King JiluX
Member
- Jan 30, 2018
- 52
- 38
Naomba nianze na salamu wana jukwaa la siasa. Hapa jamvini jamii Forum.
Kutokana na kipindi tulichopo(kuelekea uchaguzi mkuu 2020) kumekuwa na majina mengi ya wagombea nafasi ya urais hasa kupitia upinzani ambako ndiko jicho la ushindani wa kupewa nafasi lipo huko (CCM alipita bila kupingwa), Hivyo kuna majina kadhaa yamekuwa yakipewa nafasi na wapo waliokwisha kuchukua fomu na kurudisha lakini pia wapo walioishia kutia nia na kisha nia zao zikayeyuka ghafla.
Naomba niwaongelee wawili hapo juu maana ndio wanaopewa na kupigiwa chapuo sana na wengi wa wanavyama wao hasa makada maarufu na viongozi wenza. MH. BERNARD KAMILIUS MEMBE na MH TUNDU ANTIPHAS LISSU
MHE. BERNARD MEMBE
Huyu anapigiwa debe sana na ACT-WAZALENDO. Huyu kwangu sioni kama ni sahihi kupeperusha bendera kwa kupitia upinzani (MUUNGANO) lakini simaanishi kwamba hana sifa kabisa kugombea urais hapana. Ila kwa kupitia upinzani, watakuwa wameamua kubutua.
Kwa sababu:
-Kwa alichokifanya MH E. Lowasa kurudi CCM kimewavunja sana moyo upinzani katika kuamini hawa hamahama hivyo akipitishwa kuna possibility kubwa ya kutokuungwa mkono na wengi ya wanachama wa upinzani ukizingatia huyu yeye hana mob la wanachama wa ccm aliohama na mioyo yao kama Lowasa.
-Kwa kipindi alichokuja, ni ngumu kuwaaminisha wananchi kwamba ana mapenzi na taifa na si tamaa zake binafsi za kutimiza lengo la kuwa mgombea wa urais ukizingatia kutoboa sio rahisi mwaka huu.
-Tatu, endapo akipitishwa na muungano wa vyama vya upinzani anaweza kuleta mpasuko mkubwa hasa ukizingatia kuna MH Lazaro NYalandu ambaye naye anaonekana yupo serious sana kutaka kupewa nafasi hiyo pengine kuliko mtia nia yeyote wa upinzani
MHE. TUNDU A LISSU
Huyu anapigiwa debe sana na CHADEMA wanachama makada na viongozi waandamizi. Kwangu mimi sioni kama ni chaguo lao sahihi kwa uchaguzi huu wa 2020 lakini angeweza kufaa kama ni maandalizi ya 2025.
Kwa sababu:
-Licha ya kwamba amefanya mengi sana kujitolea na kusaidia raia wanaoonewa ukisoma katika historia yake lakini ukiangalia wengi walimuona anafaa kuwania kiti ni kutokana na shambulio lake (HURUMA ambayo kwa sasa naona wengi wameanza kusahau tukio) hivyo hiyo huruma haiwezi kumbeba kwa sasa na ni ukweli kwamba mengi aliyoyafanya tangu enzi hizo wananchi wengi hawayajui kutokana na kutokuwa na desturi ya kusoma historia au pengine kutokana na kwamba aliyafanya katika kipindi ambacho mitandao ya kijamii haikuwa imechukua nafasi katika kumtangaza.
-Pili, Kwa upinzani kulingana na upepo wa sasa ulivyo kutoboa ni ngumu sana hasa katika kiti cha urais na Mh Tundu A Lissu sioni kama ni sahihi kwa yote aliyoyafanya kumtunuku nafasi ya kwenda kujaribu nafasi iliyo finyu sana kwa sasa ( nearly hawezi kushinda), Sitamani kuona Lissu akishindwa, sitamani…!!! Atafaa 2025 uchaguzi utakapokuwa serious.
NINAVYOONA
Ni vema sana kwa sasa wakimpa ridhaa ya kupeperusha bendera Mh L.Nyalandu au yule DR wa kike. Naona sifa za kuwabeba wao zipo n ahata kushindwa kwao sio pigo la kukatisha tamaa kwa mapambano ya demokrasia