Ripoti ya hali ya ukeketaji nchini inaonesha Mkoa wa Manyara ni kidedea kwa kukeketa wasichana ukifuatiwa na Dodoma

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
RIPOTI ya hali ya ukeketaji nchini inaonesha kuwa Mkoa wa Manyara ni kidedea kwa kukeketa wasichana huku ripoti hiyo ikieleza kuwa wasichana wanaozaliwa au kulelewa na mama aliyekeketwa hukeketwa pia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukeketaji kwa Mikoa ya Kanda ya Kati iliyoandaliwa na Redio ya C-FM ya Jijini hapa jana, Msimamizi Mkuu wa vipindi wa Redio hiyo, Emmanuel Likuda alisema kwa mujibu wa ripoti ya Tanzania Demographic and Health Survey and Malaria (TDHS) wa mwaka 2015-2016 inaonesha Mikoa inayoongoza kwa ukeketaji nchini.

Kampeni hiyo imepewa jina nisitiri nina haki ya kutimiza ndoto zangu, usinikekete, usinipe mimba utotoni ambapo balozi wa kampeni hizo ni Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Diana Exavery maarufu kwa jina la Malaika.

Likuda aliutaja Mkoa wa Manyara unaongoza kwa ukeketaji kwa asilimia 58 ukifuatiwa na Dodoma kwa asilimia 47, Arusha asilimia 41, Mara 32 na Singida asilimia 31.

Alisema ripoti hiyo imefafanua kuwa ukeketaji hufanywa kwa asilimia 86 na mangariba au wakeketaji wa jadi na asilimia 25 hukeketwa katika umri wa miaka 13 na zaidi.

“Ripoti hiyo pia imeeleza pia kuwa wasichana wanaozaliwa au kulelewa na mama aliyekeketwa hukeketwa pia na kuwa na asilimia 95 ya asilimia 86 ya wanawake waliokeketwa hawakubaliani na kitendo hicho na wanatamani kisiwepo kabisa,” alisema Likuda.

Alisema kutokana na hali hiyo ndio maana kituo cha CFM cha jijini hapa kimeamua kuja na kampeni hiyo lengo likiwa ni kusaidia wasichana wasikeketwe hususani katika Mikoa ya Kanda ya Kati.

“Tumezindua kampeni yetu leo (jana) na tutaendelea kufanya hivyo kwa juhudi kubwa bila kuchoka lengo letu ni kuhakikisha tunafikia malengo ya kuhakikisha mwanamke hakeketwi,” alisema.

Kwa upande wake, Balozi wa kampeni hizo, Malaika alisema madhara ya ukeketaji ni makubwa kiafya kwa mtoto wa kike ikiwemo kupata athari za kisaikolojia kama msongo wa mawazo kwani wengi hufanya hivyo bila ridhaa yao.

“Madhara ya afya ya uzazi ambayo hupelekea kuongezeka kwa vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua pia maumivu makali wakati wa kukeketwa,kumwaga damu nyingi, kovu la kudumu sehemu za siri pamoja na kutokufurahia tendo la ndoa,” alisema.
 
Aisee haya mambo kumbe bado yapo? Mila na desturi za ajabu sana hizi.



Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Serikali na the so called NGOs, should reflect the real effects of FGM.

Waachane na visababu vya kusoma ili kujibu mitihani. Madhara ya ukeketaji yapo lakini siyo hizo zinazoelezwa kwa wanajamii. Eti ukamuambie inasabisha vifo, watakuambia tangu tumezaliwa mpaka sasa hakuna mwanamke aliyefariki kwa kukeketwa. Watakuitikia hapo ulipo, ukiondoka wanakucheka.

Eti inasababisha matatizo wakati wa kujifungua. Wanasahau kuwa asilimia nyingi wanajifungulia nyumbani bila hata ya msaada wa wakunga wa hospitalin.

Ukiwaambia inasabisha magonjwa kwa kushirikisha nyembe moja, watakuambia tupo kwenye digitali. Kila mtu na wembe wake.

Madhara ya Ukeketaji yapo kisaikolojia zaidi. Na hii huwakumba wenye elimu za kidato cha 6 kuendelea. Wanapokutana na jamii zingine na kuanza kuhadithiana juu ya mambo ya ngono.
 
Wanakeketa kuzuia uasherati,alafu ndio kwanza wanawake wa mikoa tajwa wanaongoza kwa kutokuwa waaminifu.
 
Yaani hadi karne hii watu bado wamekumbatia mila za enzi hizo?!!!!.Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa,maana sio kwa juhudi kubwa zilizofanyika kuondoa mila hizo.
 
Back
Top Bottom