Ripoti Maalum: Buriani Nelson Mandela

Ripoti Maalum: Buriani Nelson Mandela

‘Never, never and never again shall it be that this beautiful land will again experience the oppression of one by another'.- Nelson Mandela.


 
‘It is what we make out of what we have, not what we are given, that separates one person from another.' - Nelson Mandela.


 
gari ya mandela.jpg
Gari likiutoa mwili wa Mzee Mandela nyumbani kwake kwenda hospitali.
 
Kumbukumbu nzuri sana kutoka kwa Mzee Mwanakijiji. Mzee Nelson Mandela Tata Madiba pumzika kwa amani umeacha nafasi pekee ambayo kwa wengi kuiziba ni ngumu sana. Pumzika Tata Madiba kumbukumbu ya uliyoyafanya na kuyapigania itadumu vizazi na vizazi na moyo wako wa kusamehe na ulioujenga wa kusameheana utadumu daima. Pumzika Tata Madiba kwa amani.
 
Asante kwa kwa makala yako kwa moja ya viongozi wa kipekee kabisa hapa ulimwenguni.
RIP Nelson M, Uliutumia vema wakati wako hapa ulimwenguni!
 
Hatimaye umekamilisha safari yako hapa duniani, umeondoka lakini daima utaishi katika nyoyo na fikra za watu hasa wenye mapenzi mema, maana katika kuishi kwako hapa duniani ulikuwa na hazina ya wema na upendo usio na kikomo kwa watu wako na dunia kwa ujumla.

Mungu mwenyezi alikuleta hapa duniani na kupitia kwako dunia imeshudia mengi yaliyo mapenzi ya Mungu hasa upendo usio na masharti katika kusamehe akupokee tena katika makazi yako ya milele. Amina.
 
Asante sana Mzee Mwanakijiji, umefanya kazi kubwa katika kutoa elimu kuhusu maisha ya Nelson Mandela (RIP!) Kama Watanzania tunajivunia mchango mkubwa ambao nchi yetu, pamoja na uchanga na umasikini wake, iliweza kutoa kwa nchi mbalimbali kusini mwa bara Afrika katika harakati za ukombozi. Hii picha hapa chini ni kielelezo kimojawapo tu kati ya michango mingi tuliyoitoa kama taifa.

B32-933-670x539.jpg


Wakufunzi wa chuo cha ANC Mazimbu Morogoro enzi hizo
 
Asante sana Mzee Mwanakijiji, umefanya kazi kubwa katika kutoa elimu kuhusu maisha ya Nelson Mandela (RIP!) Kama Watanzania tunajivunia mchango mkubwa ambao nchi yetu, pamoja na uchanga na umasikini wake, iliweza kutoa kwa nchi mbalimbali kusini mwa bara Afrika katika harakati za ukombozi. Hii picha hapa chini ni kielelezo kimojawapo tu kati ya michango mingi tuliyoitoa kama taifa.

B32-933-670x539.jpg


Wakufunzi wa chuo cha ANC Mazimbu Morogoro enzi hizo

Mag3; once upon a time we were a strong nation... Kissinger aliwahi kusema kuwa "Tanzania is a leader in Africa; where Tanzania goes, Africa goes"... sasa hivi tumekuwa tunafuata wengine...
 
Ahsante MM

Wengi wanajiuliza kipi kikubwa Mandela alichofanya kuliko viongozi wengine duniani ili hali alikuwa Magereza?

Si lazima kuwa shujaa kwa kusukuma mlima, waweza fanya jambo moja dogo ukawa shujaa.
Leo Major Landmarks zote duniani zimeomboleza, Magazeti yote duniani yameandika na Mataifa yote yanaomboleza.

Alichokifanya Mandela ni kuunganisha watu wake na leo anunganisha dunia. Ni kuacha chuki na ubinafsi na kutanguliza ubinadamu. Ni kuheshimu mwanadamu bila kujali rangi, kabila au dini. Ni kutaka usawa wa binadamu.
 
Back
Top Bottom