Hivi karibuni, kuna habari tatu zinazostahiki kuangaliwa kwa pamoja. Ingawa zinaonekana hazihusiani, lakini zote zinafichua mabadiliko yanayotokea Afrika katika jukwaa la dunia.
Habari ya kwanza ni kwamba michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar ilifunguliwa, ikiwa ni mara ya kwanza kwa bara la Afrika kuandaa michezo ya ngazi ya Olimpiki. Kwa muda mrefu, matukio makubwa ya Olimpiki yaliandaliwa barani Ulaya, Amerika, na Asia, huku wanariadha wa Kiafrika mara nyingi wakisafiri mbali kushindana katika nyanja za nchi nyingine. Safari hii, jukwaa liko Dakar, Senegal. Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa Kirsty Coventry alisema, huu ni wakati wa kihistoria kwa Senegal, Afrika, na michezo yote ya Olimpiki. Kuipa Afrika haki za mwenyeji ni uthibitisho wa uwezo wake wa uandaaji na sifa yake kama jukwaa la kimataifa kwa vijana kuwasiliana na kufunzana. Afrika si mwangalizi tena, pia inaweza kuwa mwenyeji.
Habari ya pili ni kwamba Umoja wa Afrika hivi karibuni ulizindua rasmi shirika lake la ukadiriaji wa mikopo. Kwa miaka mingi, tathmini ya ustahiki wa mikopo huru wa nchi za Kiafrika ilidhibitiwa na mashirika machache ya ukadiriaji ya nchi za Magharibi, huku ukadiriaji ukiamua moja kwa moja gharama za ufadhili. Takwimu za Umoja wa Afrika zinaonyesha kwamba malipo ya deni la nje la Afrika yanaongezeka kutoka dola bilioni 61 mwaka 2010 hadi dola bilioni 163 mwaka 2024. Mwezi Juni mwaka jana, Fitch ilishusha kiwango cha Benki ya Uagizaji na Usafirishaji ya Afrika hadi BBB-, na benki hiyo baadaye ilitangaza kukomesha ushirikiano wake na Fitch Januari mwaka huu. Kisha Fitch ilishusha kiwango tena hadi BB+ na kuondoa kiwango chake. Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf, alisema kwamba shirika hilo jipya halikusudiwi kuchukua nafasi ya mashirika ya ukadiriaji ya kimataifa yaliyopo, wala kupata ukadiriaji mzuri kwa wakopaji, bali kutoa mtazamo wa ziada, huru, unaozingatia Afrika. Kutoka kukubali ukadiriaji wa nje bila kujali hadi kuchukua kipimo chake, hii inaonyesha hamu ya Afrika ya kudai haki yake ya kufafanua sheria za uchumi wa kimataifa.
Hoja ya tatu inavutia zaidi. Waziri Mkuu wa Uingereza Andy Burnham aliandika makala katika gazeti la The Guardian, kwamba yuko tayari kuomba msamaha rasmi kwa niaba ya nchi yake kwa jukumu la Uingereza katika biashara ya utumwa ya kupitia bahari ya Atlantiki, mada inayotarajiwa kuwa mezani katika mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Madola wa wiki hii. Hii si nia njema kutoka Uingereza, kwani kwa miaka mingi, serikali za Uingereza zilikataa kutoa msamaha katika ngazi ya kitaifa. Ilikuwa ni kupitia utetezi endelevu wa makoloni ya zamani barani Afrika na Caribbean ambapo suala hili lilihama kutoka pembezoni hadi meza ya mazungumzo katika Mkutano wa Jumuiya ya Madola wa mwaka huu, jambo lenyewe lnawakilisha mabadiliko.
Baada ya kujadili habari hizi tatu, mabadiliko yanaibuka: hapo awali, Afrika mara nyingi ilikuwa upande usio na msimamo, uwanja wake wa kucheza ulichaguliwa na wengine, sifa yake ilipimwa na wengine, na simulizi yake ya kihistoria ilitawaliwa na wengine. Leo, mafanikio yanatokea kwa wakati mmoja katika pande tatu. Hata hivyo, hatuwezi kuwa na matumaini makubwa kupita kiasi: Mchezo mmoja wa Olimpiki ya Vijana hauwezi kutatua matatizo ya maendeleo ya muda mrefu; shirika jipya la ukadiriaji wa mikopo linakabiliwa na safari ndefu ya kutambuliwa na watu wengi katika masoko ya mitaji ya kimataifa; na madai ya fidia bado yamekataliwa waziwazi na upande wa Uingereza.
Lakini kuongezeka kwa hadhi ya kimataifa mara chache kulitokea ghafla; badala yake, hupatikana kupitia mfululizo wa matukio ya michezo, utaratibu mpya, na juhudi endelevu katika majukwaa ya pande nyingi. Afrika ikiwa mtazamaji wa muda mrefu imekuwa kmshiriki muhimu katika masuala ya kimataifa, hii inaonyesha haswa ongezeko la jumla la nguvu ya Dunia ya Kusini!