mtoto mdogo sana
JF-Expert Member
- Apr 16, 2020
- 460
- 1,337
Muandishi:- Joseph .D. Migini
Call/txt:- +255766604683
Josephdeo70@gmail.com
#10
"mbona sikuelewi kiongozi". Nikaongea huku nikioneshwa kushangazwa na kile alichokuwa akikisema.
"utaelewa tu sababu ni wengi wanaokuja hapa wanakuwa kama wewe mwanzoni ila mwishoni akili inawakaa sawa sawa na kutueleza". Akaingiza tena mkono wake kwenye mfuko ule na kutoa kitu ambacho ilikuwa mara yangu ya kwanza kukiona.
"hii ndio imefanya sisi kufika kwako ni GPRS ambayo ilikuwa kwenye mwili wa mama. Na bahati nzuri ni kuwa ulipoitoa ukaisahau kwako na wewe kukimbilia huko unapopaita Maisome sio!!?. Mshangao wa dhahiri ukanivaa huku mwili sasa ukipoteza uhimili wa ujasiri.
"nadhani walinao niframe hii kesi wamejipanga sana na bahati iliyo mbaya hata nyinyi mmeingia kwenye mtego huo". Nikamwambia bwana yule aliyeendelea kunionesha tabasamu pana kwenye sura yake.
"vizuri kama unaweza kutufundisha kile tulichokuwa na taaluma nacho, na hiyo ni kwa sababu wewe ni bora kutuliko. Kama uliweza kumchukua na kumficha tusipoweza kumuona basi uko vizuri kushindana na idara". Kauli yake ikanifanya kuwa nifahamu watu wanao nishikilia nao ni idara ya usalama wa taifa.
Japo sikuwa na uhakika wa moja kwa moja. Ila idara ya usalama wa taifa ndio ilikuwa ikihusishwa na kuwashikiria watu kwa stahili ambayo mimi nimeshikiriwa.
INAENDELEA….
Unakaribishwa kwa maoni na ushauri.
GPRS