziada
kujiuliza analitatuaje. Muda mchache anakuja bwana
Manuali kwa mwenyekiti.
Mzee manuali hakika alikuwa na majonzi sana
kupotelewa na mjukuu wake ambae alikuwa
anamtegemea sana kwenye mambo ya utabibu wa
pale kijijini. Alikaribishwa na mwenyekiti huyo na
kupewa kigoda ili akalie. Baada ya kukaa
anaonekana Mzee Manualiakianza kulia taratibu.
Ilibidi mwenyekiti asitaajabu kwa nini mzee mzima
kama huyo aanze kulia mbele yake. "bwana SEMENI
aaah hii siku ya tatu sasa mjukuu wangu haonekani
kabisa jamani sijui mmechukua uamuzi gani".
Mwenyekiti alishtyuka kama ndio kwanza
anafunguliwa kichwa na masikio. Mwenyekiti huyu
anayejulikana kwa jina la SEMENI ambae alipewa
wadhfa wa kuongoza kijiji cha Bwawani alitulia kwa
muda sana huku mzee Manuali yakimtoka maneno.
"unajua bwana Manuali haya mambo sasa yanazidi
kuwa magumu kila baada ya siku hapa sasa hivi
nimeletewa taarifa kuwa bwana Mambo sasa
kaondoka bila hata ya taarifa yani kaama kabisa".
Baada ya kusikia kuwa mzee Mambo sasa
kaondoka, ndipo manuali akanyamaza kidogo
kuongea.
"Mwenyekiti ina maana kaondoka kabisa hapa, je?
sababu gani ambayo imemfanya aondoke".
Mwenyekiti huyo alitikisa kichwa kuonyesha kuwa
hakuwa na la kumjibu kabisa kwa upande wake.
"Labda tufanye hivi, nitaitisha kikao cha dharura
alafu tuone tunasaidia vipi haya mambo". Mzee
Manuali aliondoka pale kuelekea nyumbani kwake.
Alikutana na kijana Ndunya njiani alimpatia taarifa
iliyotoka kwa mwenyekiti na pia akamueleza kuhusu
kuondoka kwa bwana Mambo sasa.
Ndani ya kijiji cha SHISHIMO anaonekana bwana
Chito ambae alijulikana sana kama Mambo sasa
kipindi yupo bwawani, na alitumia jina la baba yake
mzee mambo sasa kwa malengo yake yeye
mwenyewe, kwa wakati huo yuko shambani
akipalilia mahindi pamoja na mihogo. Wakati
anaendelea huku akiwaza vitu vingivingi ndipo
aliposimama na kuanza kubana kidole kuashiria
kama kuna jambo ambalo analifikilia sana.
alionekana akibeba jembe lake na kuondoka Katika
tembea yake ndani ya shamba hilo alishangaa sana
kwa kutoiona njia ya kutokea kwani ndio ilikuwa
mara yake ya kwanza kufanya kazi shambani baada
ya maelewano ya kifamilia. Alizunguka shamba
zima njia haioni, Huku nyumbani mkewe na baba
mkwe wake mzee Mambo sasa wanaendelea
kuongea ndipo mada ya chito ilivyoingia. "Mh!
mbona mume wangu mpaka sasa hivi jioni inaingia
hajarudi?" Mama sikitu alihoji kwa hofu, " Usiwe na
shaka atakuwa ana hasira ya maendeleo yani
wanangu wote wana akili ya maendeleo kama jina
langui lilivyo Mambo sasa hivyo ndivyo walivyo".
baada ya kuambiwa hivyo alitulia na wakaendelea
na shughuli zao, lakini kadri muda ulivyozidi ndipo
kiza kilianza kuingia na Chito au baba sikitu
hakuonekana kabisa. Ilimbidi kwa hofu kubwa sana
mama sikitu aondoke pale na kumfuata huko
shambani ili ajue nini sababu inayomfanya achelewe
sana.
Wakati anaelekea huko ndipo na mzee mambo sasa
anashtuka kuwa muda umekwenda sana alimuita
mkwewe lakini hakuitika alimtafuta kwa kuzunguka
nyumba nzima lakini hakufanikiwa kumuona kabisa
"Au atakuwa kamfuata mumewe shambani, lakini
chito na yeye mpaka sasa kulima tu" aliamua
kuongoza njia japo kwake ni tabu sana kutembea
hatua zake ni kama kinyonga ambae yupo kwenye
mwendo wa malingo, alikuwa anatembea na
mkongojo wake, kumbe mama sikitu katembea na
kwa bahati mbaya alishindwa kabisa kutambua wapi
shamba lipo hivyo aliamua kugeuza njia ili kuepuka
kupotea.
wakati anarejea kwenye moja ya kona alifanikiwa
kumuona mzee huyo ndipo aliamua kumfuata
taratibu bila hata kumstua ili amuone anataka
kwenda wapi kwani alishakuwa na mashaka nae
tangu mwanzo wanafika pale na yale matatizo
ambayo ambayo waliyapata tangu mwanzo. Kwenye
mwendo wao walifika shambani hapo giza likiwa
limeingia tayari na sauti na za wanyama pamoja na
wadudu mbalimbali zikipishana.
Kwenye shamba hilo chito alikata tamaa kabisa
ndipo alishangaa kuona mwanga ukiwa unamulikwa
mahala fulani, kumbe yule mzee kuna kitu fulani
ambacho kilitoa mwanga kama taa inayotumia
nguvu ya umeme ikiwa imewashwa. Mama Sikitu
alishangaa ndipo akajiziba mdomo ili asije kutoa
ukelele ambao utamchanganya pale alipo, alivumilia
kisha akatulia,
""Nyamyena Nyamyena, kulumbila kulumba,
mwanenu kalumbilolo Chito, kumchamba mwangu,
kamililombile kulilima mpaka kujioni Nyamyena
Nyamyena kulumbila kulumba"".
Ni maneno yaliyomtoka mzee mambo sasa kwa
wakati huo, ghafla Mama sikitu anashangaa
kumuona mumewe akitoka shambani humo, alitaka
kupiga ukelele lakini alishindwa alikuwa sawa na
mtu ambae kawekewa gundi kali mdomoni na
hatimae anapatwa na usingizi mzito sana.
Alilala pale na hakutambua nini ambacho kiliendela
pale, muda mchache tu alizinduka kutoka usingizini
na kupata nguvu kubwa ambayo ilimfanya kukimbia
toka pale na kuelekea nyumbani kwao. Alikuwa na
hofu kubwa sana juu ya baba mkwe wake.
Aliwakuta wakimsubilia yeye ndipo aliposhtukia kofi
la maana toka kwa mumewe alipohitaji kuhoji
akatandikwa lingine na lingine hadi akadondoka
chini kwani alikuwa akipiga kwa hasira sana,
Hakumjali kabisa pale alipodondoka mama Sikitu
alimuacha huku akilopoka maneno ya ajabu sana.
Majira ya usiku wa manane mama sikitu anazinduka
toka usingizi wa nusu kifo kutokana na kipigo kikali
kutoka kwa mumewe lakini anashangaa kama
kabanwa na kitu kizito ambacho hakukifahamu, fikra
zake zilikuwa mbali kuwa mumewe kamkumbatia
wakiwa wawili kitandani, alishindwa kuwa na
maamuzi kwa kuwa raha aliyokuwa akiihisi ya joto
ilimfanya kuwa kama mtoto anayedeka.
Lakini ajabu anashangaa kuona kichwa chake
kinaburuzwa taratibu huku akianza kupata maumivu
taratibu. Wakati huo mvua ilianza kutia nanga toka
safari ya mbali na kuanza kuporomosha neema ya
mwenyezimungu, chini ya ardhi ya Shishimo na
kufanya mimea kufurahi kutokana na hiyo neema
inayoendelea kushuka kwa muda huo.
Mama sikitu akili yake bado ilikuwa inatafuta
mtandao ili iweze kuchambua data kuwa yuko
sehemu gani maana hata kichwa chake kilianza
kupigwa na matone ya mvua,
Wakati huo Mzee chito akiwa ndani anashtuka na
kukaa kitandani baada ya mvua kuanza kupenya
kwenye tundu za nyasi zilizoshoindikana kuzibwa
huko juu ya paa, alipapasa pembeni kama kawaida
yake kuwa atamkuta wa ubavu wake wa kushoto
lakini wapi. Alishuka toka kitandani na kwenda
kuangalia mlango kama umefunguliwa lakini alikuta
umefungwa. Alisimama kama sekunde kadhaa
ndipo akakumbuka kuwa usiku alimpiga mkewe na
hakumjali kabisa na muda wa kulala alikuja kulala
peke yake.
"mke wangu mke wangu" alianza kuweuka pale bila
hata kujua nini ambacho kilimfanya amfanye vile
mkewe na sasa anajilaumu kwa sana. Alifungua
mlango na kwenda nje mpaka pale alipomuachaga
mkewe lakini hakumkuta kabisa, mvua iliendelea
kulindima na radi za kutosha zilikuwa nyingi sana.
Alimpenda sana mkewe kuzidi neno nakupenda
aliangaika sana huku na kule ndipo akaanza kuita
kwa nguvu "Mama sikituuuuuu mama sikituuuu mke
wangu uko wapiii!".
Ile sauti ilisafiri kwa umbali fulani kwa kasi sana
hadi pale alipopatikana mama sikitu mwenyewe.
Mama sikitu aliipata sauti hiyo ndipo akaondoka
kwenye fikra zake na ndipo akajiuliza wakati hata
macho hajafumbua, kama huyu aliyembana hivi ni
mumewe je huyo anayeniita mke wangu ni nani pia
akili ilimjia muda ambao alipigwa na akaachwa pale
kama zigo la kuni, alifumbua macho kumbe
alibebwa na kitu hatari sana ndipo alipopiga ukelele
mkubwa sana uliompa taarifa bwana Chito kuwa
mkewe kapatwa na matatizo makubwa yanayohitaji
msaidizi.
Ndani ya kijiji cha KILIMALONDO, baada ya miezi
kadhaa kupita lyoto alikuwa na afya nzuri sana tena
sana na alikuwa kamili. Matatizo yake yote yalipona
alisikia vyema aliona vyema aliongea vyema kama
kawaida na sasa lyoto kawa binti mzuri sana wakati
huo akilelewa na kijana Katunje ambae yeye kama
mwanaume alijihisi hata kumtamani binti huyo,
lakini alishindwa baada ya kumchukulia kama ndugu
yake wa karibu hivyo baada ya kutambua kuwa
alibakwa hakutaka kumpa taarifa yeyote kuwa
alikuwa wapi kipindi cha nyuma.
Binti lyoto tatizo alilonalo ni moja tu kuwa alipoteza
kumbukumbu kuwa yeye ni nani na alikuwa wapi
alijihisi kama mtu ambae kazaliwa upya katika
ulimwengu wa Kilimalondo.
siku moja kijana katunje alimkalisha chini lyoto
akifikilia jambo la kumuambia. "Ndugu yangu lyoto,
siku moja ikifika mimi nikipotea machoni mwako
basi familia yangiu inapatikana kijiji cha Shishimo
kwamba utajitahidi kufika hapo na kupeleka taarifa
yeyote ambayo itanilazimu mimi kupoteana na
wewe kwa muda mrefu umenielewa". lyoto
alitabasamu na kumuuliza.
"sawa nimekuelewa lakini mbona hujawahi
kunionyesha mama yangu wala baba yangu na
wewe umeniambia kuwa kaka yangu sasa baba yetu
na mama yetu wako wapi na wanaitwa akina nani".
Swali hilo lilimchesha bongo kijana katunje na
alifikilia ili amjibu vyema "yani kiukweli dada yangu
baba na mama wanaishi mbali sana ila mimi
nikaamua niishi na wewe ila siku zishafika za
kuwajua wewe wazazi sawa, ila ngoja kwanza
niende kijijini nikatafute chakula alafu nitarejea".
Walikuwa wanaishi huko polini na hapakuwa na mtu
ambae anapafahamu zaidi ya wao kama wahusika.
Alifanya safari ya kwenda kijijini ambako watu
wengi huwa wanaishi huko.
Katunje lifanikiwa kufika kwenye nyumba ya mama
mwaija ambae alimuamini kuwa ni mmoja kati ya
watu ambao wanampa msaada wakati wote. lakini
alikuwa anajiuliza sana kwa nini moyo wake
umetokea kuridhika sana kumsaidia mtu ambae
hamfahamu kabisa lakini aliachana na hayo mambo.
baada ya kufika kwa mama huyo alimkuta akiwa
anaanda chakula, "mama mama upoo katunje hapa".
alijitambulisha ili aweze kujulikana mapema na
mama huyo asipate wasiwasi wowote.
"Mwanangu katunje haya ingia ndani haraka sana":
aliingia baada ya kuhakikisha kuwa hakuna mtu
ambae anamuona wakati huo, "katunje muda sasa
bado hujaniambia wapi ambapo unaishi kwa sasa
na wala hujawahio kuniambia maendeleo ya huyo
mgonjwa anaendeleaje". katunje alishusha pumzi
kwanza kisha akamueleza jambo fulani. "mama
kweli lakini haina budi kukuambia leo hii, mama
hali yangu bado kwa sasa mbaya sana itabidi leo
hii nikueleze wapi ambako ninaishi ili chochote
kitakachonitokea basi uweze kumsaidia binti yule
kumrudisha kwake, pia naomba iwe siri yako kabisa
kwa sasa niko pale karibu na makorongo, na binti
hali yake ni mzima kabisa tena utamshangaa sana"
Basi mama mwaija akafurahi sana ndipo
akamueleza kuwa Mzee Swai kwa sasa hawezi
kukufuatilia kwani anasumbuliwa na maradhi na
anapoonyesha kuwa anaenda ukingoni kabisa".
Kumbe wakati huo mzee Kauzibe alikuwa nje ya
nyumba hiyo akimfuatilia bwana Katunje, aliposikia
kauli ya kusema kuwa yule binti kafichwa kwenye
pori lililokaribu na makorongo basi aliondoka kwa
haraka sana ili kwenda kuhakikisha, aliondoka na
mitego yake ili ajulikane kuwa ni mzee mtegaji
kama kawaida yake, alipofika ndani ya msitu huo
basi alianza kutafuta lakini hakupata mafanikio
kabisa ndiopo akatafuta mahali na akaanza kutega
mitego yake ya wanyama. Baada ya kumaliza hapo
akaondoka akiwa na matumaini kuwa siku moja
atafanikiwa kumkamata binti huyo. Haikujulikana
kwa nini mzee huyo anafanya hivyo yani anamfuatilia
binti lyoto.
Upande wa kijiji cha bwawani mambo si mambo
sasa bada ya wazee wawili maarufu sana mapato
na sikujua kushirikiana kwenda mahali ambapo
wamemficha kijana susu, waliamua kumtoa kwa
sababu tayari vitisho vimeshatoka kwa mzee
Manuali kuwa yeyote ambae kahusika kumpoteza
kijana wake basi ajiandae kuipata cha mtema kuni
kwani hatoweza kumvumilia kamwe mtu yeyote.
Waliulizana sasa watamfanya nini kijana huyo na
endapo wakimuacha basi na wao watajulikana ndipo
wakaamua kumpiga na gongo la kichwa yani
upande wa kisogo ambako upo ubongo wa kutunza
kumbukumbu.
kitu hiko kilimfanya aanguke chini na azimie kabisa,
walimuinua na kwenda nae karibu na kijiji kwenye
nyumba moja ndipo wakambwaga nyuma ya
nyumba hiyo, waliondoka pale na wakaenda
kuungana na wengine ambao walikuwa kwwnye
kikao. Kwa bahati mbaya walishindwa kukumbuka
kuwa kule mahala ambako walifanya unyama ule
waliacha vitu ambavyo ni kama ushahidi tosha
kabisa endapo mtu ataamua kufuatilia.
Kila mtu sasa alikuwa tayari kumtafuta kijana huyo
na huku wengine wakisema kwamba itakuwa ni
mzee mambo sasa ndie alikuwa anayafanya haya ili
kulipisha malipo ya mwanae ambae alipotea kwa
muda sasa na ndipo kaamua kumpoteza kijana
huyo. kauli hiyo ilishikiliwa na sikujua kuwa itakuwa
kweli japo kijana ndunya na Mzee manuali walipinga
vikali sana kuwa haiwezekani kabisa mtu kama yule
afanye vile "nasemaje mtu aliyempoteza kijana
wangu yumo humuhumu kijijini sasa asipoonekana
leo hii atanitambua"
alimaliza hivyo na yeye akaondoka zake.
Kijijini shishimo mama sikitu anaonekana kulia
baada ya kukoswa kuuliwa na mnyama mkali
ambae alimbana, kumbe alikuwa chatu mkubwa
sana ambae alionekana kumvirigia huku akimburuta,
ndipo chito kwa ujasiri alimfuata lakini ajabu nyoka
hilo lilimuachia na kukimbia zake kusikojulikana
alimchukua mkewe na kuondoka nae kwenda ndani
lakini anamshangaa kumuona baba yake akiwa
uwanjani, wao waliingia ndani na kulala. kwa
upande wa mama sikitu hakuweza kabisa kulala
kwani kwa yale yaliyomtokea ni tosha kabisa kuwa
yuko hatarini.
Alimueleza mumewe kuwa pale hawako salama
"mume wangu nakuapiza kuwa hapa hatupo salama
kabisa ni bora hata kule ambako tumetoka lkakini si
hapa" kauli hiyo ilikuwa kero sana kwa bwana chito
kwani anampenda sana baba yake kuliko kitu
kingine..........
