Rev. Mtikila Confirms Hosting FDLR Commanders in Dar es Salaam


hahahaha...great-thinker!!!! more like a great-stinker.
 
UN nao wanacheza mziki tu wa mataifa makubwa...hawana meno kazi kutii amri ya mataifa makubwa
 
Hata mimi sasa nimeanza kuwa na question motive za waleta thread kuhusu Rwanda na Tz...isije kuwa kuna watu wako kazini...

Japo kuna uhuru wa habari....ningekuwa mod ningekuwa na block hizi thread...naona kuna agenda imejificha.

Mutuwache na amani yetu wa Tz.

Japo wengine tunachangia kama wazalendo ku defend nchi yetu...lakini ukichunguza nyingi ni za ku victimize Tz...meaning zinaanzishwa na pro Rwanda



 
tunalalama sana lakini tukumbuke kuwa strength ya inteligence yoyote ile inategemea sana credibility ya wanaorun system... corruption ndio number one killer wa good intelligence sasa kwahilo jamaa kwa kiasi kikubwa (PK) amefanikiwa kusimamia...

maybe we need to do a self assessment kama tuko njema na intact
 

ni kweli kabisa na hasa ukichunguza vizuri posts za waleta mada na historia zao za uchangiaji katika jamvi hili utaona kabisa ni wahamiaji haramu, watusi au watanzania wenye asili ya Rwanda wasio na uzalendo hata chembe na TANZANIA yetu! stuka.
 
Hapo wanaaza kumchafua mchungaji ashindwe kutetea hoja ya serikali tatu na Tanganyika ndo mambo ya kuzushiwa kesi kama akina l
Jilwakatale hapo hakuna jipya si wagemkamata wakati ule huyo jamaa akaa kwake acheni kuchezea akili zetu bhana
 
Hawa WATUTSI kama walijua mchungaji C Mtikila anahifadhi makamanda wa FDRL kwa nini hawakulisema hilo mapema kabla huyu afande hajapotea????.Hawa watu wana lao jambo.Inavyoelekea hawa watu watakuja watufanyie SUPRISE Kama mzaha vile!!!!..
 
mambo mengine humu huwa yanachekesha sana, inawezekana pastor kakutana na wapigaji wa dhahabu na almasi , toka kongo na uganda wakajifanya waasi, wapo kibao wanatapeli wazungu kwa dhahabu feki kwa kujifanya ni rebels..funny..
 


Ufafanuzi. Hii habari niliikuta allafrica.com ambao walisema wameitoa News of Rwanda. Nikatafuta News of Rwanda na kuikuta hiyo habari. Hata hivyo, News of Rwanda haikuwa primary source ya hiyo habari kwa sababu nao wenyewe wamesema kuwa wameitoa kwenye ripoti ya Wataalam wa Umoja wa Mataifa nchini Congo iliyochapishwa mwezi uliopita.

So, I had to find the actual report ya hao wataalam na kuisoma na kukuta kwamba actually News of Rwanda wamekopi sehemu ya hiyo report ku-justify habari ambazo wamekuwa wakiandika huko nyumba kuhusuana na suala hili. Kwa hiyo, the primary source ya hii habari siyo News of Rwanda, bali ni ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa nchini Congo iliyowasilishwa na kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Tutofautishe kati ya primary source and secondary source.

Nilijua haya yatajitokoza na ndiyo maana niliweka mpaka link ya inapopatikana hiyo ripoti kwa ajili ya wale ambao siyo wavivu wa kusoma ripoti ndefu. Hata hivyo, wapo ambao wamedai kuwa kuwa link yenye hiyo ripoti haifunguki. Inawezekana kwa sababu ni ripoti ndefu kidogo ( ni PDF file lenye ukubwa wa zaidi ya 22MB), maana hata mimi ilinibidi nikatafute kinywaji kwanza wakati nikisubiri ripoti ifunguke.

For the avoidance of any double, badala ya kutoa link tuu, nime-download hiyo ripoti na kui-attach hapo chini. I hope sasa itafunguka. Riporti ina jumla ya kurasa 277. Kama ni mvivu wa kusoma au huna muda wa kuisoma ripoti nzima, nenda moja kwa moja kwenye ukurasa wa 27 hadi 28 (paragraphs 109 -110) na utaikuta hiyo habari kama ilivyonakiliwa na News of Rwanda.

Kuhusina na hiyo picha ya nyumba ya Mchungaji Mtikila pia News of Rwanda wameinakili kutoka kwenye hiyo ripoti. Picha inapatikana kwenye annex 42 iliyoko kwenye ukurasa wa 134 wa hiyo ripoti.

Kuna suala ambalo nilitegemea wachangiaji wangehoji lakini so far hakuna hata mmoja amefanya hivyo. Sijui kama ni usahaulifu au ni ignorance. Kama mtakumbuka hawa wataalam wa Umoja wa Mataifa walishawahi kutoa ripoti nyingine iliyoishutumu Rwanda kujihusisha na mgogoro huko DRC. Katika speech yake moja (ipo Yutube), Rais Kagame aliiwakandia sana hao wanaojiita "experts on the ground" na kuhoji wako accountable kwa akina nani. Kimsingi, aliitupilia mbali ile ripoti na experts wenyewe because they lacked accountability.

Lakini katika ripoti hii, inaonekena Rwanda wanakubaliana moja kwa moja baadhi ya findings za "experts" wale wale ambao Kagame aliwakandia na kuhoji uhalali na utaalam wao. How come ghafla, wamekubaliana na findings za hao "experts on the ground"? Ina maana sasa accountability ya hawa experts imebadilika tokea watoe ile ripoti ya awali?

Kwa upande mwingine, kabla ya shambulio la kigaidi la Westgate, kuna group la wataalam wengine wa Umoja wa Mataifa nafikiri on the Horn of Africa walitoa ripoti ndefu iliyokuwa na taarifa kuhusina uwezekano shambulio la kigaidi maeneo ya Afrika Mashariki. Katika ripoti hiyo, watalaamu hao walifanikiwa kuwahoji baadhi ya wapinganaji wa Al-Shabaab. Hata hivyo, inaonekana hapa Afrika Mashariki hakuna aliyehangaika na hizo findings za hiyo ripoti na shambulio la kigaidi Westgate lilitokea miezi michache tuu baada ya ripoti hiyo kuchapishwa.
 

Attachments


kwa nini usingeweka hiyo report tu bila kuhusisha news of Rwanda, tena kinyemela? this is suspect by any standards. News of Rwanda limekuwa likichochea uhasama baina ya nchi zetu kwa muda sasa, any news from them hata kama ziko based on any report haziaminiki, lazima watakuwa wamechambua mambo wanavyotaka wao. Anyway thanks for the report.
 
@'jmali', kweli wewe kiboko aisee. Thanks sana.
 

Niliweka link ya ripoti sijui ni wewe ulidai haifunguki. Mara ya kwanza nilipoisoma hiyo habari kwenye News of Rwanda nilidhani ni propaganda zile zile.

Hata hivyo, waliweka source ya walipoipata hiyo habari and I had find the actual source kujua kama ni kweli au wamefanya spin.

Nilijua kama niweka tuu habari kutoka News of Rwanda wengi wenu mngedai ni zile zile propaganda na wengi wenu mngeanza kunibadilishia uraia.

Maana you guys never stop to amaze me. Kwenye threads za mgogoro wa mpaka na Malawi baadhi huwa wananipa uraia wa Malawi; kwenye kwenye threads za Rwanda, uraia wa Rwanda; kwenye threads dhidi ya Chadema, MwanaCCM; na kwenye threads dhidi ya CCM, Mwana-Chadema.

Anyway, sasa hapa you either have to agree or disagree with Kagame's assertion kuwa hao "experts on the ground" ni waongo, wanafiki, hawana credibility and also question their accountability.
 

mkuu wewe nitaendelea kukutilia shaka milele na yeyote anayefuatilia uchangiaji wako katika jukwaa hili, sina shaka umetumwa kuwa sehemu ya walioandaliwa kuifuruga nchi hii, kamwe wewe na aliyekutuma hamtafanikiwa, na utalaaniwa zaidi ya kizazi cha nyoka. VIVA TANZANIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…