Richard Kasesera Mwenyekiti Bodi ya Madini, Anazo sifa Stahiki??

Jamaa yangu kwa kujipendekeza mwisho...sijui ila tushukuru Mungu nachelea kusema sijui ingekuwaje angekuwa she. Kubwa kupita yote ni Serikali/Nchi yetu kutokuwa na taratibu makini za kuteua viongozi...Msishange sana kuona watangazaji redio/TV wanajikomba kwa watawala, wasomi, wezi, mafisadi etc. Ni kwa sababu wanastand chance kubwa ya kuteuliwa vyeo kama zawadi.
 
@ Kimbunga: Aisee, umenikumbusha mbali sana. Hivi gogogo bado wanapatikana kweli!?
 
Si ndo alietishia bastola pale Kiwira,he! Wenye taaluma ya madin wanasota mtaani,ajira urafikinaizeshen after undugunaizesheni,end up 2015
 
Anatumika huyo, kiujumla ni kwamba hafai maana ni mtu wa kujikomba kwa mafisadi-magamba. Ana mpango wa kugombea ubunge Rungwe magharibi 2015. Hafai kabisa huyu jamaa.

Ubunge wa Rungwe magharibi atausikia tu kwani hela zake atakazokusanya na mafisadi wenzie zitaliwa na ubunge kama safari iliyopita ataukosa hasa kwavile mkweree anabifu na watu kutoka Mbeya na wao wanajua kuwa huyu jamaa ni kibaraka wake!!
 
Nadhani alimaliza 1996! Alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Basketball hapa Nchini na alichofanikiwa kufanya ni kuua mchezo wa basketball hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuulia mbali yale mashindano maarufu ya KILI RBA!

Wakati anagombea uwenyekiti wa basketball alijitambulisha kwamba ametumwa kugombea na Rais Kikwete aliyekuwa Mlezi wa chama hicho, lakini badala yake Kikwete akajitoa na kumuacha Kasesela aliyekuwa amembeba Riz one kwenye uongozi aklibaki kukudidimiza mchezo!!! jamaa huyu ni niksi kila anakopita!!!
 
Tuache ushabiki, mnaweza toa mfano wa mtu/ kiongozi yeyote mnaedhani yuko pahala kutokana na credibilties zake, warioba tu Leo baada ya kupewa ulaji wa katiba mpya mmemsema ATI anajipendekeza. Nipeni mimi basi hizo post.
 
Mungu wangu hii nchi inakwenda wapi huyu jamaa ni mpenda vijisenti mwisho,waulize waliofanya nae pale TMARC,yeye anawaza dili tu ,sasa kweli huyu kweli ana ujasiri wa kusema NO kwa mapapa wa kimataifa wanaojishughulisha na madini,lalaa watu wanapenda pesa lakini kwa huyu jamaa hana mfano,jamaa wa kujipendekeza sana,kila mkulu anakokuwa naye hufuata mara kwenye mpira wa kikapu (mkulu amewahi kuwa mlezi wa mchezo huo).Hapo ni porojo tupu ,hivi jamani usalama wa taifa kazi yao nini,je hapo zamani sio ndio walikuwa wanakusanya data kabla ya mtu kupewa cheo?hakika hapo ndio umuhimu wa katiba mpya unaonekana,watu wa hovyo ndio wanapewa nafasi nyeti,wapi tunaenda,HII NI AIBU
Mkuu mfianchi
Tulikutana kule kwenye uzi wa Lissu na kujikumbusha jinsi CCM walivyomshitaki.Nakuona tena hapa
 
Nadhani alimaliza 1996! Alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Basketball hapa Nchini na alichofanikiwa kufanya ni kuua mchezo wa basketball hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuulia mbali yale mashindano maarufu ya KILI RBA!
hahahaha, nimecheka sana
 
Back
Top Bottom