Ripoti maalum: Kupotea kwa Ben Saanane

Hii ni ripoti maalumu?
Ni kimya kimetawala Kitongoji cha Hiti kilichojificha katikati ya mashamba ya migomba, kahawa na miti mikubwa. Ni katika miteremko ya Mlima Kilimanjaro wilayani Rombo ndiko kinakopatikana Kijiji cha Mrere. Sauti pekee unayosikika ni ya upepo unaovuma katika migomba, sauti za wanyama na watoto wanaocheza maeneo ya karibu.

Renatha Saanane, 54, mama mzazi wa Ben Saanane, anaendelea na shughuli zake za kila siku za nyumbani, lakini inambidi asimame na kumkaribisha mgeni ambaye ujio wake ametaarifiwa dakika chache zilizopita. Uso wake hauna tabasamu ya kawaida anayopaswa kuwa nayo kwa wageni. Uchungu alioubeba moyoni mwake kwa zaidi ya miezi tisa baada ya kutoweka kwa mtoto wake wa kwanza, Ben Saanane, unasomeka waziwazi usoni kwake.

“Sijui kama ameuawa, ametekwa au anashikiliwa na vyombo vya ulizi na usalama. Hili naiachia serikali,” anasema Bi Saanane. Baadaye machozi yanachuruzika kwa muda lakini anajikaza na anajipa nguvu na kuendelea kujadili fumbo la kupotea mwanaye. Mara ya mwisho kuongea na mwanaye ilikuwa ni Novemba 11 mwaka jana, siku tatu tu kabla Ben hajatoweka.

Waliongea masuala mbalimbali, ikiwamo maandalizi ya harusi ya ndugu yao aishiye Dodoma. “Hayo ndiyo mawasiliano yangu ya mwisho na yeye,” anasema, na kuongeza kuwa kwa kawaida hakuwahi kuingiwa hofu kuhusu ukimya wa muda mrefu wa mwanaye, ikizingatiwa kuwa nafasi yake kama msaidizi wa karibu wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ilimfanya awe na shughuli nyingi.

Kwa siku kadhaa zilizofuata baada ya kuongea na mwanaye kwa simu kwa mara ya mwisho, Bi Saanane aliendelea kumpigia Ben mara kwa mara lakini hakufanikiwa kumpata.

Alichukulia hali hiyo kama jambo la kawaida. Hata hivyo, anasema, kwa mshangao alijua baadaye kuwa hata mdogo wa Ben aitwaye Erasto na dada yake Agripina ambao pia wanaishi Dar es Salaam, pia hawakuweza kumpata kwa njia ya simu licha ya kumpigia mara kwa mara. “Hapo wote tukaanza kuwa na wasiwasi lakini wengine wakaamini anaweza kuwa amesafiri nje ya nchi au maeneo yasiyofikiwa na mtandao wa simu ukizingatia uanaharakati wake wa kisiasa,” alisema Renatha. “Bado hatukuweza kupata jibu, lakini wasiwasi wetu ulizidi baada ya suala la kutoonekana Ben liliripotiwia polisi Dar es Salaam na baadaye kuanza kuandikwa magazetini.” Mama Saanane hafichi juhudi zilizofanywa na familia yake kumtafuta mwanaye baada ya taarifa za vyombo vya habari kujirudiarudia kwamba anaweza kuwa ametekwa.

Mara ya mwisho mwanasiasa huyo kijana wa upinzani kufika kijijini kwao, kwa mujibu wa mama yake, ilikuwa kati ya Agosti au Septemba mwaka jana alipokwenda kumzika bibi yake.

Suala la kupotea kwa Ben halikuchukuliwa kwa urahisi katika kijiji chake cha Mrere kilicho Kata ya Mashati, takriban kilomita 60 kutoka Moshi na Wilaya ya Rombo kwa jumla.

Wananchi wa kawaida katika eneo hilo wana ufahamu wa kutosha kuhusu hali ya kisiasa nchini na mara nyingi viongozi wa kisiasa wamejikuta wakikamatwa na kushtakiwa wakituhumiwa kutotii mamlaka, uchochezi na mambo kama hayo.

Ben mwenyewe hakuwa mgeni na siasa za Rombo. Wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aligombea ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema na kushika nafasi ya pili baada ya kushindwa na mbunge wa sasa, Joseph Selasini (Chadema) katika kura za maoni. “Anajulikana na watu wengi kwa sababu alikuwa machachari wakati wa kampeni,” anasema mama yake, akiongeza kuwa kutoweka kwake kuliwagusa watu wengi pia.

Baba yake, Focus Saanane, 63, anasema anaumizwa na kutoweka kwa mtoto wake lakini anainyooshea Serikali kidole cha lawama kwa jinsi walivyoshughulikia suala hilo. “Tunaiachia Serikali kila kitu. Taarifa kutoka mamlaka hazijawahi kuwa za kuaminika,” anasema katika mahojiano mjini Moshi anakofanya biashara.

Anaonyesha kuwa familia yake inazidi kupoteza matumaini ukizingatia juhudi walizofanya bila ya mafanikio za kumtafuta kijana wao, ambaye licha shughuli zake ndani ya Chadema alikuwa pia akisomea shahada ya uzamivu ya uchumi.

Mzee Saanane anasema japokuwa Ben alilelewa na kukua kama mtu mwenye uhuru wa kwenda popote alipotaka, anazidi kukerwa na taarifa zinazokinzana kuhusu kutoweka kwake. “Hatujui kama yuko hai au la.

Mara ya mwisho kukutana naye ilikuwa wakati wa mazishi ya bibi yake,” anasema. ”Na ilikuwa mara ya mwisho kusikia kuhusu mwanangu. Familia inaumia sana lakini hatuna la kufanya.

Mama yake ana uchungu mkubwa kijijini. Sisi kama familia kubwa tumejaribu sana kumsaka lakini hakuna mafanikio Mzee Saanane anasema namba ya simu ya Ben ya Vodacoma imezuiwa na hawezi kujua mwanaye aliwasiliana na nani mara ya mwisho kabla ya kutoweka.

Suala la kupotea kwake liliripotiwa kituo cha polisi Tabata jijini Dar es Salaam.

Anaisihi Serikali isaidie katika kumtafuta mtoto wake na kuwaondolea wasiwasi wa wapi alipo na usalama wake, akisema hata maofisa wa Chadema hawajatoa msaada wa kutosha katika kumtafuta mwanaye kama wanavyoonekana pia kuchanganyikiwa.

Godbless Lema, mbunge wa Arusha Mjini ni kiongozi pekee wa juu wa Chadema aliyewahi kumtembelea Mzee Saanane nyumbani kwake Moshi kumtuliza na kujaribu kutafuta namna ya kulifumbua fumbo hilo, anasema mzee huyo.
 
Something, somewhere is critically wrong!siasa sawa,hatukatai lakini hayo maelezo ya mzee ambayo naamini ni kweli yanaacha changamoto nyingi kwa wasaka maisha...kua ukuavyo lakini wazazi waheshimiwe kwani hawana mbadala na ndiyo waathirika wakubwa wa freestyle tunazoamua kufuata.
 
Trace za Ben zipo za kutosha ni vile wenye Mamlaka hawataki..

Wakija independent investigator hata wiki haitaisha mahali Ben alipo au kama alishakufa itajulikana..

Ndio maana serikali hawataki wachunguzi huru..

Na ndicho CDM ambacho wamekuwa wakikipigania, waruhusiwe wachunguzi huru wa nje kama serikali haita aibika hapa..

Swali dogo.. Kwanini no ya simu ya Ben imekuwa BLOCKED na Vodacom?? Nani amewa instruct Vodacom kuiblock hii no na kutotoa mawasiliano ya mwisho ya Ben..?
Namba isipotumika kwa miezi 3 mtandao husika huzifungia hii ni kawaida,Tangu Ben amepotea umeshapita mwaka mzima
 
Ni kimya kimetawala Kitongoji cha Hiti kilichojificha katikati ya mashamba ya migomba, kahawa na miti mikubwa. Ni katika miteremko ya Mlima Kilimanjaro wilayani Rombo ndiko kinakopatikana Kijiji cha Mrere. Sauti pekee unayosikika ni ya upepo unaovuma katika migomba, sauti za wanyama na watoto wanaocheza maeneo ya karibu.

Renatha Saanane, 54, mama mzazi wa Ben Saanane, anaendelea na shughuli zake za kila siku za nyumbani, lakini inambidi asimame na kumkaribisha mgeni ambaye ujio wake ametaarifiwa dakika chache zilizopita. Uso wake hauna tabasamu ya kawaida anayopaswa kuwa nayo kwa wageni. Uchungu alioubeba moyoni mwake kwa zaidi ya miezi tisa baada ya kutoweka kwa mtoto wake wa kwanza, Ben Saanane, unasomeka waziwazi usoni kwake.

“Sijui kama ameuawa, ametekwa au anashikiliwa na vyombo vya ulizi na usalama. Hili naiachia serikali,” anasema Bi Saanane. Baadaye machozi yanachuruzika kwa muda lakini anajikaza na anajipa nguvu na kuendelea kujadili fumbo la kupotea mwanaye. Mara ya mwisho kuongea na mwanaye ilikuwa ni Novemba 11 mwaka jana, siku tatu tu kabla Ben hajatoweka.

Waliongea masuala mbalimbali, ikiwamo maandalizi ya harusi ya ndugu yao aishiye Dodoma. “Hayo ndiyo mawasiliano yangu ya mwisho na yeye,” anasema, na kuongeza kuwa kwa kawaida hakuwahi kuingiwa hofu kuhusu ukimya wa muda mrefu wa mwanaye, ikizingatiwa kuwa nafasi yake kama msaidizi wa karibu wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ilimfanya awe na shughuli nyingi.

Kwa siku kadhaa zilizofuata baada ya kuongea na mwanaye kwa simu kwa mara ya mwisho, Bi Saanane aliendelea kumpigia Ben mara kwa mara lakini hakufanikiwa kumpata.

Alichukulia hali hiyo kama jambo la kawaida. Hata hivyo, anasema, kwa mshangao alijua baadaye kuwa hata mdogo wa Ben aitwaye Erasto na dada yake Agripina ambao pia wanaishi Dar es Salaam, pia hawakuweza kumpata kwa njia ya simu licha ya kumpigia mara kwa mara. “Hapo wote tukaanza kuwa na wasiwasi lakini wengine wakaamini anaweza kuwa amesafiri nje ya nchi au maeneo yasiyofikiwa na mtandao wa simu ukizingatia uanaharakati wake wa kisiasa,” alisema Renatha. “Bado hatukuweza kupata jibu, lakini wasiwasi wetu ulizidi baada ya suala la kutoonekana Ben liliripotiwia polisi Dar es Salaam na baadaye kuanza kuandikwa magazetini.” Mama Saanane hafichi juhudi zilizofanywa na familia yake kumtafuta mwanaye baada ya taarifa za vyombo vya habari kujirudiarudia kwamba anaweza kuwa ametekwa.

Mara ya mwisho mwanasiasa huyo kijana wa upinzani kufika kijijini kwao, kwa mujibu wa mama yake, ilikuwa kati ya Agosti au Septemba mwaka jana alipokwenda kumzika bibi yake.

Suala la kupotea kwa Ben halikuchukuliwa kwa urahisi katika kijiji chake cha Mrere kilicho Kata ya Mashati, takriban kilomita 60 kutoka Moshi na Wilaya ya Rombo kwa jumla.

Wananchi wa kawaida katika eneo hilo wana ufahamu wa kutosha kuhusu hali ya kisiasa nchini na mara nyingi viongozi wa kisiasa wamejikuta wakikamatwa na kushtakiwa wakituhumiwa kutotii mamlaka, uchochezi na mambo kama hayo.

Ben mwenyewe hakuwa mgeni na siasa za Rombo. Wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aligombea ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema na kushika nafasi ya pili baada ya kushindwa na mbunge wa sasa, Joseph Selasini (Chadema) katika kura za maoni. “Anajulikana na watu wengi kwa sababu alikuwa machachari wakati wa kampeni,” anasema mama yake, akiongeza kuwa kutoweka kwake kuliwagusa watu wengi pia.

Baba yake, Focus Saanane, 63, anasema anaumizwa na kutoweka kwa mtoto wake lakini anainyooshea Serikali kidole cha lawama kwa jinsi walivyoshughulikia suala hilo. “Tunaiachia Serikali kila kitu. Taarifa kutoka mamlaka hazijawahi kuwa za kuaminika,” anasema katika mahojiano mjini Moshi anakofanya biashara.

Anaonyesha kuwa familia yake inazidi kupoteza matumaini ukizingatia juhudi walizofanya bila ya mafanikio za kumtafuta kijana wao, ambaye licha shughuli zake ndani ya Chadema alikuwa pia akisomea shahada ya uzamivu ya uchumi.

Mzee Saanane anasema japokuwa Ben alilelewa na kukua kama mtu mwenye uhuru wa kwenda popote alipotaka, anazidi kukerwa na taarifa zinazokinzana kuhusu kutoweka kwake. “Hatujui kama yuko hai au la.

Mara ya mwisho kukutana naye ilikuwa wakati wa mazishi ya bibi yake,” anasema. ”Na ilikuwa mara ya mwisho kusikia kuhusu mwanangu. Familia inaumia sana lakini hatuna la kufanya.

Mama yake ana uchungu mkubwa kijijini. Sisi kama familia kubwa tumejaribu sana kumsaka lakini hakuna mafanikio Mzee Saanane anasema namba ya simu ya Ben ya Vodacoma imezuiwa na hawezi kujua mwanaye aliwasiliana na nani mara ya mwisho kabla ya kutoweka.

Suala la kupotea kwake liliripotiwa kituo cha polisi Tabata jijini Dar es Salaam.

Anaisihi Serikali isaidie katika kumtafuta mtoto wake na kuwaondolea wasiwasi wa wapi alipo na usalama wake, akisema hata maofisa wa Chadema hawajatoa msaada wa kutosha katika kumtafuta mwanaye kama wanavyoonekana pia kuchanganyikiwa.

Godbless Lema, mbunge wa Arusha Mjini ni kiongozi pekee wa juu wa Chadema aliyewahi kumtembelea Mzee Saanane nyumbani kwake Moshi kumtuliza na kujaribu kutafuta namna ya kulifumbua fumbo hilo, anasema mzee huyo.
Taratibu za polisi zinasema wa kwanza kuulizwa ni yule wa mwishi kumuona akiwa hai yaani mama yake (kama ni mtoto mchanga) au bosi wake kama ni mtu mzima. Mbowe kaulizwa? Akajibuje?
 
I have a feeling that Ben is alive and safe
sijawahi kuamini kuwa Ben ni mwana chadema
I have a feeling yuko kozi na exit style yake pale chadema ilipangwa kuwa hivyo..baada ya kumaliza kazi
My heart never agreed kuwa huyu jamaa amefariki
cc GENTAMYCINE BAK mshana jr

Kwahiyo sisi uliotumensheni hapa ndiyo tunahusika ' directly ' na upoteaji wake au una maanisha nini labda Mkuu?
 
Atakapo potea mamako ndo utaelewa
Kwan hautakuja kuzaa subr malipo ni hapa hala Mungu yupo
Mtu amepotelewa na mtt wake w unakejeli eti

Mbona hata Wewe ' Basha ' wako kapotea lakini hulalamiki Mkuu? au umeshampata mwingine wa kutiririka na kuserereka na ' Unyabeni ' Kwako?
 
Ila tuwe wa kweli na kuweka itikadi zetu za kisiasa pembeni.....Hivi kwanini CHADEMA hawalipi suala la UPOTEVU wa ben UZITO UNAOSTAHILI???
Hili liwe fundisho kwa nyie vijana humu ndani mnaotumiwa na CHADEMA siku mkipotea thamani yenu pia upotea....Mjifunze kupambna na hali zenu na si kutegemea migongo ya watu kujinufaisha

Kama ishu iko polisi, CHADEMA wafanye nini kingine unadhani zaidi ya hilo?

Au unataka kutuambia CHADEMA nao siku hizi wana vyombo kama polisi, TISS nk vya kufanya uchunguzi?

Hukumalizia tu, lakini nia na lengo lako ni kutaka kutuambia kuwa CHADEMA ndiyo washukiwa wakuu wa kupotea kwa huyu ndugu....

Lakini if that is the case, kwa nini polisi, TISS na vyombo vingine vya serikali uchunguzi wao usifike mpaka huko CHADEMA na kisha watoe majibu kuituliza familia hii??

Si hivyo tu, bali kwa kumbukumbu zangu, CHADEMA wametaka mpaka kuundwe tume ya kimahakama ama kuita wachunguzi huru kutoka nje ya nchi yetu kama CIA, Scotland Yard na mengine ili kuchunguza mambo haya lakini serikali na CCM wamekataa katakata na wakati huohuo Polisi wao are doing nothing about this...!!

I don't get your point at all....
 
Back
Top Bottom