Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Watu bado tu wanapinga alichofanya jamaa kuwa co fair rudishen bac muda nyuma mumsaidie yule malaya kabla hayajamkuta.

Nadiliki kusema mtu pekee wa kumfananisha na KOROE ni Zabron Zabron yule wa penzi la Mfungwa jukwaa la burudani full stop...
 
Ana ushahidi nimeliwa?nakana kama sio mimi vile,hakuna anaeweza kuamini kila kitu just because jamaa kasema,naweza kuwaambia hizo msg kazitengeneza as yeye ndo hanitaki ila mimi sijawahi fanya hizo mishe!
Yan in short kwa hilo tukio personally ningekua unbreakable!ningesonga mbele afu ndo ningezidi kumuundermine jamaa as ningegundua kumbe alinipenda sana kashindwa kumove on kaona alipize
We utakuwa umeshindikana .

Uhuni tu unakusumbua

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Umesoma huu uzi wote lakini? Kwanini unasema ni chai?

Nimesoma original post ila miendelezo ya kwenye links nimekosa muda wa kusoma ,mara nyingi mtu kama anataka kueleza kitu huwa anaandika kwenye post ya kwanza,lakini kuanza jamaa naona ametoa episode kibao ndio nika conclude ni CHAI.
 
Kwa hiyo ssa tunafanyaje Anne
Inuka tumsifu Bwana na Tulitii Neno la Mungu.
Naona watu wanajaribu kunifanyia personal attacks kwa kukadiria tu! mimi naita wapiga ramli..
Nawaambia sibadili mtazamo wangu katika hili,pigeni ramli zote..Mimi sijali.
Ila neno langu ambalo ni la Mungu ndilo nitakalolisimamia.
Rum 12:19

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ufupi hii ni taarifa tu, so ushauri wako hautabadili chochote wala kuongeza chochote, vipi lakin uzima upo??

Ni hivi, mi huwa siumizwi alafu anayeniumiza akabaki salama, nikiumizwa mi nakuumiza mara 10 alafu fresh, maisha yenyewe mafupi haya, mi niwe na stress alafu wew ucheke ili kiwe nini... sipendagi ubwege kabisa, na nitabaki kwenye kumbukumbu zako milele ukijifanya kuniletea habari za ajabu..

Miez 8 iliyopita nilidate na dada mmoja hivi mrembo, height moja hivi mauzo sana na mzigo wa kuvuta huko nyuma haukuwa haba, kifupi mvuto wa yule dem hauna shaka, kama ni maksi basi A ya 95+... mapema nikamwambia mambo ya kiboya sitaki, km utacheat jitahidi nisijue, nikijua umeumia....Akajifanya hadi kulia pale kwamba ananilove nyang'anyang'a na kamwe hakuna mwanaume kama mimi, nikasema poa but take my words ukinizingua hutoamini nitakachokufany, na km hunitaki niache uende, na kama pia itakuw mechi za dharula tu alafu kimya tuambiane, moyo wangu hauchezewi.. akasema nisiwe na shaka ananipenda, nikasema poa.

Tabia yangu ni kwamba kamwe siwezi kuwa na mpenzi zaid ya mmoja kwa wakati mmoja, so nikiwa na mmoja huyo huyo. Sasa mwezi mmoja nyuma nikausoma mchezo dizain kama demu wangu analiwa hivi, sikumuuliza, nikakomaa hadi nikapata password zake facebook na insta.. nikazama inbox yake, daah ni balaa tupu, ashapigwa mashine na mshikaji mmoja hivi, then jamaa dizain kama anakomaa naye amle 0715 hiv sema demu anabana.. text yake hii hapa..

"Baby naridhika sana nawew, ila unanibania side B, nyimbo za side A zote nimeskiliza why uninyime za side B mpenz?, kama side A nilsikilza kwa elfu 70 bas side B lazma dau lipande.. nielewe bas"

Demu akajibu..

"Mi nina mtu na tuna malengo je akigundua na kuniacha itakuwaje"

Jamaa..

"Hawezi gundua, kwani huwa anakagua huko, ila navyokujua huwez nibania.. nitakutoa out ukafanye shopping ya maana, na nitakutumia 100,000 kesho"

Demu...

"Mmh poa tutaangalia tukikutana tar.22 jamaa akiondoka kama tulivyopanga".

Zipo nyingi nying but hizo kiufupi,....

Mimi kwa huyu demu..., nampa nachopata, najinyima sana apate yeye, nishamtoa shopping za maana mara kibao na tayari nishaandaa pesa nzuri tu kwa ajili yake, Krismass na mwaka mpya, maana tar.hizo sitakuwepo kutokana na majukum ya kazi yangu, nammudu kiujumla, nguo, usafiri, pesa ya kula, malazi nafanya mimi.. yeye hana chochote zaid ya gamba lake la diploma. Muda wote huo sina demu zaid yake.. na on bed naperfom fresh hadi anaomba poo yeye..

Nilichokifanya baada ya kugundua hilo, nimescreenshot charting zote hadi picha walizopiga wakiwa lodge wametumiana kupitia fb messenger nimejitumia kwenye simu yangu, then nimeuchuna.. kifupi tayari nimeshampiga chini ila siwez kumwambia tuachane kiboya boya hiv bila yeye kuonja joto la jiwe kidogo, na kamwe sitafanya naye mapenz tena.. ambacho kimebaki kwake ni kumpa kidonda cha milele..

Ifahamike ananipenda japo tamaa anazo, ashanitambulisha kwa rafiki zake wote, dada yake, hadi mama yake.. kifupi anaitwa mrs mimi... na uchafu anaoufanya ni siri kubwa sana na ndo maana anatumia fb messenger maana anajua siwez hisi chochote huko.. tayari tarehe ya kupeleka barua ishapangwa, tarehe 07 jan... mashangazi zake wote wanajiandaa kwa tukio hilo.. upande wetu pia tunajiandaa..

Nataka nifanye nini?? Siku hiyo ya tukio la kwenda kwao kujitambulisha rasmi ndo siku yangu ya kumuumiza, maana kwao anaaminika sana, anaimba kwaya kanisan, ana vyeo vingi ving vya huko kanisani.. na huwezi mzania hata kidogo kama ni mshenzi.. siku hiyo mbele ya Mchungaji wake, ndugu zake, mama ake, mashangazi na marafiki zake wakiwa na smartphone zao naenda umiza mtu vibaya sana, sio kwamba nitampiga hapana, ila nataka nimafanyie tukio ambalo litaweka maumivu ya kudumu kwenye moyo wake na kamwe hatokuja nisahau..

Tarehe 7 january, save the date....

USIPOTEZE MUDA KUNISHAURI CHOCHOTE, HUWA NIKIPANGA SIPANGUI..
========

UPDATE: Mrejesho tayari fuatilia

Kufuatilia mrejesho wa tukio hili bonyeza link hapo chini

Mrejesho: Sehemu ya kwanza
Mrejesho: Sehemu ya pili

Mrejesho: Sehemu ya tatu
Mrejesho: Sehemu ya nne

Mrejesho: Sehemu ya tano
Mrejesho: Sehemu ya sita

Mrejesho: Sehemu ya saba
Mwisho
Fanya tu kwa wengine ila ukifanya kwa dada yangu kumbuka kwenda na maji
 
Kumbe hii stori ilikuja endelea na kufika tamati...

Kongole sana kwako KOROE , kitendo cha kurudi na kuleta mrejesho baada ya miaka kadhaa ni cha kiungwana...

Hongera pia kwa sababu wewe ni mwandishi wa maisha yako, ni shuhuda wa matendo yako na mwamuzi wa hatma yako.
 
Hongera kwa msimamo! Forgiveness is for the weak!!! Ni either revenge au kupotezea( ghosting, cutting off). Naona wengine bado wameshikilia mafundisho yao ya sunday school hahaahaaa

Hiyo kupotezea ndio kusamehe yenyewe mkuu...

Hata kwa Mungu, ukimzingua huwa anakupotezea (anakusamehe lakini anakushusha vyeo faster)
 
Back
Top Bottom