Richmond mpya Singida | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Richmond mpya Singida

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Isango, Aug 12, 2011.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Uwekezaji wa Umeme wa Upepo mnaousikia, umegubikwa na utata mtupu.

  Kampuni zinaingia kinyemela, watu wanatoka moja kwa moja nje ya nchi na kufika kijijini kulaghai wananchi, viongozi wa serikali wanapewa kitu kidogo wanatulia, imefikia hadi wiki iliyopita amekuja kutembelea hadi balozi wa Uingereza kushiriki Ufisadi huu.

  Wanaharakati fuatilieni sakata hili nchi yetu inauzwa tena kwa watu wasiofuata sheria, wanaojali kitu kidogo, miradi hiyo huenda isikamilike kama ilivyokuwa Richmond, au kutakuwa na mgogoro mkubwa kwani wananchi hawajui kama maeneo yao yameuzwa.

  Vinara wa dili hili ni Mkurugenzi wa Manispaa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida
   
 2. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kajiandae upya utuletee taarifa yenye kueleweka, uwekezaji huo unafahamika lakini unachokisema hakijaeleweka
   
 3. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mkuu Isango, naomba habari zaidi juu ya huo mradi. Eneo ambako mradi huo utakuwa, pale Siuyu-Misimbwa ni eneo la babu yangu mzaa mama. Nilipokuwa Singida nikasikia wanapigwa dana dana kwenye fidia. Nataka kupata details ili nione nitawasaidiaje kisheria. Hilo eneo liko jimbo la Nyalandu, Dewji au Tundu Lissu? Tafadhali nijuze.
   
 4. R

  Radi Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mnyampaa Tzpride kwa taarifa yako hili jimbo lipo kwa Dewji. kwa Tundu Lissu hawawezi kufika kwani wanamjua jinsi alivyo mwanaharakati.
   
 5. h

  hoyce JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  &lt;br /&gt;<br /> Jamaa yangu kanipigia simu jana akiwa Singida, alimwona Lowassa anaingia mjini humo, baadaye akaingia Chenge, alishangaa kuona wanafuatana. isijekuwa ndio dili lao?
  &lt;br /&gt;
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  I am tired with those two pipo. sitaki hata kuwasikia, mafisadi hawa. Agghhhh!!!!!
   
 7. M

  Mzee wa Posho Senior Member

  #7
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umekurupuka sana Mkuu na thread yako! Aina ya Ufisadi hujaonesha unachosema ni suala la wananchi kulipwa fidia?
   
 8. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Wewe una-post saba tu humu, ina maana unaleta majungu tu humu ndiyo maana thread yako iko hewani haieleweki.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0

  Umetumwa? si ukaombe kazi kwenye huo mradi badala ya kulalamikia maendeleo? au weka wewe basi umeme wa mavi ya ng'ombe usaidie gridi ya taifa.
   
 10. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #10
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Bwana isango naona kukosa ubunge kumepelekea uchanganyikiwe kabisa...uandishi wa aina gani huu mkuu...
   
 11. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anyway ,tafadhali msimuone Isango katumwa .Mimi nalifahamu eneo la mradi.Linacover eneo la DEWJ NA LISSU. Ulivyotaja Tzpride ni eneo la Lissu . Ni kweli wananchi wananchi wanasainishwa vitu wasivyojua na wanapewa fidia kimafungu ,yaani wenye kuletaleta mdomo wanapewa fidia sio vingine.
   
 12. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Salanga nakushukuru mkuu. Nafanya utafiti kama ni jimb0 la Lissu, nitamshirikisha ili tulifuatilie hili la fidia, Siwezi kusema juu ya mradi huu kwa sasa maana details sina kabisa...ila ndugu zangu mmoja wao mama yangu) walinilalamikia kwa fidia imekaa kifisadi zaidi. Kama kuna mtu na details za kamapuni inayofanya huo mradi anaisaidie nianzie hapo.
   
 13. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Asante sana Radi. Tafadhali nipe details zaidi za huu mradi.
   
 14. I

  Isango R I P

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nawashukuru wote waliochangia hata kwa kutoa matusi, suala hili si la kwangu ni suala la uzalendo, ni suala la utaifa. Umeme sio kwa faida yangu ni kwa faida ya Taifa, Detail zote tumepata tutaweka hadharani wakati ukifika. Ila Watanzania kufanya utani katika mambo ya msingi ya Taifa ndo kumetufikisha hapa. Tunaharibu hata fikra zetu kwa sababu tu ya pesa, NINAJUA YOTE YANA MWISHO, SIKU ukweli ukibainika nitaenda kusali na kumwomba Mungu AWASAMEHE wote wanaokubali watu wasiojua sheria wanaouzwa kwa bei ndogo kwa manufaa ya wengine. UKOLONI.................. IPO SIKU WATU WATASEMA TUMECHOKA!
   
Loading...