Riwaya: Hatia (Mipango nyuma ya kisogo changu)

josephdeo

Member
Nov 23, 2015
95
196
Muandishi:- Joseph .D. Migini
Call/txt:- +255766604683
Josephdeo70@gmail.com

Ndani ya chumba hichi cha wastani kilichoja samani za kufanya kuitwa sebule ya kisasa kwa waingiao. Nilikuwa nimeketi kijana Mimi umri wa miaka thalathini na mbili toka niwepo kwenye ulimwengu huu. Binafsi haiba yangu ni mtu mtaratibu hata nisipende Shari na yeyote.

Majira haya ya asbuhi nilikuwa nikipata kahawa iliyotayarishwa na mke wangu Brenda. Huku hisia za mawazo yangu zikiwa mbali na ulipo mwili wangu. Hata sikuweza kusikia kilio cha binti yangu wa miezi miwili niliyekuwa nimembeba mikononi mwangu.

Hisia hizi zilikuwa zimenichukua na kunirudisha nyuma. Kwa kadri ya miaka mitatu na kunikumbusha ni vitu gani nilipitia katika kipindi hicho. Mawazo mengi yalikuwa ni juu ya kuweka visa na mikasa hiyo kwa njia ya maandishi. Japo sio muandishi mahiri au mashuhuri lakini naweza kuyaelezea vyema haya yaliyonikumba kwa njia hiyo.

Sasa sina jibu la moja kwa moja juu ya sababu inayofanya kuyaandika haya. Zaidi ya nafsi yangu kunisukuma kufanya hivyo. Nilisogea mahali ambapo nahifadhi tarakishishi yangu ili niweze kutimiza haja hizi za moyo wangu.

Maisha yamekuwa fumbo gumu kulipatia ufumbuzi. Unaweza kudhani kuwa maisha yako binafsi yapo chini ya udhibiti wako na Mwenyezi Mungu kumbe hapana!. Bali maisha yako yanatengenezewa njia na binadamu wenzio.

Wapi upite, wapi ukanyage na wapi huruke yote hayo wanadamu wenzio ndio wanakutengenezea. Na mwisho kabisa waamua kuwa uwe wapi na nini kiwe hitimisho lako.

Nami nilikuwa kama wewe hapo unayesoma. Nilikuwa kama wewe kwa kudhani kuwa maisha yangu yapo kwenye udhibiti wangu na Mungu pekee. Mpaka pale yaliponikuta yale ambayo sikuyapanga wala kuyatenda mimi mwenyewe ila yalikuja kuhusu mimi.

Kama bado ujaelewa ninachokisema fuatana nami kwenye mkasa huu.

Nafikiri hii si namna nzuri, bora au pengine ya kufurahisha katika kuanza uandishi wangu. Je, mimi nimeonewa?, Lakini kabla ya kuwapa jibu hilo mnaweza kunijibu uonevu ni nini?. Hakika Mimi sijui ila naweza kuyaelezea yale yaliyo nikuta kisha wewe msomaji ndio unipe majibu kama nilionewa au la!.

***

Maisha yangu yote nimeishi nikiwa na ndoto ya kuwa mwalimu ili niinufaishe jamii iliyonizunguka kwa maarifa yangu. Lakini nilicholipwa ndio imebaki kama kovu moyoni mwangu. Nakumbuka vizuri sana, nakumbuka kila kitu kwa sababu hata ingekuwa vipi nisingeweza kuja kusahau hichi nilicho kipitia. Siwezi kabisa labda niwe mfu.

Nilikuwa mimi pamoja na watu wawili ambao nilikuwa nimewapatia kibarua cha kunilimia shamba langu. Tukiwa tunatoka shambani huku tukiwa kwenye barabara kuu ya kisiwa cha Maisome sehemu ambayo niliamua nifanye biashara ya kilimo. Siku hiyo tulipishana na gari tatu. Ilikuwa ni nadra sana kuliona gari ndani ya kisiwa kile. Achana na gari za kifahari kama hizo zilizotupita kwa kasi.

Nami nikaungana na wanakijiji wengine kushangaa hali ile ngeni sehemu ile iliyo na umasikini wa kutupa. Huku miundo mbinu ikiwa imezorota kiasi cha kufanya umasikini uote mizizi.
Walitupita kwa kasi sana na walipoondoka kwenye upeo wa macho yetu sisi tukaendelea na simulizi zetu zilizokuwa zimekatizwa na kupita kwa magari yale.

Umbali wa kutoka eneo nililokuwa nikiishi mpaka shambani ilikuwa inachukua hadi saa moja kwa mwendo wa haraka haraka na mwendo wa taratibu ilikuwa inachukua saa moja na nusu. Hivyo tulikuwa tunatembea haraka haraka wakati wa asbuhi wakati ambao tulikuwa tukienda shambani na wakati wa kurudi tulitembea taratibu taratibu.

Tukiwa njiani mara tukaona zile gari zikirudi na zilipofika usawa ambao tulikuwa mimi na wale wenzangu zikafunga breki za ghafla. Sisi tulikuwa kando ya barabara na tuliweza kulishuhudia hilo vyema. Baada ya kufanikiwa kuzishika breki na gari hizo kusimama wakatoka wanaume kumi kwa idadi yao huku wote wakituelekezea bunduki zao.

Sikuwa mtaalamu wa maswala ya intelijensia ila nilikuwa nimesoma baadhi ya simulizi kadhaa zilizokuwa zinaongelea mambo hayo. Huku pia nikiwa nimetazama filamu nyingi zilizokuwa zinaelezea dhahiri maswala ya kijasusi. Kwa elimu yangu ndogo eneo hilo ikanipa taarifa ya kutofanya chochote kile huku panga ambalo lilikuwa mkononi mwangu likianguka chini.

"weka mikono yenu juu!!". Mmoja kati ya wale wanaume akaamrisha nami nikawa wakwanza kutii.

Katika uelewa wangu mdogo nilielewa vyema saikolojia ya askari kuwa mara zote ujiona anayo mamlaka juu yako. Na yuko juu yako kimaamuzi hivyo haipaswi kumkosoa wala kuonekana wewe huko sahihi huku yeye akiwa kakosea. Hivyo jambo moja muhimu kuwahusu ni kwenda sawa sawa na wanavyotaka. Wote tukanyoosha mikono juu huku nikiwa sina wasi wasi kama wenzangu. Angalau mimi nilikuwa naelewa kidogo maswala hayo kuliko wenzangu ambao ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kukutana nayo.

"nani anaitwa Sospiter Muhinga kati yenu?". Moja kati ya Wanaume wale akatuuliza huku wakiongeza umakini zaidi juu yetu.

Hili lilikuwa ni jina langu ambalo nililitumia pote kwenye utambulisho wangu. Hivyo kusikia wanaume wale wakiliita jina langu kwa ufasaha kabisa nikashtuka. Huku hisia mbaya zikijengeka kwenye fikra zangu.

"Sospiter Muhinga ni nani kati yenu?". Mwanaume yule akarudia tena huku awamu hii akitoa sauti ya kuamrisha.

Haraka nikajibu. "mimi hapa boss".

"sogea pembeni mikono yako ikiwa juu!!". Akaongea huku sasa umakini ukiongezeka kwa watu wale huku midomo yote ya bunduki ikinilenga na wakanizunguka.

Japo sikuwa mtaalamu maswala ya kiusalama lakini nilihisi hatari inayonikabili huku nikiwa sina namna ya kujitetea. Kingine kibaya zaidi nilikuwa sijui wale ni wakina nani na wanataka nini kwangu. Haraka wakanisogelea huku wakiwa makini mno na kuanza kunikagua mwili mzima. Bado sikuelewa kile ni nini kwani mpaka wakati huo nilikuwa gizani nisielewe lolote lile.

Walipomaliza ukaguzi wao uliochukua dakika moja wakakunja mikono yangu iliyokuwa juu kutii amri yao. Kuigeuza kwa nyuma huku nikiwa bado kwenye tahamaki bwana yule akachukua pingu na kisha kuivalisha mikono yangu.

Sikutaka kuwa mbishi kwani niliijua saikolojia ya askari kama nilivyokwambia awali. Kuwa hawependi kuonekana wamekosea huku wewe ukiwa sahihi. Baada ya kumaliza zoezi hilo bado walionesha umakini wa hali ya juu kwangu kwa sababu ambazo sikuzielewa sababu tayari nilikuwa kwenye udhibiti wao.

Wakati wananingiza kwenye gari nikajikaza na kuuliza. "boss kuna tatizo gani?". Lakini hakuna aliyeonesha nia ya kunijibu swali langu licha ya kutumia sauti ambayo kila mmoja aliisikia.

Msobe msobe wakaniingiza kwenye gari yao huku maswali lukuki yakinitafuna kwenye kichwa changu. Kama vile hawa ni kina nani?, wanataka nini kwangu? na mengine mengi yaliendelea kuzunguka akilini mwangu pasipo majibu yoyote.

Kati ya yote sikuruhusu akili yangu kuchanganyikiwa juu ya hali hiyo ambayo imenikumba. Niliamini kwenye kutuliza akili hili niweze kutambua ni nini ambacho kinanikabili.

Watu wale wakanivika soksi kichwani mwangu ambayo ikaondoa uwezo wangu wa kuona. Kisha nikahisi kitu kikonichoma ambapo kwa kuhisi ncha yake nikafahamu kuwa ilikuwa sindano. Baada ya kuchomwa na sindano ile nilihisi mwili wangu ukiwa mzito ghafla kisha nikapoteza fahamu.

INAENDELEA......

Kwa maoni na ushauri nifuate kwenye mitandao ya kijamii kama:-
Fb:- falsafa70
Insta:- falsafa70
Twitter:- falsafa70

falsafa70_1650054375363419.jpg
 
Habari wapendwa, sikukuu ya pasaka ilikuwaje?. Jumatatu ya pasaka na siku njema ya kuendelea na riwaya yetu pendwa ya HATIA.

Muandishi:- Joseph .D. Migini
Call/txt:- +255766604683
Josephdeo70@gmail.com

********

Wakati naanza kuandika sikuwa na sababu sahihi za kwanini nina yaandika haya. Ila Sasa ninazo sababu na sio kwamba ni sahihi bali zenye mashiko. Kwani ukiniuliza Sasa kwanini nayaandika haya ambayo yalistahili kuwa siri nitakujibu ya kuwa.

Kila nikimtizama binti yangu Tina ambaye wakati huu anayo miezi miwili toka awepo duniani. Siku moja atakuja kuwa mkubwa Kisha kuyasoma haya ili afahamu asili ya jina lake Tina. Pia afahamu ni maswahibu gani yalitupata Mimi na mama yake. Ili atakapo muona mjomba wake Joh atambue ujasiri wake aliotuonesha sisi wazazi wake. Hatari na misukosuko yote tuliyokutana nayo wakati wa heka heka hizi.

Kwani pengine nikisubiri nije kumuelezea kwa mdomo nitasahau. Au sita muelezea kama itakavyotakiwa hivyo kuyaandika ni njia nzuri ya kuyatunza ili yaje kumfikia huku nikiyathibitisha kwa kinywa changu kwake.

***
Tuendelee sasa tulipoishia.

Ufahamu uliporejea tena kwenye mwili wangu nilijihisi niko ovyo sana tofauti na awali. Uchovu ulikuwa ndani ya mwili wangu na hapo nikajiweka sawa kisha kujikumbusha ni kipi kilinisibu kabla sijapoteza fahamu. Lakini kabla sijafanya hivyo macho yangu yakavutiwa na mazingira haya mapya ambayo nilikuwa, ilikuwa ni tofauti na kwenye gari. Ama Maisome kwenye barabara iliyojaa vumbi bali kwenye chumba safi kilichopakawa rangi ya kijani chini na nyeupe juu. Huku mlangoni kukiwa na kamera ambayo ilifiatilia kila lililokuwa likiendelea ndani ya chumba kile.

Mazingira haya mapya yalifanya woga zaidi mwilini mwangu tofauti na mwanzo kwani sikuwa nafahamu wapi nilipo na dhamira ya watu wale kwangu. Nikajikaza kisha nikanyanyuka na kuelekea mlangoni na kuanza kugonga ili kama kuna mtu karibu basi aweze kunipa msaada. Kutekwa ndio wazo pekee ambalo lilikuwa likishambulia akili yangu huku mtekelezaji wake wala dhamira ya kutekwa nikiwa bado sihifahamu.

Mara nyingi nilikuwa nikizisoma stori za watu kupotezwa na watu wasiojulikana. Stori hizo zilikuwa maarufu mno nchini kwani ziliwakumba mpaka wasanii maarufu. Mimi pia nikawa kwenye hali hiyo ya kuhisi nilichukuliwa na watu wasio julikana.

Kelele zangu za kugonga mlango ule wa chuma hazikusaidia lolote kwani ni kama eneo lile nilikuwa mwenyewe. Mapigo ya moyo yalianza kukimbia nje ya mpangilio wake wa kila siku huku taharuki ikiwa ndani yangu. Utulivu ulikuwa umepotea kabisa ndani ya akili mpaka mwili. Lakini nikakumbuka kuwa sikutakiwa kuwa kwenye hali hiyo kwa sababu ingeniondolewa usanifu akili yangu.

Elimu ndogo juu ya saikolojia ambayo niliipata wakati nachukua shahada ya ualimu katika chuo kikuu cha mtakatifu Agustino, Mwanza. Ilinifahamisha kuwa taharuki huondoa ufanisi wa akili hivyo ilinibidi kuurudisha utulivu.

Nikavuta pumzi nyingi kwa nguvu kisha kuzitoa kwa taratibu taratibu na kwa mafungu. Hii ikasaidia kwa kiasi fulani akili yangu kuwa kwenye utulivu ambao niliuhitaji. Wakati nimetulia mlango ule ambao nilikuwa nikiupiga dakika kadhaa nyuma ukafunguka.

Akaingia mwanaume mmoja mwenye makamo ya miaka thalathini na mbili. Ambaye alikuwa mrefu wa kimo mwenye kufika futi sita na nchi mbili huku umbile lake likionesha kuwa limejengeka kimazoezi na rangi yake ya maji ya kunde.

Nyuma yake kulikuwa mwanaume aliyeshikiria viti viwili. Huyu sikujishughulisha naye kwani alionesha kila dalili ya kuwa kibaraka wa bwana yule aliyekuwa ndani ya suti nadhifu. Bwana yule mwingine akaweka viti na mimi pamoja na bwana yule tukakaa kwenye viti vile.

Akatabasamu nami nikamjibu kwa tabasam kisha akaliita jina langu kwa ufasaha kama walivyofanya wale wanaume walionileta hapo. Nami nikaitikia kisha akanikabidhi picha mbili ambazo nikaishia kuzitazama tu nisielewe chochote.

Kisha bwana yule akafukuza ukimya kwa kuniuliza. "wako wapi hawa?". Kabla sijajibu akaongeza swali lingine. "je, wako salama mpaka sasa!!". Sauti yake ilikuwa nene na aliongea taratibu.

Sikuwa naelewa kile alichokuwa akikisema na niliona kama vile ananiongezea mzigo mzito tofauti na ule ambao nilikuwa nao. Awali wa kutaka kufahamu kwanini watu wale wanichukue kunileta pale.

"sikuelewi kaka, kwani hawa ni kina nani?". Ili kuelewa kinachonikabili na ukubwa wake ikanibidi kuuliza.

Huku akitabasamu akanitazama kwa tambo kisha akaongea. "yaani watu uwashikirie wewe alafu uwaulize wengine?. Au waliokupa kazi hawakukueleza vyema!!".

Bwana yule alizidi kuichanganya akili yangu kwa namna alivyonielezea. Sikuwa nawafahamu watu wale na hata nilipo ilazimisha akili yangu kuniambia kama nawafahu au hata nilishawahi kuwaona bado ilinikatalia kabisa na kunipa taarifa kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwaona pale.

"pengine sasa unaweza usiwe na majibu. Nakuacha ila nikirudi ni vyema ukanieleza kwa sababu hatuna mda wa kutosha juu ya hilo!". Alipokwisha kusema hayo akanyanyuka na kuanza kuondoka nami sikujishughulisha naye bali macho yangu yalisalia kwenye picha zile.

Mlio wa kufungwa kwa mlango ukafanya nitizame sehemu ambayo mlango huo upo na baadae nikarudisha macho yangu kwenye picha. Hapo nikapata majibu ambayo mwanzo sikuwa nayo, majibu hayo yalikuwa ni watu wale kwenye picha wana uhusiano wa moja kwa moja. Na inawezekana ikawa ni mtu na dada yake au mama na mwana. Hii ilitokana na kuendana hasa kwenye maeneo ya uso na upishano wa umri wao.

Nilipoligundua hilo nikairudisha akili yangu kwenye jambo ambalo natuhumiwa nalo juu ya watu wale. Ambao kiuhalisia sikuwa najua lolote lile kuwahusu. Nikawaza hata kama nikisema nidanganye isingesaidia kwa sababu ili uongo wako ukubalike au uaminike ni lazima uukaribie ukweli kwa asilimia kadhaa. Nami sikuwa naujua ukweli wowote kuwahusu watu wale ni vipi ningeweza kudanganya?.

Wakati niko kwenye lindi la mawazo mlango ule ukafunguliwa na ulikuwa na sauti kubwa wakati wa kufunguliwa na kufungwa kwake kiasi cha kukufanya utizame ulipo. Akaingia mwanamke ambaye hakunipa kazi kutambua kuwa alikuwa mpishi na mkononi alikuwa sahani lililosheheni wali na maharage pamoja na maji ya kunywa. Akakalisha na kutoka kisha mlango ukafungwa nami nikatumia mda huo kukila chakula kile pamoja na kunywa maji yale.

Nilipomaliza kula chakula kile mlango ukafunguka nami nikatupa macho yangu kuelekea mlangoni. Nikaomuona bwana yule aliyekuwa akinihoji mara ya kwanza na awamu hii aliongozana na wanaume wengine wawili na kufanya idadi yao kuwa watatu huku idadi ya watu tuliokuwa kwenye chumba kile kuwa wanne. Mkononi mwa bwana yule alikuwa na begi ambalo sikujua lilikuwa la kazi gani. Ila nilijipa utulivu ili kufahamu kazi yake kwa sababu wanasema mda utoa majibu muafaka nami nilikuwa muumini mzuri wa hilo.

Walipofika usawa nilipo bwana yule akakaa kwenye kiti kile huku wale alioingia nao wakisalia kusimama. Akafungua ndani ya begi lile na kutoa mfuko wa naironi ulikuwa mweupe hivyo ukanipa nafasi ya kuona vilivyo ndani. Japo hakukuwa na taswira nzuri ya kuwezesha kuona vyema vilivyo ndani ila niliona vitu kadhaa.

Bwana yule akatoa kitambulisho changu cha mpiga kura akanipatia na kuniuliza. "huyu ni nani?"

Nami nikamjibu huku nikikitazama kwani aliruhusu kukishika. "mimi. Lakini sina hicho kitambulisho toka miaka miwili nyuma na taarifa zangu ziko polisi". Jibu langu lilifanya anitazame kisha akaingiza mkono tena kwenye mfuko ule na kutoa bastola.

"ilinunuliwa na mnunuzi ni huyu hapa". Alitoa karatasi ambayo ilikuwa na picha yangu ya pasipoti kulia juu kisha jina langu na maelezo mengine ambayo sikuyasoma.

Kisha akaendelea "mnunuaji wa hii ni wewe na ilikutwa eneo la tukio". Bado sikujua tukio hilo lilikuwa ni lipi linalonikabili.

"nimeona maelezo yote yaliyotumika ni ya kwenye kitambulisho changu cha mpiga kura na nimekwisha kwambia kuwa sikuwa na kitambulisho hicho. Na tarehe zinaonesha kuwa ni mwaka uliopita ina maana hakikuwa kwenye umiliki wangu!". Akanitazama kama mtu ambaye najifanya mjuaji huku wanavyo vitu vingine vingi kwenye tuhuma hizo.

Akatoa kitambaa kilichokuwa na damu ambayo ilikuwa imekauka kisha akatoa picha ambayo ilionesha kitambaa hicho kilipokutwa. Nikatahamaki kwani picha ile ilionesha mazingira ya chumba changu nilichopanga maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza.

Kabla hata sijatoka kwenye mshangao bwana yule akaniambia.
"hichi ni kitambaa cha mke wa waziri mkuu ambacho kilikutwa kwako. Inaonesha kuwa mke wa waziri mkuu na mwanae walikuwa hapo kabla ya kuondoshwa na kupelekwa mafichoni ambapo sisi sasa tuanataka wewe utueleze ni wapi?". Akamaliza kwa kuweka msisitizo.
Mshituko wa dhahiri ukanikamata na hapo nikajua hatia rasmi zinazonikabili. Kumteka mke wa kiongozi mkubwa nchini ambaye analindwa na ulinzi mkali. Kitu ambacho sikuelewa ni kuwa kwanini watu wale waamini kuwa mimi ndie nimehusika wakati hata sikwenda kucheza mgambo zaidi ya mafunzo ya miezi mitatu ya lazima ya JKT baada ya kumaliza kidato cha sita.

"miezi sita iliyopita nilikiacha chumba changu na kuelekea Maisome, sehemu ambayo watu wako walinikuta. Hivyo yaliokuwa yanendelea kilipochumba changu sikuwa naelewa chochote na mama mwenye nyumba wangu analifahamu hilo". Nikaitimisha kwa kumuangalia bwana yule kwa jicho ambalo lilimaanisha kuwa hawakuwa na weledi wa kutosha juu ya walichokuwa wakikifanya.

"sawa pengine na hii unaweza kuwa na kisingizio pia". Akatoa picha ambayo ilinanaswa na kamera za ulinzi picha hiyo ilimuonesha mtu ambaye mwanzoni nilidhani kuwa alikuwa kavaa nguo ambazo zilifanana na zangu.

Lakini nilithibitisha kuwa zilikuwa zangu baada ya kuona tobo kwenye suruali ambalo mimi mwenyewe nililisababisha kwa kuunguza suruali hiyo wakati nikiionyoosha kwa pasi.
Ila sikuwa mimi wala hakuna hata picha moja kati ya hizo nne ambazo zilionesha sura ya mtu yule.

"huyo anawezaje kuwa mimi ikiwa hakuna hata picha ambayo inaonesha sura yake?". Swali langu likamfanya bwana yule kutengeneza suti yake vyema kisha akaniambia.

"unafikiri wewe ni mjinga kiasi hicho!!!". Kisha akacheka na kunitizama vyema huku akiniambia. "kuingia na kuondoka kwenye nyumba yenye ulinzi wa juu unategemewa utanaswa na CCTV kweli!". Akaendelea kucheka kama aliyoyaongea yanafurahisha. "kweli unafurahisha kaka!".

"mbona sikuelewi kiongozi". Nikaongea huku nikioneshwa kushangazwa na kile alichokuwa akikisema.

"utaelewa tu sababu ni wengi wanaokuja hapa wanakuwa kama wewe mwanzoni ila mwishoni akili inawakaa sawa sawa na kutueleza". Akaingiza tena mkono wake kwenye mfuko ule na kutoa kitu ambacho ilikuwa mara yangu ya kwanza kukiona.

"hii ndio imefanya sisi kufika kwako ni GPRS ambayo ilikuwa kwenye mwili wa mama. Na bahati nzuri ni kuwa ulipoitoa ukaisahau kwako na wewe kukimbilia huko unapopaita Maisome sio!!?. Mshangao wa dhahiri ukanivaa huku mwili sasa ukipoteza uhimili wa ujasiri.

"nadhani walinao niframe hii kesi wamejipanga sana na bahati iliyo mbaya hata nyinyi mmeingia kwenye mtego huo". Nikamwambia bwana yule aliyeendelea kunionesha tabasamu pana kwenye sura yake.

"vizuri kama unaweza kutufundisha kile tulichokuwa na taaluma nacho, na hiyo ni kwa sababu wewe ni bora kutuliko. Kama uliweza kumchukua na kumficha tusipoweza kumuona basi uko vizuri kushindana na idara". Kauli yake ikanifanya kuwa nifahamu watu wanao nishikilia nao ni idara ya usalama wa taifa.

Japo sikuwa na uhakika wa moja kwa moja. Ila idara ya usalama wa taifa ndio ilikuwa ikihusishwa na kuwashikiria watu kwa stahili ambayo mimi nimeshikiriwa.

"ningependa kuwa kama ulivyosema lakini trust me bro sijafanya, na siwezi kufanya chochote kile kibaya".

"sawa, vipi kuhusu hii". Alitoa picha ambayo ilinionesha niko nazungumza na watu fulani ambao hawakuwa wanaonekana kwani picha ile iliwapiga wakiwa wamempa mgongo mpigaji.

"inahusiana na nini hii?". Nikamuuliza kwani nilikuwa nakumbuka kuwa watu wale ndio walinipa taarifa ambazo ndio zilinifanya nami nikaingia kwenye kilimo.

Siku ambayo picha hii ilipigwa ilikuwa siku ya kawaida tu ambapo nilitoka nyumbani na kwenda shule ya msingi kitangiri mahali ambapo ndipo kibarua changu kilikuwa. Nilifika shuleni hapo na kuingia kwenye kipindi cha hesabu darasa la nne. Nilipotoka kwenye kipindi nikaenda kupata kifungua kinywa kwenye ofisi ya waalimu. Baada ya hapo ndipo walipokuja watu wale ambao sikuwa nawafahamu ila nilivutiwa na namna walivyokuwa wakizungumza kuhusu fursa za kilimo.

Watu wale walijitambulisha kama SHAMBA HURIA COMPANY walijinasibu kuwa ni wanunuzi wa mazao kwa bei shindani. Watu wale walitoa miongozo mingi katika kilimo huku wakiwa na ushahidi kadhaa za watu waliofanikiwa kwenye kilimo na wale walioshindwa.

Huku wakitupa sababu nyingi za kwanini kama waajiliwa tuwekeze kwenye kilimo kwani mnunuzi wa mazao ambayo tutalima wapo na wananunua kwa bei shindani sokoni.
Ili likanivutia zaidi na hapo ndipo nikaomba kuongea na watu wale pembeni na huo ndio wakati ambao picha ile ilipigwa.

Kwani nilikuwa na watu wanne kutoka kwenye kampuni hiyo na tulisogea pembeni kabisa na jengo la shule na mazingira ya kwenye picha hiyo yalionesha vile. Sasa ikiwa tulikuwa tukiongea habari za kilimo kwanini picha ile ije kutumika kwenye tuhuma za kupotea kwa mke wa waziri mkuu?.

Hili swali likanifanya nirudishe mawazo yangu pale ambapo nikakumbuka kuwa kulikuwa na picha mikononi mwangu ambapo niliulizwa swali. "hawa ni jamaa ambao walinishawishi kuingia kwenye kilimo kwa sera zao. Nashangaa kuona picha hii leo wakati tukio hilo lina zaidi ya miezi sita sasa!".

Bwana yule akatabasamu kidogo kisha akatoa picha nyingine ambayo iliwaonesha watu wale wale. Wakiwa sehemu nyingine ambayo ilikuwa ni kama yenye usiri na picha ile ilionesha kuwa watu wale walikuwa wakijadiliana jambo. Kisha akatoa picha nyingine tena ikiwaonesha watu wengine kabisa lakini kati ya hao wawili walikuwa ni wale ambao nimekwisha kuwaona ila bado sikuelewa kwanini nioneshwe zile picha na zina uhusiano gani na hatia zangu.

INAENDELEA......

Kwa maoni na ushauri nifuate kwenye mitandao ya kijamii kama:-
Fb:- falsafa70
Insta:- falsafa70
Twitter:- falsafa70.
Asanteni!!!
 
Muandishi:- Joseph .D. Migini
Call/txt:- +255766604683
Josephdeo70@gmail.com

Ndani ya chumba hichi cha wastani kilichoja samani za kufanya kuitwa sebule ya kisasa kwa waingiao. Nilikuwa nimeketi kijana Mimi umri wa miaka thalathini na mbili toka niwepo kwenye ulimwengu huu. Binafsi haiba yangu ni mtu mtaratibu hata nisipende Shari na yeyote.

Majira haya ya asbuhi nilikuwa nikipata kahawa iliyotayarishwa na mke wangu Brenda. Huku hisia za mawazo yangu zikiwa mbali na ulipo mwili wangu. Hata sikuweza kusikia kilio cha binti yangu wa miezi miwili niliyekuwa nimembeba mikononi mwangu.

Hisia hizi zilikuwa zimenichukua na kunirudisha nyuma. Kwa kadri ya miaka mitatu na kunikumbusha ni vitu gani nilipitia katika kipindi hicho. Mawazo mengi yalikuwa ni juu ya kuweka visa na mikasa hiyo kwa njia ya maandishi. Japo sio muandishi mahiri au mashuhuri lakini naweza kuyaelezea vyema haya yaliyonikumba kwa njia hiyo.

Sasa sina jibu la moja kwa moja juu ya sababu inayofanya kuyaandika haya. Zaidi ya nafsi yangu kunisukuma kufanya hivyo. Nilisogea mahali ambapo nahifadhi tarakishishi yangu ili niweze kutimiza haja hizi za moyo wangu.

Maisha yamekuwa fumbo gumu kulipatia ufumbuzi. Unaweza kudhani kuwa maisha yako binafsi yapo chini ya udhibiti wako na Mwenyezi Mungu kumbe hapana!. Bali maisha yako yanatengenezewa njia na binadamu wenzio.

Wapi upite, wapi ukanyage na wapi huruke yote hayo wanadamu wenzio ndio wanakutengenezea. Na mwisho kabisa waamua kuwa uwe wapi na nini kiwe hitimisho lako.

Nami nilikuwa kama wewe hapo unayesoma. Nilikuwa kama wewe kwa kudhani kuwa maisha yangu yapo kwenye udhibiti wangu na Mungu pekee. Mpaka pale yaliponikuta yale ambayo sikuyapanga wala kuyatenda mimi mwenyewe ila yalikuja kuhusu mimi.

Kama bado ujaelewa ninachokisema fuatana nami kwenye mkasa huu.

Nafikiri hii si namna nzuri, bora au pengine ya kufurahisha katika kuanza uandishi wangu. Je, mimi nimeonewa?, Lakini kabla ya kuwapa jibu hilo mnaweza kunijibu uonevu ni nini?. Hakika Mimi sijui ila naweza kuyaelezea yale yaliyo nikuta kisha wewe msomaji ndio unipe majibu kama nilionewa au la!.

INAENDELEA....
Unakaribishwa kwa maoni na ushauri. Asante!!
IMG_20220705_194525_347.jpg
 
Muandishi:- Joseph .D. Migini

Call/txt:- +255766604683

Josephdeo70@gmail.com

#02

Maisha yangu yote nimeishi nikiwa na ndoto ya kuwa mwalimu ili niinufaishe jamii iliyonizunguka kwa maarifa yangu. Lakini nilicholipwa ndio imebaki kama kovu moyoni mwangu. Nakumbuka vizuri sana, nakumbuka kila kitu kwa sababu hata ingekuwa vipi nisingeweza kuja kusahau hichi nilicho kipitia. Siwezi kabisa labda niwe mfu.

Nilikuwa mimi pamoja na watu wawili ambao nilikuwa nimewapatia kibarua cha kunilimia shamba langu. Tukiwa tunatoka shambani huku tukiwa kwenye barabara kuu ya kisiwa cha Maisome sehemu ambayo niliamua nifanye biashara ya kilimo. Siku hiyo tulipishana na gari tatu. Ilikuwa ni nadra sana kuliona gari ndani ya kisiwa kile. Achana na gari za kifahari kama hizo zilizotupita kwa kasi.

Nami nikaungana na wanakijiji wengine kushangaa hali ile ngeni sehemu ile iliyo na umasikini wa kutupa. Huku miundo mbinu ikiwa imezorota kiasi cha kufanya umasikini uote mizizi.

Walitupita kwa kasi sana na walipoondoka kwenye upeo wa macho yetu sisi tukaendelea na simulizi zetu zilizokuwa zimekatizwa na kupita kwa magari yale.

Umbali wa kutoka eneo nililokuwa nikiishi mpaka shambani ilikuwa inachukua hadi saa moja kwa mwendo wa haraka haraka na mwendo wa taratibu ilikuwa inachukua saa moja na nusu. Hivyo tulikuwa tunatembea haraka haraka wakati wa asbuhi wakati ambao tulikuwa tukienda shambani na wakati wa kurudi tulitembea taratibu taratibu.