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO 15
Endelea....................
Katika eneo moja anaonekana kijana akiwa na Baba
yake wakiwa wanaongea, kijana huyo alikuwa
anamueleza mzazi huyo kiuwa anahitaji kupata
mwanamke wa kumuoa kabisa "baba ukweli siwezi
kukuongopea namtafuta mwanamke popote pale
alipo ambae ninaweza kumuoa laini siwezi
kumchukua mwanamke wa hapa nyumbani kama
wewe unavyohitaji".
Ndipo mzee huyo alivuta pumzi za kutosha kisha
akamshika mwanae bega na kumumbia jambo
"Sawa mwanangu ngoja nikuambie kitu kimoja,
fahamu kuwa ndani ya kijiji chetu hakuna mtu
a,mbae tunamtarajia kuwa atachukua kiti hiki cha
uongozi zaidi yako sasa lazima umchukue
mwanamke wa hapa kwetu lakini si kwingine zaidi"
Kijana huyo hakuweza kabisa kuelewa ndipo
alinyanyuka na kuondoka zake pale alipo.
Kijiji hiki kinajulikana kwa jina la CHAMLO ambacho
kinapatikana umbali mrefu kidogo na vijiji vya
KILIMALONDO. Kijna ambae alitarajiwa kuwa
kiongozi baada ya mzazi wake kuwa na hali mbaya
ya kiafya lakini hakuruhusiwa kuwa kupata nafasi ya
uongozi mpaka pale atakapokuwa na mwanamke
ambae atakuwa nae na kumsaidia katika kazi zake
za uongozi.
Alijulikana kwa jina la BAMUZI na baba yake ambae
ndie kiongozi wa kijiji cha CHAMLO, alijulikana kwa
jina la NGOLOLO, Ndipo kijiji kizima cha chamlo
kila mwanamke alipata taarifa ya kuwa mtoto wa
kiongozi Ngololo kuwa anatarajia kuwa na
mwanamke wa kumuoa ili aruhusiwe kuwa kiongozi.
Ndipo kila mwanamke ambae alijihisi kuwa ni mzuri
zaidi alianza kujipitisha sehemu ambayo
anapatikana kijana BAMUZI.
Majira ya mchana akiwa nyumbani kwake pamoja
na vijana wake wa karibu sama aliweza kuwaeleza
jambo moja muhimu sana ambalo linamfanya yeye
akatae kuoa mwanamke wa pale kijijini kwao.
"jamani mnafahamu kwa nini mimi sipendi kuwa na
mwanamke yeyote hapa kijijini na nahitaji kwenda
mbali ya kijiji hiki ili niweze kupata mwanamke
ambae ataniheshimu?"
Hawakuweza kumjibu zaidi ya kutikisa mabega
kuonyesha kuwa hawafahamu chochote kabisa juu
ya hilo na wanamshangaa kwa nini afanye hivyo,
"Kiongozi hata mimi nashangaa kwa nini mana
unamkataa mpaka msichana mzuri wa hapa kijijini
kwetu yule binti wa mzee KILIMBI nani yule
NAOMI".
Alianza kucheka kwanza Bamuzi kisha ndipo
akawaambia "mwanamke yeyote ambae utamuoa
akiwa anatoka ndani ya kijiji chako elewa kuwa huyo
mwanamke atakuwa msumbufu sana kwa sababu,
akili yake yote hatoweza kunisaidia zaidi ya
kujionyesha kaolewa na nani tu basi hiko ndiko
nisichokifahamu lakini pia katika ndoto zangu
sijawahi kumuota mwanamke wa hapa".
aliwashangaza sana wenzake ambao walianza kwa
kumcheka sana. Moja ya nyumba ndani ya kijiji hiko
cha Chamlo alionekana binti mzuri sana akiwa na
mama yake wakiongea huku akiwa anajisifia sana
"Mama hakika Bamuzi mtoto wa kiongozi wetu
mzee Ngololo hakika hana ujanja kabisa atanioa
mimi tu au unanionaje mama yangu" Basi alikuwa
anajigeuzageuza kama nyama choma au kuku
aliyebanikwa na kugeuzwa huku na kule.
"mwanangu hakika kwa uzuri uliuo nao Bamuzi
hawezi kwenda mbali lakini jitahidi kufanya haya
yafuatayo".
Binti huyo alishtuka kwanza "yapi hayo tena mama".
"Wewe kama mwanamke unabidi upendeze muda
wowote na alafu uwe na adabu zaidi ya wanawake
wengine pia ujifunze kuwasaidia kazi watu
ikiwezekana ukimuona mzee Ngololo heshima yako
iwe kubwa zaidi kwani yeye ndie atakayekufanyia
mpango mwanae akuoe kwani hapa kijijini hakuna
zaidi ya wewe NAOMI mwanagu".
Basi Naomi alijikweza kwa uzuri alionao kwa
kuamini kuwa mtoto wa Ngololo hatokwenda kokote
zaidi ya kwake, na alifikia hatua ya kuwatambia
wenzake ambao nao walikuwa wanawania nafasi ya
kuwa na kijana huyo.
Siku moja ilipofika wazee wapale kijijini Chamlo
walikaa kama faragha na bwana Ngololo kumueleza
jambo fulani.
Swala kubwa amablo waliweza kugusia swala la
mwanae amefikia wapi mpango wa yeye kuoa.
"Haya kiongozi wetu tupatie habari mwanao kaamua
nini kuhusu mwanamke?".
Walitulia wakisubiria jawabu nzuri kutoka kwa mzee
wa busara ambae huwa wanamtumia sana katika
kutatua matatizo ya pale kijijini.
"Nashukuru sana kwa kuniita na kuniuliza kwa
maswali kama hayo, kwanza mwanangu nimemlea
kwa mambo muhimu mengi sana ikiwemo na kutii
amri ya mzazi pamoja na mtu aliyempita umri, kwa
hiyo basi nimemuelza kanikubalia kuwa yuko tayari
kumvchagua binti ambaye atakuwa mchumba wake
na harakati za yeye kuwa kiongozi zitaanzia pale tu
baada ya ndoa kupita".
Walianza kufurahi kwa nguvu sana kwani jambo
ambalo walilitarajia kuwa litafanikiwa basi limetimia
vile watakavyo.
"Basi itatakiwa iandaliwe siku maalumu sana
ambayo itakuwa hatua nzuri ya yeye kuwaeleza
wanawake wote na watu wote wa kijiji cha Chamlo
kuwa fulani ndie atakaechaguliwa kuwa mchumba
wake". Mzee Ngololo alikubali na aliomba aitwe
kwanza Bamuzi ili athibitishe kama yuko tayari kwa
jambo hilo.
Bamuzi aliitwa na alifanikiwa kufika pale, alishangaa
kuwaona wazee muhimu sana na ambao atakuwa
nao endapo siku anakabidhiwa kuwa kiongozi rasmi
wao ndio ambao watamsaidia sana katika
kumuandalia mambo mengi na kumshauri zaidi.
Jambo ambalo alielezwa pale lilimstaajabisha sana
lakini alishindwa kukataa kutokana na heshima ya
wao wazee, alifikilia sana kisha akasema yuko
tayari na kamuandaa atamtaja siku hiyo,
"Sawa wazee nimewaelewa lakini nataka kesho
iandaliwe sherehe ambayo itakesha usiku mzima
alafu kuamkia asubuhi ndipo watu wote wakusanywe
na mimi nimchague huyo mwanamke".
Jambo aliloliongea hapakuwa na mtu ambae
alikaidi zaidi ya wao kukubaliana na hali ile kwani
sio baya kwao na upande wa kijiji kizima kwani
linaingiliana na furaha kubwa ambayo inakuja mbele
yao. Taarifa zilifika na kijana mmoja maarufu sana
katika utangazaji wa taarifa zozote zinazohitaji watu
wazisikie na kuzifanyia kazi.
""Lmgambooooo....lamgambooo....likilia
linajambo.. wanakijiji wooote wa CHAMLO
mnahitajika leo mjiandae kwa vinywaji na ngoma
kwa ajili ya kusherehekea kwa mtoto wa kiongozi
kukubali kumchagua binti mmoja ambae atamiuoa
ili na yeye akabidhiwe rasmi mikoba ya baba yake
Ngololo, kesho utakuwepo mkesha pamoja wote na
asubuhi mabinti wotee mjitokeze ili ajulikane nani
ambae atapata nafasi hiyo tafadhali ukipata taarifa
hii mtaarifu na mwenzio"
Wwatu walifurahi sana na wakaona kama bahati
imewaangukia wao, kwa upande wa binti NAOMI
hakuwa na tabu kabisa kwani alijitia imani kuwa
hakuna zaidi yake.
Majira hayo ya Asubuhi na map[ema ambapo
maandalizi yanafanyika, huku upande wa kijiji cha
KILIMALONDO mzee KAUZIBE kutokana na dhamira
yake ya kumteka binti LYOTO bado iliendelea ndipo
Lyoto alifanikiwa kumuonaakimnyemelea, alisimama
na kuanza kukimbia sehemu ambako hapafahamu
binti wa watu, Mzee Kauzibe alimsii sana asikimbie
kwani atamuua kwa mshale alionao kwa muda ule,
mzee hiuyo alizidi kumkimbiza lakini Lyoto
alikimbia zaidi yake kwa bahati mbaya sana
aliangukia kwenye korongo kubwa sana ambalo ni
ngumu kuona chini zaidi ya mingurumo ya maji
yaendayo kwa kasi kusikika yakisukumana.
Mzee Kauzibe alishtuka baada ya kuona kuwa tayari
kasababisha mauaji kwa binti wawatu, "jamani
wewe binti si ungesimama tu jamani, mpaka
unaangukia humo kwenye korongo, sikuwa na nia
mbaya na wewe ooooh! pole sana binti Lyoto
pumzika salama kabisa".
Alirudi kidogokidogo huku akishika mikono yake na
kuiweka kwenye kichwa chake huku akionyesha
kuwa ana wasiwasi na lile swala ambalo limetokea
kwa muda ule. Alikuwa anatetemeka mzee Kauzibe
. Ndani ya kijiji hiko cha kilimalondo, kijana
KATUNJE ana haha huku na kule baada ya kumkosa
Lyoto alirudi kijijini na kumpa tyaarifa mama Mwaija
na ndipo wakasaidiana kumtafuta ndani ya msitu ule
mkubwa.
Katika pitapita yao walifanikiwa kuona nyayo
ambazo zilikuwa tofauti, Katunje akachuchumaa na
kuzikagua kwa makini ndipo akasema "Mama huu
ni mguu walyoto ila huu ungine ni wa mtu mzima
kabisa lakini sijamfahamu" Ndipo mama mwaija
akainama na yeye kuziangalia kwa makini "Haaa ni
kweli sasa twende tuzifuatishe kwanza tujue mwisho
wake wapi, alafu tujue tunafanya nini".
Walizidi kuzifuatilia huku Katunje akiwa na hasira
sana baada ya kumkosa binti wa karibu sana,
hatimae mbio za sksfuni huishia ukingoni kwani
walifika mpaka pale kwenye korongo na
wakashuhudia kuna mikwaruzo ya miguu ambayo
ilionyesha dhahiri kuwa mtu kadondokea mule.
"Mama yangu binti wawatu katumbukia ndani humu
jamani laaaah!". Mama mwaija alimtuliza aondoe
kwanza zile fikra
"Hapana usiseme hivyo mwanangu, twende kwanza
nyumbani mana hapa sasa hivi tuko peke yetu
tukifika nyumbani tutajua nini cha kufanya." wakiwa
wanarejea Mama Mwaija akamuomba katunje
achume ganda la mgomba ambalo ni nene sana,
katunje alilileta baada ya kuligandua ganda hilo
kwenye mgomba uliokaribu na hapo. mama huyo
kwa ustadi usio wa kawaida akainama chini na
kuanza kufanya mambo yake ambayo hata katunje
yalimchanganya sana
"Unafanya nini mama" Aliuliza katunje.
"hapa mwanangu napima hii miguu naifananisha
kisha tunakaa nalo hili siku moja litatusaidia kumjua
huyu mtu aliyekuwa akimfukuza Lyoto" kwa wazo
hilo hata lyoto alilikubalibila wasiwasi, waliendelea
kutafuta njia ya kurudi pale ambapo walikuwa
wanakaa zamani, katunje alikusanya kila kitu kwa
kuwa hapakuwa na sababu yeyote ambayo
ingemfanya aendelee kuishi pale ndipo wakawa
wanarudi kijijini.
kabla hawajarudi walifanikiwa kuiona mitego kadhaa
"Mama hii mitego ya ndege na mnyama
naifananisha zamani sana baba yangu alikuwa
akiitega alafu ni mizuri sana yani". Alitaka kuitoa ile
mitego ;lakini mama Mwaija akagoma kwanza "
hapana mwanangu usiitoe kwa sababu aliyetega
hapo aliwaona nyinyi mnaishi karibu sasa tuiache
alafu siku ya kesho njoo ujifiche uangalie nani
ambae anakuja kuangalia mitego hii labda anaweza
kujua nani ambae kamkimbiza lyoto mpaka
kuangukia mule korongoni". Katunje aliondoka na
mama huyo wakiwa na huzuni kubwa, kijiji kizima
taarifa ilimfikia na kwa upande wa mzee Swai
alihuzunika kiasi kwani lengo lake halikutimia.
Ilitimu majira ya saa nane za ,chana maji yenye
nguvu za ajabu sana yalisukuma mizigo yote
ambayo iliingia humo bila kujai kama kuna
binaadamu ambae yupo mule ndani. Mungu
hamtupi mja wake lyoto alikuwemo mule ndani ya
maji akiwa hana habari yeyote baada ya kuzimia
kutokana na ile hali iliyomkuta, maji yalishirikiana
kumsukuma lyoto umbali mrefu sana ambao
hauwezi kutabirika ila ilikuwa nje kabisa ya kijiji cha
Kilimalondo.
Upande wa kijiji cha Chamlo watu walikuwa na
hamsha hamsha za hapa na pale ili wafanikishe
swala lile la sherehe ambayo ni muhimu sana
kwao.
Wanawake walianza kwenda kuchukua maji mtoni
na wengine walichukua nyavu ili kuvua samaki mtoni
hapo ili wapate kuchemsha wale pamoja na pombe
ambazo wanaziandaa "Hakika naamini NAOMI ndie
atakae chaguliwa kuwa mke wa Bamuzi lakini sisi
wengine hatuna uzuri zaidi yake"
Binti mmoja ambae alikuwa akimueleza mwenzake
huku wakielekea kuchukua maji, "wewe mbona
unakata tamaa hivyo wewe pia mzuri ndugu cha
kufanya hapa wakati wa mkesha basi tujikweze kwa
Bamuzi na atatukubali baada ya kumfanya
atukubalie kimapenzi sisi najua kesho tukivalishwa
na kuandalia vyema atatukubali". walishauliana kwa
kila jambo ili nafasi hiyo waipate.
Majira ya jioni kijana Bamuzi alimuita mmoja wa
kijana ambae yupo nae karibu sana na kumuambia
jambo "sasa mambo ndio kama hayo, nakuomba
ufanye jambo moja usiku ukifika mtafute NAOMI na
umchunguze kila afanyalo alafu uje uniambie mana
baada ya huyo hakuna mwingine naweza
kumchagua". Kijana huyo alimsikiliza kwa makini na
kumuahidi kuwa atalifanya kwa ukamilifu sana hilo
jambo.
Mama NAOMI alionekana kumsii sana mwanae
huko aendako asidiriki kabisa kunywa pombe na
alafu asikeshe arudi mapema sana ili aweze
kumuandaa. Wakati huohuo Nomi akielekea kwa
rafiki zake njiani alikutana na kijana mmoja ambae
alimsimamisha na kuongea nae mawili matatu.
"NAOMI samahani sana naomba unipe jibu langu
kwani nakupenda sana". Kijana huyo ambae
alijikakamua kuongea mbele ya mrembo wa kijiji.
"Kha! weee mbona king`ang`anizi kama kupe
kwenye mfugo, nimekuambia huna hadhi ya kuwa na
mimi najiandaa hapa nataka kuwa mke halali wa
BAMUZI sasa naomba usiniharibie".
Baada ya kuongea hayo alinyoosha na njia kuondoka
pale. Kijana huyo alibaki kuduwaa pale alipo ndipo
muda mchache walifika wenzake na kumuuliza nini
kimetokea, walimcheka sana kwani walimuambia
kuwa Naomi ni mtu tofauti sana hawezi kuwa nae
yule ndie mrembo wa kijiji hivyo ni ngumu sana
kumkubalia yeye ni bora amuache aolewe na
Bamuzi. "lakini kama kweli unampenda ngoja leo
tumfanyie mchezo usiku na sisi tumharibie " Vijana
hao walipanga njama za kumharibia NAOMI ili
asipate nafasi ya kuwa na Banuzi na zaidi yake awe
huyu kijana aliyemkataa.
Majira ya usiku yamefika tayari Mzee NGOLOLO
akiwa na washauri pamoja na BAMUZI walikuwa
mahala husika ambako wameandaliwa kwa ajili yao,
huku watu waklianza kupiga ngoma na kuanza
kunywa pombe za kutosha. Wakisubilia asubuhi
nani atatajwa, kijana ambae alipewa kazi na bwana
Banuzi alijitahidi sana kumtafuta NAOMI mpaka
akafanikiwa kumuona na akaanza kumchunguza.
Wale vijnana ambao waliahidi kumharibia Naomi
walifika na kuwa karibu sana na Naomi. "Sasa
itabidi hii pombe utie ile dawa alafu ukampatie
Naomi". Ndipo wakafanya hivyo na mmoja wa
kijana akaenda kwa Naomi na kumuambia "Naomi
tafadhali ebu pokea kinywaji hiki kutoka kwa mtoto
wa Ngololo kijana Bamuzi kakutunuku kuwa mmoja
wa watakaotajwa hapo kesho". NAOMI alishindwa
kuamini kama kweli, alichukua na akakinywa chote
bila kufahamu kuwa ulikuwa ni mtego tu. Kukataa
alishindwa kwani jina la Banuzi ni kubwa sana pale
kijijini na watu hawajawahi kulitumia vibaya jina hilo,
ila hao vijana kwa kuwa walidhamilia kufanya hivyo
walifanikiwa.
Ngoma zilianza ndipo yule kijana ambae alikuwa
anampenda sana Naomi alienda na kumshika
mkono na kuanza kucheza nae wakati huo NAOMI
hajielewi kutokana na kinywaji kilichochanganywa na
dawa za usingizi.
"nasikia usingizi nipeleke nyumbani" sauti za kilevi
na uchovu alizozitoa NAOMI zilidhihilisha kuwa
dawa inafanya kazi, na kijana huyo hakufanya
makosa ndipo akamshika vyema na kumpitisha
karibu na wale wazee na alipo BAMUZI, kijana
aliyepewa kazi ya kumchunguza alifanikiwa kuona
yote japo Bamuzi hakushuhudia zaidi. Safari hii
ilifika hadi kwenye moja ya fumutu ambalo lipo
mbali kidogo na pale kwenye shsrehe yao.
Kijana alifanikiwa kufanya machafu aliyoyakusudia
kwa kumuingilia kimwili mpaka alipotosheka na
akamuacha palepale alipo huku akiwa hoi NAOMI.
Baada ya hapo walishauliana kuwa wampeleke kwa
mama yake, safari ilianza na kumfikisha hadi kwa
mzazi wake na kumuambia kuwa kichwa
kinamuuma ndipo alijisikia kizunguzungu na wao
wakamsaidia kumleta pale, alimuingiza ndani na
kulala mama akiwa hana hili wala lile juu ya
mwanae.
Asubuhi na mapema sanawatu wakiwa wanajiandaa
ndipo Mzee mmoja ambae alijiimia kwenye mitego
yake aliyoiweka kwenye maji ili apate kunasa
samaki wakubwa sana. alifika na kuanza kuvuta
kamba ya mtego ule aina ya dema lakini ajabu
dema linatoka lakini anaushuhudia mkono wa mtu
ukizama tena ndani.
Ilimfanya aogope na kushangaa na kwa kuwa ni
mzoefu sana aliamua kuingia ndani ya maji hayo na
hatimae anamtoa binti Mzuri sana mpaka mzee
akashangaa kwa nini awe mule ndani na anatokea
wapi ni maswali ya haraka haraka ambayo alipata
kujiuliza kwanza.
Alimtoa nje na kumsukuma tumbo kwa
kumminyaminya ili ayatoe majia mabayo kayanywa,
yalitoka mengi sana lakini hakuzinduka, ilibidi
afanye jitihada za hali ya juu kumfikisha nyumbani
kwake na wakati huo watu wote wapo kwa mzee
Ngololo ili kushuhudia tukio hilo la kumcgagua
mchumba wa Bamuzi.
Huduma zote za kiafya zinatolewa chini ya amri ya
Banuzi ndipo alikimbia sana na kumfuata mmoja wa
kijana na kumueleza ana shida ya kuonana na
Bamuzi, hakika aliitwa na yeye akaitika wito kufika
pale.
"Vipi kijana tayari umeshamuona ni mwanamke
gani?" aliuliza mzee huyo
"Daah hapana kwani yule niliyemtarajia jana kafanya
vitu vya ajabu sana, kwa hiyo itabidi niifuate ndoto
yangu ilikonielekeza niende". "kijana banuzi nina
shida nyumbani kwangu naomba tuongozane
ukaone shida yangiu haraka sana". "sasa muda
unafika sasa hivi wa kuchagua" "ndio najua ila mimi
nina shida na wewe kama unakuja kuwa kiongozi
wetu basi njoo unisaidie".
Walionekana kukimbia kuelekea kwa bwana huyo.
Shughuli ilianza kuwa na hofu baada ya kutoonekana
kwa kijana Bamuzi na wanawake wamejipanga kwa
kweli kumsubilia yeye. Wakiwa kwa mzee huyo
ndipo Bamuzi anamshuhudia binti mrembo ambae
hakuwahi kumuona ndani ya kijiji kile.
Ndni ya kijiji cha SHISHIMO sasa mambo hayakuwa
vizuli baada ya ugomvi mkubwa sana kuzuka baina
ya Mama SIKITU na Baba SIKITU juu ya kile
kinachomfanya mama sikitu kumtuhumu mkwewe
kuwa ni mshirikina na baba sikitu kukataa katakata.
"nakuambia ukweli baba yako mwanga yani
mchawi" maneno hayo yalimfanya baba sikitu
ambae ni mzee Chito kukasirika sana "hapana
naona sasa umemchoka baba yangu hawezi kuwa
mchawi baba yangu aliyenilea kwa muda mrefu
sana".
"Najua huwezi kuniamini kabisa ila unakumbuka ile
siku ambayo ulikwenda shambani nini kilikutokea
unataka kuniambia wewe shamba la baba yako
hulijui wapi unaingilia na wapi unatokea?'" Mama
sikitu aliuliza swali na wakati huo wakiwa mbali na
nyumbani kwao.
"Mh! kidogo inaleta utata kwani ukweli ile siku
nilishindwa kuamini" Alithibitisha bwana Chito
kuonyesha kuwa kweli siku hiyo haikuwa nzuri sana.
"Kingine unaweza kuniambia maneno haya
aliyokuwa akiongea baba yako kule shambani siku
ile?" Chito alishangaa "Maneno gani hayo tena
aliongea" Mama sikitu alianza kuigizia yale maneno
kwani aliyakariri vyema sana
"""Nyamnyena Nyamyena, kulumbila kulumba.
Mwanenu kulumbilolo Chito, kumchamba mwangu,
kamililombile kulilima mpaka kujioni Nyamnyena
Nyamnyena kulumbila kulumba......hayo ndio
maneno ambayo alikuwa anayataja je unaweza
kuniambia alikuwa ana maanisha nini"
Ndipo chito alishika kichwa chake huku akiwa
haamini kabisa. Mama sikitu aliendelea kumuambia
kuwa yeye yuko tayari kukimbia pale na kurudi Kjiji
ch BWAWANI lakini si kuendelea kukaa na mtu
mchawi kama yule.
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA 16
Endelea.................
Baada ya maneno hayo na mkewe bwana Chito
alionekana kuwa na mshangao mkubwa sana ambao
hata mkewe nae alijikuta akimuangaklia kwa
umakini sana na kutaka kujua kipi ambacho
kinamfanya ashangae kwa vile. "Vipi unaniangalia tu
wewe si unamtetea baba yako yani hata
haukumbuki mwanzo tumefukuzwa kwa ajili gani
yani sasa kama hauamini fanya uchunguzi
utanielewa".
"Mke wangu sawa lakini kumbuka kuwa yule ni
baba yangu pia usijalibu kutamka maneno hayo
asije akasikia alafu akatuachia laana hapa". Chito
alijaribu kumtetea baba yake ambae alionekana
kuwa na imani chafu ya kishirikina "Unaogopa laana
basi nikuambie hakuna laana yeyote ambayo
itatufika kutoka kwa mtu mchafu kama yule
namheshimu lakini mkwe wangu ni mchawi".
Walianza safari ya kurudi nyumbani lakini akili ya
mama SIKITU yeye ni kuondoka pale na atajua
mbele ya safari wapi ataelekea, wazo hilo lilipingwa
sana na chito kwani hakutaka kuamini kweli baba
yake anayo hayo mambo ambayo mkewe anamhisi.
Walimkuta mzee Mambo sasa akiwa peke yake na
huku uso wake ukiwa umefura kwa hasira. Ghafla
aliaga na kuwaomba yeye anaondoka mara moja
kwenda kwa rafiki yake.
"Sasa baba vipi unaelekea wapi wakati usubiri
mkweo hapa anataka kupika ugali" Japo na maneno
hayo mzee huyo hakutaka kusikia aliondoka na
mkongojo wake na kupotea machoni mwao. "Si
unaona niliyokuambia yale "
"Eeee weee mwanamke unataka kunikorofisha mimi
na baba yangu ebu achana na habari hizo kabisa
nisisikie".
Mzee huyo safari yake ilifika hadi kwenye nyumba
moja hivi ambapo aliingia moja kwa moja kabisa
"Eeeh bwana NYANDU afadhali nimekukuta"
Mzee ambae alimtaja kwa jina la nyandu
alimkaribisha ndani na wakaanza faragha ya
maongezi yao,
"Haya niambie kipi kimejili" Nyandu aliuliza.
"Bwana Nyandu sijajua nini nifanye kiukweli, kuhusu
pale nyumbani"
"Nini tena ebu niambie kwanza mana hata hivyo
kuna kazi yako hukuimaliza kabisa" Nyandu
alimueleza Mambo Sasa
"Unajua kipindi kile cha nyuma zamu ya kutoa kafara
ilikuwa kwangu sasa mtu mweneyewe mhusika ni
kutakla mkwe wangu mtoto atakayemzaa basi ndio
nimtoe kama nilivyoahidi"
"Haswaaaa na ndivyo wengi tunavyojua"
"Sasa, walivyokimbia mwanangu na mkwe wangu
kutoka pale nyumbani basi kumbe walikoishi
walishazaa mtoto wa kike na wakampa jina la sikitu
sasa wamerudi pale nyumbani ila nahisi kama yule
mwanamke kakomaa mana ananishtukia sana kwa
mambo yangu mengi ninayoyafanya"
Maongezi hayo yalikuwa ya siri sana ambayo
yaliongelewa chumbani kwa bwana Nyandu ambae
ni mshirika mwenzake.
"Ngoja tutapiga ramli sasa hivi na tutajua kama
kweli yupo hai au kafa na kama yuko hai hakuna
kitu kitakachoshindikana kabisa atarudi yeye
mwenyewe hadi hapa na wewe utafanikiwa kutoa
kafara yako"
Mzee Mambo Sasa alionekana kufurahi sana " Haya
twende kwanza fanya hayo mambo"
Ndipo Nyandu alitoka pale kitandani na kuchukua
furushi kubwa la mambo yake, akachukua kaniki
nyeusi mbili moja akampatia Mambo sasa na
nyingine akawa nayo yeye na ndipo walipovaa
lubega kama wamasai,
Waliufukiza udi fulani hivi ambao ulianza kuenea
taratibu mule ndani na akaanza kuongelea maneno
kwenye moja ya kibuyu, baada ya hapo akapandisha
mashetani ambayo yalisaidiwa na nyimbo maalufu
sana kwao
"Nyandu, nyandu nyandu leloooo, kulilolangula
kumwana sikitu, kulilolangula kumwana sikitu,
kulilohangaika kokote kuliliona sikitu, Nyamnyenaaa
Nyamnyenaaaa"
Baada ya kuongea maneno hayo ndipo akanyamaza
kwa muda kisha akapaza sauti kama kumuuliza
Mzee mambo sasa na akitoka kwenye ulimwengu
wa kibinaadamu na kuingia ulimwengu wa kishetani
kimaongezi baina ya Nyandu na Mambo sasa.
"Mambo sasa sema najua una shida sana"
"Nyamnyena nyamnyena kweli kabisa nina shida
nataka kujua mtoto wangu chito na mkewe kweli
walizaa mtoto wa kike?"
Alimuuliza huyo jini au shetani lenye jina la
NYAMNYENA, ndipo alipoanza kumcheka sana mara
kadhaa kisha akamjibu "Ndio walizaa na pia mtoto
wao alibakwa na mmoja wa kijiji hiko lakini
akapona baada ya kumtupa polini, lakini kasaidiwa
na mtu wa karibu yako sana":
Alishtuka sana kasaidiwa na mtu wa karibu yangu
kivipi na yupi huyo mtu wangu wa karibu ambae
alimsaidia huyo sikitu
"Mtu wangu wa karibu gani huyo Nyamnyena ambae
alimsaidia na anaendeleaje?" alianza kucheka tena.
"Siwezi kukutajia huyo mtu fahamu kuwa bado yuko
mzima na yuko mbali sana na nyinyi kwa sasa
sifahamu wapi kafikia lakini ni mzima haya kwa heri
mana tumevuka milima na mabonde mpaka kufika
hapa tunataka kurudi kwetu"
palepale yalimtoka yale mashetani na Mzee Nyandu
akarudi kwenye hali yake na kumuuliza nini
aliambiwa na shetani wao. Alimhadithia kila jambo,
mipango ilipangwa ili binti Sikitu afanyiwe mpango
afuatwe. Kwa wakati huo sasa mzee Mambo sasa
alirejea nyumbani na kuwakuta wakila ugali ndipo
akaungana na kuanza soga za hapa na pale.
"Mwanangu chito unajua kama mtoto wenu bado ni
mzima"
"mzima baba mbona unataka kutukumbusha
mambo tuliyoyasahau mpaka sasa"
"aminini hilo kuwa bado ni mzima mana nilikuwa
sina amani kumkumbuka mjukuu wangu mana sina
mjukuu kabisa nataka nifanye jitihada ya kumrudisha
nina mganga wangu ambae aliniambia kuwa
anaweza kumrejesha alipo"
Kauli hiyo iliwafanya wawe na shauku kubwa sana
ya kutaka kujua lini watafanya jitihada za
kumrejesha Mtoto wao.
Ndani ya kijiji cha CHAMLO wakati kijana BAMUZI
akiendelea kumuangalia binti yule kutokana na uzuri
wake kule wazee ambao walikuwa wanamsubiri
waliamua kutumwa na kuja hadi kwenye nyumba ya
huyu mzee ambako ilisemekana kuwa Bamuzi
kaenda. Kweli walifanya hivyo na wakamkuta "Sasa
mzee hakikisha kabla ya yote apone huyu na hali
yake iwe nzuri sana kisha unipe taarifa pia asijue
mtu yeyote kuwa uko na nani humu ndani"
Mzee huyo alimuitikia na Bamuzi akatoka nje
akakutana na wazee waliotumwa kuja kwake,
aliongozana nao na kufika kule akisubiriwa achague
nani ambae atamfaa.
Akili ya Bamuzi ilihama kabisa na ikawa imefififa
kwa NAOMI ambae alishaonekana mtu mchafu na
kuzama zaidi kwa mgeni huyo ambaye hakufahamu
katokea wapi na alionekana kumpenda sana.
alijiuliza maswali kuwa ama ile ndoto yake
iliyomuambia kuwa atasafiri kumtafuta ampendae
na hatimae ndio yeye kafika mweneyewe?.
Mtangazaji alisimama na kuanza kunadi kwa
kutumia maneno mazuri sana ambayo kila mmoja
yalimkosha lakini kwa kijana Banuzi haikuwa hivyo
kabisa akili yake ilibaki kwa yule mgeni tu. Baba
yake alimshangaa sana kuona mwanae kabadilika
ghafla alimsogelea na akamhoji "Mwanagu vipi
mbona uko na hali hiyo kipi kimekukuta huko
ulikotokea".
Bamuzi alikohoa kidogo kisha akasema
"Baba hapa siwezi kuchagua mwanamke kwa sasa
hivi kwani kichwa kinaniuma sana hapa nahisi
kuumwa" baba yake akamshika kichwa kisha
akatikisa kichwa kuashiria kweli ana homa kali.
"Sawa mwanagu sasa ngoja tunyamazishe shughuli
hii na ili wewe hali yako ikiwa nzuri basi tutawaita
na utachagua". Aliitikia na mzee huyo akaomba
nafasi ya kuongea, "Jamani hapa tunamkaribisha
kiongozi wetu mzee Ngololo ili aseme kitu "
Watu walifurahi sana kisha mzee huyo akasimama
na kuwaomba kwanza wale mabinti wasimame
kwanza kwa pamoja, waliposimama ndipo
akawasifia sana kwa uzuri wao.
"jamani wanawake wote hawa ni wazuri sana kwani
leo hii wamejipamba sana lakini mwanangu
kashindwa kumchagua yeyote kwani wote kawaona
wazuri sasa tunasubili kesho mtatangaziwa lini
afanye uchunguzi mzuri zaidi na sasa hali yake ni
mbaya kidogo hivyo tunaomba mutawanyike"
Iliwashangaza sana kauli hiyo lakini haikuwa na
shida kwani aliyesema ni mtu mubwa pale kijijini.
Baada ya siku tatu Bamuzi anaonekana kufuatilia
sana kwenye ile nyumba ya mzee kujua hali ya yule
dada. Mzee huyo ambae alimuokota binti huyo
alijulikana kwa jina la MWALAMI alikuwa anaishi na
kijana mmoja hivi wa makamo.
Siku moja kijana huyo alimshuhudia binti huyo
akitoka ndani humo na kukaa juani kwa kuwa
ilikuwa ni asubuhi sana alimfuata babu yake na
kumuuliza "babu hivi huyu mwanamke mzuri ni
nani".
Babu mwalami kwa hekima zake alijua kuwa kijana
kamtamani binti huyo sasa itambidi atumie kauli
nzuri kutengeneza heshima kwa Bamuzi. " kijana
wangu huyu ni binti wa mbali huko aliletwa na
mumewe kwa ajili ya matibabu na hivi karibuni
ataondoka kwani watakuja kumchukua".
Kijana hakuwa na neno, lakini taarifa ilianza
kusambaa kuwa kuna binti mzuri sana yupo pale
kijijini. Nyumbani kwa Mama Naomi na Naomi
mwenyewe, walikuwa na mazungumzo ya hapa na
pale "Mama mbona kama nimepoteza usichana
wangu mama". Alimueleza mama yake jambo hilo
baada ya kujigundua tofauti.
"Unasemaje wewe umepoteza usichana wako kivipi
tena"
"Mama hata sijui ila nahisi ndio hivyo". Mama yake
aliumia sana baada ya kusikia jambo hilo akawa
anamsema sana kwa nini alimuambia asijalibu
kukubali kunywa kinywaji chochote kile ili asije
kukutwa na hali kama hiyo lakini Naomi hakusikia
kabisa.
Baada ya muda kupita ndipo alipomuambia kuwa
asije kusema chochote na iwe siri yao wao wawili
na ikiwezekana basi huyo kijana aliyemharibia
usichana wake basi amuite siku moja ili aweze
kumkanya kwa tabia yake hiyo mbaya. Naomi
aliondoka na kuanza kumtafuta kijana huyo ambae
mwanzo alikuwa anamtamkia kuwa anampenda
lakini Naomi kutokana na kujiona kuwa yeye ni
mzuri sana basi alikataa na kumtolea maneno ya
kumkashifu kwa kufikilia kuwa ndoto yake ya
kuolewa na Bamuzi itatimia.
Moja ya mahali ambapo vijana wengi wa hapo
hutulia baada ya kufanya kazi nyingi na kuchoka
huja kupumzika hapo na kuanza kupiga stori za
hapa na pale. "Jamani hivi Bamuzi anaoa lini maana
ile siku sijaamini kama alikosa mwanamke wa
kumchagua kwa jinsi walivyopendeza vile?" mmoja
wa kijana alikuwa anauliza kwa kile ambacho anadai
kuwa kilimchanganya kwa nini Mtoto wa kiongozi
mkubwa sana pale CHAMLO kushindwa kuchagua
jiko lake la kujidai nae nyumbani kwake, "Aaa hata
mimi tena huwezi kuamini mpaka mrembo wa kijiji
kizima hiki NAOMI hakumchagua kabisa yani".
Ndipo kijana anayejulikana kwa jina la KIPEPE
aliinuka pale alipoketi na kuwaambia kuwa "Nyinyi
habari ya kumtaja Naomi sitaki kabisa Naomi ni
mchumba wangu mimi na Bamuzi akamchague
mwingine huko".
Wakati wanaendelea kumcheka basi alitokea Naomi
na akawafanya wote wakae kimya kabisa
"Kipepe nakuomba njoo mara moja" kauli ile
ilimfanya kipepe kushtuka na kujiuliza nini kitatokea
lakini wenzake wakimzomea kwa ile hali aliyokuwa
akiongea basi Naomi kasikia na anahitajika
kusemea uhakika wa yale.
"Kipepe kwa nini ulinifanyia vile?" Naomi aliuliza
"kukufanyia nini tena mchumba wangu eti"
"Unajifanya hujui yani umeniharibia usichana wangu
juzi kwenye ngoma baada ya kunipa pombe yenye
dawa ya usingizi kweli"
Kipepe alikuna kichwa kutafuta nini amjibu "Kwa
sababu nakupenda sana siwezi kukubali uolewe na
Bamuzi wakati mimi ndio wa kwanza
kukuhangaikia" "Sawa ila ni mapenzi gani ya
kuniharibia usichana wangu hunipendi kabisa sasa
hapa naenda kwa Mzee Ngololo naenda kumuambia
kuwa umenilazimisha ".
Kipepe kilianza kumshuka kwanza lakini kwa kuwa
ni kijana wa kiume alikomaa kwanza "Poa nenda ila
mimi mambo yangu nimepata na niko kwenye hatua
ya kutangaza kijiji kizima na najua urembo wako
utakuwa umeishia hapohapo na sijui kama utalinga
tena ".
"Sawa jigambe ila niko tayari kuaibika lakini wewe
lazima ukione cha mtema kuni". Naomi aliondoka
akiwa na huzuni kubwa sana. Kijana kipepe alienda
kuwaeleza rafiki zake kisha akawaomba nini afanye.
"Yani kaka hilo swala likifika kwa Bamuzi
umekwisha si unamjua alivyo yule jamaa yani
hacheleweshi kabisa nakuambia kama unakumbuka
yule KIBO alichofanywa baada ya kumbaka yule
mwanamke nani huyuuu.....NAMIO aaah! nilimuonea
huruma sana kwa hiyo wewe sasa hivi nenda
mtafute kabla hajaenda kusema usije ukafa".
Baada ya siku ya pili watu wakisubilia sasa mambo
yawe hadharani Bamuzi anaonekana na Mzee
Mwalami wakiongea mawili matatu.
"Bwana Mwalami nimekuambia jaribu kumdadisi
anaitwa nani anatokea wapi na nini kilimtokea".
Alisema Bamuzi
"Nilishamuuliza anaitwa LYOTO, lakini sehemu
anayotokea na kilichomkuta hafahamu kabisa ila
anajua kuna mahali ambapo alikuwapo mwanzo
kabla na anayemkumbuka ni mmoja tu anaitwa
KATUNJE basi, ila vingine hajui kabisa"
"umesema anaitwa nani?" alihoji kwa kuwa
hakulikamata vyema lile jina
"Anaitwa LYOTO pia ili iwe rahisi kumpa jina basi
tumuite LYOTO KATUNJE" Bamuzi alifurahi sana
kwa hilo jina ndipo akaweka vyakula pale kwa ajili
ya huyo LYOTO ambae kutoka KILIMALONDO
kusafirishwa na maji hadi kijiji cha CHAMLO. hakika
MWENYEZI MUNGU NI MKUBWA SANA.
Siku imefika na mapambo yaliendelea kutanda kila
aina kwa mabinti wazuri sana wenye kupendeza
akiwemo NAOMI ambae alikubaliana tayari na
Kipepe kuwa watatunziana siri nzito hiyo.
Mtangazaji wa habari za pale kijijini aliifanya kazi
yake kwa umahiri mkubwa sana kiasi watu
walipenda. wanawake walijaana wanaume pia na
vijana rika za akina Kipepe walikuwa wengi sana
kushuhudia mtoto wa kiongozi akichagua
mwanamke ambae atamfanya achukue kiti cha baba
yake amsaidie majukumu.
"sasa naomba kumkaribisha BAMUZI aweze
kuwatembelea kuwaangalia na atujuze kwa
kumshika mkono ampendae aje nae mbele yake"
Makofi yalikuwa mengi sana. Nyumbani kwa Mzee
Mwalami basi alimchukua LYOTO na kwa kuwa
hakuwa na nguo nzuri alikuja nae hivyohivyo kama
kushuhudia tukio zima la kijana Bamuzi.
Bamuzi alifika pale na kuangalia nje ya uwanja kwa
watu ili amuone Lyoto lakini hakufanikiwa, watu
wakawa wanamshangaa sana kwa nini sasa
asichague na anawapita huku akiwaangalia wasio
wahusika jamani. Ukimya ulitanda sana huku
wakisubili.
upande wa NAOMI alikuwa hoi kwani hakuamini
kama klweli anampita tu bila hata kumshika mkono,
mpaka dakika kadhaa Bamuzi anakata tamaa na
akawa anamuendea Naomi ili amshike rasmi huku
akijiuliza kwa nini huyu mzee Manuali anamfanyia
mambo tofauti na walivyoelezana.
Anapeleka mkono kwa Naomi na Naomi moyo wake
unafurahi akiusindikiza ili aushike haraka, ndipo
mzee Mwalami akasema "Bamuziiiiiiiii usifanye
makosa" Baada ya neno hilo ndipo watu
wakatazama kule ilikotokea sauti
"LYOTO KATUNJEEEEE.....".alitamka neno hilo
ndipo binti Lyoto akaitikia Bamuzi aliurejesha
mkono kutoka kwa Naomi na akamkimbilia Lyoto
na kumshika mkono.
"Jamani huyu ndie mke ambae nilikuwa namuwaza
kila siku atakuja kutokea" makofi hayakupigwa kwa
kuwa walimuangalia mgeni huyo aliyewakosha kwa
umbo dogo lililopendeza tena bado anaonekana
kuwa mbichi kabisa. Watu waliruhusiwa baada ya
kupata maelezo kamili kuhusiana na mwanamke
yule.
Siku iliyofuata Bamuzi,Lyoto na wazee akiwemo
baba yake walienda kuwakogesha dawa za ulinzi na
kuwakinga na maadui wowote ambao watajaribu
kuutumia uchawi wa aina yeyote washindwe kwani
Bamuzi anakuwa kiongozi akishikilia kiti cha baba
yake.
Ndani ya kijiji cha BWAWANI siku hiyo walionekana
kukutana ili kuelezana jambo fulani, Ajabu kubwa ni
juu ya kuonekana kwa SUSU akiwa kwenye hali
mbaya sana na haijulikani nani ambae kayafanya
hayo. Mzee Manuali alisimamia kesi hiyo huku
akiwataka wajitokeze wao ambao wamefanya ujinga
huo, pia ikishindikana basi yeye atamsubulia apone
na akija kuwataja basi watamtambua. Bwana
Mapato alimshauli ndugu yake kuwa sasa muda wa
mapambano umefika kwani wajiandae kwa lolote na
chochote,
Hadi hapo wamemuuzia kesi Mzee Mambo sasa
lakini walichokosea baada ya kumuonyesha susu.
"Mapato tuachane na hayo ya Manuali sasa unajua
kuwa kule bwawani kuna jambo ulilifanya vipi na
ulitegemea kuwa sadaka hiyo itamuhusu bwana
Mambo sasa vipii sasa." Sikujua aliuliza
"kweli lakini ndio hivyo hayupo ila nahisi kama ile
mizimu ya bwawani imeshakufa maana
haijanilazimisha chochote mpaka sasa nafikilia
kwenda kwa mtaalamu mpya ambaye atanisaidia
kwa hilo". Majira ya usiku wa manane Mzee mapato
akiwa kalala na mkewe basi upepo ulivuma na sauti
za ajabu zikiendelea kutoka na wanyama
wakiendelea kulia huko polini.
Mapato alishangaa sana ndipo sauti ambayo ilikuwa
ikijirudia rudia ikimpa taarifa ambayo ilimuogopesha
"Mapatoo...kazi yetu hujaifanya...tunahitaji damu na
kwa nini unatukabidhi ya mzeee sana klijana
unatiutania?" Mapato alishindwa kuamini kwa zile
kauli ambazo alikuwa akizipata "Sasa tutahitaji na
mtoto wake Mambo sasa ndipo damu itimie na
wewe utaifanya shughuli hiyo ya kuwaleta bwawaani
muda wa siku tano".
Mapato kashtuka sana na hakuamini kama atakuja
kupata shughuli kama hiyo. Asubuhi na mapema
anaenda kwa sikuja na kumuambia kuwa "Bwana
weee mambo magumu".
"Magumu kivipi tena" "Sikujua jana usiku sasa
kuamkia leo, wameniletea vitisho kuwa Mambo
sasa ni mzee sana sasa wanamhitaji na mtoto wake
yani sikitu na mtoto mwenyewe hatujui kafia wapi
mwaka huu unakaribia." Sikujua aliuma meno kwa
mshangao na huku akiwa anafikilia sana. "Kweli
jambo zito sasa hawajui kama mtoto wa mambo
sasa kafa?"
Walishindwa kujua mtoto gani wa mambo sasa
anayezungumziwa na watamshawishi vipi bwana
Mambo sasa aje Bwawani, ndipo mipango
ikatengenezwa ya kumfanya mzee Mambo sasa
arudi bwawani na wao wafanye yao.
"Sasa itabidi mapato uondoke hadi kijiji cha
SHISHIMO ukifika kule chunguza kwanza upajue
kwao ukipajua mtafute mkewe alafu ujue wana
matatizo gani ambayo utajua wewe pakuingilia".
Mapato alikubali na akaanza kujiandaa kwa safari.
Ndani ya kijiji cha SHISHIMO sasa Mzee Mambo
sasa baba wa chito alienda kwa rafiki yake ili
kuanza kufanya kazi ya kumtuma jini wao kwenda
kumchukua SIKITU kokote aliko. "Sasa tuambizane
hapa tunamtuma yupi?' aliuliza Mambo sasa "
Nyamnyena ndie tunamtuma kazi na yeye atajua jini
gani atamtumia kwenda kumchukua SIKITU kokote
aliko" Basi walifanya kazi yao na hatimae
wakafanikiwa Mizimu ya Nyamnyena ikakubali
kumtuma jini wao ili kwenda kumchukua SIKITU.
"Lakini Mambo sasa wewe rafiki yangu mpaka sasa
nimeona kuna watu wanakutafuta wewe wakutoe
sadaka kwa hilo jina lako Mambo sasa" Mzee huyo
alishangaa mbona mageni hayo
"Fahamu hivyo na wako mbioni tayari wamemtuma
mmoja wao kuja hapa kijijini ili wapate kile
wanachokihitaji sasa ni hatua ya kuchunguza kila
mgeni anayeingia hapa tumkague kama mkubwa wa
mambo basi tumjue anakuja kwa lengo gani na nani
ambae anamtumikia". Kumbe harakati za mapato na
sikujua zilishajulikana.
Ndani ya KILIMALONDO majonzi kwa kijana
KATUNJE kwa kupotelewa na Lyoto na hajui wapi
ambako kapotelea, mama mwaija alikuwa karibu
sana katika kuhakikisha kuwa anakuwa kwenye hali
salama muda wowote ule "Katunje naomba hili
ganda la mgomba tafuta viatu vya Mzee Kauzibe
ufananishe kwa kuwa hawa wazee ndio wawindaji
hodari hapa ukimaliza kwa huyo nenda kwa mzee
UDEVU utafahamu ukubwa ukifanana njoo niambie
nijue nakusaidiaje kumpata huyo binti yetu.
Katunje alitulia huku akiwa na mipango yake ya
chinichini kutaka kurudi basi nyumbani kwao maana
hata hivyo aliona hakuna sababu kubwa ya kuishi
mbali na kwake. "Lakini siwezi kumuacha huyu binti
akiwa huko aliko na ni bora hata mwili wake niuone
alafu nimrejeshe kule alikotokea na nikamkuta na
naamini baada ya hapo najua baba mambo yake ya
kichawi atakuwa kayaacha kabisa ".
 
SEHEMU YA KUMI NA SABA 17
Endelea............
................Haikuwa kazi rahisi kwa Mzee Mapato
kutaka kufanikisha lengo ambalo alilipangilia
kulifanya kwa Mzee Mambo sasa ambae ndani ya
kijiji cha SHISHIMO anajulikana kwa jina la CHITO.
Jina hilila Mambo sasa ni la baba yake ikiwa
kipindi ambacho bwana Chito yupo kijiji cha
BWAWANI alitumia jina la baba yake na watu wote
wa kijiji hiko wakamjua kwa jina hilo. Pia kwa
upande wa Mzee Mambo sasa baada ya kupewa
taarifa na rafiki yake kupitia mizimu yao ya
NYAMNYENA alijiandaa vyema sana kuhakikisha
kuwa hakuna mgeni yeyote ambae ataingia ndani ya
kijiji chaobila wao kumtambua, hali hiyo ilipelekea
kuwa makini sana pindi pale atakapohisi kuwa kuna
mtu mgeni kaingia laziam wamfuate.
Bwana Mapato aliona muda muafaka wa kuanza
kuzoea pale kijijini umefika kwanza alifika kwa
Mwenyekiti ambae alijulikana kwa jina la MASANJA
huyu bwana alichaguliwa kuwa mweneyekiti wa pale
kutokana na elimu ambayo aliyokuwa nayo na pia
anatokea kijiji tofauti na Shishimo. Mzee mapato
baada ya kuhakikisha kuwa kafika tayari ndani ya
kijiji hiko ambacho kinasadikishwa kuwa mtu
ambae anamtafuta anapatikana pale, ndipo aliulizia
kwa mwenyekiti na kupelekwa. Hakika
alijitambulisha vyema kabisa huku akiomba msaada
wa kile ambacho alidai kuwa anakitafuta.
"Mwenyekiti naitwa SUMAE natokea kijiji cha jirani
hapo, shida yangu kubwa ni kumtafuta ndugu yangu
ambae kanipotea kwa miaka mingi yani kulikuwa na
ugomvi wa kifamilia sasa yeye akaondoka mpaka
sasa namtafuta sijampta". Mzee Mapato aliamua
kumuongopea bwana Masanja ambae alionekana
kusikiliza kwa makini huku akionyesha sura ya
huzuni. "Mh! pole sana ndugu yangu kwa jambo hilo
lililokukuta, sasa ulihitaji msaada gani nikusaidie
kwa sasa?" Mzee Masanja alimuuliza bwana Mapato
ambae alijitambulisha kwa jina la Sumae.
"Mwenyekiti nashukuru sana kwa ukarimu wako pili
ninachoomba nipate hifadhi, pili sitaki taarifa ya
kufika mimi hapa isambae kwani kama yupo hapa
kijijini nina imani kubwa atakimbia na kutoweka".
Mzee mapato alitumia nguvu ya ziada sana
kumfanya mwenyekiti amuamini yeye kwa lile
alisemalo.
Alifanikiwa kupata nafasi ya kuishi pale baada ya
kuonyeshwa kibanda ambacho ataishi pale, Mapato
aliona moja ya mbinu zake zinaendelea vyema
kutimia kwani atampata mzee Mambo sasa na
kumshawishi kurudi kule kijijini na kumpeleka moja
kwa moja kule bwawani ili iwe rahisi yeye kuuliwa
na bwana mapato kufaidika kwa maisha yake na
mikosi aliyo nayo. Kwa kuwa ilikuwa ni usiku
walilala, majira hayo ya usiku kwa upande wa Mama
Sikitu hakupata usingizi kabisa, alisikia kelele za
ajabu zikiendelea huko nje, ajabu zaidi akimuangalia
mumewe hana hata habari alikuwa anakoroma sana
kiasi ilikuwa inamchukiza sana Mama Sikitu.
Aliondoka kwenye kitanda kisha akaanza kufungua
mlango wa chumbani kwane ili atoke nje aende
kushuhudia kile ambacho anakihisi kwa muda ule.
Alifanikiwa kupiga hatua kadhaa mpaka kwenye
sebule ya nyumba hiyo ambayo inatenganisha
chumba chao na baba mkwe yani mzee Mambo
sasa, "Mh! hizi sauti zinatokea chumbani kwa Mkwe
kuna nini tena humu?". Alijiuliza maswali ambayo
alishindwa kupata majibu yake, kadri sauti
zinapozidi mshangao ulimzidi zaidi mama Sikitu
huku akiwa na hofu kubwa sana pale alipo.
Alisogea taraibu taratibu karibu na chumba cha
mkwewe alipofika mlangoni akachungulia kwenye
moja ya uwazi ambao upo kwenye mlango wa
chumba hiko, alishika mdomo na palepale
akadondoka chini na kuzimia.
Anaonekana mzee Mambo sasa akiwa na kaniki
nyekundu ambayo alikuwa kaivaa lubega mithili ya
watu aina ya wamasai, alichungulia huku na kule
ndani humo hapakuwa na mtu ndipo akamburuza na
kumuingiza chumbani mwake. alitoka tena na
kuufungua mlango wa kutokea nje kisha akauacha
wazi na yeye akarudi chumbani kwake. Asubuhi na
mapema sana CHITO kama kawaida yake aliamka
lakini akipapasa wa ubavu wake hakuhisi kuwepo
kwake. alishtuka kwani ndani ya nyumbaq hiyo chito
ndie mfunguaji mlango na kumuamsha baba yake
kisha huelekea shambani sasa kwa wakati huo
ilikuwa kama ajabu kwake. Aliinuka na kutoka
kuangalia mlango wa nje anashangaa kuona mlango
ukiwa wazi. Ndipo akaenda kumgongea baba yake
mlango ulikuwa umefungwa akajua baba yake
alikuwa kalala.
"Baba, umemuona mke wangu huku nje?" alimuuliza
baba yake "Mh! mwanangu tangu lini mimi kuamka
kisha nikaweza kutoka nje na baridi hili, kaenda
wapi tena na yeye". Alikuwa anajibu huku akiwa
anamjia pale mlangoni. "Yani nashangaa sio
kawaida yake kutoka nje naona mlango
umefunguliwa kama vile uko wazi pia mlango
wangu chumbani ulikuwa wazi" Mzee Mambo sasa
aliusogelea ule mlango wa nje akawa anasikitika
sana ndipo akatoka nje na chito nae alimfuata baba
yake kule nje "Aaaah! mwanagu hawa wanawake sio
watu kabisa vichwa vyao vinafanana nadhani hata
wana akili moja kama mama yako na yeye
aliondoka hivihivi hapa nyumbani" Chito
alichanganyikiwa sana baada ya kuambiwa kuwa na
mama yake kapotea kwa mazingira yaleyale. Lakini
ajabu iliyoje usiku wake mvua za rasharasha
zilinyesha na asubuhi kuacha alama ambazo mtu
angekuwa anapita basi angejulikana lakini hilo hapo
halikuwepo.
Mapato ambae kwa sasa alijiita kwa jina la Sumae
alianza kukaa na mwenyekiti huyo ili aanze kumjuza
kwa mambo fulanifulani, "Bwana mwenyekiti nina
swali kidogo hapa?" alisema mapato " Sumae
usihofu sema kile kitu ambacho unahisi kitakufaa
kwenye uchunguzi wako" "Nilikotokea kuna
ushirikina sana watu wanauliwa na wanagombanisha
watu kupitia uchawi ndio maana mpaka sasa ndugu
yangu kapotea kwa ajili ya hayo mambo vipi huku
hayo mambo yapo?". Aliuliza swali ambalo alijua
kuwa atapata makubwa ya kumsaidia sana. "Sumae
kweli hapa pia yapo hayo mambo mfano kuna
wazee kadhaa ambao wanasumbua sana hapa na
nakutaka uwe makini sana na hawa watu" Mzee
Mapato akashuku huku akiwa na hamu ya kujua nani
hao "Sawa hivi unaweza kunitajia ili nijilinde na hao
watu nikiwasikia ili njiepushe nao". Mwenyekiti
alipumzika kidogo na kusema "Kuna mzee mmoja
hapa anaitwa MAMBO SASA....." "Anaitwa naniiii?"
Ndani ya kijiji cha KILIMALONDO anaonekana kijana
KATUNJE akiwa njiani kuelekea kwa bwana
KAUZIBE alionekana kuwa na hasira sana ambazo
zilikuwa zinamruhusu hata kujeruhi mtu, ghafla
anatokea mama Mwaija ambae alikuwa
anamshangaa sana. alimshika mkono na kumuomba
asifanye jambo kwa hasira kwani atakuja
kusababisha matatizo ambayo atashindwa kuyazuia
"Ngoja nikuambie kitu kijana wangu, kila kitu kina
mipango yake fanya mambo kwa utaratibu na
utakuja kumjua mapema sana, nimegundua kuwa
hilo ganda halitotusaidia kitu kwa sasa " Alisema
mama mwaija na kumfanya Katunje amshangae
kumuambia kuwa halina faida yeyote, "Kwa nini
sasa useme halina faida yeyote kwa sasa?" Katunje
aliuliza "Chakufanya nenda kijiji cha MPOLONI huko
kuna mzee maarufu sana wa kuagua (kutambua)
nyayo, huyu ukimuambia kuwa Mama Mwaija
kaniagiza basi atakusaidia anaitwa Mzee UKELELE
pia utakapo toka hapa mtu yeyote asikujue".
Katunje alifikilia sana ndipo akalitupa lile ganda la
mgomba ambalo lilitengenezwa kufananisha na
nyayo za miguu ambayo ilionekana kule wakati
wanamfuatilia LYOTO. Siku hiyohiyo kijana Katunje
alijitolea kufa na kupona kwenda kijiji cha
MPOLONI, safari yake ilianza kama masihara sana
lakini kadri muda ulivyozidi ndipo safari ilikolea
huku akiwa na kifaa ambacho alibebea maji. Majira
ya usiku sana ndipo alikiona kijiji cha mpoloni na
kumfanya afurahi sana kijiji hiko kilikuwa bondeni
hivyo ilikuwa ni rahisi sana kuonekana. Hakuwahi
kufika ndani ya kijiji hiki kwani ni mara yake ya
kwanza na kwa kuelekezwa tu na Mama Mwaija.
Akiwa njiani kukikaribia kijiji hiko ndipo alisikia
sauti za vicheko vya watu ambao yeye hakuweza
kuwaona, "Ahaaa kumbe na huku kuna upumbavu wa
kichawi kama shishimo, nashukuru baba yangu
alinikabidhi dawa ya kujilinda" Aliendelea kutembea
bila wasiwasi hadi ndani ya kijiji hiko kikiwa na
ukimya mkubwa sana. alifika kwenye nyumba moja
ambayo aliona kuwa kuna watu wakizungumza
mawili matetu kama familia, alifika na akawasalimia
wote kwa pamoja "Shikamoni wakubwa zangu"
katunje alitoa heshima " Malaaba abadi gadi gadi
gijada" Wazee hao walikuwa wanaongea kama watu
ambao wanaumwa mafua kwa muda mrefu maneno
hayakai sawa yani yanapandanapandana. "Naitwa
Katunje natokea KILIMALONDO nimekuja hapa
kijijini kwa shida ya kutaka kumuona mzee
UKELELE". walionekana kukaa kimya kwanza kisha
mmoja wapo akasema "ugelele adabadigana mbali
da hapa sasa bola ulale hapa kecho achubuhi
tuguojeshe wabi anabadigana bwana ugelele"
Ilimuia ngumu sana yeye kukubali kulala pale lakini
akijiangalia kachoka na anashida ya kweli ya
kumuona huyo mzee na kaambiwa ni mbali ambako
anakopatikana, hatimae alifanikiwa kukubali kulala,
Kabla ya yote aliandaliwa chakula chenye nyama
nyingi ambazo hakuwahi kuamini kama atapatiwa
kiasi kile, alianza kula na nyama ya kwanza
hakuielewa ya pili, "Mh huyu mnyama gani" alijiuliza
yeye mwenyewe bila hata kujibiwa akaendelea kula
lakini ile nyama ilimshinda tabia kabisa. "Mgedi
kalibu jisigie gama ugo jumbani kwako gilimalondo"
Ndipo akaonyeshwa sehemu ya kulala, Katunje
alikuwa na wasiwasi mkubwa sana kwani tumbo
lilianza kumchefua huku usingizi hakuupata kwani
alikuwa na dawa ambayo ilimsaidia kiasi fulani
kutodhurika. Asubuhi aliwaaga baada ya kuelezwa
na hatimae akafika hadi kwa mzee UKELELE.
Alikaribishwa na baada ya kujitambulisha kuwa
kaambiwa na nani aje pale " Aaah kumbe Mama
Mwaija mimi ndio baba yake mzazi, na binti yake
ninae mimi hapa ninaishi nae" lakini ghafla akawa
anasumbuliwa na tumbo ndipo yule mzee
akamshika vizuri tumboni akamuangalia kwa makini
ndipo akachukua dawa fulani na kumkabidhi ainywe
katunje alikunywa, alianza kutapika nyama zote na
jinsi alivyokuwa akizivamia kwa fujo. aAliishika
moja na kuanza kusikitika " Kijana ulikula wapi hizi
nyama" Ukelele aliuliza " Mwanzo wa kijiji nilipofika
na kuuliza" Katunje akajibu "Mwanangu umelishwa
nyama ya mtu" Mzee ukelele akamueleza kuwa
katunje kalishwa nyama ya mtu " Nyma ya
mtuuuu......Mamaaaaa".
Ndani ya kijiji cha CHAMLO, ilianza kuwa gumzo
kubwa sana kwa LYOTO kuolewa na Kijana wa mzee
kiongozi pale Chamlo bwana BAMUZI. Wanawake
wa pale hasa NAOMI alishindwa kuamini kabisa
kama Bamuzi kaamua kumuacha yeye na
kumchukua mwanamke ambae hafahamiki wapi
ambako anatokea, haikuwa kwa wasichana tu bali
hata kwa watu wa kawaida ilikuwa ni ajabu sana
kwao wao kufanya vile. Mzee Mwalami ndie ambae
alimuokota yule mwanamke aliitwa kwenye moja ya
kikao cha viongozi ili aulizwe maswali kadhaa
kuhusiana na binti LYOTO KATUNJE, mzee huyo
alifika siku hiyo ambayo aliambiwa kuwa anahitajika
wazee kadhaa akiwemo mzee ngololo, pamoja na
Bamuzi mwenyewe huku Lyoto aliachwa akiwa na
wanawake ambao wanamtazama kwa umakini kama
moja ya kazi yao kuhakikisha anakuwa salama
muda wowote pale.
"Jamani siku ambayo nilifanikiwa kuonana na huyu
binti ilikuwa kama bahati kwani aliletwa na maji
yaendayo kasi sana kupitia ule mto lakini pale alipo
anafahamu jina lake pamoja na la baba yake ambae
ni huyo KATUNJE hajui wapi anatokea ndipo
nikaona vyema nimsaidie kwa kuwa kiongozi wetu
anasaidia watu". Walifurahi kwa maelezo mazuri ya
mzee yule japo wengine walikataa kabisa yale
maelezo lakini BAMUZI alimaliza kwa kusema yule
ndie chaguo lake watake wasitake.
Mama Naomi pamoja na Naomi walisikitika sana
kitendo cha Bamuzi kufanya vile " Hivi mwanangu
anakasoro gani mpaka amchukue mwanamke wa
kuja tu hapa?" Naomi na yeye alikuwa anamlilia
mama yake amsaidie kwani anampenda sana
Bamuzi kupita maelezo. "Mama...mmaaa...nisaidie
mama yangu... nampenda sana unadhani nitaiweka
wapi sura yangu na mimi najulikana kijiji kizima
kuwa ni msichana mzuri sana jamani alafu anaamua
kwenda kumchukua mwanamke asiejulikana...
.Mama wewe kama kweli unanipenda fanya mpango
wa kuharibu ndoa yao..." "Naomiiii...kuharibu ndoa
ya mfalme mtarajiwa Bamuzi huoni kuwa ni laana
hiyo mwanangu!" Naomi hakutaka kuelewa "Kama
hivyo ni bora hata mimi njinyonge kuliko kuonekana
nje nachekwa na watu" Naomi alifikia hatua ya
kutaka kujinyonga "Basi mwanagu nitasafiri umbali
japo mrefu hadi kwa mzee UKELELE kule MPOLONI
nimuombe atusaidie ikiwezekana amuondoe huyu
mwanamke kwani akiondoka yeye wewe ndie
utatawala na kuwa na nafsi kubwa kwa BAMUZI.
Muda mchache baada ya kumaliza kikao cha wazee
wale ghafla mwanamke mmoja ambae ni
mwangalizi wa binti mfalme mtarajiwa LYOTO alifika
pale hukua akihema na kuonyesha kuwa ndani kuna
tatizo, Bamuzi alikuwa wa kwanza kwenda kumuona
mkewe alikuwa kazimia hana fahamu kabisa japo
walihojiwa hakuna jibu sahihi zaidi ya lile
walilosema kuwa walishtuka tu anaanguka chini na
kuzimia. Aliitwa mzee ambae anahusika na
matibabu katika jengo lile la Mzee Ngololo
alimpima na kumuangalia kisha akasema " Jamani
hapa kuna kazi kubwa, huyu mwanamke kakoswa
na uchawi wa kijini kwa hiyo kuna madhara
makubwa sana ambayo kayapata na hapa hawezi
kuamka mpaka nikague uchawi gani na umetokea
wapi mpaka umkusudie huyu, nikitambua kuwa ni
aina gani ya uchawi basi nitajua dawa ya kumtibu
na atakuwa vizuri", Alimaliza kwa kumfunika na
nguo kama mtu aliyekata roho huku akijiandaa
kufanya utaratibu wa kujua chanzo cha ugonjwa huo
wa ghafla.........
 
SEHEMU YA KUMI NA NANE 18
Endelea...........
Wakati LYOTO kalazwa kwenye moja ya kitanda
pale ndani huku kijana BAMUZI alianza
kuchanganyikiwa kwa kutoamini kwa lile jambo
ambalo limemtokea mchumba wake mpya. Walikaa
na kumsikiliza Mzee NGOLOLO atasema nini
kuhusiana na matibabu ya Lyoto. Baadhi ya
wanawake wa makamo ambao walichaguliwa kama
wasaidizi katika nyumba ile ya Mzee Ngololo
walianza kulia sana kwa kuhofia maisha ya yule
mwanamke. Mzee mmoja alimfuata Kiongozi bwana
Ngololo na kumuuliza swali "Mzee samahani hivi
huyu mwanamke mnamjua kweli mpaka mmekubali
kumuozesha mfalme wetu mtarajiwa?".
Swali hilo lilikuwa kama kidonda kwa mzee huyo
ambaye alikuwa na majonzi juu ya lile tukio
lililomtokea pale kwake. "Ukweli ndani ya kijiji cha
CHAMLO hakimtupi mtu kama sisi tusivyomtupa
yeyote hapa kwetu, kwa hiyo huyu binti ilitulazimu
kumkubali kwa sababu mwanangu kampenda pia
maelezo ya mzee Mwalami yanadhihilisha kuwa
anahitaji msaada mkubwa". Baada ya hapo hakuwa
na swali lolote japo alionekana kuwa na maswali
mengi baada ya kumuona kuwa kiongozi kakasirika
kutokana na kuchanganyikiwa juu ya lile swala.
Muda ulipita masaa yaliyoyoma kama sekunde,
Mfalme wa pale Ngololo alimuita yule daktari aje
kumpatia jawabu ambalo litamsaidia sana katika
kumuokoa yule binti, kwa upande wa Bamuzi
hakubali la kuambiwa kwa jinsi alivyotokea
kumpenda sana Lyoto Katunje alikuwa yuko tayari
kufanya jambo lolote ambalo hata kama litakuwa na
madhara kwake lakini lengo afanikishe. Mzee
daktari ambaye ni mahususi sana kwa kutibia watu
wote ambao wanapatikana pale kwa mfalme
Ngololo, pamoja na wanakijiji wote wa Chamlo.
