🤣🤣🤣 Sisi wabongo unaenda kumuokota Single father miaka 46 au Single mother miaka 30 afu unataka ndoa idumu🤣🤣 Mtu ana ndoa bubu kibao zilomshinda🤣 Watu wasichojua ndoa sio makaratasi ya vyeti, ndoa ni watu, watu ni tabia.Watu wanaoana late. Hamna bond ya ujana pamoja.
Mnakutana wote mkiwa above 28. Eti ndio mnapendana na kufunga ndoa. Mshacheza mechi kibao huko nyuma na timu ya watu
Mume na mke wote wana ma X kibao. Ndoa haiwezi kudumu.
Wahindi na waarab wapo kibao Tanzania.. ndoa zao zinadumu sababu wanafunga ndoa mapema under 24. Na familia zinajuana kitambo ndipo vijana wao wanafungishwa ndoa