Ripoti kutoka Kijiweni kwako kuhusu Upepo wa Kisiasa na Uchaguzi 2020

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
568
1,563
Wanajanvi Tupeane Ripoti ya Upepo wa Kisiasa unavyoendelea kijiweni pako kadri ya siku zinavyoenda.

Hapa kijiweni pangu napocheza Drafti kila jioni hali kidogo imebadilika baada ya Tundu Lissu kuteuliwa kugombea Uraisi wa JMT.

Sifa kidogo alizokua akipewa Mfarume wa Uajemi zimepungua sana. Na watu wameanza kumtafakari zaidi Mh Tundu Antipasi Lissu. Na Swali kubwa linaloendelea hapa kijiweni ni Kwa Nini Walitaka Kumuua Tundu Lissu kwa Malisase.

Kwa Upande wa Zanzibari hapa kijiweni Swali kubwa ni kuhusu Je? safari hii Watakubari Kumpa Mh Maalim Seif Uraisi wake maana inatathiminika na wataalamu tulio nao hapa kijiweni kua this time arround Maalim atatoa kichapo kisichoelezeka kwa Mwinyi Mtoto.

Nitaendelea kuwajuza mambo yatavyokua yakibadirika kadri ya muda.

Tupe Ripoti huko kwenu vipi?
 
117195765_3213508722074131_2911542144163865371_n.jpg
 
Kumbuka kura ni siri na kelele za chura hazimzui tembo kunywa maji.

Kichapo kipo pale pale haijalishi ni mlemavu au la..
Uongozi wa kuoneana huruma Tanzania hii haupo.
 
Bila kujali matokeo yatakuwaje mwisho, ila ujio wa Lisu umebadilisha hali ya mchezo kabisa. Mwanzoni wapiga kuwa wengi wa upinzani walikuwa wameamua kutokupiga kura, jambo lililowafurahisha ccm kuwa watajitangaza washindi goli likiwa wazi. Ila toka Lisu amerejea, wapiga kura wa upinzani wamepata moyo wa kwenda kupiga kura, hivyo ushindi wa mezani ambao ccm walitarajia kuupata umetoweka na kufanya mshindi apatikane kwa kura, ama kama ccm watashinda ni lazima hujuma iwe kete yao ya uhakika.
 
Kelele za organism utadhani dunia inapauska. Lisu akipata 5% ya kura nawajengea chadema ofisi
 
Kelele za organism utadhani dunia inapauska. Lisu akipata 5% ya kura nawajengea chadema ofisi
Kuna mmoja hapa yeye kasema eti atalinyea draft. Wajumbe wamemuuliza atalinyea hapahapa au ataenda nalo akalinyee nyumbani alafu atuletee kijiweni. Hajajibu.
 
Bila kujali matokeo yatakuwaje mwisho, ila ujio wa Lisu umebadilisha hali ya mchezo kabisa. Mwanzoni wapiga kuwa wengi wa upinzani walikuwa wameamua kutokupiga kura, jambo lililowafurahisha ccm kuwa watajitangaza washindi goli likiwa wazi. Ila toka Lisu amerejea, wapiga kura wa upinzani wamepata moyo wa kwenda kupiga kura, hivyo ushindi wa mezani ambao ccm walitarajia kuupata umetoweka na kufanya mshindi apatikane kwa kura, ama kama ccm watashinda ni lazima hujuma iwe kete yao ya uhakika.
Kumbe utakuwepo....ila siyo wa mezani?!Kwa jina ni...........
 
Back
Top Bottom