SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
Usiku uleule Tano alirudi Kilwa Kivinje. Kuendelea na kazi yake ya ulinzi pamoja kumuwinda Dr Yusha. Maana usiku wa siku hiyo pia, ilikuwa lazima waipata mioyo kumi na tano katika chumba cha kuhifadhia maiti. Alifika Kivinje mishale ya saa tano usiku. Na kuikuta kazi ya kutoa mioyo imeshaanza.
Asubuhi mji wa Kilwa Masoko uliamka na taarifa mbaya tena. Taarifa ya kifo cha Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya Kilwa, Ndugu Alex Mwasola. Mwasola alikutwa ameuwawa nyumbani kwake. Muuza maziwa ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kushuhudia maiti ya Mwasola. Alikuwa na ratiba ya kumpelekea maziwa kila siku. Siku hiyo aligonga sana mlango nje, aliposukuma mlango ulifunguka na alipoingia ndani, alilakiwa na maiti ya bosi wake. Mwili wa Mwanasheria Mwasola, umelala juu ya sofa huku ukiwa umetapakaa damu kifuani. Alirudi nyuma na kuondoka bila kuaga. Hakumsimulia mtu kuhusu tukio lile, muuza maziwa aligeuka bubu.
Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, katika ofisi ya Mwanasheria watu walikuwa wamejaa. Ilikuwa siku ya kazi kwahiyo watu walijaa kufata huduma katika ofisi hiyo, watu wengi walikuwa wamekaa nje ya ofisi hiyo kwa kadri ya saa tano, bila Mwanasheria kutokea. Walijaribu kumpigia simu lakini simu yake iliita bila kupokelewa. Bahati mbaya Mwasola alikuwa hajaoa na wala hakai na mtu yeyote nyumbani kwake. Ilibidi atumwe mlinzi kwenda kwa Mwanasheria kumwangalia. Ilipo ofisi ya mwanasheria na mtaa wa National hakukuwa mbali sana. Yule mlinzi aliyetumwa kwa Mwanasheria alikutana na balaa.
Picha mbaya kama aliyokutana nayo Muuza maziwa. Mwili wa Mwanasheria ukiwa umelala sofani huku kisu kikiwa kinaning'inia kifuani mwake, na d ht 4 kwa sikuamu zilizoanza kukauka kifuani. Yule mlinzalishindwa kuvumilia, alipiga makelele, makelele yaliyowajaza kwa kasi majirani...
ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA.