Richard S Mabala:Vyerehani vitatu ni Karakana au Kiwanda??

Richard S Mabala:Vyerehani vitatu ni Karakana au Kiwanda??

britanicca

Platinum Member
Joined
May 20, 2015
Posts
18,180
Reaction score
48,115
Richard S Mabala anauliza vyerehani vitatu ni karakana au kiwanda?

Swali hivi nani hasa mwenye jukumu la kufungua viwanda na kuanzisha viwanda?

Jibu linarudi pale pale kwamba sector ya viwanda duniani huwa inaanzishwa na watu binafsi ba wawekezaji toka nje,

Tujue hata nchi za viwanda vikubwa zilianza na karakana za vyerehani na viwanda vidogo vidogo

China ya mwaka 1963 ilikuwa na karakana nyingi sana kulinganisha na nchi yeyote ulimwenguni, hata USA ya mwaka 1772 ilikuwa na karakana nyingi kuliko nchi yeyote ulimwenguni,

Kwanini Tanzania ya sasa isiwe na karakana nyingi kuzidi zote ulimwenguni Ili Tanzania ya viwanda iwe 2100?

Kwa mujibu wa Mwijage, waziri wa viwanda na biashara, vyerehani vitatu ni kiwanda na siyo karakana.

Ndiyo maana akajitokeza waziri mwingine ambaye yeye anadhani dawati ni kiwanda, hivyo akaagiza kila mkuu wa mkoa aanzishe viwanda 100 ( bila shaka alimaanisha kila mkuu wa mkoa achonge madawati 100).

Nchi hii bado kidogo tuanze kuvaa chupi juu ya suruali.
 
Inategemea na mtazamo wa mtu
 
Huyo mabara achunguzwe uraia wake, anapata wapi ujasiri wa kuhoji kauli za waziri mwijage! Hajui kuwa mwijage bado anaitaka ile kazi!?
 
Kwa mujibu wa Mwijage, waziri wa viwanda na biashara, vyerehani vitatu ni kiwanda na siyo karakana.

Ndiyo maana akajitokeza waziri mwingine ambaye yeye anadhani dawati ni kiwanda, hivyo akaagiza kila mkuu wa mkoa aanzishe viwanda 100 ( bila shaka alimaanisha kila mkuu wa mkoa achonge madawati 100).

Nchi hii bado kidogo tuanze kuvaa chupi juu ya suruali.
Mtu serious hawezi kuongelea viwanda bila kuonhea kilimo cha uhakika, uvuvi, ufugaji, rasilimali watu na nishati ya umeme wa uhakika. Ukiona mtu anaongelea viwanda bila kwanza kuzungumzia haya kwa msisitizo wake. Narudia kwa msisitizo huyo hana tofauti na yule mzalendo mwenye uchungu na nchi hii mpaka kupata frastration kiasi cha kuhamisha ujenzi wa bandari bwagamoyo na kupelekwa ujenzi wa kiwanja cha ndege kwao sawa na alichofanya mzee wa speed na viwango samweli sitta.mungu atunusuru na unafiki huu wa kuunga mkono jitihada hizi za kubomoa awamu zilizopita na kufunika awamu yetu kwa kujiuzulu na kutia taifa hili hasara kubwa ya kuitisha chaguzi zisizo huru
 
Wakuu kiukweli hii Sera ya viwanda may be it is a dream of our gvt,, itabaki kwenye majukwa ya siasa na makabulasha ya chama tawala tu tena kwa asilimia 1200%.
1.Hatuwez kufikia kujenga nchi ya viwanda Kwa kukopa!
2. Hatuwez kujenga nchi ya viwanda kwa kilimo dhaifu na cha kishenzi chini ya chama tawala.
3. Hatuwez kujenga nchi ya viwanda kwa kupunguza mifugo.
4. Hatuwez kujenga nchi ya viwanda kwa kuboresha soko la manunuzi ya wanasiasa wakati tumbaku inaoza huko TABORA, SHINYANGA.
5. hatuwez kujenga nchi ya viwanda kwa kutishiana uhai na usalama wa wananchi, kubinya uhuru wa kujieleza wananchi.
6. Utajengaje viwanda wakati wafanyakazi unawaongezea 6000 kwa miaka miwili!!
7. Huwezi kujenga viwanda bila kuboresha afya ya wananchi (labor force) kwa ajili ya uzalishaji katika sekta zote.
NB: TUTAJENGA VIWANDA KWA SERA THABITI NA ENDELEVU NA SIO FRUSTRATION ZA WATU NA.
sipingi maendeleo ila maendeleo hayaji kwa kelele na kupayuka hovyo hovyo!!! Kila kiongozi anaamka na Lake jambo kila kukicha. Viwanda tutajenga ila vya kufyatua watoto bila mpango.
 
Richard S Mabala anauliza vyerehani vitatu ni karakana au kiwanda?

Swali hivi nani hasa mwenye jukumu la kufungua viwanda na kuanzisha viwanda?

Jibu linarudi pale pale kwamba sector ya viwanda duniani huwa inaanzishwa na watu binafsi ba wawekezaji toka nje,

Tujue hata nchi za viwanda vikubwa zilianza na karakana za vyerehani na viwanda vidogo vidogo

China ya mwaka 1963 ilikuwa na karakana nyingi sana kulinganisha na nchi yeyote ulimwenguni, hata USA ya mwaka 1972 ilikuwa na karakana nyingi kuliko nchi yeyote ulimwenguni,

Kwanini Tanzania ya sasa isiwe na karakana nyingi kuzidi zote ulimwenguni Ili Tanzania ya viwanda iwe 2100?

1972 USA ilishakuwa nchi ya viwanda vikubwa kwa kiwango cha juu wala si vikarakana! Labda china sijui
 
kuhamisha ujenzi wa bandari bwagamoyo na kupelekwa ujenzi wa kiwanja cha ndege kwao
Mkuu mbona kuna taarifa kuwa maana mfalme wa Oman ndiye atajenga bandari ya Bagamoyo na kuiendesha kwa miaka 50? Wanadai serikali haitahusika. Na ile meli kubwa iliyotoka Oman na kuja Tanzania hivi karibuni inadaiwa ilienda Bagamoyo.
Hebu nipe ukweli wa mambo mkuu juu ya hiki kizungumkuti.
 
Katika mawaziri viazi basi ni huyo wa viwanda, alipaswa kua anasaka wawekezaji huko nje na kuandaa mazingira rafiki ya uwekezaji lakini yeye ni mtu wa kuropoka ropoka pumba zisizo na msingi.
 
Back
Top Bottom