Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Link inaenda.Ila lazima ulilie 500 kusoma hilo gazeti la citizen.
Kwa kifupi hilo gazeti linasema kuwa bora asingejiuzulu mwaka 2008.
Lakini ukisoma ripoti ya mwakyembe hakuna jinsi angepona
Richmond ni yeye na JK....ila kulinda Serikali JK kamtosa.....subiri tribute ya jK monduli....asiposema hatasema tena bora afe nacho tu unafiki kiwango cha lami......JK aseme ukweliii ....siku mazishii hana jinsi
 
LEO KATIKA HISTORIA 2008

“TATIZO NI UWAZIRI MKUU”

"Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli. Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.

Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni “Natural Justice”. Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.

Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo. Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema ulitoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.

Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwahiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, “Nimefadhaika Sana, Nimedhalilishwa Sana, Nimeonewa Sana Katika Hili.” Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza.

Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.

Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais. Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Waziri, nawshukuru Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa CCM tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nashukuru……”.

Wabunge makofi pwa pwa pwa pwa pwa pwa

Nimekumbuka Hotuba ya Mh. LOWASA
 
Richmond ni yeye na JK....ila kulinda Serikali JK kamtosa.....subiri tribute ya jK monduli....asiposema hatasema tena bora afe nacho tu unafiki kiwango cha lami......JK aseme ukweliii ....siku mazishii hana jinsi
 
FB_IMG_1707597550375.jpg
 
Wakati hii thread inaanzishwa mwaka 2008 nilikua natoka Mpanda kuelekea Tabora kwa train kwa safari ya kuelekea Meatu mkoa wa Simiyu zamani ikiwa Shinyanga. Nilikua namiliki Nokia jeneza. Watu walikua wanamwaga madini huku JF.
 
Link inaenda.Ila lazima ulilie 500 kusoma hilo gazeti la citizen.
Kwa kifupi hilo gazeti linasema kuwa bora asingejiuzulu mwaka 2008.
Lakini ukisoma ripoti ya mwakyembe hakuna jinsi angepona

Kwa nguvu alokuwa nayo wasinge mfanya kitu, tungeweza rudi ktk uchaguz haraka.

Sema hata ile plan ya kujiuzuru nadhani he missed some clues ama alikuwa na over confidence na hakika aliithibitisha hiyo.
 
Sijaona na ile ya Mwakyembe baada ya PM kutoa hotuba ya kujiuzuru, namnukuu Mwakyembe tumeshindwa kusema mengine kulinda serikali, je walikuwa wanalinda nini?
 
Kwa nguvu alokuwa nayo wasinge mfanya kitu, tungeweza rudi ktk uchaguz haraka.

Sema hata ile plan ya kujiuzuru nadhani he missed some clues ama alikuwa na over confidence na hakika aliithibitisha hiyo.
Huyu alishauriwa na mwenzie yule burushi,kwamba kishanuka jikate ili asiwajibike .maana issue ilikua nzito.
 
WEKA WI-FI ZA T¡G0 ZINA SPEED KUBWAA MNOO!
HUU SIO MDA TENA WA KUWAZA KUISHIWA NA DATA, ROUTER NI BEI NAFUU SANA!

⚫KWENYE BISASHARA YAKO WEKA WI-FI

⚫KWENYE SHULE WEKA WI-FI
⚫KANISANI WEKA WI-FI

⚫KAZINI WEKA WI-FI
⚫KWENYE KAMPUNI WEKA WI-FI

⚫NYUMBANI KWAKO WEWE NA FAMILIA YAKO WEKA WI-FI
⚫CHUONI WEKA WI-FI

⚫UNA SECURITY CAMERA FUNGA WI-FI

⚫SEHEM ZINGINE AMBAZO SIJAZITAJA WEKA WI-FI

TUMIA DATA UNLIMITED, YANI BILA KUWAZA KUA GB ZITAISHA?

NJOO NIKUPE ROUTER ZENYE UWEZO MKUBWA TECNOLOJIA YA 5G SPEED HADI 200mbps, NA UNAWEZA KULIPA KIDOGO KIDOGO !

MKOA WOWOTE ULIPO DELIVERY NI FREEE!!

GHARAMA NI NAFUU, SPEED KUBWAA (pia laini pekeyake bila router nakuwezeshea bando unlimited kwa bei poa)
NICHEKI: 0717700921
 
Posted Date::2/4/2008
Bunge: Fukuto la Richmond,Spika aahirisha ziara ya Marekani
  • Waziri Mkuu, Makamba wateta kwa saa tatu
  • Wabunge CCM kukutana leokuweka mkakati

* Yadaiwa kuna mpango wa kuzuia mjadala

Na Tausi Mbowe, Dodoma
Mwananchi

SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta ameahirisha safari yake ya kwenda Marekani.

Taarifa ya kusitishwa kwa ziara hiyo ilitolewa jana na Naibu Spika, Anna Makinda na kufahamisha kwamba leo Spika atakuwepo Bungeni kuendelea na shughuli za Bunge.

Hata hivyo katika tangazo hilo la Naibu Spika Makinda hakutaja sababu ya Spika kuahirisha safari hiyo.

"Wabunge kama mnakumbuka, Spika alitangaza kuwa atasafiri leo na kurudi siku ya Alhamisi, ameniagiza kutangaza kuwa amesitisha safari hiyo ya Marekani na kwamba kesho (leo) atakuwepo bungeni kuendelea na shughuli za Bunge kama kawaida," alisema Makinda.

Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa Spika amefikia uamuzi huo ili kuokoa jahazi kutokana na hali ya kisiasa kuchafuka kufuatia msimamo ulionyeshwa na wabunge kutaka ripoti ya Richmond iletwe bungeni kwanza kwaajili ya kujadiliwa.

Wakati anawaaga wabunge, Spika Sitta alimuagiza Naibu Spika, Anna
Makinda asije akakurupuka na kuyavamia mambo yote nyeti na kuyazungumza au kuyatolea maamuzi katika bunge hilo wakati yeye hayupo.

Sitta alisema kuwa mambo yote 'nyeti' yatasubiri mpaka atakapokuwepo na kwamba Naibu Spika asije akarudhusa kujadili mambo makubwa wakati hayupo.

Spika alitolea mfano wa sakata la ufisadi la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na la Richmond na kusisitiza kuwa ili kujadili masuala hayo lazima yeye awepo.

Kauli hiyo ya Spika ina maana kuwa ripoti hiyo isingejadiliwa mpaka yeye yaani wiki ya mwisho ya kikao cha 10 cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma.

Juzi wabunge walisusia semina iliyoandaliwa na na Wizara ya Nishati na Madin ikwa lengo la kuwaelimisha kuhusu muswaada wa Sheria za Umeme na Biashara ya mafuta ya Petrol wakidai wapewe kwanza ripoti ya Kamati ya Richmond ili waijadili kabla ya kuupitisha muswada huo.

Wabunge hao pia walisema kuwa hawana imani na wizara hiyo pamoja na Shirika lake la Umeme Tanesco kwa kuwa taasisi hizo zimejaa uchafu na kwamba hawawezi kujadili masuala ya mikataba mengine mpaka wajisafishe.

Taarifa zilizopatikana kutoka miongoni mwa wabunge mjini hapa, zilieleza kuwa ili kuua mjadala bungeni, serikali inataka kutumia Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (Takukuru), kukamata baadhi ya maafisa na kuwafikisha mahakamani.

Chanzo chetu cha habari kilisema, juhudi zilikuwa zikifanyika tangu mwishoni mwa wiki kwa viongozi wakuu wa serikali kuwasiliana na Takukuru kwa ajili ya kuchukua hatua hizo.

Inadaiwa kuwa, kupelekwa kwa maafisa hao kuwatanyima haki wabunge kujadili suala hilo kwasababu ya utaratibu wa kuheshimu utawala wa sheria, lengo likiwa ni kuwaziba midomo wabunge hasa kutokana na cheche walizoonyesha mwishoni mwa wiki.

"Viongozi wanahaha kuhusu Richmond. Zimeenea habari kuwa viongozi wanaotaka kuua hoja hiyo bungeni wataitumia Takukuru kuwafungulia kesi maafisa kadhaa wa serikali kuwa walikula njama za kuihujumu Tanesco, iliwa na lengo la kuzuia mjadala bungeni," alisema Mbunge mmoja wa CCM na kuongeza:

"Upo uwezekano mkubwa watu hao watakamatwa kabla ya kikao cha wabunge wa CCM kinachofanyika leo."

Hata hivyo, Takukuru iliwahi kutoa taarifa za kuwasafisha maafisa waliohusika na kwamba hakuna rushwa iliyotumika kwenye mchakato mzima wa kufikia utoaji wa zabuni yenye mashaka ya Richmond.

Taarifa hiyo ya Takukuru ilipingwa na wananchi, huku Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Edward Hosea akisimama kidete kuwa hisia za rushwa ni juu ya mkataba huo ni majungu.

Kwa mujibu wa maelezo ya awali ya Spika, safari ya nchini Marekani ilikuwa na lengo la kuliongezea Bunge uwezo katika masuala mbalimbali yanayohusu shughuli zake na kwamba ingekuwa ya muda mfupi na kuahidi kurudi siku ya Alhamisi na kuendelea na shughuli kama kawaida na kujadili mambo hayo nyeti.

Siku hiyo pia Spika aliliambia Bunge kuwa bado mashauriano baina ya ofisi yake na serikali yanaendelea kuhusu ripoti nzima ya Mahesabu ya Akaunti ya Nje ya Nchi (EPA), kupelekwa bungeni kwaajili ya kujadiliwa.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Yussuf Makamba jana walikutana kwa dharura kuweka mikakati itakayowezesha Wabunge wa CCM kuwa na kauli moja kutokana kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa kwa wabunge hao dhidi ya ripoti ya Richmond.

Viongozi hao wajuu wa chama hicho walikutana jana kwa zaidi ya saa tatu katika Ofisi za Bunge ili kuokoa jahazi kutokana na mgawanyiko huo unaonekana kutokea wazi wazi.

Habari zaidi zinasema kuwa wabunge wote wa CCM watakutana leo kwa ajili ya kuweka mkakati kabambe ikiwa ni pamoja na kuwa na kauli moja katika sakata hilo lilosababisha Spika Sitta kukatisha safari yake ya Marekani.

Kwa upande wa wabunge wengi walionekana kuwa na shauku kubwa kutaka ripoti hiyo ifikishwe bungeni kwanza ili wapate fursa ya kuijadili kwa undani ripoti hiyo.
Duuh we jamaa uliwaza nini kuchapisha bandiko kwa maandishi yanayoumiza macho hivi?
 
Mara baada ya kuahirishwa kikao cha Bunge jana jioni, Waziri Mkuu aliitisha kikao cha Mawaziri na Manaibu wao akidai ni kikao cha KIKAZI.

Katika kikao hicho aliwaambia kwamba serikali ilikua na nia njema katika suala zima la Richmond na kwamba mawaziri wanaothubutu kushabikia ripoti ya Richmond watajuta na itawagharimu. Akawaambia watumie nafasi zao "Kuwaelimisha" wabunge wote kuhusu nia njema ya serikali katika Richmond ili wasiishambulie. Wanasema aliingia akiwa hana raha na alipotoka wenzake walibaki wameduwaa na wakitafakari kwamba wanaambiwa watetee ripoti ambayo hawajui inasema nini!

Wakasema wanasubiri waione ili wajue ni wapi imekosewa ndipo wajue nini cha kusema, lakini hawawezi kujadili ama kutetea HEWA kwani na wao ni Wabunge ambao wametumwa na wapiga kura wao na hawana UHAKIKA na nafasi za UWAZIRI bali UBUNGE ndio walikotumwa. HATA HIVYO wakaambiwa kwamba SERIKALI HAITAWASILISHA TENA LEO ripoti ya Richmond katika kikao cha wabunge wa CCM bali itawasilishwa kwa wabunge wote na kujadiliwa. LOLOTE linaweza kutokea kati ya LEO (Jumanne) NA KESHO (Jumatano) siku ambayo JK alitoa nafasi ya mwisho kwa wabunge wa CCM KUWATOSA Mawaziri wanaoona kuwa ni MZIGO kwao.


Soma

Hapa Dodoma kuna TENSION ya hali ya juu

Na ifuatayo ndiyo ripoti ya kamati ya kina Mwakyembe:
Tunechezewa sana
 
Back
Top Bottom