Revised question: Kosa la Gwajima ni lipi?

Kuzuia utekaji
 
Narudia kwa mara nyingine kusema kuwa serikali na kiafrika ni za kishetani,ni serikali ambazo hazipendi kuambiwa ukweli wala kukosolewa.Tuungane na gwajima la sivyo kesho mtasikia kanisa jingine linafungiwa.wakristo tupate sauti kupinga udhalimu waliofanyiwa wenzetu.kanisa ni mali ya waumini na si gwajima.kulifungia kanisa hilo ni kuwanyima haki ya kuabudu na hilo halikubaliki.
 
Acha hizo. Gwaji boy ni kamanda wa shida
 
Maombi yana nguvu ni silaha ya hatari.uzuri ni kwamba maombi hayazuiliki kwa sheria,bunduki,cheo au kufunga kanisa
 
Sasa INAENDA fungwa akaunti yake ya U tube.
 
Maswali haya ni ya msingi na yanagusa kiini cha uhuru wa kuongea na kuabudu. Ikiwa kosa la Gwajima ni kusema ukweli juu ya utekaji na kuonesha mshikamano na wahanga kwa njia ya sala, basi tunapaswa kujiuliza kama bado tunathamini misingi ya haki, utu na maadili ya kidemokrasia.

Katika taifa linalojali haki na uhuru wa raia, kukemea maovu hakupaswi kuwa kosa. Kuwasemea walionyamazishwa si kosa. Kufanya maombi kwa ajili ya nchi ni tendo la imani, si jinai. Tunapofika mahali ambapo sauti za maombi na huruma zinaanza kuzuiwa, tunapoteza utu wetu na tunatengeneza taifa la hofu badala ya matumaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…