Ripoti ya CAG: CCM kuweni kama Dismas Mnyang'anyi waoneeni Huruma Yusuf na Mariam kwa sababu Wana mtoto mdogo Yesu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Unajua wizi wa serikalini ni mifumo iliyo katika mtindo wa Siasa zetu na asipotokea Mnyang'anyi mmoja mwenye Huruma ujue tumekwisha

Kisa cha Dismas na Dema waliosulubiwa Pamoja na Yesu kinaweza kuwa funzo zuri kwa CCM

Wakati Herode akitaka kumuua mtoto Yesu iliwabidi Yusuf na Mariam wasafiri kujificha Misti na wakiwa njiani walikutana na Vibaka Wawili Dismas na Dema ambao walitaka kuwapora

Dismas akamwambia Dema " Tuwaache waende tusiwapore kwa sababu Wana mtoto"

Dema alikataa lakin Dismas akamwambia " Hawa Tuwaache na tutakapomkaba mtu mwingine mgao wangu utachukua wewe kama fidia ya kuwaachia hawa"

Dismas na Dema ndio hawa Wanyang'anyi Wawili ambao miaka 33 baadae wakasulubiwa Pamoja na Yesu na Dismas ndiye aliyepata Neema ya ahadi ya Msalaba " Hakika Leo Hii Utakuwa Pamoja nami Peponi"

CCM na Vya Upinzani Wanaishi Kwenye mifumo ya Unyang'aji kama walivyoishi Dismas na Dema

Ripoti ya CAG imewasikitisha, Kuwahuzunisha na Kuwakatisha tamaa wengi tuwaombe Ndugu zetu CCM wawe na huruma hata ya kiwango cha Dismas kwa sababu " Watanzania Maskini Wana Watoto"

Sabato Njema!
 
Back
Top Bottom