Ripoti hii ilifichwa: Chanzo cha kuporomoka Elimu Tanzania!

..."Kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka kila
mwaka kwa mfululizo wa miaka minne 2007 (90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na
2010 (50.4%)." ...
kwa observation hii ya tume mwanzoni tu mwa ripoti yao kunaoyesha hii ni trend..., Ehee Mola angalia Taifa hili..., watu hatuwajibiki licha ya kupewa mustakabali wa kuongoza na kutumikia wananchi
 
"Maamuzi ya kitaalamu yahusuyo elimu pamoja na uendeshaji wake hufanyika
kisiasa na hivyo kuleta athari katika utekelezaji wa mipango ya utoaji wa elimu
bora nchini;" uk.115
Hili ni moja ya mapendekezo yaliyotolewa na kamati hii. Leohii serikali inalazimisha matokeo yabadilishwe ili yawe wnavyotaka. Tunajua hili hufanywa kwenye kura lakini sasa serikali ya CCM inavuka mpaka. Tuache mambo ya kitaalamu yafuate taaluma. Hata kama watapasishwa je vichwa vyaovitaelimika kwa kiwango hicho? Tusitafute mchawi kwani matokeo ni kielelezo cha ukubwa wa tatizo katika utoaji wa elimu hapa nchini.
 
Baada ya kumwona Tundu Lissu akiigusia Ripoti hii, nimeonelea ni vema niwashirikishe ripoti yenyewe kwakuwa haikuwahi kuwa kwenye public domain.

Ni Ripoti ya utafiti iliyokuwa commissioned na ofisi ya Waziri Mkuu kuchunguza matokeo mabaya ya Kidato cha Nne mwaka 2010 ambayo ilitoka mwaka 2011.

Ajabu ni kwamba ripoti hii haikufanyiwa kazi na mwaka huu Ofisi hiyohiyo ya Waziri Mkuu imeunda kamati nyingine kuchunguza tatizo hilohilo! What a waste of resources and our time, all to deviate our attention from discussing pressing matters!

Sijui tunaelekea wapi?

Watanzania, bila kujali tofauti zetu kisiasa tusikubali mambo kama haya. Ni kuchezea raslimali zetu na hatari kwa vizazi vyetu na mustakbali wa Taifa letu.
mkuu nashukuru sana kwa taarifa hii,nimeisoma kwa makini hiyo taarifa ya tume,ingawa ni kipindi cha nyuma lakini hakika ina sababu za msingi sana na kama ingefanyiwa kazi sidhani kama yaliyowakuta wadogo zetu wa K4 mwaka wa jana kupata zero kiasi hicho,wengi tuliishia kulaamu mitandao ya kijamii hasa facebook kuwa ndio chanzo kikuu kumbe kuna mambo ya kitaalamu zaidi
 
Pinda is not there to defend Public interests, he is there as a SHOKAMZOBA/shockabsorber for JK's government to defend JK's na wahujumu's interests. Pinda amewezesha mambo mengi sana yenye sura za wizi/kifisad kupita bila kuwa discussed coz anayakingia kifua. So ndugu zangun tusitegemee jipya kwa huyu babu labda hadi atoke 2015.

Suala la ufisadi wa Jeshi, Pinda alitueleza kuwa hata tumfanye nn, masuala ya jeshi hayawezi jadiliwa Bungeni. Kwa kauli hiyo alitufanya tusipate ukweli juu ya ufisadi ulofanyika jeshin via mgodi wao wa Meremeta. Yapo matukio mengi sana ya wizi huyu mzee kayakingia kifua suala linalonifanya niamini kuwa yupo pale kudefend JK's interests na sio wananchi.

Hapo umenena kweli kabisa
 
Hivi interest ya hiyo Necta ni nini? Kuona watoto wanafeli au ? Ukisoma hii riport utaona vitu vinafanyika kinyume kabisa na jinsi inavyotakiwa viwe. Unajiuliza wanatunga swali ambalo haliko kwenye sylubus , hao watoto wataoata?

Nimechukia hiyo secta, na hiyo waizara hadi basi.
 
hakika ni huzuni na majonzi kudanganywa huku ukweli ukifichwa maskini tanzania nchi angu nakulilia sana
 
Invisible; Shukran sana.

Jamani mimi sielewi rationale ya kuunda tume kuchunguza kitu ambacho tayari hata majibu yake unayo tena kama report. Kisha siku zote sielewi why should a failure in one subject compromise a grading?

Tuna desturi ya kutofatilia hizi reports za tume zetu wenyewe!!!! Hii ni aibu sana
 
Hivi interest ya hiyo Necta ni nini? Kuona watoto wanafeli au ? Ukisoma hii riport utaona vitu vinafanyika kinyume kabisa na jinsi inavyotakiwa viwe. Unajiuliza wanatunga swali ambalo haliko kwenye sylubus , hao watoto wataoata?

Nimechukia hiyo secta, na hiyo waizara hadi basi.

Kwa mimi Iam particularly touched na sincerity ya hii tume. Wajua kwenye vyuo vingi kuna desturi ya kuingiza maksi za CA (continuos assessment) kama sehemu ya score ya mwanafunzi kwenye final scores. Na kwa kweli ingekuwa ni ahueni hata kwa shule nyingi lakini hili nalo tatizo liko wapi? Ukisikia ubabaishaji ndio huu. This is so frustrating.
 
Hakika yote niliyokuwa nafikiria kuwa ni sababu za matokeo mabaya ya kidato cha nne 2012 yamo kwenye ripoti hii. Hatuhitaji tume nyingine kabla mapendekezo ya ripoti hii hayajafanyiwa kazi,
Kuhusu suala la kuichafua serikali; mimi naona ni matumizi mabaya ya lugha; ripoti hii ilichofanya ni kuiambia ukweli serikali. Mtu anayekwambia ukweli ndiye rafiki na anayekwambia uongo ili uzidi kuwa rafiki (kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa) ni adui.
Serikali ijifunze kuupokea ukweli hata kama unauma namna gani.
 
Hii nchi inatafunwa na viongozi wetu wa chama tawala kwa kubuni mbinu za kula hela kila kukicha inauma sana Watanzania tusikubali, ifike mahala tuseme sasa basi tumechoka
 
Hivi kuna siku matatizo ya umaskini yataisha nchi hii? Manake hii ni ufujaji wa kodi ya mtanzania, badala ya kumpunguzia makali ya maisha unazidi kumtwika mzigo wa umaskini kwa kukesha kurudiadia kupigia mistari kitu ambacho kinajulikana wazi.

Sijui hii serikali ya kwetu ipo kwa ajili ya nani toba yarabi....Looks like ipo kwa ajili ya existence yake yenyewe na si vinginevyo.
 
Haya wanajamii forum kila mtu achuje mawazo yake na comments zake. Ukweli ni kwamba kubatilisha matokeo ya form four ni interest za siasa. Matumizi ya viwango vipya vya ufaulu yalijadiliwa na kuafikiwa na wajumbe kadhaa serikali ikiwamo ikihusisha wazir wa elimu na naibu wake, wadau wa elimu, ndalichako nk. Mtasari uliandikwa na kwa pamoja kumruhusu ndalichako atumie viwango hvyo. Na hata hvyo viwango hvyo vipya pia vilitumika kupanga matoke ya form six mwaka 2012, jiulize kwa nini serikali hiyo haikuunda tume kuchunguza matokeo yale na badala yake iunde tu kwa matokeo haya ya form 4, hivyo ni viini macho tu kutaka kuwapumbaza watanzania kuwa serikali yetu inaufanisi. Maajabu sana na ni haibu kwa taifa letu na amin kuwa wajinga wanazid kuongezeka na kufikia asilimia 75. We acha 2 hii ndo bongo bhana!
 
hili ni fundisho kwetu. tujenge wigo wa kimfumo wa kuwawajibisha hawa wateule wetu kwa kupitia nguvu na ushiriki dhabiti wa umma. vinginevyo tutaendelea kuwa watu wa kulialia, kukerwa, kuchoshwa, kufadhaishwa na madudu haya. tuliangalie hili katika katiba mpya.
 
baada ya kumwona tundu lissu akiigusia ripoti hii, nimeonelea ni vema niwashirikishe ripoti yenyewe kwakuwa haikuwahi kuwa kwenye public domain.

Ni ripoti ya utafiti iliyokuwa commissioned na ofisi ya waziri mkuu kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2010 ambayo ilitoka mwaka 2011.

Ajabu ni kwamba ripoti hii haikufanyiwa kazi na mwaka huu ofisi hiyohiyo ya waziri mkuu imeunda kamati nyingine kuchunguza tatizo hilohilo! What a waste of resources and our time, all to deviate our attention from discussing pressing matters!

Sijui tunaelekea wapi?

Watanzania, bila kujali tofauti zetu kisiasa tusikubali mambo kama haya. Ni kuchezea raslimali zetu na hatari kwa vizazi vyetu na mustakbali wa taifa letu.
mkuu kali ya mwaka.

Kaka mbona hii kali
 
Back
Top Bottom