Tukiwa njiani mara tukaona zile gari zikirudi na zilipofika usawa ambao tulikuwa mimi na wale wenzangu zikafunga breki za ghafla. Sisi tulikuwa kando ya barabara na tuliweza kulishuhudia hilo vyema. Baada ya kufanikiwa kuzishika breki na gari hizo kusimama wakatoka wanaume kumi kwa idadi yao huku wote wakituelekezea bunduki zao.

Sikuwa mtaalamu wa maswala ya intelijensia ila nilikuwa nimesoma baadhi ya simulizi kadhaa zilizokuwa zinaongelea mambo hayo. Huku pia nikiwa nimetazama filamu nyingi zilizokuwa zinaelezea dhahiri maswala ya kijasusi. Kwa elimu yangu ndogo eneo hilo ikanipa taarifa ya kutofanya chochote kile huku panga ambalo lilikuwa mkononi mwangu likianguka chini.

INAENDELEA….

Unakaribishwa kwa maoni na ushauri.
IMG_20220705_194525_347.jpg
 
Muandishi:- Joseph .D. Migini

Call/txt:- +255766604683

Josephdeo70@gmail.com

#03

"weka mikono yenu juu!!". Mmoja kati ya wale wanaume akaamrisha nami nikawa wakwanza kutii.

Katika uelewa wangu mdogo nilielewa vyema saikolojia ya askari kuwa mara zote ujiona anayo mamlaka juu yako. Na yuko juu yako kimaamuzi hivyo haipaswi kumkosoa wala kuonekana wewe huko sahihi huku yeye akiwa kakosea. Hivyo jambo moja muhimu kuwahusu ni kwenda sawa sawa na wanavyotaka. Wote tukanyoosha mikono juu huku nikiwa sina wasi wasi kama wenzangu. Angalau mimi nilikuwa naelewa kidogo maswala hayo kuliko wenzangu ambao ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kukutana nayo.

"nani anaitwa Sospiter Muhinga kati yenu?". Moja kati ya Wanaume wale akatuuliza huku wakiongeza umakini zaidi juu yetu.

Hili lilikuwa ni jina langu ambalo nililitumia pote kwenye utambulisho wangu. Hivyo kusikia wanaume wale wakiliita jina langu kwa ufasaha kabisa nikashtuka. Huku hisia mbaya zikijengeka kwenye fikra zangu.

"Sospiter Muhinga ni nani kati yenu?". Mwanaume yule akarudia tena huku awamu hii akitoa sauti ya kuamrisha.

Haraka nikajibu. "mimi hapa boss".

"sogea pembeni mikono yako ikiwa juu!!". Akaongea huku sasa umakini ukiongezeka kwa watu wale huku midomo yote ya bunduki ikinilenga na wakanizunguka.

Japo sikuwa mtaalamu maswala ya kiusalama lakini nilihisi hatari inayonikabili huku nikiwa sina namna ya kujitetea. Kingine kibaya zaidi nilikuwa sijui wale ni wakina nani na wanataka nini kwangu. Haraka wakanisogelea huku wakiwa makini mno na kuanza kunikagua mwili mzima. Bado sikuelewa kile ni nini kwani mpaka wakati huo nilikuwa gizani nisielewe lolote lile.

Walipomaliza ukaguzi wao uliochukua dakika moja wakakunja mikono yangu iliyokuwa juu kutii amri yao. Kuigeuza kwa nyuma huku nikiwa bado kwenye tahamaki bwana yule akachukua pingu na kisha kuivalisha mikono yangu.

INAENDELEA….

Unakaribishwa kwa maoni na ushauri.
 
Muandishi:- Joseph .D. Migini

Call/txt:- +255766604683

Josephdeo70@gmail.com

#04

Sikutaka kuwa mbishi kwani niliijua saikolojia ya askari kama nilivyokwambia awali. Kuwa hawependi kuonekana wamekosea huku wewe ukiwa sahihi. Baada ya kumaliza zoezi hilo bado walionesha umakini wa hali ya juu kwangu kwa sababu ambazo sikuzielewa kwani tayari nilikuwa kwenye udhibiti wao.

Wakati wananingiza kwenye gari nikajikaza na kuuliza. "boss kuna tatizo gani!!?". Lakini hakuna aliyeonesha nia ya kunijibu swali langu licha ya kutumia sauti ambayo kila mmoja aliisikia.

Msobe msobe wakaniingiza kwenye gari yao huku maswali lukuki yakinitafuna kwenye kichwa changu. Kama vile hawa ni kina nani?, wanataka nini kwangu? na mengine mengi yaliendelea kuzunguka akilini mwangu pasipo majibu yoyote.

Kati ya yote sikuruhusu akili yangu kuchanganyikiwa juu ya hali hiyo ambayo imenikumba. Niliamini kwenye kutuliza akili hili niweze kutambua ni nini ambacho kinanikabili.

Nikiwa bado kwenye tahamaki na maswali kede kede. Watu wale wakanivika soksi kichwani mwangu ambayo ikaondoa uwezo wangu wa kuona. Kisha nikahisi kitu kikonichoma ambapo kwa kuhisi ncha yake nikafahamu kuwa ilikuwa sindano. Baada ya kuchomwa na sindano ile nilihisi mwili wangu ukiwa mzito ghafla kisha nikapoteza fahamu.

INAENDELEA….

Unakaribishwa kwa maoni na ushauri.
IMG_20220705_194525_347.jpg
 
Muandishi:- Joseph .D. Migini

Call/txt:- +255766604683

Josephdeo70@gmail.com

#05

Wakati naanza kuandika sikuwa na sababu sahihi za kwanini nina yaandika haya. Ila Sasa ninazo sababu na sio kwamba ni sahihi bali zenye mashiko. Kwani ukiniuliza Sasa kwanini nayaandika haya ambayo yalistahili kuwa siri nitakujibu ya kuwa.

Kila nikimtizama binti yangu Tina ambaye wakati huu anayo miezi miwili toka awepo duniani. Siku moja atakuja kuwa mkubwa Kisha kuyasoma haya ili afahamu asili ya jina lake Tina. Pia afahamu ni maswahibu gani yalitupata Mimi na mama yake. Ili atakapo muona mjomba wake Joh atambue ujasiri wake aliotuonesha sisi wazazi wake. Hatari na misukosuko yote tuliyokutana nayo wakati wa heka heka hizi.

Kwani pengine nikisubiri nije kumuelezea kwa mdomo nitasahau. Au sita muelezea kama itakavyotakiwa hivyo kuyaandika ni njia nzuri ya kuyatunza ili yaje kumfikia huku nikiyathibitisha kwa kinywa changu kwake.

***

Ufahamu uliporejea tena kwenye mwili wangu nilijihisi niko ovyo sana tofauti na awali. Uchovu ulikuwa ndani ya mwili wangu na hapo nikajiweka sawa kisha kujikumbusha ni kipi kilinisibu kabla sijapoteza fahamu. Lakini kabla sijafanya hivyo macho yangu yakavutiwa na mazingira haya mapya ambayo nilikuwa, ilikuwa ni tofauti na kwenye gari. Ama Maisome kwenye barabara iliyojaa vumbi bali kwenye chumba safi kilichopakawa rangi ya kijani chini na nyeupe juu. Huku mlangoni kukiwa na kamera ambayo ilifuatilia kila lililokuwa likiendelea ndani ya chumba kile.

Mazingira haya mapya yalifanya woga zaidi mwilini mwangu tofauti na mwanzo kwani sikuwa nafahamu wapi nilipo na dhamira ya watu wale kwangu. Nikajikaza kisha nikanyanyuka na kuelekea mlangoni kisha kuanza kugonga ili kama kuna mtu karibu basi aweze kunipa msaada. Kutekwa ndio wazo pekee ambalo lilikuwa likishambulia akili yangu huku mtekelezaji wake wala dhamira ya kutekwa nikiwa bado sihifahamu.

Mara nyingi nilikuwa nikizisoma stori za watu kupotezwa na watu wasiojulikana. Stori hizo zilikuwa maarufu mno nchini kwani ziliwahusisha mpaka watu maarufu. Mimi pia nikawa kwenye hali hiyo ya kuhisi nilichukuliwa na watu wasio julikana.

INAENDELEA….

Unakaribishwa kwa maoni na ushauri.
 
Muandishi:- Joseph .D. Migini

Call/txt:- +255766604683

Josephdeo70@gmail.com

#06

Kelele zangu za kugonga mlango ule wa chuma hazikusaidia lolote kwani ni kama eneo lile nilikuwa mwenyewe. Mapigo ya moyo yalianza kukimbia nje ya mpangilio wake wa kila siku huku taharuki ikiwa ndani yangu. Utulivu ulikuwa umepotea kabisa ndani ya akili mpaka mwili. Lakini nikakumbuka kuwa sikutakiwa kuwa kwenye hali hiyo kwa sababu ingeniondolewa usanifu akili yangu.

Elimu ndogo juu ya saikolojia ambayo niliipata wakati nachukua shahada ya ualimu katika chuo kikuu cha mtakatifu Agustino, Mwanza. Ilinifahamisha kuwa taharuki huondoa ufanisi wa akili hivyo ilinibidi kuurudisha utulivu.

Nikavuta pumzi nyingi kwa nguvu kisha kuzitoa kwa taratibu taratibu na kwa mafungu. Hii ikasaidia kwa kiasi fulani akili yangu kuwa kwenye utulivu ambao niliuhitaji. Wakati nimetulia mlango ule ambao nilikuwa nikiupiga dakika kadhaa nyuma ukafunguka.

Akaingia mwanaume mmoja mwenye makamo ya miaka thalathini na mbili. Ambaye alikuwa mrefu wa kimo mwenye kufika futi sita na nchi mbili huku umbile lake likionesha kuwa limejengeka kimazoezi na rangi yake ya maji ya kunde.

Nyuma yake kulikuwa mwanaume aliyeshikiria viti viwili. Huyu sikujishughulisha naye kwani alionesha kila dalili ya kuwa kibaraka wa bwana yule aliyekuwa ndani ya suti nadhifu. Bwana yule mwingine akaweka viti na mimi pamoja na bwana yule tukakaa kwenye viti vile.

Akatabasamu nami nikamjibu kwa tabasam kisha akaliita jina langu kwa ufasaha kama walivyofanya wale wanaume walionileta hapo. Nami nikaitikia kisha akanikabidhi picha mbili ambazo nikaishia kuzitazama tu nisielewe chochote.

INAENDELEA….

Unakaribishwa kwa maoni na ushauri.
 
Muandishi:- Joseph .D. Migini

Call/txt:- +255766604683

Josephdeo70@gmail.com

#07

Kisha bwana yule akafukuza ukimya kwa kuniuliza. "wako wapi hawa?". Kabla sijajibu akaongeza swali lingine. "je, wako salama mpaka sasa!!". Sauti yake ilikuwa nene na aliongea taratibu.

Sikuwa naelewa kile alichokuwa akikisema na niliona kama vile ananiongezea mzigo mzito tofauti na ule ambao nilikuwa nao. Awali wa kutaka kufahamu kwanini watu wale wanichukue kunileta pale.

"sikuelewi kaka, kwani hawa ni kina nani?". Ili kuelewa kinachonikabili na ukubwa wake ikanibidi kuuliza.

Huku akitabasamu akanitazama kwa tambo kisha akaongea. "yaani watu uwashikilie wewe alafu uwaulize wengine?. Au waliokupa kazi hawakukueleza vyema!!".

Bwana yule alizidi kuichanganya akili yangu kwa namna alivyonielezea. Sikuwa nawafahamu watu wale na hata nilipo ilazimisha akili yangu kuniambia kama nawafahu au hata nilishawahi kuwaona bado ilinikatalia kabisa na kunipa taarifa kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwaona pale.

"pengine sasa unaweza usiwe na majibu. Nakuacha ila nikirudi ni vyema ukanieleza kwa sababu hatuna mda wa kutosha juu ya hilo!". Alipokwisha kusema hayo akanyanyuka na kuanza kuondoka nami sikujishughulisha naye bali macho yangu yalisalia kwenye picha zile.

Mlio wa kufungwa kwa mlango ukafanya nitizame sehemu ambayo mlango huo upo na baadae nikarudisha macho yangu kwenye picha. Hapo nikapata majibu ambayo mwanzo sikuwa nayo, majibu hayo yalikuwa ni watu wale kwenye picha wana uhusiano wa moja kwa moja. Na inawezekana ikawa ni mtu na dada yake au mama na mwana. Hii ilitokana na kuendana hasa kwenye maeneo ya uso na upishano wa umri wao.

INAENDELEA….

Unakaribishwa kwa maoni na ushauri.
 
