Riwaya: Bring back our girls

Riwaya: Bring back our girls

mtugani wa wapi huyo

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2012
Posts
1,239
Reaction score
1,477
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA KWANZA
MTUNZI: PATRICK.CK

Mlango wa ikulu unafunguliwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anajitokeza mbele ya waandishi wa habari walioitwa kwa dharura.Vituo vyote vya televisheni vilikatisha matangazo yao kwa muda na kurusha moja kwa moja hotuba ya rais. “ Ndugu wananchi ,siku ya leo ni siku ambayo nchi yetu kwa mara nyingine tena imekuwa muathirika wa mashambulio ya kigaidi. Mwaka huu nchi yetu ilichaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa Sullivan ambao niliufungua jana jijini Arusha.Katika mkutano huo wamehudhuria watu wengi akiwamo mke wa raisi wa Marekani Bi Glory Bishop.Mambo mbali mbali yanaendelea katika mkutano huo na kwa mujibu wa ratiba ya leo hii mabinti kumi na mbili kutoka Marekani wakiambatana na wenzao wa hapa Tanzania wakiwamo pia binti yangu mimi na binti wa waziri mkuu walitakiwa kwenda kutembelea shule ya sayansi ya wasichana iliyoko nje kidogo ya jiji la Arusha ikiwa ni mojawapo ya kampeni ya kuhamasisha watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi.Baada ya kutembelea shuleni hapo mabinti hawa pamoja na wanafunzi ishirini walielekea katika makumbusho ya viumbe wa kale yaliyoko nje kidogo ya jiji la Arusha.Wakiwa katika makumbusho hayo mabinti hawa pamoja na walinzi wao walivamiwa na kutekwa na kikundi kinachosadikiwa kuwa ni cha kigaidi na kupelekwa mahala kusikojulikana .Katika tukio hilo watu zaidi ya ishirini wanasadikiwa kuuawa baada ya kutokea milipuko miwili kubwa ya mabomu. Baada ya kuwateka watoto wetu magaidi hawa walikwenda pia katika hospitali ya mkoa ya Mount meru na kwa kutumia hewa yenye sumu wameweza kuua watu zaidi ya mia moja na ishirini.Kama hiyo haitoshi hivi ninavyoongea nanyi ndugu zangu ,wajumbe zaidi ya mia tatu waliokuwa ndani ya ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa KICC wameshikiliwa mateka na magaidi hawa.Bado hatujui nini lengo la kufanya mambo kama haya yasiyokuwa ya kibinadamu. Mke wa rais wa marekani pamoja na mke wangu nao pia wamenusurika kuuawa na mlipuko katika soko la bidhaa za utamaduni.Mlipuko huo uliowalenga wao ulitokea ndani ya soko dakika chache kabla hawajaingia humo sokoni.Watu ishirini wanasadikiwa kuuawa katika mlipuko huo. Ndugu zangu haya ni mashambulio makubwa kuwahi kufanywa na magaidi katika nchi yetu.Vyombo vya usalama vinaendelea na juhudi za kuwatafuta na kuwakomboa pamoja na watu wote wanaoshikiliwa mateka katika ukumbi wa mikutano wa KICC wengi wao wakiwa raia wa kigeni.Tumeimarisha usalama katika mipaka yetu yote na katika sehemu zote ambazo tunahisi zinaweza kuwa shabaha ya magaidi hawa.Naomba niwatoe wasi wasi ndugu wananchi kwamba vikosi vyetu viko imara na vimejiweka tayari kukabiliana na shambulio lolote lile ambalo linapangwa kufanywa na magaidi ndani ya ardhi yetu Ninapenda kuwahakikishia ndugu wananchi kwamba tutawasaka wote waliofanya kitendo hiki katika ardhi ya Tanzania ,kokote duniani na kuwatia nguvuni.Hatutamuacha hata mmoja wao.Serikali ya Tanzania haitavumilia kitendo kama hiki na vingine vyote visivyo vya kibinadamu.Tutapambana na yeyote Yule ambaye ana mkono wake katika jambo hili hata kama ana nguvu kiasi gani na mwisho tutahakikisha tunawakomboa mabinti zetu na wote wanaoshikiliwa mateka wakiwa hai. Kwa wazazi ,ndugu na jamaa ambao binti zenu wamepotea,nawasihi muwe watulivu na mviachie vyombo vya usalama vifanya kazi yake.Tukishirikiana na jumuiya ya kimataifa tutahakikisha mabinti wote wanarejeshwa mikononi mwenu wakiwa salama salimini.Tutawatafuta watoto wetu usiku na mchana,tutawatafuta mtaa kwa mtaa,nyumba kwa nyumba,pori kwa pori hadi tuhakikihsie watoto wetu wote wamepatikana.Napenda kuwasihi ndugu watanzania wenzangu tushikamane katika kipindi hiki kigumu na yeyote ambaye anaweza kuwa na taarifa zozote ambazo zinaweza kutusaidia kuwapata mabinti zetu na watu waliofanya kitendo hiki cha kinyama washirikiane na vyombo husika.Vita hii ni yetu sote,makatili hawa wamevamia nchi yetu basi tusimame pamoja na tuwaonyeshe kwamba watanzania siku zote ni wamoja na katu hawavumilii kitendo chochote kisicho cha kibinadamu kwa kusimama pamoja na kupinga vitendo hivi visivyo na hata chembe ya ubinadamu. Narudia tena kutoa pole kwa wale wote walipotelewa na wapendwa wao katika tukio hili.Watanzania na jumuia ya kimataifa tuko pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu.Ninachowaomba ndugu zangu tukio hili lisitugawe na kuvuruga umoja wetu .Tusibaguane kwa misingi ya dini,rangi wala kabila.Sikuzote watanzania ni wamoja na hata pale wanapopatwa na masahibu bado wanaendelea kuwa wamoja.Tushikamane na kwa pamoja tuipigane vita hii ngumu. Mungu ibariki Tanzania Ahsanteni kwa kuniskiliza. Hii ilikuwa ni hotuba fupi ya rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania akiutaarifu umma wa watanzania kuhusiana na kile kilichotokea na kinachoendelea jijini Arusha na hatua ambazo serikali imechukua na inaendelea kuchukua. Maeneo ya kati kati ya Jiji la Arusha kwa siku nzima yalikuwa kimya na tupu.Hii ilitokana na amri iliyotolewa ya kuwataka watu wote wakae ndani na wasizurure hovyo.Magari ya vikosi vya usalama ndiyo yaliyoonekana kuzunguka katika barabara za jiji hili tulivu.Mamia ya askari polisi walitawanyika katika kila kona ya jiji wakifanya doria na kuhakikisha amani inarejea.********************* Baada ya kumaliza kutoa hotuba yake kwa taifa,mheshimiwa rais akaelekea moja kwa moja katika kikao cha dharura na wakuu wa vyombo vya usalama nchini ili kujadili hali ya usalama na namna ya kukabiliana na tukio lililotokea.Wakati wakiwa katika kikao,mmoja wa walinzi wake akaingia na kumnong’oneza kitu.Mheshimiwa raisi akasimamisha kikao kwa muda na kusema “ Nimepewa taarifa kwamba katika laini ya simu kuna mtu anayedai ndiye kiongozi wa kundi linalohusika na mashambulio yote ya leo na anahitaji kuongea nami.” akasema Dr Faustine mkwaza raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Chumba chote kikawa kimya watu wote wakitaka kumsikia kiongozi huyo wa kikundi cha kigaidi.Mheshimiwa rais akabonyeza kitufe cha kupokelea simu katika simu iliyokuwa mbele yake. “ Hallo.Rais wa jamhuri ya muungano anaongea hapa ” akasema Dr Faustine “ Hallo mheshimiwa rais” ilikuwa ni sauti nzito ya kiume toka upande wa pili.Watu wote wakatazamana.Walistuka baada ya kumsikia mtu Yule akiongea Kiswahili safi “ Wewe ni nani na unataka nini? Akauliza mheshimiwa rais “ Huna haja ya kunijua jina langu lakini mimi ndiye kiongozi wa mashambulio yote ya leo.Mimi na vijana wangu tunawashikilia wasichana zaidi ya sabini .Wote wako salama kabisa na hatuna lengo la kuwafanya chochote endapo utakubaliana na matakwa yetu.Tunawashikilia vile vile wajumbe zaidi ya mia tatu katika ukumbi wa mikutano wa KICC .Tumefanya pia shambulio katika hospitali ya mkoa ya Mount meru kwa kuachia gesi ya sumu ya kuua watu wengi.Mheshimiwa rais haya yaliyotokea leo jijini Arusha ni sehemu ndogo tu mashambulio ambayo tumepanga kuyafanya hapa nchini,bado kuna mashambulio makubwa sana yanakuja endapo hautakubaliana nasi.Hivi tunavyoongea kuna watu wetu ambao wako tayari katika sehemu mbali mbali zenye mikusanyiko ya watu hapa nchini wakisubiri amri yangu tu ili waweze kuiachia gesi hiyo inayoua baada ya dakika mbili.Nakuhakikishia mheshimiwa rais kutakuwa na msiba katika kila mtaa endapo nitawapa amri vijana wangu ya kuachia gesi hiyo.” “ Kwa nini mnafanya mambo haya ya kikatili ndani ya ardhi ya tanzania? ?!!..akasema kwa ukali Dr Faustine. “ Relax Mr president.Tumeyafanya haya yote kwa sababu maalum.Tuna ombi moja tu mheshimiwa rais na liko ndani ya uwezo wako” “ Mnataka nini? Akauliza tena Dr Faustine kwa ukali “ Tunataka umuachie huru kiongozi wetu Yasin abdulkadir Husein ndani ya msaa matatu toka sasa.Tutakapompata kiongozi wetu tutawaachia wasichana wote pamoja na wajumbe tunaowashikilia katika ukumbi a mikutano.Chaguo ni lako mheshimiwa rais,utimize matakwa yetu au upeleke msiba katika kila mtaa wa nchi hii” Dr Faustine akavuta pumzi ndefu na kuwatazama wajumbe wake,kisha akasema “ Naomba unisikilize kwa makini sana.” “ Nakusikiliza mheshimiwa rais” “ Tanzania hata siku moja haiwezi kuingia mkataba na magaidi.Futa kabisa wazo kwamba tutafikia makubaliano mimi na ninyi.Kitu cha pili huyo kiongozi wenu Yasin Abdulkadir Husein hataachiwa huru kamwe.Na jambo la tatu na la mwisho ninalotaka ulifahamu ni kwamba serikali ya Tanzania itawakomboa wasichana wote mnaowashikilia ikiwa ni pamoja na kuwatia nguvuni wewe na wenzako wote” akasema kwa ukali dr Faustine “ Mheshimiwa rais tayari nimekwisha kutaarifu tunachohitaji na nimekupa masaa matatu toka sasa.Kila baada ya dakika ishirini katika saa ya kwanza tutaua watoto wawili kwa kuwachinja na katika saa ya pili tutachinja watoto wanne.Saa ya tatu na na ya mwisho tutaua watoto watano kila dakika ishirini.Muda unaanza kuhesabiwa sasa” simu ikakatwa. “ Mheshimiwa rais !!..” akasimama waziri mkuu mara baada ya simu kukatwa “ Tuko katika janga.Nchi yetu imekumbwa na mashambulio makubwa ya ugaidi.Watoto wetu wametekwa na wengine bado wanashikiliwa mateka .Watu hawa hawatanii mheshimiwa rais.Wamekwisha ua watu wetu na wataendelea kuua watu kama walivyoahidi.Tulitakiwa kuongea vizuri na mtu huyu na kujaribu kufanya makubaliano ambayo yanaweza kututoa katika janga hili.Maisha ya wat……..” “ Mheshimiwa waziri mkuu “ Dr Faustine akamkatisha. “ Naomba tuelewane kwamba tuko katika janga zito kwa maana hiyo basi lazima tuwe makini sana katika kila jambo tunalolifanya,na maamuzi tunayoyachukua.Maisha ya watanzania yako hatarini na bado kuna vitisho vingine vya mashambulio zaidi .Tunachotakiwa ni kutafuta namna ya kuhakikisha maisha ya watanzania yanakuwa salama na hakuna tena tishio lolote la mashambulio.Msimamo ninaouweka hapa ni kwamba hatutajadiliana chochote na watu hawa.Wametushambulia ,wameua raia wetu wasiokuwa na hatia,wamewachukua mateka watoto wetu na wanaendelea kuwashikilia wajumbe zaidi ya mia tatu kwa hiyo watu kama hawa si wa kujadiliana nao hata kidogo na ninaomba katika kikao hiki kusiwe na mazungumzo yoyote yanayohusiana na kujadiliana na magaidi hawa.Tutawatafuta katika kila kona ya nchi na tutawapata.Tumechokozwa na lazima tuwaonyeshe kwamba Tanzania si mahala ambapo unaweza ukafanya chochote unachokitaka na ukaachwa.” Akasema Dr Faustine kwa sauti ya amri na hakuna aliyejibu chochote .Kikao kizito kikaendelea.************************** Dakika ishirini baada ya raisi kuzungumza katika simu na kiongozi wa kikundi kilichofanya mashambulio jijini Arusha , kulirushwa video katika mtandao wa intanet iliyomuonyesha mtu mmoja aliyejifunika sura yake akitoa onyo na vitisho kwa serikali .Mtu huyo alikuwa akiongea kwa Kiswahili fasaha kabisa “ Ndugu watanzania, mmetangaziwa na rais wenu kuhusiana na kile kilichotokea jijini Arusha.Ni kweli tumefanya shambulio,tumewachukua mateka wasichana zaidi ya sabini miongoni mwao ni mtoto wa rais wenu na mtoto wa waziri mkuu.Pia tunao wasichana zaidi ya kumi na mbili wa kutoka nchini Marekani.Mateka wote wako salama na wamehifadhiwa katika sehemu salama.Hatuna nia wala lengo la kuwadhuru wasichana hawa na hatutafanya hivyo endapo matakwa yetu yatatimizwa.Tunawashikilia vile vile wajumbe zaidi ya mia tatu katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa KICC.Tuna watu wetu pia katika sehemu mbali mbali nchini zenye mikusanyiko ya watu kama mahospitalini,mashuleni n.k ambao wako na gesi ya sumu na endapo wataiachia gesi hiyo mamia ya watanzania watapoteza maisha yao.Tunachotaka ni kuachiwa kwa kiongozi wetu Yasin Abdulkadir Husein.Tumempa rais wenu masaa matatu awe ametekeleza ombi letu.Tumemwambia katika kila dakika ishirini tutaua wanafunzi wawili.Tunataka kumuonyesha kwamba tukiongea kitu hatutanii,tayari dakika ishirini za kwanza zimepita na tunaua watoto wawili na tutaendelea hivyo kila baada ya dakika ishirini.” Akafanya ishara na wasichana wawili waliokuwa wamefungwa vitambaa machoni wakiwa na sare zao za shule wakaletwa na kupigishwa magoti mbele yake. Akawafungua vitambaa.Macho yao yalikuwa mekundu na yamevimba kwa kulia. “ Binti unaitwa nani? Akamuuliza mmoja wao “ naitwa Lucy Nswami” “ Lucy una miaka mingapi? “ Nina miaka kumi na tano” “ Na wewe unaitwa nani? Akamuuliza na Yule mwenzake “ Naitwa Husna ayoub” “ Husna una miaka mingapi? “ Nina miaka kumi na sita.Tafadhali naomba msituue.Ongeeni na baba yangu ni tajiri anafanya biashara ya madini atawapa kiasi chochote cha pesa mnachohitaji.Tafadhali naomba msituue….” Yule jamaa akamtazama na kusema “ Husna angalia ile kamera na umuombe rais wako awaokoe kwa kutupa kile tulichomwambia atupatie”. Huku uso wake umefunikwa na machozi Husna akaiangalia kamera na kusema “ Mheshimiwa rais baba yetu, tunaomba utuokoe.Tumetekwa na tunahitaji msaada wako.Tumeambiwa kwamba usipowapatia wanachohitaji watatuua wote. Tunakuomba rais tuokoe tusiuawe.Sisi bado ni wasichana wadogo na tuna malengo mengi ya maisha.Tuokoe mheshim……..” akashindwa kuendelea akaangua kilio. “ Ndugu watanzania,wasichana hawa wanakwenda kupoteza uhai wao angali wadogo kwa sababu ya ukaidi wa rais wenu,mtu mliyemuamini mkampa kura na akaahidi kuwalinda.Kila baada ya dakika ishirini uhai wa wanafunzi kadhaa utapotea ikiwemo na mtoto wa rais.” Akasema Yule jamaa na kunyoosha mkono akatokea tena mtu mwingine aliyejifunika sura na mwenye mwili uliojaa akiwa na kisu kikali .Akawafunga vitambaa usoni wale wasichana na bila kupoteza muda kwa kutumia mkono wenye nguvu akamkata kichwa Lucy Nswami na kukitenganisha na kiwili wili.Mwili wa msichana Yule mdogo ukaanguka chini akakiweka kichwa juu yake halafu akamuinamisha Husna Ayoub na kumchinja. Kiongozi wa magaidi wale akaigeukia kamera na kusema “ Hawa ni wa kwanza .Tutaendelea kuua kila baada ya dakika ishirini.Mheshimiwa rais damu ya wasichana hawa ni juu yako.Muda unazidi kuyoyoma” Video ile ya kutisha ikafika mwisho.

ULIMWENGU UNASTUSHWA NA TUKIO LA KIGAIDI LINALOTOKEA JIJINI ARUSHA TANZANIA.ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII HAPA HAPA MASIMULIZI
 
BRING BACK OUR GIRLS


SEHEMU YA 2


MTUNZI: PATRICK.CK

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Ndugu watanzania,wasichana hawa wanakwenda kupoteza uhai wao angali wadogo kwa sababu ya ukaidi wa rais wenu,mtu mliyemuamini mkampa kura na akaahidi kuwalinda.Kila baada ya dakika ishirini uhai wa wanafunzi kadhaa utapotea ikiwemo na mtoto wa rais.” Akasema Yule jamaa na kunyoosha mkono akatokea tena mtu mwingine aliyejifunika sura na mwenye mwili uliojaa akiwa na kisu kikali .Akawafunga vitambaa usoni wale wasichana na bila kupoteza muda kwa kutumia mkono wenye nguvu akamkata kichwa Lucy Nswami na kukitenganisha na kiwili wili.Mwili wa msichana Yule mdogo ukaanguka chini akakiweka kichwa juu yake halafu akamuinamisha Husna Ayoub na kumchinja. Kiongozi wa magaidi wale akaigeukia kamera na kusema
“ Hawa ni wa kwanza .Tutaendelea kuua kila baada ya dakika ishirini.Mheshimiwa rais damu ya wasichana hawa ni juu yako.Muda unazidi kuyoyoma” Video ile ya kutisha ikafika mwisho

ENDELEA……………………………………..

Kikao kizito kikiwahusisha viongozi wakuu wa nchi na wakuu wa vyombo vyote vya uslama kiliendelea ikulu jijini Dar kujadili hali ya usalama wa nchi na namna ya kukabiliana na kikundi cha kigaidi kilichowateka wasichana wa shule na kuwashikilia mateka wajumbe wa zaidi ya mia tatu wanaohudhuria mkutano wa Sullivani jijini Arusha.Wakati kikao kikiendelea mmoja wa walinzi wa rais akaingia na kumnong’oneza jambo.Dr Faustine akainamisha kichwa akafikiri kidogo halafu akasema
“ Ndugu wajumbe nimetaarifiwa kwamba kuna video imerushwa katika mtandao wa intaneti na magaidi.Ngoja tuiangalie” akasema rais na wajumbe wote wakaigeukia runinga kubwa iliyokuwa ukutani.Mlinzi wa rais akaiwasha runinga na video ikaanza kucheza ikimuonyesha kiongozi Yule wa magaidi akijitapa na baadae wasichana wawili wakaletwa mbele ya kamera na mmoja wao akalazimishwa kumuomba rais awaokoe
“ Mheshimiwa rais baba yetu, tunaomba utuokoe.Tumetekwa na tunahitaji msaada wako.Tumeambiwa kwamba usipowapatia wanachohitaji watatuua wote. Tunakuomba rais tuokoe tusiuawe.Sisi bado ni wasichana wadogo na tuna malengo mengi ya maisha.Tuokoe mheshim……..” Maneno haya ya msichana aliyepigishwa magoti akiwa tayari kuuliwa na magaidi yalimchoma sana Dr Faustine rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,akainama chini.
“ Turn it off” akaamrisha rais baada ya kuwaona wasichana wale wadogo wakichinjwa kama kuku
“ Ouh Mungu wangu huu ukatili wa namna gani? Kwa nini wanawaua wasichana wadogo vile bila hatia kwa kuwachinja kama kuku? Akawaza Dr Faustine.Hali katika chumba cha mikutano ilibadilika. Wajumbe walikuwa katika taharuki kubwa.Tukio kama lile la wasichana kuchinjwa na kuonyeshwa hadharani halikuwahi kutokea nchini Tanzania.Liliwastua sana.Sasa waliamini kwamba magaidi wale hawakuwa wakitania.Ukimya mkubwa ulitawala mle chumbani kwa dakika kadhaa.Ni waziri mkuu ambaye aliuvunja ukimya na kusema “ Mheshimiwa rais na ndugu wajumbe nadhani nyote mmeiona video hii.Wasichana wetu wawili tayari wamechinjwa kama kuku na kila baada ya dakika ishirini wasichana wengine watachinjwa. Nilisema toka awali kwamba watu hawa hawatanii.Wakisema wataua wanaua kweli. Naomba tufanye maamuzi ya busara na ya haraka sana ya kuweza kuwakomboa wasichana wetu. Tumekaa hapa kwa muda sasa lakini bado hatuna jambo la msingi tuliloliamua na ndani ya dakika ishirini zijazo mabinti wengine wanakwenda kuuawa. Mheshimiwa rais this is a very serious matter.Hivi ndivyo tunavyowatendea raia waliotuweka madarakani kwa kukubali watoto wao wachinjwe kama kuku? Akasema kwa ukali waziri mkuu? Dr Faustine akafuta jasho na kusema
“ Mheshimiwa waziri mkuu naomba utulize jazba kwani jambo hili linatakiwa lijadiliwe kwa umakini mkubwa. Ninafahamu wasi wasi wako kwani mtoto wako ni mmoja wa mateka wanaoshikiliwa,lakini hata mimi pia nina mtoto wangu katika mateka hao pia kwa hiyo tukae na kujadili jambo hili kwa busara na kufikia mamuzi ya namna bora ya kukabiliana na watu hawa.Tukienda kwa papara tutawapoteza watoto wetu na watu wengi watakufa.Tunatakiwa kulimaliza suala hili bila ya kumwaga damu nyingi.” Akasema Dr Faustine.Waziri mkuu anaye akasema
“ Mheshimiwa rais hauoni muda unazidi kwenda? Dakika ishirini zijazo wasichana wengine watauawa.We need to act faster.” Akasema waziri mkuu kwa jazba.Tayari alikwisha pandwa na hasira.Dr Faustine naye alionekana kukerwa na maneno ya waziri mkuu
“ Ndugu waziri,nchi haiendeshwi namna hiyo.Janga hili ni kubwa na lazima itumike busara na mbinu kubwa katika kulishughulikia jambo hili. Hatuwezi kukurupuka tu na kuanza kushambulia bila kujua tunamshambulia nani na yuko wapi. Tunavyo vymbo vya usalama ambavyo viko katika kulishughulikia suala hili kwa hiyo hakuna haja ya kuwa na wasi wasi.”
“ Hakuna haja ya kuwa na wasi wasi?!!..waziri mkuu akahamaki
“ Watoto wetu wanachinjwa kama kuku halafu unasema hakuna haja ya kuwa na wasi wasi?!!..Unataka kutuaminisha kwamba nchi iko shwari? Ndiyo tuna vyombo vya dola lakini vimefikia wapi hadi hivi sasa? Ndani ya dakika kumi zijazo toka sasa itarushwa video nyingine wasichana wetu wakichinjwa.Please Mr president wake up.Act like a president…” akasema kwa ukali waziri mkuu.Dr Faustine akafura kwa hasira na kumtaka waziri mkuu watoke wakaongee nje.
“ Mheshimiwa waziri mkuu sintavumilia tena vitendo vyako vya dharau mbele ya wajumbe.Umenionyesha dharau kubwa sana.Mimi ndiye rais na ndiye mwenye maamuzi ya nini kifanyike.Kama una njia bora ya kuweza kulishughulikia suala hili tueleze tukusikie.Tuko katika kipindi kigumu tunatakiwa tushikamane,tuwe kitu kimoja ,tukianza kuvurugana sisi viongozi hatutaweza kukabiliana na suala hili” wakati mheshimiwa rais akiendelea kuongea na waziri mkuu ,mmoja wa walinzi wake akamsogelea na kumfahamisha kwamba rais wa marekani alikuwa katika laini ya simu akitaka kuongea naye.Mheshimiwa rais na waziri mkuu wakareja tena ndani ya chumba kile cha mikutano.Runinga ikawashwa.
“ Mheshimiwa rais kwanza nakupa pole sana wewe na wananchi wa Tanzania kwa tukio hili la kigaidi lililotokea nchini mwako.Ulimwengu mzima umestushwa mno na tukio hili lililotokea katika nchi yenye amani kubwa .Hii inaonyesha kwamba vita ya ugaidi ni kubwa zaidi ya vile tunavyoifkiria.” Akasema rais wa marekani Bw.Brown bishop
“ Ahsante sana mheshimiwa rais.Ni tukio kubwa na zito kuwahi kutokea katika nchi yetu”akajibu Dr Faustine
“ Je mmekwisha wabaini waliofanya kitendo hiki?
“ Ndiyo mheshimiwa rais ,ni kikundi cha Alshabaab ambao wamefanya hivi kwa ajili ya kushinikiza kuachiwa kwa kiongozi wao Yasin Abdulkadir Hussein ambaye anashikiliwa na mahakama ya afrika.” Dr Faustine akamueleza rais wa marekani kila kitu kilichotokea na hatua wanazozichukua.
“ Mheshimiwa rais narudia tena kutoa pole zangu nyingi kwa wananchi wa Tanzania kwa tukio hili.Watanzania hawajazoea mambo kama haya.Katika kuunga mkono hatua mlizozichukua na mnazoendeela kuzichukua ninatuma kikosi maalum cha wanajeshi mia mbili wenye utaalamu wa hali ya juu wa kupambana na matukio ya kigaidi ili kuungana na vikosi vyenu na pia kuwaokoa raia wa marekani wanaoshikiliwa mateka.Endapo kama kuna msaada mwingine wowote mnaouhitaji serikali yangu iko tayari kuwasaidia”
“ Nashukuru sana mheshimiwa rais. Nadhani hakuna haja ya kuongeza vikosi vya jeshi kwa sababu tayari tuna vikosi vya kutosa na vyenye ujuzi wa kuweza kupambana na matukio kama haya ya kigaidi.Kwa sasa vikosi hivyo unavyotaka kutuma vinaweza kuwekwa katika utayari na pindi tukihitaji msaada tutakutarifu mheshimiwa rais lakini naomba kwa sasa vikosi vyetu vya ndani viendelee na zoezi la kuwakomboa mateka na vile vile kuwatafuta wasichana wote waliotekwa nyara.” Akasema Dr Faustine halafu akaagana na rais wa marekani. Mara tu alipomaliza kuongea na rais wa Marekani ,waziri mkuu akasimama huku akiwa na sura ilyokunjamana
“ Mheshimiwa rais,naomba utueleze una sababu yoyote ya kuukataa msaada wa kikosi maalum toka marekani? Kikosi chenye uzoefu mkubwa wa kupambana na matukio ya kigaidi? Dr Faustine akafuta jasho na kuwatazama wajumbe kisha akasema
“ Tuviachie vikosi vya ndani viendelee na kazi yake bila kuvihusisha vikosi vya kigeni.Hata sisi vikosi vyetu vina ujuzi na mbinu za kuweza kupambana na matukio kama haya.Tutautumia msaada wao pale itakapotulazimu lakini kwa sasa tunatumia vikosi vyetu wenyewe” akasema Dr Faustine
“ Mheshimiwa rais,” akasema waziri wa ulinzi “nadhani waziri mkuu ana point ya msingi sana.Binafsi nadhani kikosi kile kingetufaa sana kwani wao wana uzoefu mkubwa wa matukio kama haya.Wenzetu wamekuwa wakikutana mara kwa mara na matukio kama haya kwetu sisi hili ni tukio la kwanza kubwa kuwahi kutokea.Kuna haja ya kuongeza nguvu ya kimataifa kwani suala hili si la kwetu peke yetu.Vita ya ugaidi inapiganwa na dunia nzima.” Wajumbe wakatikisa vichwa kuonyesha kukubaliana na mawazo yake ya waziri wa ulinzi.Dr Faustine akasema kwa ukali
“Gentlemen,naomba tuelewane.Mimi ndiye rais na nimesema kwamba kwa sasa hatuna haja ya kutumia vikosi vya nje ya nchi.Tutatumia vikosi vyetu vya ndani na tutawakomboa mateka wote na hali ya usalama itakuwa shwari.Kutumia vikosi vya nje ni sawa na kuwahakikishia magaidi hawa kwamba Tanzania haina uwezo wa kushughulikia matukio ya kigaidi. Nataka tuionyeshe jumuiya ya kimataifa kwamba tunao uwezo wa kupambana na ugaidi na hivyo kutoa onyo kwa vikundi vingine kutothubutu kuigusa nchi yetu” akasema Dr Faustine
“ Mheshimiwa rais,hii si namna bora ya kushughulika na mambo makubwa kama haya.Kikatiba wewe ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kama mkuu wa nchi lakini si kila jambo unaloliamua linakuwa na maslahi kwa nchi.Naomba niwe wazi kwako mheshimiwa rais kwamba katika maamuzi yako ya leo hauko sahihi kabisa. Kwa nam……..” waziri mkuu akakatishwa na rais
“ Stop !..nadhani sasa tumeanza kuvuka mipaka.Mimi ndiye kiongozi wa nchi na ndiye mwenye maamuzi ya mwisho.Najua wengi wenu hapa mna suluhisho moja tu nalo ni kukubaliana na magaidi hawa na kumuachia kiongozi wao.Naomba mfute katika vichwa vyenu mawazo hayo.Yasin kamwe hataachiwa na tutapambana na magaidi hawa kwa kutumia vikosi vyetu vya ndani hadi tuhakikishe tumewasambaratisha.Wametutangazia vita na sasa ni zamu yetu kuwaonyesha kwamba Tanzania si nchi ya kuchokozwa.Tutawafuata hadi katika kambi zao huko nchini kwao na kuhakikisha tunawasambaratisha wote.Tumeelewana? akauliza kwa sauti ya juu
“ Tumeelewana” wakajibu wajumbe kwa pamoja
“ Good ! kwa sasa twendeni tukashughulikie mambo ambayo tumekubaliana na baada ya masaa matatu tukutane hapa kwa ripoti.” Akasema rais na wajumbe wakaondoka wakamucha peke yake.
“Sikuwahi kuota kama siku moja katika utawala wangu nitakumbana na jambo zito kama yhili.Huu ni mtihani mkubwa sana kwangu na kwa mara ya kwanza najihisi kushindwa kuchukua maamuzi ya kufaa kulishughulikia suala zito kama hili.” Akawaza Dr Faustine akiwa mwenyewe ndani ya chumba cha mikutano.Maneno ya msichana akiomba msaada yakamrudia tena kichani
“ Mheshimiwa rais baba yetu, tunaomba utuokoe.Tumetekwa na tunahitaji msaada wako.Tumeambiwa kwamba usipowapatia wanachohitaji watatuua wote. Tunakuomba rais tuokoe tusiuawe.Sisi bado ni wasichana wadogo na tuna malengo mengi ya maisha.Tuokoe mheshim……..”Alichomwa mno na maneno haya ,akainama na kuzama katika mawazo .
“ Nahisi kuchanganyikiwa.Mwanangu pia yuko katika kundi hili la wasichana waliotekwa.Nitafanya nini ili kumuokoa? Je nikubaliane na matakwa ya magaidi? Akawaza Dr Faustine akakosa jibu ,akaangalia saa yake ya mkononi na kukuta zimebaki dakika tano kabla ya magaidi kuua wanafunzi wengine.Akamuita mlinzi wake
“ Tunaelekea idara ya ujasusi ya taifa” akasema

MAMBO YANAZIDI KUPAMBA MOTO…..RAIS ANAKWENDA KUFANYA NINI IDARA YA UJASUSI YA TAIFA? ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII
 
BRING BACL OUR GIRLS

SEHEMU YA 3

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Mheshimiwa rais baba yetu, tunaomba utuokoe.Tumetekwa na tunahitaji msaada wako.Tumeambiwa kwamba usipowapatia wanachohitaji watatuua wote. Tunakuomba rais tuokoe tusiuawe.Sisi bado ni wasichana wadogo na tuna malengo mengi ya maisha.Tuokoe mheshim……..”Alichomwa mno na maneno haya ,akainama na kuzama katika mawazo . “ Nahisi kuchanganyikiwa.Mwanangu pia yuko katika kundi hili la wasichana waliotekwa.Nitafanya nini ili kumuokoa? Je nikubaliane na matakwa ya magaidi? Akawaza Dr Faustine akakosa jibu ,akaangalia saa yake ya mkononi na kukuta zimebaki dakika tano kabla ya magaidi kuua wanafunzi wengine.Akamuita mlinzi wake “ Tunaelekea idara ya ujasusi ya taifa” akasema


ENDELEA…………………………

Kazi zilisimama kWa muda baada katika ofisi kuu ya idara ya ujasusi baada ya rais kuwasili.Mkurugenzi wa idara idara ya ujasusI Tanzania akamkaribsha mheshimiwa rais na wakati wakielekea katika ofisi yake,rais akasimama na kuwasalimu wafanyakazi.
“ Ndugu zangu poleni na kazi.Nadhani nyote mnafahamu kinachoendelea hapa nchini kwetu.Tumeshambuliwa na magaidi na wasichana wetu zaidi ya sabini wametekwa nyara na kupelekwa mahala kusikojulikana.Zaidi ya hayo,watu zaidi ya mia tatu wanashikiliwa katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha KICC jijini Arusha.Ukiacha hayo bado kuna vitisho toka kwa kikundi hiki cha mashambulio zaidi.Dakika chache zilizopita watoto wawilI wamechinjwa na katika dakika chache zijazo tutawapoteza watoto wengine na tutaendelaea kuwapoteza watoto wetu hadi hapo nitakapokubaliana na matakwa yao. Ndugu zangu usalama wa n chi na wanachi uko mikononi mwetu.Kuanzia sasa kila mmoja ajitume,tufanye kazi kama mchwa usiku na mchana na tuhakikishe kwamba tunazuia shambulio lolote lisitokee tena katika nchi yetu na vile vile kuwatafuta na kuwakomboa wasichana wote waliotekwa nyara pamoja na wajumbe wote wanaoshikiliwa mateka katika ukumbi wa mikutano wa KICC.” Akasema rais halafu akauongozana na mkurugenzi kuelekea ofisini kwake.Akawaomba walinzi iwake wabaki nje wakati akiongea kwa faragha na mkurugenzi
“mkurugenzi nadhani unaelewa kipindi tulichonacho. Nimekuja hapa kwa ajili ya kitu kimoja tu,kufahamu mahala idara yako ilikofikia kuhusiana na tukio hili. Mpaka sasa hivi kuna fununu zozote kuhusu mahala walipo wasichana waliotekwa? “
“ Mheshimiwa rais,mpaka sasa hivi bado hatuna taarrifa zozote za kuhusiana na mahala waliko watoto waliotekwa lakini bado tunaendelea na uchunguzi.Kuna timu ya vijana wetu ambayo tayari imekwisha tua jijini Arusha na tunategemea ripoti kamili toka kwao .”
Rais akainama akashika kichwa akafikiri kidogo halafu akasema
“ Kama tusipofanya haraka hawa magaidiwataendelea kuua watoto wetu kila baada ya dakika ishirini.Tayari wamekwisha chinja wanafunzi wawili na wataendelea hivyo kila baada ya dakika ishirini. Mkurugenzi ninyi ni tegemeo letu la mwisho kwa hiyo naomba mfanye kila linalowezekana ili vijana hawa wapatikane . Ninyi mna kila aina ya miundo mbinu ya kuweza kuwabaini maharamia hawa waliofanya kitendo hiki tofauti na vyombo vingine vy a usalama.Chochote mnachokihitaji nitawapatia ili kufanikisha jambo hili.Kitu kingine ni kuhusu video iliyosambazwa mtandaoni na magaidi wakiwachinja wasichana wetu.Video hii najua itazusha taharuki kubwa miongoni mwa jamii.Hakuna namna mnayoweza kuiondoa mtandaoni? Hakuna namna mnayoweza kubaini chanzo cha video hiyo ?
“ Mheshimiwa rais,kusema ukweli kuizuia video hiyo isiwepo mtandaoni ni jambo gumu kidogo kwa sababu mpaka sasa imekwisha sambaa kila mahala. Mimi nadhani tuelekeze nguvu katika kuwasaka watoto waliotekwa kuliko kutumia nguvu katika kuizuia video isisambae mtandaoni..Usijali mheshimiwa rais,tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba watoto wote waliotekwa wanapatikana na kuwatia nguvuni watekaji wote.Vijana wangu wana ari ya kazi na ninaamini ndani yamudamfupi ujao tayari tutakuwa tumepata mwangaza” akasema mkurugenzi.rais akainuka na kuanza kuzunguka zunguka mle ofisini na mara simu ya mkurugenzi ikaita.Akapokea na kuongea kwa sekunde kadhaa halafu akamgeukia rais.
“ Mheshimiwa rais,nimetaarifiwa kuna video nyingine imerushwa mtandaoni na magaidi”
“ ouh My God ! wanaua tena wasichana wengine..What am I going to do? Akasema rais halafu wakaongozana kuelekea katika chumba kidogo cha mikutano kulikokuwa na runiga tatu kubwa.
“ Ndugu watanzania,nimerejea tena kama nilivyowaahidi. Rais wenu bado hajakubaliana na matakwa yetu na kama nilivyotoa ahadi kwamba kila baada ya dakika ishirini kama hatakuwa amekubaliana nasi basi nitapunguza idadi ya watoto.Nitaendelea hivyo mpaka nihakikishe watoto wote wamekwisha na hapo ndipo mtakaposhuhudia damu ambayo haijawahi kumwagika hapa Tanzania” akasema Yule jamaa kiongozi wa kikundi cha kigaidi ambaye hakutaka kutaja jina lake na kisha wasichana wawiliwakaletwa mbele ya kamera.
“ Wasichana hawa wanakwenda kupoteza tena maisha kutokana na ukaidi wa rais wenu”: akasema Yule jamaa halafu akatokea tena Yule mchinjaji wa mara ya kwanza na bila huruma akawakata vichwa wasichana wawili.
“ Zoezi hili litaendelea kila baada ya dakika ishirini na kama rais wenu bado hajakubaliana na matakwa yetu basi tutahakikisha wasichana wote wameuawa.” akasema Yule kiongozi na kamera ikazimwa.
Mheshimiwa rais alikuwa akitiririkwa na jasho.Alichanganyikiwa na hakujua afanye nini.
“ Mheshimiwa rais,watu hawa wataendelea kuua wasichana kama walivyoahidi hadi pale utakapokubaliana na matakwa yao.” Akasema mkurugenzi
“ Siwezi kukubaliana kamwe na matakwa yao.Tunatakiwa tutafute namna ya kufanya ili kuwakomboa watoto na kusitisha mauaji ya watoto.Naomba wewe na idara yako mfanye kila linalowezakana ili suala hili liwezekane.Sitaki tena kuona magaid…..” mheshimiwa rais akakatishwa na mlinzi wake aliyeingia ghafla mle ndani
“ Mheshimiwa rais kuna mtu anapiga simu anadai yeye ndiye kiongozi wa kundi lililofanya shambulio la arusha.” Rais akastuka na akasita kuipokea ile simu
“ Mheshimiwa rais, jaribu kumongea naye ili tuvute muda kidogo wakati tukiendelea na mikakati lakini kwa wakati huu wasitishe kwanza mauaji ya watoto.Mwambie kwamba unakubaliana na matakwa yake na uko tayari kumuachia huru mtu wanayemtaka” akasema mkurugenzi
Mheshimiwa rais akachukua ile simu na kubonyeza kitufe cha kupokelea
“ Hallow” akasema
“ Mheshimiwa rais,nadhanio tayari umeiona video ya pili.Sisi huwa tunasema kwa vitendo..Endapo hautakubalaiana nasi sasa hivi,tutaendelea na kuua atoto mfululizo kama nilivyokuahidi.” Akasema kiongozi wa magaidi
“ Kwa nini mnaua watoto wadogo wasio na hatia?
“ Tunawaua kutokana na ukaidi wako mheshomiwa rais. Endapo ungekubaliana na matakwa yetu basi haya yote yasingetokea.”
“ Nawaomba tafadhali msitishe mauaji ya watoto wetu ,hawana hatia.Nipeni muda kidogo niweze kushughulikia suala hili. “
“ Nimekupa masaa matatu mheshimiwa rais ,Yasin awe ameachiliwa.”
“ Masaa matatu ni kidogo sana kwani Yasin anashikiliwa na mahakma ya afrika namimi sina jukumu la kumuachia .Nipeni muda zaidi nione namna nitakavyofanya ila nawaomba msiendelee kuua watoto.”
“ Tutaacha kuua watoto endapo utatuhakikishia kwamba utamuachia huru Yasin,vinginevyo tutaendelea kuua kila baada ya dakika ishirini,tena usisahu mheshimiwa rais kwamba hata mtoto wako na mtoto wa waziri mkuu ni miongoni mwa watoto tunaowashikilia.”
‘ Nalifahamu hilo ,na ndiyo maana ninawasihi kwamba msiendelee kuwadhuru watoto.Niko tayari kuwapatia mtu mnayemuhitaji lakini kwanza mnihakikishie kwamba mtasitisha mauaji ya watoto na kuwaachia huru mateka wote.”
“ Sisi hatuna shida mheshimiwa rais,endapo tutampata kiongozi wetu basi tutawaachia huru wasichana wote pamoja na mateka wote tunaowashikilia.”
“ Nitaaminije kama mtatimiza ahadi yen?
“ Kwa sasa hatutaua mtoto yeyote lakini baada ya masaa matatu kupita na bado hujamuachia kiongozi wetu,utakuwa umekiuka makubaliano yetu na hatutakuwa na namnanyingine zaidi ya kuwaua wasichana wote na kuendeleza mashambulio makubwa .Kitu kingine mheshimiwa rais mmekuwa mkipeleka vikosi vingi vya askari na jeshi katika ukumbi wa KICC.Nawaonya msitubutu kujaribu kutaka kuingia ndani.Vijana wangu waliomo mle ukumbini wote tayari wamekwisha yatoa maisha yao kwa ajili ya kiongozi wetu ,na ukumbi wote umezungukwa na mabomu hivi sasa.Kitendo chochote cha kutaka kuingia mle ukumbini kwa nguvu mtawapoteza watu wote zaidi ya mia tatu kwani tutaulipua ukumbi wote .Kwa hiyo kuanzia sasa virudisheni nyuma viko vyenu vyote visikaribie kabisa jengo lile kama mnataka kuwapata mateka wenu wakiwa.salama.”
Ok sawa nimekuelewa.Tutafanya hivyo ila tafadhali naomba msimdhuru mtu yeyote Yule tena wakati ninashughulikia suala lenu”
“ Sawa mheshimiwa rais,nitatekeleza maagano yetu lakinikumbuka yamebaki masa mawili tu katikamuda uliopewa hivyo jitahidi kutekeleza maagizo yetu ili kuiepusha Tanzania na damu nyingi itakayomwagika” akasema kiongozi Yule na kukata simu
Rais akatoa kitambaa na kujifuta jasho.
“ You did great Mtr President” akasema mkurugenzi
“ Sikutegemea kabisa kama ningeweza kufikia makubaliano na magaidi.Moyo unaniuma sana nikimfikiria mwanangu. Sitaki mwanangu apotee lakinisiko tayari kuingia katika mgogoro na kumkabidhi Yasin kwa magaidi.Tafadhali mkurugenzi jaribu kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha wasichana wote wanakombolewa ndani ya masaa haya mawili yaliyobaki.Vinginevyo wote watauawa” akasema rais kwa uchungu
“ Tutajitahidi mheshimiwa rais.Ndani ya msaa hayo mawili tutakuwa tumepiga hatua kubwa “
“ Ok mkurugenzi,nifahamishe kila kitakachokuwa kinaendelea” akasema rais na kutoka mle ofisini akaelekea katika gari lake na kuondoka kurejea ikulu

***************************

Baada ya kutoka katika kikao na rais ,waziri mkuu akaelekea ofisni kwake kichwa chake kikiwa kizito kwa mawazo mengi aliyokuwa nayo.Kitu kikubwa kilichotawala kichwa chake kwa wakati huu ni picha ya mwanae Grace ambaye anashikiliwa na kikundi cha magaidi.
‘ Sintakubali kamwe mwanangu achinjwe kama kuku.Ni mwanangu wa pekee na sina mtoto mwingine zaidi yake kwa hiyo lazima nifanye kila juhudi ya kumuokoa.Chochote kinachowezekana kufanyika ili kumuokoa mwanangu niko tayari kukifanya lakini siwezi kukaa na kushuhudia katika televisheni mwanangu akichinjwa kama kuku.Siwezi kamwe kuvumilia jambo kama hilo.I must do something” akawaza waziri mkuu kuchukua siku yake akampigia simu Mr MeshackJumbo,mkurugenzi wa zamani wa idara ya ujasusi wa Taifa nakumuomba wakutane kwa siri bila ya mtu yeyote kujua.Hakutaka kupoteza muda ofisini kwake akatoka akaingia garini na kuelekea mahala walikopanga wakutane na Mr Jumbo.

WAZIRI MKUU ANATAKA KUONGEA NININA MESHACK JUMBO? TUKUTANE TENASEHEMU IJAYO……………
 
BRING BACK OUR GIRLS

SEHEMU YA 4

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Baada ya kutoka katika kikao na rais ,waziri mkuu akaelekea ofisni kwake kichwa chake kikiwa kizito kwa mawazo mengi aliyokuwa nayo.Kitu kikubwa kilichotawala kichwa chake kwa wakati huu ni picha ya mwanae Grace ambaye anashikiliwa na kikundi cha magaidi.
‘ Sintakubali kamwe mwanangu achinjwe kama kuku.Ni mwanangu wa pekee na sina mtoto mwingine zaidi yake kwa hiyo lazima nifanye kila juhudi ya kumuokoa.Chochote kinachowezekana kufanyika ili kumuokoa mwanangu niko tayari kukifanya lakini siwezi kukaa na kushuhudia katika televisheni mwanangu akichinjwa kama kuku.Siwezi kamwe kuvumilia jambo kama hilo.I must do something” akawaza waziri mkuu kuchukua siku yake akampigia simu Mr MeshackJumbo,mkurugenzi wa zamani wa idara ya ujasusi wa Taifa nakumuomba wakutane kwa siri bila ya mtu yeyote kujua.Hakutaka kupoteza muda ofisini kwake akatoka akaingia garini na kuelekea mahala walikopanga wakutane na Mr Jumbo.

ENDELEA……………………

Meshack Jumbo,mkurugenzi wa zamani wa idara ya uajsusi wa Taifa,aliwasili katika makazi ya waziri mkuu kuitikia mwito wa waziri mkuu aliyetaka waonane kwa dharura .Tayari walinzi walikuwa na taarifa zake hivyo wakamruhusu apite bila kipingamizi chochote.Alipokewa na mtumishi wa waziri mkuu na kupelekwa ndani ambako tayariw aziri mkuu alikuwa akimsubiri.
“ Meshack Jumbo !!..akasema waziri mkuu huku wakipeana mikono na kusalimiana.
“ Hallo Mheshimiwa waziri mkuu.Habari za siku?
“ habari za siku nzuri Meshack.Habari za maisha? Umekuwa mtu adimu sana kuonekana siku hizi”
“ Ni kweli mkuu,kwa sasa nimejichimbia katika shughuli zangu mbali mbali za kilimo na ufugaji,nina shamba nalima pamoja na kufuga,kuku,mbuzi,ng’ombe n.k Karibu utembee siku moja” akasema Meshack Jumbo
“ Ahsante sana Meshack.Nitakuja kutembea siku moja na mimi nijifunze machache ili hata nikistaafu niwe na kitu cha kufanya” akasema waziri mkuu halafu kikapita kimya kifupi
“ Meshack nimekuita kwa dharura kuna jambo nataka tuongee,naomba tuelekee katika chumba cha maongezi ya faragha” akasema waziri mkuu kisha wakainuka na kuelekea katika chumba cha maongezi ya faragha
“ Ndiyo mheshimiwa waziri ,nimeitika wito wako wa dharura” akaanzisha mazungumzo Meshack Jumbo.
“ MeshackJumbo nimekuita hapa kutokana na jambo ambalo limetokea na linaloendelea hapa nchini.Natumai umekwisha lisikia.”
“ Nimesikia mheshimiwa waziri.Ni jambo la kustusha mno.Mmekwisha fahami ni nani waliofanya kitendo hiki ?”
“ Waliofanya kitendo hicho ni kikundi cha kigaidi cha Alshabaab ambao wanadai kuachiwa huru kwa kiongozi wao Yasin ambaye anashikiliwa na mahakama yaAafrika.Wametoa muda wa saa tatu kwa kiongozi wao awe ameachiwa vinginevyo damu itaendelea kumwagika.Wataendelea kuwachinja watoto waliowateka kila baada ya dakika ishirini na hadi hivi sasa tayari wamekwisha chinja watoto wanne na bado wanaendelea kuwashikilia mateka wajumbe zaidi ya mia tatu katika ukumbi wa mikutano wa KICC. Arusha.Watu wengi wameuawa pia katika shambulio jingine walilolifanya katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru baada ya kuachia hewa ya sumu.Bado wametishia kuachia hewa hiyo ya sumu katika sehemu mbali mbali hapa nchini endapo matakwa yao yasipotimizwa” akasema waziri mkuu
“ Mhh !! Hili ni janga kubwa sana.Taifa linapitia wakati mgumu mno.Mpaka hivi sasa mmefikia wapi kuhusiana na kuwapata wasichana waliotekwa na kuzuia mashambulizi zaidi toka kwa Alshabaab ? Akauliza Meshack Jumbo
“ Mpaka hivi sasa bado hakuna hatua yoyote kubwa iliyopigwa.Hatujui wasichana hao wako wapi,na hakuna dalili zozote kwamba tunaweza kuwapata ndani ya muda huo mfupi walioutoa.”
Meshack Jumbo akakuna kichwa .Ilionyesha wazi mambo yale yalikuwa magumu hata kwake pia.Waziri mkuu akaendelea.
“ Meshack Jumbo,hawa magaidi si watu wa kufanyia masihara hata kidogo.Tayari wamekwisha jitolea kufa na wako tayari kuua muda wowote ule.Wakisema wataua watoto waliowateka ,hawatanii,wataua kweli na tayari wamekwisha ua wanne” akasema waziri mkuu kwa uchungu
“ Hakuna namna ambayo mmeweza kufanya ya kuongea na magaidi hawa ili kujaribu kuvuta muda wakati mikakati ya kufahamu mahala walipo watoto ikiendelea? Akauliza Meshack Jumbo
“ Hilo ndilo haswa nililokuitia hapa.Tulikuwa katika kikao na kiongozi wa magaidi hao akampigia simu mheshimiwa rais na kumtaka amuachie kiongozi wao ili awaachie huru watoto waliowateka pamoja na wajumbe wanaoshikiliwa katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha KICC.Rais alikataa kata kata kuafikiana chochote na magaidi wale.Rais wa marekani pia alimpigia simu akamtaarifu kwamba kuna kikosi cha wanajesh zaidi ya mia mbili ambacho anataka kukituma ili kuja kuongeza nguvu lakini rais alikataa pia.”
“ What ?! Meshack Jumbo akashangaa
“ Kwa nini alifanya vile? Hikisi kipindi cha kukataa msaada wowote ambao unapewa.Alitakiwa kuupokea msaada huo toka Marekani.Wale wenzetu wamekuwa wakipigana vita ya ugaidi kwa miaka mingi na wana uzoefu wa kutosha na vifaa pia.Msaada wao unahitajika sana katika kipindi hiki. Vile vile rais alitakiwa kuzungumza vizuri na kiongozi wa magaidi ili kujaribu kuvuta muda na kuvipavikossi vyetu nafasi ya kuweza kupanga mikakati.”
“ That’s the problem with our President.Sote tunafahamu namna alivyo mtu wa misimamo na katu hataweza kuzungumza wala kukubaliana chochote na magaidi na wataendelea kumwaga damu kama walivyoahidi endapo matakwa yao yasipotekelezwa” akasema waziri mkuu
“ Idara ya ujasusi inafanya kazi gani? Haikuweza kupata taarifa za shambulio hili kabla halijatokea? Wamefikia wapi hivi sasa katika kufahamu ni wapi walipo watoto waliotekwa? Nina amini lazima kulikuwa na uzembe mkubwa kwani haiwezekani shambulio kubwa kama hili lifanyike bila ya idara ya ujasusi kuwa na taarifa.Wale wana rasilimali zote ambazo zinaweza kusaidia kufahamu na kudhibiti mashambulio kama haya kabla hayajatokea” akasema Meshack Jumbo
“ Sina hakika kama walikuwa na taarifa zozozte za kiintelijensia kuhusuana na shambulio hili nawala sijui mahalq walikofikia hadi hivi sasa.Meshack wewe uliiongoza idara ya ujasusi kwa mafanikio makubwa sana na kwa sasa taifa linakuhitaji mno.”
“ nakusikiliza mkuu,kama kuna lolote ninaloweza kusaidia katika suala hili niko tayari kufanya hivyo” akasema Meshack Jumbo
“ Mr Jumbo,nimekuita hapa kwa sababu nahitaji mno msaada wako.Mwanangu ni mmoja kati ya wasichana waliotekwa nyara na magaidi.Binti wa rais pia ni mmoja wao wa mateka.Jumbo wewe ni mzazi na unaelewa uchungu wa mtoto.Ninaamini hauko tayari kumuona mwanao akichinjwa kama kuku na kuonyeshwa katika mtandao.Huu ni ukatili uliovuka mipaka na hakuna mzazi yeyote anayeweza kukubali kitu kama hiki kimtokee mwanae kwa hiyo basi nimekuita hapa ili kwa pamoja tusaidiane namna ya kufanya.”
“ Ni kweli mkuu,kama mzazi ni vigumu sana kuona mwanao akichinjwa kama kuku na kuonyeshwa mtandaoni.Ni jambo linalouma sana.Unataka tufanye nini mheshimiwa waziri mkuu?
“ Jumbo wewe ni mzoefu sana katika msauala kama hayana vile vile wewe ni rafiki yangu mkubwa.Kabla hujastaafu kazi kuna mambo mengi ambayo tumeyafanya pamoja ,naomba unisaidie pia katika hili,kama ndugu yako,kama rafiki yako..Nataka unisaidie namna yoyote inayowezekana ili kuzuia watoto wetu wasiendelee kuuawa.”
“ nakusikiliza waziri mkuu na niko tayari kukusaidia kwa lolote lile linalowezekana kufanyika”
“ Ahsante Meshack.Siko tayari mwanangu auawe na magaidi huku nikiangalia kwa hiyo ninataka kufanya jambo ambalo litamuokoa mwanangu na wasichana wote waliotekwa.”
“jambo gani hilo waziri mkuu unafikir ia kulifanya?
“ Nataka kumkabidhi Yasin kwa magaidi “
“ What ?! .. Meshack Jumbo akashangaa.
“ Nadhani umenisikia vizuri Mr Jumbo.Nataka kuwapa magaidi kiongozwao ili kuwaokoa wasichana wetu na kusitisha mashambulio zaidi”
Meshack Jumbo akahisi kijasho chembamba kikimchuruzika.


TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO……………………..
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA SDEHEMU ILIYOPITA
“ Jumbo wewe ni mzoefu sana katika msauala kama hayana vile vile wewe ni rafiki yangu mkubwa.Kabla hujastaafu kazi kuna mambo mengi ambayo tumeyafanya pamoja ,naomba unisaidie pia katika hili,kama ndugu yako,kama rafiki yako..Nataka unisaidie namna yoyote inayowezekana ili kuzuia watoto wetu wasiendelee kuuawa.”
“ nakusikiliza waziri mkuu na niko tayari kukusaidia kwa lolote lile linalowezekana kufanyika”
“ Ahsante Meshack.Siko tayari mwanangu auawe na magaidi huku nikiangalia kwa hiyo ninataka kufanya jambo ambalo litamuokoa mwanangu na wasichana wote waliotekwa.”
“jambo gani hilo waziri mkuu unafikir ia kulifanya?
“ Nataka kumkabidhi Yasin kwa magaidi “
“ What ?! .. Meshack Jumbo akashangaa.
“ Nadhani umenisikia vizuri Mr Jumbo.Nataka kuwapa magaidi kiongozwao ili kuwaokoa wasichana wetu na kusitisha mashambulio zaidi”
Meshack Jumbo akahisi kijasho chembamba kikimchuruzika.

ENDELEA………………….
“ Umenielewa Meshack ? akasema waziri mkuu.Meshack Jumbo alisimama akainama na kufikiri kwa muda halafu akasema
“ Mheshmiwa waziri mkuu,hata mimi nimeguswa sana na jambo hili na niko tayari kutoa msaada wangu mkubwa kadiri inavyowezekana lakini kwa jambo hilo unalotaka tulifanye haliwezekani na ni la hatari kubwa sana mheshimiwa waziri mkuu.”
“ Mr Jumbo ninafahamu kwamba hili ni jambo la hatari lakini kwa sasa hatuna budi kulifanya.Hilo ndilo suluhisho pekee kwa sasa ambalo litaweza kuzuia mauaji ya wasichana wetu na kuzuia mashambulio mengine kuendelea.” Akasema waziri mkuu
Meshack Jumbo akafikiria kwa muda na kusema
“ Mheshimiwa waziri mkuu,Yasin ni mtuhumiwa katika mahakama ya afrika.Hakuna namna ya kuweza kufanya ili kumpata na kumkabidhi kwa magaidi.Kwanza mahala alipo si sehemu ambayo mtu unaweza ukaingia na kumchukua kirahisi .Ninachoweza kusema ni kwamba suala hili haliwezekani mheshimiwa waziri mkuu”
“ Jumbo wewe ndiye tumaini langu la mwisho na ndiyo maana nimekuita hapa .Tafadhali naomba ulichukulie suala hili kama la kwako.Chukulia binti yako ni miongoni mwa mateka na muda wowote yuko katika hatari ya kuchinjwa na kuonyeshwa moja kwamoja katika mtandao namna anavyotenganishwa kichwa na kiwili wili.Unafikiri ungefanyaje ? Right now our only option is to give them what they want.They want Yasin and we must give them .Ndiyo ni suala ambalo adhabu yake ni kubwa lakini historia itatukumbuka kwamba tulifanya hivi kwa ajili ya kuwaokoa watoto wetu na kuzua umwagikaji mkubwa wa damu nchini.Haiwezekani watoto wetu wanachinjwa and we are not doing anything.We have to do something for our children and for our nation.” Akasema waziri mkuu..Bado Meshack Jumbo alikuwa ameinama akifikiria.
“ Mr Jumbo nielewe kwamba hakuna suluhisho lingine kwa sasa zaidi ya hili ninalokwambia.Wewe una mbinu na unafahamu ni namna gani tunaweza kufanya kumpata Yasin.Sema chochote nitakitekeleza.Please Meshack I need your help”
Meshack Jumbo akainama akafikiri kwa muda na kusema
“ mheshimiwa waziri mkuu si kwamba sijaguswa na jambo hili lakini kila nikijaribu kufikiria namna ya kulitekeleza jambo hilo nakosa jibu.Lakini kuna jambo moja ninalifikiria.”
“ Jambo gani hilo Meshack?akauliza waziri mkuu
“ Kuna mtu ambaye anaweza kuwa na msaada mkubwa kwetu kwawakati kama huu.?
“ Ni nani huyo ?
“ Kuna kijana mmoja anaitwa Tonny.Kabla sijastaafu yeye ndiye alikuwa kijana tegemeo katika idara ya ujasusi ya Taifa na ndiye aliyefanikiwa kumkamata Abdool bins ahel gaidi aliyefanya mashambulio katika balozi za Marekani jijini Dar es salaam na Nairobi.Ni Tonny ndiye aliyezima mpango wa kikundi cha kigaidi cha Alqaeda wa kumtorosha Abdool.Ni kijana mahiri sana na anayeweza kuwa na msaada mkubwa sana kwetu” akasema Meshack Jumbo
“ Yuko wapi huyo Tonny? Wakati huu tunamuhitaji sana mtu kama huyu” akasema waziri mkuu
“ Kwa bahati mbaya sana Tonny anashikiliwa katika gereza la Uwangwa na ninadhani mpaka hivi sasa bado hajaachiwa”
“ Anashikiliwa kwa kosa gani? Akauliza waziri mkuu
“ Kwa kosa la kuhatarisha usalama wan chi.Alikuwa na taarifa muhimu zenye kuhusiana na usalama wa nchi lakini hakuzifikisha sehemu husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi.”
“ Una hakika bado atakuwa katika gereza la Uwangwa?
“ Nina uhakika huo kwa sababu kama angekuwa ameachiwa basi ningejua,lakini mpaka sasa sina taarifa zozote za kuhusiana na kuachiwa kwake.”
“ Una hakika anaweza akawa na msaada kwetu huyu kijana endapo tukifanya mpango wa kumtoa huko gerezani ili aweze kuja kutusaidia?
“ Nina uhakika mkubwa.Ninamfahamu Tonny kiundani na ninauelewa uwezo wake katika mambo kama haya.Atakuwa msaada mkubwa sana kwetu na kwa taifa kwa ujumla.Kama kuna uwezekano wa kumtoa basi ifanyike hivyo mapema”
“ Ok niambie tutampataje huyo kijana?
“ Tunachotakiwa kufanya kwanza ni kuwasiliana na mkuu wa gereza la uwangwa Insector Alfred Tijenda na kupata uhakika kama Tonny yuko pale halafu baada ya hapo mimi nitaelekea huko gerezani na kumchukua Tonny nitakuja naye hapa tutaongea naye na kumpa jukumu hili.Nakuhakikishia mheshimiwa waziri mkuu.Tonny hashindwi na kitu.Nina hakika ndani ya muda mfupi kuna mambo ambayo anaweza akayafanya na sote tukabaki tunashangaa” akasema meshackJumbo.Bila kupoteza muda waziri mkuu akachukua simu yake na kumpigia katibu wake akiomba amuunganishe na mkuu wa gereza la Uwangwa.Baada ya dakika mbili tayari akawa ameungwanishwa
“ hallo mheshimiwa waziri mkuu” akasema mkuu wa gereza la uwangwa
“ Heshima yako mkuu? Niko hapa pamoja na MeshackJumbo nadhani unamfahamu”
“ Tunafahamiana lakini ni muda mrefu sasa hatujaonana.Nilisikia alistaafu”
“ Inspector Alfred .Jambo lililonfanya nikupigie simu ni kutaka kupata taarifa za kijana mmoja anaitwa Tonny ambaye anashikiliwa hapo gerezani kwa kosa la kuhatarisha usalama wa n chi.Aliwahi kufanya kazi na idara ya ujasusi wa taifa.je bado yuko hapo gerezani?
“ Mheshimiwa waziri mkuu,Tonny bado yuko hapa na siku ya jana alikuwa anahitaji kuonana nawe kwa ajili ya kuzungumza jambo la msingi sana kuhusiana na tukio lililotokea jijini Arusha lakiniwasaidizi wako wakasema kwamba hauko tayari kuonana naye”
“ What?!.. Sijapata taarifa zozote kwamba ninatakiwa kuonana na mtu kama huyo,laiti kama ningepata taarifa hizo nisingesita kuonana naye.”
“ Mheshmiwa waziri mkuu,Tonny alikuwa anajaribu kutoa angalizo kuhusu kutokea kwa shambulio jijini Arusha .Hata mimi nilimpuuza lakini baada ya kusikia kilichotokea,sasa ninamuamini”
“ Ouh Mungu wangu kumbe Tonny alikuwa na taarifa za kuwepo kwa shambulio kama hilo? Kwa nini basi idara ya ujasusi walishindwa kuwa na taarifa kama hizo wakati wana kila kitu? Akauliza waziri mkuu
“Siwezi kufahamu mheshimiwa waziri mkuu”
“ Alfred kuna jambo moja ambalo nimekupigia simu kukuomba.”
“ Omba chochote mheshimiwa waziri mkuu”
“ Ninamuomba Tonny ili atusaidie katika wakati huu mgumu na baada ya kumaliza kazi yake nitamrejesha tena kwako ”
“ Mheshimiwa waziri mkuu,Tonny amewekwa katika kundi la watu hatari kwa taifa kwa hiyo kumuachia hivi hivi bila kufuata taratibu ni kuniweka mimi na sisi sote katika kesi kubwa ya kuhatarisha usalama wa n chi”
“ Nalifahamu hilo ndugu yangu lakini kwa sasa hatuna namna nyingine ya kufanya.Taifa linamuhitaji mno Tonny kuliko wakati wowote ule.Watoto wetu wanashikiliwa mateka na magaidi na tayari wamekwisha anza kuchinjwa,vile vile wajumbe zaidi ya mia tatu wanashikiliwa katika ukumbi wa mikutano wa KICC na endapo hakuna juhudi za kupambana na magaidi hawa ndani ya muda mfupi ujao basi wote tutawapoteza” akasema waziri mkuu
“ Mr Alfred Tijenda ,Meshack Jumbo hapa ninaongea” akaingilia Meshack Jumbo
“ Meshack Jumbo nafurahi kukusikia tena.” Akasema Alfred Tijenda mkuu wa gereza la Uwangwa.
“ Alfred,naomba nikuweke wazi kwambaTonny anahitajika sana kwa sasa.Taifa linapitia wakati mgumu na mchango wake unahitajika kwa hiyo naomba jambo hili tulifahamu sisi watatu tu,mimi wewe na mheshimiwa waziri mkuu na baada ya kazi kukamilika ninakuahidi nitamrejesha Tony gerezani mimi mwenyewe.” Akasema Meshack Jumbo
Kimya che sekunde kadhaa kikapita na Alfred Tijenda akasema
“ ok ,kutokana na uzito wa jambo hili nitatumia uwezo wangu kumtoa Tonny .”
“ Ahsante sana Alfred.Meshack atakuja kumchukua Tonny muda si mrefu” akasema waziri mkuu na kukata simu
“ Hakuna muda wa kupoteza.Ngoja nielekee uwangwa Prison kumchukua Tonny” akasema Meshack Jumbo
“ Ahsante sana Meshack Jumbo”

WAZIRI MKUU ANAFANYA KILA LINALOWEZEKANA ILI KUHAKIKISHA WATOTO WALIOTEKWA WANAKOMBOLEWA. ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII..
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 6
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Alfred,naomba nikuweke wazi kwambaTonny anahitajika sana kwa sasa.Taifa linapitia wakati mgumu na mchango wake unahitajika kwa hiyo naomba jambo hili tulifahamu sisi watatu tu,mimi wewe na mheshimiwa waziri mkuu na baada ya kazi kukamilika ninakuahidi nitamrejesha Tony gerezani mimi mwenyewe.” Akasema Meshack Jumbo
Kimya che sekunde kadhaa kikapita na Alfred Tijenda akasema
“ ok ,kutokana na uzito wa jambo hili nitatumia uwezo wangu kumtoa Tonny .”
“ Ahsante sana Alfred.Meshack atakuja kumchukua Tonny muda si mrefu” akasema waziri mkuu na kukata simu
“ Hakuna muda wa kupoteza.Ngoja nielekee uwangwa Prison kumchukua Tonny” akasema Meshack Jumbo
“ Ahsante sana Meshack Jumbo”

ENDELEA……………………..

“ Usijali mheshimiwa waziri mkuu.Nisubiri nitarejea baada ya muda mfupi” akasema Meshack Jumbo na kutoka kwa kasi akaingia katika gari lake
“ Tunaelekea Uwangwa Prison “ Meshack Jumbo akamwambia dereva wake na safari ikaanza
“ .Inaonekana uongozi ulioko madarakani hivi sasa katika idara ya ujasusi ya taifa wame msahau kabisa Tonny.Hawafahamu mchango wake katika taifa.Mimi nilimuweka kizuizini kwa muda ili kumuepusha na mashitaka ambayo angeweza kufunguliwa ya kuhatarisha usalama wa nchi .Wakati ninamaliza uongozi wangu niliwataarifu waliobaki kuhusu uwepo wa Tonny kizuizini na wakaniahidi kwamba watashughulikia suala lake lakini nashangaa mpaka hivi sasa hakuna juhudi zozote zilizofanywa kumtoa kizuizini.This is over.I’m going to free him today.” Akawaza meshack Jumbo .
“ kama Tonny angekuwepo natumai jambo hili lisingefika hapa lilipofika. Ana vyanzo vIngi vya taarifa toka sehemu mbali mbali duniani .Sina hakika kama atakubali kuifanya kazi hii kutokana na namna alivyotendewa lakini nitajaribu kumshawishi akubali ingawa haitakuwa rahisi” akaendelea kuwaza Meshack Jumbo huku gari likienda kwa kasi kuelekea Kigamboni.
“ Nina mashaka na uwezo wa mkurugenzi wa idara ya ujasusi katika kushughulikia masuala makubwa kama haya.kwa nini aliacha jambo kama hili litokee? Kwa nini hakuwa na taarifa za kuwepo kwa shambulio kama hili? Haya ni maswali ambayo anatakiwa aulizwe kwa sababu haiwezekani watu wakapanga mashambulio kama haya na kuyatekeleza kama vile nchi haina idara ya ujasusi yenye kila aina ya miundo mbinu ya kuwawezesha kunasa taarifa za mipango ya namna hii.Huu ni udhaifu mkubwa wa idara hii.Wakati wa uongozi wangu mambo kama haya hayakuwepo” akawaza Meshack
Kutokana na mwendo mkali waliokuwa wakienda,iliwachukua dakika arobaini na mbili kuwasili Uwangwa Prison. Meshack Jumbo alifahamika sana mahala hapa,akasalimiana na askari waliokuwepo mapokezi na kisha akapelekwa moja kwa moja katika ofisi ya mkuu wa gereza la Uwangwa.
“ Hallo Meshack Jumbo” akasema Alberto Mkuruga mkuu wa gereza la Uwangwa baada ya Meshack Jumbo kuingia ofisini kwake
“ Hallo Alberto” akasema Meshack na kupeana mikono
“ Karibu sana Meshack Jumbo.Nimefurahi kukuona tena.Toka umestaafu kazi hatujawahi kuonana.Maisha yanakwendaje baada ya kustaafu utumishi ? akauliza Alberto
“ Maisha yanakwenda vizuri lakini inategemea na namna ulivyojipanga.Kwa sasa ninajishughulisha na miradi ya kilimo na ufugaji.”
“ Hongera sana Meshack.Nitakuja kujifunza kwako kuhusiana na ufugaji kwani hata sisi tuko mbioni kustaafu utumishi”
“ Unakaribishwa sana Alberto” akasema Meshack Jumbo na kimya kifupi kikapita.
“ Alberto hatuna muda mrefu sana wa maongezi nadhani unafahamu kilichonileta hapa” akasema Meshack Jumbo
“ Nafahamu Mr Jumbo .Lakini kabla ya yote kuna jambo a nataka kufahamu kuhusiana na huyu kijana Tonny”
“ Jambo gani unalotaka kufahamu? Akauliza meshack Jumbo
“ This guy Tonny do you trust him?
“ I trust him with my life. Ni kijana wa aina yake ambaye ana uwezowa ajabu.Sijawahi kufanya kazi na mtu wa aina yake.Kwa nini unaniuliza?
“ Nashukuru kusikia hivyo.Laiti ningepata uhakika toka kwako mapema kwamba ni mtu anayepaswa kuaminia basi nisingekuwa na shaka naye na pengine haya yaliyotokea yasingetokea.Nchi isingetikiswa na mashambulio makubwa yaliyotokea” akasema Alberto
“ Kwa nini unasema hivyo Alberto? Akauliza MeshackJumbo
“ Tonny alitoa angalizo mapema kuhusiana na jambo hili lililotokea lakini nilipuuzia.Alinitaka nimuachie huru ili aweze kuzuia jambo hili lisitokee lakini sikumuamini nilidhani ni moja ya janja yake ya kutaka kutoroka.”
“ Unataka kuniambia kwamba tayari alikuwa na taarifa za tukio hili ? akauliza Meshack Jumbo
“ Ndiyo alikuwa na taarifa.Sijui alizipata vipi lakini aliniambia kwamba kuna jambo zito litatokea na sikumuamini.”
“ Ouh Alberto hilo ni kosa kubwa sana ulilifanya.Ulitakiwa umuamini” akasema Meshack
“ Isingekuwa rahisi kumuamini kwa haraka Meshack.Tonny aliletwa hapa kwa kosa la kuhatarisha usalama wa nchina faili lake linasema kwamba ni mtu hatari ambaye haruhusiwi kupewa nafasi yoyote ile.Na mimi nilifuatamaelekezo hayo na sikutaka kuhatarisha usalama wan chi.Laiti ungeniambia mapema kwamba ni mtu ambaye taifa linamuhitaji sana basi ningemsikiliza .Alipoona nimempuuza alinitaka niwasiliane na waziri mkuu .Alitaka amweleze waziri mkuu kuhusiana na tukio hili lakini wasaidizi wa waziri mkuu wakasema kwamba kwa wakati ule waziri mkuu alikuwa na kazi nyingi na asingeweza kuonana na mtu yeyote Yule.” Akasema Alberto
“ Alberto tayari makosa yamekwisha fanyika,hatuna muda wa kuendelea kupoteza hapa.Nipeleke kwa Tonny tuangalie namna tunavyoweza kuliokoa taifa toka katika maangamizi makubwa” akasema Meshack Jumbo.Wakatoka mle ofisini na kutembea kwa kasi kuelekea mahala alikofungiwa Tonny.
“ Umewahi kuonana naye toka alipowekwa kizuizini? Akauliza Alberto
“ Hapana sijawahi kuonana naye hata mara moja” akasema Meshack.
“ Tonny ametelekezwa hapa.Hakuna hata mtu mmoja anayekuja kumuangalia ,inaonekana hata ndugu zake hawafahamu mahala alipo.Lakini kwa huduma tunamhudumia vizuri anapata kila kitu anachokihitaji” akasema Alberto
“ Nilifanya makosa sana kustaafu na kumuacha Tonny humu ndani.Nilipaswa kuhakikisha kwamba anatolewa kabla sijamaliza muda wangu wa utumishi.Uongozi wa sasa umemsahahu kabisa na hauna habari naye tena.He must be angry with me,angry with us,angry with his country.” Akasema Meshack
Waliyapita mageti kadhaa yenye askari hadi kufikia mahala aliko Tonny
“ Mhh sikutegemea kama Tonny angewekwa mahala kwenye ulinzi mkali namna hii”
“ Eneo hili ndiko wanakowekwa wale watu ambao ni hatari kwa taifa na ndiyo maana unaona ulinzi wake ni mkubwa sana.” Akasema Alberto na kusimama nje ya chumba cha Tonny.
“ We’re here” akasema Alberto.Akamuamuru askari aliyekuwa amesimama nje ya mlango ule akiwa na silaha aufungue mlango.Akabonyeza namba Fulani katika kisanduku kilichokuwa nje ya mlango na mlango ukafunguka.Tonny alikuwa amejilaza kitandani akitazama Runinga.Alberto na MeshackJumbo wakaingia mle chumbani ,wakasimama kwa sekunde kadhaa kati kati ya chumba wote wakimtazama Tonny ambaye hakusumbuka kuwatazama.Aaliendelea kuelekeza macho yake runingani
“ Hallo Tonny” akasema Meshack Jumbo” Tonny hakujibu kitu aliendelea kuitazama runinga.MeshackJumbo akamgeukia Alberto na iumfanyia ishara atoke nje na lango likafungwa.Meshack Jumbo akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Tonny nafahamu mimi ni mtu pekee ambaye hupendi na hukutegemea kuniona hapa muda huu.Nafahamu nilichokifanya na hakuna siku inayopita bila kukuwaza na kujilaumu kwa jambo hili laiti kungekuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi basi ningefanya ili usiweze kuingia kizuizini lakini kwa wakati ule hakukuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya h ii. Sikutegema kama ungekaa kwa muda mrefu namna hii.Bbaada tu ya kumaliza muda wangu wa utumishi nilipokuwa nakabidhi ofisi nilimkabidhi pia mkurugenzi mpya suala lako na kumtaka ahakikishe kwa kila namna anakutoa humu gerezani haraka iwezekanavyo.Aliniahidi kulifanyia kazi lakini nasikitika kwamba alilipuuzia suala hili na kukuacha ukiendelea kuteseka gerezani hadi leo hii.I’m so sorry for that Tonny” akasema MeshackJumbo.Tonny akazima runinga na kumgeukia Meshack Jumbo
“ sorry ? You are sorry? Akauliza Tonny
“ Unadiriki kusema samahani ? akauliza tena Tonny huku akiinuka na kukaa kitandani .Uso wake ulikuwa umejikunja kwa hasira.MeshackJumbo akaogopa sana kwani alimfahamu Tonny alivyo pindi akiwa amekasirika
“ Baada ya yote niliyoyafanya kwa taifa hili haya ndiyo malipo yake.Nimejitolea kila kitu kwa ajili ya nchi y angu lakini malipo yakeni kunitelekeza gerezani !!..Thank you so much.” Akasema Tonny.Meshack Jumbo akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Tonny,najua mimi na wewe kwa sasa hatutazamani vizuri usoni lakini tuyaweke hayo pembeni .Jambo kubwa lililonileta hapa ni kuja kukutaarifu kwamba tulikosea lakini taifa linakuhitaji kwa sasa kuliko mtu mwingine yeyote Yule.” Akasema na kutulia kidogo halafu akaendelea.
“ Taifa letu limeshambuliwa kwa mara nyingine tena na magaidi .Ni shambulio kubwa ambalo halijawahi kutokea hapa nchini.Magaidi wameteka watoto wa kike zaidi ya ishirini na hivi tunavyoongea tayari wamekwisha wachinja watoto wanne na wataendelea kuwachinja watoto hao kila baada ya dakika thelathini hadi rais atakapo timiza hitaji lao.Miongoni mwa watoto waliotekwa yumo pia mtoto wa rais na mtoto wa waziri mkuu.” Meshack akanyamaza akamtazama Tonny halafu akaendelea
“ Mgaidi vile vile wanawashikilia mateka wajumbe wa mkutano mkuu wa Sullivan katika ukumbi wa mikutano wa KICC jijini Arusha.Kama hiyo haitoshi walitumia pia gesi ya sumu na kuua mamia ya watu katika hospitaliya mkoa ya Mount Meru na wametishia kuiachia gesi hii ya sumu katika sehemu mbali mbali za nchi na kuua mamia ya raia wasio na hatia.Tonny damu nyingi inamwagika ,raia wasio na hatia wanaendelea kuuawa,na mpaka hivi sasa hakuna anayejua afanye nini.” Akasema Meshack Jumbo
“ I wish you and your fellows were the first ones to die “ akasema Tonny
“ C’mon Tonny ,this is not the time.Tutatafuta muda mwingine wa kuongelea masuala hayo lakini kwa sasa tuangalie mambo ya msingi yanayolikabili taifa” akasema Meshack Jumbo
“ Taifa ?! akauliza Tonny kwa ukali
“ Taifa lipi? Sina cha kulifanyia taifa hili.Nimekwisha wafanyia mambo mengi sana lakini haya ndiyo malipo yake ?.I’m done with you people,I’m done with the Nation.Please leave me alone ! akafoka Tonny.MeshackJumbo akamtazama kwa macho makali na kusema
“ Tonny nikwambie kitu gani unielewe kwamba damu inamagika hivi sasa nchini ?
Tonny akainuka na kumsogelea Meshack
“ Please go now !. Ondoka kabla sijabadilika na kukufanyia kitu kibaya sana “ akasema Tonny
“ No Tonny, I wont leave.Sintoondoka mpaka utakaponisikia”
“ Sitaki kukusikiliza Jumbo.I hate you ” akasema Tonny
“ Nakubali ukinichukia mimi lakini fikiria kuhusu wale watoto wadogo wanaoendelea kuuawa kila baada ya dakika thelathini.Tonny nimekulea kama mwanangu katika kazi hii ya ujasusi.Ninakufahamu vyema namna unavyowachukia magaidi na hauko tayari kuona wakifanikiwa katika malengo yao.Please Tonny don’t shut me down on this.Wake up be a man and fight these terrorists.” Akasema Meshack Jumbo
Tonny akakaa kitandani akainama na kuzama katika mawazo.Baada ya dakika mbili akainua uso wake uliokuwa umeloa machozi
“ What do you want from me? Akauliza Tonny.MeshackJumbo akavuta pumzi ndefu na kusema
“ We need you Tonny.We need you in this war” akasema MeshackJumbo.
“ From now you are free.You are out of this hell” akasema Meshack na kumfanya Tonny azidi kutoa machozi.Hakuwa ametegemea kama angeachiwa huru kirahisi namna ile.
“ Tonny uko huru lakini kwa sharti moja tu.”
“ Sharti gani hilo?
“ Waziri mkuu anahitaji mtoto wake akombolewe kwa gharama yoyote ile.Anahitaji kuonana nawe sasa hivi” akasema Meshack.Tonny akaiinama akafikiri tenakisha akasema
“ Ok twende nikaonane naye” akasema Tonny huku akivaa shati .

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………..
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 7
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Tonny akakaa kitandani akainama na kuzama katika mawazo.Baada ya dakika mbili akainua uso wake uliokuwa umeloa machozi
“ What do you want from me? Akauliza Tonny.MeshackJumbo akavuta pumzi ndefu na kusema
“ We need you Tonny.We need you in this war” akasema MeshackJumbo.
“ From now you are free.You are out of this hell” akasema Meshack na kumfanya Tonny azidi kutoa machozi.Hakuwa ametegemea kama angeachiwa huru kirahisi namna ile.
“ Tonny uko huru lakini kwa sharti moja tu.”
“ Sharti gani hilo?
“ Waziri mkuu anahitaji mtoto wake akombolewe kwa gharama yoyote ile.Anahitaji kuonana nawe sasa hivi” akasema Meshack.Tonny akaiinama akafikiri tenakisha akasema
“ Ok twende nikaonane naye” akasema Tonny huku akivaa shati .


ENDELEA……………………………..

Vikosi vya jeshi vilivyokuwa vimelizingira jengo la mikutano ya kimataifa la KICC vilianza kusogea nyuma kufuatia amri waliyopata toka kwa makamanda wao.Hili lilikuwa ni agizo toka kwa rais baada ya kuonywa na kiongozi wa kikundi cha magaidi kinachowashikilia mateka wajumbe zaidi ya mia tatu wa mkutano mkuu wa Sulivan.Magaidi walimuonya rais kwamba aondoe vikosi vyote vya jeshi vilivyolizunguka jengo lile vikipanga mipango ya kulivamia na kuwakomboa mateka.Magaidi walionya kwamba endapo vikosi vile visingeondolewa au jaribio lolote la kutaka kuwakomboa mateka wale basi ungekuwa ndio mwisho wao kwani wangeulipua ukumbi wote kwa bomu ambalo liko ndani ya ukumbi
“ Mheshimiwa rais una hakika kwamba huu ni uamuzi sahihi? Akauliza Dr Edward Elimule mshauri mkuu wa rais .
“ Kwa sasa hatuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuwasikiliza hawa magaidi wanachokisema ili kujaribu kuwapotezea muda na kujipanga vizuri.We must save the kids today,we must save all the hostages..” akasema mheshimiwa rais
“ Rais wa afrika ya kusini amepiga simu na amesema kwamba yuko tayari kwa msaada wowote endapo utahitajika.Rais wa Kenya pia alipiga simu na kukupa pole.Wote wako tayari kwa msaada wowote endapo utahitajika” akasema Dr Edward
“ Dr Edward, kwa sasa hatuhitaji msaada toka sehemu yoyote.Bado hatujashindwa kuwakomboa mateka.Tutatumia vikosi vyetu vya ndani na tutawadhibiti magaidi na kuwakomboa mateka wote” akasema rais
“ Nakubaliana nawe Mheshimiwa rais lakini muda waliotoa hawa magaidi ni mfupi na unazidi kuisha.Nina wasi wasi unaweza ukafika muda walioutoa na tukawa hatujafika popote .Hawa magaidi hawatanii,wataendelea kumwaga damu hadi lengo lao litimie.” Akasema Dr Edward
“ Naomba niongee na generali Sixmund” akasema mheshimiwa rais na Dr Edward akapiga simu na kumpata mkuu wa majeshi
“ Generali Sixmund yuko katika laini ya simu mheshimiwa rais” akasema Dr Edward.Rais akaisogelea meza na kuchukua mkono wa simu
“ hallo General Sixmund.Nakuomba hapa Ikulu mara moja”
“ Ok Mheshimiwa rais,nakuja sasa hivi “ akajibu Generali Sixmund na kukata simu
“ Unataka kujadili nini na General ixmund? Akauliza Dr Edward
“ Tunatakiwa tutafute kila namna ya mbinu ya kuweza kuwakomboa wmateka na kuwadhibiti magaidi.Binti yangu yuko mikononi mwa magaidi na siko tayari kumuona akichinjwa kama kuku.Nitafanya kila linalowezekana ili kumuokoa.” Akasema mheshimiwa rais.
Mlango ukafunguliwa na mlinzi wa rais akaingia
“ Mheshimiwa rais kuna video imerushwa tena katika mtandao.” Akasema Yule mlinzi.Mheshimiwa rais na Dr Edward wakatoka na kuingia katika chumba cha mikutano ili kuitazama video ile.Ilikuwa ni video iliyochukuliwa ndani ya ukumbi wa mikutano wa KICC.Mateka wote walionekana wakiwa wamekusanywa sehemu moja huku wakilindwa na watu zaidi ya saba wenye silaha nzito na waliojifunga mabomu mwilini.Mtu mmoja aliyejifunga kitambaa usoni alikuwa mbele ya kamera akitoa onyo.Kama ilivyokuwa kwa Yule kiongozi wa kikundi hiki aliyeonekana katika video zilizopita huyu naye alitumia lugha ya Kiswahili
“ Ndugu watanzania na dunia kwa ujumla,mimi ni Habib Aljabir Samir ambaye ninaongoza mapambano toka ndani ya ukumbi wa mikutano wa KICC.Humu ndani tunawashikilia wajumbe zaidi ya mia tatu wa mkutano wa Sulivan.Wote wako salama kabisa na hakuna hata mmoja aliyedhurika na hatutamdhuru mtu yeyote endapo tutatimiziwa matakwa yetu.Mkuu wetu amekwisha muonya rais wenu kuhusu jaribo lolote la kutaka kuingia humu ndani kuwakomboa mateka hawa.Endapo mtajaribu kufanya jaribio lolote la kuwakomboa mtakuwa mmewaangamiza.Vijana wangu wote wamejifunga mabomu mwili mzima na wako tayari kufa muda wowote na vile vile tuna bomu liko humu ndani na hatutasita kuulipua ukumbi wote endapo mtapuuzia onyo hili.Onyo lingine tunamtaka rais wenu aamrishe vikosi vyake vya jeshi vinavyolikaribia jengo hili virudi nyuma kabisa na kuliacha jengo tupu.Narudia tena kuwasisitiza kwamba ndugu zenu wote wako salama na wataendelea kuwa salama mpaka hapo rais wenu atakapotekeleza matakwa yetu” akasema Habib na video ile ikaisha
“ Hawa jamaa inaonekana walitumia muda mrefu kujiandaa kwa shambulkio hili.Sielewi ni kwa nini vikosi vyetu vya usalama havikuweza kuufahamu mapema mpango wa shambulio kama hili.Huu ni udhaifu mkubwa sana katika idara zetu za usalama ” akasema Mheshimiwa rais.
“ Kweli mheshimiwa rais kuna udhaifu katika vyombo vyetu vya usalama kiasi kwamba vimeshindwa kabisa kugundua mipango ya kuwepo kwa shambulio kubwa kama hili. Hili ni suala ambalo linahitaji kuutizama upya mfumo wetu wa ulinzi lakini kwa muda tulionao hivi sasa tuelekeze nguvu zetu katika kuangalia namna tutakavyoweza kuwadhibiti magaidi na kuwakomboa mateka.” Akasema Dr Edward



***********************

“ Nimefurahi kukuona tena Tonny..” akasema Meshack Jumbo akiwa garini wakielelekea katika makazi ya waziri mkuu .Tonny hakujibu kitu .Safari yao ilikuwa ya kimya kimya .Muda wote Tonny alikuwa akiangalia nje kushuhudia mabadiliko makubwa yaliyofanyika baada ya muda wa zaidi ya mwaka wa kuwepo kizuizini
“ Dare s salam imebadilika sana katika kipindi nilichokaa kizuizini.Ninajiona kama mgeni ndani ya jiji langu..Ni huyu mzee na timu yake ndio waliosababisha yote haya.Laiti angejua namna ninavyomchukia wala asingethubutu kunisemesha tena.Nilifanya kazi kwakujitolea lakini hawakuiona thamani yangu na sasa imewalazimu kunitafuta baada ya mambo kuwachachia.Nimekubali kumsikiliza kwa sababu nimechoka kukaa mle ndani.Ngoja niifanye kazi wanayoitaka lakini hii itakuwa ni ya mwisho.Sitaki tena kuendelea na kazi hii.Nitatafuta shughuli nyingine ya kufanya na kuachana na kazi hii.Nahitaji kuishi maisha ya kawaida.” Akawaza Tonny huku gari likienda kwa kasi kubwa
“ Inaonekana ujumbe ule nilioutuma kwa idara ya ujasusi nikiwataarifu kuhusiana na kuwepo kwa mpango wa shambulio waliupuuzia.Sijui ni nani ambaye anaiongoza idara ile kwa sasa.Nina mashaka na uwezo wake wa kuiongoza idara nyeti kama ile.Wakati huyu mzee akiwa ndiye mkurugenzi mambo kama haya ilikuwa ni nadra sana kutokea.Tuliweza kuzipata taarifa mapema mno na kuyadhibiti.Lakini yote haya wameyasababisha wenyewe kwa kunifungia kizuizini eti ninahatarisha usalama wa taifa.Nilipambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba magaidi hawafanikiwi mpango wao wa kumtorosha gaidi Abdool Bin Sahel na nikafanikiwa na badala ya kunipa tuzo au pongezi ninawekwa kizuizini.Linaniuma sana jambo hili na ndiyo maana baada ya kuikamilisha kazii hii ,sintahitaji tena kuendelea na kazi hii.” Akawaza Tonny
Hatimaye waliwasili katika makazi ya waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kukaribishwa ndani.Mheshimiwa waziri mkuu alikuwa akiwasubiri kwa hamu
“ Thank you so much Meshack Jumbo for doing this” waziri mkuu akamshukuru Meshack kwa kumleta Tonny
‘Karibu sana Tonny” akasema waziri mkuu
“Nimekwisha karibia mheshimwa waziri mkuu”
“ Nadhani ni mara ya kwanza mimi na wewe tunaonana” akasema waziri mkuu
“ Ni kweli mzee.Hii ni mara ya kwanza”
“ Nafurahi sana kukutana nawe Tonny.Napenda vile vile nikupe pole sana kwa masahibu yote yaliyokukuta kijanawangu wakati ukitimiza majukumu yako.Sikuwa na habari yoyote kuhusiana nawe hadi aliponipa taarifa zako Meshack leo.Laiti ningekuwa na taarifa zako mapema usingekaa kizuizini hadi leo hii.Wewe una mchango mkubwa sana katika taifa hili na ulitakiwa upongezwe na kutunukiwa tuzo ya ushujaa badala ya kuitwa mhaini au msaliti. Naomba ufahamu kwamba kuanzia sasa wewe uko huru na hautarejea tena kizuizini.”
“ Nashukuru sana mheshimiwa waziri mkuu kwa kunitoa katika kile kizuizi.Sina neno zuri la kuweza kukushukuru zaidi ya ahsante sana.Simlaumu sana mzee Jumbo lakini kwa wakati ule alikuwa akitekeleza matakwa ya sheria.Yawezekana nilivunja sheria za nchi lakini ni kwa nia njema tu ya kuhakikisha kwamba nchi yetu inakuwa salama.” Akasema Tonny
“ Nafurahi kusikia hivyo kijana wangu.” Akasema waziri mkuu halafu ukimya mfupi ukapita akaendelea
“ Tonny nina hakika umelisikia tukio lililotokea jijini Arusha.Nchi yetu imevamiwa na magaidi wa kikundi cha Alshabaab na wamewateka wasichana zaidi ya arobaini na wanawashikilia mateka wajumbe wa mkutano wa Sulivan katika ukumbi wa mikutano wa KICC.Magaidi hawa wamewaua mamia ya watu katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru kwa kuachia gesi ya sumu na wametishia kuendelea kuachia gesi hiyo ya sumu katika sehemu mbali mbali hapa nchini zenye mikusanyiko ya watu. Hivi tunavyoongea tayari wamekwisha wachinja wasichana wanne kati ya waliowateka.Tonny miongoni mwa wasichana waliotekwa yumo binti yangu na binti wa rais.”Waziri mkuu akanyamaza kidogo na kuendelea
“ Rais wetu amekuwa mgumu sana kukubaliana chochote na magaidi hawa na sikufichi usalama wa wasichana hawa na mateka wote uko mashakani.Muda unazidi kusonga na mpaka sasa hakuna hatua yoyote kubwa iliyokwisha pigwa katika kuwakomboa wasichana wetu ingawa vikosi vya ulinzi viko kazini katika kutafuta kila aina ya mbinu ya kuwakomboa wasichana hao ambao hatujui wako wapi”
“ Magaidi hawa wanahitaji nini? Akauliza Tonny
“ Wanahitaji kiongozi wao anayeshikiliwa hapa nchini na mahakama ya afrika aachiwe huru.Rais hayuko tayari kwa hilo kwa hiyo muda waliotoa utakapofika nahitaji lao halijatimizwa basi wataendelea kuwaua mateka wote” akasema Waziri mkuu
Ukimya ukatanda pale sebuleni halafu Tonny akauliza
“ Mheshimiwa waziri mkuu ,muda uliotolewa na magaidi ni mfupi sana na hatuna muda mrefu wa hadithi,niambie unahitaji nini nikufanyie?
“ Tonny nataka kumkomboa binti yangu na wasichana wote waliotekwa kabla ya muda walioutoa kuisha.Siko tayari kumshuhudia binti yangu akichinjwa kama kuku na kuonyeshwa katika televisheni.I’m ready to do anything.I’m ready to give them what they want hata kama ni kwa kuvunja sheria na taratibu lakini ili mradi mtoto wangu asiuawe.”
“ Mheshimiwa unasema uko tayari kuwapa wanachohitaji magaidi,ina maana uko tayari kuwapa kiongozi wao wanayemuhitaji ?
“ Yes I’m ready..Chochote wanachokihitaji n iko tayari kuwapatia.Nataka utafute namna tutakavyoweza kumchukua huyo kiongozi wao na kumkabidhi kwao ili mateka wetu waachiwe” akasema waziri mkuu.
Tonny akaanza kuhisi joto,kijasho kikaanza kumchuruzika

TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO
 
BRING BACK OUR GIRLS

SEHEMU YA 8

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Mheshimiwa waziri mkuu ,muda uliotolewa na magaidi ni mfupi sana na hatuna muda mrefu wa hadithi,niambie unahitaji nini nikufanyie?
“ Tonny nataka kumkomboa binti yangu na wasichana wote waliotekwa kabla ya muda walioutoa kuisha.Siko tayari kumshuhudia binti yangu akichinjwa kama kuku na kuonyeshwa katika televisheni.I’m ready to do anything.I’m ready to give them what they want hata kama ni kwa kuvunja sheria na taratibu lakini ili mradi mtoto wangu asiuawe.”
“ Mheshimiwa unasema uko tayari kuwapa wanachohitaji magaidi,ina maana uko tayari kuwapa kiongozi wao wanayemuhitaji ?
“ Yes I’m ready..Chochote wanachokihitaji n iko tayari kuwapatia.Nataka utafute namna tutakavyoweza kumchukua huyo kiongozi wao na kumkabidhi kwao ili mateka wetu waachiwe” akasema waziri mkuu. Tonny akaanza kuhisi joto,kijasho kikaanza kumchuruzika

ENDELEA……………

Sekunde kadhaa zilipita sebuleni kwa waziri mkuu kukiwa kimya.Walikuwa wakitazamana huku kila mmoja akiwaza lake.Tonny akauvunja ukimya na kusema
“ Mheshimiwa waziri mkuu ninafahamu wasi wasi ulionao kuhusiana na mwanao kuwa mikononi mwa magaidi na ninayaheshimu mawazo yako ya kutaka kuwapatia magaidi kile wanachokitaka yaani kuwapatia mkuu wao.Ni wazo zuri lakini kwa sasa nadhani ni mapema mno kuwaza jambo kama hilo.Japokuwa linaweza kuwa na msaada lakini ni jambo lenye hatari kubwa sana.Sikushauri tufanye kitu kama hicho” akasema Tonny
“ Tonny ninalifahamu jambo hili ni la hatari kubwa na mimi niko tayari kukabiliana na lolote lile au hata kufungwa gerezani au adhabu yoyote ile ili mradi mwanangu awe huru.Kwa sasa hakuna njia nyingine ya haraka ya kuweza kuwakomboa watoto waliotekwa.Muda walioutoa ni mfupi sana na unamalizika.” Akasema waziri mkuu
“ Mheshimiwa waziri mkuu naomba unisikilize vizuri.Umenitoa kifungoni kwa lengo moja tu la kusaidia kuwakomboa watoto waliotekwa nyara na magaidi ambao miongoni mwao yuko pia mtoto wako.Niko tayari kuifanya kazi hiyo lakini kwa sharti moja tu,”
“ Sema chochote unachokitaka Tonny” akasema waziri mkuu
“ Nitaifanya kazi hii kwa namna ninavyojua mimi na tafadhali sihitaji maswali wala mahojiano.Nitawarudisha wasichana waliopotea akiwemo na binti yako.” Akasema Tonny
“ Utafanyaje Tonny?
“ Nitaifanya kazi hiyo nikiwa eneo la tukio yaani Arusha.Namna gani nitaifanya kazi yangu hiyo ninajua mwenyewe lakini nakuhakikishia kwamba lazima niwarejeshe watoto wote waliotekwa.Nahitaji usafiri wa haraka wa kunipeleka Arusha” ´akasema “ Usafiri wa haraka wa kukufikisha Arusha ni kwa ndege au helkopta.let me see what I can do” akasema waziri mkuu
“ Ok Mheshimiwa waziri mkuu,wakati ukiendelea na mchakato wa kutafuta usafiri,ninaomba nielekee kwanza nyumbani kwangu.Kuna vitu ambavyo natakiwa kuvichukua .” akasema Tonny
“ Mr Jumbo shughulikia suala la Tonny.Mimi nafanya utaratibu wa kupata usafiri wa haraka kuelekea Arusha”akasema waziri mkuu.
“ Ok mheshimiwa “akasema Meshack Jumbo na kumfanyia Ishara Tonny waondoke.Waliekea moja kwa moja katika gari la Meshack Jumbo
“ Tonny funguo za nyumba yako zimehifadhiwa katika ofisi za idara ya ujasusi.Nilipomaliza muda wangu nilimkabidhi mkurugenzi mpya funguo zile azihifadhi hadi hapo utakapotoka.Ili kuzipata tunatakiwa tuelekee huko tukazichukue”
“ Hapana mkurugenzi hatutakiwi kufanya hivyo.Hatuna wa kumuamini ndani ya idara ile kwa sasa .Hatakiwi mtu yeyote afahamu kwamba nimetoka gerezani.jambo hili tutalifanya kimya kimya sana.Tutafute namna nyingine ambayo itatuwezesha kuingia mle ndani mwangu.” Akasema Tonny .Meshack Jumbo akawasha gari wakaondoka.Walipita katika dua la vifaa vya ujenzi na kununua baadhi ya vifaa ambavyo angevihitaji kwa ajili ya kuingilia ndani mwake.
“ Tonny narudia tena kukukumbusha kwamba sikuwa nikifahamu kwamba bado uko gerezani mpaka leo.Nilipoondoka nilimuachia jukumu la kushughulikia suala lako kwa mkurugenzi mpya lakini yeye amepuuza na hakumbuki tena.Tafadhali naomba tusameheane yaliyopita na tuufungue ukurasa mpya” akasema Meshack Jumbo wakiwa njiani kuelekea nyumbani kwaTonny
“ Usijali mzee,tutaongea masuala haya baada ya jambo hili kumalizika.” Akajibu Tonny kisha safari ikaendelea kimya kimya. Walifika hadi nyumbani kwa Tonny na toka wakiwa mbali waligundua kwamba nyumba ile ilikuwa inalindwa na walinzi wawili toka kampuni binafsi ya ulinzi.
“ Nyumba yako iko katika usalama.Toka ninaacha kazi niliingia mkataba na kampuni moja ya ulinzi ili kuhakikisha nyumba yako inalindwa na inakuwa salama.” Akasema Meshack Jumbo
“ Ahsante kwa hilo”akajibu Tonny
“ Tutaingia vipi mle ndani bila ya wale jamaa kufahamu? Kwa mujibu wa mkataba tuliowekeana ni kwamba mwenye uwezo wa kuingia ndani ya nyumba ile kwa muda wote ambao utakuwa kizuizini ni mkurugenzi pekee kwa sababu yeye ndiye mwenye ufunguo.Kitendo chochote cha kujaribu kuingia mle ndani lazima watakiripoti katika ofisi yao na hivyo kujulikana kwamba umetoka kizuizini jambo ambalo linaweza kusababisha matatizo kwa upande wetu.”akasema Meshack Jumbo.Tonny alikuwa ameyaelekeza macho yake katika geti akiitazama nyumba yake .
“ Tonny nina wazo moja.Ni vifaa gani ambavyo unahitaji? Akauliza Meshack Jumbo.Tonny hakujibu kitu aliendelea kuitazama nyumba yake kana kwamba hakusikia alichoulizwa na Meshack Jumbo
“ Tonny !! akaita tena mzeeJumbo na Tonny akastuka
“ Nimekuuliza ni vifa gani unavyovihitaji? Akauliza tena MeshackJumbo
“ Ninahitaji vifaa vya kuniwezesha kufanya kazi.” Akasema Tonny “Nina vifaa vingi pale nyumbanikwangu ikiwa ni pamoja na silaha na nina hakika vinawaeza vikakusaidia sana.Kuliko kusumbuana na askar wale kwa nini tusiende nyumbani kwangu ukachukue vifaa unavyoona vinaweza kukufaa? Akashauri meshackJumbo.Tonny akafikri kidogo kisha akasema
“ Ok twende” MeshackJumbo akawasha gari wakaelekea nyumbani kwake.Alimpelea Tonny katika chumba kimoja alikohifadhi vifaa mbalimbali pamoja na silaha.Tonny akachukua kila alichoona kinaweza kumfaa kisha wakarejea katika makazi ya waziri mkuu.
“ Mmefanikiwa? Akauliza waziri mkuu
“ Tumefanikiwa mzee” akajibu Tonny
“ Ok vizuri.Hata mimi nimefanikiwa kupata helkopta ya kukodi.Tayari imekwishatua pale uwanjani .Ingawa ni gharama kubwa lakini si kitu katika kuokoa uhai wa mwanangu.”akasema waziri mkuu
“ Tonny nimekata shauri nitaongozana nawe kuelekea arusha.” Akasema waziri mkuu
“ Mheshimiw a waziri mkuu suala hili ni la hatari sana na ningekushauri ukae hapa na uniache nikafanye kazi.Arusha ni sawa na uwanja wa mapambano kwa hiyo sikushauri uende huko.Kuongozana nami kutaniongezea kazi kwani nitakuwa na kazi ya kuwatafuta wasichana waliotekwa, kuwakomboa mateka na kukulinda na wewe pia” akasema Tonny
“ Tonny siko tayari kukaa hapa wakati binti yangu yuko katika hatari ya kuchinjwa muda wowote .Hapana siwezi kukubali jambo kama hilo.Nitaongozana nawe katik auwanja wa mapamabano na nitapa,bana akuhakikisha ninamuokoa mwanangu.kama ni kufa basi nife wakati nikijaribu kumuokoa mwanangu” akasema wazir mkuu.Tonny akamuangalia na kusema
“ Are you sure about this Mr Prime minister?
“ I’m sure Tonny.Sina cha kuhofia kwa sababu baada ya suala hili kumalizika na kuwapata mabinti zetu wakiwa hai sintakuwa waziri mkuu tena.Nitakuwa katika mikono ya dola kwa hiyo tunaongozana wote kwenda Arusha.Ninafahamu kutumia silaha,nimewahi kupitia jeshi kwa hiyo ninaweza kupambana na kujilinda mwenyewe kwa hiyo usitie shaka”akasema waziri mkuu
“ Ok kama ni hivyo basi tusiendelee kupoteza muda.Tuelekeeni iliko hiyo helkopta na tuwahi eneo la tukio.Mpaka muda huo walioutoa hao jamaa kumalizika lazima tuwe tumepiga hatua Fulani kuelekea kuwapata watoto waliotekwa ”akasema Tonny .
“ Ok naomba nisubiri kidogo”akasema waziri mkuu na kuwaita walinzi wake wawili wakaingia katika chumba cha maongezi
“ Erick na Evarist ,mmekuwa walinzi wangu kwa kipindi kirefu sasa.Mambo yangu mengi mnayafahamu na ninyi ni kati ya watu ninaowaamini sana.Nadhani mtakuwa mmeshuhudia katika muda mchache uliopita,kumekuwa na pilika pilika nyingi hapa nyumbani hii ni kutokana na tukio lililotokea.Mwanangu anashikiliwa na magaidi pamoja na wasichana wengine na muda wowote anaweza kuuawa.Tunajaribu kutafuta kila namna ya kufanya ili kuweza kuwakomboa wasichana waliotekwa na magaidi na ndiyo maana mnawaona watu hao hapo wawili.Yule mzee anaitwa MeshackJumbo ni mkurugenzi wa zamani wa idara ya ujasusi ya taifa.Yule mwingine anaitwa Tonny.Ni mfanyakazi wa zamani wa idara ya ujasusi ya taifa.Tunakwenda Arusha.Tunakwenda kumkomboa mwanangu pamoja na wasichana wote waliotekwa na magaidi.Siwaambii tunakwenda kufanya nini lakini nawahakikishia kwamba nitakaporejea nitakuwa na mwanangu.Nimeona niwataarifu ili mkae mkifahamu kuhusu hilo.Najua ni jukumu lenu kuongozana nami kila mahala lakini katika hili siwashauri muongozane nami kwani ni hatari sana.” Akasema waziri mkuu “Mheshimiwa waziri mkuu,kama ulivyosema tumekuwa walinzi wako kwa muda mrefu.Unatulea kama watoto wako.Sote tumeumizwa sana na jambo lililotokea na kauli yetu ni kwamba tunaongozana nawe kueleka Arusha.Tutapambana na sisi bega kwa bega kuhakikisha kwamba wasichana waliopotea wanapatikana.” Akasema Erick “Erick are you sure about this?akauliza waziri mkuu
“ Ndiyo mzee.Tuna uhakikahuo.Tutaongozana nawe kuelekea Arusha” akasema Erick.
“ Ahsanteni ,nawashukuruni sana.Kama ni hivyo basi tusiendelee kupoteza muda.Twendeni tuondoke.Narudia tena kuwakumbusha kwamba this is between us.Asifahamu mtu yeyote kama ninaelekea Arusha.” akasema wazir mkuu kisha wakatoka mel chumbani .
“ Tonny,nguvu imeongezeka.Hawa ni walinzi wangu Erick na Evarist.Kwa hiari yao wanajiunga nasi kueleka Arusha.Tutasaidiana nao katika mapambano.” Akasema waziri mkuu
“ Ok hakuna shida mzee,twende tuondoke” akasema Tonny wakaelekea mahala ilikokuwa imetua helkopta wakaingia na safari ya Arusha ikaanza.Tonny akaegemeza kichwa chake katika kiti alionekana kuzama mawazoni
“ Back on game again “ akawaza
“ sikuwa nikitegema kabisa kama ningeweza kurejea tena katika mapambano ,lakini kwa hali ilivyo na kwa maombiya mheshimiwa waziri mkuu lazima nipambane lakini sintosahau namna nilivyoteseka kizuizini bila kosa lolote.” akaendelea kuwaza na picha ya mambo yote yaliyotokea na kumfanya awekwe kizuizini ikamjia.
“ Nakumbuka ilikuwa ni asubuhi na mapema nikiwa kitandani nimejilaza nikiangalia kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na televisheni ya Taifa kila siku asubuhi.Siku ya hii kilikuwa kikiongozwa na Marini hassan Marini mmoja kati ya watangazaji mahiri sana nchini Tanzania ambaye huchoki kumsikia au kumtazama atangazapo .Nikiwa nimenogewa na mahojiano aliyokuwa akiyafanya na wageni wake ,mara simu yangu ikaita.Nikajivuta kiuchovu na kuichukua.Kutazama mpigaji alikuwa ni Vick,katibu muhtasi wa mkurugenzi wangu.
“Halloo” Nikaita kwa sauti ya kichovu. “Hallo Tonny mambo vipi? Akajibu Vick
“ Mambo poa Vick,umeamkaje? “Nimeamka salama Tonny .Vipi wewe bado umelala? “Niko kitandani naangalia luninga.Wewe uko wapi ? si kawaida yako kunipigia simu asubuhi namna hii” “ Niko hapa ofisini toka saa kumi za usiku” Akasema Vick.Sikushangaa kwa kusikia Vick alikuwa ofisini asubuhi vile kwa sababu nazifahamu vema kazi zetu.Hakuna muda maalum wa kuingia wala kutoka. “Kuna taarifa gani hapo ofisini?” Nikauliza “Mkurugenzi anakuhitaji baadae ofisini.”Nikakaa kimya kidogo nikitafakari.Nilipatwa na wasi wasi juu ya mwito ule wa mkurugenzi..
“Ok Vick nitafika asubuhi hii” Nikajibu na kukata simu. Nilijiinua na kukaa kitandani nikajaribu kuwazua kwa haraka haraka ni jambo gani ambalo naweza kuwa naitiwa.Sikuweza kupata jibu la haraka haraka lakini moja kwa moja nilijua ni lazima nitakuwa naitiwa kazi.Ni juzi tu nimetoka Rwanda kikazi na nikapewa mapumziko ya siku nne kutokana na kazi kubwa niliyoifanya huko.Hata siku nilizopewa kupumzika hazijakwisha ninaitiwa tena kazi nyingine. Hii ndiyo adha tuipatayo sisi tunaofanya kazi katika idara hizi za ujasusi.Saa ya ukutani ilionyesha ni saa moja na dakika ishirini na saba.Nikajiinua hapo kitandani na kuelekea bafuni kuoga.Kishaoga nikaelekea katika kabati langu la nguo na kuchagua suti ya kijivu.Hii ni moja kati ya suti nizipendazo sana.Nilipojiangalia katika kioo nikaona niko safi,sikutaka kupoteza muda nikafunga nyumba yangu na kuondoka kuelekea ofisini. Ilinichukua muda mrefu kidogo kuwasili ofisini hasa kutokana na msongamano mkubwa wa magari asubuhi hii katika jiji la Dar.Nilipofika ofisini nikafululiza moja kwa moja hadi katika ofisi ya mkurugenzi.Vick ,katibu muhtasi wa mkurugenzi hakuwepo hapo ofisini hivyo nikafungua mlango wa mkurugenzi na kujitoma ndani.Nikamsalimu naye akaitika kwa kichwa huku akinipa ishara kwa mkono nivute kiti niketi.Mara nyingi huyu mkurugenzi wetu huwa haitikii salamu na sisi tulikwisha mzoea.Kwa muda wa kama dakika saba hivi alikuwa akiendelea na kazi zake za kupitia ripoti kadhaa zilizowekwa mezani kwake.Sikuhisi kama kuna jambo lolote baya kwa dalili nilizoziona humo ofisini kwa mkurugenzi.Ukimya uliotawala humo ni kutokana tu na dharau za huyu mzee.Simsemei vibaya lakini ni mmoja kati ya watu wenye dharau nyingi katika hii dunia.Nadhani ni kwa sababu ya cheo na usomi wake. “Visto 01” Alianza kunisalimu mkurugenzi kwa salamu yetu ya kikazi.Visto 01 ndilo jina langu la kikazi. “Nimekuita hapa ili kukutaarifu kuwa maombi yako ya likizo yamekubaliwa kama ulivyoomba kwa hiyo unatakiwa ujaze fomu na uanze likizo mara moja.Ila ukumbuke kuwa muda wowote ikijitokeza dharura basi utahitajika kurudi ofisini haraka iwezekanavyo,hivyo muda wote jitahidi uwe unapatikana .” Hakuwa na maongezi marefu ,akanipa fomu za kujaza nikakaa katika meza ya pemBeni na kuanza kujaza.Nilikuwa na furaha isiyo kifani.Nilifurahi mno kupata mapumziko haya hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.Wakati naijaza fomu hiyo picha za namna mapumziko yangu yatakavyokuwa zilikuwa zikija katika kichwa changu.Kichwani nilikuwa na lengo moja tu nalo ni kwenda kupumzika Arusha,mji ninaoupenda kuliko yote nchini.Imepita miaka miwili sasa sijakwenda Arusha lakini safari hii ni lazima nifike huko.Likizo yangu yote ni lazima nikaimalizie kule.Arusha ni Geneva ya Afrika.Kwa wewe ambaye hujawahi kufika katika jiji hili basi jitahidi walau mara moja katika maisha yako ulitembelee .Ni jiji lililobarikiwa mambo mengi.Licha ya kujaaliwa mito mingi ibubujikayo mwaka mzima toka mlima Meru pia kuna hewa safi na murua.Vipo pia vivutio vingi vya utalii vinavyoifanya nchi yetu kusifika duniani na kuwaleta mamia ya watalii kila mwaka . Pale Arusha ninaye rafiki yangu aitwaye Ben anayefanya kazi katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC .Huyu ndiye huwa mwenyeji wangu kule.Nilimaliza kuijaza fomu ile niliyopewa nikairudisha kwa mkurugenzi ambaye aliipitia na kuniandikia hundi ya malipo ya shilingi millioni nne na nusu.
“nakutakia Krismass njema na mwaka mpya wenye amani.Ila usisahau tarehe 4 mwezi wa kwanza tutakuwa na tafrija ya kufungua mwaka hivyo hutakiwi kukosa.” “Ahsante sana mzee,nitajitahidi kuwepo katika tafrija hiyo.Nakutakia krismass njema pia na mwaka mpya mzuri” Tukashikana mikono tukaagana.Nikaufugua mlango na kutoka..Ile natoka tu nikagonganisha macho na Vick katibu muhtasi wa mkurugenzi. “Hallo Tonny kumbe umeshafika? akasema Vick “Nimefika kitambo ila wakati naingia hukuwepo ofisini” “Vipi kuna kazi nyingine tena? Akauliza kwa shauku ya kutaka kujua baada ya kuniona nimeshika hundi yangu ya malipo ya likizo “Hapana Vick si kazi .Likizo yangu imekubaliwa hivyo naenda zangu kupumzika.”
“Wow ! una bahati sana Tonny.Mimi nimejaribu kuomba lakini nimekataliwa hadi mwaka kesho.Sasa unasafiri au utakuwepo hapa hapa Dar?
“Nasafiri naenda zangu Arusha.Krismass na mwaka mpya nitakuwepo kule” Msichana huyu mrembo akaniangalia kwa jicho ambalo niling’amua mara moja lilimaaninsha nini.Binti huyu mrembo kupita maelezo alikuwa akinipenda mno lakini sikutaka matatizo na mkurugenzi wangu kwa sababu hizo ni mali zake na amekuwa akumuhudumia mtoto huyu kupita maelezo. Vick akaukamata mkono wangu kwa nguvu huku amenikazia macho na muda huo huo msichana mmoja aitwaye Rahel akaingia humo ofisini na kunipa mimi mwanya wa kuondoka.Wakati nikiwa garini nikiondoka maeneo haya ya ofisini ,nikachukua simu na kumpigia rafiki yangu Ben kule Arusha kumfahamisha kuhusu safari yangu.
“Haloo Tonny.How are you brother” Akanisalimu Ben kwa furaha
“I’m fine brother.Habari za siku nyingi? “Habari shwari Tonny.Vipi huko Dar?
“Huku kwema kabisa.Tonny nimekupigia kukutaarifu kwamba kesho nitatua hapo jijini Arusha” “Usinitanie Tonny !!.. Ben akastuka. “Kweli kabisa Ben.Kesho natua hapo Arusha kwa mapumziko ya krismass na mwaka mpya.Naomba uje unipokee uwanja wa ndege wa Kilimanjaro saa sita mchana.Nategemea kupata mapumziko mazuri huko Arusha.Yule miss sijui nani yule….. “Ney??”
“Exactly .Msalimu sana mwambie kesho nitakuwepo hapo jijini”
“Ney siku hizi hajishughulishi tena na mambo ya mitindo.Anafanya kazi katika hoteli moja kubwa ya kitalii hapa karibu na kituo chetu.Ila Mariam na Pendo wapo.Nitawapa taarifa kuwa unakuja,nadhani watafurahi sana.” “Sawa Ben fanya maandalizi tutaongea vizuri baadae”
“Ok Tonny.

********************************************

“Abiria wote mnaombwa mfunge mikanda tunakaribia kutua katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro.Ni matumaini yetu kuwa mmezifurahia huduma zetu na mtaendelea siku zote kusafiri na ndege zetu kwa huduma safi na zenye uhakika.” Ilikuwa ni sauti tamu ya mwanadada katika ndege hii ya shirika la ndege la V air linalofanya safari zake katika miji ya Dar es salaam,Kilimanjaro ,mwanza na Zanzibar.Tulifunga mikanda yetu tayari kwa kutua. Ndege ikatua na iliposimama watu walianza kushuka lakini mimi nikatulia kitini kwa dakika kadhaa ili kuhakikisha usalama wangu.Ni kawaida yetu sisi majasusi kuhakikisha usalama wetu kwanza tuwapo katika kadamnasi ya watu.Nilipohakikisha hakuna mtu yeyote mwenye kunijali ,nikashuka.Nilikuwa nikitembea taratibu nikikifurahia kijua kitamu na upepo mwanana wa mchana.Nilipiga kama hatua kumi hivi nikasikia sauti kwa nyuma yangu. “Kaka samahani” Ilikuwa ni sauti tamu, na laini.Nikageuza shingo yangu kuangalia aliyekua akiniita na mara macho yangu yakakutana na mrembo ambaye alinifanya nipigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa nikimuangalia.Nilihisi ni kama ninatazamana na kiumbe wa kiroho kwa uzuri aliokuwa nao mwanamke Yule.
“kaka samahani naomba nikuulize”Alitamka tena kwa sauti yake nyororo. Alikuwa ni msichana mrembo mno.Alikuwa mrefu wastani,mwembamba kiasi,mwenye sura ya mviringo,yenye macho meupe mazuri yenye kuonyesha ukarimu ,pua yake ndefu na nyembamba ambayo chini yake kulikuwa na midomo laini iliyokolezwa na rangi nzuri ya mdomo na kumfanya msichana yule aonekane kama malaika.Kwa dakika kama mbili hivi nilijikuta nikiwa kimya nikiufanyia usaili wa macho mwili wa mrembo huyu.Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilihisi midomo inakuwa mizito kufunguka.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………..
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 9
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Kaka samahani” Ilikuwa ni sauti tamu, na laini.Nikageuza shingo yangu kuangalia aliyekua akiniita na mara macho yangu yakakutana na mrembo ambaye alinifanya nipigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa nikimuangalia.Nilihisi ni kama ninatazamana na kiumbe wa kiroho kwa uzuri aliokuwa nao mwanamke Yule.
“kaka samahani naomba nikuulize”
Alitamka tena kwa sauti yake nyororo.
Alikuwa ni msichana mrembo mno.Alikuwa mrefu wastani,mwembamba kiasi,mwenye sura ya mviringo,yenye macho meupe mazuri yenye kuonyesha ukarimu ,pua yake ndefu na nyembamba ambayo chini yake kulikuwa na midomo laini iliyokolezwa na rangi nzuri ya mdomo na kumfanya msichana yule aonekane kama malaika.Kwa dakika kama mbili hivi nilijikuta nikiwa kimya nikiufanyia usaili wa macho mwili wa mrembo huyu.Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilihisi midomo inakuwa mizito kufunguka
ENDELEA………………….
“Samahani kaka wewe ni mwenyeji wa Arusha? Aliuliza mwanadada yule ambaye kwa sasa alikuwa mita chache toka nilipokuwa nimesimama.Lafudhi yake ilionyesha kama si mtu anayekijua vizuri kiswahili au kama ni mswahili basi amekaa sana nje ya nchi.Nikarekebisha koo na kusema
“ Si mwenyeji sana wa Arusha lakini ndiko naelekea.Mwenzangu unaelekea wapi? Nikauliza swali.
“Mimi pia naelekea huko huko Arusha .Ni mara yangu ya kwanza kufika huko na sina mwenyeji ndio maana natafuta mtu anayeifahamu Arusha vizuri aweze kunielekeza mambo kadhaa”
Uso wangu ukachanua kwa tabasamu pana mno. Kwa mwanamke mrembo kama huyu hata kama ningekuwa nakwenda sehemu nyingine tofauti na Arusha ningeahirisha safari ili niongozane naye
“Kama ndio hivyo basi naomba niwe mwenyeji wako kama hutajali.” nikasema huku nikitabasamu
“I don’t mind” Akajibu kwa tabasamu pevu.
“I’m Tonny” Nikasema huku nikimpa mkono.
“I’m Rosa Stevens ”
Tukasalimiana kisha tukaongozana kukamilisha taratibu za uwanjani kabla ya kutoka.
Mwenyeji wangu Ben tayari alikwisha fika hapo uwanjani kunipokea.
“Ben kutana na Rosa stevens” Nilianza utambulisho bila kuchelewa kwani tayari Ben alikwisha anza kumtumbulia machoRosa.
“Rosa kutana na Ben.Huyu ni rafiki yangu lakini pia ni mwenyeji wangu niwapo Arusha.Kwa hivi sasa atakuwa ndiye mwenyeji wetu sote”
Ben na Rosa wakasalimiana kwa kushikana mikono ,halafu Ben akatuongoza liliko gari lake .Tuliingia garini na safari ya kuelekea Arusha ikaanza.
“Mimi nilidhani unaishi Arusha kumbe na wewe ni mgeni? Akauliza Rosa wakati tumeishika bara bara kuu ya kuelekea Arusha.
Nikacheka kicheko kikubwa ,nikajibu.
“Kusema ukweli mi si mwenyeji wa huku kama nilivyokwambia ila huwa ninakuja huku mara kwa mara na kila nijapo huku Arusha basi mwenyeji wangu huwa ni huyu hapa Ben” wote tukacheka.
Wakati safari ikiendelea nilikuwa nikimtazama kwa kuibia binti huyu mwenye uzuri wa shani.Hapo ndipo nilipobaini kuwa Rosa alikuwa ni binti mrembo ambaye ni vigumu hata kumuelezea.Nilimsifu Mungu kwa uumbaji wake huu uliotukuka..

***************************************************

Saa saba na nusu mchana tukawasili jijini Arusha.Rosa hakusita kuonyesha furaha yake kwa kuingia katika jiji hili zuri la kimataifa.
“Arusha is wonderfull” Akasema Rosa huku amechanua tabasamu pana
“Its more than wonderfull”Nikajibu huku na mimi nikitabasamu.
Kama ilivyo ada yangu niwapo mjini arusha huwa napenda sana kufikia Gazzele hoteli,hoteli kubwa ya kitalii yenye hadhi ya kimataifa.Nilimfahamisha Rosa iwapo angependa kufikia hapo naye bila kipingamizi akakubali.
Kukubali kwake kufikia hoteli moja na mimi ilikuwa ni furaha kubwa kwangu kwa sababu tayari nimekwisha anza kuvutiwa kuwa karibu na kimwana huyu mwenye uzuri usiolinganishwa.Niliufurahia uamuzi wangu wa kuja jijini arusha ambako nimekutana na kiumbe wa pekee kabisa.Raha ya mapumziko uwe na wakupumzika naye.
Pale Gazzele hoteli tulipatiwa vyumba viwili tofauti.Alipohakikisha tayari tumekwisha pata vyumba na tuko salama Ben akatuaga na kuondoka kwa muda kuelekea ofisini kwake alikokuwa akihitajika kwa dharura.
Nilikikagua chumba chote kuhakikisha usalama wangu kwanza.Ni ada yetu sisi kuhakiki usalama kila mahala tunapokuwa.Chumba kilikuwa kikubwa,kizuri na kilichojitosheleza.Wakati nikiendelea kukikagua chumba kile simu yangu ikaita.Alikuwa ni Ben
“Haloo Ben” Nikasema
“Haloo Tonny.Nataka nikuulize umepaonaje hapo Gazzele,panakufaa? Kama unaona hapakufai basi tuhame mara moja .Hoteli ziko nyingi sana hapa Arusha.”
Huku nikitabasamu nikasema
“Ben hii ni hoteli nzuri na muafaka kabisa.Wewe mwenyewe unajua jinsi ninavyoipenda hoteli hii ndiyo maana kila nijapo Arusha huwa nafikia hapa.
“Ok Tonny vipi kuhusu Rosa anasemaje?
“Hana maneno na amepafurahia sana.”
“sawa Tonny.Ratiba ya leo itakuwa kama hivi.Nitakuja hapo Impala saa kumi za jioni nikiwa na waubani wangu ambaye bado sijakutambulisha.Tukitoka hapo tutaelekea Club Afrique ambako tutapata vinywaji mpaka usiku.Tukitoka hapo tutaelekea katika ukumbi mpya kabisa wa burudani unaitwa Mnama social club.Pale kutakuwa na onyesho kubwa la Bendi ya Fm academia.Tukitoka hapo tutaelekea La fame club pale kuna shoo ya nguvu itakayodondoshwa na wanamuziki wakali wa kizazi kipya wa afrika mashariki.Hakuna kulala leo ni kusherehekea mpaka asubuhi.Mpaka hapo kuna kipingamizi chochote kuhusu mkesha wa Krismas? “ akauliza Ben.
“Mpaka hapo mimi sina kipingamizi chochote Ben.Wewe ndiye mwenyeji wetu .Mimi naona ratiba imetulia sana.”
“Ok Tonny tutaonana baadae”
Nilipomaliza kuongea na Ben,nikaingia bafuni kuoga.Kisha oga nikavaa nguo za mapumziko,nikajitazama nikaona niko safi,nikainua simu na kupiga chumba cha Rosa.
“Haloo “ Ilikuwa ni sauti tamu ya Rosa
“Hallow Rosa Tonny hapa”
“ouh Tonny Thank you very much .U mkarimu wa ajabu.” akasema Rosa.
Huku nikicheka kichini chini nikasema.
“Usijali Rosa.Vipi huduma za hapa unazifurahia? Kama hujapapenda basi tunaweza kutafuta hoteli nyingine .Hapa Arusha ziko hoteli nyingi sana”
“ No !No ! Tonny hoteli hii ni nzuri na nimeifurahia.Its cool na huduma zake ni nzuri sana."
“Nafurahi kusikia hivyo.Nina kila jukumu la kuhakikisha kuwa unapata huduma nzuri kwa sababu wewe ni mgeni wangu”
“Nashukuru sana Tonny.hapa ni pazuri na panatosha”
“Ok Rosa basi naomba tukutane kule chini kwa ajili ya chakula cha mchana
“Ok I’ll be there soon”akajibu.
Nilitoka chumbani na kuelekea ukumbi wa hoteli.Watu walikuwa wengi kiasi na nyuso nyingi nilizoziona zilikuwa za wageni yaani watalii.Si watalii peke yao waliokuwa wakipata chakula hapa hotelini bali hata wazawa nao walikuwepo kwa sababu hii ni hoteli pekee ambayo inaweza kukidhi wageni halikadhalika wazawa kutokana na bei zake kuwa nafuu.”
“Hey Tonny “
Nilistuliwa na sauti laini ya Rosa toka nyuma yangu.
“Ouh Rosa “ Nikasema
“sorry for being late”
“Its ok” Nikajibu
Mara moja muhudumu akafika na kutuuliza kama kuna chakula tungependa tuletewe.Tuliipitia orodha ya vyakula,kila mmoja akachagua chakula anachokipenda.
Kwa sekunde kadhaa tulikuwa kimya pale mezani .Nilikuwa nikijaribu kumsaili zaidi kiumbe aliyeko mbele yangu.Mchana huu alivaa kinguo chepesi kidogo ambacho kilifunika sehemu ya matiti yake.na kuyaacha wazi maeneo mengine ya juu.Nilikitupia macho kifua chake cheupe na kukutana na dodo mbili ndogo zenye kusisimua ..Chini alivaa sketi fupi ambayo iliacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi na kunipa wakati mgumu sana.
“Nafurahi kukutana nawe Tonny ,u mkarimu wa ajabu” Rosa aliuvunja ukimya uliotawala hapo mezani na kunistua toka katika usaili ule niliokuwa naufanya mwilini mwake.
“Hata mimi nimefurahi mno kukutana nawe Rosa.Najiona ni mtu mwenye bahati kubwa kukutana na kukaa na mwanamke mrembo kama wewe.To be honnest you are so pretty Rosa ” Rosa akatabasamu,akacheka kidogo.
“napenda sana kuwa nawe karibu.,you are so fun” akasema
Mara moja mhudumu akafika na vyakula tulivyokuwa tumeagiza,akaandaa meza na kutukaribisha.
“karibu chakula Tonny” akasema Rosa
“ahsante Rosa ila umewahi sana ,mimi ndiye niliyetakiwa nikukaribishe kwa sababu mimi ndiye mwenyeji wako"
Wote tukacheka na kuendelea kula taratibu

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………….
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 9
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Kaka samahani” Ilikuwa ni sauti tamu, na laini.Nikageuza shingo yangu kuangalia aliyekua akiniita na mara macho yangu yakakutana na mrembo ambaye alinifanya nipigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa nikimuangalia.Nilihisi ni kama ninatazamana na kiumbe wa kiroho kwa uzuri aliokuwa nao mwanamke Yule.
“kaka samahani naomba nikuulize”
Alitamka tena kwa sauti yake nyororo.
Alikuwa ni msichana mrembo mno.Alikuwa mrefu wastani,mwembamba kiasi,mwenye sura ya mviringo,yenye macho meupe mazuri yenye kuonyesha ukarimu ,pua yake ndefu na nyembamba ambayo chini yake kulikuwa na midomo laini iliyokolezwa na rangi nzuri ya mdomo na kumfanya msichana yule aonekane kama malaika.Kwa dakika kama mbili hivi nilijikuta nikiwa kimya nikiufanyia usaili wa macho mwili wa mrembo huyu.Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilihisi midomo inakuwa mizito kufunguka
ENDELEA………………….
“Samahani kaka wewe ni mwenyeji wa Arusha? Aliuliza mwanadada yule ambaye kwa sasa alikuwa mita chache toka nilipokuwa nimesimama.Lafudhi yake ilionyesha kama si mtu anayekijua vizuri kiswahili au kama ni mswahili basi amekaa sana nje ya nchi.Nikarekebisha koo na kusema
“ Si mwenyeji sana wa Arusha lakini ndiko naelekea.Mwenzangu unaelekea wapi? Nikauliza swali.
“Mimi pia naelekea huko huko Arusha .Ni mara yangu ya kwanza kufika huko na sina mwenyeji ndio maana natafuta mtu anayeifahamu Arusha vizuri aweze kunielekeza mambo kadhaa”
Uso wangu ukachanua kwa tabasamu pana mno. Kwa mwanamke mrembo kama huyu hata kama ningekuwa nakwenda sehemu nyingine tofauti na Arusha ningeahirisha safari ili niongozane naye
“Kama ndio hivyo basi naomba niwe mwenyeji wako kama hutajali.” nikasema huku nikitabasamu
“I don’t mind” Akajibu kwa tabasamu pevu.
“I’m Tonny” Nikasema huku nikimpa mkono.
“I’m Rosa Stevens ”
Tukasalimiana kisha tukaongozana kukamilisha taratibu za uwanjani kabla ya kutoka.
Mwenyeji wangu Ben tayari alikwisha fika hapo uwanjani kunipokea.
“Ben kutana na Rosa stevens” Nilianza utambulisho bila kuchelewa kwani tayari Ben alikwisha anza kumtumbulia machoRosa.
“Rosa kutana na Ben.Huyu ni rafiki yangu lakini pia ni mwenyeji wangu niwapo Arusha.Kwa hivi sasa atakuwa ndiye mwenyeji wetu sote”
Ben na Rosa wakasalimiana kwa kushikana mikono ,halafu Ben akatuongoza liliko gari lake .Tuliingia garini na safari ya kuelekea Arusha ikaanza.
“Mimi nilidhani unaishi Arusha kumbe na wewe ni mgeni? Akauliza Rosa wakati tumeishika bara bara kuu ya kuelekea Arusha.
Nikacheka kicheko kikubwa ,nikajibu.
“Kusema ukweli mi si mwenyeji wa huku kama nilivyokwambia ila huwa ninakuja huku mara kwa mara na kila nijapo huku Arusha basi mwenyeji wangu huwa ni huyu hapa Ben” wote tukacheka.
Wakati safari ikiendelea nilikuwa nikimtazama kwa kuibia binti huyu mwenye uzuri wa shani.Hapo ndipo nilipobaini kuwa Rosa alikuwa ni binti mrembo ambaye ni vigumu hata kumuelezea.Nilimsifu Mungu kwa uumbaji wake huu uliotukuka..

***************************************************

Saa saba na nusu mchana tukawasili jijini Arusha.Rosa hakusita kuonyesha furaha yake kwa kuingia katika jiji hili zuri la kimataifa.
“Arusha is wonderfull” Akasema Rosa huku amechanua tabasamu pana
“Its more than wonderfull”Nikajibu huku na mimi nikitabasamu.
Kama ilivyo ada yangu niwapo mjini arusha huwa napenda sana kufikia Gazzele hoteli,hoteli kubwa ya kitalii yenye hadhi ya kimataifa.Nilimfahamisha Rosa iwapo angependa kufikia hapo naye bila kipingamizi akakubali.
Kukubali kwake kufikia hoteli moja na mimi ilikuwa ni furaha kubwa kwangu kwa sababu tayari nimekwisha anza kuvutiwa kuwa karibu na kimwana huyu mwenye uzuri usiolinganishwa.Niliufurahia uamuzi wangu wa kuja jijini arusha ambako nimekutana na kiumbe wa pekee kabisa.Raha ya mapumziko uwe na wakupumzika naye.
Pale Gazzele hoteli tulipatiwa vyumba viwili tofauti.Alipohakikisha tayari tumekwisha pata vyumba na tuko salama Ben akatuaga na kuondoka kwa muda kuelekea ofisini kwake alikokuwa akihitajika kwa dharura.
Nilikikagua chumba chote kuhakikisha usalama wangu kwanza.Ni ada yetu sisi kuhakiki usalama kila mahala tunapokuwa.Chumba kilikuwa kikubwa,kizuri na kilichojitosheleza.Wakati nikiendelea kukikagua chumba kile simu yangu ikaita.Alikuwa ni Ben
“Haloo Ben” Nikasema
“Haloo Tonny.Nataka nikuulize umepaonaje hapo Gazzele,panakufaa? Kama unaona hapakufai basi tuhame mara moja .Hoteli ziko nyingi sana hapa Arusha.”
Huku nikitabasamu nikasema
“Ben hii ni hoteli nzuri na muafaka kabisa.Wewe mwenyewe unajua jinsi ninavyoipenda hoteli hii ndiyo maana kila nijapo Arusha huwa nafikia hapa.
“Ok Tonny vipi kuhusu Rosa anasemaje?
“Hana maneno na amepafurahia sana.”
“sawa Tonny.Ratiba ya leo itakuwa kama hivi.Nitakuja hapo Impala saa kumi za jioni nikiwa na waubani wangu ambaye bado sijakutambulisha.Tukitoka hapo tutaelekea Club Afrique ambako tutapata vinywaji mpaka usiku.Tukitoka hapo tutaelekea katika ukumbi mpya kabisa wa burudani unaitwa Mnama social club.Pale kutakuwa na onyesho kubwa la Bendi ya Fm academia.Tukitoka hapo tutaelekea La fame club pale kuna shoo ya nguvu itakayodondoshwa na wanamuziki wakali wa kizazi kipya wa afrika mashariki.Hakuna kulala leo ni kusherehekea mpaka asubuhi.Mpaka hapo kuna kipingamizi chochote kuhusu mkesha wa Krismas? “ akauliza Ben.
“Mpaka hapo mimi sina kipingamizi chochote Ben.Wewe ndiye mwenyeji wetu .Mimi naona ratiba imetulia sana.”
“Ok Tonny tutaonana baadae”
Nilipomaliza kuongea na Ben,nikaingia bafuni kuoga.Kisha oga nikavaa nguo za mapumziko,nikajitazama nikaona niko safi,nikainua simu na kupiga chumba cha Rosa.
“Haloo “ Ilikuwa ni sauti tamu ya Rosa
“Hallow Rosa Tonny hapa”
“ouh Tonny Thank you very much .U mkarimu wa ajabu.” akasema Rosa.
Huku nikicheka kichini chini nikasema.
“Usijali Rosa.Vipi huduma za hapa unazifurahia? Kama hujapapenda basi tunaweza kutafuta hoteli nyingine .Hapa Arusha ziko hoteli nyingi sana”
“ No !No ! Tonny hoteli hii ni nzuri na nimeifurahia.Its cool na huduma zake ni nzuri sana."
“Nafurahi kusikia hivyo.Nina kila jukumu la kuhakikisha kuwa unapata huduma nzuri kwa sababu wewe ni mgeni wangu”
“Nashukuru sana Tonny.hapa ni pazuri na panatosha”
“Ok Rosa basi naomba tukutane kule chini kwa ajili ya chakula cha mchana
“Ok I’ll be there soon”akajibu.
Nilitoka chumbani na kuelekea ukumbi wa hoteli.Watu walikuwa wengi kiasi na nyuso nyingi nilizoziona zilikuwa za wageni yaani watalii.Si watalii peke yao waliokuwa wakipata chakula hapa hotelini bali hata wazawa nao walikuwepo kwa sababu hii ni hoteli pekee ambayo inaweza kukidhi wageni halikadhalika wazawa kutokana na bei zake kuwa nafuu.”
“Hey Tonny “
Nilistuliwa na sauti laini ya Rosa toka nyuma yangu.
“Ouh Rosa “ Nikasema
“sorry for being late”
“Its ok” Nikajibu
Mara moja muhudumu akafika na kutuuliza kama kuna chakula tungependa tuletewe.Tuliipitia orodha ya vyakula,kila mmoja akachagua chakula anachokipenda.
Kwa sekunde kadhaa tulikuwa kimya pale mezani .Nilikuwa nikijaribu kumsaili zaidi kiumbe aliyeko mbele yangu.Mchana huu alivaa kinguo chepesi kidogo ambacho kilifunika sehemu ya matiti yake.na kuyaacha wazi maeneo mengine ya juu.Nilikitupia macho kifua chake cheupe na kukutana na dodo mbili ndogo zenye kusisimua ..Chini alivaa sketi fupi ambayo iliacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi na kunipa wakati mgumu sana.
“Nafurahi kukutana nawe Tonny ,u mkarimu wa ajabu” Rosa aliuvunja ukimya uliotawala hapo mezani na kunistua toka katika usaili ule niliokuwa naufanya mwilini mwake.
“Hata mimi nimefurahi mno kukutana nawe Rosa.Najiona ni mtu mwenye bahati kubwa kukutana na kukaa na mwanamke mrembo kama wewe.To be honnest you are so pretty Rosa ” Rosa akatabasamu,akacheka kidogo.
“napenda sana kuwa nawe karibu.,you are so fun” akasema
Mara moja mhudumu akafika na vyakula tulivyokuwa tumeagiza,akaandaa meza na kutukaribisha.
“karibu chakula Tonny” akasema Rosa
“ahsante Rosa ila umewahi sana ,mimi ndiye niliyetakiwa nikukaribishe kwa sababu mimi ndiye mwenyeji wako"
Wote tukacheka na kuendelea kula taratibu

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………….
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 10
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Nafurahi kukutana nawe Tonny ,u mkarimu wa ajabu” Rosa aliuvunja ukimya uliotawala hapo mezani na kunistua toka katika usaili ule niliokuwa naufanya mwilini mwake.
“Hata mimi nimefurahi mno kukutana nawe Rosa.Najiona ni mtu mwenye bahati kubwa kukutana na kukaa na mwanamke mrembo kama wewe.To be honnest you are so pretty Rosa ” Rosa akatabasamu,akacheka kidogo.
“napenda sana kuwa nawe karibu.,you are so fun” akasema
Mara moja mhudumu akafika na vyakula tulivyokuwa tumeagiza,akaandaa meza na kutukaribisha.
“karibu chakula Tonny” akasema Rosa
“ahsante Rosa ila umewahi sana ,mimi ndiye niliyetakiwa nikukaribishe kwa sababu mimi ndiye mwenyeji wako"
Wote tukacheka na kuendelea kula taratibu

ENDELEA…………………

Baada ya kumaliza kula tukaelekea katika sehemu ya kupumzikia.
“Rosa nadhani ni wakati mzuri sasa kama tutaitumia nafasi hii kufahamiana zaidi.Tumekutana na tumefahamiana kwa majina tu ,nafikiri kuna kila sababu ya kujuana kwa undani kidogo,kama hutajali ”
Rosa akaitikia kwa kichwa kuonyesha kukubaliana na wazo langu.
“Mimi kama nilivyokwisha kufahamisha naitwa Tonny.Ninaishi Dar es salaam na huku Arusha nimekuja kwa mapumziko.Kazi yangu mimi ni mfanyabiashara.Nina kampuni yangu ya kuagiza na kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi”
Nilitoa utambulisho huo mfupi wa uongo. Rosa akatabsamu kidogo na kusema
“kwa kifupi ninaitwa Rosa.Ni mkaazi wa Mombasa Kenya lakini mara nyingi napatikana Dar es salaam na Nairobi.Mimi pia ninajishughulisha na biashara.Nina kampuni yangu ya urembo na hapa arusha nimekuja kuangalia uwezekano wa kufungua tawi na ndio maana ninahitaji mwenyeji wa kunisaidia katika suala hilo.”
“Usijali Rosa mwenyeji umeshampata.Mimi na Ben tutahakiksha kwa kila hali unafanikiwa kufungua tawi la kampuni yako hapa Arusha” Nilisema kwa kujiamini huku nikitabasamu.
“Nitashukuru sana Tonny kama mtanisaidia kufanikisha suala hilo.Nina imani pia tutajenga mahusiano mazuri ya kibiashara na kuna uwezekano mkubwa wa kuanza kuitumia kampuni yako katika kuagiza na kusafirisha mizigo yetu”
Tulikaa kimya kwa dakika kama mbili hivi halafu Rosa akauliza.
“Tonny umeoa?
Sikuwa nimelitegemea swali hili kwa haraka namna hii.
“Hapana sijaoa”Nikajibu kwa mkato
“Unasubiri nini? Akauliza tena
“Bado sijapata yule ambaye ataufanya moyo wangu usimame”Nikajibu huku nikitabasamu
“wewe je vipi umeolewa? Nikamtwanga swali
“hapana bado , kama wewe bado sijampata yule ambaye naweza kusema ameziteka fikra zangu kiasi cha kumkabidhi moyo wangu.”
“Itabidi umuombe sana Mungu akupatie mpenzi wa kweli” Nikasema
“ You too .You need to pray .True love is hard to find these days”
" Unayosema ni ya kweli Rosa..Imekuwa vigumu sana kulipata penzi la kweli siku hizi.Watu wamekuwa wabinafsi sana " nikasema halafu tukaendelea na maongezi mengi yanayohusiana na biashara na maisha ya kawaida.Tulipochoka kila mtu akaenda kupumzika chumbani kwake.

**********************************************



Saa sita za usiku tuliondoka Mnama social club kulikokuwa na onyesho kabambe la Bendi ya FM academia wazee wa ngwasuma.Hakika nilisuuzika kwa burudani waliyoitoa.Ngwasuma lililoporomoshwa hapa lilikuwa la uhakika.Ben yeye ni mpenzi mkubwa wa bongo fleva na ndiye aliyetutaka tuondoke hapo Mnama club kuelekea La fame club kulikokuwa na shoo kubwa ya wasanii wakali wa afrika mashariki.
La fame club moja ya klabu mpya na ya kisasa kabisa kuwahi kujengwa jijini arusha ilikuwa imefurika watu.Jukwaani onyesho lilikuwa linaendelea.Tukatafuta sehemu nzuri tukaketi tukitazama onyesho huku tukipata vinywaji taratibu.Wakati tukiendelea na vinywaji Rosa akainuka na kuelekea maliwato.Baada ya dakika kadhaa akarudi lakini alionekana kama ana mawazo mengi.Ninajua kumsoma mtu hivyo niligundua mapema kuwa Rosa hakuwa sawa.
“is there anything wrong? Nikamuuliza
“Nothing wrong Tonny.I’m ok” Akasema Rosa huku akijilazimisha kutabasamu.Nikapuuzia hali ile nikainua glasi yangu ya mvinyo na kupiga funda kubwa.Mida hiyo ilipata saa saba za usiku.Bado watu walikuwa wakiingia na kutoka.Kwa sasa jukwaani ilikuwa ni mapumziko,ukapigwa wimbo mmoja ambao siukumbuki vizuri ni wa msanii gani na kuufanya ukumbi ulipuke kwa shangwe.Irene mchumba wa Ben akanishika mkono na kuniomba tuinuke tukacheze.Ben yeye huwa hapendi mambo ya kucheza cheza.Wimbo ule ulipoisha tukarudi mezani lakini kabla hatujakaa ukapigwa wimbo mmoja wa taratibu sana wa Mariah carey uitwao My all.Nilisisimka mwili kwa sauti tamu ya mwanamama huyu.Nikamshika mkono Rosa nikamwinua nikamuomba tukacheze.Nilizungusha mikono yangu kiunoni mwake naye akanikumbatia kwa nguvu na kukilaza kichwa chake kifuani kwangu.
“Ouh My God I cant believe this.Dancing with such a prettiest lady in the world” Nikawaza.Ni bahati ilioje ya kucheza namna ile na kiumbe mrembo kama huyu.Watu walikuwa wakitupiga vijicho wakiustaajabia uzuri wa Rosa.
Wakati tukiendelea kucheza,nikasikia mtetemo wa simu yangu.Nilipatwa na hasira za ghafla kwa kupigiwa simu hasa kwa wakati adimu kama ule.Niliipuuzia simu ile nayo ikaendelea kutetema kuashiria kuwa mpigaji bado aliendelea kupiga.Wimbo ulipokwisha ,nikamuomba samahani Rosa kuwa ninaenda nje kupokea simu.Rosa alitaka kulipinga wazo hilo lakini hakupata nafasi tayari nilikwisha anza kupiga hatua kuelekea nje ya jengo.Nilipiga hatua kadhaa nikageuka na kumuona Rosa bado amesimama akiniangalia.
Nilitoka nje kabisa ya jengo na kuelekea sehemu ya kuegeshea magari ambako ndiko kulionekana kidogo kuna utulivu.Nikaitoa simu yangu na kuangalia mpigaji.Zilikuwa ni namba ngeni kabisa.Nikasimama pemBeni ya Toyota Hiace nikabonyeza kitufe cha kupokelea simu.
“Halloo” Nikaita
“hallow” Ilijibu sauti ya upande wa pili.Ilikuwa ni sauti nzito ya mwanaume.Sikuwahi kuisikia kabla sauti hii
“Naongea na nani tafadhali?Niliuliza.
“Tonny sauti hii umeisahau? akajibu yule jamaa.
Nilistuka baada ya kusikia kuwa mtu yule alikuwa akinitambua lakini mimi sikuwa na kumbu kumbu naye.Taa ya tahadhari ikawaka kichwani.
“hebu nikumbushe ndugu yangu wewe ni nani? nikamuuliza
“Mimi naitwa zuk………………………..”
Kabla hajamaliza sentensi yake nikasikia kishindo cha muanguko wa kitu kizito kama mtu karibu na nilipokuwa nimesimama.Nilitazama mbele yangu sikuona kitu.Niliipapasa bastora yangu na kuikuta imetulia mahala pake.Nikazunguka nyuma ya gari ili kuhakiki usalama zaidi kwa sababu nilikwisha hisi mahala hapo kama si salama.Nilitembea hatua tano za kunyata na mara mbele yangu akaanguka mtu aliyevaa koti refu na kofia.Kwa umbali niliokuwapo niliweza kumuona dhahiri mtu yule akiwa ameshika bastora mkononi.Kama umeme nikatoa bastora yangu ,niilikwisha anza kuisikia harufu ya damu eneo hili..
Kwa kasi ya aina yake nikajibanza pemBeni ya ile Hiace na kuangaza pande zote bila kuona mtu yeyote aliyekuwa hapo karibu.Taratibu na kwa tahadhari nikamwendea yule jamaa aliyeanguka pale chini na kuanza kumchunguza.Nilimgeuza na kugundua tayari alikwisha fariki kitambo.Kifuani kwa yule jamaa kulikuwa na matundu sita ya risasi nilipoyachunguza kwa haraka nikagundua muuaji alitumia bastora yenye kiwambo cha sauti.Niliichukua bastora ya yule jamaa iliyokuwa imeanguka pemBeni yake .Ilikuwa ni bastora aina ya 43 spark automatic inayotengenezwa Korea.Bastora za namna hii huwa ni silaha hatari. Kabla sijaamua nifanye nini,nikasikia kishindo cha muanguko wa kitu.Nyuma yangu kuna mtu alianguka.Nikaruka haraka na kujibanza tena nyuma ya ile Hiace.Sikuona mtu yeyote pale karibu na mahala nilipokuwa .Bastora zangu mkononi nikanyata na kumsogelea mtu yule aliyeanguka.Alikuwa amevaa suti nyeusi naye alikuwa na bastora mkononi.Hali ile ikaendelea kunichanganya ..
" Watu hawa ni akina nani? Nani anawaua kwa kutumia bastora yenye kiwambo cha kuzuia sauti? Nilijiuliza bila kupata majibu.Kitu kimoja tu nilichokifahamu kwa wakati huo ni kwamba eneo lile halikuwa salama hata kidogo.Kuna jambo zito sana lililokuwa linaendelea pale.Kuuawa kwa watu wale wawili kimya kimya tayari kulikwisha niwashia taa ya hatari kichwani.
Kitendo cha mimi kuonekana na walinzi wa klabu ile nikizunguka zunguka maeneo ya maegesho ya magari kiliwapa udadisi walinda usalama wale na taratibu nikawaona walinzi watatu wakijivuta taratibu kuelekea mahala nilipokuwa.Kabla hawajanifikia milio ya risasi ikasikika na wale walinzi wakaanguka.Moja kwa moja nikajua tayari wamepigwa risasi.Mwili ukanisisimka kijasho kikanitoka.Swali nililokuwa najiuliza kwa sasa ni huyu mtu anayefanya mauaji haya ni nani? yuko wapi? na lengo lake ni nini? . Nilihisi yupo mahala ambako anaweza kuona kwa urahisi kila kinachoendelea.Kama ndivyo kwa nini aue kila mtu anayenikaribia? Swali lingine nililokuwa najiuliza na kunifanya nitafakari kabla ya kufanya chochote ni uhusika wangu katika sakata hili.Sikuelewa nipambane na nani,nani ni adui yangu na nani siyo.Wakati nikijiuliza maswali haya nikasikia milio ya risasi kulekea kule nilikokuwa nimejificha.Vioo vya gari vikavunjwa vyote na gari kuharibiwa vibaya.Mimi nilikuwa nimejilaza chini ya uvungu wa gari.Milio ile ya risasi zilizokuwa zikivuma iliwafanya watu waliokuwa maeneo ya karibu wapatwe na taharuki na kukimbilia ndani ambako walipeleka taarifa juu ya vurumai ile iliyokuwa ikiendelea pale nje.Watu wakaanza kutoka ndani ya ukumbi kwa lengo la kutaka kushuhudia mapambano yale.Wote walijua kuna ujambazi ulitaka kufanyika.Baada ya idadi kubwa ya watu kuanza kutoka ndani kuja nje kushuhudia tukio lililokuwa likiendelea ghafla risasi zile zikakoma Taratibu nikajivuta na kutoka chini ya uvungu wa gari,nikatambaa hadi katika gari moja dogo aina ya Corola.Nikiwa pale niliweza kuliona gari moja likija kwa kasi toka katika lango la kuingilia klabuni hapo.Lilikuwa likija kwa kasi ya ajabu kuelekea kule nilikokuwa.Kabla halijafika maeneo yale ya maegesho kukasikika kishindo kizito na mlipuko mkubwa ukatokea .Gari lile lililipuka.Magari mengine yaliyokuwa katika maegesho nayo yakaanza kuwaka moto.Pamoja na ujasiri wangu lakini niliogopeshwa sana na tukio lile.Lile gari aidha lililipuliwa au lilikuwa limebeba mlipuko mkubwa.Kwa dakika hizi chache mahala hapa paligeuka kama sehemu ya kuchezea sinema.mambo yaliyokuwa yakiendelea hapa ni kama vile tuonavyo katika filamu,lakini hapa yalikuwa ni ya kweli.Kilikuwa ni kizaa zaa cha aina yake kuwahi kutokea nchini..
Wakati mlipuko ule unatokea nilijitupa chini na baada ya dakika mbili hivi nikasikia nimeguswa na kitu cha baridi shingoni ambacho moja kwa moja nilitambua kuwa ulikuwa ni mtutu wa bunduki.Mwili ukaingiwa na baridi.Nikajua kama mimi ndiye niliyekuwa mlengwa wa mashambulio yale basi tayari nimepatikana.Unapowekewa kitu kama hiki kichwani hutakiwi kufanya lolote lile kwa pupa .Inakubidi utii kila utakachoambiwa na mtu aliyekulenga na bunduki au bastora.Mtu anapokuwa amekuelekezea bunduki au bastora tayari anakuwa na moyo wa kuua na ukienda kinyume na matakwa yake basi dakika yoyote anaweza akakutoa uhai.Sikutikisika wala kuinua mkono wangu uliokuwa na bastora.
“Put your gun down and get up slowly” Nikaamriwa

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………..
 
Back
Top Bottom