1999?
Sina hakika kama RIP yako ina mashiko. It's too late
Nilidhani Mwezi huu ni kumbukumbu ya SOKOINE; Sikujua pia ya JK Nyerere
Au ndio watu wameanza na vilembwe vyao vya kutokuwa Makini na kushusha hadhi ya Jamii Forum?
Mkuu nadhani alijua yote haya na alikuwa na busara ya kutokumaliza mali asili za wajukuu zetu mpaka tutakapopata akili kuyachimba na kutunufaisha.., sio kwamba hakujua bali alijua zaidi kwamba bila busara tunaweza tukawa shamba la bibi kama hivi sasaMwenyezi Mungu angekupa uhai zaidi basi ungegundua kwamba nchi yetu si maskini kabisa tuna utajiri mkubwa sana wa rasilimali ambazo kama zingetumika vizuri nchi yetu ingekuwa mbali sana kimaendeleo.
Kwa busara na diplomatically asingeweza kusema hayo maneno mbele ya kadamnasi ile alisema the same thing in not so many words... "kwamba chagueni kiongozi bora.., na kama hayupo ndani ya CCM wananchi watamtafuta nje ya CCM"Na pia baada ya kusikia na kufahamu ufisadi mkubwa uliofanywa na Viongozi mbali mbali toka CCM basi ungebadili kauli yako na kusema Kiongozi bora wa Tanzania ni lazima atoke nje ya CCM maana hao wote waliotoka CCM wameendeleza ufisadi mkubwa na kuongeza kwa kiwango kikubwa gharama za maisha ya ya kila siku kwa Watanzania
Nyerere ndio chanzo cha matatizo yote haya tuliyinayo, mfumo alioutengeza, umekuwa mgumu sa na kuuondoa, sijui kwanini mnakuwa mnamrejea kila wakati wakati huu tunaotaka mabadiliko, embu fikiria, asingeiingilia uchaguzi 1995 tungekuwa wapi sasa, kama asingeanzisha mfumo wa chama kimoja leo tungekuwa wapi?
nnguu07
Nilidhani Mwezi huu ni kumbukumbu ya SOKOINE; Sikujua pia ya JK Nyerere
Au ndio watu wameanza na vilembwe vyao vya kutokuwa Makini na kushusha hadhi ya Jamii Forum?
Raia Fulani,Hii kauli ya kusema kiongozi bora lazima atoke ccm ilitoka baada au kabla ya kusema 'ccm si mama yangu?'
nnguu07
Sokoine alifariki April 14. Birthday ya Mwalimu ni April 13.
nnguu07
Sokoine alifariki April 14. Birthday ya Mwalimu ni April 13.
Hotuba safi sana (short and clear)
Tena kuna moja aliyosema "IKULU NI MAHALA PATAKATIFU, MIMI SIKUCHAGULIWA NA WANANCHI WA TZ KUJA KUBAGEUZA KUWA PANGO LA WALANGUZI"...Ndiyo maana bado Watanzania wengi tunazienzi hotuba za Mwalimu kwa sababu zina hekima na busara ya hali ya juu na pamoja na kuwa alizitoa miaka mingi iliyopita lakini nyingi bado ziko valid hata leo hii....Sijui kama wapo Watanzania wanaozienzi hotuba za Mwinyi, Mkapa au Kikwete.