Ripoti: Rwanda inaongoza kwa utawala bora Afrika Mashariki

Shobi

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
3,401
Reaction score
4,391
Rwanda inaongoza kwa utawala bora katika kanda ya Afrika Mashariki, kwa mujibu wa ripoti mpya kuhusu utawala barani Afrika iliyotolewa na wakfu wa Mo Ibrahim.

Kati ya mataifa 54 barani, Rwanda inashikilia nambari 11 ikiwa na alama 60.7.

Inafuatwa na Kenya iliyo nambari 14 na alama 58.8 kwa mujibu wa ripoti hiyo ya orodha ya Ibrahim Index of African Governance.

Tanzania na Uganda zinafuatana katika nambari 18 na nambari 19 mtawalia. Mataifa hayo mawili hata hivyo yameshuka kwa viwango vya utawala, Tanzania ikishuka alama moja hadi alama 56.7 nayo Uganda alama 1.3.

Rwanda na Kenya zinazoongoza katika kanda hii zimeimarika, Rwanda kwa alama 2.9 nayo Kenya kwa alama 4.3.

Orodha hiyo ilianzishwa mwaka 2007 na wakfu wa Mo Ibrahim kwa lengo la kugeza hatua zinazopigwa na mataifa ya Afrika katika kuimarisha utawala.

Ripoti hiyo iliangazia sana mambo manne: Usalama na Utawala wa Sheria, kushirikishwa kwa wananchi na haki za kibinadamu, fursa ya kuendeleza hali ya kiuchumi na maendeleo ya binadamu.

„Matokeo ya 2015 kwa jumla yanaonyesha ingawa kwa jumla Waafrika wana afya bora na wanaishi katika mataifa yenye demokrasia zaidi kushinda miaka 15 iliyopita, upigaji hatua katika nguzo nyingine za utawala bora barani umekwama," alisema mwenyekiti wa wakfu huo Bw Mo Ibrahim.

Burundi inashika mkia ikiwa nambari 38 na alama 45.8, ikiwa imepanda kwa alama 1.2.

Taifa linaloongoza barani Afrika ni Mauritius lililo na alama 79.9 na linaloshika mkia ni Somalia na alama 1.2.

Chanzo:
BBC
 
cc: jMali haya njoo huku nako tukupe definition! mikakati yetu taratiiiiiiiibu inaanza kulipa...
 
Hongera sana Warwanda, nimeshawakubali aisei na muendelee vivyo hivyo, boresha nchi kabisa na watachoka tu mahasidi wenu. Chura hata apige kelele aje, hazuii ng'ombe kufurahia maji. Mfahamu kwenye mpira, wakati mchezaji anakaribia kufunga bao, ndivyo makelele ya mashabiki wa wapinzani huzidi, akisita ili kuskliza wanaomkemea, basi anachemsha.
Iconoclastes njoo huku uwape hongera hawa ndugu zetu.

Pia hongera kwa nchi yangu ya Kenya maana hatuchezei mbali, tunafuatilia kwa karibu.
 
Corruption, insecurity and tribalism.....these are the factors that I believe, lower our Kenya's rankings in those indexes.

Rwanda is above the rest of us cos it has striven more to eradicate those challenges.

Congratulations, Rwanda!
 
Hongera sana Rwanda. Na mimi natoa ripoti yangu: Tanesco inaongoza kwa usambazaji bora wa umeme Afrika mashariki! :wink:

U are kidding, right? What then with the complaints about constant power cuts in Tz?
 
Corruption, insecurity and tribalism.....these are the factors that I believe, lower our Kenya's rankings in those indexes.

Rwanda is above the rest of us cos it has striven more to eradicate those challenges.

Congratulations, Rwanda!

You see my brother, the difference between you and some of these guys here "read" jMali, is that while you take this as a challenge to contribute in achieving more for your country, and improving on the ranking, the others take this as platform to downplay the achievement of Rwanda which by all account gained true independence in 1994. So you are looking at 25 years of hard work, raising from the ashes of genocide and catching up to and passing big countries with enormous resources like tanzania.
 
Last edited by a moderator:
U are kidding, right? What then with the complaints about constant power cuts in Tz?

Masuala ya umeme Bongo bora unyamaze tu, yaani walahi Watanzania ni watu wavumilivu zaidi ya kila mtu hii dunia. Mimi nikiwa Bongo huwa natumia inverter iliyounganishwa na battery. Umeme huwa kero, generator zinarindima mjini kama nini, watu wanaingia hasara noma noma. Na bado utakuta kwa mahangaiko hayo yote, wanashabikia CCM full.

Chama tawala kinafaa kibadilike jamani, maana wananchi wake wanakipenda kwa vyovyote vile, viongozi wake wanafaa kuwaonea huruma na kubadilisha jinsi wanavyo ongoza nchi.

Jamaa wamekua wakitoa vijisababu, mara sijui wanaunganisha gesi ya Kinyerezi, mara hiki mara kile. Jana nimeona Magufuli na Lowassa wote wameongelea kuhusu uzembe wa TANESCO na natumai hilo shirika litatia akili sasa na kudumisha umeme wa uhakika, bila hivyo watapigwa chini wengi.
 
Rwanda hakuna uchaguzi ukichukua fomu unapotea.hizi ripoti sijui wanatayarisha wakiwa wamekunywa viroba
nani kakwambia uchaguzi ndio kipimo cha utawala bora????je huo uchaguzi unafanywaje????
rwanda kuna utawala unaoheshimu sheria na matakwa ya raia
rwanda hata mabosi, vigogo wa serikali wanafuata foleni na sheria,,,,,hapa bongo ni nani mkubwa anayefuata utaratibu wa sheria????
 
Masuala ya umeme Bongo bora unyamaze tu, yaani walahi Watanzania ni watu wavumilivu zaidi ya kila mtu hii dunia. Mimi nikiwa Bongo huwa natumia inverter iliyounganishwa na battery. Umeme huwa kero, generator zinarindima mjini kama nini, watu wanaingia hasara noma noma. Na bado utakuta kwa mahangaiko hayo yote, wanashabikia CCM full.

Chama tawala kinafaa kibadilike jamani, maana wananchi wake wanakipenda kwa vyovyote vile, viongozi wake wanafaa kuwaonea huruma na kubadilisha jinsi wanavyo ongoza nchi.

Jamaa wamekua wakitoa vijisababu, mara sijui wanaunganisha gesi ya Kinyerezi, mara hiki mara kile. Jana nimeona Magufuli na Lowassa wote wameongelea kuhusu uzembe wa TANESCO na natumai hilo shirika litatia akili sasa na kudumisha umeme wa uhakika, bila hivyo watapigwa chini wengi.

achana na wabongo hawapendi ukweli, waambie tz ndio inaoongoza upewe likes.
just imagine our bdgt is around tsz 23 trilions, compared to kenya 41 trillions wakati tz ni kubwa with virgin lands suitable for agriculture vs 80% semi-jangwa, jangwa KENYA. imagine WAKENYA NDIO WANGEKUWA NA RESOURCES ZA TZ leo wangekimbizana na south Africa.

Kama sababu ni uchaguzi hata ZIMBWABWE kunafanyikaga uchaguzi na sote tunajua matokeo yake.
 
Utawala bora ndo kufanya "hot pursuit" kwa wapinzani wa kisiasa na kuwauwa huko walipo?

The World is not fair.Afrika hakuna kiongozi aliyeruhusu upinzani kufanya shughuli zake kwa uhuru kama JK akifuatiwa na UHURU.
 
Hooooooome Rwanda Kigali the beauty rwanda Oooh yeah Nyie Tz endeleeni kupiga kelele na Tanesco yenu sie huku mgao tunauskia kwenye clouds fm
 
Back
Top Bottom