Ridhiwani Kikwete ang'aka tena

Ridhiwani Kikwete ang'aka tena

duh,hii kali kweli,....hizi saba saba ni ishara za shetani nini?
kila mtu natoa nini 7,7,7,7,7 duh

Mkuu nilikuwa sina umeme ndio wamerudishia sasa hivi, vipi ile thread yangu ya Magaidi wa Markaz mods wameshaitrash? maana siioni kwenye folder yangu, na nimeisearch lakini siioni hebu nijuze.
 
The most stupid way of interpreting things. What do you know about prima facie evidence? Huyu dogo alitoa siku saba kwa waropokaji hawa kuja na ushahidi, ku-retract porojo zao au wafikishwe mahakama. If you are saying the seven days expired yesterday, did you expect him to knock the court doors today? He needs time to prepare court documents that institute proceedings that will sure take a few days. This is not like sighting of the moon, it is a process that starts the moment the accuser fails to take heed to the demand notice.

Lakini ambacho ni cha kushangaza ni taarifa kwamba huyo anayeitwa Dr. na mnayemtukuza sana ame-despatch watu kwenda mikoani kutafuta ushahidi baada ya kupokea demand notice na hii inamaanisha kwamba alitumwa kuropoka na mafisadi wanaomtumia wakati hakuwa na ushahidi wowote ule na kwa sababu amezoea watu kutishia bila kuchukua hatua, sasa ameona kabisa hatari iliyo mbele yake. case ya Mtikila hatuwezi kuisemea kwa sababu case yake ya insanity ni well documented na sasa anachofanya ni kutafuta ajira ya kusogeza siku baada ya kugeuka kuwa irrelevant kwenye political equation ya nchi hii.

Nadhani huyu ni Ridhiwan Mwenyewe . Kama si yeye ni mdogo wake kama si mdogo wake ni baba yake . Hawezi kuwa mwingine aliyechangia huu upupu.

Usijali ni nani aliyechangia. Jibu hoja na kama ni upupu weka hoja ili tupambanue upupu na ukweli maana vinginevyo inawezekana wewe ndo unatoa uharo na ndiyo maana uko busy kujua ni nani aliyechangia. Sina uhusiano naye na wala sihusiki lakini hatuwezi kulea uzushi kwa kuogopa kuonekana kuwa na uhusiano na Riz 1 kwani kuna aibu gani hata kuhusishwa naye?
 
Mkuu nilikuwa sina umeme ndio wamerudishia sasa hivi, vipi ile thread yangu ya Magaidi wa Markaz mods wameshaitrash? maana siioni kwenye folder yangu, na nimeisearch lakini siioni hebu nijuze.

Kamanda nyeti kama zile inabidi unakuwa na back up kuna viranja hapa wasipoipenda wanaichana chana! Kama unayo weka tena
 
Semina Elekezi hiyo imeanza kufanyakazi.
Tujuze cheo chako basi na uko Wizara gani.
Huyu wala hana cheo wala wizara ndo walewale vibaraka wa akina R1. Au ndo R1 mwenyewe manake ana jazba ya kuua mtu.
 
Hakika suala la upumbavu wako lilikuwa hisia mpaka wewe mwenyewe uliapojitolea kulithibitisha kupitia hii thread yako ya kijinga ambayo kwa mara ya kwanza inakiuka misingi ya sheria iliyowekwa na waasisi wa sheria ambao waliidadavua kwa umahiri. Msingi muhimu wa sheria ni ule unaosema "He who alleges must proove". Hawa makanjanja wawili wametoa broadsides ambazo mpaka leo hazina chembe ya uthibitisho. Badala ya kuwataka waonyeshe ukomavu na kuaminika kwao kwa kuja na ushahidi unaothibitisha tuhuma zao basi wewe unaandaa mob justice ambayo nina hakika haitapata uungwaji mkono na yeyote mwenye akili timamu, labda watu wa aina yako.

