Ripoti ya CAG: Mkataba wa Mlimani City na Chuo Kikuu cha UDSM ni wizi mtupu

Kazi nzuri kwa CAG, chuo kilichosifiwa ndio kwanza kinaongoza kwa mikataba ya uongo na kupigwa chenga, eti kuna school of law, kumbe blaa blaa, shame on u udsm.
 
Hii report kazi yake ni nini haswa?? Kila mwaka ni madudu ila sioni rekebisho!
 
Siku nilipo sikia eti kile chuo wanasoma "vipanga" niliwahurumia sana vifaranga.


Kwa hesabu za haraka ni kuwa kuanzia mwaka 2006 mpaka 2014 kodi ilitakiwa kuwa 309,458 usd kwa mujibu wa mkataba ina maana kila mwaka ni 309,458 unagawanya kwa 8 yaani miaka nane from 2006 mpka 2014 maana yake ni kuwa kwa mwaka chuo kinapata dola 38682.25 hiyo ni sawa na kuwa kwa mwezi mzima (ukigawanya kwa 12) wanakusanya kiasi cha dola za kimarekani 3223.52.Hiyo ni kwa majengo yote ya Mlimani city pamoja na parking systems.Kwa hili hata mtoto wa darasa la pili hawezi kukubali
 
kazi nzuri sana CAG!ni aibu kubwa kwa chuo kikuu kilichobobea wataalam wa sheria na utawala kuingia mkataba mbovu kama huo na kutofanya ufuatiliaji wa uhakika na wa umakini.
Jana kuna watu walisema UDSM ni chuo bora vingine ni takataka tu. Chuo bora si taaluma tu bali jinsi taaluma hizo zinavyotumika na Chuo chenyewe na jamii ya Watanzania kwa ujumla. CAG amewaumbua. The evidence of a disorganized entity!
 
Hichi si ndo chuo bora kwa mujibu wa mkuu?

Kwa kuwa ndio kasoma yeye Shahada zake zote tatu, hata ange soma Enkenford University bado ndio angesema Chuo bora!

Pamoja na yote bado Udsm ndio Chuo bora zaid hapa Nchini japo wawili watatu wanamaliza Phd hawajui hata cha kuombea Maji!
 
Wabongo wengi wasomi upo kwenye vyeti na makaratasi tuu matendo yao sifuri sifuri kabisa na ukifatilia hapo ni Rushwa ilipita sio uzembe wa kufatilia...
 
Chuo chenye wataalamu kinapigwa chenga vipi hao wataalamu wanaozalishwa?
 
Mkandara is seriously thieving University's money, defiling University's integrity and reputation. He is a stooge at the helm!

Mukandara kageuza chuo kuwa ni kama sekondari na yeye akiwa ni mwalimu wa nidhamu. useless Professor!
 
Heri mangungo alikuwa hajui kusoma na kuandika kuliko hawa wanaojitapa kila siku!
 
Acha kujitoa akili ccm ndio watawala mikataba yao yote ya kinyonyaji hakuna lolote ambalo mtz ananufaika,2015 kabla ya uchaguzi walipitisha mkataba wa kinyonyaji wa gesi wapinzani walisusa kupitisha wao akiwemo sizonje walipitisha huku wakikata viuno kma baikoko....sasa lissu anaingiaje kwenye huo mkataba wa mlimani city
 
Further proof kuwa elimu ya Tz ni majanga.
Pale school of law na udbs kuna wahadhiri/wataalamu "waliobobea" lakini bado chuo kimepigwa chenga ya mwili. We have a long way to go.
Yaani umemaliza kila kitu. Hawa wataalam wetu ni hodari wa kukariri na kumezesha. Hawana uthubutu wala creativity. Nchi hii ina changamoto. Hata pale tunapojaribu kumsihi Raisi ajenge taasisi za kumsaidia kiutendaji, atapata wapi watu kama wanapozaliwa watendaji kwenyewe chenga.
 
Mmmmm! Kama hiki ndicho chuo kinachozalisha wanasheria wa nchi hii, naanza kuona ni kwa nini serikali huwa inabwaga mahakamani mara kwa mara, kama sio mara zote, kwenye kesi zake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…