Ripoti hii ilifichwa: Chanzo cha kuporomoka Elimu Tanzania!

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Baada ya kumwona Tundu Lissu akiigusia Ripoti hii, nimeonelea ni vema niwashirikishe ripoti yenyewe kwakuwa haikuwahi kuwa kwenye public domain.

Ni Ripoti ya utafiti iliyokuwa commissioned na ofisi ya Waziri Mkuu kuchunguza matokeo mabaya ya Kidato cha Nne mwaka 2010 ambayo ilitoka mwaka 2011.

Ajabu ni kwamba ripoti hii haikufanyiwa kazi na mwaka huu Ofisi hiyohiyo ya Waziri Mkuu imeunda kamati nyingine kuchunguza tatizo hilohilo! What a waste of resources and our time, all to deviate our attention from discussing pressing matters!

Sijui tunaelekea wapi?

Watanzania, bila kujali tofauti zetu kisiasa tusikubali mambo kama haya. Ni kuchezea raslimali zetu na hatari kwa vizazi vyetu na mustakbali wa Taifa letu.
 
Attachments

  • Rasimu ya 2 ya Taarifa ya Utafititi-Ufaulu K4 2010[1].pdf
    1.9 MB · Views: 15,042
Invisible Tuna kushukuru ngoja niisome kwa umakini
Kinachosikitisha ni kuwa baada ya ripoti hii kuwasilishwa, ilizuiliwa kabisa isiende public ati inaichafua serikali. Matokeo yake mwaka huu wamelazimika kufanya kilekile kilichofanyika awali lakini wakihitaji kupata ripoti wanazotaka ziseme kile walichotarajia kuambiwa.

Fedha za walipa kodi zinatumika visivyo!
 
yaani huu upumbavu sijui mpaka lini. Matatizo ya elimu nchi hii kwanza ni ya kuundiwa tume? Yaani mambo ambayo tunaweza kuyaona hata kwa machotu na kuelewa kwa akili ya kawaida?

Na lini findings za tume zikafanyiwa kazi nchi hii?
 
Hivi tatizo la Pinda ana dharau yuko bize au ana hamu ya kuundiwa zengwe ajiuzuru?

Report ya Lowassa kuhusu majengo kaikalia na hii ya elimu kaikalia yuko bize kila leo na safari za KATAVI.

Piga chini tuu huyu mtu maana ameshiba madaraka
 
Kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka kila mwaka kwa mfululizo wa miaka minne 2007 (90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na 2010 (50.4%). Kutokana na hali hiyo, Serikali iliamua kufanya utafiti ili kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu na kuchukua hatua sahihi za kukabiliana na tatizo hilo.

Hapo tatizo ni Serikali dhaifu isiyojali watoto wetu hasa sisi walalahoi ndio tunaoathirika na watoto wetu. Kushuka kwa Elimu yetu Kikwete ndio anatakiwa kuwa muwajibikaji. Tangu 2005 mpaka sasa majanga juu ya majanga badala ya kuzalisha wasomi tunazalisha wajinga.

Kikwete he must go now,
hatuhitaji Kiongozi wa misiba au kusafiri
 
Sidhani kama anajua hata kwa nini yuko pale

Ivi tatizo la Pinda ana dharau yuko bize au ana hamu ya kuundiwa zengwe ajiuzuru.
Report ya Lowasa kuhusu majengo kaikalia na hii ya elimu kaikalia yuko bize kila leo na safari za KATAVI
Piga chini tuu huyu mtu maana ameshiba madaraka
 
Hakuna maneno yanayonikera kwenye siasa za Tanzania kama maneno "kuichafua serikali".
Hii si sawa hata kidogo kwenye serikali inayofuata miiko na uadilifu wa demokrasia.
Wengi wa viongozi serikalini huenda hawaelewi dhana nzima ya demokrasia au wanafanya makusudi.
Serikali yoyote iliyowekwa madarakani na watu, kwanza inapaswa ijitambue kuwa ipo hapo kuwatumikia wananchi.
Hivyo kukosolewa ni sehemu ya mchakato wa kidemokrasia na wala sio malumbano au uvunjifu wa amani.
Sasa wao serikalini wakishafanya madudu, basi watajifaragua kana kwamba walijiweka wenyewe kwenye madaraka.

Kinachosikitisha ni kuwa baada ya ripoti hii kuwasilishwa, ilizuiliwa kabisa isiende public ati inaichafua serikali. Matokeo yake mwaka huu wamelazimika kufanya kilekile kilichofanyika awali lakini wakihitaji kupata ripoti wanazotaka ziseme kile walichotarajia kuambiwa.

Fedha za walipa kodi zinatumika visivyo!
 
Baada ya kumwona Tundu Lissu akiigusia Ripoti hii, nimeonelea ni vema niwashirikishe ripoti yenyewe kwakuwa haikuwahi kuwa kwenye public domain.

Ni Ripoti ya utafiti iliyokuwa commissioned na ofisi ya Waziri Mkuu kuchunguza matokeo mabaya ya Kidato cha Nne mwaka 2010 ambayo ilitoka mwaka 2011.

Ajabu ni kwamba ripoti hii haikufanyiwa kazi na mwaka huu Ofisi hiyohiyo ya Waziri Mkuu imeunda kamati nyingine kuchunguza tatizo hilohilo! What a waste of resources and our time, all to deviate our attention from discussing pressing matters!

Sijui tunaelekea wapi?

Mkuu Invisible Watanzania ndivyo tulivyo. Report juu ya Report. Si unakumbuka hata report ya ghorofa la Chang'ombe?
 
Last edited by a moderator:
"Baadhi ya shule za sekondari za serikali zilizofanyiwa utafiti zina wastani wa uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi zaidi ya 100 (1:100).

Wastani wa uwiano huu haulingani na 1:40 unaotakiwa kitaifa hali inayodhihirisha upungufu wa walimu. Kwa upande wa shule zisizo za serikali wastani wa mwalimu kwa wanafunzi ni 1:11-1:38 hali inayoonesha kutokuwa na tatizo la walimu.

Hata hivyo wastani wa uwiano wa mwalimu kwa idadi ya wanafunzi kitaifa katika elimu ya sekondari unaonesha kuwa mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi 51 (BEST, 2010) hali ambayo inaonesha kuwepo kwa upungufu wa walimu hivyo kuathiri ufundishaji na ujifunzaji."

Source: Ukurasa wa 102, Mchanganuo wa Jedwali Na. 4.3
 
Ninapoyaona haya mpaka leo nashindwa kuelewa hivi hawa wanaoendelea kuisapoti hii serikali wana akili ya aina gani??, matatizo ya kushuka elimu yako wazi kabisa, na tume ilishaundwa watu wakala pesa, muda, na malighafi mbalimbali zikatumika, then kwa makusudi pinda akakataa ripoti hii isitolewe hadharani 2011 leo miaka 2 baadae anaunda tena tume ya kuchunguza tattizo lilelile kwa kutumia gharama zaidi... Na hii ripoti ya hiyo kamati haitasolve lolote wala kusomwa popote tena..

adui wa maendeleo ya watanzania ni watanzania wenyewe...
 
Back
Top Bottom