Ridhiwani Kikwete ang'aka tena




Tatizo lako hufuatilii vyombo vya habari! Tarehe 03/05/2011 Dr Slaa na Mch Mtikila walimjibu Fisadi Ridhiwani Kikwete kwamba hakuna haja ya kusubiri mambo ya siku saba, kwa hiyo aende tu mahakamani!

Slaa, Mtikila wamtega mtoto JK

Tuesday, 03 May 2011 21:50
Leon Bahati na Raymond Kaminyoge

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amemtega mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani, akisema akifanikiwa kukifikisha chama hicho mahakamani atakuwa amefanikiwa kula mfupa ambao uliwashinda vigogo waliowatangazwa hadharani kuwa ni mafisadi nchini.

Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana alipotakiwa kutoa msimamo wake kuhusu kauli ya Ridhiwani aliyoitaoa Dar es Salaam juzi, kuwa atamfikisha mahakamani ili kuthibitisha kauli yake kwamba mtoto huyo wa rais ni bilionea aliyepata utajiri wa kutisha kipindi kifupi.

Ridhiwani alimpa siku saba Dk Slaa, kuanzia jana awe amekanusha kauli hiyo ya kumtuhumu kuwa fisadi, vinginevyo atamfikisha mahakamani.
"Sisi tunasema atangulie huko mahakamani sisi tutakuja nyuma," alisema Dk Slaa.

Dk Slaa ambaye katika uchaguzi uliopita aligombea urais na kutoa upinzani mkubwa kwa Rais Kikwete aliyetangazwa kuwa mshindi, alisema kauli za kushtakiwa wanapotangaza taarifa za ufisadi hadharani zimekuwa za kawaida.

Alisema wengi waliwahi kutoa kauli kama hiyo kupitia vyombo vya habari baada ya kuwatuhumu hadharani kuwa ni mafisadi, lakini wakashindwa kwenda mahakamani.

"Chadema tuna uzoefu tulipotaja orodha ya mafisadi walitutishia kuwa watatushtaki mahakamani tukawaambia watangulie sisi tutakuja nyuma, lakini walishindwa kutekeleza ahadi yao," alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa, iwapo Ridhiwani atafanya hivyo atakuwa amevunja rekodi ambayo imewashinda watu wazito.

Katibu huyo ambaye umaarufu wake ulikuja kwa kasi kipindi cha miaka 15 aliyokuwa Mbunge wa Karatu, Arusha, alijigamba kuwa hawazungumzi jambo bila vielelezo ndio maana wanajiamini kwa kila wanachokisema hadharani.

Dk Slaa alitupia lawama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwamba amekuwa akisisitiza ifutwe kwa sababu inashindwa kufanya kazi yake, ikiwamo kufanya uchunguzi kwa watu wanaotuhumiwa kupata utajiri katika mazingira yenye utata.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Ridhiwani alikanusha kuwa kijana bilionea kama Dk Slaa anavyomtuhumu.Alisema anamiliki shamba mkoani Pwani, lenye ukubwa wa ekari 1.5, gari ndogo na akaunti kwenye benki ya CRDB, NBC na Stanbic, ambazo hakutaja kiasi cha fedha.

Dk Slaa alipinga vikali kauli hiyo na kwamba, alimaliza shule miaka michache iliyopita, lakini sasa ni bilionea na utajiri huo aliupata kwenye mazingira ya utata.

Wakati huohuo, Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila, alisema atatoa uthibitisho mahakamani kuhusu mali alizozitaja kuwa zinamilikiwa na Ridhiwani.“Siwezi kumuomba radhi mtu, nina uhakika wa kuwa kijana yule anamiliki mali ambazo hajazipata kwa njia halali, itakuwa vizuri ikiwa atanipeleka mahakamani, kwani huko ndiko nitakakoonyesha uthibitisho wangu,” alisema Mchungaji Mtikila.

Jumamosi iliyopita, Mtikila alikaririwa na vyombo vya habari akisema, Ridhiwani ni bilionea anayemiliki nyumba za ghorofa, malori, kampuni za ujenzi wa barabara na ardhi.


Source: Mwananchi.
 


Namkumbuka sana Uday na Qusay watoto wa Sadam Hussein
 

Join Date : 29th January 2008
Posts : 413
Thanks:
0
Thanked 70 Times in 45 Posts
Rep Power : 24


Umri wako humu kwenye JF haulingani na kile unachoongea. Mbona mnapoteza issue hapa? Aliyeropoka ni nani? na kwanini uje na madai hayo...nadhani mwenye uwezo wakupinga haya ni Riz aliyekanusha habari zilizotolewa na Dr. Slaa. Ulinganisho wako na kina Churchill unalenga nini? bado sijaelewa unalinganisha uwezo wa JK na hao viongozi au ni namna gani...hebu weka clear. Kama unamlinganisha Slaa na hao sioni relevancy hapa.
My Take: Nachokiona hapa either wanaojifanya kutetea huu ujinga ni watu wa karibu na huyu accused or else ni wapambe wanaofaidi kwa njia moja ama nyingine, coz haiingii akilini issue ambayo ipo wazi kwa kila mtu lakini bado kuna watu wado wanajifanya vipofu...hii imekaaje!
 
Si amejiingiza kwenye siasa badala ya kukaa mahakamani akipambana na sheria? Siku saba zimekwisha sasa atawapeleka mahakamani? au alikuwa anatishia nyau?
 
Mchizi anajiamini kimtindo.. Ngoja tuone atalianzisha au atakula tu ganzi..
 

Polisi wapi hao unaowazungumzia? Hao ambao ni walinzi wa majambazi waliobomoa bank ya umma na kuiba pesa za EPA, Meremeta, IPTL Richmond etc ama kuna wengine?
 

hoja ya msingi ni kwamba RIZI 1 atekeleze ahadi yake kama alivyotoa kwa vitisho kwa vyombo vya habari.Sasa wewe mkuu MBOPO kwa nini unamtetea huyu dogo kuwa yeye siyo bilionea wakati chombo pekee ambacho kingeweza kuamua ni mahakama?labda utuambie kuwa wewe ndio RIZI 1 au ndugu yake au wakili wake.
Mimi ninaona tuendelee kuamini kuwa hoja za wazee wetu ni za msingi na wala sio za kupuuza hadi hapo mahakama itakapo amua kama itafikishwa huko.Halikadhalika RIZI 1 naye aone kuwa shutuma hizi si za kupuuza kwani zinaweza kumgharimu.
 
Kumbe kuambiwa wa chama flani wakati c kweli inakuwa tusi? Na unatetea yule ambae ametumia lugha isiyokuwa ya kistaarabu kwenye jukwaa kama hili basi wewe c kiongozi mzuri. Sidhani kama ni sahihi kutetea matusi kwasababu tu mtukanaji ana mawazo kama ya kwako.
Si lazima Riz 1 aende mahakamani, kwani alichofanya Dr slaa ni siasa na si facts,
Mnaotaka kumona huyo kijana mahakani basi mngembana Slaa kwanini kama ana ushahidi asingeenda mahakamani?
 


wala asishauriwe akae kimya mwache aropoke afundishwe adabu anafikiri cheo baba yake ambaye hata hatuelewi kwa nini ni raisi ni chake, hajafunzwa huyu,
 

Mimi ningekuwa Ridhwani ningechukua huu ushauri
 

atakuwa mwanafamilia au ndg wa karibu au maswahiba wa riz1
 
Baba anakoroga. Mtoto ndo kabisaaa. Alafu wewe mtz unaendekeza upuuzi huu. AMKA tujenge TZ mpya bana.
 

ulishaona kichaa akashaurika, waliokaribu nae wazidi kumuongezea mafuta?
 
angekuwa kule tarime hakuna cha kumpeleka court tunamalizanna tu wala hakuna haja ya hakimu au jaji
 
kalikoroga dogo alinywe sasa,baba yake alikuwa mentioned kwenye list of shame akaufyata sasa yeye anajifanya kidume,imekula kwake dogo,namsikitikia sana.
 
Nenda mahakamani mtoto wa mkuu wa kaya ili tuweze kujua ukweli ni upi. Lasivyo watakufiria vibaya watanzania wenzako, au ndio yale yale ya kwani watanifanya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…