Mwana Mapinduzi
Member
- Feb 28, 2008
- 16
- 0
Richmond kubwa zaidi yaibukia Mwanza
*Ni mkataba wa umeme wa Sh155 bilioni
*Ulisainiwa na serikali Oktoba 2006
*Mitambo haijawahi zalisha umeme
*Mwekezaji analipwa Sh9bn kila mwezi
Na Waandishi Wetu
MKATABA wa Sh155.2 bilioni wa Kampuni ya Marekani kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharura kutokana na tatizo la umeme lililojitokeza mwaka 2006, ni wa mashaka baada ya kubainika kuwa kampuni hiyo haikuwahi kuzalisha hata Megawati (Mw) moja .
Kampuni hiyo ya kimarekani licha ya kutozalisha umeme, bado inaendelea kulipwa mabilioni ya shilingi na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zikiwa ni gharama za mitambo hiyo.
Kampuni hiyo ya Alstom Power Rental Energy (APR Energy LLC) iliingia mkataba na Tanesco wa kuzalisha Mw 40, lakini haikusambaza umeme hata kidogo kwa kuwa haijaombwa kufanya hivyo.
Mtambo wa kampuni hiyo ambao ulikodishwa Oktoba mwaka 2006, ulifungwa Mwanza baada ya makubaliano ya kusambaza umeme katika gridi ya taifa Kaskazini mwa Kanda ya Ziwa, kutokana na kuwapo kwa tatizo la umeme ambalo lilisababishwa na ukame wa muda mrefu.
Uchunguzi umebaini kuwa Tanesco inalazimika kulipa karibu Sh9bilioni kila mwezi, ili kugharamia mitambo hiyo ya kufua umeme ambayo iliagizwa kutoka Marekani.
Tanesco pia ililipa Sh150milioni kusaidia kufunga na kuunganisha mitambo hiyo katika gridi ya taifa.
Mkataba wa Alstom ni miongoni mwa mikataba ya kusambaza umeme wa dharura, iliyoingia na serikali kwa ajili ya kumaliza tatizo la umeme ambalo liliikumba nchi mwaka juzi.
Wadau wamedai kuwa Tanesco haikuwa na haja ya kulipa gharama hizo kwa kuwa wakati huo mabwawa ya kuzalisha umeme yalikuwa yamejaa.
Wafanyabiashara katika Mkoa wa Mwanza, wameeleza kuwa jenereta za kampuni hiyo, hazijawahi kuwashwa hata umeme wa Tanesco unapozimika ghafla.
Hata hivyo, haijafahamika kama Alstom, itaendelea na mkataba huo licha ya kuelezwa kuwa mkataba wake umekwisha.
Awali aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alishambuliwa baada ya mtambo huo kuzinduliwa na kuelezwa kuwa serikali ingebadilisha jenereta hizo na kutumia gesi ili kupunguza gharama za uendeshaji.
Waziri wa sasa wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema hayuko katika mazingira ya kueleza kama Serikali itasaini tena mkataba na kampuni hiyo au la.
Naye Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mwanza, Christopher Masasi alikataa kusema lolote kuhusiana na suala hilo na kumtaka mwandishi kuwasiliana na Makao Makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam, ili kupata maelezo kuhusiana na mkataba huo.
Meneja Uhusiano wa Tanesco, Daniel Mshana alipoulizwa kuhusiana na mtambo huo, alisema shirika hilo halina haja ya kutumia umeme kutoka Kampuni ya Alstom kwa sababu inazalisha umeme wa kutosha.
�Ni kweli mtambo ulijaribiwa lakini hatukuwahi kutumia umeme wake kwa sababu hatuuhitaji hivi sasa,� alisema Mshana.
Naye Meneja wa Alstom ambaye yuko Mwanza, Keith �Bo� Thomas, alikataa kutoa maelezo kuhusiana na mkataba wao na Tanesco.
�Hawezi kutoa majibu zaidi bila mwandishi kuwa na kibali cha maandishi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco. Hii ni sehemu ya makubaliano yetu na Tanesco,� alisema Thomas.
Kashfa hii imeibuka wakati serikali inadaiwa kuingia mkataba tata na Kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond. Kashfa ya mkataba wa Richmond imesababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na waliokuwa mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Nizar Karamagi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Ibrahim Msabaha.
Viongozi hao walijiuzulu kutokana na kutuhumiwa na Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza kashfa hiyo kwamba, walihusika moja kwa moja kuhakikisha kuwa serikali inaingia mkataba na kampuni hiyo.
Richmond ambayo hivi sasa ni (Downs), inalipwa na serikali kiasi cha Sh152 milioni kwa siku, kiasi ambacho ni mzigo mkubwa kwa Tanesco kumudu kuulipa.
Mikataba mingine ambayo serikali imeingia katika sekta ya umeme ambayo inaliumiza Tanesco ni IPTL, Songas na Aggreko.
Kwa mara ya kwanza habari hii ilichapishwa katika Gazeti dada la The Citizen toleo la juzi