Muandishi:- Joseph .D. Migini

Call/txt:- +255766604683

Josephdeo70@gmail.com

#08

Nilipoligundua hilo nikairudisha akili yangu kwenye jambo ambalo natuhumiwa nalo juu ya watu wale. Ambao kiuhalisia sikuwa najua lolote lile kuwahusu. Nikawaza hata kama nikisema nidanganye isingesaidia kwa sababu ili uongo wako ukubalike au uaminike ni lazima uukaribie ukweli kwa asilimia kadhaa. Nami sikuwa naujua ukweli wowote kuwahusu watu wale ni vipi ningeweza kudanganya?.

Wakati niko kwenye lindi la mawazo mlango ule ukafunguliwa na ulikuwa na sauti kubwa wakati wa kufunguliwa na kufungwa kwake kiasi cha kukufanya utizame ulipo. Akaingia mwanamke ambaye hakunipa kazi kutambua kuwa alikuwa mpishi na mkononi alikuwa sahani lililosheheni wali na maharage pamoja na maji ya kunywa. Akakalisha na kutoka kisha mlango ukafungwa nami nikatumia mda huo kukila chakula kile pamoja na kunywa maji yale.

Nilipomaliza kula chakula kile mlango ukafunguka nami nikatupa macho yangu kuelekea mlangoni. Nikaomuona bwana yule aliyekuwa akinihoji mara ya kwanza na awamu hii aliongozana na wanaume wengine wawili na kufanya idadi yao kuwa watatu huku idadi ya watu tuliokuwa kwenye chumba kile kuwa wanne. Mkononi mwa bwana yule alikuwa na begi ambalo sikujua lilikuwa la kazi gani. Ila nilijipa utulivu ili kufahamu kazi yake kwa sababu wanasema mda utoa majibu muafaka nami nilikuwa muumini mzuri wa hilo.

Walipofika usawa nilipo bwana yule akakaa kwenye kiti kile huku wale alioingia nao wakisalia kusimama. Akafungua ndani ya begi lile na kutoa mfuko wa naironi ulikuwa mweupe hivyo ukanipa nafasi ya kuona vilivyo ndani. Japo hakukuwa na taswira nzuri ya kuwezesha kuona vyema vilivyo ndani ila niliona vitu kadhaa.

Bwana yule akatoa kitambulisho changu cha mpiga kura akanipatia na kuniuliza. "huyu ni nani?".

INAENDELEA….

Unakaribishwa kwa maoni na ushauri.
 
Muandishi:- Joseph .D. Migini

Call/txt:- +255766604683

Josephdeo70@gmail.com

#09

Nami nikamjibu huku nikikitazama kwani aliruhusu kukishika. "mimi!!, Lakini sina hicho kitambulisho toka miaka miwili nyuma na taarifa zangu ziko polisi". Jibu langu lilifanya anitazame kisha akaingiza mkono tena kwenye mfuko ule na kutoa bastola.

"ilinunuliwa na mnunuzi ni huyu hapa". Alitoa karatasi ambayo ilikuwa na picha yangu ya pasipoti kulia juu kisha jina langu na maelezo mengine ambayo sikuyasoma.

Kisha akaendelea "mnunuaji wa hii ni wewe na ilikutwa eneo la tukio". Bado sikujua tukio hilo lilikuwa ni lipi linalonikabili.

"nimeona maelezo yote yaliyotumika ni ya kwenye kitambulisho changu cha mpiga kura na nimekwisha kwambia kuwa sikuwa na kitambulisho hicho. Na tarehe zinaonesha kuwa ni mwaka uliopita ina maana hakikuwa kwenye umiliki wangu!". Akanitazama kama mtu ambaye najifanya mjuaji huku wanavyo vitu vingine vingi kwenye tuhuma hizo.

Akatoa kitambaa kilichokuwa na damu ambayo ilikuwa imekauka kisha akatoa picha ambayo ilionesha kitambaa hicho kilipokutwa. Nikatahamaki kwani picha ile ilionesha mazingira ya chumba changu nilichopanga maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza.

Kabla hata sijatoka kwenye mshangao bwana yule akaniambia.

"hichi ni kitambaa cha mke wa waziri mkuu ambacho kilikutwa kwako. Inaonesha kuwa mke wa waziri mkuu na mwanae walikuwa hapo kabla ya kuondoshwa na kupelekwa mafichoni ambapo sisi sasa tuanataka wewe utueleze ni wapi?". Akamaliza kwa kuweka msisitizo.

Mshituko wa dhahiri ukanikamata na hapo nikajua hatia rasmi zinazonikabili. Kumteka mke wa kiongozi mkubwa nchini ambaye analindwa na ulinzi mkali.

Kitu ambacho sikuelewa ni kuwa kwanini watu wale waamini kuwa mimi ndie nimehusika wakati hata sikwenda kucheza mgambo zaidi ya mafunzo ya miezi mitatu ya lazima ya JKT baada ya kumaliza kidato cha sita.

INAENDELEA….

Unakaribishwa kwa maoni na ushauri.
 
Muandishi:- Joseph .D. Migini

Call/txt:- +255766604683

Josephdeo70@gmail.com

#10

"mbona sikuelewi kiongozi". Nikaongea huku nikioneshwa kushangazwa na kile alichokuwa akikisema.

"utaelewa tu sababu ni wengi wanaokuja hapa wanakuwa kama wewe mwanzoni ila mwishoni akili inawakaa sawa sawa na kutueleza". Akaingiza tena mkono wake kwenye mfuko ule na kutoa kitu ambacho ilikuwa mara yangu ya kwanza kukiona.

"hii ndio imefanya sisi kufika kwako ni GPRS ambayo ilikuwa kwenye mwili wa mama. Na bahati nzuri ni kuwa ulipoitoa ukaisahau kwako na wewe kukimbilia huko unapopaita Maisome sio!!?. Mshangao wa dhahiri ukanivaa huku mwili sasa ukipoteza uhimili wa ujasiri.

"nadhani walinao niframe hii kesi wamejipanga sana na bahati iliyo mbaya hata nyinyi mmeingia kwenye mtego huo". Nikamwambia bwana yule aliyeendelea kunionesha tabasamu pana kwenye sura yake.

"vizuri kama unaweza kutufundisha kile tulichokuwa na taaluma nacho, na hiyo ni kwa sababu wewe ni bora kutuliko. Kama uliweza kumchukua na kumficha tusipoweza kumuona basi uko vizuri kushindana na idara". Kauli yake ikanifanya kuwa nifahamu watu wanao nishikilia nao ni idara ya usalama wa taifa.

Japo sikuwa na uhakika wa moja kwa moja. Ila idara ya usalama wa taifa ndio ilikuwa ikihusishwa na kuwashikiria watu kwa stahili ambayo mimi nimeshikiriwa.

INAENDELEA….

Unakaribishwa kwa maoni na ushauri.
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom