Revealed: Tanzanian Thieves have Sh315bn in Swiss Banks!

Hii habari jana nilipoisoma the citizen...I was just wondering...the world has started coming to its sense. Hawa wazee wa vijisent wanaona wamejificha kweli wakitubia. Ipo siku dunia yote itajua nini kinaendelea
 
La hasha, unajuwa sana kuwa hakuna awamu inayoshughulikia ubadhirifu kama hii, wako waliozipeleka, wengi sana. Nakuhakikishia ukija kuwakuta na vigogo wa chadema wamo usione ajabu. Wizi walikuwepo na wapo wengi sana tu, mwizi hana chama wala alama usoni kuwa huyu ni mwizi.

Cha kusikitisha ni kuwa, kabla ya Kikwete hatujaona wakishughulikiwa ipasavyo, ni awamu hii tunaona kuna kesi zaidi ya 1,000 za rushwa Tanzania nzima (haijawahi kutokea kwa awamu zote) na bado zinakuja. Na sasa hivi tutaona wimbi lingine la kesi za Wilayani, Mashirika ya umma na ma wizara, kwani CAG sasa imeanza kufanyishwa kazi inavyotakikana. Ni mwanzo mzuri sana na matokeo tunayaona.

Duh.. Wanikumbusha title ya novel moja ya James Hadley Chase "believe this.. you'll believe anything"..
 
Wanachukua hela kwa ajili ya uchaguzi wa 2015............hamna cha kushangaza hapo kama wizara imetenga mabilioni ya shilingi kwa ajili ya mafunzo wakati hawajishughulishi na utengenezaji wa kitu chochote unategemea nini.
Tukisema rais dhaifu mnachukia
 
Na bado watu wetu hawana hasira!!! watakuja watu kujaribu kuhalalisha kwanini kufanya hivyo ni "modern banking" na kama mtu "ana fedha zake kwanini asiweke huko Uswisi"...

Hawaishi kusema hiyo ni "pensheni na marupurupu ya ubunge! ... " Nachelea kusema kwamba, TAKUKURU et al ni legelege....Kama kuna kampuni lolote ambalo limeorodheshwa kwenye masoko ya hisa , Marekani ni muda muhafaka kuyachongea kwa Dept of Justice - Marekani kwa kutoa hongo kwa watanzania hao 6. Sheria ya marekani ninayooiongelea hapa ni hii hapa:
fcpa-bar.jpg

An Overview
The Foreign Corrupt Practices Act of 1977, as amended, 15 U.S.C. §§ 78dd-1, et seq. ("FCPA")

Shadow.
 
KITENGO cha Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kinachunguza Sh303.7 bilioni ambazo zinadaiwa kukutwa kwenye akaunti sita za Watanzania, wakiwamo wanasiasa, katika benki mbalimbali nchini Uswisi.

Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya Interpol kilichonukuliwa na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen, kimesema baadhi ya wanasiasa nchini na watu wengine ndiyo wanahusika na ufisadi huo kwa kuwa na akaunti zenye fedha nyingi nchini Uswisi.
Fedha hizo zimeelezwa ziliingizwa katika akaunti hizo na kampuni za uchimbaji mafuta na kampuni za uchimbaji madini, ambazo zinafanya kazi Tanzania.

Chanzo hicho kiliongeza kwamba fedha hizo zipo katika akaunti sita tofauti, zinazomilikiwa na Watanzania wakiwamo wanasiasa.

Kiasi hicho cha fedha kilichofichwa Uswisi, kinatosha kuendesha Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa miaka mitano, au kusaidia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kuendesha shughuli zake kwa miaka miwili.

Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi moja.

"Wenzetu wa Uswisi wameeleza fedha hizo zimeingizwa na kampuni kadhaa ambazo zinahusika na mafuta pamoja na madini hapa nchini," kilidokeza chanzo hicho.

Mabilioni hayo yamebainika kufichwa wakati takwimu zilizotolewa na Umoja wa Taasisi za Kupambana na Rushwa barani Afrika ikiwamo Tanzania, zikionyesha kwamba Sh22 trilioni, zimekuwa zikitoroshwa nchini humo na kufichwa katika nchi za kigeni, ikiwamo Uswisi.

Fedha hizo zimebainishwa na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB), iliyotolewa hivi karibuni, ikibainisha nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania, na kiwango cha fedha zake zilizohifadhiwa huko.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) hivi sasa inafuatilia suala hilo kwa mamlaka za Uswisi, ili kujua fedha hizo ziliko na nani anazimiliki.

Mbali ya Tanzania, nchi nyingine ambazo zina fedha nyingi katika benki za Uswisi ni Kenya (dola 857 milioni), Uganda (dola 159 milioni), Rwanda (dola 29.7 milioni) na Burundi dola 16.7 milioni.
Jumla ya fedha zilizoko katika benki za Uswisi kutoka nchi hizo nyingine za Afrika ni Faranga 1.53 trilioni za nchi hiyo na ripoti hiyo imeelezwa kuwa kuna msukumo wa kimataifa wa kuitaka nchi hiyo izitake benki zake, kubadilishana taarifa za wateja na serikali za kigeni.

Ripoti hiyo imekuja wakati pia Uswisi ikiwa na rekodi ya kuhifadhi mabilioni ya dola kutoka nchi za kigeni ikiwamo Afrika, kwani iliwahi pia kuhifadhi dola zaidi ya bilioni 1.5 za aliyekuwa Kiongozi wa Kijeshi wa Nigeria, Jenerali Sani Abacha na dikteta Mobutu Seseseko wa iliyokuwa Zaire.

Gavana azungumza
Akizungumzia ripoti hiyo, Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Beno Ndulu (pichani) alisema uamuzi huo wa Uswisi wa kuanza kufungua milango utaiwezesha BoT kuwa na rekodi ya kiasi halali cha fedha zilizopo katika nchi hiyo.

Profesa Ndulu alifafanua kwamba katika siku za nyuma, Uswisi haikuwa imefungua milango kwa kutaja kiasi cha fedha za wateja wake walioweka fedha katika benki zake, hivyo ilikuwa vigumu kwa mamlaka za ndani kuweza kufanya uchunguzi.

"Ndiyo kwanza wameanza kufungua milango, sisi siku zote tulikuwa hatuwezi kujua nini kinaendelea. Lakini, angalau sasa tutaweza kujua na kuwa na rekodi baada ya uamuzi huo wa kufichua kiasi cha fedha kilichomo katika benki zake," alifafanua gavana.
Kiutaratibu, BoT inapaswa kuwa na rekodi ya fedha halali za Watanzania zilizopo nje ya nchi.

Kauli ya Takukuru
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alikaririwa na The Citizen hivi karibuni alisema kuwa ofisi yake ina taarifa kuhusu suala hilo na kwamba wanaanza mawasiliano na Serikali ya Uswisi kujua ukweli wake.

Dk Hoseah alisema taasisi hiyo inataka kujua jinsi gani fedha hizo ziliwekwa kwenye benki za Uswisi, watu waliohusika na namna uhamishaji wa fedha hizo ulivyofanyika.

"Tutakapogundua fedha hizo zimetoka wapi, tutafuata taratibu zinazohusika kuhakikisha zinarudi nchini," alisema Dk Hoseah na kuongeza: "Tutatumia sheria zilizopo katika nchi hizi."

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba hakutaka kuzungumzia suala hilo akieleza kuwa yuko likizo, hivyo aulizwe msemaji wa Jeshi la Polisi.
Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso alisema hawajapata ripoti hiyo na kwamba atawaomba watu wa uchunguzi kumpatia, ili aweze kutoa taarifa.

 
Nchi ichukue hatua bac..hivi usalama wa wataifa unatusaidia nini..kama hela nyingi hivyo zinapotea usalama wa taifa ni fedha zote zinazotengwa bila kuhojiwa matumizi yake wantusaidia nini? kwa nini kashfa hizi wasihusishwe nazo pia?kwamaba hawana msaada kwa nchi?
 
unamaanisha nini hapa?au wewe nae ni mmoja wa hawa wezi?wewe kuwa airforce kwako kutatusaidia nini sisi masikini wa TANZANIA?Jaribu Tena baadae!!!!!!!!!!!!!!

The Most High God,the leader of this constellation in which we live in,that is his name,The Most High;he chooses the leaders of every country. If one leader does not serve his people well,he replaces him with another leader.
The Most High leads a government composed of 12 Most Highs. That is his government,it is the government of the constellation.
There is also the parliament of the constellation,which has three chambers. The Lower House,which has a 1000 evolutionary ascending creatures[humans];a midchamber consisting of 100 seraphim, an upper house ,a house of peers,consisting of 10 members,high sons of the universe,and there is the combined house of legislators composed of varying proprtions of these three chambers,theis combined house of legislators is led by the juniour most high.
The Most High is the leader of the costellation,he has two assistants,the senoir most high[who deals with spiritual matters],and the juniour most high.[who deals with matters of material development] It is the juniour most high who leads the combined house of legislators,just like Jpe Biden leads the Senate.
All the laws of a universe proceed for the constellation. Then there is the Court of the most High. The Universe is led by this same syatem of executive,legislature,and Courts.
But I would like to stop here,because I am sure you are now most anxious to recomment to a good mental hospital.
 