Unadhani watu watababaishwa na kauli zako ambazo kimsingi zinafanana na hao watoa tuhuma ambao shida yao ni political expedience badala ya kuangalia madhara ya uropokaji wao kwa reputation zao, vyama vyao na kikubwa zaidi, wahanga wa tuhuma zao za kupandikizwa na kutumwa na vinara wa ufisadi wa nchi hii. Tengeneza polisi wako wenye ufinyu wa fikra kama wewe ndipo uwatume wafanya hizo un-ethical behaviours halafu uone kama zitapata uungwaji mkono. Mimi ningekushauri uwe na ujasiri wa kuwashauri hao miungu wako wawili kuja na vielelezo vitakavyotufanya tumtie adabu huyo dogo badala ya kugeuka kunguru ambaye kazi yake ni kunyea watu huku akiendelea kuruka bila kujua madhara ya uchafuzi huo. Kilicho wazi ni kwamba wazee hawa wawili wataburutwa mahakamani na hakika hakuna kipindi muafaka cha kuwavua nguo mbele ya jamii kama hiki. Wakati wewe unashabikia, kwa taarifa yao huyo Dokta wako kachanganyikiwa na sasa ame-deploy watu mikoani kuunga unga kile anachodhani ni ushahidi ambayo maskini haitamsaidia kwani ni afterthought ambayo haina hata chembe ya ukweli.

Brother ni vizuri ukahakikisha kwamba kiungo kilicho katikati ya masikio yako unakishughulisha kabla hujaingia humu jamvini.

Mkuu Mbopo,

Heshima mbele. Kwa nchi inayoendeshwa kisanii kama hii ya kwetu, ni vizuri tukaanza kuhamasishana na kujichukulia sheria mkononi. Kijana kama RIZ1 anaitumia nafasi ya baba yake vibaya kwa kujitajirisha na kufanya biashara haramu kwa kuwa vyombo vya dola vinaogopa kumgusa. Kama vyombo vya dola vinamuogopa, dawa yake ni nini? Kwa nini huyu kijana hakutaka kujifunza kutoka kwa watoto wa maraisi waliopita? Anajitakia matatizo mwenyewe na wala huna haja ya kumtetea kwa kumshambulia mleta hoja!!!!

Tiba
 
Natoa siku sita chuo kikuu cha dar es salaam kiwe kimemnyang'anya huyu mpuuzi hiyo shahada ya sheria.
Kama ameshindwa kujitetea atawezaje kutetea wengine?
 
Sihusiki katika maandalizi yake but I can predict with a degree of reliability kwamba siyo siku nyingi waropokaji hawa watalipa gharama kwa kuacha midomo yao iugue kuhara

If you are not R1 then you must among the group to know what is going on about preparations and become confident that R1 gona win the case thus you predicted the negative results to Slaa and Mtikila.

Lets wait now the dance has started!
 
yeye wacha apige kelele lakini siku saba limesha anza kumenyeka.
nchi inaendeshwa kama saccos,
wanajitajilisha kishwa wanakana mali zao
 
Wewe Kilaza hebu badili font ili usomeke! Huyu RizOne lazima achunguzwe kwa wizi kutumia mgongo wa babaye!

Hakuna kilaza kushinda wewe. Unadhani kuropoka tu kunatosha. Polisi siyo wajinga wa kupiga mbizi bila kujua anachokwenda kukiopoa. Toa basi angalau kitu credible cha kufanyia uchunguzi, siyo hopeless matamko ya ku-justify ruzuku ndiyo yawe basis ya needless investigation.
 
Huyu wala hana cheo wala wizara ndo walewale vibaraka wa akina R1. Au ndo R1 mwenyewe manake ana jazba ya kuua mtu.

Jamaa ana munkari na hasira ile mbaya kwenye kutetea...kesha lipiwa huyo wacha tumsubirie maana kuna thread nyingine humu anadai wanaandaa taratibu za kufungua hiyo kesi.

Wacha tusubiri tuone!
 
Kamanda nyeti kama zile inabidi unakuwa na back up kuna viranja hapa wasipoipenda wanaichana chana! Kama unayo weka tena
Wacha sasa nije kivingine na ushaidi wa picha za majengo ambazo zinaonesha kabisa contractor wa jengo lile la kule Aboterbad Pakistan, na haya majengo ambayo yapo hapa kwetu niliyoyataja ni contractor mmoja. kuna kainzi kangu kanaongea kiarabu kataenda kuniletea picha za yale majengo.
 
Mbopo, duh! Katekenywa Riz1 unanyegereshwa wewe?
Nahisi unapalilia kitu au ndo maisha yenu vijana ya 'kimjinimjini'?

Matumizi ya lugha zinazopambanua upuuzi na ukosefu wa maadili notwithstanding, ukweli unabaki kwamba maisha yangu hayajawahi kuendeshwa kwa favours zozote na wala huyo dogo sifahamiani naye lakini nikiona haki na ukweli unapotoshwa basi hata wewe ***** ambaye sikufahamu nitakutetea tu maana mimi ninachotetea hapo ni ule ukweli. Wewe utafaidika na utetezi wangu kama tu ukweli ule umelalia kwako. Labda wewe unaishi kwa favours za wanasiasa ndiyo maana unadhani Slaa akiongea basi maneno yake ni gospel truth kumbe ni uzushi tu!
 
Hakuna kilaza kushinda wewe. Unadhani kuropoka tu kunatosha. Polisi siyo wajinga wa kupiga mbizi bila kujua anachokwenda kukiopoa. Toa basi angalau kitu credible cha kufanyia uchunguzi, siyo hopeless matamko ya ku-justify ruzuku ndiyo yawe basis ya needless investigation.
Mbona huweleweki mkuu?
 
Jamaa ana munkari na hasira ile mbaya kwenye kutetea...kesha lipiwa huyo wacha tumsubirie maana kuna thread nyingine humu anadai wanaandaa taratibu za kufungua hiyo kesi.

Wacha tusubiri tuone!

Tusubiri baba lakini sitaogopa kusema kwa kuwa tu wewe mwenye mtindio utafikiria kwamba nimelipiwa chochote!
 
Matumizi ya lugha zinazopambanua upuuzi na ukosefu wa maadili notwithstanding, ukweli unabaki kwamba maisha yangu hayajawahi kuendeshwa kwa favours zozote na wala huyo dogo sifahamiani naye lakini nikiona haki na ukweli unapotoshwa basi hata wewe ***** ambaye sikufahamu nitakutetea tu maana mimi ninachotetea hapo ni ule ukweli. Wewe utafaidika na utetezi wangu kama tu ukweli ule umelalia kwako. Labda wewe unaishi kwa favours za wanasiasa ndiyo maana unadhani Slaa akiongea basi maneno yake ni gospel truth kumbe ni uzushi tu!

Unachopaswa kujuwa tu ni kwamba hili sio jukwaa la majuha na misukule. ilitolewa list of shame akiwemo baba yake Riziwan, Je mpaka leo bado anajadiliana na wanasheria? yuko wapi Nimrodi Mkono?
 
Wacha sasa nije kivingine na ushaidi wa picha za majengo ambazo zinaonesha kabisa contractor wa jengo lile la kule Aboterbad Pakistan, na haya majengo ambayo yapo hapa kwetu niliyoyataja ni contractor mmoja. kuna kainzi kangu kanaongea kiarabu kataenda kuniletea picha za yale majengo.

Lazima tupingane na ugaidi kwa gharama zozote! Safi kamanda
 
The most stupid way of interpreting things. What do you know about prima facie evidence? Huyu dogo alitoa siku saba kwa waropokaji hawa kuja na ushahidi, ku-retract porojo zao au wafikishwe mahakama. If you are saying the seven days expired yesterday, did you expect him to knock the court doors today? He needs time to prepare court documents that institute proceedings that will sure take a few days. This is not like sighting of the moon, it is a process that starts the moment the accuser fails to take heed to the demand notice.

Lakini ambacho ni cha kushangaza ni taarifa kwamba huyo anayeitwa Dr. na mnayemtukuza sana ame-despatch watu kwenda mikoani kutafuta ushahidi baada ya kupokea demand notice na hii inamaanisha kwamba alitumwa kuropoka na mafisadi wanaomtumia wakati hakuwa na ushahidi wowote ule na kwa sababu amezoea watu kutishia bila kuchukua hatua, sasa ameona kabisa hatari iliyo mbele yake. case ya Mtikila hatuwezi kuisemea kwa sababu case yake ya insanity ni well documented na sasa anachofanya ni kutafuta ajira ya kusogeza siku baada ya kugeuka kuwa irrelevant kwenye political equation ya nchi hii.

jk.jpg

Tatizo lako hufuatilii vyombo vya habari! Tarehe 03/05/2011 Dr Slaa na Mch Mtikila walimjibu Fisadi Ridhiwani Kikwete kwamba hakuna haja ya kusubiri mambo ya siku saba, kwa hiyo aende tu mahakamani!

Slaa, Mtikila wamtega mtoto JK

Tuesday, 03 May 2011 21:50
Leon Bahati na Raymond Kaminyoge

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amemtega mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani, akisema akifanikiwa kukifikisha chama hicho mahakamani atakuwa amefanikiwa kula mfupa ambao uliwashinda vigogo waliowatangazwa hadharani kuwa ni mafisadi nchini.

Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana alipotakiwa kutoa msimamo wake kuhusu kauli ya Ridhiwani aliyoitaoa Dar es Salaam juzi, kuwa atamfikisha mahakamani ili kuthibitisha kauli yake kwamba mtoto huyo wa rais ni bilionea aliyepata utajiri wa kutisha kipindi kifupi.

Ridhiwani alimpa siku saba Dk Slaa, kuanzia jana awe amekanusha kauli hiyo ya kumtuhumu kuwa fisadi, vinginevyo atamfikisha mahakamani.
"Sisi tunasema atangulie huko mahakamani sisi tutakuja nyuma," alisema Dk Slaa.

Dk Slaa ambaye katika uchaguzi uliopita aligombea urais na kutoa upinzani mkubwa kwa Rais Kikwete aliyetangazwa kuwa mshindi, alisema kauli za kushtakiwa wanapotangaza taarifa za ufisadi hadharani zimekuwa za kawaida.

Alisema wengi waliwahi kutoa kauli kama hiyo kupitia vyombo vya habari baada ya kuwatuhumu hadharani kuwa ni mafisadi, lakini wakashindwa kwenda mahakamani.

"Chadema tuna uzoefu tulipotaja orodha ya mafisadi walitutishia kuwa watatushtaki mahakamani tukawaambia watangulie sisi tutakuja nyuma, lakini walishindwa kutekeleza ahadi yao," alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa, iwapo Ridhiwani atafanya hivyo atakuwa amevunja rekodi ambayo imewashinda watu wazito.

Katibu huyo ambaye umaarufu wake ulikuja kwa kasi kipindi cha miaka 15 aliyokuwa Mbunge wa Karatu, Arusha, alijigamba kuwa hawazungumzi jambo bila vielelezo ndio maana wanajiamini kwa kila wanachokisema hadharani.

Dk Slaa alitupia lawama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwamba amekuwa akisisitiza ifutwe kwa sababu inashindwa kufanya kazi yake, ikiwamo kufanya uchunguzi kwa watu wanaotuhumiwa kupata utajiri katika mazingira yenye utata.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Ridhiwani alikanusha kuwa kijana bilionea kama Dk Slaa anavyomtuhumu.Alisema anamiliki shamba mkoani Pwani, lenye ukubwa wa ekari 1.5, gari ndogo na akaunti kwenye benki ya CRDB, NBC na Stanbic, ambazo hakutaja kiasi cha fedha.

Dk Slaa alipinga vikali kauli hiyo na kwamba, alimaliza shule miaka michache iliyopita, lakini sasa ni bilionea na utajiri huo aliupata kwenye mazingira ya utata.

Wakati huohuo, Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila, alisema atatoa uthibitisho mahakamani kuhusu mali alizozitaja kuwa zinamilikiwa na Ridhiwani."Siwezi kumuomba radhi mtu, nina uhakika wa kuwa kijana yule anamiliki mali ambazo hajazipata kwa njia halali, itakuwa vizuri ikiwa atanipeleka mahakamani, kwani huko ndiko nitakakoonyesha uthibitisho wangu," alisema Mchungaji Mtikila.

Jumamosi iliyopita, Mtikila alikaririwa na vyombo vya habari akisema, Ridhiwani ni bilionea anayemiliki nyumba za ghorofa, malori, kampuni za ujenzi wa barabara na ardhi.

Source: Mwananchi.
 
Back
Top Bottom