Uko sahihi kabisa. Kigezo kikuu cha kukusanya mapato kinapaswa kuwa pato la taifa. Kiwango kilichowekwa kitaalamu kwa kuzingatia mazingira ya hapa kwetu ni kukusanya kodi isiyopungua 25% ya pato la taifa (GDP). Hivyo mwaka huu TRA ingepaswa kukusanya angalau Shs 22tri/- (pato la taifa mwaka huu litakuwa Sh 90tri). Kuweka lengo kiduchu la kukusanya mapato (Sh 12tri au 13% ya GDP) kama ilivyo sasa ni sehemu ya ufisadi wa kitaasisi unaoliangamiza hili taifa. Kwa kuzingatia hii hesabu ni kwamba tabaka la mafisadi (watawala ndani) wamejiwekea lengo la kupora Sh 10tri/- mwaka huu kupitia tax fraud!!