The Government can Claim the Money if the person who Deposited does not have a legit Business that's what happened

to Ibrahim Babangida, all those Nigerian Senator's who stole OIL Money, Shehu Shagari etc; In Swiss Bank if you do

not have a valid Transactions or you cannot name any of your business investment then they can withheld your

Bank Account and contact your Home Country; That's why it is very inashangaza kwanini yule Mhindi wa EPA aliyekimbia

Serikali haijaomba pesa zake zizuiliwe; ina Maana Serikali pia imecheza Mchezo Mchafu.

Serikali Dhaifu haiwezi kutia neno. Cha kushangaza Msanii DHAIFU alias muhesabu tofali hajatoa kauli yoyote kuhusu pesa hizi na sitashangaa kama ataendelea kuwa kimya kuhusu pesa hizi chungu nzima. Kuhusu pesa za yule mhindi mwizi wa EPA nazo inabidi Serikali ishinikizwe ili zirudishwe na kama kanunua majumba katika nchi yoyote duniani basi nyumba hizo ziuzwe na pesa zitakazopatikana zirudishwe Tanzania
 
Hizo zipo njiani kurudishwa. Wala usiwe na shaka na kazi zimeshaanza kufanywa kupitia sheria za Umoja wa Mataifa.

zomba, kama zimeanzwa kurudishwa lazima kutatokea misiba ya hapa na pale na tusisahau waafrika mila zetu hatuwezi kumuacha mtu alie mwenyewe. Tukaribishane tuwe tunalia wote.
On the other hand, I believe move ya aina hii itampa image nzuri JK kama itatekelezwa na hela kupelekwa kwenye ujenzi wa Taifa.
 
Last edited by a moderator:
The anti-graft czar further said, “People should stop laundering money to Swiss banks because they are no longer a safe haven as they used to be in the past.Things have changed so much that in today’s world, no matter how long it might take, in the end all the culprits would be known and arrested.”
Mimi sijamuelewa vizuri huyu Mkurugenzi wa PCCB ina maana waende kuweka hizo pesa kwenye bank nyingine kwa sababu Waswiss wameacha kulinda pesa za ufisadi

Kama hujamuelewa hilo ni tatizo la NECTA kuwapasisha tu shule bila kuwa na uwezo.
 
Usimsahau pia mpangaji wetu pale Magogoni.

As the hauling gets longer day by day, we learn more about the really people who benefit from these poor contracts we sign with mineral and oil&gas exploration companies.
Time heals everything Jasusi
 
Last edited by a moderator:
Wasiwasi wangu ni kuwa tunadhani kila mwenye pesa nje ya nchi ni mwizi/fisadi. Taarifa za watu wenye akaunti nje haimaanishi wote ni wezi. Si vema kushabikia halafu kesho tukakosa wa kumshtaki, kwanza tunajua wapi tulipoibiwa? Nyumbani kwako ukikuta pameibiwa utajua, ila sio umesikia nje ya nyumba yako kakamatwa mtu ana rundo la pesa basi unakuja juu na kusema "nimeibiwa". Ila hatua hii ya Uswisi ni jambo la kutia matumaini.
 
Kitu mnachoshindwa kuelewa kwenye hiyo report ni kuwa hizo habari wamezitowa Interpol ya Tanzania, hii ina maanisha kwamba Serikali inafanya kazi katika hili suala hili halijaibuka tu lenyewe, kwani Iterpol hufanya kazi zake kwa kuombwa na nchi husika na nchi husika hapa ni Tanzania:


The International Police Organisation (Interpol) in Dar es Salaam has said some local political bigwigs are behind the stashing of colossal amounts of money in Swiss banks, The Citizen can reveal today
 
Some corrupt Tanzanians, including prominent business tycoons and some top government officials, have secretly stashed away a whopping Sh315.5 billion ($196.87 million) in Swiss banks, The Guardian has learnt.

The amount is a quarter of the amount Kenya’s tycoons and politicians have secretly stashed away in Swiss banks.

According to a report released by the Swiss central bank, Swiss National Bank, early this week Tanzania is among eleven African countries whose nationals have secretly stashed away millions of dollars in the country’s banks.

This is the first time the Swiss central bank has released financial details on various culprits who have stolen billions of dollars from Africa - an indication that gone are the days when African thieves enjoyed strong protection of their looted billions by Swiss banks and authorities.

The report further shows that Kenya is the leading offender in East Africa in terms of the amount of money that has been stashed away in Swiss banks. According to the report, a staggering Ksh72 (Tsh1.296 trillion) is in the country’s banks.

The report shows further that other countries whose nationals have stashed stolen wealth in Switzerland, in billions of Swiss francs, include Uganda (154m), Egypt (798m), South Africa (795m) and Seychelles (2.515bn), Zimbabwe (96m), Senegal (150m), Rwanda (29m), Sierra Leone (29m), Somalia (1m) and Sudan (179m).

One Swiss franc is equivalent to Sh1,900, according to current exchange rates in the domestic financial market.

“The total overseas funds in Switzerland’s banking system stood at 1.53 trillion Swiss francs,” the report adds.

For the past one decade global pressure has been mounting on Switzerland to ask its banks to share information about their clients with foreign governments.

Reacting to the report by the Swiss central bank yesterday, director general of the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) Dr Edward Hosea (pictured) said, “ We are going to write to the Swiss authorities on Monday (next week) to demand a copy of the report.”

“We want to know the names of those who have secretly stashed billions of shillings in Swiss banks…we promise to recover the stolen billions once we have the list,” the PCCB chief told The Guardian over the phone.

The anti-graft czar further said, “People should stop laundering money to Swiss banks because they are no longer a safe haven as they used to be in the past.

Things have changed so much that in today’s world, no matter how long it might take, in the end all the culprits would be known and arrested.”

Early this week Dr Hosea, who is also chairman of the African Union’s Advisory Board on Anti-corruption (AU-ABC), expressed dismay over the continuing ‘rampant corruption’ in the continent, blaming some leaders for abusing their offices and condoning the malpractice.

Dr Hoseah made the remarks in Arusha when addressing the board’s members who are preparing its annual report to be presented to the AU summit scheduled to take place in Addis Ababa, Ethiopia, next month.

He said Africa has been losing billions of dollars annually through corruption, adding: “On a yearly basis Africa loses more than USD148 billion due to the practice, and the perpetrators of corruption are taking the money from the continent to banks based in the developed world.”

Citing an African Development Bank’s (AfDB) recent report, Dr Hosea said: “It is estimated that 50 percent of tax revenues and USD30 billion in aid for Africa ended up in corruption. Today the scenario has not changed, as some African leaders have become thieves in government offices while petty corruption continues to ravage the continent.”

Between 2001 and 2008 Tanzania lost an estimated $1 billion (Sh1.6 trillion) due to corrupt deals masterminded jointly between corrupt tycoons and some top government officials. Among the scandals that cost the nation dearly were the Bank of Tanzania’s Twin Towers project, looting of the External Payments Arrears (EPA) account, Meremeta gold scandal, Deep Green Finance Ltd, British Aerospace Engineering (BAE) Systems and the controversial radar deal.

Mimi hawa nawaona siyo threat sana kwangu ukilinganisha na mtu ambaye anataka kunidhulumu laki tatu yangu ambayo nilikuwa nimepanga nimtumie mama mzazi anunu e chakula wadogo zangu karibia wanaklufa na njaa huko kijijini. Huyu nayetaka kudhulumu hela yangu, assuming kweli akiidhulumu, na hao wanaotuhumiwa kuchota hayo mabilluion, nani ni threat zaidi kwangu? Siyo kwamba najiona mbinafsi, hapana. Halafu, assuming huyu anayetaka kunidhulumu, angepata na yeye chance ya kuchota hayo mabillion, unadhani angechota mangapi, kiasi gani? Pengine angeweza kuwazidi hata hao wote waliotajwa hapo juu, .... sitetei lakini!
 
Kua na mtu mwenye PhD kama Hosea ni ualakini wa uteuzi na uwajibikaji wa aliemteua, kumbuka matukio ya Rushwa kubwa kubwa ambazo hata leo uchunguzi unaendelea
 
Kitu mnachoshindwa kuelewa kwenye hiyo report ni kuwa hizo habari wamezitowa Interpol ya Tanzania, hii ina maanisha kwamba Serikali inafanya kazi katika hili suala hili halijaibuka tu lenyewe, kwani Iterpol hufanya kazi zake kwa kuombwa na nchi husika na nchi husika hapa ni Tanzania:



Zomba,
Usipotoshe. Chanzo cha hizi habari ni Interpol nje ya nchi. Tanzania ni tawi tu la Interpol. Kwa hiyo hizi habari zimetolewa Switzerland. Chanzo chake kingekuwa ni Tanzania, au serikali yetu, Hosea ndiye angetoa hiyo statement. Lakini Interpol Tanzania ni tawi tu la International Police Organization. Watanzania tumekuwa kama reactive tu. Hata zile hela za Chenge, chanzo chake hakikuwa Takukuru, chanzo chake kilikuwa ni nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom