Rex Attorneys ni kashfa kubwa zaidi ya DOWANS

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Godfrey Dilunga
Januari 12, 2011

MCHAMBUZI wa nadharia za kisiasa na mwanafalsafa wa Roma ya Kale, Marcus Tullius Cicero, anayesifika kubuni maneno, hasa misamiati katika Kilatini, amepata kueleza nadharia za uamuzi kwa kuzingatia upeo wa akili za mhusika.

Cicero ambaye kwa wanahistoria wa Roma ni maarufu kama Tully, alizaliwa Januari 3, miaka 106 kabla ya Kristo na kufariki Desemba 7, miaka 43 kabla ya Kristo (BC). Kwa lugha rahisi, alikufa akiwa na miaka 63.

Tully anasema; mtu mwerevu huelekea kutoa uamuzi kwa kuzingatia sababu za kimantiki (reasoning); mwenye akili za wastani huamua kwa kuegemea uzoefu; mpumbavu kwa kulazimishwa; katili huamua ili kukidhi matakwa ya hisia.

Katika mgogoro wa Arusha, tukio zima la maandamano hadi vifo linahusisha werevu, wenye akili za wastani, wapumbavu na hata wenye ukatili. Sitajadili hilo leo.

Mjadala wa leo ni malipo ya kampuni ya Dowans. Nitajidili kwa kushirikisha mtazamo huo wa Tully na kidogo nitahusisha mtazamo wa Victor-Marie Hugo.

Huyu ni raia wa Ufaransa, aliyezaliwa Februari 26, mwaka 1802 na kuiaga dunia Mei 22, mwaka 1885, akiwa mzee wa miaka 83. Ni mshairi, mtunzi wa vitabu vya hadithi na mwanakampeni wa haki za binadamu.

Victor-Marie Hugo historia inamuelezea kuwa siku moja alielekeza fikra zake akijaribu kutofautisha kero zinazomzonga mtu mwerevu dhidi ya neema ‘inayomzunguka’ mpumbavu.

Katika fikra zake akahitimisha kuwa, bora kero za mwerevu kuliko neema ya mpumbavu. Pengine kwa upande mmoja, aliamini ni vigumu mpumbavu kutumia vizuri zaidi fursa za kunufaisha.

Lakini kwa upande mwingine, aliamini mwerevu anaweza kupambana kutatua kero zinazomzonga, kuliko mpumbavu anavyoweza kutumia neema aliyonayo.

Wanafalsafa hawa wanaweza kusaidia kueleweka kwa nitakachokijadili leo. Ni kuhusu hatua ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuthibitisha rasmi Serikali itailipa kampuni ya Dowans.

Malipo hayo yatafanyika kama hukumu hiyo itasajiliwa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kama nilivyoeleza, kwa kuzingatia mitazamo ya Tully na Victor – Marie Hugo, hebu tuhoji inapobidi.

Tutafakari na kuhoji kwa kurejea taarifa na kauli za viongozi wa serikali kuhusu sakata hili la Dowans na hukumu ya sasa katika vipengele vifuatavyo.

Kuvunjwa mkataba wa Dowans

Msingi wa kuvunjwa mkataba kati ya TANESCO na Dowans ni ushauri wa wanasheria kutoka kampuni ya Rex-Attorneys. Ni Kampuni hii ya kisheria iliyonadiwa bungeni kuwa, imebobea katika masuala ya sheria za kimataifa.

Agosti 28, mwaka 2008, Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda (mwanasheria kitaaluma) aliimwangia sifa kampuni ya Rex-Attorneys bungeni.

Waziri Mkuu alisema; “Kutokana na utata uliojitokeza katika mchakato mzima kuhusu mkataba baina ya TANESCO na Richmond uliotiwa saini tarehe 23 Juni 2006...”

“...Serikali kupitia TANESCO iliamua kufanyike mapitio ya mkataba huo na kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wanasheria waliobobea katika masuala ya mikataba ya kimataifa wa Kampuni ya Rex Attorneys.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, uchunguzi wa Rex Attorneys ulibaini mambo matatu aliyoainisha kati ya mengi.

Mosi; manunuzi ya huduma ya umeme na kuingia mkataba na Richmond Development Company LLC ulikiuka Sheria ya Manunuzi wa Umma ya mwaka 2004.

Pili, kutokana na ukiukwaji huo, mkataba baina ya TANESCO na Richmond Development Company LLC, haukuwa halali na hauna nguvu kisheria.

Tatu, hata kama mkataba husika ungekuwa halali, uhamishaji (assignment) wa mkataba huo kutoka RDEVCO badala ya Richmond Development Company LLC kwenda Dowans Holdings S.A. na hatimaye Dowans Tanzania Limited, haukuwa halali.

Yatokanayo na kauli ya Waziri Mkuu

Maelezo hayo ya Waziri Mkuu yanaibua mengi. Kwanza, uamuzi wa kuvunja mkataba haukuwa wa kisiasa.

Si uamuzi uliotokana na shinikizo la kisiasa kama inavyopotoshwa bali ni uamuzi uliojengwa au kufikiwa kutokana na ushauri wa kisheria. Kwa mujibu wa Pinda, ni ushauri kutoka kwa wanasheria wabobeaji.

Pili, kwa kupambanisha hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Kibiashara ya Usuluhishi na maelezo ya Waziri Mkuu hasa katika kuipa sifa za ‘kutukuka’ Rex-Attorneys, tunajikuta tukilazimika kuhoji suala moja kati ya mawili au yote mawili na kimsingi tukawa na haki ya kuanza kupuuza upande mmoja kama si pande zote.

Masuala hayo mawili ni pamoja na umakini wa serikali (Waziri Mkuu) hasa kutokana na kuinadi kampuni ya Rex-Attorneys au tuhoji uwezo wa Rex Attorneys.

Hapa izingatiwe ile kauli kuwa serikali “ina mkono mrefu” kama ingeweza kutafiti kwa umakini kama kweli hakuna maslahi binafsi yaliyopiganiwa ili kupiga kumbo maslahi ya nchi.

TANESCO imetakiwa sasa kuilipa Dowans mabilioni kwa kuvunja mkataba na kukataa kulipia huduma za kampuni hiyo kwa TANESCO katika kipindi cha mkataba.

Hukumu hii inatoka katika wakati ambao ushauri wa Rex-Attorneys (wazoefu wa mikataba ya kimataifa) ukiwa katika makabati ya TANESCO.

Fedha zimetumika kununua huduma ya ushauri wa kisheria kutoka Rex-Attorneys. Kampuni hiyo bila shaka, imelipwa mamilioni (kodi za wananchi). Bila shaka, katika kupima thamani ya matumizi ya fedha (value for money) malipo kwa Rex Attorneys ni kashfa.

Na kwa maana hiyo, hasara kwa taifa si tu malipo yatakayofanywa kwa Dowans bali hata kwa kampuni iliyotoa ushauri ‘tasa’ wa kisheria.

Ushauri kwa mbunge yeyote makini

Kwa mbunge yeyote makini, ambaye anaweza kujitambua yupo kundi gani la watu kwa mujibu wa mtazamo wa Tully, anaweza kuhoji haya na mengine bungeni.

Ashinikize kuchunguzwa pia kwa Rex Attorneys ambayo ushauri wake umegeuka gharama kwa Taifa. Je, kampuni hii ilitoa ushauri usiongiliwa na maslahi ya pamoja kati ya wamiliki wa Dowans na kampuni husika?

Lakini pia ashinikize uchunguzi wa uhusiano kati ya kampuni hii na viongozi wa serikali, ikiwamo ofisi ya Waziri Mkuu iliyoipamba kampuni hiyo bungeni.

Ikumbukwe, kwa mara nyingine kampuni hii imefuatwa tena baada ya hukumu ya ICC ili kushauri kama Dowans ilipwe au la. Wameshauri ilipwe.

Ni kama vile kampuni hiyo mwanzo ilitoa ushauri wenye malengo ya kuandaa mazingira ya Dowans kushinda kesi na kulipwa.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari wiki iliyopita, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema; “Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO ilishauriwa na kampuni ya Rex Attorneys Advocates kukubaliana na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Usuluhishi bila kuipinga endapo itasajiliwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania.”

Hapa, Rex Attorneys ndiyo iliyosifiwa na Waziri Mkuu bungeni, ikatoa ushauri wa kuvunja mkataba. Baada ya kuvunja mkataba, TANESCO ‘imehukumiwa’ kulipa mabilioni.

Lakini baada ya hukumu kutoka, TANESCO imerudi kwa kampuni iliyotoa ushauri wa kuvunja mkataba, kampuni hiyo inashauri tena TANESCO ifanye malipo?!

Je, vigezo vya awali vya Rex Attorneys kushauri mkataba uvunjwe vimepotelea wapi hadi wakimbilie kushauri TANESCO ifanye malipo? Je, kuna uhusiano gani au kunaweza kuibuka uhusiano gani kati ya mabilioni itakayolipwa Dowans na kampuni hii ya kisheria? Je, kuna mgawo wa malipo hayo baadaye?

Kwa nini kampuni iliyoshauri kwa vigezo vya kisheria mkataba uvunjwe, baadaye igeuke ikipuuza vigezo hivyo na kutoa ushauri mpya wa kulipa mabilioni? Kwa mbunge makini bila shaka hapa kuna jambo la kuhoji.

Serikali kupitia TANESCO imevunja mkataba kwa ushauri wa kampuni hii, leo inakwenda kulipa faini kwa ushauri pia wa kampuni hii, je, kuna nini?

Katika mjadala uliopita niliandika kuhusu Katiba mpya na diplomasia ijayo, nikinukuu sehemu ya maneno ya Mwalimu Nyerere kutoka gazeti la The Nationalist, la Mei 22, 1967 ambalo pia lilinakili habari ya gazeti la Sunday Times, Afrika Kusini. Haikuwa sahihi kusema Nyerere alikuwa ziarani Afrika Kusini, bali alifanya mahojiano tu na Sunday Times. Naomba radhi kwa wasomaji.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

Simu: 0787-643151​

source:Rex Attorneys ni kashfa kubwa zaidi ya Dowans
 
Big up mkuu umeichambua vizuri, tatizo la viongozi wa tz ni kwamba wanajua hata wakifanya makusudi kutuingiza ktk mikataba inayowafaidisha wao, at the end of the day hakuna atayewa jibishwa! Ni utamaduni ambao haufai, wale wote wanaokutwa na kashfa kwa kuthibitishwa au kwa kukisiwa wanatakiwa wastaafishwe kwa manufaa ya umma simple as that.

Kuna belief imewaingia hawa viongozi wetu kuwa bila wao nchi haiendi, wakati ni kinyume nchi ingeenda mbali kimaendeleo bila wao, kama unajikuta miaka mingi inazidi kwenda na hauna maendeleo unachotakiwa kufanya ni complete change, inatakiwa sisi tubadilike kwa kuwashinikiza wawajibishwe maana wenyewe hawawezi ku step down wala mkwere hawezi kumstaafisha mtu yeye mfumo wake ni status quo.
 
Vipi wanaJF JK bado yuko mapumziko ya mwisho wa mwaka? Jana nimemtuma kijana kununua gesi ya kilo 15, karudi bila gesi anasema gesi imepanda na inauzwa kwa Tsh. 75,000. Wakati miezi 2 tu iliyopita gesi ilikuwa Tsh. 30,000. Na umeme ndo huoooo bei juu!

Kweli Maisha Bora kwa kila mtanzania ndo haya?
 
Dr Eve Hawa Sinare is a partner of Rex Attorneys, one of the largest corporate law firms in Tanzania. She heads the firm's banking and financial services department. For more than 12 years she has represented some of the largest local, regional and international banks and financial institutions in projects or corporate syndicated lending in Tanzania in telecommunications, gas, oil, energy, industry, mining, manufacturing, coal mining and agriculture sectors, among others.

Prior to practising she was senior government adviser for privitisation of public corporations, and before that she was director of legal and institutional affairs of the Common Market for Eastern and Southern Africa, and before that Dr Eve was an assistant lecturer at the University of Dar es Salaam.

She is a frequent speaker at legal and business conferences, such as the annual conference of financial institutions in Tanzania (attended by representatives from all the banks and financial institutions in Tanzania) and at the annual general meeting of the World Services Group (held in Costa Rica and focused on risk management in project finance), a worldwide network of firms in all continents.

She is also an author of numerous articles on legal topics. A graduate of the University of Dar es Salaam (LLB and LLM) and the University of Konstanz, Germany (LLD in international economic law – trade and finance), she is a member of the East African Law Society, the Tanganyika Law Society and the Tanzania Women Lawyers Association.

Dr Sinare is a member of the board of the Capital Markets and Securities Authority; a vice chairperson of the Tanzania Tourist Board; a vice chairperson of the advisory board of A/C BEST, working for a better business environment; a member of the lands working group of the National Business Council; a member of the lands working group of the National Business Council; a commissioner at the joint Finance Commission (a constitutional board for the union of Tanzanian government finance issues); a member (until 2006) of the board of Stanbic Bank Tanzania Limited, one of the banks owned by the Standard Bank of South Africa; a member of an ad hoc task force set up by the BOT to advise on a study concerning the facilitation of mortgage finance in Tanzania; a member of the Board of Mkombozi Commercial Bank; a member of the Board of the Tanzania Investment Centre; and as a commissioner, part of six-person team appointed by the president of Tanzania to review the privatisation and private-sector participation in utilities and infrastructure.
 
hii mkala uilikuwa mwana halisi la jana........imetulia sana
huwa nafika mahali nasema hivi tuna waziri mkuu kivuri........pinda amepinda ni hovyo kuliko
 
Hivi Dilunga unatukumbusha kwamba hasara hii yote kwa walipa kodi te yumo jumla jumla hivi 'Mtoto wa Mkulima' naye??? Basi dunia imekwisha!!!!!!!!!!!!!!!
 
vipi wanajf jk bado yuko mapumziko ya mwisho wa mwaka? Jana nimemtuma kijana kununua gesi ya kilo 15, karudi bila gesi anasema gesi imepanda na inauzwa kwa tsh. 75,000. Wakati miezi 2 tu iliyopita gesi ilikuwa tsh. 30,000. Na umeme ndo huoooo bei juu!

Kweli maisha bora kwa kila mtanzania ndo haya?
tunarudi kwenye kuni tu mzee
 
Duh jamaa kafanya uchambuzi akinifu
wadau wananchi tumeachiwa nafasi yetu na wabunde pia.
 
Hivi Dilunga unatukumbusha kwamba hasara hii yote kwa walipa kodi te yumo jumla jumla hivi 'Mtoto wa Mkulima' naye??? Basi dunia imekwisha!!!!!!!!!!!!!!!

huyu pinda ni hovyo sana mkuu...... kama alikuwa anaropoka bila kujua sasa inakula kwake........ halafu yupo yupo tu hivi wadau mnaona tuna waziri mkuu nchii hii?!
 
Vipi wanaJF JK bado yuko mapumziko ya mwisho wa mwaka? Jana nimemtuma kijana kununua gesi ya kilo 15, karudi bila gesi anasema gesi imepanda na inauzwa kwa Tsh. 75,000. Wakati miezi 2 tu iliyopita gesi ilikuwa Tsh. 30,000. Na umeme ndo huoooo bei juu!

Kweli Maisha Bora kwa kila mtanzania ndo haya?

wewe acha bwana unantisha? Mwezi uliopita nimenunua 44,000, haki ya nani twafa!
 
REXATTORNEYS
Legal Services

Rex House, 145 Magore Street, Upanga
P.O. Box 7495
Dar es Salaam
Tanzania

Phone: +255 22211 4291
Fax: +255 22211 2830

\
Website: REX Attorneys
Main Contacts: Hawa Eve Sinare

Alex Thomas Nguluma

Firm's Overview

REX ATTORNEYS was established on 1st February 2006 following the merger between Maajar, Rwechungura, Nguluma & Makani (Advocates) and Epitome Advocates. Both firms were already leading corporate law firms in Tanzania and have brought their experience and goodwill into the merged firm. It is most identified with mining, oil and gas; and banking and financial services

REXATTORNEYS is an integrated corporate legal business deriving its strength from a good team of partners, associate partners and other legal experts with an all round corporate law experience and from a network of law firms across Africa represented in the Lex Africa network at Home - Lex Africa: Network of Law Firms in Africa. in 28 African countries. The firm boasts of repeat clients allowing it to understand clients� corporate and labor issues better enabling it to render more practical advice to clients.

REXATTORNEYS focuses on seven key corporate areas: corporate; mining gas and oil; project finance, banking and financial services; employment; legislative and regulatory regime review; intellectual property; commercial litigation and arbitration.

Year this Office was Established: 1991
Lawyers Worldwide: 10

Languages: English, French, German and Kiswahili
Areas of Practice

Arbitration / Mediation
Banking
Capital Markets
Commercial Litigation
Conveyance
Corporate and Business
Employment
Energy
Finance
Financial Services
Foreign Investment Franchising
Gas
General Practice
Immigration
Insolvency
Intellectual Property
International Law
Labor Law
Land Use and Zoning
Leasing
Legislative & Regulatory Review and Consultantcies Mergers & Acquisitions
Mining
Natural Resources
Oil
Patents
Project Finance
Securities
Taxation
Trademarks

Partners

James S. Friedlander
Partner Christopher Giattas
Partner
George Mpeli Kilindu
Partner Mwanaidi Sinare Maajar
Partner
Tabitha Maro
Partner Lugano S. Mwandambo
Partner
Alex Thomas Nguluma
Partner Hawa Eve Sinare
Partner
Sinare Zaharan
Partner

Other

Farija Bridget Ghikas
Associate
 
Kama ulivyoyachambuwa hapo, hii inaonyesha kuwa Dowans hawana makosa, au sio?
 
Huyu Mwanaidi Majaar Senare ni yule Balozi wa Tanzania nchini Uingereza. Ni swahiba mkubwa sana wa JK, Rostam na Lowassa. Ana undugu kikabila na Lowassa. Ndiye leading partner wa Rex, yeye na mdogo wake Hawa Senare. Kampuni yao kupata kazi za serikali si jambo la kuuliza.

Wanafikiri wako smart saana, but there comes a day. A hell for them all.

Mungu wabariki maskini wa Tanzania.:Cry:
 
Rekebisho kidogo, Dr. Hawa ndie mkubwa, Mwanaidi ni mdogo mtu.

Wajameni nawaombeni sana tujiangalie tujegeuka hate preachers. Ushauri wa kisheria 'legal opinion' ni professional job na inafuata kanuni za due diligency.

Dr. Sinare amenifundisha Investment Law pale UD, na kusema kweli, she was one of my inspirational, kwanza ana utu, ndiye mwalimu pekee kati ya miaka yangu 4 ya sheria pale UD ambaye somo lake, aligharimia kila kitu kwa fedha zake za mfukoni, huu ni utu wa zida.

Alikuja kufundisha, sio ili apate mshahara, (kwa pesa gani pale Ud), bali alijitolea tuu ili ku impart vast knowledge yake kwa wengine.
Ndie aliyenifungua macho kuhusu wanasheria corporate lawyers na hawa wa litigation nadhani ndio maana mpaka leo sisi wengine tumejikuta ni wazito sana kukanyaga mahakamani, degree ya sheria imeishia kabatini, huku tunaendelea kuchezea key board newsroom!.

Hata wanasheria mabingwa, kuna wakati wanashindwa kesi, na kuna washeria wa hovyo kabisa na wanashinda kesi.

Naamini Huyu Mama ni mmoja wa wanasheria vichwa funika bovu tulionao humu nchini.
 
Vipi wanaJF JK bado yuko mapumziko ya mwisho wa mwaka? Jana nimemtuma kijana kununua gesi ya kilo 15, karudi bila gesi anasema gesi imepanda na inauzwa kwa Tsh. 75,000. Wakati miezi 2 tu iliyopita gesi ilikuwa Tsh. 30,000. Na umeme ndo huoooo bei juu!

Kweli Maisha Bora kwa kila mtanzania ndo haya?

The revolution is not an apple that falls when it is ripe. You have to make it fall [che guavara]
 
Rekebisho kidogo, Dr. Hawa ndie mkubwa, Mwanaidi ni mdogo mtu.

Wajameni nawaombeni sana tujiangalie tujegeuka hate preachers. Ushauri wa kisheria 'legal opinion' ni professional job na inafuata kanuni za due diligency.

Dr. Sinare amenifundisha Investment Law pale UD, na kusema kweli, she was one of my inspirational, kwanza ana utu, ndiye mwalimu pekee kati ya miaka yangu 4 ya sheria pale UD ambaye somo lake, aligharimia kila kitu kwa fedha zake za mfukoni, huu ni utu wa zida.

Alikuja kufundisha, sio ili apate mshahara, (kwa pesa gani pale Ud), bali alijitolea tuu ili ku impart vast knowledge yake kwa wengine.
Ndie aliyenifungua macho kuhusu wanasheria corporate lawyers na hawa wa litigation nadhani ndio maana mpaka leo sisi wengine tumejikuta ni wazito sana kukanyaga mahakamani, degree ya sheria imeishia kabatini, huku tunaendelea kuchezea key board newsroom!.

Hata wanasheria mabingwa, kuna wakati wanashindwa kesi, na kuna washeria wa hovyo kabisa na wanashinda kesi.

Naamini Huyu Mama ni mmoja wa wanasheria vichwa funika bovu tulionao humu nchini.

....Yule Professor wa sheria alikuwa Italia nae ni bingwa na kichwa pia...alinifundisha LLM sisemi wapi nisije ingilia kesi yake mahakamani
 
Partner Christopher Giattas - Ex mzumbe secondary student, son of a Morogoro SUA professor, najaribu kulink connection yake hapa, will update you soon

Partner George Mpeli Kilindu - Son of Mr Kilindu, a close friend of Lowassa

Partner Tabitha Maro - Daughter of Mama mkapas cousin, or something. (Chunguzeni hiyo sir name ya MARO)

Hawa hapo juu ni vijana waliomaliza university mwanzoni mwa miaka ya 2000, and i am not wrong, wawili hapo kama sio wote, walisomea fani hiyo nje ya nchi for starters, sina uhakika kama walijiendeleza. UKIANGALIA THEY ARE ALL CONNECTED NA EITHER LOWASS, MKAPA or KIKWETE.

SHADOW nakushukuru sana kwa uchambuzi wako wa kina, mungu akubariki daima. Hakika taifa hili linaongozwa na watu wasio na uchungu na taifa lao na waliotanguliza maslahi yao wenyewe mbele na kuwasahau wananchi wengine, wengi wao wanyonge wanaoishi maisha ya chini ya dola moja kwa siku.

Cha kufanya sasa ni kuungana na kupiga vita maovu haya yanayotokea, si kwa ku comment kwenye JF tu, bali ku act. Wabunge wetu, it is high time you start doing something kuokoa janga hili la ufisadi lililoikumba nchi yetu, otherwise, TWAFA!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom