Ridhiwani Kikwete ang'aka tena

Ridhiwani Kikwete ang'aka tena

The most stupid way of interpreting things. What do you know about prima facie evidence? Huyu dogo alitoa siku saba kwa waropokaji hawa kuja na ushahidi, ku-retract porojo zao au wafikishwe mahakama. If you are saying the seven days expired yesterday, did you expect him to knock the court doors today? He needs time to prepare court documents that institute proceedings that will sure take a few days. This is not like sighting of the moon, it is a process that starts the moment the accuser fails to take heed to the demand notice.

Lakini ambacho ni cha kushangaza ni taarifa kwamba huyo anayeitwa Dr. na mnayemtukuza sana ame-despatch watu kwenda mikoani kutafuta ushahidi baada ya kupokea demand notice na hii inamaanisha kwamba alitumwa kuropoka na mafisadi wanaomtumia wakati hakuwa na ushahidi wowote ule na kwa sababu amezoea watu kutishia bila kuchukua hatua, sasa ameona kabisa hatari iliyo mbele yake. case ya Mtikila hatuwezi kuisemea kwa sababu case yake ya insanity ni well documented na sasa anachofanya ni kutafuta ajira ya kusogeza siku baada ya kugeuka kuwa irrelevant kwenye political equation ya nchi hii.

jk.jpg


Tatizo lako hufuatilii vyombo vya habari! Tarehe 03/05/2011 Dr Slaa na Mch Mtikila walimjibu Fisadi Ridhiwani Kikwete kwamba hakuna haja ya kusubiri mambo ya siku saba, kwa hiyo aende tu mahakamani!

Slaa, Mtikila wamtega mtoto JK

Tuesday, 03 May 2011 21:50
Leon Bahati na Raymond Kaminyoge

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amemtega mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani, akisema akifanikiwa kukifikisha chama hicho mahakamani atakuwa amefanikiwa kula mfupa ambao uliwashinda vigogo waliowatangazwa hadharani kuwa ni mafisadi nchini.

Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana alipotakiwa kutoa msimamo wake kuhusu kauli ya Ridhiwani aliyoitaoa Dar es Salaam juzi, kuwa atamfikisha mahakamani ili kuthibitisha kauli yake kwamba mtoto huyo wa rais ni bilionea aliyepata utajiri wa kutisha kipindi kifupi.

Ridhiwani alimpa siku saba Dk Slaa, kuanzia jana awe amekanusha kauli hiyo ya kumtuhumu kuwa fisadi, vinginevyo atamfikisha mahakamani.
"Sisi tunasema atangulie huko mahakamani sisi tutakuja nyuma," alisema Dk Slaa.

Dk Slaa ambaye katika uchaguzi uliopita aligombea urais na kutoa upinzani mkubwa kwa Rais Kikwete aliyetangazwa kuwa mshindi, alisema kauli za kushtakiwa wanapotangaza taarifa za ufisadi hadharani zimekuwa za kawaida.

Alisema wengi waliwahi kutoa kauli kama hiyo kupitia vyombo vya habari baada ya kuwatuhumu hadharani kuwa ni mafisadi, lakini wakashindwa kwenda mahakamani.

"Chadema tuna uzoefu tulipotaja orodha ya mafisadi walitutishia kuwa watatushtaki mahakamani tukawaambia watangulie sisi tutakuja nyuma, lakini walishindwa kutekeleza ahadi yao," alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa, iwapo Ridhiwani atafanya hivyo atakuwa amevunja rekodi ambayo imewashinda watu wazito.

Katibu huyo ambaye umaarufu wake ulikuja kwa kasi kipindi cha miaka 15 aliyokuwa Mbunge wa Karatu, Arusha, alijigamba kuwa hawazungumzi jambo bila vielelezo ndio maana wanajiamini kwa kila wanachokisema hadharani.

Dk Slaa alitupia lawama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwamba amekuwa akisisitiza ifutwe kwa sababu inashindwa kufanya kazi yake, ikiwamo kufanya uchunguzi kwa watu wanaotuhumiwa kupata utajiri katika mazingira yenye utata.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Ridhiwani alikanusha kuwa kijana bilionea kama Dk Slaa anavyomtuhumu.Alisema anamiliki shamba mkoani Pwani, lenye ukubwa wa ekari 1.5, gari ndogo na akaunti kwenye benki ya CRDB, NBC na Stanbic, ambazo hakutaja kiasi cha fedha.

Dk Slaa alipinga vikali kauli hiyo na kwamba, alimaliza shule miaka michache iliyopita, lakini sasa ni bilionea na utajiri huo aliupata kwenye mazingira ya utata.

Wakati huohuo, Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila, alisema atatoa uthibitisho mahakamani kuhusu mali alizozitaja kuwa zinamilikiwa na Ridhiwani.“Siwezi kumuomba radhi mtu, nina uhakika wa kuwa kijana yule anamiliki mali ambazo hajazipata kwa njia halali, itakuwa vizuri ikiwa atanipeleka mahakamani, kwani huko ndiko nitakakoonyesha uthibitisho wangu,” alisema Mchungaji Mtikila.

Jumamosi iliyopita, Mtikila alikaririwa na vyombo vya habari akisema, Ridhiwani ni bilionea anayemiliki nyumba za ghorofa, malori, kampuni za ujenzi wa barabara na ardhi.


Source: Mwananchi.
 
That is a side issue and irrelevant at the best. Come up with a position on the veracity of the allegations made by this demigod of yours. kwani Phd si hata Che Mponda anayo lakini mwisho wa yote anaishia kutoa gabbage kila anaponyanyua mdomo. Hiyo siyo hoja maana hata Obama hana Phd lakini anakata issues. Churchill hata chuoni hakufika lakini ameingia kwenye historia kama the best PM Britain has ever produced. Hivi kuwa na Phd ndo uwe mzushi na mropokaji?

Join Date : 29th January 2008
Posts : 413
Thanks:
0
Thanked 70 Times in 45 Posts
Rep Power : 24


Umri wako humu kwenye JF haulingani na kile unachoongea. Mbona mnapoteza issue hapa? Aliyeropoka ni nani? na kwanini uje na madai hayo...nadhani mwenye uwezo wakupinga haya ni Riz aliyekanusha habari zilizotolewa na Dr. Slaa. Ulinganisho wako na kina Churchill unalenga nini? bado sijaelewa unalinganisha uwezo wa JK na hao viongozi au ni namna gani...hebu weka clear. Kama unamlinganisha Slaa na hao sioni relevancy hapa.
My Take: Nachokiona hapa either wanaojifanya kutetea huu ujinga ni watu wa karibu na huyu accused or else ni wapambe wanaofaidi kwa njia moja ama nyingine, coz haiingii akilini issue ambayo ipo wazi kwa kila mtu lakini bado kuna watu wado wanajifanya vipofu...hii imekaaje!
 
Si amejiingiza kwenye siasa badala ya kukaa mahakamani akipambana na sheria? Siku saba zimekwisha sasa atawapeleka mahakamani? au alikuwa anatishia nyau?
 
Mchizi anajiamini kimtindo.. Ngoja tuone atalianzisha au atakula tu ganzi..
 
Hakuna kilaza kushinda wewe. Unadhani kuropoka tu kunatosha. Polisi siyo wajinga wa kupiga mbizi bila kujua anachokwenda kukiopoa. Toa basi angalau kitu credible cha kufanyia uchunguzi, siyo hopeless matamko ya ku-justify ruzuku ndiyo yawe basis ya needless investigation.

Polisi wapi hao unaowazungumzia? Hao ambao ni walinzi wa majambazi waliobomoa bank ya umma na kuiba pesa za EPA, Meremeta, IPTL Richmond etc ama kuna wengine?
 
Hakika suala la upumbavu wako lilikuwa hisia mpaka wewe mwenyewe uliapojitolea kulithibitisha kupitia hii thread yako ya kijinga ambayo kwa mara ya kwanza inakiuka misingi ya sheria iliyowekwa na waasisi wa sheria ambao waliidadavua kwa umahiri. Msingi muhimu wa sheria ni ule unaosema "He who alleges must proove". Hawa makanjanja wawili wametoa broadsides ambazo mpaka leo hazina chembe ya uthibitisho. Badala ya kuwataka waonyeshe ukomavu na kuaminika kwao kwa kuja na ushahidi unaothibitisha tuhuma zao basi wewe unaandaa mob justice ambayo nina hakika haitapata uungwaji mkono na yeyote mwenye akili timamu, labda watu wa aina yako.

Unadhani watu watababaishwa na kauli zako ambazo kimsingi zinafanana na hao watoa tuhuma ambao shida yao ni political expedience badala ya kuangalia madhara ya uropokaji wao kwa reputation zao, vyama vyao na kikubwa zaidi, wahanga wa tuhuma zao za kupandikizwa na kutumwa na vinara wa ufisadi wa nchi hii. Tengeneza polisi wako wenye ufinyu wa fikra kama wewe ndipo uwatume wafanya hizo un-ethical behaviours halafu uone kama zitapata uungwaji mkono. Mimi ningekushauri uwe na ujasiri wa kuwashauri hao miungu wako wawili kuja na vielelezo vitakavyotufanya tumtie adabu huyo dogo badala ya kugeuka kunguru ambaye kazi yake ni kunyea watu huku akiendelea kuruka bila kujua madhara ya uchafuzi huo. Kilicho wazi ni kwamba wazee hawa wawili wataburutwa mahakamani na hakika hakuna kipindi muafaka cha kuwavua nguo mbele ya jamii kama hiki. Wakati wewe unashabikia, kwa taarifa yao huyo Dokta wako kachanganyikiwa na sasa ame-deploy watu mikoani kuunga unga kile anachodhani ni ushahidi ambayo maskini haitamsaidia kwani ni afterthought ambayo haina hata chembe ya ukweli.

Brother ni vizuri ukahakikisha kwamba kiungo kilicho katikati ya masikio yako unakishughulisha kabla hujaingia humu jamvini.

hoja ya msingi ni kwamba RIZI 1 atekeleze ahadi yake kama alivyotoa kwa vitisho kwa vyombo vya habari.Sasa wewe mkuu MBOPO kwa nini unamtetea huyu dogo kuwa yeye siyo bilionea wakati chombo pekee ambacho kingeweza kuamua ni mahakama?labda utuambie kuwa wewe ndio RIZI 1 au ndugu yake au wakili wake.
Mimi ninaona tuendelee kuamini kuwa hoja za wazee wetu ni za msingi na wala sio za kupuuza hadi hapo mahakama itakapo amua kama itafikishwa huko.Halikadhalika RIZI 1 naye aone kuwa shutuma hizi si za kupuuza kwani zinaweza kumgharimu.
 
Kumbe kuambiwa wa chama flani wakati c kweli inakuwa tusi? Na unatetea yule ambae ametumia lugha isiyokuwa ya kistaarabu kwenye jukwaa kama hili basi wewe c kiongozi mzuri. Sidhani kama ni sahihi kutetea matusi kwasababu tu mtukanaji ana mawazo kama ya kwako.
Si lazima Riz 1 aende mahakamani, kwani alichofanya Dr slaa ni siasa na si facts,
Mnaotaka kumona huyo kijana mahakani basi mngembana Slaa kwanini kama ana ushahidi asingeenda mahakamani?
 
swahiba... the only danger naiona hapa ni arrogance ya dogo while there are only 4 year left kwa baba kulinda familia, if it was me, i would be very careful with what i say to anyone

Tanzania iko kwenye mapito makali sana na kauli yoyote ile ni muhimu sana hasa ukiwa kwenye limelight

Nina story ya mtoto wa waziri wa siera leone ambaye ni rafiki yangu akisimulia yaliyomtokea, unaweza kupata kichaa... yeye amekimbilia UK

mlio karibu, mshaurini dogo akae kimya au hata asijibu chochote kwa waandishi, silence can be the best noise one can make


wala asishauriwe akae kimya mwache aropoke afundishwe adabu anafikiri cheo baba yake ambaye hata hatuelewi kwa nini ni raisi ni chake, hajafunzwa huyu,
 
Hivi inakuwaje mtoto baba yao ni rais na wewe unataka kuwa front line kwenye siasa. Kwa nini usifaidi mambo nyuma ya pazia tu . Watu wengine sijui hawana washauri.

Sijui kwa nini huyu Riz alikimbilia kwenye mambo ya siasa. Anamuharibia baba yake na yeye mwenyewe.
Timig yake ya kuingia kwenye siasa tena front line ni mbaya


JK leo kawaambia mawaziri kuna mambo ukikubali kuwa waziri inabidi ukubali kuyakosa. Je hajamawambia rizwani na familia yake haya kama mtoto au familia ya wa rais kuna vitu vingine wavipotezee tu na waendele kufaidi mambo nyuma ya pazia
bila kuwa front line

Mimi ningekuwa Ridhwani ningechukua huu ushauri
 
The most stupid way of interpreting things. What do you know about prima facie evidence? Huyu dogo alitoa siku saba kwa waropokaji hawa kuja na ushahidi, ku-retract porojo zao au wafikishwe mahakama. If you are saying the seven days expired yesterday, did you expect him to knock the court doors today? He needs time to prepare court documents that institute proceedings that will sure take a few days. This is not like sighting of the moon, it is a process that starts the moment the accuser fails to take heed to the demand notice.

Lakini ambacho ni cha kushangaza ni taarifa kwamba huyo anayeitwa Dr. na mnayemtukuza sana ame-despatch watu kwenda mikoani kutafuta ushahidi baada ya kupokea demand notice na hii inamaanisha kwamba alitumwa kuropoka na mafisadi wanaomtumia wakati hakuwa na ushahidi wowote ule na kwa sababu amezoea watu kutishia bila kuchukua hatua, sasa ameona kabisa hatari iliyo mbele yake. case ya Mtikila hatuwezi kuisemea kwa sababu case yake ya insanity ni well documented na sasa anachofanya ni kutafuta ajira ya kusogeza siku baada ya kugeuka kuwa irrelevant kwenye political equation ya nchi hii.


Nadhani huyu ni Ridhiwan Mwenyewe . Kama si yeye ni mdogo wake kama si mdogo wake ni baba yake . Hawezi kuwa mwingine aliyechangia huu upupu.

atakuwa mwanafamilia au ndg wa karibu au maswahiba wa riz1
 
Baba anakoroga. Mtoto ndo kabisaaa. Alafu wewe mtz unaendekeza upuuzi huu. AMKA tujenge TZ mpya bana.
 
swahiba... the only danger naiona hapa ni arrogance ya dogo while there are only 4 year left kwa baba kulinda familia, if it was me, i would be very careful with what i say to anyone

Tanzania iko kwenye mapito makali sana na kauli yoyote ile ni muhimu sana hasa ukiwa kwenye limelight

Nina story ya mtoto wa waziri wa siera leone ambaye ni rafiki yangu akisimulia yaliyomtokea, unaweza kupata kichaa... yeye amekimbilia UK

mlio karibu, mshaurini dogo akae kimya au hata asijibu chochote kwa waandishi, silence can be the best noise one can make

ulishaona kichaa akashaurika, waliokaribu nae wazidi kumuongezea mafuta?
 
angekuwa kule tarime hakuna cha kumpeleka court tunamalizanna tu wala hakuna haja ya hakimu au jaji
 
kalikoroga dogo alinywe sasa,baba yake alikuwa mentioned kwenye list of shame akaufyata sasa yeye anajifanya kidume,imekula kwake dogo,namsikitikia sana.
 
Nenda mahakamani mtoto wa mkuu wa kaya ili tuweze kujua ukweli ni upi. Lasivyo watakufiria vibaya watanzania wenzako, au ndio yale yale ya kwani watanifanya nini?
 
Back
Top Bottom