richmond nyingine yaibuka mwanza

Feb 28, 2008
16
0
Richmond kubwa zaidi yaibukia Mwanza
*Ni mkataba wa umeme wa Sh155 bilioni
*Ulisainiwa na serikali Oktoba 2006

*Mitambo haijawahi zalisha umeme

*Mwekezaji analipwa Sh9bn kila mwezi

Na Waandishi Wetu

MKATABA wa Sh155.2 bilioni wa Kampuni ya Marekani kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharura kutokana na tatizo la umeme lililojitokeza mwaka 2006, ni wa mashaka baada ya kubainika kuwa kampuni hiyo haikuwahi kuzalisha hata Megawati (Mw) moja .

Kampuni hiyo ya kimarekani licha ya kutozalisha umeme, bado inaendelea kulipwa mabilioni ya shilingi na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zikiwa ni gharama za mitambo hiyo.

Kampuni hiyo ya Alstom Power Rental Energy (APR Energy LLC) iliingia mkataba na Tanesco wa kuzalisha Mw 40, lakini haikusambaza umeme hata kidogo kwa kuwa haijaombwa kufanya hivyo.

Mtambo wa kampuni hiyo ambao ulikodishwa Oktoba mwaka 2006, ulifungwa Mwanza baada ya makubaliano ya kusambaza umeme katika gridi ya taifa Kaskazini mwa Kanda ya Ziwa, kutokana na kuwapo kwa tatizo la umeme ambalo lilisababishwa na ukame wa muda mrefu.

Uchunguzi umebaini kuwa Tanesco inalazimika kulipa karibu Sh9bilioni kila mwezi, ili kugharamia mitambo hiyo ya kufua umeme ambayo iliagizwa kutoka Marekani.

Tanesco pia ililipa Sh150milioni kusaidia kufunga na kuunganisha mitambo hiyo katika gridi ya taifa.

Mkataba wa Alstom ni miongoni mwa mikataba ya kusambaza umeme wa dharura, iliyoingia na serikali kwa ajili ya kumaliza tatizo la umeme ambalo liliikumba nchi mwaka juzi.

Wadau wamedai kuwa Tanesco haikuwa na haja ya kulipa gharama hizo kwa kuwa wakati huo mabwawa ya kuzalisha umeme yalikuwa yamejaa.

Wafanyabiashara katika Mkoa wa Mwanza, wameeleza kuwa jenereta za kampuni hiyo, hazijawahi kuwashwa hata umeme wa Tanesco unapozimika ghafla.

Hata hivyo, haijafahamika kama Alstom, itaendelea na mkataba huo licha ya kuelezwa kuwa mkataba wake umekwisha.

Awali aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alishambuliwa baada ya mtambo huo kuzinduliwa na kuelezwa kuwa serikali ingebadilisha jenereta hizo na kutumia gesi ili kupunguza gharama za uendeshaji.

Waziri wa sasa wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema hayuko katika mazingira ya kueleza kama Serikali itasaini tena mkataba na kampuni hiyo au la.

Naye Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mwanza, Christopher Masasi alikataa kusema lolote kuhusiana na suala hilo na kumtaka mwandishi kuwasiliana na Makao Makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam, ili kupata maelezo kuhusiana na mkataba huo.

Meneja Uhusiano wa Tanesco, Daniel Mshana alipoulizwa kuhusiana na mtambo huo, alisema shirika hilo halina haja ya kutumia umeme kutoka Kampuni ya Alstom kwa sababu inazalisha umeme wa kutosha.

�Ni kweli mtambo ulijaribiwa lakini hatukuwahi kutumia umeme wake kwa sababu hatuuhitaji hivi sasa,� alisema Mshana.

Naye Meneja wa Alstom ambaye yuko Mwanza, Keith �Bo� Thomas, alikataa kutoa maelezo kuhusiana na mkataba wao na Tanesco.

�Hawezi kutoa majibu zaidi bila mwandishi kuwa na kibali cha maandishi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco. Hii ni sehemu ya makubaliano yetu na Tanesco,� alisema Thomas.

Kashfa hii imeibuka wakati serikali inadaiwa kuingia mkataba tata na Kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond. Kashfa ya mkataba wa Richmond imesababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na waliokuwa mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Nizar Karamagi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Ibrahim Msabaha.

Viongozi hao walijiuzulu kutokana na kutuhumiwa na Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza kashfa hiyo kwamba, walihusika moja kwa moja kuhakikisha kuwa serikali inaingia mkataba na kampuni hiyo.

Richmond ambayo hivi sasa ni (Downs), inalipwa na serikali kiasi cha Sh152 milioni kwa siku, kiasi ambacho ni mzigo mkubwa kwa Tanesco kumudu kuulipa.

Mikataba mingine ambayo serikali imeingia katika sekta ya umeme ambayo inaliumiza Tanesco ni IPTL, Songas na Aggreko.

Kwa mara ya kwanza habari hii ilichapishwa katika Gazeti dada la The Citizen toleo la juzi
 
Hivi haya yote ni kweli ndugu Rais hakuyajua ? Au sasa yanatoka mengi kama alivyosema Zitto kwamba ulaji uko hatarini so wanasema kila siri ? Yaani Tanzania hii ya Mwanza kula mapanki lakini bado 9bn zinatoka ?
 
Rejea report ya Mwakyembe:

gharama ya kununua mtambo mpya 100MW toka kwa wazalishaji ni $45.00 million. leo hii serikali inakodisha 40MW kwa $155.00 million. Watanzania bado wanaangalia tu. Kwa nini tusimwage damu kwa week moja watakaosalia mambo yataenda sawa. na kuhakikisha kwamba wale mafisadi wote tunawatafutia sniper wa kuwamaliza mmoja baada ya mwingine. tukianzia na Mkapa/Lowasa/Karamagi/Mramba/Yona/Mwakapugi/ na wengineo. Maana gharama ya kukodi sniper mmoja toka majuu ni $100,000.00 kwa kila kichwa. Kwa vichwa kumi ni $1,000,000.00. hivyo ni bora kukodi sniper kuliko kupoteza $155,000,000.00.0 tutabaki na faida kubwa ya $154,000,000.00.
 
Wanakupua kila kona mabilioni ya shilingi kwa kusaini mikataba mibovu na kampuni ambazo hazijui chochote kuhusu umeme au mikataba ya madini ambayo Tanzania hanufaiki chochote.

Cha kushangaza zaidi, shule za msingi kuna utaratibu wa kumfukuza mwanafunzi mtukutu vivyo hivyo shule za sekondari. Sirikali yenyewe imekuwa mstari wa mbele kuwafukuza wanafunzi wa vyuo vyetu vikuu wakati mwingine bila hata kuwa na makosa yoyote na kupoteza kabisa haki zao za kupata elimu ya juu. Lakini, mafisadi wanaohusika na ufisadi mkubwa ambao Watanzania hatujawahi kuona katika nchi yetu bado wamekumbatiwa ndani ya CCM bila woga wala hata aibu tena na wengine kuingizwa kwenye kamati za Bunge hata sakata lililofanya wajiuzulu nyadhifa zao bado halijamalizika! Hii inaonyesha dharau kubwa ya CCM kwa Watanzania.

Kwa kifupi CCM inatwambia haijali chochote kuhusiana na kelele za wananchi kuhusiana na ufisadi unaoendelea ndiyo maana bado imewakumbatia mafisadi ndani ya chama hicho na kuwapa vyeo bila hata aibu! Nakulilia Tanzania!
 
Rejea report ya Mwakyembe:

gharama ya kununua mtambo mpya 100MW toka kwa wazalishaji ni $45.00 million. leo hii serikali inakodisha 40MW kwa $155.00 million. Watanzania bado wanaangalia tu. Kwa nini tusimwage damu kwa week moja watakaosalia mambo yataenda sawa. na kuhakikisha kwamba wale mafisadi wote tunawatafutia sniper wa kuwamaliza mmoja baada ya mwingine. tukianzia na Mkapa/Lowasa/Karamagi/Mramba/Yona/Mwakapugi/ na wengineo. Maana gharama ya kukodi sniper mmoja toka majuu ni $100,000.00 kwa kila kichwa. Kwa vichwa kumi ni $1,000,000.00. hivyo ni bora kukodi sniper kuliko kupoteza $155,000,000.00.0 tutabaki na faida kubwa ya $154,000,000.00.
ni wazo zuri sana kuliko kupoteza maisha ya wasio na hatia bora hili lifanyike
 
Rejea report ya Mwakyembe:

gharama ya kununua mtambo mpya 100MW toka kwa wazalishaji ni $45.00 million. leo hii serikali inakodisha 40MW kwa $155.00 million. Watanzania bado wanaangalia tu. Kwa nini tusimwage damu kwa week moja watakaosalia mambo yataenda sawa. na kuhakikisha kwamba wale mafisadi wote tunawatafutia sniper wa kuwamaliza mmoja baada ya mwingine. tukianzia na Mkapa/Lowasa/Karamagi/Mramba/Yona/Mwakapugi/ na wengineo. Maana gharama ya kukodi sniper mmoja toka majuu ni $100,000.00 kwa kila kichwa. Kwa vichwa kumi ni $1,000,000.00. hivyo ni bora kukodi sniper kuliko kupoteza $155,000,000.00.0 tutabaki na faida kubwa ya $154,000,000.00.

Ukitaka kujua kwamba watanzania hawajali na ndiyo maama na CCM wanapenda nenda kwenye ma bar ma kona za kahawa utakuta watu wanakunywa pombe mapema asubuhi na kuongelea hizi kashfa kama vile mambo ya Simba na Yanga na JK kesha jua kwamba wana wakejeli hata wapinzani na yeye anawaita watani zake wa jadi .Who is serious by the way hado kuwazia haya ?Watanzania wako tayari kuongelea kwa ushabiki na kulala hata kama hawana umeme wala chakula ili maradi kesho ana ka hela ka bia mjini kijijini Mama na ndugu zake wanakufa njaa wanakula mizizi na kufa kwa malaria and cannot afford hata kununua pain killer .Tanzania sawa na watu wa Zimb sijui nani kawaroga hawa .
 
..Ama kweli Waafrika ndivyo tulivyo. Bundala as quoted by Nyani Ngabu. Evidence by Watson.
 
Inawezekana mimi ni msahaulifu, Kumbukumbu yangu ni kwamba Issue ya Mwanza ilikuwa TANESCO inanua generator... haikuwa issue ya ku-outsource generation of power.

Ndio maana kwenye kikao cha CCM walisema wangehamisha ile generator kupeleka Kigoma, lakini baadaye wakasema ile ilikuwa high speed generator hivyo haifai kwa matumizi ya Kigoma.

Wenye kumbukumbu nzuri karibuni... lakini habari hiyo naiona kama mwandishi amekurupuka.
 
Kasheshe unajikanganya .Unasema kumbukumbu si sawa za kwako tena unasema mwandishi kakurupuka namna gani ? Wanasoma hapa so ngoje waje na maelezo sahihi.Haya ni mambo ya ndani baada ya watu kutemwa nk .So it is a revenge kiasi tunapata nafuu kwa kuyajua haya .
 
Hiyo Generator ni ya kukodi siyo kununua.

Unless utuambie wewe ni TANESCO, ili tukuamini basi tupatie reference!!!

Angalizo... Ukodishaji wa aina yoyote ni Ghali achilia majenerator... hata vifaa vya kawaida vya maofisini... sasa wakati tunayajadili haya tufahamu hivyo...

Kukodi, Taxi, Nyumba, Office space etc...power generation ni ghali sio sawa na ukiwa mmliki.

Issue ni je? kulikuwa kuna umuhimu wa kukodi au kununua? Jibu la hili ni wewe kuthibitisha kama mulikuwa na fedha za kununua hizo generators kwa wakati huo.

Generator hizo haziwezi kuwashwa sasa kwa kuwa umeme wa Hydro ni nafuu kuliko wa Thermal...

Lakini capacity charge,,, ni kitu cha kawaida kulipwa kwenye kila kitu kinachokodishwa.

Labda hoja iwe ni fedha nyingi zaidi ya current best practises in the world. na hapa hatutaki longo longo mutuletee hizo data.

Nanusa tunaelekea kufikia mahali kusema kila aliyepo serikalini hana akili, sisi tuliko kwenye mitandao kutoka sehemu mbalimbali duniani ndio tunajua, uhandisi, negotiations, procurement/purchasing, drafting and enforcing and monitoring contracts...
 
Rejea report ya Mwakyembe:

gharama ya kununua mtambo mpya 100MW toka kwa wazalishaji ni $45.00 million. leo hii serikali inakodisha 40MW kwa $155.00 million. Watanzania bado wanaangalia tu. Kwa nini tusimwage damu kwa week moja watakaosalia mambo yataenda sawa. .

Wee unaenda skejo, unataka nani akumwagie damu wewe..Mob Justice ndio hii
 
Inawezekana mimi ni msahaulifu, Kumbukumbu yangu ni kwamba Issue ya Mwanza ilikuwa TANESCO inanua generator... haikuwa issue ya ku-outsource generation of power.

Ndio maana kwenye kikao cha CCM walisema wangehamisha ile generator kupeleka Kigoma, lakini baadaye wakasema ile ilikuwa high speed generator hivyo haifai kwa matumizi ya Kigoma.

Wenye kumbukumbu nzuri karibuni... lakini habari hiyo naiona kama mwandishi amekurupuka.

Hizo ni kumbukumbu zako!!!!! kama ile mitambo ingekuwa imenunuliwa na TANESCO, sidhani kama ingekuwa inamilikiwa na hilo kampuni, kwani hata ukipita na gari pale maeneo ilipo mitambo hiyo utaiona kwa maandishi makubwa ya kampuni husika na wala si jina la TANESCO. kASHESHE fanya uchunguzi kabla ya kumshambulia mwandishi.....
 
Rejea report ya Mwakyembe:

gharama ya kununua mtambo mpya 100MW toka kwa wazalishaji ni $45.00 million. leo hii serikali inakodisha 40MW kwa $155.00 million. Watanzania bado wanaangalia tu. Kwa nini tusimwage damu kwa week moja watakaosalia mambo yataenda sawa. na kuhakikisha kwamba wale mafisadi wote tunawatafutia sniper wa kuwamaliza mmoja baada ya mwingine. tukianzia na Mkapa/Lowasa/Karamagi/Mramba/Yona/Mwakapugi/ na wengineo. Maana gharama ya kukodi sniper mmoja toka majuu ni $100,000.00 kwa kila kichwa. Kwa vichwa kumi ni $1,000,000.00. hivyo ni bora kukodi sniper kuliko kupoteza $155,000,000.00.0 tutabaki na faida kubwa ya $154,000,000.00.

Wewe KOKOLO unamawazo kama yangu.
Hiyo ndiyo dawa, mmoja akienda chini wengine wataanza kutafutana na kuficha viwiliwili vyao kama Mipanya buku.
Tuone kama wana hela za kuzuia risasi za sniper.
 
Unless utuambie wewe ni TANESCO, ili tukuamini basi tupatie reference!!!

Angalizo... Ukodishaji wa aina yoyote ni Ghali achilia majenerator... hata vifaa vya kawaida vya maofisini... sasa wakati tunayajadili haya tufahamu hivyo...

Kukodi, Taxi, Nyumba, Office space etc...power generation ni ghali sio sawa na ukiwa mmliki.

Issue ni je? kulikuwa kuna umuhimu wa kukodi au kununua? Jibu la hili ni wewe kuthibitisha kama mulikuwa na fedha za kununua hizo generators kwa wakati huo.

Generator hizo haziwezi kuwashwa sasa kwa kuwa umeme wa Hydro ni nafuu kuliko wa Thermal...

Lakini capacity charge,,, ni kitu cha kawaida kulipwa kwenye kila kitu kinachokodishwa.

Labda hoja iwe ni fedha nyingi zaidi ya current best practises in the world. na hapa hatutaki longo longo mutuletee hizo data.

Nanusa tunaelekea kufikia mahali kusema kila aliyepo serikalini hana akili, sisi tuliko kwenye mitandao kutoka sehemu mbalimbali duniani ndio tunajua, uhandisi, negotiations, procurement/purchasing, drafting and enforcing and monitoring contracts...

Kasheshe,

Mkuu tunatofautiana mengi lakini hili la umeme wa Mwanza limejaa mambo na unless unajua nisichojua, nisingekushauri kuwatetea hata kidogo walihohusika hapa.

Mapesa yaliyotumika na yatakayotumika hapa ni mengi kwa umeme ambao labda hautakuja kuzalishwa kamwe. Kuna tetesi kuwa wadosi wa ccm mwanza (mmoja alikuwa waziri na mwingine bado ni waziri kwa serikali ya Kikwete) wanahusika moja kwa moja na hii skendo.

Swali langu ni kuwa, ni nini kitafanyika kumwamsha Kikwete toka katika usingizi pono aliomo sasa hivi?
 
Unamaana Tony Diallo na Lawrence Marsha ama?
 
Mimi bado sijasema haya (bado).... ila nasubiria kamati nyingine kama ya Mwakyembe iundwe ili ujue vile ccm wanakula nchi kwa mirija wakati watanzania wakifa kwa kukosa hata bidhaa muhimu kwenye maisha kama madawa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom