Ripoti ya makinika acacia yaijibu serikali

tembajr

JF-Expert Member
May 27, 2016
841
1,000
Kama kilivyo kichwa cha habari hapo juu bila kupepepesa macho KAMPUNI YA ACACIA YAIJIBU SERIKALI..
Kampuni ya ACACIA inayomiliki mgodi wa Bulyanhulu imekiri kupokea kiasi cha Trilioni 217.23 kama makisio ya awali ya ukadiriaji na uboreshaji wa mchakato endelevu wa upanuzi wa miundombinu iliyosaidia katika zoezi la kukamilisha udurufishaji wa nakala vivuli za usafirishaji na uagizaji wa vifaa ambavyo hapo awali vilisemekana kutumika katika zoezi la sensa mwaka 2002.

Katika barua iliyoandikwa leo baada ya taarifa ya kamati kusoma na kukabidhiwa kwa Mwenyekiti wa bodi ya korosho wilaya ya Namtumbo, nahodha huyo amewataka waandamanaji wawe wasikivu ili kupisha urasimishwaji wa muswada wa pili wa marekebisho ya dokezo hilo ambalo lilisomwa katika vyombo vya habari wiki iliyopita.

Hata hivyo, Dr. Dalali Kafumu amesema kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha kuwa, mchezo huo uliopangwa kufanyika Agosti 3 mwaka huu unakidhi matakwa ya sheria ya usafirishaji wa saruji katika maeneo yote ya mipaka ya Tanzania na eneo la maziwa makuu

Duru za kisiasa zinamuhusisha bingwa huyo wa zamani wa ndondi kwa uzito wa kati afrika kujiunga na kundi la TYCS huku kukiwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika mrahaba uliotumika kutaifisha nyenzo muhimu za kilimo cha mkonge katika wilaya ya Uyui, mkoani Rukwa.

Katika kujibu hoja hiyo, msemaji mkuu wa jeshi la Polisi amewaomba wanafunzi kuwa watulivu ili kuruhusu randama ya sheria hiyo ipitiwe upya na wadau wa sekta ya uvuvi ili kuongeza kiasi cha makinikia katika mkongo wa Taifa ifikapo mwaka 2019. Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa MKUKUTA, Jaji Mkuu Haji S. Manara aliomba apewe muda ili azungumze na asasi za kiraia kupata mawazo yao juu ya ulazima wa uanzishwaji wa mamlaka za maji safi na maji taka katika mji mdogo wa Hai.

Katibu mkuu wa Chama cha walimu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo..

Ukimind njoo nipige, niko home naangalia Tv
 

pecial

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
638
500
kumejaa wehu humu kumbe,, hii pesa ya viroba mnapata wapi na hali ngumu hii?
 

MPHINGU

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
519
1,000
Tembajr, kama unandugu alieiona ripoti hii akuwahishe MILEMBE coz umetujaza wasiwasi
 

Bishop Hiluka

Verified Member
Aug 12, 2011
6,340
2,000
:):oops:o_O:rolleyes::eek::p:mad::( yaani... kwa vyovyote wewe utakuwa mtoto wa mjomba wake na shangazi wa babu yake na mtoto wa binamu yake na jirani wa demu wa mwano kabisa! Nashindwa kushangaa...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom