Risasi zafyatuliwa Manzese kutawanya wafanyabiashara

Masikini CCM, mnazidi kupandikiza mbegu za chuki kwa vijana . . .

Mi nilishasema kwamba JK na wenzake ni kama wanashangaa mbona hiyo nguvu ya umma haijawafikia. Sasa inabidi wahamasishe kwa namna mbali mbali kama kuua watu arusha, kukamata Dr. Slaa, na sasa timua wafanya biashara Dar. Na sisi bado tunaogopa na kusema bado muda haujafika!
 
nilisikia risasi kwenye saa nne kasoro nikajua wenye vyao wanachukua kumbe hawa walipaushuru wa kinondoni
 
hakuna uvivu hapo,unaongea kwa kuwa upo nje ya system,mwana watu hawaelewi ni wabishi waking'ang'ania jambo basi,tangu mda walielezwa lakini hawakutaka,je ulitaka serikali ifanyeje,kuwaongoza wtz ni issue bana,tumeweka blabla mbele

ok,kwanini walikataa kutoka,ukiwauliza wanadai wateja ni wengi pale,kwa hiyo tusifanye ujenzi wa barabara ,tuwe na msongamano eti kwa kulinda wateja
chapa tuuuuu
maendeleo kwa taifa letu bana

sawa, lakini tuwe wakweli, suluhisho la matatizo ya wananchi (hata kama wanasababisha wao) ni kutumia risasi na mabomu? watakufa wangapi? kwani sheria kazi yake ni nini? na hayo magereza yamejengwa kwa kazi gani? au serikali imeona magereza hayalipi ila makaburi ndio dili?
 
Mi nilishasema kwamba JK na wenzake ni kama wanashangaa mbona hiyo nguvu ya umma haijawafikia. Sasa inabidi wahamasishe kwa namna mbali mbali kama kuua watu arusha, kukamata Dr. Slaa, na sasa timua wafanya biashara Dar. Na sisi bado tunaogopa na kusema bado muda haujafika!


ingekua ni hapa arusha ungekuta kuna machalii wamejifanya mohamed boazizi na ingekuwa tayari wako wpi karibu na jangwani
 
Huyo Magufuli anataka sifa za kijinga. Keshalewa sifa, na atapoteza umaarufu soon.
wabongo sisi bana,tuache watu wafanye kazi bana,tunaweka siasa ktk mambo ya msingi,angalieni msije ingiza siasa hata ktk ndoa zetu

mimi naunga mkono acha wakione,nasisitiza barabara ni zaidi ya kukuza uchumi,mkichelewa kazini mnalalamika,watu wameamuwa kufanya kazi ili kuweka mambo sawa mnalalamika,hehehehe,hii ndio tz bana na watu wake tulio wavivu wa kufikilia,
hapa china,serikali ikisema tu kuwa kesho eneo hili tunalihitaji kwa kazi maalumu hata kama mnapata pesa kuzidi maelezo,asubuhi hutamwona mtu eneo litakuwa wazi tayari kwa manufaa ya taifa
 
Wakati wanalijenga hawakujua hayo?
Je unajua historia ya hilo soko?kama hujui kaa kimya
Hilo soko lilijegwa kwa ajili ya wafanyabiashara waliokua wanafanya biashara
Manzese na kuvunjiwa Mabanda yao na kuhamishiwa hapo sasa wakivunjiwa na hapo waende wp?....
ndugu unaongelea maswala ya histolia wakatu huuu,mbona mnashangaza jamani,hata ujerumani wamevunja baadhi ya maeneo ya kihistolia kwa anjili ya kuweka kitu kitakacho waingizia pesa wewe unaleta history hapa
ebu tuachane na huo ujima tuna taka maendeleo yatakayo weza kurahisishia kupanda kiuchumi kirahisi zaidi na si kuangalia mambo ya histolia,waende machinga wakafanye kazi

tulidai kariakoo hapalipi,wamekuja wachina pakaanza kulipa tumelalamika wametolwa juzi watu wanalalamika kuwa biashara hazilipi

ukimwangalia mtu husoni haswa bongo hufanyi kazi
tokekeni bana,tumechoka blabla
 
Ndugu zangu, mabanda hayo nadhani yalivunjwa either usiku au alfajiri ya leo maana mimi nimepita hapo saa kumi na mbili leo asubuhi, mabanda yote yalikuwa yameangushwa. Hakuna hata moja lililosimama. Nikajiuliza maswali haya:
  1. Kama hawa walivunja usiku in maana kuwa wenye mitumba yao hawajachukua chochote,
  2. Kama hawajachukua na sasa hivi hayaonekani, ina maana mamlaka iliyovunja na wavunjaji wamewaibia wafanya biashara na kuwafilisi
  3. Hawa ambao sasa wamefilisiwa na hawana ajira yoyote nyingine, watafanya nini? Maana Manzese ya miaka ya tisini itarudi, hukatizi pale na saa, simu, cheni, kiatu wala mkanda mzuri
  4. Je hao watu watakufa njaa wakiona au watajiingiza katika magenge ya uhalifu wakidai yakuwa heri kifo kinikute najitahidi kutafuta anfalau niishi kwa siku moja?
  5. Je hizo familia ambazo zilikuwa zinawategemea hao watu sasa wataishi vipi? Kama kuna wafanyabiashara mia tano, na kwa uchache kabisa mtanzania mmoja mwenye shughuli anategemea na watu kumi ina maana watu elfu tano maisha yao yamebadilishwa kabisa na tutazalisha watoto wengi wa mitaani na malaya wengi, pamoja pia na mashoga
  6. Ikumbukwe pia hao watu walihamishiwa hapo kutoka pale darajani Manzese na soko la ndizi likahamishiwa ndani, sasa kuwavunjia bila kuwapa maeneo mbadala tunategemea nini?
  7. Naunga mkono kusafisha jiji na maneno ya barabara lakini lazima tuwape watu sehemu mbadala ya kuendeshea kazi yao.
  8. Watawala wetu hawafikirii hata kidogo kuwa Tunisia imeanzia wapi!!!! Labda hawasomi habari kwa maana labda haiwahusu lakini hata Misri ilidhani vivyo hivyo. Kwa wale wasiojua ni kwamba, hao unaowaita mgambo wa jiji ndiyo waliowasha moto Tunisia baada ya kuharibu biashara ya kijana mmoja msomi lakini kwa kukosa kazi akabuni biashara yake ndogo ya kujikimu na hapo jamaa wakaja wakateketesa na ndivyo yule kijana akaona sasa mwisho wangu umefika maana hata serikali hainitaki tena na akasema sasa mateso basi akanunua petroli akajimwagia akijiwasha moto na hapo ikawa ndiyo mwisho wake, lakini ikawa ndiyo mwanzo wa mwisho ya Benali na Chama chake, na sasa hivi Chama cha Benali kimukufa na ile regime yake yote ya utawala haipo pia. Hivyo basi hata kwa CCM na Kikwete, hili laonekana dogo lakini waangalie sana. Paka ni rafiki wa binadamu na tunaishi naye majumbani lakini siku ukifunga madirisha na milango yote unataka kumpiga atajua sasa hapa nauawa na lazima nijitutumue kujiokoa na hapa anaweza akawa hatari kuliko hata chui. Jamani watawala angalieni sana maamuzi yenu hasa yanayogusa maisha ya watu. Nasema watawala maana hapa Tanzania sidhani kama tuna viongozi, wengi ni watawala. They are Rulers NOT Leaders, "We want Leaders NOT Rulers"
  9. Mheshimiwa Rais J.M.Kikwete naomba uvae ngozi ya chui sasa kwa wasaidizi wako, la sivyo wameshakupaka matope kiasi cha kutosha. Kama unawasaidizi wa ukweli ni wachache sana, maana wengi wanajisaidia wenyewe na wanakutumia wewe kama mhimili wao!!!!
  10. Ndugu zangu naomba tuiombee nchi yetu ili tusiende katika machafuko. Machafuko leo yakianza polisi wengi wa vyeo vya chini pamoja na wanajeshi wanaweza haraka sana kujiunga na raia kwa maana wote tupo katika hali hii ngumu ya maisha!!!
TANZANIA NCHI YANGU NAKUPENDA SANA. KILA WAKATI NAKUOTA WEWE JINSI MAJIRANI WANAVYOKUONA NCHI YA AMANI. MUNGU TUBARIKI WATANZANIA, UTUONDOLEE WATAWALA WADHALIMU UTUBAKIZIE VIONGOZI WAZURI WA KUONGOZA WATU WAKO. EWE MUNGU USKIYE KUOMBA KWETU!!!
 
Dah! mi nimechoka kabisa....mabomu ya nini sasa?? hivi hamna njia nyingine nzuri ya kutuliza mambo bila kutumia mabomu.....where this country is going is not good....serikali inawafanya watu wawe sugu, alafu matokeo yake mtayaona.
 
Nawaonea huruma sana CCM!,

Eee mungu wasamehe waja wako CCM maana hawajui walitendalo, Naomba uwape vijana moyo wa kuikataa CCM kwa Amani na Kuikubali CHADEMA kwa Amani ili tuendelee kuishi kwa Amani Daima Kama mwanzo na Sasa na Hata milele!.
 
Kuna kitu viongozi wetu wanashindwa kukiona....

na maoteko yake?

Kuna kitu wanashindwa kujifunza....!

in that case... they should be waiting for the worse...!!
 
safi sana waliambiwa watoke wakabisha

Kweli unafikia hatua yakufurahia mateso ya mlala hoi????? check vizuri brain yako.
 
kwani kuan maeneo mangapi yapo katika hifadhi ya barabara mkaamua kuanza na hapo? mbona magufuri kasema tanesco ubungo ipo ndani ya hifadhi kwa nini asianze na pale?
 
tatizo letu tumekuwa na ile tabia ya kuwa hapa mpaka waje polisi ndio tuondoke,je mbona wale jamaa waliondoka mapema hawakubughudhiwa? na serikali inapo kuelkeza kuwa huruhisiwi kufanya biashara haba tunahitaji eneo kwa ajili ya kufanya kazi ya kijamii ni lazima ukubaliane nae na isitoshe tayari walishatengewa maeneo ya kufanya kazi mafano machinga complex lakini wakapuuza

jamani umefika wakati sasa kuweka siasa pembeni
mfano ktk nchi za wenzetu unapoingia supermarket utakuta
-kuku
-mchele
-viazi
-nguo
-mikate
-maziwa
-sim-pen
-ndizi
-nyama
-maziwa
-mifagio
-madaftari
lakini hapa bongo hatutaki kiubadilika na kwenda na wakati hii ingesaidia kupunguza misongamano ya watu ktk visoko vidogovidogo,na kinacho tusumbuwa tunadhani kuwa supermarket ni za watu maarufu tu hiyo zana ndio inatupelekea kuto kuamini mazingira ya Machinga Complex kwa kuwa pale karume pamekaa kisupermarketi
so wateja hawatakwenda na tutapunguza kipato,sio kweli wanaohitaji huduma wataifuata tu kwani itapatikana hapo tu kwanini asiifuate?

kwa hiyo tunapendelea tusiwe na masoko mengi kila sehemu ni kujaza nafasi ambazo tungeweza kuzitumia kwa mambo mengine

kwa hiyo huu ni wakati wa kumwacha magufuri afanye kazi yake,yeye huwa habaatishi

ebu angalia linabomolewa jengo la Tanesco pale Ubungo kwa maendeleo ya Taifa letu,leo tuwaache machinga eti kuwatowa ni kuto watendea haki,na hawa wanaopata taabu ya usafiri je?
hamuoni barabara za wenzetu zilivyo? wamefanya kazi na waliweka bla bla za kisiasa pembeni wakafika hapo walipo

TUACHE WATU WAFANYE KAZI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU,TUSIWEKE SIASA KTK MAMBO YA MSINGI
 
kwani kuan maeneo mangapi yapo katika hifadhi ya barabara mkaamua kuanza na hapo? mbona magufuri kasema tanesco ubungo ipo ndani ya hifadhi kwa nini asianze na pale?

WEWE upo apa kisiasa,walinza kubomoa jengo la tanload na kinachofuata ni lilejengo lefu la Tanesco kwani kuchelewa kwetu kulibowa ni kumsababisha mkandalasi kuchelewa kumaliza kazi kwa wakati,na utambue kuwa kila kifaa kilicho site cha mkandalasi pindi mda ukifika wa kumaliza ujenzi nyinyi hamjabomoa ina maanisha mtalipa riba ya vifaa kukaa site bila kufanya kazi na pengine mkandarasi angetaka kuvitumia sehemu nyingine

kwa hiyo maeneo yote yalio ktk hifadhi ya barabara yatabomolewa kabla mkandalasi hajaanza kazi

lile soko lilikuwa ktk ratiba ya kubomolewa tangu mda tu,na walipewa nafasi ya kuondoka hawakuondoka,ulitaka serikali ifanyeje?
towa jibu mkuu
 
Back
Top Bottom