"Haya bwana KELEBU, nadhani sasa muda
umewadia wa wewe kutupatia majawabu nini zaidi
kimefanyika na nini kifanyike ili tufanikiwe kuokoa
maisha ya mkwe wangu yani huyu binti".
Aliuliza swali kwa bwana Kelebu ambaye anahusika
na swala la utibabu wa Lyoto ambae mpaka mudas
huo hajielewi kabisa yani kazimia kabisa hajitambui
kwa masaa kadhaa baada ya kupigwa kwa uchawi
ambao haujulikani wapi umetokea. "Mzee wa
Chamlo pamoja na mtoto wako ambae ni mrithi wa
Chamlo, ninachokisema mbele yako hakika ni
ukweli mtupu, kwamba....Lyoto kapigwa na uchawi
wa kijini na mizimu, iliyotumwa mbali ambako
sijapafahamu". Ndipo Mzee MWALAMI alidakia kwa
kuwa yeye ndie anamfahamu yule binti tangu siku
ambayo alimuokota kutoka kwenye bwawa, " Sasa
bwana Kelebu samahani umefahamu hiyo dawa ya
kumponya?".
Aliuliza mzee huyo ili apate kujua "Ndio ila
inapatikana mbali na hapa kwani kuna Miti ya
zamani sana ambayo inapatikana Msituni, huo ni
mkubwa sana lakini kabla ya kuingia ndani ya msitu
huo umezungukwa na miti hiyo mikubwa sana, sasa
utomvu wake pamoja na majani yake ndiyo dawa
sahihi katika kumtibu binti huyu". Baada ya kusikia
vile kila mmoja alikaa kimya kabisa huku wakiwa
wanawaza na wasijue nini wafanye, ndipo BAMUZI
alifungua kinywa chake na kusema "Sasa, mganga
wetu hakuna jinsi nyingine ya kumsaidia mke
wangu?" Hapo waliinua vichwa vyao na kumuangalia
muulizaji na anayetakiwa kujibu "Mkuu samahani
kuwa hakuna njia rahisi zaidi ya hiyo kwani hayo
majani ndio maalumu kwa kuponya hayo maradhi".
Baada ya muda kupita majira ya jioni waliendelea
kujadili mpaka walipokubaliana kuwa kuna umuhimu
wa kumtafutia dawa hiyo kokote iliko, waliomba
sasa nafasi ya kuwapata wale vijana ambao
wakaojitolea kwenda umbali huo wote. Ndipo siku
ya pili waliitwa wanakijiji wote wa Chamlo ili
wapewe taarifa na wajue ni nani ambae atakubali
kwenda msituni ili kutafuta dawa hiyo ya kumsaidia
Lyoto.
"Wanakijiji wa Chamlo tuna habari ya huzuni hapa
tulipo, kwani mke wa ambae Kijana wangu
alimchagua kwa bahati mbaya kapatwa na maradhi
makubwa sana ambayo yamethibitishwa na Mganga
wetu wa hapa kijijini bwana KELEBU, na akasema
kuwa dawa yake haipatikani hapa bali inapatikana
Ndani ya msitu mkubwa uliopo mbali kidogo na sisi
hapa, sasa kilichoombwa kutoka kwetu ni vijana
wajitokeze ambao watakuwa bega kwa bega na
BAMUZI mpaka huko na kuchukua hiyo dawa ili
kumsaidia mke wake...sasa tupo tayari kumpokea
yeyote kwani mpaka sasa hivi mgonjwa anaharibika
mwili wake".
Waliendele kusubiliana pale huku wengine
wakinong`onezana kimyakimya huku wengine
wakitoa kama maneno ya kulaumu sana 'Tulisema
sisi mnamchukua mwanamke ambae wa mbali
matokeo yake ndio hayo, hamumju hata chembe
ataenda mwenyewe huyo aliyekuwa nae` ni maneno
ambayo yalikuwa yakisemwa na watu baadhi
wakiwa kwenye kundi la watu kubwa wakijiamini
kuwa sauti hiyo haitowafikia walengwa. Mpaka
muda unapita hapakutokea yeyote pale. Upande wa
nyumba ya mama NAOMI akiwa na mwanae, Naomi
alimueleza mama yake kila kitu kwa kilichotokea
kule " Mama kwani wewe ndio uliemuendea kwa
mganga ?" Alimuuliza swali mama yake huku mama
huyo akiwa kama anapumbazwa haelewi chochote
"Unaongelea nini?" " Yani nasikia kuwa yule
mwanamke, anaumwa na wanatakiwa wapatikane
vijana kwenda na BAMUZI kuufikia msitu ambao
dawa inapatikana" Naomi aliongezea. "Hapana
mwanangu, mimi sijafanya hivyo mana nilikuambia
kuwa nitaenda kwa mzee UKELELE kule MPOLONI
ili niwaachanishe lakini si kumuua".
Maneno mabaya yalipandikizwa kwa wanachi wa
Chamlo kutohitikia wito wa mfalme wao na
kupelekea Mzee Ngololo kuhuzunika sana "Hivi ni
kweli mimi leo nitoe kauli na watu wasiifuate, ama
kweli undugu kwenye raha na shida". Bamuzi yeye
kama mwanaume alijitokeza na kumuambia baba
yake japo alikuwa anamkataza " Baba naomba
niruhusu mimi mwenyewe nielekee huko sitojali nani
kanifuata nataka kumsaidia Mke wangu". Hakuna
ambae aliweza kuamini kama Mtoto wa mfalme
ambae anatarajiwa kuwa Mfalme ajitoe kwenda
kutafuta dawa hiyo, Mzee Kelebu alimueleza kuwa
anatakiwa ndani ya siku mbili kuanzia kesho yake
awe tayari amesharudi, Kijana Bamuzi alijiandaa
kwa ukamilifu huku machozi yakimtoka kwa wingi
kutokana na machungu ya mtu wake wa karibu
sana. Siku ya pili yake aliondoka na walinzi kama
watatu hivi wakumsaidia chochote kibaya ambayo
kitaweza kutokea mbele yao wakiwa safarini, Safari
ilianza kwa kuagwa na watu kadhaa waliojitoa na
kwa moyo japo hawakuwa na uwezo wa kwenda
nao kwa pamoja, walionekana kupotea na njia
ambayo iliwaonyesha kule ambako wanaelekea.
Mzee UKELELE ndani ya kijiji cha MPOLONI
alipomaliza kumueleza KATUNJE kuwa kalishwa
nyama ya mtu hakuweza kuamini alianza kutema
mate ovyoovyo kana kwamba mtu mwenye dini ya
kiislamu anapolishwa nguruwe hali ya kuwa wao
hawaruhusiwi kuila na akaambiwa kuwa umelishwa
nyama ya nguruwe, laaah! kitakachotokea hapo
Mwenyezimungu shahidi, Katunje alihamaki sana
kwa kusema maneno mengi sana "Haaa! asalalee
yani nikirudi pale watanitambua mbona watu
wanakuwa na unyama hivi ina maana hapa
mnakulana nyama wenyewe kwa wenyewe?".
Hayo maneno yote aliyamaliza huku Mzee huyo
akimuangalia tu, alimtuliza wakati Katunje akiwa na
hamasa ya kutaka kulia kwa yale aliyofanyiwa na
wanakijiji wa pale MPOLONI. "Kijana haya kabla ya
yote ebu nieleze vyema sana shida yako ni nini
mpaka mwanangu kakuelekeza kuja hapa". Mzee
ukelele alimuuliza swali ili ajue kwanza shida
ambayo ilimpeleka pale kwake kutoka kijiji cha
KILIMALONDO ."
" Baba samahani yani mpaka sasa yani sijielewi
kabisa mimi natafunishwa nyama ya mtu aaaah
jamani!, sawa ila shida yangu kubwa nimekuja pale
kijijini naishi na binti mmoja ambae nilimuokota
Ndani ya kijiji cha BWAWANI nikiwa na harakati za
kumtafuta kaka yangu CHITO, nimeishi nae pale
kwa muda mrefu huku mzee KAUZIBE aliyekuwa
akinisaidia kumuuguza lakini mpaka sasa binti huyo
kapotea kwa mazingira ya kutatanisha siyaelewi na
baada ya kufuatilia naziona nyayo ambazo zilinipa
akili kuwa alikuwa anafukuzwa, ndipo Mama Mwaija
akanielekeza huku kwani wewe una agua nyayo za
watu zilikopita."
Mzee Ukelele alishusha pumzi nzito kisha
akamuuliza swali kijana Katunje " Huyo mzee wa
hapo kijijini kwenu anajihusisha na nini?" Mzee
Ukelele alimuuliza katunje "Kuna wazee wawili pale
nyumbani kuna KAUZIBE na UDEVU huyu Kauzibe ni
mwindaji na Mganga wa miti shamba kwani ndie
aliyemsaidia huyo binti mpaka akawa na hali nzuri,
na huyu Mzee Udevu huyu ni mfugaji wa kuku na
mbuzi wawili pale kijijini" Alimaliza kwa kutoa na
kwikwi za hasira ya kulishwa na nyama ya mtu.
"Kijana tulia usiwe na shaka kwani kazi uliyoingia
hapa ni kubwa sana, kuna misaada miwili ambayo
naweza kukusaidia mmoja wapo upo tayari?".
Katunje alikuwa kachanganyikiwa kwani tangu afike
hajapumzika na kapata habari mpya ya kulishwa
nyama ya mtu pale kijijini wakati anafika hivyo
alikuwa anajibu bila hata kufikilia majibu yake "Baba
niko tayari"
"Sasa msaada wa kwanza una vipengele vitatu
ambavyo utahitaji nikusaidie kimoja wapo, la
kwanza kumfuatilia huyo mtu ambae alikuwa
anamkimbiza huyo binti kama madai yako, pili
kumfuatilia huyo binti wapi kaishia tatu kukusaidia
wewe uliyelishwa Nyama ya mtu ili usiendelee
kulishwa na ukafanywa msukule hai bila kujijua Ipi
nikusaidie?"
Katunje alikodoa macho kama panya aliyebanwa
kwenye mlango.
"Baba, yani kumfuatilia mtu aliyemkimbiza Binti!,
Kumfuatilia Binti aliko au kujisaidia mimi
niliyelishwa nyama ya mtu ili nisifanywe msukule
hai! Mh mbona ngumu baba basi na msaada wa pili
upoje"
Aliuliza Msaada wa pili ili auangalie kama utakuwa
ni mwepesi aufanye,
"Msaada wa njia ya pili utahitajika kusafiri kwenda
msituni ambako kunapatikana Miti mikubwa
iliyozunguka msitu huo mti huo una faida kadhaa
kwanza kuondoa mikosi,nuksi na uchawi wowote
ambao umekupata pia unaweza kutambua kitu
kilichopotea endapo tukichanganya na dawa nilizo
nazo hapa". Hapo ndipo kijana Katunje aliona hali
imekua tete alijitahidi kudadisi kujua huo msitu uko
mahali gani ili aweze kwenda kwani ni bora aufanye
huu na yeye ajisaidie moja kwa moja na amsaidie
binti LYOTO.
Aliambiwa kuwa kesho ajiandae yani hakuna
kupumzika." Utaondoka hapa usiku wakati
unakaribia asubuhi safari yako itapita kijiji kimoja
kinaitwa CHAMLO hapo utaulizia njia moja ambayo
inaelekea huko ila ukishindwa kwa kuona kuwa
umechoka utamuulizia Mzee MWALAMI na yeye
atakuelekeza bila wasiwasi. Asubuhi na mapema
kweli safari yake ilianza na Mzee Ukelele
alimsindikiza huku akimsii awe makini sana katika
safari yake. Katunje kwa kuwa ni mgeni alikwenda
huku akiwa makini sana njiani huku akifuata
maelekezo yale ambayo kapewa na Mzee Ukelele.
Ndipo Mzee huyo aligeuza njia na kurudi nyumbani
kwake huku akiwa na imani kubwa kuwa kijana huyo
atafanikiwa kufika salama na kurudi na hiyo dawa
ambayo kamuelekeza.
Anaonekana Mzee KAUZIBE akirandaranda kwenye
moja ya pori huku akiwa kama mwenye kutafuta kitu
ambacho kilimpotea kwa muda mrefu sana. Baada
ya dakika kadhaa alifika kwenye mtiu mmoja ambao
alichuchumaa na kuanza kufukua kwenye mizizi ya
mti huo, alikata moja ya mizizi na kutia kwenye
kikoba chake muhimu ambacho alikuja nacho.
Baada ya kumaliza hapo ndipo akaelekea kwenye
yale maporomoko kisha akachuchumaa tena alitoa
zile dawa zake na ile mizizi ambayo aliichimbua
muda mfupi uliopita, alichukua jiwe na kuanza
kusugua mzizi mmoja baada ya kumaliza alilamba
huku akiugulia uchungu uliotokana na mzizi huo.
baada ya kumaliza alisugua tena kisha akachukua
unga ambao ulionekana una rangi ya nyeusi.
Aliinuka na kwenda sehemu fulani ambako
ulionekana kuna mti ambao uliokuwa unaungua
akachukua kuni moja ulioshika moto vyema kisha
akarudi pale alipokuwa mwanzo. akachukua unga
mwingine ambao aliuweka kwenye moto na
ukaanza kufuka moshi mzito sana alianza kuongea
maneno ambaypo alikuwa anayafahamu yeye
mwenyewe, baada ya kumaliza alinyanyuka na
kurudi nyumbani kwake, wakati hayo yanafanyika
Mama Mwaija alikiuwa anayashuhudia kwani
hakuwa mbali na maeneo hayo "Ahaa kumbe huyu
mzee ndio alivyo kha! ngoja arudi kwanza KATUNJE
nimueleze".Mama huyo alifikilia kwanza ndipo
akaenda kwa Mzee SWAI ambae alionekana kwa
kipindi hiko hali yake kuwa si nzuri sana, Baada ya
kufika pale alimueleza yote ambayo alihisi kuwa
aliyaona kwa ufasaha akiyafanya mzee Kauzibe
"Babu, niliyoyaona kweli nadhani huyu mzee
atakuwa anahusika kabisa kwenye swala la kupotea
kwa binti Lyoto".
Mzee huyo wa makamo sasa akiwa anasimamiwa
na kijana maarufu bwana KIMOLO, lakini hali ya
mzee huyo ilikuwa ngumu sana kufanya chochote
ndio maana hata swala la kumfuatilia binti LYOTO
ilishindikana kabisa na aliweza kutamka kuwa
asiendelee kufuatiliwa yeyote kuhusiana na huyu
binti na baada ya kuambiwa na mama huyo
kuhusiana na Mzee Kauzibe alishtuka kidogo na
kuanza kutaka kusimama lakini alishindwa kutokana
na hali yake "Mh! haya mambo sasa yanazidi
kuchanganya kichwa changu, huyu bwana sijajua
ana nia gani na mimi mpaka sasa wakati
nilishaamua kuachana nayo sasa wewe nenda alafu
alafu sisi tutakuja kukupa taarifa". Mama Mwaija
aliondoka huku akiwa na imani kubwa sana kuwa
mzee huyo atajulikana ile tabia yake. Huku mzee
SWAI alimuita Kimolo na kumuambia kitu "Kijana
hali yangu sio nzuri sana kwa sasa nakuomba
umuagize yule kijana ambae huwa anauza mifugo
aende kuuza tena ili ipatikane fedha za kuniuguzia
na pia wewe mtafute kijana ambae nitamuelekeza
akamtafute Mganga ambae atanihudumia kutokana
na hali yangu".
Kimolo aliitikia na mara moja alienda kumuita yule
kijana na kumpatia maelekezo muhimu ambayo
yalimfanya aelekee kufanya hilo jambo. Kijana huyo
alienda kuchukua baiskeli yake na kumpakia mbuzi
mkubwa kwenye tenga ambalo huwa analitumiaga
kwa muda mrefu, Wakati akiwa njiani alifaniiwa
kukutana na vijana wenzake ambao walimuuliza
kuwa wapi ambako anaelekea ni maeneo gani, kwa
kuwa yeye ni mmoja wa kijana wa pale aliwaeleza
wapi anaelekea na anaenda kufanya nini.
Ndani ya kijiji cha BWAWANI ambako kijana huyo
anaelekea kuuza mbuzi huyo kwa kuwa mara ya
kwanza alifanikiwa kuuza kwa muda mfupi, Mzee
MANUALI akiwa nyumbani kwake akiwa anaendelea
na kumuuguza mjukuu wake SUSU ambae alipigwa
gongo la kichwani na kupoteza kumbukumbu,
matibabu yalifanyika kwa muda mrefu huku
akionyesha matumaini kwani susu aliweza kuongea
lakini kumbukumbu zilikuwa zishapotea. Huku pia
Mzee SIKUJUA ambae na yeye alikuwa nyumbani
kwake akiwa na mawazo makubwa sana juu ya
maisha ambayo aliyafanya kipindi cha nyuma na
kusababisha kuishi kwa wasiwasi sana. "Haya
maisha mpaka lini jamani, naishi kwa wasiwasi
mang`amung`amu kila siku nikilala mala jana usiku
MAMA MENGI namuotea kuwa anakuja kurejesha
kuniua,mama Mengi anakuja na kisu kuja kuniua
mimi mh! hapana kabisa itabidi nifanye jambo
muhimu kwa sasa".Muda mchache ndipo anaingia
yule kijana huku akinadi mbuzi kuuzwa kwa bei
rahisi "Mbuziiiiii, mbuziiiiiii kwa bei rahisi sana".
alikuwa anaongea hayo maneno akiwa ndani ya kijiji
akizunguka mitaa ya hapa na pale. Alifanikiwa
kufika hadi kwenye nyumba ya mzee mwalami ndipo
anamkuta kijana SUSU ambae alitokea
kumkumbuka.
Alishuka kwenye baiskeli yake na kwenda
kumsalimia kijana huyo "Babu vipi rafiki yangu
anaendeleaje na hali yake" aliuliza huyo kijana
muuza mbuzi wa mzee swai. "Salama kabisa kijana
umekuja kuuza mbuzi tena baada ya muda mrefu
kupita," Mzee mwalami aliongea. "Mbona kama
rafiki yangu hali yake si nzuri sana kimemtokea
nini". Mzee mwalami alimueleza kila kitu na ndipo
kijana huyo akendelea na kazi yake ya kutangaza
mbuzi.
Kwa ujasiri mkubwa sana bwana CHITO anaonekana
kuwa na jazba kubwa sana juu ya baba yake pale
nyumbani mzee MAMBO SASA, "Kwa hali kama hii
baba lazima ataniambia mke wangu yuko wapi yani
haiwezekani mke wangu kwa nini hamtaki naamini
yeye ndie kampoteza" Upande wa bwana Mambo
sasa akiwa na rafiki yake walionekana kufurahi sana
katika kazi ambayo wameifanya " Sasa bwana
Mambo sasa hapa tumemaliza kazi kabisa lile
kombola ambalo tumelipeleka kule hakika
litamrudisha kabisa hadi hapa" Aliongea bwana huyo
ambaye ni rafiki wa mzee Mambo sasa. "Sasa una
maana kuwa hii itamfanya popote alipo atarudi yeye
mwenyewe kabisa". Mzee huyo aliuliza "Ndio kwani
ule mzimu naufahamu kabisa yani muda hautofika
kuwa siku nyingi majibu tutayaona hapahapa sasa
wewe nenda nyumbani ila kumbuka kuwa usiku
utaenda kumueleza mkuu kuwa mambo yanakaribia
kuwa mazuriu kwani yule mtu uliyemuahidi anakuja
". Mzee mambo sasa alionyesha kufurahi "Lakini
kuna yule mkwe wangu ambae nimemuweka kule
ndani si nilikuambia?" "Ahaaah! kumbe, huyo nenda
kamkate ulimi kabisa mapema alafu chukua hii
dawa ambayo utamnywesha baada ya kumkata
ulimi wake." Ndipo mzee huyo aliondoka kwenye
nyumba ya rafiki yake na kuelekea nyumbani kwake.
Wakatii huo kijana CHITO aliondoka nyumbani
kwake na kwenda mtaani kumtafuta baba yake
popote alipo, lakini kwa bahati iliyoje bwana
MAPATO anafanikiwa kumuona Chito ambae yeye
anamjua kwa jina la Mambo sasa bila kufahamu
kuwa mzee mambo sasa ni baba wa chito ambae
anamuona kwa muda huo. Mzee Mapato alimuuliza
Mwenyekiti bwana MASANJA "Baba hivi yule mzee
unamfahamu ambae anapita kule mbali". Mzee
masanja aliangalia kwa makini sana kisha
akamshika bega na kumuambia kuwa "Namfahamu
vyema huyu mzee anaitwa bwana CHITO" mapato
alishangaa kwanza "Naniii?" "Anaitwa chito
aliondoka hapa kijijini kwa muda mrefu sana baada
ya kugombana na baba yake ambae hakumtaka
mke wake ndipo akaondoka kwa muda mrefu na
sasa karudi tena" Baada ya kupata taarifa hiyo ndipo
mzee Mapato akashtuka sana " Kama anaitwa chito
na baba yake anaitwa nani?" Mzee Masanja
alimshangaa sana kijana huyo "Nashangaa sana
kijana kwani unamfahamu huyu?" " Hapana ila
nimependezwa na habari yake ndio maana nataka
nimfahamu baba yake pia". mzee masanja alifurahi
sana "Ndio baba yake anaitwa Mzee MAMBO SASA
na ni mmoja katika wale wazee ambao ni hatari
sana katika wale wazee niliokutajia " Mzee MAPATO
alishtuka sana ndipo akawa anashangaa mno " Ina
maana kuwa ahadi niliyoweka kwenye ile mizimu
Mzee Mambo sasa si huyu kabisa mamaaa itanibidi
nirudi kabisa nyumbani kwanza au ngoja nimfuatilie
nipajue anapoishi kwanza". Hapo ndipo alipojua
kuwa kaingia sehemu siyo mtu aliyemkusudia ni
tofauti na alivyokuja kuelezwa sifa yake ndipo
aliamua kumfuatilia taratibu ili ajue wapi ambako
anaishi yule mzee..
Mzee Mambo sasa alifika nyumbani huku akiwa na
jukumu la kwenda kumkata ulimi mkwewe. lakini
kabla ya hayo yote alifikilia kitu tofauti na hapo
ambacho kinaweza kumfanya asijulikane na
mwanae kuwa yeye ndie ana nia ya kumuweka
msukule mkwewe, ghafla mwanae bwana Chito
anaingia nyumbani hapo huku akiwa na panga lake
mkononi "Baba nakuomba uniambie mke wangu
siku ya pili hii haonekani umemuweka wapi?" Mzee
mambo sasa alihamaki pia baada ya kumuona
mtoto wake kaja kwa hasira " Nataka uniambie
ukweli juu ya mke wangu hii ndio sababu hata
katunje leo hatujui yuko wapi tuliondoka kwa
mambo yako ya kijinga mama umemuua wewe nina
uhakika utabadilika lini yani hapa nakuambia
huniambii chochote nahitaji uniambie la sivyo
nakuua na ni bora ufe huna faida mzee kama wewe"
alimfuata kwa hasira huku akinyoosha mkono wake
na kutaka kuushushia kwenye mwili wa baba yake
ambae anamtuhumu kuwa kampoteza mkewe,
ghafla mkono wake unashikwa nyuma na kufanya
akose umakini wa kumshushia panga baba yake
aligeuka nyuma anashangaa kabisa kumuona bwana
MAPATO yupo pale na ndie ambae kamshika
mkono akimsimamisha asifanye maamuzi magumu
"Yani Mzee MAPATO umepajuaje hukuuu?"......
 
SEHEMU YA KUMI NA TISA 19
Endelea......................................
.............CHITO alishtuka na kustaajabu sana baada
ya kuona mkono wake ukiwa umeshikwa na mtu
ambae hakumtarajia kabisa kuwa atakuwa pale kwa
muda ule, kama binaadamu wa kawaida lazima hali
ya mshangao itakukuta kwa kuwa unakiona kitu
ambacho hukutarajia kuwa kitakuja na kwa wakati
gani hasa kwa bwana Mapato kuja ndani ya kijiji
cha SHISHIMO bila hata yeye kujua kama takuja
pale na kupafahamu nyumbani kwake,
Alibaki kuduwa kwani neno lake la mwisho lilikuwa
ni kumshangaa kwa kuja pale na kumzuia kufanya
kile kitendo ndipo mkono wake ulipooza na kurudi
chini na hatimae kuachia panga lake.
Bila bwana mapato ilionyesha wazi kuwa Mzee
Mambo sasa alikuwa anakula panga la mwili kabisa
bila kujali kuwa ni baba yake, hayo yote alikuwa
anayafanya kwa uchungu wa mkewe na kwa ajili ya
kuyajua maovu ya baba yakle kuwa anajishirikisha
na mabo ya kishirikina kwa muda mrefu hivyo
hakuwa na imani juu ya baba yake na alimtuhumu
kuwa moja kwa moja baba yyake chito na ndie
ambae atakuwa anahusika kumfanyia vibaya mkewe
kwani siku zote mchawi hana huruma hata mwanae
atamtafuta.
Mapato alichukua muda huo kuutumia udhaifu wa
Chito na kwenda kumtoa baba yake chito na
kumuweka pembeni kwanza huku akimuonyeshea
huruma, mzee Mambo sasa nae alikuwa hamfahamu
huyu kijana kwani kwake mzee mapato ni kama
kijana tu japo uzee ulikuwa unamuanza, aliendelea
kumuangalia kwa makini lakini akaona kuwa ni sura
ngeni machoni mwake. "haya Mambo sasa twende
nje kwanza tukaongee punguza jazba kwani hasira
ni mbaya sana huyu baba yako bwana".
Kitu kilichokuja kumshangaza sana bwana Mambo
sasa wakati kijana huyo asiyemfahamu anakuja
kumtoa Chito alimuita kwa jina la Mambo sasa,
'itakuwa hawa wanajuana hawa ila kwa nini amuite
kwa jina langu'. Walitoka nje na kwenda mbali
kidogo na nyumbani kwa baba yake Chito, lengo
lilikuwa ni kumtiulioza jazba aliyonayo kwa muda
ule kwanza asije kuharibu mazingira.
Wakati wao wanaendelea huku nyumbani mzee
Mambo sasa aliingia ndani mwake, hatimae mama
sikitu anaonekana akiwa kwenye pembe ya chumba
akiwa kafunikwa kaniki jeusi huku akitetemeka
kama mtu ambae alikuwa anatetema baridi kali
sana. Mzee huyo nbila huruma alitoka na kwenda
kuchota makana ya Mahindi kwenye sebule ya
nyumba hiyo ambayo yaliwekwa kwa nia ya kuuza
kwa wale wanaopika pombe za kienyeji aina ya
ULAKA unaotengenezwa kwa makana ya mahindi,
lakini wakati anayafanya hayo alikuwa na wasiwasi
wa kukutiwa na Chito hivyo ilimfanaya
kumwagamwaga yale makana hadi kwenye chumba
chake.
Baada ya kufika kule alimpiga kidogo mdomoni
ndipo akaachama na akamlisha makana yale kwa
wingi baada ya hapo akaenda kuchukua maji na
yaliendelea kumwagika vilevile mpaka kule
chumbani na akamywesha. Hakika Mama sikitu kwa
huruma sana alikuwa anatoa chozi tu bila kuongea
chochote kabisa. "Yani kupona kwako wewe mpaka
pale Mtoto wako atakapopatikana na mimi nikaenda
kulipa nyama kwa wenzangu ndipo utatoka humu la
sivyo milele utakuwa hivyohivyo nyooooooo".
Maneno hayo yalionekana kama anayaelewa kwani
alikuwa anatoa machozi kwa huruma kwa unyama
ule ambao anafanyiwa. Ni mtu gani ambae anakosa
hata huruma kabisa na mwanadamu mwenzake hadi
kudiriki kumfanyia unyama kama anaofanyiwa
mama Sikitu. Baada ya kumaliza kumfanyia yale
aliyomfanyia akachukua dawa fulani na kunyunyuzia
kwenye mlango wake huku akisema maneno kadhaa
bila kusahau kumtaja kiongozi wao Nyamnyena
kwani ndie anayewafanya kuwa wakubwa pale ndipo
akaondoka.
"Rafiki yangu nilitoka Bwawani kwa sababu moja tu
pale, nilitumwa na Mzee SEMENI yule mwenyekiti
nikutafute wewe popote ulipo ili wajue kwa nini
umetoka kule kijijini wakati Mzee Mambo sasa
ulionekana kuwa na msaada mkubwa pale kijijini" ni
maneno ambayo alikuwa akliyaongea bwana
Mapato kumuambia Chito.
"Aaaah! kwanza ahsante kwa ushauri wako wa
mwanzo ila kwa nza siitwi Mambo sasa hivyo
nisingependa kuwepo kwako hapa uniite kwa jina
hilo" Mapato alijifanya kushangaa japo taarifa ya
jina lake analifahamu fika baada ya kuambiwa na
mzee Masanja.
"Aaaah! mbona unanichanganya sasa ehee jina lako
nani " Aliuliza mapato.
"Eheee! mimi ninaitwa CHITO nilitumia Mambo sasa
baada ya kufika kijijini kwenu kwa sababu kama ile
uliyonikutana nayo pale ukweli matatizo ya kifamilia
na nilishawishika kurudi nyumbani hapa baada ya
kule Bwani kupotelewa na mwanangu kipenzi
SIKITU" Mapato alionekana kuhuzunika sana huku
akimpa pole kubwa sana "Mh! pole hayo
nayafahamu sana hata mimi niliagizwa kukuomba
ufike kule lakini kwa hali hiyo ehee kuna habarii yule
kijana SUSU unamjua " alihoji "Yeye tena namfahamu
vyema mbona yani siku chache tu hizi niwe
nimesahau jamani"
walicheka kwa pamoja huku wakionyeshana vidole.
"sasa yule kijana alikamatwa na watu ndipo mzee
wake MANUALI akamtafuta kama unavyomjua
akitoa kauli zake pale ajabu siku moja anaonekana
lakini akiwa na matatizo ya kichwa yani hata jina
lake sijui kama atakuwa analikumbuka pale alipo
maana" Mzee chito alionekana kushangaa sana "Hivi
kile kijiji chenu kina shetani gani jamani maana
lakini huyu kijana naamini kama hakufanya mabaya
maana nakumbuka alinifanya nikose haki yangu
baada ya mimi na mzee SIKUJUA kwenda kwa
mzee SEMENI kama mwenyekiti na shahidi yangu
alikuwa yule lakini alinigeuka ila pole yake"
Baada ya maongezi ya muda mrefuwaliagana na kila
mmoja alielekea kwake.
Mzee Chito alifika nyumbani kwake akiwa na imani
kuwa baba yake atamkuta lakini haikuwa hivyo
baada ya kufungua mlango na kutomkuta mtu,
aliangalia chini akakuta makana na maji
yaliyomwagika yakielekea chumbani kwa baba yake
alishangaa sana huku akishika mdomo wake 'Aaah!
haya makana na maji huku yanafuata nini' aliendelea
kukagua akapata akili ya kufungua mlango wa baba
yake lakini akapuuzia 'hivi inawezekana kuwa baba
ana nia ya kumuweka mke wangu ndondocha au
maan kama kuondoka Mama Sikitu namfahamu
hawezi kuondoka bila hata kuniambia hata kama
tumegombana kiasi gani'.
Hapo ndipo alip[oanza kukumbuka maneno ya
mkewe kabla kupotea nini alikisema 'baba yako ni
mchawi....unaogopa laana kwa mtenda mambo
mabaya hakika laana hiyo haitokufika....nyamnyena
maana yake nini....hakika mimi nitaondoka siwezi
kuishi na mtu mchawi' hayo yote aliweza
kuyakumbuka kwa nyakati tofautitofauti. "Hamna
baba kuna namna ambayo kaifanya na nitaigundua
tu kwa nguvu maana nikimbembeleza hatosema
kwanza kamuua mama, kamfanya ndugu yangu
kupotea huko aliko".
Ndipo alipoondoka na kuelekea kwa mwenyekiti
bwana MASANJA ili aweze kumsaidia kwa mawazo
kadhaa kwa mambo yale ambayo yanamsumbua
sana. wakati anatembea akili yake inamtuma kuwa
mkewe bado yumo mule ndani lakini akili hiyo
ianamjia na kumpotea kwani alikuwa anaonekana
kusimama kwa sekunde kadhaa na kuendelea na
safari, alipofika alimkuta mwenyekiti lakini
alishangaa zaidi kumuona bwana Mapato kwani
alikuwa hafahamu kuwa mapato kafikia kwa
mwenyekiti.
"Oooh! kumbe umefikia kwa mwenyekiti wetu
bwana MASANJA karibu bwana ila bwana masanja
ningekuomba faragha kidogo kuna mambo tuje
kuteta". Bwana huyo asiyekuwa na makuu alisimama
na kumuomba radhi bwana Mapato kuwa atarejea
muda mchache tu. Mapato nafsi yake ilimsuta sana
kwani aliona uongo wake utajulikana pale aliomba
sana mwenyekiti asije kugusia mambo yake, lakini
ilikuwa tofauti sana na fikra zake.
"Mwenyekiti samahani kwanza vipi mpango wako
wa kuutoa ufalme na kuingiza uongozi mpya wa
mwenyekiti na wajumbe unaendeleaje?''. alimuuliza
bwana masanja ambae ana kampeni ya kuondoa
uongozi ule wa kifalme na kuuweka wa kisasa
ambao kila mmoja ana haki ya kuwa kiongpozi kwa
kila kijiji,
"Aaah! kuhusu hilo lipo mbioni kwani sasa ninahitaji
kutembelea kila kijiji nijue uongozi wao unaongozwa
vipi kama ni wa kifalme basi nitajitahidi mpaka
unabadilishwa". Chito alionekana kufurahi sana
"sawa ila nina shida kubwa iliyonileta hapa, najua
nilishakuja hapa kukuambia kuwa mke wangu
kapotea hii ni siku ya tano sijamuona lakini
ninamshuku baba yangu mzazi kuwa anaweza kuwa
ni mmoja wa waliomfanya jambo baya mke wangu
sasa sijui unanisaidiaje" Mwenyekiti alishusha pumzi
kwanza kabla ya kujibu, " Una vigezo gani ambavyo
vimekufanya umtuhumu kuwa mzee Mambo sasa
anahusika kwa hilo".
mwenyekiti alihoji " Yani juzi nilikuta maji
yamemwagwa lakini yakielekea kwake yani
chumbani, jana makana ila leo nimeyaona maji
pamoja na makana sasa nina wasiwasi isije kuwa
anamlisha mke wangu hivyo vitu". Mwenyekiti
alicheka sana ila alimtoa wasiwasi na kumuambia
aende akapumzike kisha atamuita pale "Eti
ulivyofika hapa ukanikuta nipo na mgeni alafu
mkasalimiana kama mnajuana". Mzee chito akasita
kisha akauliza " hapana kwani jina lake nani ?"
"Anaitwa SUMAE kafikia hapa". Chito ilibidi aage tu
maana hilo jina alilotajiwa ni tofauti ila hakuelewa
kwa nini mapato na yeye kabadili jina.
Mzee Mambo sasa anaonekana kwa rafiki yake
NYANDU ambae ni mtu wake wa karibu sana kwa
muda mrefu mno hata katika kazi zao huwa
wanafanya pamoja, walionekana wawili hawa
kutokuwa na furaha kabisa kwa hali ambayo
walikuwa nayo kila mmoja alikuwa kimya akimtaka
mwenzake aanzishe mazungumzo ndipo Nyandu
akaanzisha mazungumzo "Bwana unajua kuwa Mkuu
anatuta hata sijajua kuna nini huko maana wakati
nipo hapa kuna ujumbe wa mizimu ulinipa baada ya
dawa yangu ya hapa mkononi kukaza sana tena si
kawaida"
Ilionekana kuwa ni taarifa ya umuhimu sana kwao
kuitekeleza kwa wakati huo bila hata kuchelewa
"Sasa tunafanyaje" Baba yake chito alihoji "
Tunafanyaje itabidi tuende na akatueleze hata ile
kazi itabidi tukamuulize kama imefanikiwa"
walikubaliana ndipo Mzee Nyandu kwa ustadi wake
wa nguvu za giza walivaa makaniki na
wakakumbatiana ghafla wakatoweka mithli spidi ya
mwanga unavyosafiri. Safari yao iliwafikisha mahali
fulani kama jangwani hivi palivyo baada ya kufika
kwao ndipo watu kadhaa pia walitokea mbele yao
hao walionekana kama walinzi kwani walikuwa na
nguo sare huku wakiwa na umakini wa kutosha
sana.
Walionyeshwa njia ya kupita mahali fulani ambapo
palionekana kuwa kama pango, waliingia humo kwa
wao ni wenyeji kiasi fulani na hizo kazi hivyo
hawakuwa na presha wala wasiwasi wowote.
Hatimae walifika sehemu fulani ambako palikuwa na
kiti kikubwa mbele yao, ghafla alitokea mtu ambae
hakueleweka jinsi alivyo kwani ilisikika sauti na
harufu kali sana ambayo Mzee Nyandu na Mambo
sasa waliivumilia hivyohivyo, pia pale kwenye kiti
palionekana kivuli tu kama moshimoshi hivi ambao
una umbo la binaadamu.
" Nyamnyenaaaaa.....Nyamnyenaaaaa kulumbila
kululmbilolooooo" kwao ilikuwa kama salamu
ambayo walianza nayo kumsalimia mkuu huyo.
ndipo alipoanza kusema nini kawaitia pale, wakati
huo wafuasi wake wako pembeni wengi sana.
"'NDIO..NIMEWAITA HAPA KUWAPA TAARIFA
KUWA NYAMNYENA KAFANYA KAZI NGUVU
IMEPELEKWA LAKINI INAONEKANA HUYO BINTI
ANA NGUVU ZA AJABU AMBAZO ZILISHINDANA NA
NGUVU ZA NYAMNYENA, ILA ZIMEMJERUHI...T
AARIFA ILIYORUDI KUTOKA KWA NYAMNYENA
LAKINI INAONEKANA KWENYE MSITU KUNA
KIJANA AMBAE ANAFANYA JITIHADA ZA
KUCHUKUA DAWA KWENDA KUMTIBIA SASA
NIMESHAMTUMA MZIMU ANAYETOKEA KWENYE
MILIMA YA LYOTO ( Joto) ATAKWENDA KUMZUIA
KINGINE NAMHITAJI YULE MAMA ULIYEMKAMATA
BAADA YA SIKU MBILI,..." Maneno makali na yenye
msisitizo yalitoka kwea kiongozi huyo na kuwafanya
wao wawe na butwaa, walimsalimu tena kama njia
ya kumuaga ndipo wakageuza kurudi hapo ndipo
mzee Nyandu akamkumbatia tena mzee Mambo
sasa na wakapotea kwa haraka zaidi. wakati huo
huku CHITO anafika kwenye nyumba ya mzee
Nyandu akiwa na Imani kuwa baba yake yupo pale
kwa rafiki yake, aligonga mlango ghafla anasikia
kishindo humo ndani """"Vuuuuuuupp!"""".
Ndani ya msitu ambao umekaribia kijiji cha
CHAMLO anaonekana kijana BAMUZI ambae alijitoa
kutafuta hiyo dawa akiwa na vijana wake kadhaa
kama watatu ambao alitoka nao, Walifika hadi
karibu na miti ambayo waliambiwa kuwa iko mirefu
sana, wakati huo pia kuna kijana alionekana
akirandaranda kwa upande wake anafika kwenye
kijiji cha Chamlo bila hata kufahamu kama hapo
ndipo mwanzo wa safari yake kuanza. kwa bahati
ambayo alikuwa nayo kwa siku hiyo alimkuta kijana
mmoja ambae aliweza kumuuliza swali " Kijna
samahani sana Nahitaji unielekeze kwa Mzee
MWALAMI ".
Yule kijana hakuwa na hiyana kabisa alianza
kumuelekeza lakini kwa bahati nzuri alitokea NAOMI
akiwa njiani kuelekea matembezi yake, "Dada
Naomi samahani naomba umsindikize huyu jamaa
kwa Mzee Mwalami kule'. Naomi alisimama
akimsubiri mtu huyo. Kijana alikuwa makini sana
kwa kila hatua.Naomi alikuwa anamuangalia sana
Kijana huyo kwa kuwa alikuwa hamfahamu
jinaaliendelea kumuibia ibia mwishowe akashindwa
kuvumilia ndipo akamuuliza "Kaka unaitwa nani
samahani" Naomi alitoa kibwagizo pale ili kijana
huyo amalizie
"Ahsante Naomi utanifahamu mapema sana ngoja
nifike kwanza alafu nitakujuza yote utakayo siku
tukionana kwani mimi nipo hapa kwa siku nyingi
kidogo". Naomi hakuwa na neno zaidi ya kuendelea
na safari hadi kwenye nyumba ya MWALAMI
alimkuta ndipo Naomi akaondoka zake. Mzee
mwalami alimkaribisha vyema sana ndipo
akamuuliza kipi ambacho amekijia pale.
" Mzee Natokea MPOLONI kwa bwana UKELELE
mimi ni kijana wake ambae kaniagiza nipitie hapa
ili wewe unielekeze kwenye msitu ambao
unapatikana miti ya dawa kwani kuna dawa ambayo
kaniagiza ikiwemo ni njia ya kunifundisha kazi za
mitishamba" Kijna huyo alijieleza vyema sana
mpaka mzee Mwalami akafurahi sana. "Kijana
umefika na unahitaji kwenda lini huko?" Aliulizwa
kijana " Nahitaji leo niianze safari kwani muda bado
upo na kule kuna matatizo ambayo haitakiwi dawa
hiyo kucheleweshwa."
"Jambo zuri zaidi ni kuwa hapa mtoto wa mfalme
kampata mke sasa huyo mwanamke kapata tatizo,
ndipo huyo kijana wa mfalme akajitoa kwenda
kufuata dawa kwenye huohuo msitu ambao wewe
nakuelekeza hii ni siku ya pili inaanza itakuwa
vyema mkienda kusaidiana au kama utahitaji
ukamuone huyo mke wa kijana unaekwenda
kukutana nae" Kijana huyo alimwambia mzee
atakuja kumuona siku nyingine, ndipo akaelekezwa
njia fupi sana ya kufika kwa siku hiyohiyo
"Ila kumbuka kijana msaidie mfalme wetu huko
ukimkuta, alafu wote murudi kwa pamoja sawa
kijana ?" Mwalami alimsisitiza "Sawa mzee usijali".
Wakati anakatiza kijiji kuielekea njia fupi hiyo
anakutana na NAOMI ambae alimsubiria kwa hamu
baada ya kumuoana moyoni mwake tayari donge la
penzi lilisha anza kuingia 'Mh! huyu kijana sasa
nikimuambia kuwa nampenda ataniona mimi sina
adabu, sijiheshimu,sina thamani ila nampenda sana
ngoja hata nimuulize jina'. Alijisemea hayo wakati
yeye kijana anakuja Naomi alijiandaa kwa kumuuliza
jambo. "Oooh! Naomi tumekutana tena " Naomi
alitabasamu kwa kuona dalili zinajileta, " Kumbe
ulitaka kuondoka bila hata kuniambia jina lako
yako". Kwa kuwa Kijana huyo alionekana kuwa na
haraka sana alimtamkia jina huku akiondoka " Usijali
naitwa KATUNJE naelekea kwanza mahali fulani
nikirejea tutaongea vyema sawa". Naomi moyoni
mwake mlijaa furaha ya ajabu kwani tayari
anaonekana kumpenda sana kijana Katunje. Baada
ya muda kupita jioni sana alifika karibia na msitu
lakini anashtuka anakamatwa na vijana watatu
ambapo anageuzwa nyuma anakutana na BAMUZI
kwa upande wake yeye hakumfahamu.
walimhoji maswali kuna aliyoweza kujibu na
mengine hakuweza kabisa "Mimi ni mmoja wa
kijana wa mzee MWALAMI hivyo alinielekeza nije
kukusaidia lakini mimi nilikuwa naishi kijiji cha
mbali hivyo jana ndipo nilifika Chamlo" Uongo
alioutumia ulimsaidia wao kumuelewa ndipo
wakaungana na kuwa timu moja ya kutafuta huo
mti.
Jua sasa lilizama kabisa na giza likawa kinala kwa
muda huo na kuwafanya wao waanze kuzoea
mzingira ya giza, kumbuka ndani ya kijiji cha
Shishimo kupitia Mzee Nyandu kutoka kwa mkuu
wao tayari jini ambae atakuja kuwazuia hawa
anatokea kwenye mazingira ya moto au joto kama
maelezo ya mkuu wao alivyowaeleza kule pangoni,
hivyo basi kwa upande wa Bamuzi pamoja na wale
wengine akiwemo Katunje ambae hakujitambulisha
jina pale, Walikuwa wamepumzika ghafla katunje
anashtuka kwa pale alipo lala anashangaa kuona
kizinga cha moto kikiwa kwa mbali kitu ambacho ni
cha ajabu kwa mazingira kama hayo kutokea.
Alimuamsha Bamuzi, "Hey hey amka kwanza uone
hiki ni nini jamani" Bamuzi aliamka na wale vijana
watatu nao wakaamka, walishuhudia kweli kizinga
cha moto kikiwa kwa mbali kikiwaka, " Kijana
itabidi tufike pale inaonesha kuwa kuna watu
wanaishi wanaweza kutueleza kuwa hiyo miti iko
wapi" Yalikuwa ni mawazo ya Bamuzi ambae
alikuwa hana chochote anachokielewa.
Alionekana kijana Katunje kutikisa kichwa huku
akiangalia kwa makini ghafla akashangaa ile dawa
ambayo kaifunga kwenye mkono wake kwa juu
inamvuta sana mpaka anahisi maumivu, aliwaza
akakumbuka kuwa
'Mjukuu wangu hii dawa ninayokufunga hata baba
yako pamoja na mambo yake ya kichawi hatoweza
kukudhuru sasa pindi ukihisi maumivu basi jua
kuwa kuna hatari na unahitajika kuondoka haraka
maeneo hayo usije kudharau....' alikuwa
anakumbuka kauli kutoka kwa babau yake Katunje
ambae bado hatujajua mpaka sasa yuko wapi,
tunaweza kutambua mbele ya safari.
Alisimama na kuwaambia "jamani hapa kuna hatari
inatubidi kwa haraka sana tuondoke kabla
haijatokea fanyeni haraka tuondoke jamani
mniamini". Japo walikuwa wagumu kumuamini
lakini iliwabidi ndipo wakatoka pale kwa haraka
sana ghafla wanaona kabisa vizinga vya moto
vikiwa pale walipotoka kwa wingi na vingine vikawa
kama vinarushwa hivi kuwafukuza. Bamuzi
hakuamini kwa kile ambacho anakiona mbele yake.
Walitafuta mahali pengine ambako walihisi kuwa
watafanikiwa kwa bahati [palikuwa salama kabisa,
walilala mpaka asubuhi. Walianza kusaka mti huo
ndani ya msitu huo lakini wakikumbana na vizngiti
vya ajabu ajabu, hatimae wanafanikiwa kuifikia miti
hiyo ndipo wakachimba mizizi yake na magome
kadhaa pamoja na majani yake waliyachukua.Safari
ya kurudi sasa ilikuwa ni kasheshe kwani kila
wanakopita Katunje anawaambia ni hatari kila njia
kwao ni hatari kabla hawajaendelea anajitokeza jitu
lililooza sura mbele yao likitoa midenda huku
akishikilia kijiti kinachotoa moto alikuwa
anakilamba bila wao kuamini kuwa moto
anavyouchezea, ndipo kijana mmoja kati ya wale
watatu akajitokeza na kuwaambia " Mfalme huku ni
porini tumekuja bila hata kutoa sadaka ya damu ili
kama kuna mizimu kama hii basi ituache
kutusumbua" kila mmoja alikubaliana na lile swala
swali likaja tunafanyaje sasa.
"Mfalme wangu wewe nenda kapeleke dawa kwa
mkeo apone pia nawatakia maisha marefu acha
mimi nijitoe muhanga kwa hili " walianza
kumshangaa sana baada ya yule kijana kwenda
kujitoa mbele ya yule kiumbe fasta sana akararuliwa
kwa haraka bila huruma,
Bila utata wao wakapata nafasi ya kupita kuelekea
majumbani kwao, lakini majonzi mazito ya
kumpoteza kijana wao mmoja wakiwa mbele
Bamuzi ana angalia nyuma hawamuoni kijana yule
ambae walikuwa nae yani KATUNJE. Bamuzi
alishtuka sana akaanza kuangalia huku na kule lakini
hawakufanikiwa kumuona kijana huyo. "Yani huyu
jamaa kanisaidia sana sasa atakuwa wapi jamani".
Walianza kumtafuta huku na kule lakini walishundwa
kumuona kabisa, walisikitika wakajua kuwa lile jitu
la ajabu litakuwa limemmeza. Basi waliondoka huku
wakipita kukimbia ovyo hadi walipofika kwenye kijiji
chao. Wanakijiji waliwaona wakiingia ndani ya kijiji
kile na vijana ndipo walipoanza kuwa na aibu kubwa
sana kwa kuwa mwanzo walikataa kabisa kuungana
na Bamuzi kwenda kumsaidia kwenda kuchukua
dawa na hatimae sasa Bamuzi anarudi akiwa na
vijana wake wawili baada ya mmoja wao kujitoa
sadaka.
Baada ya kufika alipokelewa lakini hakuwa na furha
kabisa kwa kupotelewa mtu muhimu sana kama
Kijana yule ambae walikutana nae. Walifika baadhi
ya vijana kama Mwalami na Mzee Kelebu ambae ni
daktari wa pale kwao. Mzee Ngololo alimuendea
mwanae Bamuzi akamuuliza "Mwanangu ehee habari
za huko " Bamuzi alifuta chozi kwanza kisha
akamshika mkono baba yake na kumuambia " Baba
inatakiwa tumuombe radhi mzee mwalami pamoja
na familia ya kijana ZWELI, "Kwa nini unasema hivo
mwanangu?"
"Kuna kijana alikuja kutusaidia kule polini ila hata
jina lake hakuniambia kwa kuwa sikumuuliza ila
alisema alitokea kwa mzee Mwalami sasa kafariki
pamoja na kijana zweli kafariki lakini walijitolea
muhanga kwa ajili yetu kabisa baba itatubidi tufanye
hivyo" Walimuita mzee mwalami wakamueleza huku
wakimpa pole lakini mzee huyo alishindwa kuelewa
kabisa kwa nini anaombwa msamaha wakati yeye
ahusiki na chochote kuhusiana na kijana huyo
aliyekuja. " Yule kijana alikuja jana mapema sana
hapa kasema anatokea kwa mzee mmoja rafiki
yangu bwana Ukelele aliomba nimsaidie
kumuelekeza kwenye uo msitu nikaona ni vyema
sana akasaidiana na wewe sasa kama kafariki
itabidi tupange siku tuende kwa mzee Ukelele kijiji
cha MPOLONI ili tukamueleze kwa yaliyotokea.".
Kijana Katunje ambae alipita kijiji cha Chamlo bila
hata kujulikana kuwa yeye ni nani zaidi kwa binti
Naomi ndie ambae kaacha taarifa zake lakini
Katunje bila hata kufahamu kuwa ndani ya kile kijiji
alichoshindwa kujitambulisha vizuri ndipo mahali
husika ambako Lyoto yupo kweli jambo usilolijua ni
kama usiku wa kiza.................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom