Bila kujali matokeo yatakuwaje mwisho, ila ujio wa Lisu umebadilisha hali ya mchezo kabisa. Mwanzoni wapiga kuwa wengi wa upinzani walikuwa wameamua kutokupiga kura, jambo lililowafurahisha ccm kuwa watajitangaza washindi goli likiwa wazi. Ila toka Lisu amerejea, wapiga kura wa upinzani wamepata moyo wa kwenda kupiga kura, hivyo ushindi wa mezani ambao ccm walitarajia kuupata umetoweka na kufanya mshindi apatikane kwa kura, ama kama ccm watashinda ni lazima hujuma iwe kete yao ya uhakika.