Tajiri wa kinyankole
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 1,971
- 4,890
Kwa taarifa ya tume ya uchinguzi wa mambo yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa raisi wabunge na madiwani october 29.2025 na jaji chande imeonesha kuwa baadaya ya uchunguzi tume imebaini kuwa
1.Polis walikuwa kwenye vituo vya kupiga kura bila siraha.
Sasa maswali mengi watu wanajiuliza je watu waliojeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali je walijeruhiwa na watu gani wakati wa maandamano.
2.kuwepo kwa vifo zaidi 500
Kama vyombo vya dola havikutumia silaha hao waandamanaji waliuawa na nani na wauaji walitumia nini.
3.watu kujiteka kwasababu ya madeni na imani za kishirikina pamoja na usafirishaji wa binadamu nchi za nje
Je ni kweli polepole na watu wengine walijiteka kama anavyosema yeye kwenye uchunguzi kwasababu ya madeni na imani za kishirikina ?
4.kwamba tume haijajikita kutaja watu waliohusika na yaliyotokea october 29 isipokuwa vichocheo vilivyofanya yatokee ya october 29.sawa tumeelewa.
Je hii kauli ya kusema upelelezi ufanyike tena kujuwa watu waliosababisha yatokee ya october 29 na wawajibishwe mnaona yupo sawa huyo mliyemkabidhi makaburasha ya uchunguzi? Unasema unataka kuridhiana ! Unaridhiana na nani na unafanya upelelezi kubsini wahusika wawajibishwe.
Hivi viongozi wa serikali hamuoni mnateketeza fedha za umma kwa hadaa na ulaghai kwa mambo ambayo mnajuwa hamuwezi kuyatekeleza.
Hivi ni lini viongozi wa serikali mtaelewa kuwa kwa sasa tanzania ya sasa haina watu wa miaka 1980 wa kudanganywa kila kitu.
Madaraka yanaisha ipo siku mtajibu kwa matendo yenu ya hatari mliyoyaratibu kabla wakati na baada ya uchaguzi mkuu.
Mtambue kuwa jinai haifi na sheria huwa zinabadilika msishangae kuja kuwa wafungwa wa baadae kwa matendo mliyoyafanya.