Kaka si kweli kuwa Mwang'onda alikuwa mtandao. Yeye alifanya kila njia ya kupambana na mtandao hadi mwisho alipoona upepo mkali mno ndipo alipojipeleka ktk mtandao na kufanya makubaliano maalum nao halafu ndipo alipobebeshwa dozi iliyomfanya Mzee Ben kuingia line na kukubali yaishe. TOM alikuwa karibu "kiasi" na mtandao lakini sababu ya kupewa ubunge ni kuhakikisha kuwa Mzee Mwang'aonda anaendelea kuwa loyal kwa JK na kumfanya ajione ni mdau huko hata kama sio kweli.
Ahsante kaka, ninachojua ni mstaafu alipoenda Kenya ku-monitor uchaguzi kule kwa miezi mitatu aliogopeshwa sana na kushindwa kwa Uhuru kilichomfanya amkatae Kigoda chaguo la mkapa, aliporudi ndipo alipojiunga rasmi na mtandao kupitia kwa Rostam na Lowassa, lakini kwa siri kubwa sana kwa sababu at the same token yeye pia ndiye aliyekua mmoja wa wafadhili wakubwa financially wa JM, sipendi kuyarudia tena na tena maana nilishayasema sana awali, mtandao walitaka kumlipa kwa kumpa uwazri mdogo tom, mstaafu aliposikia akakimbia kwa mkulu mmoja na kumuuliza kama ni sawa, ni huyu mkulu ndiye aliyemuambia kwamba hapana kubali apewe ubunge tu, lakini omba rafiki yako na patner wako wa biashara mwakipesile apewe u-RC.
Mstaafu alifanya mambo mengi sana tena kwa siri kubwa sana, kama sio mtoto wake kupewa ubunge hakuna ambaye angejua mimi nilipewa ujumbe mapema na waziri mmoja wa sasa, lakini hata mimi nilikuwa ninamuaminia sana mstaafu sikukubali kabisa nikasema ni uongo na majungu, haiwezekani mtu atoe mahela yote yale kwa JM lakini yuko kwa mtandao, baada ya kugundulika kuwa ni kweli mstaafu alikua nao, siku hizi hata jm haongei naye tena siku hizi, na huyu ndiye aliyekuwa kipenzi chake.
Mkuu OmaryIlyasi ni habari ndefu sana siwezi kuzirudia zote, kuna siku moja mtoto mmoja wa jm aliwakamata lowassa, rostam na mstaafu kwa bahati mbaya usiku sana mahali Dodoma, alipofikisha ujumbe kwa kambi ya jm wakamkatalia kua sio kweli labda amefananisha tu, mimi nilipowapelkea ujumbe toka huyu waziri mmoja wa sasa walikataa kabisa sio kweli, baadaye tena niliambwia na mama ntimizi ambaye by then alikuwa karibu sana na sumaye, the same story lakini wakagoma kuwa sio kweli, only now ndio wamekubali.
Kazi ya Mangula haikufanywa na UWT kama asasi bali ilifanywa na sekretariat ya CCM maadili ambayo inahusishwa watu wa UWT. Na ukweli ni kuwa ripoti hiyo ipo imejaa kibao na wala sio tunu kama inavyodhaniwa hapa. Ripoti imejaa ukweli, uongo na habari za kusadikika. Hata hivyo kutoka hadharani kwa kweli ni hatari kwa chama na hata serikali iliyopo madarakani kama ilivyo kwa ripoti nyingine nyingi za aina yake.
Siku tu alipoapishwa kuwa rais, muungwana the first thing alitaka kumtoa mangula kazi na makatibu wote wa mikao na wilaya, akidai ndio waliohusika na kuandika yale mafaili, lakini akatulizwa na mkulu mmoja wkamba ukiwafukuza huko mikoani watajiunga na upinzani na wataitwanga CCM kwenye uchaguzi, na besides akaambwia yeye bado hajawa mwenyekiti wa CCM, ni rais tu, ndio mtandao wakaanza kampeni chafu ya kumlazimisha mkapa atoke mapema kwenye uenyekiti, alipotoka tu kitu cha kwanza muungwana alimtoa mangula na sekretariati yake yote kulipa kisasi cha yale maafaili na mengine mengi lakini hii ni kwa ufupi ninachojua, huenda pia kuna tofauti zingine, lakini this is what I know!