Ripoti ya "ajabu" ya NAPE huko Houston...!



Kwa hiyo unatutangazia kuwa Raisi Kikwete ana uwezo mdogo wa siasa za kimataifa, mahusiano na diplomasia kwa kushindwa kutatua mgogoro huo wa Houson?. Ina maana Nape ni za di ya Kikwete? Hayo siyo matusi ya rejareja kwa mwenyekiti wenu?

Kwanza elewa kuwa mgogoro huo wa Houston siyo wa kimataifa na wala hahuhitaji diplomacy katika kutatua.
 
Wengi wao unaweza kukuta hawana uwezo wa kurudi Tanzania, si kwa kusosa hela....bali makaratasi yamebumba.
 
inasikitisha!
Kama watanzania hao waliridhika na majibu ya nape, huku wakijua waziwazi hali halisi ya mtanzania wa kawaida, basi nashawishika kuzua shaka juu ya uzalendo wao, na huenda walifika tanzania zamani mno!

du kijana anajitahidi mwache na yeye atanue kwani silva head akija sijui atajificha wapi
 

Chakula cha mabata (pumba)...
 
mbona juzi nape alionekana yupo class.na huko anawadanganya tu mana hawajui jinsi wa2 wanavyoteseka huku hasa vijijini kwa kulinda mafisadi
 
watu wanakosa cha kuandika
mtanzania kwa umaskini wako huku nchi ikiuzwa na kubakiwa mashimo unaandika pumba za kumsifia mtu kasuluhisha mgogoro wa kitoto
hilo lina faida gani kwa tanzania? kiuchumi? kisiasa au kijamii??
kwa akili za mfukoni utabakia kuwa maskini hata wa mawazo.
 
mi naomba akasuruishe Arusha uvccm aone km hawajamtoa nduki, au asuluhishe magamba mzalendo(sita,kyembe na wengine) na magamba ufisadi(mapacha3) hapo nitamuaminia kinoma
 

we mbona unajikoti mwenyewe!?!?!
 
Yeye nape anajua kusuluisha ya nje tu ya ndani yanamshinda basi abaki huko huko aeendelee kuwadanganya hao vilaza wake.
 
Ila mi nampongeza kwa kuonyesha ukomavu wa kidemokrasia kwa kuwapokea vijana wa chadema waliodamana na mabango na kuwakaribisha akisema wametumia hako yao ya kidemokrasia kuonyesha hisia zao na kufikisha ujumbe wao na akawahakikishia ujumbe umefika,lowassa ama jk ama yeyote huko ccm anaweza kuwa na uvumilivu wa kisiasa kama huyu kijana??tuliona hapa yale maandamano ya washington jk alivyoyahujumu kwa kutumia tax payer money!!huyu dogo mi namtabiria kuja kushika nafasi ya juu kabisa hapa nchini,wekeni maneno yangu kama akiba,mwenye kununa anune mwenye kucheka acheke,nape anatusumbua cdm vichwa vyetu!
 
Baada ya CCM kumtuhumu Nape kuisambaratisha zaidi CCM badala ya kuijenga wakaamua wamweke kiporo kwanza kwa kisingizio cha kwenda kuchukua nondoz za uongozi, maana akibaki ni sawa na toto tundu lisilosikia wala kuambilika, wakimshika shati asiende Arusha huyo anatafuta upenyo na kundi lake wanaibukia Mwanza. Mwanza walipomshtukia na kupiga mayowe, hapakuwa na jinsi ila haraka haraka kumpeleka kushikishwa adabu kwa Obama. Huko kalishika kundi dogo la vijana pungufu ya 15 na kujiita anasuluhisha migogoro. Nape mwenyewe ni chanzo cha migogoro atawezaje kuluhisha migogoro aliyoianzisha mwenyewe? Nape ni pandikizi babu kubwa la CCJ ndani ya CCM ndio maana wanazidi kugongana vichwa kila kukicha bila kumtambua mchawi wao. Kiwalacho CCM ki nguoni mwao.
 
Yaani I am so embarassed na nilichokisoma hapa, leo ndio nakubali kwamba huyu mtoto Nape ni empty. kwanza hii hadithi yake ya Houston siielewi maana haina kichwa wala miguu, tunajua amepewa trip kumpooza juu ya manung'uniko yake ya kutoswa katika sakata la kujivua gamba. Sisi wote tulisikitishwa na kudhalilishwa kwake na chama chake lakini sasa inaonyesha kwamba alistahili kutoswa. Maswali ya moja kwa moja kwa ndugu Nape, kwanza je ni kweli kuna mpango wa kukuvua gamba kwa kukunyang'anya cheo cha ukatibu mwenezi kwa kuwa umeonekana umeshidndwa kazi ndio maana leo hii Wassira anafanyakazi zako? Hivi ni wapi umeweka mipaka kati ya kazi za chama chako na zile za serikali yetu ambayo haikuhusu kabisa ki utendaji? Hii ndio tatizo la kutokua na msimamo, hivi hujioni kwamba umegeuzwa kideo na chama cha ko na wewe badala ya kutafuta kurudisha heshima yako na baba yako, unacheza makida makida? Nape chati yaki ilipanda sana baada ya mdahalo, sisi vijana tulianza kuone tumepata mwanaharakati mwanasiasa mwenye msimamo, japo ulipwaya kwa kuonekana dhahiri kushindwa kutetea ufisadi na ushenzi wa chama chako, lakini ulionekana walau unakubali kuwa chama chako kimeshindwa katika mambo mengi, sasa mbona umepoteza muelekeo kabisa na hivyo pia mvuto?
 
Eti mgogoro wa Watanzania Houston! Wabongo kwa kujipa umuhimu, as if anyone gives half a shyt kuhusu mgogoro Houston.
 
hivi nani anaweza kunionyesha ofisi za matawi ya democrats na republicans hapa tanzania?

hahahahahahahhaaaaaaaaa! Sisi waswazi ndio zetu! Eti anaenda kukagua matawi ya chama marekani! Matawi ya magamba houston na texas yatatusaidia nini sie, kama haya tu yaliyopo kwa mtogole na lumumba hayatusaidii kitu?
 
kwa mujibu wa magazeti ya elo tar 02 Nov 2011, CCM inaendesha mkutano usiokuwa wa Kikatiba wa wenyeviti a mikoa, lengo la mkutano huo ni kuizika rasmi hoja ya kujivua gamba. Ndio maan dogo akapelekwa marekani ili awe mbali ni kikao hiki. Huo ndio mwanzo wa kumuondoa hapa nchini kwa kumpatia ubalozi na ili kuizika rasmi agenda ya kujivua gamba.
 


Nimekerwa sana na kitendo cha huyu kijana Nape Nauye ambaye ni katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama tawala huko home CCM, nashindwa kuelewa nini hasa kilimleta hapa Marekani? huku akijua fika kuwa maisha ni magumu hapa yeye kwa kuwatumia baadhi ya vibaraka wao wakatupotosha tukadhani huyu dogo anakuja kuongelea maswala ya uchumi na hali ya maisha huko home, just imagine nimetoka Newyork mpaka Huston for nothing! nothing , hakuna la maana aliloongea Nape, yaani kanikera! eti kasema tufungue matawi ya CCM, what is it? .....hey kwani Republican wana matawi Bongo? huyu vipi lakini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…